XI Maneno Bora Zaidi Juu ya Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli

(IX) Maneno Juu ya Kutimiza Wajibu Wako Kwa Kutosha

104. Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

kutoka katika “Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote” katika Neno Laonekana katika Mwili

105. Jinsi unavyochukulia agizo la Mungu ni jambo zito sana! Ikiwa huwezi kukamilisha kile ambacho Mungu hukuaminia, basi wewe hufai kuishi katika uwepo Wake na unapaswa kuadhibiwa. Ni amri ya Mbingu na kanuni ya dunia kwa wanadamu kumaliza kile ambacho Mungu huwaaminia; hili ndilo jukumu lao la juu kabisa, muhimu kama maisha yao. Ikiwa hulichukulii agizo la Mungu kwa uzito, basi unamsaliti Mungu kwa njia kuu zaidi; hili ni la kusikitisha zaidi kuliko Yuda na linakufanya ustahili kulaaniwa. Watu lazima wapate ufahamu mzuri kabisa kuhusu jinsi ya kutazama kile Mungu anachowaaminia na, angalau, lazima waelewe kwamba Mungu anawaagiza wanadamu: Huku ni kutukuzwa kukuu na mapendeleo maalum kutoka kwa Mungu, jambo la utukufu kuu zaidi. Kila kitu kingine kinaweza kuachwa—hata ikiwa itamlazimu mtu kutoa maisha yake bado lazima atimize agizo la Mungu.

kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

106. Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.

kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

107. Kila mtu anayemwamini Mungu anapaswa kuelewa mapenzi Yake. Ni wale tu wanaotimiza wajibu wao vizuri ndio wanaweza kumridhisha Mungu, na ni kwa kukamilisha tu kazi ambazo Yeye huwaaminia ndio wao kutimiza wajibu wao kutakuwa sawa kama kawaida. Katika kutimiza kazi, wakati watu hawaweki ukweli katika vitendo au hawatafuti ukweli, wakati hawatoi mioyo yao kwa ukweli, yaani, wakati wanatumiwa tu akili zao kukariri, wakitumia tu mikono yao kutenda, na kutumia tu miguu yao kukimbia, basi hawajatimiza agizo la Mungu kwa kweli. Kuna viwango vya ukamilishaji wa agizo la Mungu. Viwango hivi ni vipi? Bwana Yesu alisema: “Wewe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima.” Kumpenda Mungu ni kipengele kimoja cha kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa watu. Kwa kweli, wakati Mungu anawapa watu agizo, wakati wanatimiza wajibu wao kutoka kwa imani yao, viwango ambavyo Anahitaji kwao ni hivi: kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima, na kwa nguvu zako zote. Ikiwa wewe upo lakini moyo wako haupo, ukifikiria juu ya kazi kwa kichwa chako na kuziweka kwenye kumbukumbu, lakini huweki moyo wako ndani yake, na ikiwa unatimiza mambo kwa kutumia uwezo wako, je, huko ni kukamilisha agizo la Mungu? Kwa hiyo ni aina gani ya kiwango ambacho lazima kitimizwe ili utimize wajibu wako vizuri na kukamilisha yale ambayo Mungu amekuaminia, na kutimiza wajibu wako kwa uaminifu? Hiyo ni kufanya kazi yako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima, kwa nguvu zako zote. Ikiwa huna moyo wa kumpenda Mungu, basi hutafaulu katika kujaribu kutekeleza wajibu wako vizuri. Ikiwa upendo wako kwa Mungu hukua thabiti zaidi na halisi zaidi, basi utaweza kutekeleza wajibu wako kwa urahisi kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu yako yote.

kutoka katika “Kile Ambacho Watu Wamekuwa Wakiishi tu Kulingana Nacho” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

108. Haidhuru nini ufanyalo, unapaswa kwanza kuelewa kwa nini unalifanya, nia inayokupeleka kulifanya jambo hili ni gani, umuhumu ni gani katika wewe kulifanya, asili ya jambo hilo ni ipi, na iwapo ufanyalo ni jambo chanya au jambo hasi. Lazima uwe na ufahamu dhahiri kuhusu masuala haya yote; hii inahitajika sana kuweza kutenda kulingana na kanuni. Ikiwa unafanya kitu kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe tu? Unapaswa kusogea karibu na Mungu katika jambo hili. Kusogea karibu na Mungu kunamaanisha kutafuta ukweli katika jambo hili, kutafuta njia ya kutenda, kutafuta mapenzi ya Mungu, kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu. Hivi ndivyo jinsi ya kusonga karibu na Mungu katika kila jambo ufanyalo. Haihusu kufanya taratibu za kidini au tendo lionekanalo kwa nje; inafanywa kwa kusudi la kutenda kulingana na kweli baada ya kutafuta mapenzi ya Mungu. Ikiwa daima unasema “Asante Mungu” wakati hujafanya chochote, lakini unapofanya kitu, unaendelea kukifanya jinsi upendavyo, basi aina hii ya asante ni tendo la kuonekana kwa nje tu. Unapotimiza wajibu wako au kushughulikia kitu, unapaswa daima kufikiri: Ninapaswaje kutimiza wajibu huu? Kusudi la Mungu ni lipi? Sogea karibu na Mungu kupitia unachofanya; kwa hufanya hivyo unazitafuta kanuni na ukweli wa matendo yako pamoja na nia za Mungu, na hutapotea kutoka kwa Mungu katika chochote utendacho. Mtu wa aina hii tu ndiye anayemwamini Mungu kwa kweli.

kutoka katika “Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

109. Haijalishi ni wajibu upi unaotimiza, lazima utafute kushika mapenzi ya Mungu na kuelewa mahitaji Yake ni yapi kuhusiana na wajibu wako; ni hapo tu ndipo utaweza kushughulikia mambo kwa njia ya maadili. Katika kutekeleza wajibu wajo, huwezi kabisa kufuata upendeleo wako binafsi, kwa kufanya chochote ambacho ungependa kufanya, chochote ambacho unngefurahia na kuridhika unapokifanya au chochote ambacho kingekufanya uonekane kuwa mzuri. Ukimlazimishia kwa nguvu upendeleo wako kwa Mungu au kuutenda kama kwamba ni ukweli, ukiyafuata kana kwamba ni kanuni za ukweli, basi huko si kutekeleza wajibu wako, na kutekeleza wajibu wako kwa njia hakutakumbukwa na Mungu. Watu wengine hawaelewi ukweli, na hawajui kutekeleza wajibu wao kunamaanisha nini. Wao huhisi kuwa kwa kuwa wamejitolea na kutia juhudi, na kuteseka kwa sababu ya kunyima mwili, utimizaji wao wa wajibu wao unapaswa kuwa wastani—lakini kwa nini, basi, kila mara Mungu haridhiki? Je, watu hawa wamekosea wapi? Kosa lao lilikuwa kutotafuta matakwa ya Mungu, na badala yake kutenda kulingana na dhamira zao; walichukulia matakwa, upendeleo, na madhumuni yao wenyewe kama ukweli, na walivichukulia vitu hivyo kama kwamba vilikuwa upendeleo wa Mungu, kana kwamba vilitosheleza viwango na mahitaji Yake. Waliona walivyoamini kuwa sahihi, mema, na mazuri kuwa ukweli; hii si sahihi. Hata ingawa unaweza kudhani kuwa jambo fulani ni sahihi, bado lazima utafute kanuni za ukweli na uone ikiwa kile unachofikiria kinatosheleza matakwa ya Mungu. Ikiwa kinapingana na matakwa Yake, basi si sahihi hata ukifikiria ni sahihi, kwa kuwa hiyo ni fikira ya binadamu, na ni lazima uitupilie mbali. Wajibu ni nini? Ni agizo lililoaminiwa kwako na Mungu. Hivyo unapaswaje kutimiza wajibu wako? Kwa kutenda kwa mujibu wa matakwa na viwango vya Mungu, na kutegemeza tabia yako kwa kanuni za ukweli badala ya matamanio ya dhahania ya binadamu. Kwa njia hii, wewe kutimiza wajibu wako kutakuwa kumefikia kiwango kinachohitajika.

kutoka katika “Unaweza tu Kutekeleza Wajibu Wako Vizuri kwa Kutafuta Kanuni za Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

110. Kwa kila mmoja wenu anayetimiza wajibu wake, haijalishi jinsi unavyoelewa ukweli kwa kina, iwapo ungependa kuingia katika uhalisi wa ukweli, basi njia rahisi zaidi ya kutenda ni kufikiria maslahi ya nyumba ya Mungu katika kila kitu unachofanya, na kuachana na tamaa zako za kibinafsi, nia zako binafsi, dhamira, heshima na hadhi. Yaweke maslahi ya Mungu kwanza—hili ni jambo la msingi kabisa ambalo unapaswa kufanya. Ikiwa mtu anayetimiza wajibu wake hawezi hata kufanya kiwango hiki, basi anawezaje kusemwa kuwa anatimiza wajibu wake? Huku si kutimiza wajibu wa mtu. Unapaswa kwanza kufikiria maslahi ya nyumba ya Mungu, ufikirie maslahi ya Mungu mwenyewe, na ufikirie kazi Yake, na kuweka maslahi haya kwanza kabla kitu kingine; ni baada ya hapo tu ndipo unafaa kufikiria kuhusu uthabiti wa hadhi yako au jinsi wengine wanavyokuona. Je, huhisi kwamba inakuwa rahisi kidogo unapoyagawa katika hatua hizi na kufanya maafikiano fulani? Ukifanya hivi kwa muda, utakuja kuhisi kwamba kumridhisha Mungu si jambo gumu. Aidha, ikiwa unaweza kutimiza wajibu wako, kutenda faradhi na majukumu yako, kuweka kando tamaa zako binafsi, kuweka kando dhamira na nia zako mwenyewe, kufikiria nia ya Mungu na kuweka maslahi ya Mungu na nyumba Yake kwanza, basi baada ya muda wa uzoefu wa aina hii, utahisi kwamba hii ni njia nzuri ya kuishi: Ni kuishi kwa uhalisi na kwa uaminifu, bila kuwa mtu wa thamani ndogo au asiye na manufaa, na kuishi kwa haki na heshima badala ya kuwa na mawazo finyu au mchoyo. Utahisi kwamba hivi ndivyo mtu anapaswa kuishi na kutenda.

kutoka katika “Unaweza Kupata Ukweli Baada ya Kumkabidhi Mungu Moyo Wako Halisi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

111. Ikiwa unataka kujitolea kuyaridhisha mapenzi ya Mungu katika kila kitu unachofanya, basi huwezi kutekeleza wajibu mmoja tu; lazima ukubali agizo lolote akupealo Mungu. Liwe linalingana na upendeleo wako au halilingani, lipo ndani ya maslahi yako, ni kitu ambacho hufurahii au hujawahi kukifanya hapo awali, au ni ki kigumu, bado unapaswa kulikubali na kutii. Sio tu kwamba lazima ulikubali tu, lakini pia lazima ushirikiane kwa bidii, ujifunze kulihusu, na uwe na uingiaji. Hata ukiteseka na hujaweza kuonekana na kung’aa, bado lazima utende kujitolea kwako. Lazima ulione kama wajibu wako wa kutimiza; si kama kazi yako binafsi, lakini kama wajibu wako. Je, watu wanapaswa kuelewaje wajibu wao? Ni wakati ambapo Muumbaji—Mungu—anampa mtu kazi ya kufanya, na wakati huo, wajibu wa mtu huyo unatokea. Kazi ambayo Mungu anakupa, agizo ambalo Mungu anakupa—huu ni wajibu wako. Unapoyafuatilia kama malengo yako, na kwa kweli una moyo wa kumpenda Mungu, je, utakataa agizo la Mungu? (La.) Sio suala la ikiwa unaweza au la; ni kwamba hupaswi kukataa. Unapaswa kulikubali, sivyo? Hii ndiyo njia ya kutenda. Njia ya kutenda ni nini? (Kujitolea kabisa katika kila kitu.) Jitolee katika vitu vyote ili kufikia mapenzi ya Mungu. Jambo la kulengwa ni lipi? Ni “kila kitu.” “Kila kitu” haimaanishi kwa sharti mambo unayoyapenda au ambayo wewe ni hodari katika kuyafanya, sembuse mambo unayoyajua. Wakati mwingine utahitaji kujifunza, wakati mwingine utakumbana na matatizo, na wakati mwingine lazima uteseke. Hata hivyo, bila kujali ni kazi ipi, almradi ni agizo la Mungu, lazima ulikubali kutoka Kwake, ulichukulie kama wajibu wako, ujitolee kulitimiza, na kufikia mapenzi ya Mungu: Hii ndiyo njia ya kutenda.

kutoka katika “Mtu Anaweza Tu Kuwa na Furaha ya Kweli Kwa Kuwa Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

112. Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu Hatamtendea mtu yeyote vibaya ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

113. Sasa nitawaambia kuhusu kanuni ya utendaji: Haijalishi kile unachokumbana nacho, kiwe ni kitu ambacho kinakushawishi na kukujaribu, au hali ambayo unashughulikiwa, na haijalishi jinsi wengine wanavyokutendea, kwanza lazima uweke kitu hicho kando na uombe mbele ya Mungu. Lazima urudi kwa roho, urejeshe upatanifu katika roho yako na urekebishe upya hali yako. Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho kinapaswa kutatuliwa: “Haijalishi kitu hiki ni kikubwa kiasi gani, liwe liwalo, lazima nitekeleze wajibu wangu vizuri; almradi napumua, siwezi kuuacha wajibu wangu.” Basi, unawezaje kutekeleza wajibu wako vizuri? Sio tu kwa kufanya mambo bila shauku, wala sio kwa kuwapo kimwili lakini haupo kimawazo. Lazima uuweke moyo wako katika kutekeleza wajibu wako. Haijalishi jinsi suala unalokumbana nalo linavyoweza kuwa kubwa, lazima uliweke kando na umrudie Mungu, na utafute jinsi ya kutekeleza wajibu wako vizuri kiasi cha kumridhisha Mungu. Unapaswa kutafakari, “Katika kukumbana na swala hili leo, napaswa kufanya nini ili nitekeleze wajibu wangu? Hapo awali, nilifanya vitu kwa njia ya uzembe tu, lakini leo lazima nibadilishe mbinu yangu na kujitahidi kuifanya vizuri ili isiwe na dosari kabisa. Jambo la muhimu ni kwamba ni lazima nisimsikitishe Mungu; lazima nimpe amani na kumfanya Aone kuwa wakati natekeleza wajibu wangu, sitendi tu vizuri na kutii, lakini pia mimi ni mwenye kujitolea.” Ukitenda kwa njia hii, na ukiweka jitihada yako katika hili, basi wajibu wako hautaathiriwa, na utaweza kuutekeleza vizuri. Na unapoendelea kuomba na kufanya marekebisho, hali yako itakuwa ya kawaida zaidi na zaidi, na baada ya hapo utakuwa mwenye uwezo wa kutimiza wajibu wako zaidi na zaidi.

kutoka katika “Uingiaji Katika Maisha Lazima Uanzie Katika Kutimiza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

114. Haijalishi kile ambacho Mungu anataka kutoka kwako, unahitaji tu kujitolea kikamilifu. Natarajia utaweza kuonyesha uaminifu wako kwa Mungu mbele Yake mwishowe, na maadamu unaweza kuiona tabasamu ya Mungu ya kupendeza Akiwa katika kiti Chake cha enzi, hata kama ni wakati wako kufa, lazima uweze kucheka na kutabasamu macho yako yanapofumba. Lazima umfanyie Mungu wajibu wako wa mwisho wakati wa muda wako hapa duniani. Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu. Kiumbe anaweza kumfanyia Mungu nini? Kwa hiyo unapaswa kujitolea kwa rehema ya Mungu mapema iwezekanavyo. Maadamu Mungu anafurahia na Anapendezwa, basi mwache Afanye chochote Atakacho. Wanadamu wana haki gani ya kulalamika?

kutoka katika “Sura ya 41” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

115. Leo hii mnachohitajika kufikia si madai ya ziada, ila ni wajibu wa mwanadamu, na kile kinachofaa kufanywa na kila mtu. Kama hamuwezi hata kufanya wajibu wenu, au kuufanya vizuri, hamuoni mnajiletea masaibu nyinyi wenyewe? Hamwuoni mnajitakia kifo? Mtatarajiaje maisha ya baadaye na matarajio? Kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu, na ushirika wa mwanadamu ni kwa minajili ya usimamizi wa Mungu. Baada ya Mungu kufanya yale yote Anayopaswa kufanya, mwanadamu anapaswa kufanya vitendo bila kukoma, na kushirikiana na Mungu. Mwanadamu hapaswi kulegeza kamba katika kazi ya Mungu, lazima aonyeshe uaminifu na asijitie katika mawazo mengi au kukaa akisubiri kifo bila kufanya kitu. Mungu Mwenyewe anaweza kujitolea kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asiweze kuwa mwaminifu kwa Mungu? Mawazo na moyo wa Mungu vipo kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asijitolee katika ushirika? Mungu huwafanyia wanadamu kazi, basi ni kwa nini mwanadamu asifanye wajibu wake kwa minajili ya usimamizi wa Mungu? Kazi ya Mungu imefika umbali huu, bado mnaona ila hutendi, mnasikia ila hamsogei. Je, si watu kama hawa wanafaa kuangamizwa kabisa? Tayari Mungu amejitolea kikamilifu kwa ajili ya mwanadamu, basi ni kwa nini siku hizi mwanadamu hafanyi wajibu wake kwa dhati? Kwa Mungu, kazi Yake ni ya kipaumbele Kwake, na kazi ya usimamizi Wake ni ya umuhimu wa hali ya juu. Kwa mwanadamu, kuweka maneno ya Mungu katika vitendo na kutimiza mahitaji ya Mungu ndiyo kipaumbele kwake. Ni lazima nyote myafahamu haya.

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: (VIII) Maneno Juu ya Jinsi ya Kumtii Mungu

Inayofuata: (X) Maneno Juu ya Kumcha Mungu na Kuepuka Uovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Sura ya 22

Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki