Sura ya 4

Muda baada ya mwingine, tutakuwa tunakesha na kusubiri, kuwa na utulivu katika roho na kutafuta kwa moyo safi. Chochote kitakachotufikia, tusishiriki kwa upofu. Twahitajika tu kuwa kimya mbele ya Mungu na daima kushiriki naye, na kisha nia Yake itafichuliwa kwetu. Roho zetu sharti daima ziwe tayari kutofautisha na sharti ziwe na bidii na zisiokubali kushindwa. Ni lazima tuteke kutoka kwa maji ya uhai mbele ya Mungu, maji yanayozilisha na kuzirutubisha roho zetu zilizo na kiu. Ni lazima tuwe tayari wakati wowote, kujitakasa kutokana na haki ya kibinafsi, kiburi chetu, kujiridhisha kibinafsi, na ridhaa yetu, kila moja kuzaliwa kutoka kwa tabia yetu ya kishetani. Ni sharti tufungue mioyo yetu ili kukubali neno la Mungu, sharti tutumainie maneno Yake tunapojishughulisha na maisha yetu. Ni lazima tupitie na tuwe na uhakika juu ya neno Lake na kutimiza ufahamu wa neno Lake, tukiruhusu neno Lake kuwa maisha yetu. Huu ni wito wetu! Sisi hushinda tu tunapoishi kwa maneno ya Mungu.

Sasa dhana zetu ni kali sana, sisi husema kwa wepesi na kuchukua hatua kwa pupa na hatuwezi kufuata Roho. Leo haitakuwa kama zamani; kazi ya Roho Mtakatifu husonga mbele kwa kasi kubwa. Sharti tupitie neno la Mungu kwa undani; kila wazo na fikira, kila mwendo na jibu ni lazima tutofautishe mioyoni mwetu. Hakuna tunachofanya mbele ya mtu au nyuma yao yanaweza kutoroka hukumu mbele ya kiti cha Kristo. Roho Mtakatifu anatuongoza katika maeneo ya uzoefu zaidi, na kwa njia hii ya uzoefu tunakaribia kuwa na uhakika juu ya mwenye Uweza.

Mungu wa ulimwengu Amefungua macho yetu ya kiroho na siri katika roho huendelea kufichuliwa kwetu. Tafuta kwa moyo safi! Kuwa tayari kulipa gharama, songa mbele kwa moyo wako wote, kuwa tayari kujinyima, usiwe na tamaa tena, fuata Roho Mtakatifu na furahia neno la Mungu na kwa ujumla mtu mpya ataonekana. Wakati umewadia, ambapo Shetani atafikia kikomo chake, mapenzi ya Mungu yatatendeka. Mataifa yote ya dunia yatakuwa Ufalme wa Kristo na Kristo Atatawala kama Mfalme duniani milele!

Iliyotangulia: Sura ya 3

Inayofuata: Sura ya 5

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp