H. Juu ya Kumcha Mungu na Kuepuka Uovu

415. Ili kuwa kiumbe halisi aliyeumbwa, sharti ujue Muumba ni nani, uumbaji wa mwanadamu ni wa umuhimu gani, jinsi ya kutekeleza majukumu ya kiumbe, na jinsi ya kumwabudu Bwana wa uumbaji wote, lazima aelewe, ashike, ajue, na kujali kuhusu nia za Muumba, mapenzi Yake, na madai Yake, na lazima atende kulingana na njia ya Muumba—kumcha Mungu na kuepuka maovu.

Kumcha Mungu kuna maana gani? Na mtu anawezaje kuepuka maovu?

“Kumcha Mungu” hakumaanishi woga na hofu isiyotajika, wala kukwepa, wala kuweka umbali, wala si kuabudu kama mungu ama ushirikina. Ila, ni kutazama na kupendezwa, sifa, imani, kuelewa, kujali, kutii, kuweka wakfu, upendo, na pia ibada isiyo na vikwazo au malalamishi, malipo na kutii. Bila ya ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na kupendezwa halisi, imani halisi, kuelewa halisi, kujali halisi ama utiifu, ila tu hofu na kukosa utulivu, shaka pekee, kutoelewa, kukwepa, na kuepuka; bila maarifa halisi ya Mungu, binadamu hawatakuwa na utakatifu na malipo halisi; bila ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na ibada halisi na kujisalimisha, uabudu kama mungu upofu tu na ushirikina; bila maarifa halisi juu ya Mungu, binadamu hawawezi kutenda kulingana na njia ya Mungu, ama kumcha Mungu, ama kuepuka maovu. Badala yake, kila tendo na tabia ambayo mwanadamu anashiriki litajaa uasi na kutotii, na kumbukumbu zinazokashifu na hukumu ya usengenyaji kumhusu Yeye, na mienendo miovu inayokwenda kinyume na ukweli na maana ya kweli ya maneno ya Mungu.

Punde wanadamu wanapokuwa na imani ya kweli kwa Mungu, watakuwa wa kweli katika kumfuata Yeye na kumtegemea; kwa imani ya kweli pekee na tegemeo kwa Mungu ndipo binadamu watakuwa na kuelewa kwa kina na ufahamu; pamoja na ufahamu wa kweli wa Mungu inakuja kumjali Kwake kwa kweli; ni kwa kumjali Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na utiifu wa kweli kwa Mungu; na ni kwa utiifu wa Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na uwekaji wakfu wa kweli; na ni kwa uwekaji wakfu wa kweli kwa Mungu pekee ndipo binadamu watakuwa na malipo yasiyo na kiwango na kulalamika; ni kwa imani na msimamo wa kweli, kuelewa na kujali kwa kweli, utiifu wa kweli, utakatifu wa kweli na malipo, ndipo binadamu watakuja kujua kwa kweli tabia na kiini cha Mungu, na kujua utambulisho wa Muumba; Watakapopata kumjua Muumba ndipo binadamu wataamsha ndani yao ibada ya kweli na kujisalimisha; watakapokuwa na ibada ya kweli na kujisalimisha kwa Muumba tu ndipo binadamu wataweza kwa kweli kuweka kando njia zao za uovu, hivyo ni kusema, kuepuka maovu.

Hii inajumlisha hatua yote ya “kumcha Mungu na kuepuka maovu” na pia ni maudhui katika kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa ujumla, na pia njia ambayo ni lazima kupitia ili kufikia kumcha Mungu na kuepuka maovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji

416. Kwanza kabisa tunajua kwamba tabia ya Mungu ni adhama, ni hasira. Yeye si kondoo ili achinjwe na yeyote; na hata zaidi Yeye si kikaragosi ili adhibitiwe na watu vyovyote vile wanavyotaka. Yeye pia si hewa tupu ili kuamrishwa huku na kule na watu. Kama kweli unasadiki kwamba Mungu yupo, unafaa kuwa na moyo unaomcha Mungu, na unafaa kujua kwamba kiini halisi cha Mungu hakifai kughadhabishwa. Ghadhabu hii inaweza kusababishwa na neno; pengine fikira; pengine aina fulani ya tabia bovu; pengine tabia ya upole tabia inayoweza kuruhusiwa kwenye macho na maadili ya binadamu; au pengine inasababishwa na falsafa, nadharia. Hata hivyo, punde unapomghadhabisha Mungu, fursa yako inapotea na siku zako za mwisho zinakuwa zimewasili. Hili ni jambo baya! Kama huelewi kwamba Mungu hawezi kukosewa, basi pengine humchi Mungu, na pengine unamkosea Yeye kila wakati. Kama hujui namna ya kumcha Mungu, basi huwezi kumcha Mungu, na hutaweza kujua namna ya kujiweka kwenye njia ya kutembelea kwa njia ya Mungu—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Punde unapokuwa na habari, unaweza kuwa na ufahamu kwamba Mungu hawezi kukosewa, kisha utajua ni nini maana ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

417. Ingawa sehemu ya kiini halisi cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau hoja kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Anao upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na kwamba Yeye hana hisia zozote, au mijibizo yoyote. Kwamba Anayo rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote kuhusiana na namna Anavyoshughulikia watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Yeye si kikaragosi kilichofikiriwa au kitu kingine tu. Kwa sababu Yeye yupo, tunafaa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake siku zote, kutilia makini mwelekeo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatufai kutumia kufikiria kwa watu ili kumfafanua Mungu, na hatufai kulazimisha fikira na matamanio ya watu kwa Mungu, kumfanya Mungu kutumia mtindo na fikira za binadamu katika namna Anavyomshughulikia binadamu. Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu mlio hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusiana na namna mnavyoshughulikia Mungu, mnapokuwa makini zaidi na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi! Wakati huelewi mwelekeo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kama unaweza kutimiza hoja hii kati ya zote, na kumiliki mwelekeo huu kati ya yote, basi Mungu hatakulaumu wewe kwa upumbavu wako, kutojua kwako, na ukosefu wa kuelewa kwa sababu zinazosababisha vitu. Badala yake, kutokana na hofu yako ya kumkosea Mungu, heshima yako kwa nia za Mungu, na mwelekeo wako wa kuwa radhi kumtii Yeye, Mungu atakukumbuka, atakuongoza na kukuangaza wewe, au kustahimili kutokuwa mkomavu kwako na kutojua kwako. Kinyume chake, endapo mwelekeo wako kwake Yeye utakuwa usioheshimu—kuhukumu Mungu kiholela, kukisia kiholela, na kufafanua maana ya Mungu—Mungu atakupa hukumu, nidhamu, au hata adhabu; au Atakupa taarifa. Pengine kauli hii inahusisha matokeo yako. Hivyo basi, Ningali bado nataka kutilia mkazo jambo hili kwa mara nyingine: Unapaswa uwe makini na mwenye busara katika kila kitu kinachotoka kwa Mungu. Usiongee kwa uzembe, na usiwe mzembe katika matendo yako. Kabla ya kusema chochote, unafaa kufikiria: Je, kufanya hivi kutamghadhabisha Mungu? Kufanya hivi ni kumcha Mungu? Hata katika masuala mepesi, bado unafaa kujaribu kuelewa hakika maswali haya, yafikirie kwa kweli. Kama unaweza kwa kweli kutenda haya kulingana na kanuni hizi kila pahali, katika hali zote, katika vitu vyoye, nyakati zote, na kushikilia mtazamo wa aina hiyo hasa wakati huelewi kitu basi Mungu siku zote atakuongoza wewe, na kukupa na hata njia ya kufuata.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

418. Ninawashawishi kuwa na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu nyinyi hamna maadili katika matendo yenu, kufanya na kutenda kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili sana katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa kuzimu. Kwa binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote zaidi. Je, una habari, hata hivyo, kwamba katika macho ya Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwake hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za utawala za Mungu zaidi ya mara moja na hujaonyesha ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia kuzimu pale ambapo Mungu anamwadhibu mwanadamu. Katika wakati wao wa kufuata Mungu, idadi ndogo ya watu ilitenda matendo yaliyoenda kinyume na kanuni, lakini baada ya kushughulikiwa na kuongozwa, waligundua polepole upotovu wao, na kisha wakachukua njia iliyo sawa ya uhalisi, na leo wanabaki wenye msingi imara katika njia ya Bwana. Binadamu kama hawa ndio watakaobakia mwisho. Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya kiwango kilichowekwa. Yeyote asiyemcha Mungu na asiye na moyo unaotetema kwa woga atakiuka amri za utawala za Mungu kwa urahisi. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya hisia kali, na hawajui katu amri za utawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyokatiza usimamizi wa Mungu. Kwa hali za uzito sana, wanatupwa nje na kunyang’anywa fursa yoyote zaidi ya kumfuata, na wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba ya Mungu unakoma. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa bila jitihada. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si mafungu wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu, na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na hujajiandaa ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

419. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi haitawezekana kwako kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, haitawezekana wewe kumwonyesha heshima na uchaji, lakini badala yake utakuwa tu mzembe asiyejali na kuepuka kusema ukweli wote, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Ingawa kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakini au kudadisi masuala haya. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuzilia mbali amri za utawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na tunda la msingi la tendo lako linakuwa ni kosa dhidi ya amri ya utawala. Sasa unafaa kutambua kwamba kuelewa tabia ya Mungu huja na kujua dutu Yake, nakwamba pamoja na kuelewa tabia ya Mungu huja kuelewa amri za utawala. Bila shaka, amri nyingi za utawala zinahusisha tabia ya Mungu, lakini tabia Yake haijaonyeshwa ndani yao kikamilifu. Kwa hivyo mnawahitaji kuongeza hatua nyingine katika kukuza ufahamu wenu wa tabia ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

420. Mungu ni Mungu aliye hai, na kama vile tu watu wanavyotenda tofauti katika hali tofauti, ndivyo mwelekeo wa Mungu ulivyo katika utendakazi huu na unavyotofautiana kwa sababu Yeye si kikaragosi, wala Yeye si hewa tupu. Kupata kuujua mwelekeo wa Mungu ni jambo lenye thamani kwa wanadamu. Watu wanafaa kujifunza vipi, kwa kuujua mwelekeo wa Mungu, wanaweza kuijua tabia ya Mungu na kuuelewa moyo Wake kidogo kidogo. Unapouelewa moyo wa Mungu kidogo kidogo hutahisi kwamba kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ni jambo gumu la kutimiza. Kilicho zaidi ni kwamba, unapomwelewa Mungu, hakuna uwezekano wa wewe kufanya hitimisho kuhusu Yeye. Unapoacha kufanya hitimisho kuhusu Mungu, hakuna uwezekano wa wewe kumkosea Yeye, na bila kujua Mungu atakuongoza kuwa na maarifa Yake, na hivyo basi utamcha Mungu katika moyo wako. Utaacha kumfafanua Mungu kwa kutumia falsafa, zile barua, na nadharia ambazo umejifunza. Badala yake, kwa kutafuta nia za Mungu katika mambo yote na siku zote utaweza bila kufahamu kuwa mtu anayefuata moyo wa Mungu.

Kazi ya Mungu haionekani wala kugusika na wanadamu, lakini kulingana na Mungu, hatua za kila mmoja, pamoja na mwelekeo wake kwake Yeye—haya hayatambuliki tu na Mungu, lakini pia kuonekana vilevile. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anafaa kutambua na kuwa wazi kulihusu. Unaweza kuwa ukijiuliza siku zote: “Je, Mungu anajua kile ninachofanya hapa? Je, Mungu anajua kile ninachofikiria sasa hivi? Pengine Anajua, pengine Hajui.” Kama utakuwa na aina hii ya mtazamo, kufuata na kusadiki Mungu ilhali unatia shaka katika kazi Yake na uwepo Wake, basi hivi karibuni au baadaye siku itawadia ambapo utamghadhabisha, kwa sababu tayari unayumbayumba pembezoni pa jabali hatari. Nimewaona watu ambao wamesadiki katika Mungu kwa miaka mingi lakini bado hawajapata uhalisia wa ukweli, wala hawaelewi hata mapenzi ya Mungu. Maisha yao na kimo chao havipigi hatua yoyote, ukitii tu falsafa zile za kiwango cha chini zaidi. Hii ni kwa sababu watu hawa hawajawahi kuchukulia neno la Mungu kama maisha yao binafsi, na hawajawahi kukabiliana na kukubali uwepo Wake. Je, unafikiri kwamba Mungu huwaona watu kama hawa na kujawa na furaha? Je, wanamtuliza Yeye? Katika jinsi hiyo, ni mbinu ya imani ya watu katika Mungu ambayo inaamua majaliwa yao. Kuhusu jinsi watu humtafuta na jinsi wanavyomweleka Mungu, mitazamo ya watu ni ya umuhimu wa kimsingi. Usimwache Mungu kana kwamba yeye ni fungu la hewa kavu tu linaloelea karibu na nyuma ya kichwa chako. Usikose kumjali Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu nyuma ya kichwa chako. Siku zote fikiria kuhusu Mungu wa imani yako kama Mungu hai, Mungu halisi. Yeye hayupo kule juu kwenye mbingu ya tatu bila chochote cha kufanya. Badala yake, siku zote bila kusita Anaangalia kwenye mioyo ya kila mmoja, Akiangalia ni nini unachofanya, akichunguza kila neno dogo na kila tukio dogo, akiangalia mwenendo wako na mwelekeo wako kwa Mungu. Kama uko radhi kujitolea kwa Mungu au la, tabia yako yote na fikira zako na mawazo yako ya ndani zaidi ziko mbele ya Mungu, na yanaangaliwa na Yeye. Ni kulingana na tabia yako, kulingana na vitendo vyako, na kulingana na mwelekeo wako kwa Mungu, ambapo maoni Yake kwako, na mwenendo Wake kwako, vinaendelea vikibadilika. Mimi Ningependa kutoa ushauri fulani kwa baadhi ya watu. Msijiweke kwenye mikono ya Mungu kama watoto wachanga, kana kwamba Yeye Anapaswa kukupenda sana, kana kwamba Asingewahi kukuacha, na kana kwamba mwelekeo Wake kwako ni imara na usingeweza kubadilika, na Ninawashauri muache kuota ndoto! Mungu ni mwenye haki katika kutendea kila mtu. Anakabiliana na kazi ya ushindi wa wanadamu na wokovu kwa bidii. Huo ndio usimamizi Wake. Anashughulikia kila mmoja kwa umakinifu, na wala si kama kiumbe cha kufugwa cha kucheza nacho. Upendo wa Mungu kwa binadamu si ule wa kudekeza au kupotosha; rehema na uvumilivu Wake kwa wanadamu si dokezi au ya kutotilia maanani. Kinyume cha mambo, upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kutunza, kusikitikia, na kuheshimu maisha; rehema na uvumilivu Wake vyote vinaonyesha matarajio Yake kwa binadamu; rehema na uvumilivu Wake ndivyo ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Mungu yuko hai, na kwa hakika Mungu yupo; mwelekeo Wake kwa wanadamu unafuata kanuni, si yenye kutangazwa kama imani ya dini, na unaweza kubadilika. Mapenzi Yake kwa binadamu yanabadilika kwa utaratibu na kurekebishwa kwa muda, hali na mwelekeo wa kila mtu. Kwa hiyo, unafaa kujua rohoni mwako na uwazi wote kwamba kiini halisi cha Mungu hakibadiliki, na kwamba tabia Yake itajitokeza katika nyakati tofauti, na muktadha tofauti. Huenda usifikirie kwamba hili si suala muhimu, na wewe unatumia dhana zako za kibinafsi katika kufikiria namna ambavyo Mungu anafaa kufanya mambo. Lakini zipo nyakati ambapo kinyume kabisa cha mtazamo wako ni kweli, na kwa kutumia dhana zako za kibinafsi katika kujaribu na kumpima Mungu, tayari umemghadhabisha. Hii ni kwa sababu Mungu hafanyi kazi kama unavyofikiria wewe, Naye Mungu hatalishughulikia suala hili kama vile unavyosema Atalishughulikia. Na hivyo basi Nakukumbusha kuwa makini na mwenye hekima katika mtazamo wako katika kila kitu, na ujifunze namna ya kufuata kanuni ya kutembea kwenye njia ya Mungu katika mambo yote—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima uimarishe uelewa dhabiti katika masuala ya mapenzi ya Mungu na mwelekeo wa Mungu; kutafuta watu walio na nuru kuuwasilisha kwako, na kutafuta kwa dhati. Usimwone Mungu wa imani yako kama kikaragosi—kuhukumu kiholela, kufikia hitimisho kiholela, kutomshughulikia Mungu kwa heshima Anayostahili. Katika mchakato wa wokovu wa Mungu Anapofafanua matokeo yako, bila kujali kama Yeye atakupa rehema, au uvumilivu, au hukumu na kuadibu, mwelekeo Wake kwako wewe unabadilika. Inategemea na mwelekeo wako kwa Mungu, na uelewa wako wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

421. Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakienda kwa mikogo na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti zao na mataifa yana sheria zao; je, hali sio hivi hata zaidi katika nyumba ya Mungu? Je, matarajio sio makali hata zaidi? Je, hakuna amri nyingi hata zaidi za utawala? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea; Yeye ni Mungu anayewaua watu. Je, watu kweli hawajui hili tayari?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

422. Katika kila enzi, Mungu huwapa binadamu baadhi ya maneno Anapofanya kazi ulimwenguni, huku akimwambia mwanadamu kuhusu baadhi ya ukweli. Ukweli huu unahudumu kama njia ambayo binadamu anafaa kuitii, njia ya kutembelewa na binadamu, njia ambayo humwezesha binadamu kumcha Mungu na kujiepusha na uovu, na njia ambayo watu wanafaa kuweka katika vitendo na kuitii katika maisha yao na kwenye mkondo wa safari zao za maisha. Ni kwa sababu hizi ambapo Mungu anampa binadamu maneno haya. Binadamu anafaa kuyatii maneno haya yanayotoka kwa Mungu, na kuyatii ni kupokea uzima. Kama mtu hataweza kuyatii, na hayatii kwenye matendo, na haishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu katika maisha yake, basi mtu huyo hautilii ukweli katika matendo. Na kama hawatilii ukweli katika matendo, basi hawamchi Mungu na hawaepuki uovu, wala hawawezi kumtosheleza Mungu. Kama mtu hawezi kumtosheleza Mungu, basi hawezi kupokea sifa ya Mungu; mtu wa aina hii hana matokeo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

423. Kutembea katika njia ya Mungu hakuhusu kuangalia sheria juujuu. Badala yake, kunamaanisha kwamba unapokabiliwa na suala, kwanza kabisa, unaliangalia kama ni hali ambayo imepangwa na Mungu, wajibu uliopewa wewe na Yeye, au kitu ambacho Amekuaminia wewe, na kwamba unapokabiliana na suala hili, unapaswa kuliona kama jaribio kutoka kwa Mungu. Wakati unapokabiliwa na suala hili, lazima uwe na kiwango, lazima ufikirie kwamba suala hilo limetoka kwa Mungu. Lazima ufikirie ni vipi ambavyo utashughulikia suala hili kiasi cha kwamba unaweza kutimiza wajibu wako, na kuwa mwaminifu kwa Mungu; namna ya kulifanya bila ya kumghadhabisha Mungu; au kukosea tabia Yake. … Kwa sababu ili kutembea katika njia ya Mungu, hatuwezi kuwachilia chochote kinachotuhusu sisi wenyewe, au kinachofanyika karibu nasi, hata yale mambo madogo madogo. Haijalishi kama tunafikiria tunafaa kumakinika au la, mradi tu suala lolote linatukabili hatufai kuliacha. Lote linafaa kuonekana kama jaribio la Mungu kwetu. Mwelekeo aina hii uko vipi? Kama unao mwelekeo aina hii, basi unathibitisha hoja moja: Moyo wako unamcha Mungu, na moyo wako uko radhi kujiepusha na maovu. Kama unalo tamanio hili la kumtosheleza Mungu, basi kile unachotia katika matendo hakiko mbali na kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Kunao mara nyingi wale wanaosadiki kwamba masuala ambayo hayatiliwi maanani na watu, masuala ambayo kwa kawaida hayatajwi—haya ni mambo madogo tu, na hayana chochote kuhusiana na kutia ukweli katika matendo. Wakati watu hawa wanakabiliwa na suala kama hilo, hawalifikirii sana na wanaliachilia tu. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, suala hili ni funzo ambalo unafaa kulidadisi, funzo kuhusu namna ya kumcha Mungu, namna ya kujiepusha na maovu. Zaidi, kile unachofaa kujali hata zaidi ni kujua kile Mungu anachofanya wakati suala hili linapoibuka kukabiliana na wewe. Mungu yuko kando yako, anaangalia kila mojawapo ya maneno na vitendo vyako, anaangalia hatua zako, mabadiliko ya akili zako—hii ni kazi ya Mungu. Baadhi ya watu husema: “Basi kwa nini siihisi?” Huihisi kwa sababu namna ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu haijawa ndiyo njia muhimu zaidi kwako kushughulikiwa. Hivyo basi, huwezi kuhisi kazi ngumu ya Mungu katika binadamu, inayojionyesha kulingana na fikira tofauti na vitendo tofauti vya watu. Wewe u makini! Suala kubwa ni lipi? Swala dogo ni lipi? Masuala yote yanayohusu kutembea katika njia ya Mungu hayagawanywi kwa masuala makubwa au madogo. Mnaweza kulikubali hilo? (Tunaweza kulikubali.) Kuhusiana na masuala ya kila siku, kunayo yale ambayo watu wanayaona kuwa makubwa sana na muhimu, na mengine yanaonekana kuwa mambo madogo madogo tu. Mara nyingi watu huyaona masuala haya makubwa kuwa ndiyo muhimu zaidi, na wanayachukulia kwamba yametumwa na Mungu. Hata hivyo, kwenye mkondo wa masuala haya makubwa kujitokeza, kutokana na kimo finyu cha binadamu, na kutokana na kiwango cha binadamu kisichotosha, mara nyingi binadamu haendani sawa na nia za Mungu, hawezi kupata ufunuo wowote, na hawezi kufaidi maarifa yoyote halisi yenye thamani. Kuhusu masuala madogo, haya yanapuuzwa tu na binadamu, kuachwa kuponyoka kidogokidogo. Hivyo basi, wamepoteza fursa nyingi sana za kuchunguzwa mbele ya Mungu, kujaribiwa na Yeye. Je unafaa kuwapuuza watu, masuala na hali hizi siku zote ambazo Mungu anakupangilia wewe, hii itamaanisha nini? Inamaanisha kwamba kila siku, hata kila wakati, siku zote unakana ukamilifu wa Mungu kwako, na uongozi wa Mungu. Kila Mungu anapopanga hali hizi kwako wewe, Yeye anakuangalia kwa siri, Anauangalia moyo wako, Anaziangalia fikira na hali zako, Anaangalia namna unavyofikiria wewe, Anaangalia namna unavyochukua hatua. Kama wewe ni mtu asiyejali—mtu ambaye hajawahi kujali kuhusu njia ya Mungu, neno la Mungu, au ukweli—basi hutajali, hutatilia maanani kile ambacho Mungu anataka kukamilisha, na yale ambayo Mungu anakuhitaji wewe kufanya wakati Anapopanga hali hizi kwako wewe. Hutajua pia namna ambavyo masuala haya ya kila siku yanavyohusiana na ukweli au nia za Mungu. Baada ya kukabiliana na hali nyingi kama hizi na majaribio mengi kama haya, huku naye Mungu haoni mafanikio yoyote kutokana na wewe, ataweza kuendelea vipi? Baada ya kukabiliwa na majaribio mara kwa mara, humkuzi Mungu katika moyo wako, na hushughulikii zile hali ambazo Mungu anakupangia wewe kama zilivyo—kama majaribio ya Mungu au mitihani ya Mungu. Badala yake unakataa fursa ambazo Mungu amekupa wewe moja baada ya nyingine, na unaziacha kutokomea mara kwa mara. Je huu si kutotii kwa kiwango cha juu na binadamu? (Naam, ni kutotii.) Je, Mungu atahuzunika kwa sababu ya haya? (Naam Atahuzunika.) Mungu hatahuzunika! Mkinisikia Nikiongea hivi mnashtuka kwa mara nyingine tena. Kwani umesahau, ilisemekana hapo awali kwamba Mungu huhuzunika siku zote? Mungu hatahuzunika? Ni lini basi Mungu atahuzunika? Usijali, Mungu hatahuzunika na hali hii. Basi mwelekeo wa Mungu kwa aina hii ya tabia iliyoelezwa kwa muhtasari hapo juu ni upi? Wakati watu wanapokataa majaribio, mitihani, ambayo Mungu anawapa, wakati wanapoikwepa, kunao mwelekeo mmoja tu ambao Mungu anao kwa watu kama hawa. Mwelekeo huu ni upi? Mungu husukumia mbali aina hii ya watu kutoka kina cha moyo Wake. Kunazo safu mbili za maana ya kauli “sukumia mbali”. Ninawezaje kuzielezea? Ndani kabisa ya moyo, kauli hii inao mkazo wa kuchukiza, wa chuki. Na je, safu ya pili ya maana? Sasa hiyo ndiyo sehemu inayoashiria kukata tamaa dhidi ya kitu. Nyote mnajua “kukata tamaa” kunamaanisha nini, ni kweli? Kwa ufupi, kusukumia mbali kunamaanisha uamuzi na mwelekeo wa mwisho wa Mungu kwa watu wanaokuwa na mwenendo huu. Ni chuki ya kupindukia dhidi yao, maudhi, na hivyo basi uamuzi wa kuwaacha. Huu ndio uamuzi wa mwisho wa Mungu kwa mtu ambaye hajawahi kutembea katika njia ya Mungu, ambaye hajawahi kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

424. Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa wanadamu, na utimilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawaje hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu, na kutokana na kumcha Mungu kwake, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu uhuru wa kuchukua chochote alichokuwa nacho, ilhali hakulalamika, na akaanguka chini mbele ya Mungu na kumwambia kwamba kwa wakati huohuo, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake timilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na upole wake, Ayubu hakutikisika katika utambuzi wake na uzoefu wa uwepo wa Mungu na juu ya msingi huu aliweza kujitolea madai yeye mwenyewe na kuwastanisha kufikiria kwake, tabia, mwenendo, na kanuni za vitendo mbele ya Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake yeye na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa ameviona miongoni mwa mambo mengine yote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia. Ayubu aliumiliki ubinadamu wa uaminifu, usio na hatia, na wa upole, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kushuhudia katikati ya mashambulizi mabaya kama yale yaliyomsibu kutoka kwa Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kutosheleza kwake Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

425. Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, na sembuse yeye kuipitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliokuwa nao wakati wa majaribu unashuhudiwa na kila mmoja, na unapendwa, unafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wanayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na hata zaidi ya hayo, wanaimba sifa zao. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo mbalimbali ya maisha yake isiyo ya ajabu, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu kuliko mtu yeyote mwingine. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakuwa sanasana yenye ushupavu, wala, aidha, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole na unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea, haki, na iliyopenda mambo chanya—hakuna kati ya mambo haya yanayomilikiwa na watu wengi wa kawaida. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwangalifu sana katika kufikiria kwake. Hivyo, wakati wake usio wa ajabu duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na aliuona ukubwa, utakatifu, na kuwa na haki kwa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na aliuona utukufu na mamlaka ya Mungu mkuu zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu aweze kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa kwamba alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu na mtimilifu, na wa kuwa mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na aliyejiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuatilia mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawa alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo kwazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawa alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuza binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawa miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu kutokuwa wa ajabu kwa maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Machoni pake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Hakuwa amemwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa ajabu duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu havikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala havikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi, katika maisha yake ya kila siku, wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye Amejificha miongoni mwa mambo yote. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti ya moyo wa Mungu na maneno ya Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote lakini anaonyesha sauti ya moyo Wake na maneno kwa kutawala sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule ufahamu na maarifa sawa kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu hakuwa amemwonekania Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kumwonekania au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote yanatosha kwa mwanadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo, nguvu na mamlaka ya Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu yanatosha kumfanya mwanadamu afuate njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

426. “Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu” na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kuepuka maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli; iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kumcha Mungu kwa kweli, lazima awe na maarifa ya kweli kuhusu Mungu; Iwapo mtu anataka kupata maarifa ya Mungu, lazima kwanza ayapitie maneno ya Mungu, aingie katika ukweli wa maneno ya Mungu, apitie kuadibu na nidhamu ya Mungu, kuadibu Kwake na hukumu; iwapo mtu anataka kupitia maneno ya Mungu, lazima aje ana kwa ana na maneno ya Mungu, aje ana kwa ana na Mungu, na kumwomba Mungu Ampe fursa ya kupitia maneno ya Mungu katika hali ya aina yote ya mazingira inayowahusisha watu, matukio na vitu; iwapo mtu anataka kuja ana kwa ana na Mungu na maneno ya Mungu, lazima kwanza amiliki moyo wa kweli na mwaminifu, awe tayari kuukubali ukweli, kukubali kupitia mateso, uamuzi na ujasiri wa kuepuka uovu, na azimio la kuwa kiumbe halisi…. Kwa njia hii, kuendelea mbele hatua kwa hatua, utamkaribia Mungu zaidi, moyo wako utakuwa safi zaidi, na maisha yako na thamani ya kuwa hai, pamoja na maarifa yako kumhusu Mungu, yatakuwa ya maana zaidi na yatakuwa hata ya kupevuka zaidi. Mpaka siku moja, utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena, kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako, kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako, kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo, kwamba Muumba siye yule unayemtamania katika mawazo yako lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia zako, kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako, Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako. Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho. Mungu kama huyo Anakukubali umpende kutoka moyoni, umshikilie, umweke karibu, umtamani, uhofu kumpoteza, na kutotaka kumkataa tena, kutomtii tena, ama kumwepuka tena ama kumweka mbali. Kile unachotaka ni kumjali tu, kumtii, kulipia kila kitu Anachokupa, na kujisalimisha katika himaya Yake. Hukatai tena kuongozwa, kupewa, kuangaliwa, na kuwekwa na Yeye, hukatai tena Anachoamuru na kukitawaza kwako. Unachotaka tu ni kumfuata, kutembea kando Yake katika kushoto ama kulia Kwake, kile utakacho ni kumkubali kama maisha yako ya pekee, kumkubali kama Bwana wako mmoja na wa pekee, Mungu wako mmoja na wa pekee.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji

427. Watu wanapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu, ufahamu wao wa kwanza kumhusu ni kwamba Yeye ni asiyeeleweka, ni mwenye hekima na wa ajabu na wanamcha bila kujua na kuihisi siri ya kazi Anayoifanya, ambayo inapita akili ya mwanadamu. Watu wanataka tu kuwa na uwezo wa kukidhi matakwa Yake, kuridhisha matamanio Yake; hawatamani kumpita Yeye, kwa sababu kazi anayoifanya inazidi fikira za mwanadamu na haiwezi kufanywa na mwanadamu kama mbadala. Hata mwanadamu mwenyewe hayajui mapungufu yake, wakati Amefungua njia mpya na kumleta mwanadamu katika dunia mpya zaidi na nzuri zaidi, kwamba mwanadamu amefanya maendeleo mapya na kuwa na mwanzo mpya. Kile ambacho watu wanahisi kumhusu Mungu, sio matamanio, au sio matamanio tu. Uzoefu wake wa kina ni kicho na upendo, hisia zake ni kwamba Mungu kweli ni wa ajabu sana. Anafanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya na kusema mambo ambayo mwanadamu hawezi kusema. Watu ambao wamepitia kazi ya Mungu daima wana hisia isiyoweza kuelezeka. Watu wenye uzoefu wa kina kutosha wanaweza kuelewa ukweli wa Mungu; wanaweza kuhisi uzuro Wake, kwamba kazi Yake ni ya hekima sana, ya ajabu sana, na hivyo hii inazalisha nguvu isiyokoma ndani yao. Si woga au upendo wa mara moja moja na heshima, bali hisia za ndani za upendo wa Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Hata hivyo, watu ambao wamepata uzoefu wa kuadibu na hukumu Yake wanamhisi kuwa Yeye mtukufu na asiyekosewa. Hata watu ambao wamepitia uzoefu mkubwa wa kazi Yake pia hawawezi kumwelewa; watu wote wanaomcha wanajua kwamba kazi Yake hailingani na fikira za watu lakini siku zote inakwenda kinyume na fikira zao. Haihitaji watu wamtamani kabisa au kuwa na kuonekana kwa kujikabidhi Kwake, badala yake anataka wawe na uchaji wa kweli na kutii kikamilifu. Katika nyingi ya kazi Yake, mtu yeyote mwenye uzoefu wa kweli anahisi heshima Kwake, ambayo ni ya juu kuliko matamanio. Watu wameiona tabia Yake kwa sababu ya kazi Yake ya kuadibu na hukumu, na kwa hiyo wanamcha mioyoni mwao. Mungu anapaswa kuchiwa na kutiiwa, kwa sababu uungu Wake na tabia Yake havifanani kama ule wa watu walioumbwa na vikuu juu ya vile vya watu walioumbwa. Mungu hategemei chochote kuwepo na ni wa milele, Yeye siye kiumbe Aliyeumbwa, na ni Mungu tu anayestahili uchaji na utiifu; mwanadamu hana sifa ya kupewa hivi. Hivyo, watu wote waliopitia uzoefu wa kazi Yake na kweli wanamjua wanampatia heshima. Hata hivyo, wale ambao hawaachani fikira zao kumhusu, yaani, wale ambao hawamwoni kuwa Mungu, hawana uchaji wowote Kwake, na hata ingawa wanamfuata hawajashindwa; ni watu wasiotii kwa asili yao. Anafanya kazi hii ili apate matokeo kwamba viumbe vyote vilivyoumbwa vinaweza kumcha Muumbaji, vimwabudu Yeye, na kujikabidhi katika utawala Wake bila masharti. Haya ni matokeo ya mwisho ambayo kazi Yake yote inalenga kuyapata. Ikiwa watu ambao wamepitia kazi hiyo hawamchi Mungu, hata kidogo, kama kutotii kwao kwa zamani hakutabadilika kabisa, basi watu hawa ni hakika wataondolewa. Kama mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu ni kumtamani au kuonyesha heshima kwa mbali na sio kumpenda, hata kidogo, hivi ndivyo mtu bila moyo wa kumpenda Mungu anapofikia, na mtu wa aina hiyo anakosa hali za kumwezesha kukamilishwa. Ikiwa kazi nyingi vile haiwezi kupata upendo wa kweli wa mtu, hii ina maana kwamba mtu huyo hajampata Mungu na kwa uhalisi hatafuti kuujua ukweli. Mtu ambaye hampendi Mungu hapendi ukweli na hivyo hawezi kumpata Mungu, sembuse kupata ukubali wa Mungu. Watu kama hao, bila kujali jinsi wanavyopata uzoefu wa Roho Mtakatifu, na bila kujali jinsi gani wanapitia uzoefu wa hukumu, bado hawawezi kumcha Mungu. Hawa ni watu ambao asili yao haiwezi kubadilishwa, ambao wana tabia ya uovu uliokithiri. Wale wote ambao hawamchi Mungu wataondolewa, na kuwa walengwa wa hukumu, na kuadhibiwa kama tu wale ambao wanafanya uovu, watateseka hata zaidi ya wale ambao wamefanya matendo maovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Iliyotangulia: G. Juu ya Jinsi ya Kutimiza Wajibu wa Mtu vya Kutosha

Inayofuata: I. Kuhusu Jinsi ya Kuchagua Njia ya Mtu katika Imani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp