Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Mamlaka ya Mungu (I)

Ushirika Wangu kadhaa uliopita ulikuwa unahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kusikia ushirika huo, je, unahisi kwamba umepata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Je, umepata kiwango gani cha ufahamu na maarifa? Je, unaweza kuweka nambari kwenye kiwango hicho? Je, ushirika huo ulikupa ufahamu wa kina zaidi kuhusu Mungu? Je, inaweza kusemwa kwamba ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Je, inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya kiini chote cha Mungu, na kila kitu ambacho Anacho na Alicho? Hapana, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hiyo ni kwa sababu ushirika huo ulitoa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile ambacho Anacho na Alicho—na wala si kila kitu, au yote kwa ukamilifu. Ushirika huo ulikuwezesha kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu hapo awali; na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile ambacho Anacho na Alicho, pamoja na mbinu na fikira zilizo nyuma ya kila kitu Alichokifanya. Hata hivyo huu ni ufahamu halisi, unaozungumzwa wa Mungu, na, katika mioyo yenu, mnabakia bila uhakika kuhusu ni mangapi kwa hayo ni kweli. Ni nini hasa huamua ikiwa kuna uhalisia wowote katika uelewa wa watu kwa mambo kama hayo? Inaamuliwa na kiwango cha maneno ya Mungu na tabia ya Mungu ambayo wamepitia kwa kweli wakati wa uzoefu wao halisi, na ni kwa kiwango gani wameweza kuona na kujua wakati wa matukio hayo halisi. Je, kuna yeyote aliyesema maneno kama haya: “Ushirika kadhaa uliopita ulituruhusu kuelewa mambo yaliyofanywa na Mungu, fikira za Mungu, na, zaidi ya hayo, mtazamo wa Mungu kwa wanadamu na msingi wa matendo Yake, pamoja na kanuni za vitendo Vyake. Na kwa hivyo tumekuja kuelewa tabia ya Mungu, na tumejua ukamilifu wa Mungu?” Je, ni sahihi kusema hivi? Kwa kweli ni wazi kwamba si sahihi. Na kwa nini Nasema kwamba si sahihi? Tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho, vyote vinaonyeshwa katika mambo ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ametamka. Binadamu anaweza kuelewa kile Anacho na alicho kupitia kwa kazi ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye amenena, lakini hii ni kusema tu kwamba ile kazi na maneno humwezesha binadamu kuelewa sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya kile Anacho na alicho. Kama binadamu atataka kufaidi ufahamu mwingi zaidi na ulio wazi kuhusu Mungu, basi binadamu lazima apitie maneno na kazi nyingi zaidi za Mungu. Ingawa binadamu hufaidi tu ufahamu kiasi wa Mungu wakati anapokuwa akipitia sehemu ya maneno au kazi ya Mungu, je, ufahamu huu wa kiasi unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu? Je, unawakilisha kiini cha Mungu? Bila shaka unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu, na kiini cha Mungu; hapo hapana shaka. Haijalishi ni lini au wapi, au ni kwa njia gani ambayo Mungu hufanya kazi Yake, au ni umbo gani ambalo humwonekania binadamu, au ni kwa njia gani Anaonyesha mapenzi Yake, kila kitu Anachofichua na kuonyesha kinamwakilisha Mungu Mwenyewe, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho. Mungu hutekeleza kazi Yake na kile Anacho na alicho, na katika utambulisho Wake wa kweli; Huu ni ukweli kabisa. Hata hivyo, leo, watu wanao ufahamu kiasi tu wa Mungu kupitia maneno Yake, na kupitia kile wanachosikia wanaposikiliza mahubiri, na kwa hivyo hadi kufikia kiwango fulani, ufahamu huu unaweza kusemwa tu kuwa maarifa ya kinadharia. Kwa kuzingatia hali zenu halisi, mnaweza kuthibitisha tu ufahamu au maarifa ya Mungu ambayo mmesikia, kuona, au kujua na kuelewa katika mioyo yenu leo kama kila mmoja wenu atapitia haya katika uzoefu wake halisi, na kuja kuyajua kidogokidogo. Kama Nisingeshiriki maneno haya na wewe, je, ungeweza kutimiza maarifa ya kweli ya Mungu kupitia uzoefu wako pekee? Kufanya hivyo, Naogopa, kunaweza kuwa vigumu sana. Hiyo ni kwa sababu lazima watu wawe kwanza na maneno ya Mungu ili kujua namna ya kuyapitia. Hata hivyo wingi wa maneno ya Mungu ambayo watu hushiriki, hicho ndicho kiwango wanachoweza kupata uzoefu. Maneno ya Mungu huongoza njia iliyo mbele, na humpa binadamu mwongozo katika yale yote anayoyapitia. Kwa ufupi, kwa wale ambao kwa kiasi fulani wana uzoefu halisi, ushirika kadhaa uliopita utawasaidia kufikia ufahamu wa kina wa ukweli, na maarifa ya kweli zaidi kumhusu Mungu. Lakini kwa wale ambao hawana uzoefu wowote wa kweli, au wale ambao wameanza tu uzoefu wao, au walioanza tu kugusia juu ya uhalisia, huu ni mtihani mkubwa.

Maudhui muhimu katika ushirika kadhaa uliopita yalihusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.” Ni nini ulichoona kwenye sehemu zile muhimu na kuu kati ya kila kitu Nilichoongea? Kupitia kwenye ushirika huo, je, unaweza kutambua kwamba Yule aliyefanya kazi, na Akaweza kufichua tabia hizi, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye na ukuu juu ya mambo yote? Kama jibu lako ni ndiyo, basi ni nini kinachokuongoza katika hitimisho kama hilo? Katika kufikia hitimisho hili, ulizingatia vipengele vingapi? Je, kuna yeyote anayeweza kuniambia Mimi? Ninajua kwamba ushirika kadhaa uliopita uliwaathiri kwa kina, na uliwapa mwanzo mpya mioyoni mwenu kwa maarifa yenu ya Mungu, jambo ambalo ni kubwa. Lakini ingawa umeweza kupiga hatua kubwa katika ufahamu wako wa Mungu ikilinganishwa na hapo awali, ufafanuzi wako wa utambulisho wa Mungu bado haujasonga mbelezaidi ya majina ya Yehova Mungu wa Enzi ya Sheria, Bwana Yesu wa Enzi ya Neema, na Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme. Hivi ni kusema kwamba, Ingawa ushirika huo kuhusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” uliweza kukupa ufahamu fulani wa maneno yaliyowahi kuzungumzwa na Mungu, na kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na uwepo na vinavyomilikiwa vilivyowahi kufichuliwa na Mungu, huwezi kutoa ufafanuzi wa ukweli na mtazamo sahihi wa neno “Mungu.” Na wala huna mtazamo na maarifa ya kweli na sahihi ya hadhi na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, ambayo ni kusema, hadhi ya Mungu miongoni mwa vitu vyote na katika ulimwengu mzima. Hii ni kwa sababu, kwenye ushirika wa awali kuhusu Mungu Mwenyewe na tabia ya Mungu, maudhui yote yalitokana na matamshi na ufunuo mbalimbali wa awali kuhusu Mungu uliorekodiwa kwenye Biblia. Hata hivyo ni vigumu kwa binadamu kugundua nafsi na miliki ambazo zimefichuliwa na kuonyeshwa na Mungu wakati wa, au nje ya, usimamizi na wokovu Wake kwa mwanadamu. Kwa hivyo, hata kama utaelewa nafsi na miliki za Mungu ambazo zilifichuliwa kwenye kazi Aliyowahi kufanya, ufafanuzi wako wa utambulisho na hadhi ya Mungu ungali mbali sana na ule wa Mungu wa kipekee, Yule anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote, na ni tofauti na ule wa Muumba. Kupitia kwa ushirika kadhaa uliopita, kila mtu ana hisia hii: Watu wangewezaje kujua fikira za Mungu? Kama kweli mtu angejua, basi mtu huyo bila shaka angekuwa Mungu, kwa maana Mungu Mwenyewe ndiye anayejua fikira Zake, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anayejua msingi na mtazamo wa kila kitu Anachofanya. Inaonekana kuwa ni jambo la busara na lenye mantiki kwako wewe kutambua utambulisho wa Mungu kwa njia kama hiyo, lakini ni nani anayeweza kujua kutoka kwenye tabia na kazi ya Mungu kwamba kwa kweli hii ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na wala si kazi ya binadamu, kazi ambayo haiwezi kufanywa kwa niaba ya Mungu na binadamu? Ni nani anayeweza kuona kwamba kazi hii iko chini ya ukuu wa Yule aliye na kiini na nguvu za Mungu? Hii ni kusema kwamba, ni kupitia kwa tabia gani au kiini gani ndipo unapotambua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, aliye na utambulisho wa Mungu, na ni Yule anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote? Je, umewahi kufikiria kuhusu hilo? Ikiwa hujawahi kufanya hivyo, basi hii inathibitisha ukweli mmoja: Ushirika kadhaa uliopita umeweza kukupa tu ufahamu fulani wa sehemu ya historia ambapo Mungu alifanya kazi Yake, na mbinu, udhihirisho, na ufunuo wa Mungu kwenye kipindi cha kufanyika kwa kazi hiyo. Ingawa ufahamu kama huo unamfanya kila mmoja wenu atambue bila shaka kwamba Aliyetekeleza hatua hizi mbili za kazi ni Mungu Mwenyewe ambaye mnamwamini na kumfuata, na Yule ambaye ni lazima kumfuata daima, lakini bado hamna uwezo wa kutambua kwamba Yeye ndiye Mungu ambaye amekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na Atakayeendelea kuwepo milele na milele, na wala huwezi kutambua kwamba Yeye ndiye Anayeongoza na Anayeshikilia utawala juu ya wanadamu wote. Kwa kweli hujawahi kufikiria kuhusu tatizo hili. Awe ni Yehova au Bwana Yesu, ni kupitia kwa vipengele vipi vya kiini na maonyesho ndipo unaweza kutambua kwamba Yeye si Mungu tu ambaye unapaswa kumfuata, bali pia Ndiye anayewaamuru wanadamu na kushikilia ukuu juu ya hatima ya wanadamu, ambaye, vilevile, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee anayeshikilia ukuu juu ya mbingu na dunia na vitu vyote? Je, unatambua kupitia njia zipi kwamba Yule unayemwamini na kumfuata ni Mungu Mwenyewe ambaye ana ukuu juu ya vitu vyote? Ni kupitia kwa njia zipi ndipo unapomuunganisha Mungu unayemwamini na Mungu anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya wanadamu? Ni nini kinachokuruhusu kutambua kwamba Mungu unayemsadiki ndiye yule Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye mbinguni na duniani, na miongoni mwa vitu vyote? Hili ndilo tatizo ambalo Nitalitatua katika sehemu inayofuata.

Matatizo ambayo hujawahi kuyafikiria au ambayo huwezi kuyafikiria, ndiyo hayo ambayo yanaweza kuwa ya muhimu zaidi katika kumjua Mungu, na ambayo kwayo unaweza kutafuta ukweli usioweza kueleweka kwa mwanadamu. Wakati matatizo haya yanapokukumba, kiasi kwamba unatakiwa kuyakabili, na unahitajika kufanya uamuzi, ikiwa hutaweza kuyatatua kikamilifu kwa sababu ya upumbavu na ujinga wako, au kwa sababu uzoefu wako ni wa juujuu sana na unakosa maarifa ya kweli ya Mungu, basi yatakuwa kizuizi kikubwa zaidi na changamoto kubwa zaidi kwenye njia yako ya kumsadiki Mungu. Na kwa hivyo Nahisi kwamba ni muhimu sana kushiriki pamoja nanyi mada hii. Je, unajua tatizo lako ni nini sasa? Je, unatambua matatizo Ninayoyazungumzia? Je, matatizo haya ndiyo utakayokabiliana nayo? Je, haya ndiyo matatizo usiyoyaelewa? Je, haya ni matatizo ambayo hayajawahi kukutokea? Je, matatizo haya ni muhimu kwako? Je, ni matatizo kweli? Suala hili ni chanzo cha mkanganyiko mkubwa kwenu, ambalo linaonyesha kwamba hamna ufahamu wa kweli wa Mungu mnayemwamini, na kwamba hamumchukulii Yeye kwa umakinifu. Baadhi ya watu husema, “Ninajua Yeye ni Mungu, na kwa hivyo ninamfuata Yeye kwa sababu maneno Yake ni maonyesho ya Mungu. Hiyo inatosha. Ni uthibitisho gani mwingine unahitajika? Je, tunahitaji kuibua mashaka juu ya Mungu? Je, tunahitaji kumjaribu Mungu? Je, tunahitaji kuhoji kiini cha Mungu na utambulisho wa Mungu Mwenyewe?” Bila kujali kama unafikiria kwa njia hii, huwa Siyaulizi maswali kama haya ili kukufanya uchanganyikiwe kuhusu Mungu, au kukufanya umjaribu Mungu, sembuse kukupa mashaka kuhusu utambulisho na kiini cha Mungu. Badala yake, Ninafanya hivi ili kuhimiza ndani yenu ufahamu mkubwa zaidi wa kiini cha Mungu, na uhakika na imani kubwa zaidi kuhusu hadhi ya Mungu, ili Mungu awe Ndiye wa pekee katika mioyo ya wale wote wanaomfuata Mungu, na ili ile hadhi ya asili ya Mungu—kama Muumba, Mtawala wa vitu vyote, Mungu Mwenyewe wa kipekee—iweze kurejeshwa katika mioyo ya kila kiumbe. Hii pia ndiyo mada itakayohusu ushirika wetu.

Sasa, hebu na tuanze kusoma maandiko yafuatayo kutoka kwenye Biblia.

1. Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza.

Mwa 1:6-7 Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:9-11 Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane; na kukawa vivyo hivyo. Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema. Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:14-15 Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile.

Mwa 1:20-21 Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri.

Mwa 1:24-25 Naye Mungu akasema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.

Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu

Hebu tuangalie kifungu cha kwanza: “Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza” (Mwa 1:3-5). Kifungu hiki kinafafanua kitendo cha kwanza cha Mungu wakati wa kuanza uumbaji, na siku ya kwanza ambayo Mungu aliipitisha ambapo kulikuwa na jioni na asubuhi. Lakini ilikuwa siku ya kipekee: Mungu alianza kutayarisha nuru kwa vitu vyote, na, zaidi ya hayo, Alitenganisha nuru na giza. Katika siku hii, Mungu alianza kunena, na matamshi na mamlaka Yake vyote vilikuwa pamoja. Mamlaka Yake yalianza kujitokeza miongoni mwa vitu vyote, na nguvu Zake zikaenea miongoni mwa vitu vyote kutokana na maneno Yake. Kuanzia siku hii na kuendelea, vitu vyote viliumbwa na vikawa thabiti kwa sababu ya maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu, na vikaanza kufanya kazi kwa msaada wa maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu. Wakati Mungu aliposema maneno haya “Na kuwe na mwanga,” kulikuwepo na nuru. Mungu hakuanza kushughulikia shughuli yoyote; nuru ilikuwa imeonekana kama matokeo ya maneno Yake. Hii ilikuwa nuru ambayo Mungu aliita mchana, na ambayo binadamu angali anaitegemea kwa minajili ya kuwepo kwake leo. Kwa amri ya Mungu, kiini na thamani yake havijawahi kubadilika na havijawahi kutoweka. Uwepo wake unaonyesha mamlaka na nguvu za Mungu, na unatangaza uwepo wa Mungu, na unathibitisha, tena na tena, utambulisho na hadhi ya Muumba. Siyo isiyoonekana, au isiyo halisi, lakini ni nuru halisi inayoweza kuonekana na binadamu. Tangu wakati huo na kuendelea, kwenye ulimwengu huu mtupu ambao “nchi ilikuwa yenye ukiwa tena tupu, na giza lilikuwajuu ya uso wa vilindi vya maji,” hapo kuliumbwa kitu cha kwanza kinachoonekana. Kitu hiki kilitokana na maneno ya kinywa cha Mungu na kikaonekana kwenye tukio la kwanza la kuumbwa kwa vitu vyote kwa sababu ya mamlaka na matamshi ya Mungu. Muda mfupi baadaye, Mungu aliamuru nuru na giza kutengana…. Kila kitu kilibadilika na kilikamilishwa kwa sababu ya maneno ya Mungu…. Mungu akaiita nuru hii “Mchana,” na giza hili Akaliita “Usiku.” Kuanzia wakati huo, jioni ya kwanza na asubuhi ya kwanza ziliweza kuumbwa katika ulimwengu ambao Mungu alinuia kuumba, na Mungu akasema hii ndiyo iliyokuwa siku ya kwanza. Siku hii ilikuwa siku ya kwanza ya uumbaji wa Muumba wa vitu vyote, na ilikuwa mwanzo wa uumbaji wa vitu vyote, na ilikuwa ndio mara ya kwanza ambapo mamlaka na uwezo wa Muumba ulikuwa umeonyeshwa katika ulimwengu huu ambao Alikuwa ameuumba.

Kupitia kwa maneno haya, binadamu anaweza kuona mamlaka ya Mungu, na mamlaka ya maneno ya Mungu, na nguvu za Mungu. Kwa sababu ni Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na kwa hivyo ni Mungu pekee ndiye aliye na mamlaka haya, na kwa sababu Mungu ndiye anayemiliki mamlaka kama hayo, kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na nguvu kama hizo. Je, kuna mtu yeyote au kitu chochote kinachoweza kumiliki mamlaka na nguvu kama hizi? Je, kunalo jibu katika moyo wako? Mbali na Mungu, je, kuna kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki mamlaka kama hayo? Je, umewahi kuona mfano wa kitu kama hicho kwenye vitabu vingine vyovyote au machapisho? Je, kuna rekodi yoyote kwamba kuna mtu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote? Jambo hili halionekani katika vitabu au rekodi nyingine zozote; haya ndiyo, bila shaka, maneno ya kipekee yenye mamlaka na nguvu kuhusu uumbaji mkuu wa Mungu wa ulimwengu, yaliyorekodiwa kwenye Biblia, na maneno haya yanazungumzia mamlaka ya kipekee ya Mungu, na utambulisho wa kipekee wa Mungu. Je, mamlaka na nguvu kama hizi zinaweza kusemwa kuwa zinaashiria utambulisho wa kipekee wa Mungu? Je, yanaweza kusemwa yanamilikiwa na Mungu, na Mungu pekee? Bila shaka, Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizi! Mamlaka na nguvu hizi vyote haviwezi kumilikiwa au kubadilishwa na kiumbe chochote kingine kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa! Je, hii ni mojawapo ya sifa za Mungu Mwenyewe wa kipekee? Je, umewahi kuishuhudia? Maneno haya yanaruhusu watu kuelewa kwa haraka na kwa uwazikweli kwamba Mungu anamiliki mamlaka ya kipekee, na nguvu za kipekee, na Anamiliki utambulisho na hadhi ya juu kabisa. Kutokana na ushirika wa hapa juu, je, unaweza kusema kwamba Mungu unayemwamini ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee?

Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Anga, na Nafasi za Mahitaji ya Kuishi kwa Kimsingi Zaidi kwa Binadamu Kuonekana

Hebu na tusome kifungu cha pili cha Biblia: “Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo” (Mwa 1:6-7). Ni mabadiliko gani yaliyofanyika baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji”? Maandiko yanasema: “Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu.” Ni nini kilichokuwa matokeo baada ya Mungu kutamka hivi na kufanya hivyo? Jibu linapatikana kwenye sehemu ya mwisho ya kifungu hiki: “na kukawa vivyo hivyo.”

Sentensi hizi mbili zilizo fupi zinarekodi tukio adhimu, na zinaelezea tukio la kustaajabisha—kazi kubwa ambayo kwayo Mungu aliyatenga maji, na kuunda nafasi ambayo mwanadamu angeweza kuishi …

Katika picha hii, maji na anga vinaonekana mbele ya macho ya Mungu papo hapo, na vyote vinagawanywa kwa mamlaka ya matamshi ya Mungu, na kugawanywa kwa sehemu ya juu na ya chini kwa njia ambayo iliteuliwa na Mungu. Hivi ni kusema, anga iliyoumbwa na Mungu haikufunika tu maji yaliyo chini, lakini pia ilishikilia maji yaliyo juu…. Katika haya, binadamu hawezi kufanya chochote ila kutazama, kupigwa na butwaa, na kushusha pumzi yake kwa kuvutiwa na maajabu ya onyesho hilo ambalo Muumba aliyahamisha maji, na kuyaamuru maji, na kuumba anga, na yote haya Alifanya kupitia kwa nguvu za mamlaka Yake. Kupitia kwa matamshi ya Mungu, na nguvu za Mungu, na mamlaka ya Mungu, Mungu aliweza kutimiza tendo jingine kubwa. Je, hizi si nguvu za mamlaka ya Muumba? Hebu na tutumie maandiko haya katika kufafanua matendo ya Mungu: Mungu aliyatamka matamshi Yake na kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu kulikuwa na anga katikati ya maji. Wakati uo huo, badiliko kubwa sana lilitokea kwenye nafasi hii kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu, na halikuwa badiliko katika hali ya kawaida, lakini aina fulani ya mbadala ambao kitu kisichokuwepo kiligeuka na kuwa kitu kilichopo. Yote haya yalizaliwa kwenye fikira za Muumba, na yakawa kitu kilichopo kutoka kwenye kitu kisichokuwepo kwa sababu ya matamshi yaliyotamkwa na Muumba, na, vilevile, kuanzia wakati huo na kuendelea yangekuwepo na kuwa imara, kwa minajili ya Muumba, na yangesonga, kubadilika, na kufanywa upya kulingana na fikira za Muumba. Kifungu hiki kinaelezea tendo la pili la Muumba katika uumbaji Wake wa ulimwengu wote. Ilikuwa ni onyesho jingine la mamlaka na nguvu za Muumba, na pia ni uumbaji mwingine wa Muumba. Siku hii ndio iliyokuwa siku ya pili ambayo Muumba alikuwa ameipitia tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, na ilikuwa ni siku nyingine ya ajabu Kwake: Alitembea katika nuru, Alileta anga, Aliyapangilia na kuyadhibitimaji, na vitendo Vyake, mamlaka Yake, na nguvu Zake vyote viliweza kuanza kazi kwenye siku hiyo mpya …

Je, kulikuwepo na anga katikati ya maji kabla ya Mungu kutamka matamshi Yake? Bila shaka la! Na je, baada ya Mungu kusema “Na liwe anga katikati ya maji”? Vitu vilivyokusudiwa na Mungu vilionekana; palikuwa na anga katikati ya maji, na maji yakatengana kwa sababu Mungu alisema, "na likayatenge maji na maji." Kwa njia hii, kufuatia maneno ya Mungu, vitu viwili vipya, vitu vipya viwili vilivyozaliwa vilionekana miongoni mwa vitu vyote kama matokeo ya mamlaka na nguvu za Mungu. Je, unajisikiaje kuhusu kuonekana kwa vitu hivi viwili vipya? Je, unahisi ukuu wa uwezo wa Muumba? Je, unahisiile nguvu ya kipekee na isiyo ya kawaida ya Muumba? Ukubwa wa msukumo na nguvu kama hizo zinatokana na mamlaka ya Mungu na mamlaka haya ni kiwakilishi cha Mungu Mwenyewe, na sifa ya kipekee ya Mungu Mwenyewe.

Je, kifungu hiki kimekupa hisia nyingine ya kina zaidi kuhusu upekee wa Mungu? Lakini haya ni machache tu kati ya mengi; mamlaka na nguvu za Muumba vinazidi haya yote. Upekee wake hauko hivyo tu kwa sababu Anamiliki asili tofauti na ile ya kiumbe chochote, bali pia ni kwa sababu mamlaka na nguvu Zake ni zisizo za kawaida, zisizo na mipaka, ni kuu juu ya yote, na zinasimama juu ya vitu vyote, na vilevile, kwa sababu mamlaka Yake na kile Anacho na alicho kinaweza kuumba maisha, na kufanya miujiza, na Anaweza kuumba yaliyo ya kustaajabisha na yasiyo ya kawaida kwa kila dakika na sekunde, na wakati uo huo, Anaweza kutawala maisha Anayoyaumba na kushikilia ukuu Wake juu ya miujiza na kila mojawapo ya dakika na sekunde Anazoumba.

Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha

Sasa, hebu na tusome sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:9-11: “Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike pahali pamoja, ili ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili ardhi kavu ionekane”? Ni nini kingine kilichotokea katika nafasi hii mbali na nuru na anga? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji Akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na nchi kavu na bahari katika nafasi hii, nayo nchi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na ikawa hivyo.” Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alikamilisha haya yote, na Aliumba haya yote kwa maneno Yake.

Katika vifungu vitatu hapo juu, tumejifunza juu ya kutokea kwa matukio makubwa matatu. Matukio haya matatu makubwa yalionekana, na yakaja kuwepo, kupitia kwa matamshi ya Mungu, na ni kwa sababu ya matamshi Yake ndipo, matukio haya moja baada ya jingine, yaliweza kujitokeza mbele ya macho ya Mungu. Kwa hivyo inaweza kuonekana kwamba maneno haya: “Mungu hunena, na ikatimizwa; Yeye huamuru, na ikawa” haya si maneno matupu. Kiini hiki cha Mungu kinathibitishwa wakati ule ambao fikira Zake zinatungwa, na wakati ambapo Mungu anafungua kinywa Chake kunena, kiini Chake kinajionyesha kikamilifu.

Hebu na tuendelee hadi kwenye sentensi ya mwisho ya fungu hili: “Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.” Wakati Mungu alipokuwa anazungumza, kila kitu kilifanyika kulingana na mawazo ya Mungu, na papo hapo, aina mbalimbali za viumbe vidogo vidogo vilaini vyenye uhai vilikuwa vinachomoza vichwa vyao kwa kuyumba-yumba juu ya udongo, na hata kabla havijakung’uta chembechembe za uchafu kutoka kwenye miili yao vilikuwa vikipungiana kwa shauku katika kusalimiana, vitikisa vichwa vyao na kuufurahia ulimwengu. Vilimshukuru Muumba kwa uhai Aliowapa, na kuutangazia ulimwengu kwamba vilikuwa ni sehemu ya vitu vyote, na kwamba kila kimoja kingejitolea uhai wake ili kuonyesha mamlaka ya Muumba. Wakati maneno ya Mungu yaliponenwa, nchi ilisitawi na kuwa ya kijani kibichi , aina zote za miti ambayo ingeweza kufurahiwa na binadamu iliweza kuota na kuchipuka kutoka kwenye ardhi, na milima na nchi tambarare vyote vikawa na idadi kubwa ya miti na misitu…. Ulimwengu huu uliokuwa jangwa, ambao haukuwa na dalili yoyote ya uhai, ulifunikwa kwa kasi na wingi wa nyasi, mimea na miti na kuenea kwa kijani kibichi…. Harufu ya nyasi na harufu ya udongo ilienea kwa njia ya hewa, na safu za mimea zilianza kupumua kulingana na mzunguko wa hewa, na vikaanza pia mchakato wa kukua. Wakati uo huo, kutokana na maneno ya Mungu na kufuatia fikira za Mungu, mimea yote ilianza mizunguko isiyoisha ya maisha ambapo inakua, inachanua, inazaa matunda na kuzaana na kuongezeka. Ilianza kutii kwa umakinifu mikondo yao husika ya maisha na kuanza kutekeleza wajibu wao husika miongoni mwa viumbe vyote…. Yote ilichipuka na kuishi, kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Zingepokea utoaji na utunzaji usikoma wa Muumba, na daima zingedumu kwa ushupavu katika kila pembe ya nchi ili kuonyesha mamlaka na nguvu za Muumba, na daima zingeonyesha nguvu za uhai walizopewa na Muumba …

Maisha ya Muumba ni ya ajabu, fikira Zake ni za ajabu, na mamlaka Yake ni ya ajabu, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapotenda; Anatumia tu fikira Zake kuamuru na maneno Yake kupangilia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yalitimizwa kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.

Wakati Akiwa bado hajaanza kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake, na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika vitu vyote yalianza kutokea shukrani kwa mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali jinsi Mungu alivyofanya, au jinsi Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na dunia kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na pia yalionyesha ajabu na ukuu wa nguvu za maisha ya Muumba. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, bali ni mamlaka kuu na yenye nguvu isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha vitu vyote kubadilishwa, kuhuishwa, kufanywa upya na kupotea. Kwa sababu ya haya, vitu vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywani Mwake …

Kabla ya vitu vyote kuonekana, katika mawazo ya Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawa kwenye siku ya tatu kila aina ya mimea ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kitu kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na Angetumia mamlaka Yake na kuonyesha nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga kutayarisha kwa ajili ya vitu vyote na wanadamu Ambao Alikusudia kuwaumba. …

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya MwanadamuVilikuja Kuwepo Mungu Alipotumia Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulionekana mbele za macho Yake, na, sehemu kwa sehemu, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu. Kuonekana kwa kila kitu kipya kulikuwa sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga, na Muumba alifurahia sana picha hii ambayo iliwahi kuwa kwenye fikira Zake, lakini ambayo sasa ilikuwa imepewa uhai. Kwa wakati huu, moyo Wake uliweza kuridhika kidogo, lakini mpango Wake ulikuwa ndio umeanza tu. Kufumba na kufumbua, siku mpya ilikuwa imewadia—na je, ni ukurasa gani uliofuata katika mpango wa Muumba? Ni nini Alichosema? Na Aliwezaje kuonyesha mamlaka Yake? Na, wakati uo huo, ni mambo yapi mapya yaliyokuja kwenye ulimwengu huu mpya? Kufuatia mwongozo wa Muumba, matazamio yetu yanaangukia katika siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, siku ambayo ilikuwa ni mwanzo mwingine mpya. Bila shaka, kwa Muumba, ilikuwa ni siku nyingine ya ajabu kwa hakika, na siku nyingine yenye umuhimu mkubwa kwa wanadamu wa leo. Ilikuwa, bila shaka, siku yenye thamani isiyopimika. Je, ni kwa jinsi gani ilikuwa ya ajabu, ni kwa jinsi gani ilikuwa ya muhimu sana, na ni kwa jinsi gani ilikuwa yenye thamani isiyopimika? Hebu kwanza tusikilize maneno yaliyosemwa na Muumba….

“Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile” (Mwa 1:14-15). Haya yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka ya Mungu yaliyoonyeshwa kwa viumbe kufuatia uumbaji Wake wa nchi kavu na mimea iliyokuwa juu yake. Kwa Mungu, kitendo kama hicho kilikuwa tu rahisi kama kile Alichokuwa tayari Amefanya, kwa sababu Mungu ana nguvu kama hizo; Mungu ni mmwema kama vile tu neno Lake lilivyo, na neno Lake litatimizwa. Mungu aliamuru mwanga uonekane mbinguni, na mwanga huu haukuangaza tu angani na juu ya nchi, bali pia zilihudumu kama ishara za mchana na usiku, kwa minajili ya misimu, siku, na miaka. Kwa njia hii, kama vile Mungu alivyoongea kwa matamshi Yake, kila kitendo ambacho Mungu alipenda kutimiza kilitimizwa kulingana na mapenzi ya Mungu na kwa njia iliyoteuliwa na Mungu.

Mwanga kwenye mbingu ni kitu kilicho kwenye mbingu kinachoweza kuangaza nuru; vinaweza kuangazia mbingu, na vinaweza kuangazia ardhi na bahari. Vinazunguka kulingana na mifuatano maalum na kulingana na idadi maalum ya mizunguko ambayo imeamriwa na Mungu, na vinaangaza katika vipindi tofauti vya wakati juu ya ardhi, na kwa njia hii mizunguko ya mianga hii husababisha mchana na usiku kujitokeza upande wa mashariki na magharibi mwa nchi, na wala si tu ishara za usiku na mchana, lakini kupitia kwa mizunguko hii tofauti inaweza kuadhimisha pia siku kuu na siku mbalimbali maalum za mwanadamu. Ndizo ambazo zinakamilisha kikamilifu na kuambatana na misimu minne—masika, kiangazi, vuli,, na kipupwe—iliyotolewa na Mungu, pamoja na vile ambavyo mianga hii hutumika kama viashiria vya mara kwa mara na sahihi kwa ajili ya majira, siku, na miaka ya mwanadamu. Ingawa ilikuwa baada tu ya mwanzo wa kilimo ndipo mwanadamu alipoanza kuelewa na kukumbana na utofautishaji wa vipimo vya muda, siku, na miaka iliyosababishwa na nuru hizi zilizoumbwa na Mungu, kwa hakika, vipindi vya muda, siku, na miaka ambavyo binadamu anaelewa leo vilianza kutolewa kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa viumbe vyote na Mungu, na vilevile ndivyo ilivyokuwa kwenye mizunguko inayobadilishana ya mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe ambavyo binadamu anapitia na vinaanza kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Nuru zile zilizoumbwa na Mungu zilimwezesha binadamu kuweza kutofautisha mara kwa mara, kwa hakika, na waziwazi usiku na mchana, na kuhesabu siku, na kuweza kufuatilia waziwazi vipindi vile vya muda na miaka. (Siku ya mwezi mzima ilikuwa kukamilika kwa mwezi mmoja, na kutokana na haya binadamu alijua kwamba kule kuangazia kwa nuru kulianzisha mzunguko mpya; siku ile ya nusu mwezi ilikuwa ni kukamilika kwa nusu moja ya mwezi, jambo ambalo lilimfahamisha binadamu kwamba kipindi kipya cha muda kilikuwa kimeanza, ambapo binadamu angeweza kujua ni mchana na usiku ngapi vilikuwa kwenye kipindi cha muda, na ni vipindi vingapi vya muda vilikuwa kwenye msimu, na ni misimu mingapi ilikuwa kwenye mwaka, na vyote hivi vilionyeshwa mara kwa mara.) Kwa hivyo, binadamu angeweza kufuatilia kwa urahisi vipindi vya muda, siku, na miaka iliyowekewa alama na mizunguko ya nuru hizo. Kuanzia sasa kusonga mbele, mwanadamu na viumbe vyote viliishi bila kufahamu miongoni mwa mabadiliko yenye mpangilio ya usiku na mchana na kubadilishwa kwa misimu iliyotokana na mizunguko ya nuru. Huu ndio ulikuwa muhimu wa uumbaji wa Muumba wa nuru kwenye siku ya nne. Vilevile, nia na umuhimu wa hatua hii ya Muumba vilikuwa bado haviwezi kutenganishwa na mamlaka na nguvu Zake. Na kwa hivyo, nuru zilizoumbwa na Mungu na thamani ambayo zingeleta hivi karibuni kwa binadamu ilikuwa ni mafanikio mengine katika uonyeshaji wa mamlaka ya Muumba.

Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha jioni na asubuhi, ile anga, ardhi na bahari, nyasi, mimea na aina mbalimbali za miti, na nuru, misimu, siku, na miaka kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kitu kipya Alichokiumba, na maneno Yake na mafanikio Yake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu hata kidogo, na bila ya kuchelewa hata kidogo. Kuonekana na kuzaliwa kwa vitu hivi vyote vipya kulikuwa uthibitisho wa mamlaka na nguvu za Muumba: Anamaanisha kile Anachosema, na kile Anachosema kitatimizwa, na kile ambacho kinatimizwa kitadumu milele. Ukweli huu haujawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa zamani, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa milele yote. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu matendo ya Muumba yamechochea mioyo yenu na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.

Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza, na Anavutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kujizuia ila kutazama kwa butwaa matendo haya ya kustaajabisha yanayotokana na matumizi ya mamlaka Yake. Nguvu zake za ajabu huleta furaha baada ya furaha, na mwanadamu anaachwa akishangaa na kufurahi sana, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; zaidi ya hayo, mwanadamu anaonekana kuguswa, na kunazalishwa ndani yake heshima, hofu, na mshikamano. Mamlaka na matendo ya Muumba yana athari kubwa katika roho ya mwanadamu, na yanatakasa roho ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, yanatosheleza roho ya mwanadamu. Kila moja ya mawazo Yake, kila moja ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kazi bora kati ya vitu vyote, na ni utekelezaji mkuu unaostahili zaidi ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu aliyeumbwa. Tunapohesabu kila kiumbe kilichozaliwa kutokana na matamshi ya Muumba, roho zetu zinavutiwa kwa maajabu ya nguvu za Mungu, na tunajipata tukifuata nyayo za Muumba hadi kwenye siku inayofuata: siku ya tano ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote.

Hebu tuendelee kusoma Maandiko kifungu kwa kifungu, tunapoangalia vitendo vingi zaidi vya Muumba.

Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Mbali na Tofauti Yalionyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti

Maandiko yanasema, “Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri” (Mwa 1:20-21). Maandiko yanatwambia waziwazi kwamba, kwenye siku hii, Mungu aliumba viumbe vya majini na ndege wa angani, hivi ni kusema kwamba Aliwaumba samaki na ndege mbalimbali, na akawaainisha kila mmoja wao kulingana na aina. Kwa njia hii, ardhi, mbingu, na maji vyote vilitajirishwa na uumbaji wa Mungu …

Maneno ya Mungu yalipokuwa yakitamkwa, viumbe hai vyenye maumbo mbalimbali, papo hapo, vilipata uhai katika matamshi ya Muumba. Viliingia ulimwenguni vikigombania kupata nafasi, vikirukaruka, na kucheza kwa furaha…. Samaki wenye maumbo na ukubwa tofauti wote waliweza kuogelea majini; samakigamba wa kila aina waliweza kuzaliana kwenye mchanga, viumbe vyenye magamba, vyenye maganda na vile visivyokuwa na uti wa mgongo viliweza kukua kwa haraka kwa maumbo tofauti, haijalishi kama vilikuwa vikubwa au vidogo, virefu au vifupi. Na ndivyo pia ilivyokuwa kwa aina tofauti za magugu ya baharini yalianza kukua kwa haraka, zikiyumbayumba kwenye mwendo wa viumbe mbalimbali vya majini, zikijipindua, zikiyasukuma maji yaliyotuama, kana kwamba yanataka kuyaambia: Tikisa mguu! Walete marafiki zako! Kwa maana hautawahi kuwa peke yako tena! Kuanzia wakati huo ambao viumbe hai mbalimbali vilivyoumbwa na Mungu vilionekana ndani ya maji, kila uhai mpya ulileta uhai kwa maji ambayo yalikuwa yametulia kwa muda mrefu sana, na kuanzisha enzi mpya…. Kuanzia wakati huo na kuendelea, viumbe hivi viliishi pamoja, kimoja kando ya kingine na vikaweza kukaa kwa pamoja, na havikuweka umbali kati yao. Maji yalikuwepo kwa ajili ya viumbe vilivyokuwa ndani yake, yakistawisha kila uhai uliokaa ndani ya kumbatio lake, na kila uhai ulikuwepo kwa ajili ya maji kwa sababu ya utunzaji wake. Kila kimoja kilimpa mwenzake uhai, na wakati huo huo, kila kimoja, kwa njia hiyo, kilitoa ushuhuda wa maajabu na ukuu wa uumbaji wa Muumba, na kwa nguvu zisizo na kifani za mamlaka ya Muumba …

Kwa vile bahari haikuwa tulivu tena, ndivyo pia uhai ulivyoanza kuijaza anga. Kimoja baada ya kingine, ndege, wakubwa kwa wadogo, walipaa juu angani kutoka ardhini. Tofauti na viumbe vya baharini, walikuwa na mbawa na manyoya ambayo yalifunika maumbo yao membamba na yenye kupendeza. Walipigapiga mbawa zao, kwa maringo na majivuno wakionyesha koti lao la kupendeza la manyoya na kazi zao maalum pamoja na ustadi waliopewa na Muumba. Walipaa kwa uhuru, na kwa ustadi walisafiri huku na kule kati ya mbingu na dunia, katika ukanda wa nyasi na misitu…. Walikuwa ni vipenzi vya anga, na vipenzi vya vitu vyote. Hivi karibuni wangekuwa ndio kiunganishi kati ya mbingu na dunia, na wangepitisha ujumbe kwa vitu vyote…. Waliimba, waliruka huku na kule kwa furaha, walileta shangwe , vicheko, na uchangamfu kwenye ulimwengu huu uliojaa utupu hapo mwanzoni…. Walitumia sauti zao zinazosikika vizuri, zenye kuvutia, na walitumia maneno yaliyokuwa ndani ya mioyo yao kumsifu Muumba kwa ajili ya uhai waliopewa. Walicheza kwa furaha ili kuonyesha ukamilifu na maajabu ya uumbaji wa Muumba, na wangejitolea maisha yao yote kushuhudia mamlaka ya Muumba kupitia maisha maalum ambayo Alikuwa amewapa …

Haijalishi kama vilikuwa majini, ama angani, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishwa na viumbe vyovyote. Kamwe hawakuthubutu kuvuka mipaka waliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaliana, na kutii kikamilifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa uangalifu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na amri na maagizo ya mbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo. Walizungumza na Muumba kwa njia yao maalum, na wakaja kufahamu maana ya Muumba, na wakatii amri Zake. Hakuna kati yao aliyewahi kukiuka mamlaka ya Muumba, na ukuu na amri Yake juu yao ilitekelezwa ndani ya fikira Zake; hakuna maneno yaliyotolewa, lakini mamlaka yaliyokuwa ya kipekee kwa Muumba yalidhibiti vitu vyote kwa ukimya ambavyo havikuwa na matumizi yoyote ya lugha, na ambavyo vilitofautiana na wanadamu. Maonyesho ya mamlaka Yake kwa njia hii maalum yalimlazimisha mwanadamu kupata maarifa mapya, na kufanya tafsiri mpya, ya mamlaka ya kipekee ya Muumba. Hapa, lazima niwaambie kwamba katika siku hii mpya, utekelezaji wa mamlaka ya Muumba yalionyesha kwa mara nyingine ule upekee wa Muumba.

Kinachofuata, wacha tuangalie sentensi ya mwisho ya kifungu hiki cha maandiko: “Mungu akaona ya kuwa ni vyema.” Unafikiri hii inamaanisha nini? Hapa, tunapata kuziona hisia za Mungu. Mungu alitazama vitu vyote Alivyokuwa ameviumba vikitokea na kusimama imara kwa sababu ya matamshi Yake, na polepole vilianza kubadilika. Je, kwa wakati huu, Mungu alikuwa Ameridhika na vitu mbalimbali Ambavyo alikuwa Amevifanya kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Je unaona nini hapa? Kunawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepanga na kuamua, ili kutimiza malengo ambayo Alikuwa amekusudia kuyatimiza. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, sio tu kwamba Hakujutia chochote, bali pia Aliridhika. Inamaanisha nini kwamba Hakujutia chochote? Inamaanisha kwamba mpango wa Mungu ni sahihi, kwamba nguvu na hekima Zake ni kamili, na kwamba ni kwa mamlaka Yake tu ndipo ukamilifu huo unaweza kutimizwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kufikia ukamilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho kamili, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia ukamilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa chema, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu alipoona ya kuwa ni vyema,” kila kitu Alichokiumba kilichukua umbo la kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa nafasi maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na milele yote. Zaidi ya hayo, jukumu lao miongoni mwa vitu vyote, na safari ambayo ni lazima waichukue wakati wa usimamizi wa Mungu wa vitu vyote, ilikuwa tayari imeamriwa na Mungu, na isingebadilishwa. Hii ilikuwa ni sheria ya mbinguni iliyotolewa na Muumba kwa vitu vyote.

“Mungu akaona kwamba ni vizuri,” maneno haya mepesi, yasiyothaminiwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ni maneno ya sheria ya mbinguni na amri ya mbinguni iliyotolewa na Mungu kwa viumbe vyote. Ni udhihirisho mwingine wa mamlaka ya Muumba, ambao ni wa kivitendo zaidi, na wa kina zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kupata yale yote Aliyokusudia kuyapata, na kutimiza yale yote Aliyokusudia kuyatimiza , lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa amekiumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa amekiumba chini ya mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa na utaratibu na cha kawaida. Viumbe vyote pia viliongezeka, vikawepo, na kupotea kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kinachoweza kukiuka! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona ya kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itakapobatilishwa na Muumba! Mamlaka ya kipekee ya Muumba hayakuonyeshwa tu katika uwezo Wake wa kuumba vitu vyote na kuamuru vitu vyote vije kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya vitu vyote, na kuweka uhai na nguvu juu ya vitu vyote, na, zaidi ya hayo, katika uwezo Wake wa kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa milele yote, vitu vyote ambavyo Angeviumba katika mpango Wake vionekane na kuwepo katika ulimwengu vilivyofanywa na Yeye katika umbo kamili, na muundo kamili wa uhai, na jukumu kamili. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo mawazo ya Muumba hayakuwa chini ya vizuizi vyovyote, hayakuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia bila kubadilika milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Anazungumza, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Mawazoni Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine

Bila kujua, kazi ya Muumba ya kuumba vitu vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa vitu vyote. Siku hii ilikuwa ni mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine ya ajabu. Je, basi, mpango wa Muumba ulikuwa ni upi usiku wa kuamkia siku hii mpya? Ni viumbe gani vipya ambavyo Angevizalisha, ambavyo Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba …

“Naye Mungu akasema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri” (Mwa 1:24-25). Ni viumbe gani hai ndivyovinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, katika siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai juu ya nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vyema.”

Kama tu kwenye siku zile tano za awali, kwa sauti ile ile, siku ya sita Muumba aliamuru kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na kwamba vilionekana juu ya nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anatumia mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kilionekana wakati ule Aliochagua. Kama vile Muumba alivyosema “Nchi na ilete kiumbe kilicho hai kwa jinsi yake,” nchi ilijawa mara moja na uhai, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Katika nyika za kijani kibichi, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwingine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kukimbia…. Mara moja, eneo kubwa lenye nyasi tulivu lilijawa na uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali ilikuwa ni mandhari ya kupendeza kwenye mbuga tulivu, na kuleta uhai usio na kikomo…. Wangekuwa ni marafiki wa nyika, na wenyeji wakuu wa nyika, kila kimoja kikitegemea kingine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha lishe ya milele kwa minajili ya kuwepo kwao …

Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwingine. Hata Ingawa ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka na kunesa, wengine waliyumba-yumba; wengine walienda mbele kwa haraka, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine waliruka juu na chini…. Wote walijishughulisha katika kujaribu kujitafutia makazi: Baadhi walijipenyeza kwenye nyasi, baadhi walianza kuchimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, iliyojificha msituni …. Ingawa walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusubiri wapumzike, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kibichi yenye kung’aa yalitoa chakula kitamu …. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakuacha kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo,walikuwa na nguvu nyingi sana na uchangamfu usio na kikomo, na kwa hivyo kati ya viumbe vyote, wao ndio walikuwa hodari zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya bidii katika kazi zao kwa ajili ya siku zao za baadaye, wakijishughulisha wenyewe na kukimbia hapa na pale kwaajili ya kesho zao, kwa ajili ya kuendelea kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila chembe ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na kwa kutumia njia zao maalum za kuishi, waliweka alama katika viumbe vyote, ambavyo juu yake waliacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na udongo, nyasi, na misitu, na walileta nguvu na uhai kwenye udongo, nyasi, na misitu, na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote …

Macho ya Muumba yalikagua vitu vyote Alivyoviumba, na kwa wakati huu macho Yake yalitulia juu ya misitu na milima, mawazo Yake yalikuwa yakizunguka. Maneno Yake yalipokuwa yakitamkwa, katika misitu minene, na juu ya milima, palionekana aina ya viumbe vilivyo tofauti na vilivyokuja hapo awali: Walikuwa ni wanyama wa mwituni waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Kwa muda mrefu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, kila mmoja wao akiwa na sura yake ya kipekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa na kiunzi nje cha kujikinga, baadhi yao walikuwa wakionyesha meno yao makali, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho—makali, baadhi walikuwa na macho ya woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakiruka-ruka kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakitembea kwa kwato nne, baadhi yao walikuwa juu ya miti wakitazama kwa mbali, baadhi walikuwa wakivizia msituni, baadhi walikuwa wakitafuta mapango ya kupumzikia, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kucheza kwa furaha kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi yao walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi yao walikuwa wakibweka, wengine walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti za juu, baadhi walikuwa na sauti za chini, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti nyororo na nzuri…; baadhi walikuwa ni wakali, na baadhi walikuwa ni wapole, baadhi walikuwa wanachukiza kutazama, baadhi walikuwa wanavutia, baadhi walikuwa wanaogopesha, baadhi walikuwa wa kirafiki na wasiodhuru…. Mmoja baada ya mwingine, kila mmoja alijitokeza. Tazama jinsi wanavyojidai na walivyo wakorofi, wenye kujiachia kwa uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda wa kutazamana…. Kila mmoja akiwa amebeba maisha maalum aliyopewa na Muumba, walionekana katika misitu na juu ya milima, na ukali wao wenyewe, na ukatili wao. Viumbe vyenye dharau kati ya vyote, na vyenye kujidai na kutawala—ni nani aliyewafanya kuwa mabwana wa kweli wa milimani na misituni? Kuanzia wakati ambao kuonekana kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kumiliki” katika misitu na katika milima, kwani Muumba alikuwa tayari Amepangilia mipaka yao na kuamua upana wa eneo la kuwepo kwao. Walikuwa tu ni mabwana wa kweli wa milimani na misituni, na ndiyo maana walikuwa ni wakali sana, wenye dharau sana. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wakali sana, wakatili, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeweza kuishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Kwa upande mwingine, ilikuwa ni kwa sababu waliishi kwa umbali fulani kutoka kwa wanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na wanadamu, ndio maana waliweza kutimiza jukumu walilopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule ukali wao uliilinda milima na kuilinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la kuwepo kwao na kuongezeka kwao. Wakati huo huo, ukali wao ulidumisha na kuhakikisha usawa kati ya vitu vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na uhifadhi wa milima na misitu; kuwasili kwao kuliingiza nguvu na uzima wa kudumu kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia wakati huu na kuendelea, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu maagizo ya Muumba ili waweze kubakia katika eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kudumisha usawa wa vitu vyote vilivyowekwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!

Katika Mamlaka ya Muumba, Vitu Vyote ni Vikamilifu

Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile ambavyo vingeweza kujongea na vile ambavyo visingeweza kujongea, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu, na wanyama wa mwituni walioumbwa kwenye siku ya sita—vyote vilikuwa ni vyema machoni pa Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, vitu hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha ukamilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na udhihirisho wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya udhihirisho huu, viumbe vyote visingeweza kujizuia ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Wakati matendo ya kimiujiza ya Mungu yalipokuwa yakijidhihirisha, ulimwengu huu ulijawa, kidogo kidogo, kwa vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ulibadilika kutoka kwenye machafuko na giza hadi kwenye ubayana na nuru, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwenye uchangamfu na uhai usio na kikomo. Miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji, kutoka kwa vitu vikubwa hadi vidogo, kutoka kwa vile vidogo hadi kwa vile vinavyoweza kutazamwa tu kwa hadubini, hakuna chochote ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na vilikuwa na umuhimu wa kipekee na asili na thamani ya kuwepo kwa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule anatisha, hakuna namna ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kipumbavu kweli! Kile wanachofaa kusema ni, “Ingawa mdudu huyu ana sura mbaya sana, lakini aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Katika fikira za Mungu, Alinuia kutoa kila aina ya mwonekano, na kila aina ya jukumu na matumizi, kwa viumbe hai mbalimbali Alivyoviumba, na kwa hivyo hakuna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia mwonekano wao wa nje hadi viungo vyao vya ndani, kutoka kwenye tabia zao za kuishi hadi katika eneo ambalo wanaishi - kila kiumbe ni tofauti. Ng'ombe wana mwonekano wa ng'ombe, punda wana mwonekano wa punda, kulungu wana mwonekano wa kulungu na tembo wana mwonekano wa tembo. Je, unaweza kusema ni yupi mwenye mwonekano bora zaidi, na ni yupi mwenye mwonekano mbaya zaidi? Je, unaweza kusema ni yupi mwenye manufaa zaidi, na ni uwepo wa yupi una umuhimu mdogo zaidi? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu huonekana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui-milia wanavyoonekana, kwani mwonekano wao unavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na vitu vyote vya uumbaji, mwanadamu anapaswa kunyenyekea chini ya mamlaka ya Muumba, ambavyo ni kusema kwamba, nyenyekea katika mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika vitu vyote; huu ndio mtazamo wenye busara zaidi. Mtazamo pekee wa kutafuta, na wa kuwa mtiifu, kwa nia za asili za Muumba ndio kukubali kwa kweli na kuwa na uhakika wa mamlaka ya Muumba. Ni chema machoni pa Muumba, kwa hivyo mwanadamu ana sababu gani ya kutafuta kosa?

Hivyo basi, vitu vyote vilivyo chini ya mamlaka ya Muumba vinapaswa kucheza wimbo mpya kwa ajili ya ukuu wa Muumba, vinapaswa kuanzisha wimbo wa utukufu kwa ajili ya kazi Yake ya siku mpya, na kwa wakati huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria iliyowekwa na Muumba ya kuchipua wakati wa masika, kustawi wakati wa kiangazi, mavuno wakati wa vuli, na kuhifadhi majira ya kipupwe, vitu vyote vitaendana na mpango wa usimamizi wa Muumba, na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya na mkondo mpya wa maisha. Vitaendelea kuishi na kuzaliana kwa mfululizo usioisha ili waweze kukaribisha kila siku chini ya ukuu wa mamlaka ya Muumba …

Hakuna Kiumbe Chochote Kilichoumbwa na Kisichoumbwa Kinachoweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba

Tangu Alipoanza uumbaji wa vitu vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni kwa njia gani Aliviumba, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, vitu vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwa wakati ambao bado mwanadamu hajaonekana ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu Zake za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Yake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwa viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, mwanga, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, vikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila kimoja kilipewa uhai kwa matamshi ya Muumba, na kila kila kimoja kiliongezeka kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimoja kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawa hawakupokea pumzi ya Muumba, bado walionyesha uhai na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa maumbo na miundo yao tofauti; Ingawa hawakupokea uwezo wa kuongea waliopewa wanadamu na Muumba, kila kimoja kilipokea namna ya kuelezea uhai wao ambao wamepewa na Muumba, na ambao ulitofautiana na ile lugha ya wanadamu. Mamlaka ya Muumba sio tu kwamba yanatoa nguvu za uhai katika vitu vinavyoonekana kuwa tulivu, ili visiwahi kutoweka, bali pia, Anatoa silika ya kuzaliana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, viweze kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatumia mamlaka Yake haifuati kwa uthabiti mtazamo wa mambo makubwa makubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka na taratibu zozote; Anaweza kuamuru utendakazi wa ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya uhai na kifo kwa vitu vyote, na, vilevile, Anaweza kuendesha vituvyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala vitu vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya kipekee ya Muumba miongoni mwa vitu vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu katika maisha haya tunayoishi; kamwe hayatakoma, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kuchukua nafasi ya utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki kiini cha Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, Ingawa vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kumwakilisha Mungu. Ingawa wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba vitu vyote, kuamuru vitu vyote, na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haziwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Katika Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba vitu vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kumtuma yeyote kati ya wajumbe Wake au malaika kuumba vitu vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote vilivyoumbwa, vyote viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni bora au duni, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kuchukua nafasi ya utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!

Kupitia ushirika wa hapo juu, je, tunaweza kusema yafuatayo: Muumba na Mtawala pekee wa vitu vyote, Yule anayemiliki mamlaka ya kipekee na nguvu za kipekee, ndiye Anayeweza kuitwa Mungu Mwenyewe wa kipekee? Wakati huu, unaweza kuhisi kwamba swali kama hilo ni la kina sana. Wewe, kwa muda huu, huwezi kulielewa, na huwezi kung’amua kiini cha ndani na kwa hivyo kwa muda huu unahisi kwamba ni swali gumu kujibu. Kwa hivyo, Nitaendelea na ushirika Wangu. Kinachofuata, Nitakuruhusu uone matendo halisi ya vipengele vingi vya mamlaka na nguvu zinazomilikiwa na Mungu pekee, na hivyo basi Nitakuruhusu kuelewa kwa kweli, kufahamu, na kujua upekee wa Mungu, na maana ya mamlaka ya kipekee ya Mungu.

2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Baada ya Kuumba Vitu Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye Agano la Upinde wa Mvua

Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye sio tu kwamba Anatawala hatima ya vitu vyote, bali pia Anawatawala wanadamu, kiumbe maalum ambacho Alikiumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa maisha. Baada ya kuumba vitu vyote, Muumba hakuacha kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya vitu vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kumsimamia mwanadamu, kumtawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kumpata mwanadamu kwa kweli, kumpata mwanadamu ambaye angetawala vitu vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kufanikisha matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mahali pote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.

Kunao mfanano kati ya kifungu cha kwenye Mwanzo 9:11-13 na vifungu vilivyo hapo juu vinayohusu rekodi ya uumbaji wa Mungu wa ulimwengu, lakini pia kuna tofauti. Mfanano ni upi? Mfanano umo katika matumizi ya matamshi na Mungu kuweza kufanya kile ambacho Alinuia, na tofauti ni kwamba, kifungu hiki ni mazungumzo ya Mungu na binadamu, ambapo Alianzisha agano na binadamu, na Akamwambia binadamu kuhusu kile ambacho kilikuwa ndani ya agano hilo. Utekelezaji huu wa mamlaka ya Mungu ulitimizwa wakati wa mazungumzo Yake na mwanadamu, ambavyo ni kusema kwamba, kabla ya uumbaji wa mwanadamu, maneno ya Mungu yalikuwa maagizo, na amri ambavyo vilitolewa kwa viumbe ambavyo Alinuia kuumba. Lakini sasa kulikuwa na mtu wa kusikiliza matamshi ya Mungu, na hivyo basi matamshi Yake yalikuwa ya mazungumzo na binadamu, na pia maagizo na maonyo kwa binadamu, na zaidi ya hayo, maneno ya Mungu yalikuwa ni amri zilizobeba mamlaka Yake na ambazo zilitolewa kwa vitu vyote.

Ni hatua gani ya Mungu imerekodiwa katika kifungu hiki? Kifungu kinarekodi agano ambalo Mungu alianzisha na binadamu baada ya Yeye kuangamiza ulimwengu kwa gharika, linamwambia binadamu kwamba Mungu asingesababisha tena uharibifu kama huo juu ya ulimwengu, na kwamba, kwa mwisho huu, Mungu aliumba ishara—na ishara hii ilikuwa nini? Katika maandiko inasemwa kwamba “Mimi nauweka upinde Wangu mawinguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi.” Haya ni matamshi halisi yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu Yake mahususi kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya mbinguni yatakayobakia milele bila kubadilika, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, inaweza kusemwa, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa vitu vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba hayana mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na ilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka kufikia leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu humaanisha kile Anachokisema, na kile Anachokisema kinatimizwa, na kile Anachokitimiza kitadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inatofautisha utambulisho na kiini kinachomilikiwa na Muumba pekee na kile cha viumbe vilivyoumbwa. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kuzidiwa kiwango na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.

Uanzishaji wa agano Lake na binadamu ilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na mpaka kufikia hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa kiasi gani? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwingine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, ukamilifu wa agano la upinde wa mvua ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kufahamu, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwa kuwa hakuna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika muendelezo wa kuonekana kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, bali ni mamlaka ya Muumba yasiyobadilika. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya ajabu na ya kimiujiza ya Muumba katika mahali pa siri, na, kwa wakati huo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kupungua, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la kipengele kingine cha mamlaka ya kipekee ya Muumba?

3. Baraka za Mungu

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwako.

Mwa 18:18-19 Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa ndani yake. Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kwa nafsi yangu, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Mbinu na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

Wengi wanatamani kutafuta, na kupata, baraka za Mungu, lakini si kila mtu anayeweza kupata baraka hizi, kwani Mungu anazo kanuni Zake binafsi, na Yeye hubariki binadamu kulingana na njia Zake binafsi. Ahadi ambazo Mungu hutoa kwa binadamu, na kiwango cha neema ambacho Yeye humpa binadamu, vyote vinatolewa kulingana na fikira na vitendo vya binadamu. Hivyo, ni nini huonyeshwa kupitia kwa baraka za Mungu? Watu wanaweza kuona nini ndani yake? Wakati huu, hebu tuweke kando mazungumzo kuhusu ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki, na kanuni anazofuata Mungu katika kubariki binadamu. Badala yake, hebu tuangalie baraka za Mungu kwa binadamu kwa lengo la kujua mamlaka ya Mungu, kutoka kwenye mtazamo wa kujua mamlaka ya Mungu.

Vifungu vinne vya maandiko hapo juu ni rekodi zote kuhusu baraka za Mungu kwa mwanadamu. Vinatupa ufafanuzi wenye maelezo kuhusu wapokeaji wa baraka za Mungu, kama vile Ibrahimu na Ayubu, vilevile vinatupa sababu zinazoelezea kwa nini Mungu alitoa baraka Zake, na ni nini kilichokuwa ndani ya baraka hizi. Ile sauti na mbinu ya matamshi ya Mungu, mtazamo na nafasi ambayo Yeye alizungumza kutoka kwayo, inawaruhusu watu kufahamu kwamba Yule ambaye hutoa baraka na mpokeaji wa baraka hizo ni wa utambulisho, hadhi na kiini tofauti kabisa. Sauti na mbinu ya matamshi haya, na nafasi ambayo yalizungumzwa, ni ya kipekee kwa Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba. Anayo mamlaka na uwezo, pamoja na heshima ya Muumba, na ukuu ambao hakuna mtu yeyote anayeweza kuitilia shaka.

Kwanza hebu tuangalie Mwa 17:4-6: “Tazama, mimi agano langu nimefanya na wewe, na wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba wa mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.” Matamshi haya ndiyo yaliyokuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, pamoja na baraka za Mungu kwa Ibrahimu: Mungu angemfanya Ibrahimu kuwa baba wa mataifa, Angemfanya kuwa na uzao mwingi, na Angemfanya kuwa na mataifa mengi, nao wafalme wangetoka kwake. Je, unayaona mamlaka ya Mungu katika maneno haya? Na unayaonaje mamlaka kama hayo? Ni kipengele gani cha kiini cha mamlaka ya Mungu unachokiona? Kutokana na usomaji wa makini wa maneno haya, si vigumu kutambua kwamba mamlaka na utambulisho wa Mungu vyote vimefichuliwa waziwazi katika maneno ya matamshi ya Mungu. Kwa mfano, Mungu anaposema “agano langu nimefanya na wewe, na wewe utakuwa … kuwa nimekufanya … Mimi nitafanya uwe…,” kauli kama vile “wewe utakuwa” na “nitayaunda,” ambazo maneno yake yanasheheni thibitisho la utambulisho na mamlaka ya Mungu, kwa upande mmoja ni onyesho la uaminifu wa Muumba; kwa upande mwingine, ni maneno maalum yaliyotumiwa na Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba—pamoja na kuwa sehemu ya msamiati wa kawaida. Kama mtu atasema anatumai kuwa mtu mwingine atazidisha uzao, kwamba mataifa yatafanywa kutoka kwao, na kwamba wafalme watatoka kwao, basi hiyo bila shaka ni aina ya tamanio, na si ahadi wala baraka. Na hivyo, watu wasithubutu kusema “Nitakufanya uwe hivi na hivi, utakuwa hivi na hivi,” kwa kuwa wanajua kwamba hawamiliki nguvu kama hizo; si juu yao, na hata kama watasema maneno kama hayo, maneno yao yatakuwa matupu, na ya kipuzi, yanayoendeshwa na matamanio na maono yao. Je, yupo yeyote anayethubutu kuongea kwa sauti kuu kama hiyo ilhali wanahisi kwamba hawawezi kutimiza matamanio yao? Kila mtu hutamani mema yafikie kizazi chake, na kutumai kwamba kitafanikiwa na kufurahia mafanikio makubwa. “Ingekuwa ni bahati iliyoje kama mmoja wao angekuwa ni mfalme! Kama mmoja angekuwa gavana ingekuwa vizuri, pia—mradi tu wawe ni watu muhimu!” Haya yote ni matamanio ya watu, lakini watu wanaweza kutamani tu baraka juu ya kizazi chao, na hawawezi kutimiza au kufanya ahadi zao zozote kuwa kweli. Katika mioyo yao, kila mtu anajua waziwazi kwamba wao hawamiliki nguvu za kutimiza mambo kama hayo, kwani kila kitu chao kipo nje ya udhibiti wao, na hivyo basi watawezaje kuamuru hatima za wengine? Sababu inayomfanya Mungu kusema maneno kama haya ni kwa sababu Mungu anamiliki mamlaka kama hayo, na Anaweza kutekeleza na kusababisha ahadi zote Anazotoa kwa ajili ya binadamu, na kufanya baraka zote Anazompa binadamu kuwa kweli. Binadamu aliumbwa na Mungu, na kwa Mungu kumfanya mtu awe na uzao mwingi sana ni jambo ambalo litakuwa rahisi sana; kufanya kizazi cha mtu kufanikiwa kutahitaji neno moja tu kutoka Kwake. Hangelazimika kujishughulisha Mwenyewe na kutoa jasho kwa ajili ya kitu kama hicho, au kushughulisha akili Yake, au kujiweka katika taabu juu ya hilo; hii ndiyo nguvu halisi ya Mungu, mamlaka halisi ya Mungu.

Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Je, unaweza kuhisi ubora wa ajabu wa Muumba? Je, unaweza kuhisi ukuu wa Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au katika uwakilishi wa, ujasiri Wake katika ufanisi; badala yake, hayo ni, uthibitisho wa mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kuna maneno mawili ambayo unapaswa kuzingatia hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” je, kuna dalili ya kutoeleweka katika maneno haya? Je, kuna dalili yoyote ya wasiwasi? Je, kuna dalili yoyote ya hofu? Kwa sababu ya maneno “hakika utakuwa” na “watakuja” katika matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna ambaye angethubutu kumbariki mwingine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Kadiri maneno ya Mungu yanavyokuwa ya hakika zaidi, ndivyo yanavyothibitisha zaidi kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba utimizaji wake hauzuiliki. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, ukamilifu wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Haijalishi kile ambacho kingetokea, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uwezo mkubwa wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywani mwa Mungu, na kuna nguvu, ukuu na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na ukweli umethibitisha kwamba ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo yasiyo na maana, bali ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.

Ni nini tofauti kati ya maneno yanayotamkwa na Mungu na yale yanayotamkwa na binadamu? Unaposoma maneno haya yaliyotamkwa na Mungu, unahisi nguvu za maneno ya Mungu, na mamlaka ya Mungu. Je, unahisi vipi unaposikia watu wakitamka maneno kama hayo? Je, unafikiria kuwa wao wana kiburi kupindukia, na ni wenye kujigamba na wanajionyesha wenyewe? Kwa kuwa hawana nguvu hizi, hawamiliki mamlaka kama haya, na hivyo basi hawawezi kabisa kutimiza mambo kama hayo. Kwamba wao wana uhakika kabisa kuhusu ahadi zao, yaonyesha tu uzembe kwa matamshi yao. Kama mtu anasema maneno kama hayo, basi bila shaka watakuwa wenye kiburi, na waliozidisha ujasiri wao, huku wakijifichua kama mfano wa pekee wa tabia ya malaika mkuu. Maneno haya yalitoka kinywani mwa Mungu; je, unahisi dalili yoyote ya kiburi hapa? Je, unahisi ya kwamba matamshi ya Mungu ni mzaha tu? Matamshi ya Mungu ni mamlaka, maneno ya Mungu ni ukweli, na kabla hajatamka maneno kutoka kinywani Mwake, hivi ni kusema, wakati Anapofanya uamuzi wa kufanya kitu, tayari kitu hicho kimefanyika. Yaweza kusemwa kwamba kila kitu alichosema Mungu kwa Ibrahimu kilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, na ahadi Mungu alizozitoa kwa Ibrahimu. Ahadi hii ilikuwa ukweli uliothibitishwa, pamoja na ukweli uliotimizwa, na ukweli huu ulitimizwa hatua kwa hatua katika fikira za Mungu kulingana na mpango wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu kusema maneno kama hayo haimaanishi kuwa Ana tabia ya kiburi, kwani Mungu anaweza kutimiza mambo kama hayo. Anazo nguvu na mamlaka, na Anao uwezo kamili wa kutimiza vitendo hivi, na utimizaji wake upo ndani ya upeo wa uwezo Wake. Wakati maneno kama haya yanapotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, yanakuwa ufunuo na maonyesho ya tabia ya kweli ya Mungu, ufunuo na udhihirisho kamili wa kiini na mamlaka ya Mungu, na hakuna kitu ambacho kinafaa zaidi na kizuri kama uthibitisho wa utambulisho wa Mungu. Namna, sauti, na mpangilio wa maneno ya matamshi kama hayo ndiyo alama haswa ya utambulisho wa Muumba, na vyote hivi vinalingana kikamilifu na maonyesho na utambulisho wa Mungu, na ndani yao hakuna kujifanya, au kasoro; vyote hivi, kwa ukamilifu na kwa ujumla ni, maonyesho kamili ya kiini na mamlaka ya Muumba. Lakini Kuhusu viumbe, havimiliki mamlaka haya, wala kiini hiki, sembuse kumiliki nguvu inayotolewa na Mungu. Kama mwanadamu atadhihirisha tabia kama hiyo, basi hali hiyo itakuwa bila shaka udhihirisho wa tabia yake iliyopotoka, na itaishia katika athari ya kujihusisha visivyofaa na kiburi cha binadamu na tamaa mbaya, na kufichuliwa kwa nia ovu za yule ibilisi, Shetani, anayependa kuwadanganya watu na kuwashawishi waweze kumsaliti Mungu. Na je Mungu anachukuliaje kile ambacho kimefichuliwa kwa lugha kama hii? Mungu angesema kwamba unataka kunyakua nafasi yake na kwamba unataka kumwiga Yeye na kumbadili Yeye. Wakati unaiga sauti ya matamshi ya Mungu, nia yako ni ya kubadilisha nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, kujitwalia mwanadamu ambaye anamilikiwa kihalali na Mungu. Huyu ni Shetani, halisi na bila kukuficha; haya ni matendo ya vizazi vya malaika mkuu visivyovumilika Mbinguni! Miongoni mwenu, je, wapo ambao wamewahi kumuiga Mungu kwa njia fulani kwa kuongea maneno machache, kwa nia ya kupotosha na kudanganya watu na kuwafanya watu kuhisi kuwa maneno na matendo ya mtu huyu yana mamlaka na nguvu za Mungu, kana kwamba kiini na utambulisho wa mtu huyu ni vya kipekee, na hata ni kana kwamba sauti ya mtu huyu ni sawa na ile ya Mungu? Je, umewahi kufanya jambo kama hili? Je, umewahi kuiga sauti ya Mungu katika usemi wako, kwa ishara zinazodaiwa kuiwakilisha tabia ya Mungu, kwa kile unachodhania kuwa ni uwezo na mamlaka? Je, wengi wenu huwa mara nyingi mnatenda, au kupanga kutenda kwa njia kama hiyo? Sasa, unapoona kwa kweli, kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, na kutazama kile ulichokuwa ukikifanya, na ulichokuwa ukifichua kujihusu, je, unahisi vibaya? Je, unatambua ujinga wako na kutokuwa na aibu? Baada ya kuchambua tabia na asili za watu kama hao, je, inaweza kusemwa kuwa wao ndio walaaniwa wa jahanamu? Je, inaweza kusemwa kwamba kila mtu anayefanya mambo kama haya anajiletea udhalilishaji? Je, unatambua uzito wa asili yake? Na uzito wake ni wa kiasi kipi? Nia ya watu wanaotenda mambo kwa njia hii ni kumwiga Mungu. Wanataka kuwa Mungu, na kuwafanya watu kuwaabudu kama Mungu. Wanataka kuondoa nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, na kutupilia mbali yule Mungu anayefanya kazi miongoni mwa binadamu, ili kutimiza nia ya kuwadhibiti watu, na kuwateketeza watu, na kuwamiliki watu hao. Kila mtu ana matamanio na matarajio kama haya yaliyofichika akilini, na kila mtu anaishi katika aina hii ya kiini kipotovu cha shetani, katika asili hiyo ya kishetani ambamo wako katika uadui na Mungu, kumsaliti Mungu, na kutamanikuwa Mungu. Kufuatia Ushirika Wangu katika mada hii ya mamlaka ya Mungu, bado ungependa au ungetamani kujifanya wewe ni Mungu, au kumwiga Mungu? Je, bado unatamani kuwa Mungu? Ungali unapenda kuwa Mungu? Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawa unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga kiini cha Mungu. Ingawa unaweza kusimama katika nafasi ya Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru vitu vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, vitu vyote kuhusu wewe vipo chini ya utawala wa Muumba. Ingawa unaweza kusema baadhi ya maneno yenye ukali, hilo haliwezi kuonyesha kwamba una kiini cha Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni kiini cha Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni kiini cha Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe vilivyoumbwa hauwezi kamwe kubadilishwa. Kama tu kiumbe kimojawapo, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa makini kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Na mwanadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni machukizo kwa Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkuu, au wa kipekee, au juu zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkuu au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndilo lengo pekee ambalo watu wote wanapaswa kufuata.

Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayahesabiki

Hebu tuangalie Mwanzo 22:17-18. Hiki ni kifungu kingine kilichozungumziwa na Yehova Mungu, ambapo Alimwambia Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.” Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: “kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani.” Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao mmoja, wawili, au hata maelfu, lakini idadi isiyohesabika, kiasi kwamba wangekuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti kiasi cha uzao atakaokuwa nao? Je, hilo ni juu yake? Si hata juu ya mwanadamu kama atakua na uzao kadhaa ama la, sembuse kuwa nao wengi kama “nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani.” Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote ni juu ya Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!

Wakati Mungu alisema “uzao wako nitazidisha,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hata milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Ni Mungu pekee ndiye mwenye sifa na uwezo wa kufanya ahadi hii itimie. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yatatimizwa kwa uhakika, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Vitu vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hata milele. Kwa hakika, siku ambayo vitu vyote vitatoweka ndiyo siku hasa ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kufanya kitu kiwe si kitu, na Anadhibiti mabadiliko ya vitu vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi zaidi kama kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kulifikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kulifikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni uhalisia ambao Mungu tayari aliuona, na ambao kwa hakika utaweza kutimizwa. Je, unaelewa hili? Je, ukweli wa mambo unathibitisha kwamba wazao wa Abrahamu walikuwa wengi? Na je, walikuwa ni wengi kiasi gani? Je, walikuwa ni wengi kama “nyota za mbinguni, na kama mchanga uliokopwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, waliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza ukweli huu? Je, iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa mamia au maelfu kadhaa ya miaka baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na siku zote yaliendelea kuwa halisi; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na uthibitisho wa mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba vitu vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alimruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa kiini cha mamlaka ya Mungu, na Akamruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyopimika, na zaidi ya hayo, Alimruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.

Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua amri ya kazi hii, na ukweli ulioahidiwa kwa kinywa cha Mungu polepole unaanza kuwa halisi. Kama matokeo, mabadiliko yanaanza kuonekana kati ya vitu vyote, kama vile, wakati wa majira ya kuchipua, nyasi hubadilika kuwa kijani kibichi, maua huchanua, chipukizi huchipuka kutoka kwenye miti, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Majira ya kuchipua yanapowadia vitu yote vinahuishwa, na hili ndilo tendo la kimiujiza la Muumba. Mungu anapotimiza ahadi zake, vitu vyote mbinguni na duniani vinafanywa upya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati patano au ahadi inapotamkwa kutoka katika kinywa cha Mungu, vitu vyote vinatimiza wajibu wao, na vinaongozwa kwa minajili ya kutimizwa kwao, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kutumikia jukumu lao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Je, kuna kiwango cha mamlaka ya Mungu? Je, kuna ukomo wa wakati? Je, yanaweza kusemwa kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, yanaweza kusemwa kuwa na ukubwa fulani au nguvu fulani? Je, yanaweza kupimwa kwa vipimo vya kibinadamu? Mamlaka ya Mungu sio kitu kinachopepesa, hayaonekani na kutoweka ghafla, na hakuna mtu anayeweza kupima jinsi mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, Mungu anapombariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutamruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za uhai zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho kamili la maneno kutoka kinywani Mwake, ambayo yanaonyeshwa katika vitu vyote, na kwa wanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa kwa mamlaka Yake ni chenye ubora usio na kifani, na hakina dosari kabisa. Inaweza kusemwa kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyo na kifani, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, kila kitu kinachomhusu kinafahamika kwa Mungu kama tu sehemu ya nyuma ya mkono Wake mwenyewe, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanapoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au jinsi ambavyo mageuzi yamekuwa makubwa katika mazingira yao ya kuishi. Haijalishi ni muda gani umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kana kwamba ndio yametoka tu kutamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutimiza kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutimizwa, na, zaidi ya hayo, kukamilishwa kwake na kutimizwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba ukubwa wa mamlaka na nguvu za Mungu unatosha kuudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawa baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimepotea polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alitumia mamlaka Yake, jinsi ambavyo vitu vyote vilipangwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila sehemu ya ajabu ya onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kuinuliwa kati ya vitu vyote, vitu vyote vilijitokeza na kuzungumza juu ya matendo ya kimiujiza ya Muumba, na kila hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya vitu vyote itatangazwa na vitu vyote milele yote. Mamlaka ambayo kwayo Mungu anatawala vitu vyote, na nguvu za Mungu, zinaonyesha vitu vyote kwamba Mungu yuko kila mahali na wakati wote. Wakati utakapokua umeshuhudia kuenea kwamamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.

Baadhi ya watu wanapenda kukisia na kufikiria, lakini fikira za mwanadamu zinaweza kwenda umbali gani? Je, zinaweza kwenda zaidi ya ulimwengu huu? Je, mwanadamu ana uwezo wa kukisia na kufikiria uhalisi na usahihi wa mamlaka ya Mungu? Je, makisio na mawazo ya mwanadamu yana uwezo wa kumruhusu kupata ujuzi wa mamlaka ya Mungu? Je, yanaweza kumfanya mwanadamu afahamu na kunyenyekea kwa kweli mbele ya mamlaka ya Mungu? Ukweli unathibitisha kwamba makisio na mawazo ya mwanadamu ni zao tu la akili ya mwanadamu, na haitoi msaada au manufaa hata kidogo kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu mamlaka ya Mungu. Baada ya kusoma makala za kidhahania za kisayansi, baadhi wanaweza kufikiria mwezi, na vile nyota zilivyo. Ilhali hii haimanishi kwamba binadamu anao ufahamu wowote wa mamlaka ya Mungu. Kufikiria kwa binadamu ni hivyo tu: ni kufikiria. Kuhusiana na ukweli wa mambo haya, hivi ni kusema kwamba, kuhusiana muunganiko wao kwa mamlaka ya Mungu, hana ung’amuzi wowote. Na je, inamaanisha nini hata kiwa umeenda hadi kwenye mwezi? Je, hii inaonyesha kuwa una ufahamu wa vipengele vingi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, hii, inaonyesha kwamba wewe unaweza kufikiria upana wa mamlaka na nguvu za Mungu? Kwa sababu makisio na fikira za mwanadamu hazina uwezo wa kumruhusu kuyatambua mamlaka ya Mungu, je, mwanadamu anapaswa kufanya nini? Uchaguzi wenye busara zaidi ungepaswa kuwa kutokukisia au kufikiria, hivi ni kusema kwamba, ni lazima mwanadamu asitegemee kamwe fikira na asitegemee kamwe makisio inapokuja katika suala lakujua mamlaka ya Mungu. Ni nini ambacho Ningependa kukwambia hapa? Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho wa Mungu mwenyewe, na kiini cha Mungu hayawezi kupatikana kwa kutegemea fikira zako. Kwa kuwa huwezi kutegemea fikira ili kutambua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kupata maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na uzoefu na uthibitisho wa mamlaka ya Mungu hatua kwa hatua, na hivyo basi utapata kuelewa kwa utaratibu na kuongeza maarifa kuyahusu. Hii ndiyo njia pekee ya kupata maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuambia kwamba usifikirie sio sawa na kukufanya ukae kimya ukisubiria uharibifu, au kukuzuia usifanye lolote. Kutotumia ubongo wako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki kukisia, kutotumia maarifa kuchanganua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufahamu, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza lengo hili, lakini , je, unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Ninakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua na kuthibitisha kwa uangalifu na kwa uthabiti kile ambacho Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analonena na kwa kila kitu Anachofanya. Hii ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Kwani kile ambacho Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si kitu kisicho na maana na tupu, bali ni halisi.

Ukweli wa Udhibiti na Utawala wa MuumbaJuu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Unazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba

Vivyo hivyo, baraka za Yehova kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? “Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike” (Ayubu 42:12). Kwa mtazamo wa kibinadamu, ni vitu gani ambavyo Ayubu alipewa? Je, zilikuwa ni mali za kibinadamu? Akiwa na mali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwa kipindi hicho? Na je, aliwezaje kupata mali kama hizo? Ni nini kilichosababisha utajiri wake? Bila shaka—ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu kwamba Ayubu alikuja kuzimiliki. Jinsi ambavyo Ayubu alizitazama mali hizi, na jinsi alivyozichukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Inapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na kiasi cha mali anachoweza kupata katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—huu ni ukweli usiopingika! Mungu ana mamlaka, na Anazo nguvu za kumpatia mwanadamu mali zozote zile, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni kwa baraka za Mungu. Je, ni watu wa aina gani ambao Mungu anawabariki? Ni wale watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu wote walibarikiwa na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alimbariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalimtawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi ya Mungu kati ya vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, mwanadamu huyu aliongezeka na kuwepo kwa kasi iliyoamuliwa na Mungu, na ndani ya upeo ulioamuliwa na Mungu. Kwa hakika, uwezo wa taifa hili, kasi ya upanuzi, na muda wa kuishi vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitegemea kabisa ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea bila kizuizi na zingetekelezwa chini ya usimamizi wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, bila kujali mageuzi ya ulimwengu, bila kujali enzi, bila kujali maafa ambayo wanadamu wamevumilia, wazao wa Ibrahamu hawangekabiliwa na hatari ya kuangamizwa, na taifa lao lisingeweza kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya awe tajiri sana. Kile alichopewa na Mungu kilikuwa ni makundi ya viumbe hai, vinavyopumua, ambavyo taarifa zao kuhusu—idadi yao, kasi yao ya kuzaliana, muda wao wa kuishi, ikiwa ni wanene na wenye nguvu, na kadhalika—vyote vilikuwa chini ya udhibiti wa Mungu. Ingawa viumbe hawa hawakuwa na uwezo wa kuzungumza, wao pia walikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi kwa Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu aliwapa Ibrahimu na Ayubu, ingawa kile kilichoahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitawala vitu vyote na viumbe hai yalikuwa sawa. Kila maelezo ya mamlaka na uwezo wa Mungu unaonyeshwa katika ahadi na baraka Zake tofauti kwa Ibrahimu na Ayubu, na yanawaonyesha wanadamu, kwa mara nyingine tena kwamba, mamlaka ya Mungu ni zaidi ya mawazo ya mwanadamu. Maelezo haya yanawaambia wanadamu kwa mara nyingine tena kwamba, ikiwa wanataka kuyajua mamlaka ya Mungu, basi hili linaweza tu kufikiwa kupitia kwa maneno ya Mungu na kwa kuweza kupitia kazi ya Mungu.

Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya vitu vyote yanamruhusu mwanadamu kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika maneno “Mungu akasema, Iwe nuru, ikawa nuru, na, Kuwe na anga, na kukawa na anga, na, Kuwe na nchi, na kukawa na nchi,” lakini, zaidi ya hayo, mamlaka Yake pia yamejumuishwa katika jinsi Alivyoifanya nuru ile iendelee kuwepo, Alivyoizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, na vilevile katika maelezo ya jinsi Alivyotawala na kuvisimamia vitu Alivyoviumba: nuru, anga, na ardhi. Je, ni nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa wanadamu? Kwa uwazi, baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikukoma, kwani Alikuwa tu ameanza kuyatumia mamlaka Yake, na Alinuia kufanya kila moja ya maneno Yake kuwa halisi, na kufanya kila moja ya maelezo Aliyozungumza kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu ana mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote na vitu vyote viweze kutimizwa. Mawazo kama haya ni ya kipuuzi kabisa! Kama utachukua tu mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu wa Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na ukweli tofautitofauti kwamba mamlaka ya Mungu yanashikilia utawala juu ya uwepo wa vitu vyote, basi ufahamu wako kuhusu mamlaka ya Mungu ni mtupu na wa kipuuzi! Ikiwa mwanadamu anamfikiria Mungu kuwa hivyo, basi, ni, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anamfikiria kuwa ni kama mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande wa kivitendo wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Hakuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, mara tu Mungu alipotamka maneno Yake, chini ya uongozi wa mamlaka ya Mungu, vitu vyote vilianza kuendana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutekelezwa katika nchi nzima, na Aliweka njia ya kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, Mungu hakuwadhibiti tu wajumbe Wake, bali pia vitu vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivi ni kusema kwamba, upeo ambao mamlaka ya Mungu yalitekelezwa haukujumuisha wajumbe tu, bali, vitu vyote katika uumbaji, ambavyo viliongozwa ili kuendana na kazi Aliyokusudia kuikamilisha; hizi ndizo tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitekelezwa. Katika mawazo yenu, wengine wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao wa mamlaka ya Mungu: Mungu ana mamlaka, na Mungu ana nguvu, na hivyo Mungu anahitaji tu kubaki katika mbingu ya tatu, au sehemu moja tu, na hahitaji kufanya kazi yoyote mahususi, na ukamilifu wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, Ingawa Mungu alimbariki Ibrahimu, Mungu hakuhitaji kufanya lolote, na ilitosha Kwake tu kutamka maneno Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka, sivyo! Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisi, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka na nguvu za Mungu hufichuliwa na kuonyeshwa hatua kwa hatua katika uumbaji Wake wa vitu vyote, katika udhibiti Wake juu ya vitu vyote, na katika mchakato ambao Yeye anawaongoza na kuwasimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyote—yote yanathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo halisi wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angewapa Ibrahimu na Ayubu—ilikuwa ni uamuzi wa Mungu kuufanya. Ingawa wajumbe wa Mungu waliwatembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, matendo yao yalikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawa binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hamshuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote katika rekodi za Biblia, kwa hakika, Yule pekee ambaye kwa kweli anatumia nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kutiliwa shaka na binadamu yeyote! Ingawa umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kitu kimoja kilicho, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kitu chochote kinachoweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.

Mamlaka ya Muumba Hayabadiliki na Hayawezi Kukosewa

Ni nini umeona katika vipengele hivi vitatu maandiko? Je, umeona kuwa kuna kanuni ambayo Mungu hutumia mamlaka Yake? Kwa mfano, Mungu aliutumia upinde wa mvua kuanzisha agano na binadamu, ambapo Aliuweka upinde wa mvua katika mawingu ili kumwambia binadamu kuwa Yeye Hatawahi tena kutumia gharika kuangamiza ulimwengu. Je, upinde wa mvua tunaouona leo, bado ndio uleule uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu? Je, asili na maana yake vimebadilika? Bila shaka, havijabadilika. Mungu alitumia mamlaka Yake ili kutekeleza kitendo hiki, na agano Aliloanzisha na binadamu limeendelea hadi leo, na muda ambao agano hili litabadilishwa, bila shaka, ni uamuzi wa Mungu. Baada ya Mungu kutamka “Nauweka upinde wangu wa mvua mawinguni,” siku zote Mungu alifuata agano hili, Alilifuata hadi leo. Unaona nini katika haya? Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, Ana msimamo sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Msimamo Wake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na kutoweza kushindwa kwa mamlaka ya Muumba. Ingawa Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Bilas haka, kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Machoni pa Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi katika utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatekelezwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na yasiyokosewa kukosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!

Maneno yaliyo hapa chini ni ya lazima katika kujua mamlaka ya Mungu, na maana yake yametolewa kwenye ushirika ulio hapa chini. Hebu tuendelee kuyasoma Maandiko.

4. Amri ya Mungu kwa Shetani

Ayubu 2:6 Na Yehova akamwambia kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio

Hili ni dondoo kutoka katika Kitabu cha Ayubu, na “yeye” katika maneno haya inamrejelea Ayubu. Ingawa imeandikwa kwa muhtasari, sentensi hii inaelezea masuala mengi. Inafafanua mabadilishano fulani kati ya Mungu na Shetani kwenye ulimwengu wa kiroho, na inatwambia kuwa mlengwa wa maneno ya Mungu alikuwa ni Shetani. Pia inarekodi kile kilichosemwa hasa na Mungu. Maneno ya Mungu yalikuwa amri na shurutisho kwa Shetani. Maelezo mahususi ya shurutisho hili ni kuhusiana na kuuhifadhi uhai wa Ayubu na pale ambapo Mungu aliweka masharti ya jinsi ambavyo Shetani alipaswa kumtendea Ayubu—Shetani alilazimika kuuhifadhi uhai wa Ayubu. Kitu cha kwanza tunachojifunza kutoka kwenye sentensi hii ni kwamba matamshi haya yalitamkwa na Mungu kwa Shetani. Kulingana na maandiko halisi ya Kitabu cha Ayubu, yanatwambia usuli wa matamshi kama hayo: Shetani alitaka kumshutumu Ayubu, na hivyo lazima angepokea huo mkataba wa Mungu kabla hajamtia majaribuni. Alipokubali ombi la Shetani la kumjaribu Ayubu, Mungu aliweza kumtajia Shetani sharti lifuatalo: “Ayubu yuko mkononi mwako; lakini uuhifadhi uhai wake.” Ni nini asili ya maneno haya? Ni wazi kwamba ni amri, ni shurutisho. Baada ya kuelewa asili ya maneno haya, unafaa, bila shaka, kufahamu pia kwamba Aliyetoa shurutisho hili ni Mungu, na kwamba aliyepokea amri hii, na akaitii, ni Shetani. Bilas haka, katika shurutisho hili, uhusiano kati ya Mungu na Shetani uko wazi kwa yeyote ambaye anasoma maneno haya. Bila shaka, huu ndio uhusiano kati ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na tofauti kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani iliyoelezwa katika rekodi za mabadilishano ya mazungumzo ya Mungu na Shetani katika Maandiko, na, hadi leo, ni mfano mahususi na rekodi ya maandishi ambapo binadamu anaweza kujifunza tofauti kuu kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani. Katika hatua hii, ni lazima Niseme kwamba, rekodi ya maneno haya ni waraka muhimu sana katika ufahamu wa binadamu juu ya hadhi na utambulisho wa Mungu, na inatoa taarifa muhimu kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Kupitia mabadilishano haya ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, mwanadamu anaweza kuelewa kipengele kimoja mahususi zaidi katika mamlaka ya Muumba. Maneno haya ni ushuhuda mwingine wa kuonyesha mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Kwa nje, Yehova Mungu yuko katika mazungumzo na Shetani. Kwa kuzingatia kiini, mtazamo ambao Yehova Mungu anaongea, na nafasi ambayo Anasimama ni ya juu zaidi kuliko ya Shetani. Hivi ni kusema kwamba Yehova Mungu anamwamuru Shetani na sauti ya kushurutisha, na Anamwambia Shetani ni nini anachopaswa kufanya na asichopaswa kufanya, kwamba tayari Ayubu yu mikononi mwake, na yuko huru kumfanya Ayubu vyovyote atakavyo—lakini asiuchukue uhai wa Ayubu. Ujumbe hapa ni kwamba, ingawa Ayubu amewekwa katika mikono ya Shetani, uhai wake haujakabidhiwa kwa Shetani; hakuna anayeweza kuuchukua uhai wa Ayubu kutoka mikononi mwa Mungu isipokuwa ameruhusiwa na Mungu. Mtazamo wa Mungu unaelezwa waziwazi katika amri hii kwa Shetani, na amri hii pia inadhihirisha na kufichua nafasi ambayo Yehova Mungu anazungumza na Shetani. Katika haya, Yehova Mungu hashikilii tu hadhi ya Mungu aliyeumba nuru, na hewa, na vitu vyote na viumbe hai, au ya Mungu anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote na viumbe hai, lakini pia ya Mungu ambaye Anawaamuru wanadamu, na kuamuru Jehanamu, Mungu ambaye anadhibiti uhai na kifo cha viumbe vyote vilivyo hai. Katika ulimwengu wa kiroho, ni nani mbali na Mungu ambaye angethubutu kutoa shurutisho kama hilo kwa Shetani? Na ni kwa nini Mungu Mwenyewe Alitoa agizo Lake kwa Shetani? Kwa sababu uhai wa binadamu, pamoja na ule wa Ayubu, unadhibitiwa na Mungu. Mungu hakumruhusu Shetani adhuru au achukue uhai wa Ayubu, hivyo ni kusema kwamba kabla ya Mungu kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu bado alikumbuka kutoa shurutisho maalum kama hilo, na kwa mara nyingine Akamwamuru Shetani asiuchukue uhai wa Ayubu. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea Shetani, na hivyo Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka hiyo. Je, huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Shetani ana ufahamu wa wazi zaidi kuliko wanadamu kuhusu jinsi ya kuenenda mbele za Mungu, na jinsi ya kumtazama Mungu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazoongoza utekelezaji wa mamlaka Yake. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote ile. Ingawa ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa mamilioni ya miaka, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kuvuka alama hiyo. Ingawa ni mwovu, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maagizo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba ni kwa sababu hasa ya upekee na mamlaka ya Mungu ndio maana vitu vyote vinabadilika na kuzaliana katika njia ya mpangilio, kwamba wanadamu wanaweza kuishi na kuongezeka ndani ya mkondo uliowekwa na Mungu, hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kuvuruga mpangilio huu, na hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.

Ni Mungu Pekee, Aliye na Utambulisho wa Muumba, Anayemiliki Mamlaka ya Kipekee

Ule utambulisho maalum wa Shetani umewafanya watu wengi waonyeshe kupendezwa sana na udhihirisho wake wa vipengele mbalimbali. Kuna hata watu wengi wapumbavu wanaoamini kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani Shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwa Shetani moyoni mwake, na hata anamwabudu Shetani kama Mungu. Watu wote hawa ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya ujinga wao, na ni wa kuchukiwa kwa sababu ya uzushi wao na asili yao ovu. Kwa wakati huu, Ninahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yanaashiria ukuu na kiini cha Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani atathubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani atathubutu kusema kwamba aliumba vitu vyote, na anashikilia ukuu juu ya vitu vyote? Bila shaka hawezi! Kwa sababu hawezi kuumba vitu vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote chenye uhai. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hawezi kamwe kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hii inaamuliwa na kiini chake. Je, anazo nguvu sawa na za Mungu? Bila shaka hana! Je, tunaitaje matendo ya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Je, inaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka sivyo! Shetani anaongoza wimbi la uovu, na kuvuruga, kuharibu, na kuingilia kila kipengele cha kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kuwapotosha na kuwanyanyasa wanadamu, na kumrubuni na kumdanganya mwanadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na kumkataa Mungu, ili mwanadamu atembee kwenye bonde la uvuli wa mauti, je, Shetani amefanya jambo lolote linalostahili hata kuadhimishwa, kupongezwa, au kuthaminiwa na mwanadamu? Kama Shetani angekuwa na mamlaka na nguvu, je, wanadamu wangepotoshwa naye? Kama Shetani angekuwa na mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani anamiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu kiini cha kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani anafanya kama hila tu, ilhali Ninaamini kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, matendo maovu ya upotoshaji wake wa mwanadamu ni hila tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake la kikatili la kumnyanyasa na kumwangamiza, lisingeweza kutimizwa kwa hila tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali katika milima na vilima, walitoweka; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ulitoweka. Je, inawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kwa hila tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani anafanya yanalingana na kuingiliana na mambo mabaya kama vile kudhoofisha, kuvuruga, kuharibu, kudhuru, uovu, nia mbaya, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanaunganishwa bila kutenganishwa na matendo ya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na kiini kiovu cha Shetani. Haijalishi jinsi Shetani “alivyo na nguvu”, haijalishi jinsi Shetani alivyo jasiri na mwenye tamaa ya makuu, haijalishi jinsi uwezo wake ulivyo mkubwa katika kusababisha uharibifu, haijalishi jinsi zilivyo nyingi mbinu anazotumia kumpotosha na kumshawishi mwanadamu, haijalishi jinsi zilivyo mahiri hila na njama zake anazotumia kumtishia mwanadamu, haijalishi jinsi mfumo wa kuwepo kwake unavyoweza kubadilika, hajawahi kuweza kuumba hata kiumbe kimoja kilicho hai, hajawahi kuweza kuweka sheria au kanuni za kuwepo kwa vitu vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kitu chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Katika ulimwengu na anga, hakuna hata mtu au kitu kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kitu kimoja ambacho kinatawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume chake ni kwamba, sio tu kuwa hana budi kuishi chini ya utawala wa Mungu, lakini, vilevile, lazima atii masharti na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembe ya mchanga juu ya nchi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata uhuru wa kusogeza mchwa wanaotembea juu ya nchi, licha ya wanadamu, ambao waliumbwa na Mungu. Machoni pa Mungu, Shetani ni duni kuliko yungiyungi mlimani, kuliko ndege warukao angani, kuliko samaki wa baharini, na kuliko funza juu ya nchi. Jukumu lake miongoni mwa vitu vyote ni kutumikia vitu vyote, kuwatumikia wanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Haijalishi jinsi asili yake ilivyo na nia mbaya, na jinsi kiini chake kilivyo kiovu, kitu pekee anachoweza kufanya ni kutii jukumu lake: kuwa mtoa huduma kwa Mungu, na kutoa kipingamizi kwa Mungu. Hicho ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Asili yake haijaunganishwa na maisha, haijaunganishwa na nguvu, haijaunganishwa na mamlaka; ni kitu tu cha kuchezea mikononi mwa Mungu, ni mashine tu ya kutoa huduma kwa Mungu!

Baada ya kuelewa uso wa kweli wa Shetani, watu wengi bado hawajaelewa ni nini maana ya mamlaka, hivyo basi wacha Mimi nikuelezee! Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni chanya. Hazina uhusiano na kitu chochote kilicho kibaya, na hazina uhusiano na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba kusemwa kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni chanya. Hazina uhusiano na kitu chochote kilicho kibaya, na hazina uhusiano na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe vyote vyenye uhai. Zaidi ya hayo, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuongezeka kwa amri ya Mungu, kisha, Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote vyenye uhai, na hakutakuwa na kupotoka, milele na milele. Hakuna mtu au kitu chenye vitu hivi; ni Muumba pekee ndiye Anayemiliki na kubeba nguvu kama hizo, na hivyo yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au kiini cha mamlaka hayo, kila moja inaweza tu kuhusishwa na Muumba, kwa sababu ni ishara ya utambulisho wa kipekee na kiini cha Muumba, na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba; mbali na Muumba, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka.” Hii ni tafsiri ya mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Ingawa Shetani alimtazama Ayubu kwa macho ya tamaa, bila ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja kwenye mwili wa Ayubu. Ingawa Shetani kwa asili ni mwovu na mkatili, baada ya Mungu kutoa agizo lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo ila kutii amri yaMungu. Na kwa hivyo, hata Ingawa Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwa-mwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka maagizo ya Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba Shetani hathubutu kukiuka matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwa Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni amri, na sheria ya mbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za mbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka maagizo ya Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za mbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwa Ayubu vilikuwa ni mfano mdogo tu wa upotoshaji wake kwa mwanadamu, na Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, mipaka ambayo Mungu aliweka na maagizo ambayo Alitoa kwa Shetani ilikuwa ni mfano mdogo tu wa kanuni zilizo nyuma ya kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa Shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa vitu vyote, ikiwa ni pamoja na Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kitu kinachoweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za mbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa vitu vyote, na hivyo, haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkuu na Shetani ni namba mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwingine.

Je, sasa una maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu? Kwanza, je, kuna tofauti kati ya mamlaka ya Mungu yaliyotajwa hivi punde na nguvu za binadamu? Na tofauti ni nini? Baadhi ya watu wanasema kwamba hakuna ufanano wowote kati ya hizo mbili. Hiyo ni sahihi! Ingawa watu wanasema hakuna ufanano kati ya hizo mbili, katika fikira na dhana za binadamu, nguvu za binadamu mara nyingi zinadhaniwa kuwa mamlaka, na haya mawili yanalinganishwa sambamba mara nyingi. Ni nini kinachoendelea hapa? Je, si watu wanafanya kosa la kubadilisha moja kwa nyingine bila kujua? Vitu hivi viwili havina uhusiano wowote na hakuna ufanano wowote kati yavyo, ilhali watu bado hawawezi kuelewa. Je, hili linapaswa kutatuliwaje? Kama unapenda kwa kweli kupata suluhu, njia ya pekee ni kuelewa na kujua mamlaka ya kipekee ya Mungu. Baada ya kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, hutataja kwa mkupuo mmoja nguvu za binadamu na mamlaka ya Mungu.

Nguvu za binadamu zinarejelea nini? Kwa ufupi, ni uwezo au mbinu inayowezesha tabia potovu, matamanio na malengo ya binadamu kuweza kupanuliwa au kutimizwa hadi kiwango cha juu zaidi. Je, hii inaweza kuhesabiwa kama mamlaka? Haijalishi ni vipi ambavyo malengo na matamanio ya binadamu yalivyo makubwa au yenye faida, mtu huyu hawezi kusemekana amemiliki mamlaka; kwa kiasi kikubwa, haya majivuno na ufanisi ni maonyesho tu ya upumbavu wa Shetani miongoni mwa binadamu; zaidi sana, ni upuuzi ambao Shetani anaendeleza kama babu yake mwenyewe ili kutimiza maono yake ya kuwa Mungu.

Je, unayatazama vipi hasamamlaka ya Mungu sasa? Kwa vile sasa maneno haya yamezungumziwa kwenye ushirika, unapaswa kuwa na maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu. Na kwa hivyo Ninakuuliza: Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Je, uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, kuna mtu yeyote anayeweza kubadilisha sheria ya mabadiliko kati ya machipuko, kiangazi, vuli na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti inaweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika vuli inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka. Je, yupo anayeweza kubadilisha sheria hii? Je, hii inaonyesha kipengele kimoja cha mamlaka ya Mungu? Mungu alisema “Iwe Nuru,” na ikawa nuru. Je, nuru hii ingali ipo? Nuru hii inakuwepo kwa sababu ya nini? Inakuwepo kwa sababu ya maneno ya Mungu, bila shaka, na kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Je, hewa iliyoumbwa na Mungu bado ipo? Je, hewa ambayo binadamu anapumua inatoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kuchukua vitu vinavyotoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha asili na kazi zao? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha mpangilio wa usiku na mchana kama ulivyopangwa na Mungu, na sheria ya usiku na mchana kama ilivyoamrishwa na Mungu? Je, Shetani anaweza kufanya kitu kama hicho? Hata kama hulali wakati wa usiku, na unachukulia usiku kuwa wakati wa mchana, basi bado ni wakati wa usiku; unaweza kubadilisha mazoea yako ya kila siku, lakini huwezi kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya usiku na mchana—ukweli huu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote, sivyo? Je, kuna yeyote anayeweza kumfanya simba alime ardhi kama ng'ombe? Je, kuna mtu yeyote anayeweza kumbadilisha tembo kuwa punda? Je, kuna mtu yeyote anayeweza kumfanya kuku apae hewani kama tai? Je, kuna yeyote anayeweza kumfanya mbwa-mwitu alenyasi kama kondoo? (La.) Je, yupo anayeweza kumfanya samaki aliye majini kuishi kwenye ardhi kavu? Hilo haliwezi kufanywa na wanadamu. Na kwa nini haiwezekani? Ni kwa sababu Mungu aliwaamuru samaki kuishi ndani ya maji, na kwa hivyo wanaishi ndani ya maji. Kwenye ardhi kavu hawataweza kuishi kwani watakufa; hawawezi kukiuka mipaka ya amri ya Mungu. Vitu vyote vina sheria na mipaka ya kuwepo kwao, na kila mojawapo kina silika zake binafsi. Haya yameamriwa na Muumba, na hayawezi kubadilishwa na kukiukwa na binadamu yeyote. Kwa mfano, simba siku zote ataishi porini, umbali fulani kutoka kwenye jumuia ya binadamu, na hatawahi kuwa mtulivu na mwaminifu kama vile ng’ombe alivyo na anavyoishi na kumfanyia binadamu kazi. Ingawa ndovu na punda ni wanyama, na wote wana miguu minne, na ni viumbe vinavyopumua hewa, wao ni aina tofauti, kwa kuwa waligawanywa katika aina aina tofauti na Mungu, kila mmoja wao anazo silika zake binafsi, na hivyo hawatawahi kubadilishana. Ingawa kuku ana miguu miwili, na mabawa kama vile alivyo tai, hatawahi kuweza kupaa hewani; kama amejaribu sana anaweza tu kupaa hadi kwenye mti—na hili linaamuliwa na silika yake. Sina haja kusema, haya yote ni kwa sababu ya amri za mamlaka ya Mungu.

Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemwa kwamba imeongezeka, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kuwa mkubwa zaidi, lakini kuna utafiti mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kuufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vifaa vya angani, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu cha teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwao na mzunguko wa maisha na kifo cha kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemwe kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kuna bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliweka mipaka kwa kila moja ya bahari hizo; zilikaa popote pale Alipoziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kuzunguka kwa uhuru. Bila ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia inaamuliwa na mamlaka ya Mungu.

Ili kuiweka kwa uwazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” ina maana kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni juu ya Mungu, na sio juu ya mwanadamu; wala haiwezi kubadilishwa na mwanadamu. Haiwezi kubadilishwa kwa mapenzi ya mwanadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na huu ni ukweli usiopingika kwa binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, kile kinachoonekana na kisichoonekana kwa mwanadamu-vyote vipo, vinafanya kazi, na vinabadilika bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na maagizo ya awali ya Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Hakuna mtu au kitu hata kimoja kinachoweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu. Sasa kwa sababu haya yote yamesemwa, je, unahisi kwamba mamlaka ya Mungu ni ishara ya utambulisho na hadhi ya Mungu? Je, mamlaka ya Mungu yanaweza kumilikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au ambacho hakijaumbwa? Je, yanaweza kuigwa, kufananishwa, au kubadilishwa na mtu yeyote, na kitu chochote, au kifaa chochote?

Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hupaswi Kufuata Wazo la Imani ya Miungu Wengi

Ingawa mbinu na uwezo wa Shetani ni mkubwa zaidi kuliko ule wa mwanadamu, ingawa anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyafanya, bila kujali kama unaonea wivu au unatamani kile ambacho Shetani anafanya, bila kujali kama unachukia au unachukizwa na kile anachofanya, bila kujali kama unaweza au huwezi kuona hicho, bila kujali kiwango ambacho Shetani anaweza kutimiza, au ni watu wangapi anaoweza kuwadanganya ili wamwabudu na kumtolea kafara, na bila kujali jinsi unavyomfafanua, hauwezi kusema kwamba Shetani ana mamlaka na nguvu za Mungu. Unapaswa kujua kwamba Mungu ni Mungu, tunaye Mungu mmoja tu, na zaidi ya yote unafaa kujua kwamba ni Mungu tu aliye na mamlaka, na kwamba Anazo nguvu za kudhibiti na kutawala vitu vyote. Eti kwa sababu Shetani anao uwezo wa kuwadanganya watu, na anaweza kujifanya kuwa Mungu, na anaweza kuiga ishara na miujiza inayofanywa na Mungu, na amefanya mambo yanayofanana na yale ya Mungu, wewe unasadiki kimakosa kwamba Mungu si wa kipekee, kwamba kuna Miungu mingi, kwamba Miungu hii tofauti ina ujuzi mkubwa au mdogo tu, na kwamba kuna utofauti katika upana wa nguvu wanazotumia. Unapangilia ukuu wao katika mpangilio wa kuwasili kwao, na kulingana na umri wao, na unasadiki kimakosa kwamba kuna miungu mingine mbali na Mungu, na unafikiri kwamba nguvu na mamlaka ya Mungu si ya kipekee. Kama unazo fikira kama hizo, kama hutambui upekee wa Mungu, husadiki ni Mungu pekee anayemiliki mamlaka, na kama utadumu tu katika kushikilia imani ya kuabudu miungu wengi, basi Nasema kwamba wewe ni duni kabisa kuliko viumbe wote, wewe ni mfano halisi wa Shetani, na wewe ni mtu kamili wa maovu! Je, unaelewa kile Ninachojaribu kukufundishaa kwa kusema maneno haya? Haijalishi ni wakati gani, mahali, au historia yako, hupaswi kumchanganya Mungu na mtu mwingine yeyote, kitu, au kifaa chochote. Bila kujali jinsi unavyohisi kwamba mamlaka ya Mungu na kiini cha Mungu Mwenyewe haviwezi kujulikana wala kuweza kufikiwa, haijalishi ni kiwango kipi cha matendo na maneno ya Shetani yanavyokubaliana na mawazo na fikira zako, haijalishi ni vipi ambavyo mambo haya yanakutosheleza wewe, usiwe mjinga, usichanganye vipengele hivi, usikatae uwepo wa Mungu, usikatae utambulisho na hadhi ya Mungu, usimsukume Mungu nje ya mlango na kumleta Shetani kuchukua nafasi ya “Mungu” aliye ndani ya moyo wako na kuwa Mungu wako. Sina shaka kwamba una uwezo wa kufikiria matokeo ya kufanya hivyo!

Ingawa Binadamu Amepotoka, Bado Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba

Shetani amekuwa akiwapotosha wanadamu kwa maelfu ya miaka. Ametenda maovu mengi sana, amepotosha kizazi baada ya kizazi, na amefanya uhalifu wa kutisha duniani. Amemdhulumu mwanadamu, kumpotosha mwanadamu, kumshawishi mwanadamu kumpinga Mungu, na amefanya matendo maovu ambayo yamesumbua na kuharibu mpango wa usimamizi wa Mungu mara kwa mara. Hata hivyo, chini ya mamlaka ya Mungu, vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Ikilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata Ingawa Shetani anatembea kati ya vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia vitu vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku bado zinabadilishana bila kukoma; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje juu ya nchi wanaimba kwa mioyo yao kwenye siku za kiangazi; chenene kwenye nyasi wanaimba kwa sauti za polepole huku wakikaribisha msimu wa vuli, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia peke yao; makundi ya simba yanajitosheleza yenyewe kwa kuwinda; nao kulungu hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni moja yanatokea kwa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kuishi. Wanaishi chini ya riziki na usitawishaji wa Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawa mwanadamu, anayeishi miongoni mwa vitu vyote, amepotoshwa na kudanganywa na Shetani, mwanadamu bado hawezi kuacha maji yaliyoumbwa na Mungu, na, na, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu bado anaishi na kuzaliana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu bado hazijabadilika. Binadamu bado anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na nyayo zake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali utoaji wa Mungu umebaki bila kubadilishwa, uwezo ambao kupitia huo mwanadamu anashirikiana na Mungu haujabadilika, uwezo wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili yake haijabadilika, shauku ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi chini ya mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawa mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena ambao waliumbwa hapo mwanzo, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira, dhana na kadhalika, na amejaa tabia potovu za kishetani, machoni pa Mungu, mwanadamu bado ni mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu bado yuko chini ya ukuu na mipangilio ya Mungu, na bado anaishi ndani ya mkondo uliowekwa na Mungu, na hivyo machoni pa Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya polepole kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na ni ya zamani kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Hawa ndio wanadamu ambao Mungu anakusudia kuwaokoa. Wanadamu hawa wanahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona sura ya Muumba na atapuuzia mengine yote, na kuacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wanadamu wanapofahamu kutoka mioyoni mwao sauti ya moyo wa Muumba, watamkataa Shetani na kuja upande wa Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine tena utolewaji na utunzaji wa Muumba, kumbukumbu ya mwanadamu itarejeshwa na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.

Desemba 14, 2013

Iliyotangulia: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp