227 Kupata Ukweli Kupitia Imani kwa Mungu Kuna Thamani Sana

1 Nilimwamini Mungu kwa miaka michache, nikifanya kazi kwa shauku na kushugulika kufanya kazi kwa bidii. Nilifikiria kuwa ningenyakuliwa hadi ufalme wa mbinguni, nizawadiwe na kubarikiwa. Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu nikaona jinsi nilivyopotoka sana. Mateso na juhudi zangu zimekuwa kwa ajili ya kupata baraka, zimekuwa mabadilishano na Mungu. Kila siku natenda dhambi na kisha nakiri, bado mara nyingi nadanganya na kujaribu kumdanganya Mungu. Nikiwa nimejawa na tabia ya kishetani, nitafaaje kuingia katika ufalme wa Mungu? Nikipitia hukumu ya Mungu, hatimaye nimeamshwa. Naelewa kuwa kupata ukweli na uzima ni jambo la muhimu zaidi katika imani. Kuanzia sasa kuendelea, sitawahi tena kupambana kwa jaili ya mustakabali na hatima yangu. Nimedhamiria kufuatilia ukweli na kuishi kulingana na maneno ya Mungu.

2 Ingawa nimepitia taabu nyingi, panda shuka nyingi katika imani yangu, maneno ya Mungu yameniongoza katika mapito ya majaribu. Ingawa nimeteseka katika mwili, tabia yangu ya kishetani imebadilika. Mimi si mwenye kiburi ama muasi tena, sasa mimi ni mtiifu kwa Mungu. Kwa kupitia kazi ya Mungu, nimeelewa ukweli mwingi. Nimeona wazi kuwa Shetani ndiye kiini cha uovu duniani. Joka kuu jekundu linawatesa watu wateule wa Mungu, ni adui wa Mungu. Namchukia Shetani sana, nitaliacha kabisa joka kuu jekundu. Nina furaha kuacha kila kitu, nimeamua kwa uthabiti kumfuata Kristo. Kwa kutimiza wajibu wangu na kupata ukweli, maisha haya hayaishiwi bure.

Iliyotangulia: 226 Kile Ambacho Waumini Katika Mungu Wanapaswa Kutafuta

Inayofuata: 228 Yaliyopita Yananichoma Kama Upanga

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

137 Nitampenda Mungu Milele

1Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako.Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki