Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu

Sasa kwa kuwa mmesikiliza ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Nina imani kwamba mmejitayarisha vilivyo na maneno mengi kuhusiana na suala hili. Kuhusu kiwango unachoweza kukubali, kufahamu, na kuelewa vyote hivi vinategemea kiasi cha jitihada utakazoweka wewe binafsi katika hilo. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kulishughulikia jambo hili kwa bidii; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia kwa shingo upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kumjua Mungu kikamilifu? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe wa kipekee, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango la kujua kiini cha Mungu wa kipekee Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu mojawapo ya kumjua Mungu. Kwa hivyo sehemu ile nyingine ni ipi basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.

Nimechagua sehemu mbili kutoka kwenye Biblia ambazo ningependa tushiriki pamoja kuhusu mada ya leo: Sehemu ya kwanza inahusu kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu, ambayo inaweza kupatikana kwenye Mwanzo 19:1-11 na Mwanzo 19:24-25; sehemu ya pili ni kuhusu wokovu wa Mungu kwa Ninawi, ambayo inaweza kupatikana kwenye kitabu cha Yona 1:1-2, pamoja na sura ya tatu na ya nne ya kitabu hiki. Nadhani kwamba nyinyi nyote mnasubiria kusikia kile Nilicho nacho kuhusu sehemu hizi mbili. Kile Ninachosema hakiwezi kwenda kando na mada ya kumjua Mungu Mwenyewe na kujua kiini Chake, lakini ni nini kitakachokuwa zingatio la ushirika wa leo? Je, yupo yeyote kati yenu anayejua? Ni sehemu zipi za ushirika Wangu kuhusu “Mamlaka ya Mungu” ziliweza kuwavutia? Kwa nini Nilisema kwamba yule tu anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizo ndiye Mungu mwenyewe? Ni nini Nilichotaka kuelezea kwa kusema hivyo? Ni nini ambacho Nilipenda kukufahamisha kuhusu? Je, mamlaka na nguvu za Mungu ni kipengele kimojawapo cha jinsi kiini Chake kinavyoonyeshwa? Je, mamlaka na nguvu hizi ni sehemu ya kiini Chake ambayo inathibitisha utambulisho Wake na hadhi Yake? Je, maswali haya yamekufahamisha kile Ninachoenda kusema? Ni nini Ninachotaka uelewe? Fikiria hili kwa makini.

Kwa Kumpinga Mungu kwa Ukaidi, Mwanadamu Anaangamizwa na Ghadhabu ya Mungu

Kwanza, hebu tuweze kuangalia mafungu mbalimbali ya maandiko yanayofafanua kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu.

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na wakala. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Ondoka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mikono yao, na kumvuta Lutu katika nyumba waliyokuwemo, na kuufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka kwa Yehova mbinguni; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Kutoka kwenye mafungu haya, si vigumu kuona kwamba dhambi ya Sodoma na kupotoka kwake tayari vilikuwa vimefikia kiwango kilichochukiza binadamu na Mungu, na kwamba machoni pa Mungu mji huo ulifaa kuangamizwa. Lakini ni nini kilichotokea ndani ya mji huo hapo awali kabla haujaangamizwa? Ni msukumo upi tunaoweza kupata kutoka kwenye matukio haya? Je, mtazamo wa Mungu katika matukio haya unatuonyesha nini kuhusu tabia yake? Ili kuelewa hadithi nzima, hebu na tuweze kusoma kwa makini kile kilichorekodiwa katika Maandiko …

Kupotoka kwa Sodoma: Kunamkasirisha Mwanadamu, Kunamghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya kula, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua.” Je, ni nani waliosema maneno haya? Je, yalielekezwa kwa nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Je, unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakukera? Je, unachemkwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yanamdhihirisha Shetani? Kupitia kwa maneno haya, je,unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na unyama wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya maneno yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya uwezo wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; kule kuona tu mtu mwingine kuliwafanya watu hawa watake kuwadhuru na kuwateketeza …. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potovu na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za uovu wake na umwagaji wa damu.

Akikabiliana uso kwa uso na kundi la watu wakatili wasio na utu, watu waliokuwa wamejaa tamaa ya kuteketeza nafsi za wanadamu, je, Lutu aliwaambia nini? Kulingana na Maandiko: “Nawaomba … msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kwa sababu yoyote ile inayofaa, watu hawa walipaswa kukubaliana na masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili peke yao; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, kwa kuchochewa na asili yao ya dhambi, hawakuliachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu ufahamu zaidi kuhusu asili ya kikatili iliyopo ndani ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.

Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu ya kuwaletea madhura wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio la wajumbe hao, watu wa mji huo waliegemeza tamaa yao ya kuwadhuru kikatili wajumbe hao wawili kwa makisio yao tu; walitaka kuwadhuru watu hao wawili ambao hawakuwa na uhusiano wowote nao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potovu ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.

Walipodai watu hawa kutoka kwa Lutu, je, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandiko hayo tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawa hakujua sababu ya wao kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwatoa binti zake wawili kuwabadilisha na watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kilikuwa kitendo cha haki cha Lutu; vilevile lilikuwa onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na kiini cha Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alitaka hata awatoe mabinti zake wawili kwa mabadilishano ili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, je, kulikuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya mji huo ambaye angefanya jambo kama hili? Ukweli unathibitisha kwamba: hakuna! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa maangamizo na walipaswa kuangamizwa.

Sodoma Yaangamizwa kwa Kuikosea Ghadhabu ya Mungu

Wakati watu wa Sodoma walipowaona watu hawa wawili, hawakuuliza sababu ya wao kuja wala hakuna yule aliyeuliza kama walikuwa wamekuja kueneza mapenzi ya Mungu. Kinyume cha mambo, walikusanyika na kuwa umati wa watu na, bila kusubiri ufafanuzi wowote, walikuja kuwakamata watumishi hawa wawili ni kana kwamba walikuwa mbwa koko au mbwa mwitu. Je, Mungu aliyatazama mambo haya wakati yalipokuwa yakifanyika? Je, Mungu alikuwa akifikiria nini katika moyo Wake kuhusiana na tabia hii ya binadamu, aina ya jambo kama hili? Mungu aliamua kuangamiza mji huu; Asingesita wala kusubiri, wala Asingeendelea kuonyesha subira yake. Siku yake ilikuwa imetimia, na kwa hivyo Aliweza kuweka wazi kazi Aliyopenda kufanya. Hivyo basi, Mwanzo 19:24-25 inasema, “Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka mbinguni kwa Yehova; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.” Mistari hii miwili inawaambia watu mbinu ambayo kwayo Mungu aliuangamiza mji huu; pia inawaambia watu kile ambacho Mungu alikiangamiza. Kwanza, Biblia inasimulia kwamba Mungu aliteketeza mji kwa moto, na kwamba kiwango cha moto kilitosha kuwaangamiza watu wote na kila kitu kilichomea kwenye ardhi. Hii ni kusema kwamba, moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji; uliangamiza pia watu wote na vitu vilivyo hai ndani yake, vyote bila kuacha chochote nyuma. Baada ya mji kuangamizwa, ardhi ilikuwa tupu bila kitu chochote kilicho hai. Hakukuwa tena na maisha, wala dalili zozote za maisha. Mji ulikuwa umebadilika na kuwa ardhi iliyoharibiwa, mahali patupu palipojaa kimya cha kutisha. Kusingekuwa na matendo maovu zaidi dhidi ya Mungu mahali hapa; kusingekuwa na uchinjaji zaidi au umwagikaji wa damu.

Kwa nini Mungu alitaka kuuchoma mji huu kabisa? Ni nini unachoweza kuona hapa? Je, inawezekana kwamba Mungu hangeweza kustahimili kuona wanadamu na vitu vyote alivyoviumba vikiharibiwa hivi? Kama unaweza kutambua ghadhabu ya Yehova Mungu kutokana na moto ule ambao uliangushwa kutoka mbinguni, basi si vigumu sana kuona kiwango Chake cha hasira kali kutoka kwenye lengo la maangamizo Yake pamoja na kiwango ambacho mji huo uliweza kuangamizwa. Wakati Mungu anadharau mji, Ataweza kutekeleza adhabu Yake juu ya mji huo. Wakati Mungu anachukizwa na mji, Ataweza kutoa maonyo mbalimbali akifahamisha watu kuhusu ghadhabu Yake. Hata hivyo, wakati Mungu anaamua kukomesha na kuangamiza mji—yaani, wakati hasira na heshima Yake vimekosewa—Hataweza tena kutoa maonyo au adhabu nyingine. Badala yake, Ataweza kuuangamiza moja kwa moja. Ataufanya kutoweka kabisa. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu.

Baada ya Upinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Uadui Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Mara tu tunapokuwa na ufahamu wa jumla kuhusu tabia ya haki ya Mungu, tunaweza kurejesha umakinifu wetu kwenye mji wa Sodoma—kile ambacho Mungu aliona kuwa mji wa dhambi. Kwa kuelewa hali halisi ya mji huu, tunaweza kuelewa ni kwa nini Mungu alitaka kuuangamiza na ni kwa nini Aliuangamiza kabisa. Kutokana na haya, tunaweza kujua tabia ya haki ya Mungu.

Kwa mtazamo wa kibinadamu, Sodoma ulikuwa ni mji ambao ungeweza kutosheleza kabisa tamaa za wanadamu na maovu ya wanadamu. Walivutiwa na kutekwa akili zao, kwa muziki na kucheza densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume wavutiwe sana na kutiwa wazimu. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na wakapumbazwa hadi kufikia kukengeuka vibaya. Huu ulikuwa ni mji ambao roho wachafu na roho waovu walicharuka hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda matendo maovu yasiyohesabika ya upinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.

Ingawa vifungu hivi viwili havirekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, kuna ukweli rahisi unaoweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, jinsi walivyojaa maovu na kumpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wanachukia kuwepo kwa Mungu, wanachukia ujio wa Mungu, wanachukia adhabu ya Mungu, na hata zaidi, wanachukia maonyo ya Mungu kwao. Hawakuona kingine chochote chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote maovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao potovu ambayo imefichuliwa kwa kweli inaonekana tu kuwa ni ndogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala hakutumia tufani, tetemeko la ardhi, tsunami au njia nyingine yoyote ya kuuangamiza mji huu. Je, kulimaanisha nini Mungu kuangamiza mji huu kwa kutumia moto Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ungetoweka kabisa kutoka ulimwenguni na ungekoma kabisa katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilikoma kuwepo, zikiwa zimeangamizwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na vitu vyote vilivyohusiana na mji huu viliangamizwa. Kusingekuwa na maisha ya baadaye ama roho zao kupata mwili tena; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka kwa wanadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingekoma kuwepo na kuenea. Ilimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo lilimpatia Shetani mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, Mungu anapotumia moto ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kumpinga Mungu kwa kuwapotosha na kuwadanganya wanadamu. Pia ni ishara ya aibu katika historia ya maendeleo ya binadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.

Wakati ule moto ambao Mungu aliutuma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungekoma kuwepo, na ilimaanisha kwamba kila kitu ndani ya mji huo hakingeonekana tena. Mji uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na ukuu wa Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la Mungu la kutowahi kuutazama tena mji huo” ni ghadhabu Yake, pamoja na ukuu Wake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona tena au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo. Baada ya mji huo kumalizika kuteketea, huku yakiwa yameachwa nyuma majivu pekee, ilikuwa kwa kweli mji huo umekoma kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma na watu waliokua wamejaa maovu ndani yake, wala haukuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji huo ambavyo vilikuwa vimetiwa doa na dhambi; zaidi pia, moto huu uliharibu kumbukumbu za maovu na upinzani wa wanadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudi la Mungu la kuuteketeza mji ule.

Binadamu walikuwa wamepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na wangekufuru. Hata wakati ambao watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba na hawakuacha mwenendo wao wa maovu, lakini kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na kiini chao halisi cha uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba upinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potovu, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la kashfa au dhihaka inayotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingesababisha hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haitakiwi kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliofurika na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alitaka kuwaangamiza kabisa watu waliokuwa ndani yake na dhambi zao zote, ili kuwafanya watu wa mji huu wakome kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa isiongezeke. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kukoma kuwepo.”

Ingawaje Hasira ya Mungu Imefichwa na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Mungu huwashughulikia wanadamu wajinga na wapumbavu kwa huruma na uvumilivu. Lakini, kwa upande mwingine ghadhabu ya Mungu imefichwa mara nyingi na katika matukio mengi, na haijulikani kwa watu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati mwanadamu anapokabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya mwisho ya uvumilivu na msamaha kwa mwanadamu—yaani, wakati tukio la mwisho la Mungu la rehema na onyo Lake la mwisho linapowajia wanadamu—ikiwa watu bado wanatumia mbinu zilezile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali rehema Zake, basi Mungu hataweka tena uvumilivu na subira Yake juu yao. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu atabatilisha rehema Zake wakati huu. Kufuatia haya, Ataituma tu ghadhabu Yake. Anaweza kudhihirisha ghadhabu Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.

Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa binadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya nyama; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangekoma kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni kipengele kimoja cha dutu ya ghadhabu ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Anaacha kufichua rehema au wema wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa rehema Zake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kidogo, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira na adhama Yake, ambavyo binadamu hatakiwi kuvikosea, na pia ni maonyesho ya kipengele kimoja cha tabia Yake ya haki. Wakati watu wanamshuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuona ukuu Wake au kuhisi kutovumilia Kwake kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia binadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona kidogo upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huku ni kutovumilia kosa kwa Mungu. Tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa lolote inapita fikira za kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe visivyoumbwa, hakuna chenye uwezo wa kuiingilia au kuiathiri; hata zaidi, haiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, kipengele hiki cha tabia ya Mungu ndicho ambacho cha tabia ya Mungu ndicho ambacho binadamu anafaa kukijua zaidi. Ni Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo viovu vya Shetani—vya kuwapotosha na kuwaangamiza wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya kiini Chake kitakatifu na kiisicho na doa. Ni kwa sababu ya hali ndiyoHataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumbwa au ambavyo havikuumbwa vimpinge waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu ambaye Aliwahi kumwonea huruma, au wale ambao Aliwachagua, endapo tu wataikasirisha tabia Yake na kukiuka kanuni Zake za subira na uvumilivu, Yeye bila huruma na bila kusita Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki ambayo haiwezi kuvumilia kosa lolote.

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Kwa kuielewa mifano hii ya unenaji wa Mungu, fikira na vitendo vya Mungu, je, unaweza kuielewa tabia ya haki ya Mungu, tabia isiyoweza kukosewa? Mwishowe, hiki ni kipengele cha tabia ya kipekee kwa Mungu Mwenyewe, bila ya kujali ni kiwango kipi ambacho binadamu anaweza kuelewa. Mungu kutoweza kuvumilia kosa ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; ukuu wa Mungu ndiyo kiini Chake cha kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Ni dhahiri kwamba pia ni ishara ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ni asili Yake Mwenyewe, ambayo haibadiliki hata kidogo na kupita kwa wakati, na wala haibadilishwi na mabadiliko ya eneo la kijiografia. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Bila kujali ni nani Anayemfanyia kazi Yake juu yake, kiini Chake hakibadiliki, na wala tabia Yake ya haki haibadiliki. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika kiini Chake au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini ni kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anaijaribu ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapoijaribu mara kwa mara ghadhabu ya Mungu—na pia wakati ambapo dhambi inaenea—ghadhabu ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitakoma kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote za adui zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu unapopingwa, wakati nguvu za haki zinapozuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya kiini cha Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na zinapozuiliwa na kutoonekana na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu Asiye na dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.

Ingawa kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni kipengele kimojawapo cha onyesho la tabia Yake ya haki, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au isiyo na kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa hasira hata kidogo, na wala Yeye hakimbilii kufichua ghadhabu Yake na ukuu Wake kirahisi. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya Yeye kusikia maneno waliyomwambia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu aweze kusihi kwa niaba yao na kuwaombea, na Mungu Mwenyewe hakuyachukua makosa yao moyoni Mwake. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo wa kimsingi ambao Mungu huwachukulia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kuachiliwa kwa ghadhabu ya Mungu si onyesho la hali Yake, wala si njia Yake ya kuonyesha hisia Zake. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu haachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho na udhihirisho kamili wa tabia Yake ya haki, na ni ishara ya ufunuo wa kiini Chake kitakatifu. Mungu ni mwenye hasira, Asiyevumilia kukosewa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu waliopotoka ambao wana umiliki wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii kati ya sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Mwanadamu atawaka kwa hasira na kutoa hisia zake ili kutetea na kudumisha uwepo wa dhambi, na vitendo hivi ni njia ambazo mwanadamu huonyesha kutoridhika kwake; wamejawa na uchafu, njama na fitina, upotovu na uovu wa wanadamu, na zaidi ya kitu kingine chochote, wamejawa na malengo na tamaa mbaya za wanadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, hasira ya mwanadamu haitawaka ili kutetea uwepo wa haki; kinyume chake ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kuliondoa. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, mwanadamu anapolipukwa na hasira ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiozuilika kwa mwandamu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote zinazomdhuru mwanadamu zitasitishwa; nguvu zote za uadui zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; na watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kupotshwa naye; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ruzuku ya Mungu katika mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni ulinzi unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kuenezwa kwa nguvu, na pia ni ulinzi unaolinda kuwepo na kuenezwa kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.

Je, unaweza kuona kiini cha ghadhabu ya Mungu katika kuangamiza Kwake Sodoma? Je, kuna kitu chochote kililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Kwa kutumia maneno ya kibinadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa unajisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kuna njama yoyote? Je, kuna siri yoyote iliyofichwa? Ninaweza kukuambia kwa uwazi na kwa kweli: Hakuna sehemu yoyote ya ghadhabu ya Mungu ambayo inaweza kumsababishia mtu kuitilia shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa unajisi na haina nia au kusudi lingine lolote. Sababu zilizo nyuma ya ghadhabu Yake ni safi, hazina lawama na haziwezi kukosolewa. Ni ufunuo wa asili na onyesho la kiini Chake kitakatifu; ni kitu ambacho hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa kinachoimiliki. Hii ni sehemu ya kipekee ya tabia ya haki ya Mungu, na pia ni tofauti kubwa kati ya kiini cha Muumba na viumbe vilivyoumbwa.

Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira zao au kulinda sura zao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapotaka bila kujizuia hata kidogo. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishini kusudi gani, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na kiini chake ambacho kinalingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira ya binadamu wapotovu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ubaguzi, tabia ya mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani huanza na tamanio la kulinda upotovu, na kwa hakika ina msingi katika upotovu; hii ndiyo sababu, hasira ya mwanadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na ghadhabu ya Mungu, haijalishi jinsi hasira ya mwanadamu inaweza kuonekana kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za uovu hudhibitiwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Lengo la hasira ya Mungu si kulinda hadhi na utambulisho Wake mwenyewe, bali ni kulinda uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, ili kulinda sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni ufunuo sahihi sana wa asili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna nia potovu katika ghadhabu Yake, na wala hakuna udanganyifu au njama zozote, achilia mbali tamaa, hila, udhalimu, vurugu, uovu au tabia zingine zozote ambazo binadamu wote waliopotoka huwa nazo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua kiini cha kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila kitu Anachofanya ni wazi kabisa, kama vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hiki ndicho kipengele cha kivitendo cha ghadhabu ya Mungu, na ni kwa sababu ya kipengele hiki cha kivitendo cha ghadhabu ya Mungu kwamba ubinadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu wangeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, vyema na vizuri vingeangamizwa na kukoma kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na amri za kuwepo kwa viumbe vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki ili kulinda na kudumisha maisha ya kawaida ya binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na uadhama, watu wote waovu, mambo, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Katika kipindi cha milenia kadhaa zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na ambao wanachukua nafasi ya wasaidizi na watumishi wa Shetani katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu za haki zaidi miongoni mwa wanadamu hazijawahi kuharibiwa.

Sasa kwa kuwa unao ufahamu wa kiini cha ghadhabu ya Mungu, bila shaka lazima utakuwa na ufahamu bora zaidi wa namna ya kutofautisha maovu ya Shetani!

Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuwadanganya watu. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anatetea haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kuwapotosha na kuwachochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu aidhinishe na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za kuwa mwema na kuondoa baraka zake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kuwaangamiza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ukatili wake; tamanio lake la kuwadhuru na kuwameza watu ndipo litazidi zaidi. Anakasirika kwasababu ya mwamko wa mwanadamu katika kufuata ukweli; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka katika gereza lake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kikatili.

Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake ya uovu. Kati ya matendo yote maovu ambayo Shetani ameyafanya juu ya mwanadamu—kuanzia kwa jitihada zake za awali za kumdanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, hadi ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kumtambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua kiini kiovu cha Shetani; hakuna hata kimoja kinachoshindwa kuthibitisha ukweli kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata kimoja kinachoshindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inayalinda maovu yake, inadumisha uendelevu wa vitendo vyake viouvu inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Matendo haya ya Shetani ni uadui kwa Mungu, na yataangamizwa na ghadhabu ya Mungu. Ingawa Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake ni njia tu ya kudhihirisha asili yake mbaya. Sababu inayomfanya Shetani akasirike na kuwa mkali ni kwa sababu njama zake zilizofichika zimefichuliwa; mipango yake haiwezi tena kufanikiwa kwa urahisi; malengo yake ya kijinga na tamaa yake mbaya ya kuchukua nafasi ya Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila wakati ambao hasira ya Mungu inaachiliwa huwa haifichui tu sura ya kweli ya Shetani iliyo mbaya; bali pia inafichua na kuweka wazi tamaa mbaya ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Mlipuko wa hasira ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huashiria ulinzi na mwendelezo wa mambo mazuri, na huashiria asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!

Mtu Hapaswi Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Ukijipata unakabiliwa na hukumu na kuadibiwa na Mungu, je, utasema kwamba neno la Mungu limeghushiwa? Je, utasema kwamba kunayo hadithi inayoelezea kuhusu ghadhabu ya Mungu, na kwamba ghadhabu Yake imetiwa unajisi? Je, utamchafulia Mungu jina, ukisema kwamba tabia Yake si ya haki kwa ujumla? Wakati unaposhughulikia kila mojawapo ya vitendo vya Mungu, lazima uwe na uhakika kwamba tabia ya haki ya Mungu iko huru dhidi ya vipengele vingine vyovyote, kwamba ni takatifu na haina dosari; vitendo hivi vinajumuisha binadamu kuweza kuangushwa chini, kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu. Bila kuacha, kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu kinatekelezwa kulingana na tabia yake ya asili na mpango Wake—hii haijumuishi maarifa ya binadamu, mila na falsafa—na kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake na kiini Chake, kisichohusiana na chochote kinachomilikiwa na binadamu aliyepotoka. Mwanadamu ana dhana kwamba upendo, huruma na uvumilivu wa Mungu pekee kwa binadamu ndivyo visivyokuwa na dosari, visivyoghoshiwa na vilivyo vitakatifu. Hata hivyo, hakuna anayejua kwamba ghadhabu ya Mungu na hasira Yake vilevile vyote havijatiwa unajisi; aidha, hakuna yule aliyefikiria maswali kama vile: kwa nini Mungu havumilii kosa lolote au kwa nini ghadhabu Yake ni kubwa mno. Kinyume ni kwamba, baadhi ya watu hukosa kuelewa hasira ya Mungu na kudhania kuwa ni hasira kali sawa na ile ya binadamu waliopotoka: wanaelewa ghadhabu ya Mungu kuwa ni sawa na hasira za binadamu waliopotoka; wao hata hudhania kimakosa kwamba ghadhabu ya Mungu ni sawa tu na ufunuo wa kiasili wa tabia potovu ya binadamu. Wanasadiki kimakosa kwamba ghadhabu ya Mungu inapoachiliwa ni sawa tu na ghadhabu ya binadamu waliopotoka, jambo linalotokana na kutoridhika; wanasadiki hata kwamba Mungu anapoachilia ghadhabu Yake ni maonyesho ya hali Yake ya moyo. Baada ya ushirika huu, Ninatumai kwamba kila mmoja wenu hatakuwa tena na shaka, fikira au kukisia kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na Natumai baada ya kusikiliza maneno Yangu mnaweza kuwa na utambuzi wa kweli wa ghadhabu ya tabia ya haki ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba mnaweza kuweka kando ufahamu wowote potofu wa hapo awali kuhusiana na ghadhabu ya Mungu, na kwamba mnaweza kubadilisha imani zenu zilizopotoka na maoni yenu potovu kuhusiana na kiini cha ghadhabu ya Mungu. Vilevile, Natumai kwamba mnaweza kuwa na ufafanuzi sahihi wa tabia ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba hamtakuwa tena na mashaka yoyote kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na kwamba hamtaweka mawazo ama fikira zozote za kibinadamu kuhusiana na tabia ya kweli ya Mungu. Tabia ya haki ya Mungu ni kiini cha kweli cha Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuundwa na binadamu. Tabia Yake ya haki ni tabia Yake na haina uhusiano au muunganiko wowote na kiumbe chochote kilichoumbwa. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na kiini Chake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si sawa na kujua kitu; kumjua Mungu si kuchunguza kitu, na wala si sawa na kumwelewa mtu. Kama mwanadamu atatumia dhana au mbinu yake ya kujua kifaa au kumwelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na kiini cha kweli cha Mungu. Hutawahi kamwe kufanikiwa kama utategemea mawazo yako ili kuelewa kiini cha Mungu. Njia ya pekee ni hii: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya njaa na kiu yako ya kupenda ukweli. Na kwa haya, hebu na tuhitimishe sehemu hii ya mazungumzo yetu.

Binadamu Hupata Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya Dhati

Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”

Yona 1:1-2 Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele Yangu.

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu Yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Aakulifanya.

Yona 4 Lakini lilimwudhi Yona mno, naye alikuwa na hasira sana. Na akaomba kwa Yehova, na kusema, Nakuomba, Ee Yehova, hivi sivyo nilivyonena, nilipokuwa bado katika nchi yangu? Kwa hivyo nilitorokea Tarshishi kabla: kwa sababu nilijua kwamba Wewe ni Mungu wa neema, na mwenye huruma, asiyekasirika haraka, na wa rehema kubwa, na Wewe unaghairi maovu. Kwa hivyo sasa, Ee Yehova, chukua, nakusihi, uhai wangu kutoka kwangu; kwa sababu ni heri nikufe kuliko kuishi. Kisha Yehova akasema, Je, unafanya vizuri kukasirika? Hivyo Yona akatoka nje ya mji, na kuketi katika upande wa mashariki wa mji, na huko akajitengenezea kibanda, na akaketi chini yake katika kivuli, mpaka aweze kuona kile kingefanyikia mji huo. Naye Yehova Mungu akatayarisha mtango, na akaufanya ukuje juu yake Yona, ili uweze kuwa kivuli juu ya kichwa chake, na kumwokoa kutoka katika huzuni yake. Kwa hivyo Yona akawa na furaha sana juu ya ule mtango. Lakini Mungu akatayarisha buu siku iliyofuata wakati kulipopambazuka, nalo likaula ule mtango hadi ukanyauka. Na hivyo ikatimia, wakati jua lilipopanda, kwamba Mungu akautayarisha upepo mkali wa mashariki; na jua likapiga kichwa chake Yona, kiasi kwamba alizimia, naye akatamani afe, na akasema, Ni heri mimi nife kuliko niishi. Mungu akasema kwa Yona, Je, unafanya vizuri kukasirika kwa sababu ya mtango? Na yeye akasema, naam, nafanya vizuri kukasirika, hata mpaka kufa. Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?

Muhtasari wa Hadithi ya Ninawi

Ingawa hadithi ya “uokoaji wa Mungu wa Ninawi” ilirekodiwa kwa ufupi, inamruhusu mtu kuweza kuona kidogo tu ule upande mwingine wa tabia ya haki ya Mungu. Ili kuweza kuelewa haswa upande huo unajumuisha nini, lazima turudi kwenye Maandiko na kuangalia nyuma katika mojawapo ya matendo ya Mungu.

Hebu kwanza tuangalie mwanzo wa hadithi hii: “Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele Yangu” (Yona 1:1-2). Katika kifungu hiki kutoka kwenye Maandiko, tunajua kwamba Yehova Mungu alimwamuru Yona kwenda katika mji wa Ninawi. Kwa nini alimwamuru Yona kwenda katika mji huo? Biblia iko wazi kabisa kuhusu suala hili: Maovu ya watu walio ndani ya mji huo yalikuwa yamefika mbele za Yehova Mungu, na hivyo basi Alimtuma Yona ili kuwatangazia kile Alichonuia kufanya. Ingawa hakuna kitu kilichorekodiwa kinachotwambia Yona alikuwa nani, jambo hili, bila shaka, halina uhusiano wowote na kumjua Mungu. Hivyo basi, huhitaji kumwelewa mwanamume huyu. Unahitaji kujua tu kile ambacho Mungu alimwamuru Yona kufanya na kwa nini Alifanya kitu hicho.

Onyo la Yehova Mungu Lawafikia Waninawi

Hebu tuendelee hadi kwenye fungu la nne, sura ya tatu ya kitabu cha Yona: “Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Bila shaka, haya ndiyo maneno ambayo Yehova alipenda kusema kwa Waninawi. Maneno haya yanatwambia kwamba Mungu alianza kukerwa na kuchukizwa na watu wa mji huu kwa sababu ya maovu yao yaliyokuwa yamefika machoni pa Mungu, na hivyo basi, Alitaka kuuangamiza mji huo. Hata hivyo, kabla ya Mungu kuuangamiza mji, Aliwatangazia Waninawi, na hapo kwa hapo Akawapa fursa ya kutubu maovu yao na kuanza upya. Fursa hii ingedumu kwa siku arubaini. Kwa maneno mengine, kama watu waliokuwa ndani ya mji huu wasingetubu, na kukubali dhambi au maovu yao wenyewe na kusujudu mbele ya Yehova Mungu ndani ya siku arubaini, Mungu angeangamiza mji huu kama Alivyoangamiza Sodoma. Hivi ndivyo ambavyo Yehova Mungu alipenda kuwaambia watu wa Ninawi. Ni wazi kwamba, hili halikuwa tangazo rahisi. Halikuweza tu kuonyesha hasira ya Yehova Mungu, lakini pia lilionyesha mtazamo Wake kwa wale Waninawi; wakati uo huo tangazo hili rahisi lilitumika kama onyo kali kwa watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huo. Onyo hili liliwaambia kwamba matendo yao maovu yalikuwa yamewafanya kuchukiwa na Yehova Mungu na liliwaambia kwamba matendo yao maovu yangewaleta kwenye ukingo wa maangamizo yao wenyewe; kwa hivyo, maisha ya kila mmoja kule Ninawi yalikuwa karibu kuangamia.

Tofauti Kubwa Iliyopo Kati ya Mwitikio wa Ninawi na Sodoma kwa Onyo la Yehova Mungu

Kupinduliwa kunamaanisha nini? Kwa muktadha wa mazungumzo, kunamaanisha kutoweka. Lakini kwa njia gani? Ni nani angefanya mji mzima kupinduliwa? Haiwezekani kwa binadamu kufanya kitendo kama hicho, bila shaka. Watu hawa hawakuwa wajinga; mara tu waliposikia matangazo haya, walipata wazo hilo. Walijua kwamba yalikuwa yametoka kwa Mungu; walijua kwamba Mungu angetekeleza kazi Yake; walijua kwamba maovu yao yalikuwa yamemkasirisha Yehova Mungu na kwa hivyo hasira ya Yehova Mungu ikawajia, na Alitaka kuwaangamiza wao pamoja na mji wao. Je, watu wa mji huo walichukulia vipi suala hilo baada ya kusikiliza onyo la Yehova Mungu? Biblia inafafanua kwa undani namna ambavyo watu hawa walivyoitikia, kuanzia kwa mfalme wao hadi kwa binadamu wa kawaida. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. …”

Baada ya kusikia tangazo la Yehova Mungu, watu wa Ninawi walionyesha mtazamo uliokuwa kinyume kabisa na ule wa watu wa Sodoma—watu wa Sodoma walimpinga Mungu waziwazi, huku wakiendelea kuongeza uovu kwa uovu, lakini baada ya kusikia maneno haya, Waninawi hawakupuuza suala hilo, wala hawakuweza kulipinga; badala yake walimsadiki Mungu na kutangaza kufunga. “Walisadiki” inarejelea nini hapa? Neno lenyewe linamaanisha imani na unyenyekevu. Kama tutatumia tabia halisi ya Waninawi kuelezea neno hili, inamaanisha kwamba waliamini Mungu anaweza na angeweza kufanya vile Alivyosema, na kwamba walikuwa radhi kutubu. Je, watu wa Ninawi walihisi hofu mbele ya janga lililokuwa karibu kutokea? Imani yao ndiyo iliyotia hofu katika mioyo yao. Kwa kweli, ni nini tunachoweza kutumia kuthibitisha Imani na hofu ya Waninawi? Ni sawa na vile Biblia inavyosema: “na wao wakatangaza kufunga, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia wale walio wakubwa zaidi na hata kwa wale walio wadogo zaidi.” Hivi ni kusema kwamba Waninawi waliamini kweli, na kwamba kutoka kwenye imani hii hofu iliibuka, ambayo sasa ilisababisha kufunga na kuvaliwa kwa nguo za magunia. Hivi ndivyo walivyoonyesha mwanzo wa toba yao. Tofauti kabisa na watu wa Sodoma, Waninawi hawakumpinga Mungu tu, bali walionyesha pia waziwazi toba yao kupitia kwa tabia na matendo yao. Bila shaka, hii haikutumika tu kwa watu wa kawaida wa Ninawi; hata mfalme wao hakubakizwa.

Toba ya Mfalme wa Ninawi Inapata Sifa ya Yehova Mungu

Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo za magunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng’ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo za magunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Misururu ya vitendo alivyovifanya—kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, kulitupa joho lake la kifalme, kuvalia nguo za magunia na kukalia majivu—kulionyesha watu kwamba mfalme wa Ninawi aliweka kando hadhi yake ya kifalme na kuvalia nguo za magunia pamoja na watu wa kawaida wa nchi. Hii ni kusema kwamba mfalme wa Ninawi hakuweza kushikilia wadhifa wake wa kifalme ili aendelee na njia zake za maovu au udhalimu katika mikono yake baada ya kusikia tangazo kutoka kwa Yehova Mungu; badala yake, aliweka pembeni mamlaka aliyoyashikilia na kutubu mbele za Yehova Mungu. Kwenye kipindi hiki cha muda, mfalme wa Ninawi hakuwa akitubu akiwa mfalme; alikuwa amekuja mbele za Mungu kuungama na kutubu dhambi zake akiwa kama binadamu wa kawaida wa Mungu. Aidha, aliuambia mji mzima kuungama na kutubu dhambi zao mbele za Yehova Mungu kwa njia sawa na yeye; vilevile, alikuwa na mpango mahususi wa namna ya kufanya hivyo kama inavyoonekana kwenye Maandiko: “Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: … na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao.” Kama kiongozi wa mji, mfalme wa Ninawi alimiliki hadhi na nguvu za kimamlaka na angefanya chochote alichopenda. Alipokabiliwa na tangazo la Yehova Mungu, angeweza kupuuza suala hilo au kutubu na kuungama tu dhambi zake pekee; kuhusiana na kama watu wa mji wangechagua kutubu au la, angepuuza suala hili kabisa. Hata hivyo, mfalme wa Ninawi hakufanya hivyo kamwe. Mbali na kuinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, kuvalia nguo za magunia na kujipaka majivu na kuungama na kutubu dhambi zake mbele za Yehova Mungu, aliweza pia kuwaamuru watu na mifugo ndani ya mji huo kufanya hivyo. Aliweza hata kuamuru watu “kumlilia Mungu kwa nguvu.” Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndivyo vilivyokuwa vigumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kuvitimiza, na kwa hakika, hakuna mfalme mwingine aliyewahi kufanikisha mambo haya. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu. Tangu mwanzo wa mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake wamsihi Mungu ili kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikononi mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuwaruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa mfano wa kuigwa wa ubinadamu uliopotoka unaoungama na kutubu dhambi zao mbele za Mungu.

Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Vina vya Mioyo ya Waninawi

Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha mwenendo wao kwa ujumla wake? Kwa nini walifanya kile walichokifanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walitenda kwa njia hii kwa sababu baada ya kusikia maneno ya Mungu, waliogopa sana na kuamini kwamba Angefanya kama Alivyosema. Kwa kufunga, kuvalia nguo za magunia na kuketi kwenye majivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu azuie hasira Yake, wakimsihi Yehova Mungu Atupilie mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwakabili. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwaangamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, wote walihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alivichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, ikiwa tu ingewezekana kutomkasirisha tena Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kunafiki, wala haikuwa ya muda.

Mara tu watu wote wa Ninawi, kuanzia mfalme hadi watu wa kawaida, walipojua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila moja ya vitendo vyao, tabia zao zote, pamoja na kila uamuzi na uchaguzi walioufanya vilikuwa wazi na dhahiri mbele za Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia zao. Je, mtazamo wa Mungu ulikuwa ni upi kwa wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Maneno yafuatayo yalirekodiwa katika maandiko: “Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Hakulifanya.” Ingawa Mungu alibadilisha fikira Zake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Zake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, hisia zao za kina za jinsi matendo yao maovu yalivyoikasirisha tabia Yake, na hofu iliyotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inawakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kubwa hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.

Kama Imani Yako kwa Mungu ni ya Kweli, Utapokea Utunzaji Wake Mara Nyingi

Mungu kubadilisha nia Zake kwa watu wa Ninawi hakukuhusisha kusitasita au kutoeleweka kokote. Badala yake kulikuwa ni mabadiliko kutoka kwa hasira tupu hadi uvumilivu mtupu. Huu ni ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Mungu kamwe si wa kusitasita au asiye na uamuzi katika vitendo Vyake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake yote ni wazi na dhahiri, yasiyo na dosari wala doa, yasiyo kabisa na hila ama njama zozote zilizochanganywa ndani. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu hakina giza wala maovu. Mungu aliwakasirikia Waninawi kwa sababu vitendo vyao viovu vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na kiini Chake. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilitoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni kiini Chake. Mabadiliko haya yote yalitokana na mabadiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Katika kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyokosewa haikubadilika; kiini cha Mungu cha uvumilivu hakikubadilika; kiini cha Mungu cha upendo na huruma hakikubadilika. Wakati watu wanapotekeleza vitendo viovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itakoma. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa ukaidi, hasira Yake kali haitakoma; hasira Yake itawalemea hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hiki ndicho kiini cha tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na wema, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinaamrisha kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu. Kama Mungu anaendelea kumfanya mtu apitie hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Ni kwa sababu mtu huyu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu hupokea utunzaji wa Mungu mara nyingi na hupokea huruma na uvumilivu Wake mara nyingi, basi mtu huyo bila shaka ana imani ya kweli kwa Mungu ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Mtu huyu mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.

Maelezo haya mafupi yanaruhusu watu kuuona moyo wa Mungu, kuona uhalisi wa kiini Chake, kuona kwamba ghadhabu ya Mungu na mabadiliko katika moyo Wake yana sababu. Ingawa kuna tofauti kubwa ambayo Mungu aliionyesha Alipoghadhabishwa na wakati Alipobadilisha moyo Wake, jambo hili linaweza kuwafanya watu kuamini kwamba kuna pengo kubwa ama tofauti kubwa inayoweza kuwepo kati ya vipengele hivi viwili vya kiini cha Mungu—ghadhabu Yake na uvumilivu Wake—mtazamo wa Mungu kwa kule kutubu kwa Waninawi kwa mara nyingine kunaruhusu watu kuweza kuona ule upande mwingine wa tabia halisi ya Mungu. Mabadiliko katika moyo wa Mungu yanaruhusu kwa kweli binadamu kwa mara nyingine kuuona ukweli wa huruma na wema wa Mungu na kuona ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Binadamu hawana budi kutambua kwamba rehema za Mungu na wema Wake si hadithi za uwongo tu, wala si uzushi. Hii ni kwa sababu hisia za Mungu kwa wakati huo zilikuwa za kweli; Mabadiliko ya moyo wa Mungu yalikuwa ya kweli; Mungu kwa kweli aliwapa binadamu kwa mara nyingine tena rehema na uvumilivu Wake.

Toba ya Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Inawapa Rehema za Mungu na Kubadilisha Hatima Zao Wenyewe

Je, kulikuwa na mkanganyiko wowote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu wakati ule maalum ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotolewa katika Biblia: “Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ovu” na “kuacha vurugu iliyokuwa mikononi mwake.”

Hii “njia ovu” hairejelei kiasi kidogo cha vitendo viovu, lakini inarejelea chanzo cha maovu katika tabia ya watu. “Kugeuka kutoka kwenye njia yake ovu” kunamaanisha kwamba wale wanaozungumziwa hawatawahi kutekeleza vitendo hivi tena. Kwa maneno mengine, hawatawahi kutenda kwa njia hii ovu tena; mbinu, chanzo, kusudio, nia na kanuni za vitendo vyao vyote vimebadilika; hawatawahi tena kutumia mbinu na kanuni hizi kuleta nafuu na furaha mioyoni mwao. Kule “kuacha” katika “kuacha vurugu iliyo mikononi mwake” kunamaanisha kuweka chini au kuweka pembeni, kujitenga kabisa na mambo ya kale na kutorudi nyuma tena. Wakati watu wa Ninawi walipoacha udhalimu uliokuwa mikononi mwao, hii ilithibitisha na vilevile iliwakilisha toba yao ya kweli. Mungu huangalia kwa makini sehemu ya nje ya watu na vilevile mioyo yao. Wakati Mungu alipoangalia kwa makini toba ya kweli katika mioyo ya Waninawi bila shaka Aliona pia kwamba walikuwa wameacha njia zao ovu na kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwao, Alibadilisha moyo Wake. Hivi ni kusema kwamba mwenendo na tabia ya watu hawa na njia mbalimbali za kufanya mambo, pamoja na ungamo na toba ya dhambi ya kweli zilizokuwa mioyoni mwao, kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake, kubadilisha nia Zake, kufuta uamuzi Wake na kutowaadhibu wala kuwaangamiza. Kwa hivyo, watu wa Ninawi waliweza kufikia hatima tofauti. Waliyakomboa maisha yao binafsi na wakati uo huo wakapata huruma na uvumilivu wa Mungu, na wakati huo Mungu pia alifuta hasira Yake.

Huruma na Uvumilivu wa Mungu si Nadra—Toba ya Kweli ya Mwanadamu Ndiyo Nadra

Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo za magunia pamoja na kuketi kwenye majivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa bado ana ghadhabu juu yao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ilibadilika polepole kuwa huruma na uvumilivu kwao. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu wa vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika tukio moja. Kwa hivyo, ni kwa jinsi gani mtu anapaswa kuelewa na kujua kwamba hazihitilafiani? Mungu alionyesha na kufichua viini hivi viwili tofauti kabisa kwa mfululizo wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na kutokosewa kwa kiini cha Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu hawavumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli kwa nadra sana mbele za Mungu, na ni nadra kwa watu kugeuka kwa kweli kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ameghadhabishwa na binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kumpa binadamu huruma na uvumilivu Wake kwa ukarimu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo mbovu wa mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu kwa kweli mbele Yake, kwa wale wanaoweza kugeuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Mtazamo wa Mungu ulifichuliwa waziwazi sana katika jinsi Alivyowatendea Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu si vigumu kuvipokea hata kidogo; Anahitaji toba ya kweli ya mtu. Mradi tu watu wageuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.

Tabia ya Haki ya Muumba ni ya Kweli na Wazi

Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko kati ya vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika hili suala moja yanakuruhusu kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili kabisa; haijagawanywa hata kidogo. Haijalishi kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni ya kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au sanamu ya udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe aliye hai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Angeweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi msiba na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupenda kutumia sheria bila kupinda na kutumia sheria kama hizo ili kumwekea mipaka na kumfafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia kanuni kujaribu kuelewa tabia ya Mungu. Kwa hivyo, katika uwanja wa fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika siku zote kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, vipengele tofauti vya kiini cha Mungu vitafichuliwa. Katika kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye humfichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake mwenyewe wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, wema Wake na uvumilivu Wake. Kiini Chake kitafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia Yake ya haki hairuhusiwi kutiliwa shaka, kukiukwa, kubadilishwa au kupotoshwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi vipengele hivi kwa kila sehemu ya viumbe vyote, na Anavitekeleza kila wakati kwa uwazi. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka na muda au eneo, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kulingana na mipaka ya muda au eneo. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kukoma kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inajumuisha maneno matupu? Wakati Mungu anapoonyesha hasira kali na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu? Mungu huonyesha hasira kali kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina dosari. Moyo wa Mungu unavutiwa na toba ya watu, na ni toba hii ambayo hubadilisha moyo Wake. Anapohisi kuguswa, Anapokuwa na mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote havina kosa kabisa; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu ni uvumilivu mtupu; Huruma Yake ni huruma tupu. Tabia Yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; kiini Chake ni tofauti na ile ya kiumbe chochote kilichoumbwa. Wakati Mungu anapoeleza kanuni zinazohusu matendo Yake, mawazo Yake, fikira Zake, na kila uamuzi Anaoufanya, pamoja na kila hatua Anazozichukua, huwa hazina doa au dosari zozote. Kama jinsi ambavyo Mungu huamua na jinsi Atendavyo, ndivyo Anavyokamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe yeyote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kustahimili fikira na uzoefu.

Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, sasa mnauona upande ule mwingine wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu? Je, mnauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwa binadamu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuitisha ghadhabu kuu namna hii na kuamua kuangamiza au kuleta maafa juu yawanadamu? Na ni nani anazo sifa zinazostahili kutoa huruma kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake wa kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za kipekee; na Hayuko chini ya udhibiti au vizuizi vilivyowekwa na watu, matukio au vitu vyovyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi Yeye na kubadilisha maamuzi Yake yoyote. Tabia zote na mawazo yote yaliyopo katika viumbe vyote vilivyoumbwa vipo chini ya hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama atatumia hasira au huruma; ni kiini cha Muumba tu—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—inaweza kuamua hili. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!

Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni kipengele kimoja cha kiini cha tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua vipengele viwili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; ni isiyokosewa na isiyoweza kutiliwa shaka; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyoweza kukosewa Vivyo hivyo, kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, anayeweza kuchukua nafasi Yake au kumwakilisha Mungu katika matendo Yake, wala hakuna yeyote ambaye angeweza kuchukua nafasi Yake au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.

Hisia za Dhati za Muumba kwa Wanadamu

Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. Sababu inayomfanya binadamu kufikiria kwa kutojua kwamba Mungu amemwepuka kimakusudi, kwamba Mungu amejificha kimakusudi kutoka kwa binadamu, kwamba Mungu hana nia yoyote ya kumruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Yeye, ni kwa sababu hamjui Mungu ni nani, na wala hataki kumuelewa Mungu; na hata zaidi, hajali kuhusu fikira, matamshi au matendo ya Muumba…. Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu wakati wote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na vitu vyote, na kwamba Anatekeleza matendo mapya kila siku. Kiini Chake na tabia Yake vimeonyeshwa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafunuliwa kabisa katika matendo Yake; Anaandamana na kumtazama mwanadamu wkati wote. Yeye hutumia maneno ya kimya kumwambia mwanadamu mambo yote kwa kimya: “Mimi niko mbinguni, na Mimi nimo miongoni mwa vitu vyote. Ninaangalia, Ninasubiri; Niko kando yako….” Mikono Yake ni yenye joto na nguvu; nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake hupita na kugeuka, likiwakumbatia wanadamu wote; uso Wake ni mzuri na mpole. Hajawahi kuondoka, hajawahi kutoweka. Usiku na mchana, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu, Asiyeondoka upande wao kamwe. Utunzaji wake wa kujitolea na mapenzi Yake kwa binadamu, pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu, vilionyeshwa kidogo kidogo Alipouokoa mji wa Ninawi. Hasa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona yalifunua kikamilifu upole wa Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Alimuumba. Kupitia katika maneno hayo, unaweza kufahamu kwa kina hisia za dhati za Mungu kwa binadamu …

Kifungu kifuatacho kilirekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: “Kisha Yehova akasema, Umekitunza sana kibuyu, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kutunza Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu, kutoka katika mazungumzo kati ya Mungu na Yona. Ingawa mazungumzo haya ni mafupi, yamejaa kutotaka kwa Muumba kukata tamaa juu ya mwanadamu na utunzaji Wake kwa binadamu. Maneno haya yanaonyesha mtazamo na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kwa viumbe Wake aliowaumba. Maneno haya pia ni Mungu akieleza nia Zake za kweli kwa binadamu, kwa njia iliyo dhahiri ambayo binadamu husikia kwa nadra sana. Mabadilishano ya mazungumzo haya yanawakilisha mtazamo ambao Mungu alishikilia kwa watu wa Ninawi—lakini mtazamo huu ni upi? Ni mtazamo Alioshikilia kuhusu watu wa Ninawi kabla na baada ya kutubu kwao. Mungu huchukulia binadamu kwa njia sawa. Ndani ya maneno haya mtu anaweza kupata fikira Zake, pamoja na tabia Yake.

Je, ni fikira zipi za Mungu zinafichuliwa katika maneno haya? Ukizingatia maelezo kwa makini unaposoma, haitakuwa vigumu kutambua kwamba Anatumia neno “huruma”; matumizi ya neno hili yanaonyesha mtazamo wa kweli wa Mungu kwa binadamu.

Kwa kiwango cha maana halisi, watu wanaweza kufasiri neno “huruma” kwa njia tofauti: Kwanza, inamaanisha “kupenda na kulinda, kuhisi huruma kuhusu kitu fulani”; pili, inamaanisha “kupenda kwa dhati”; na ya mwisho, inamaanisha “kutokuwa radhi kukiumiza kitu fulani na kutoweza kuvumilia kufanya hivyo.” Kwa ufupi, inaashiria hisia za kujali na upendo wa dhati, pamoja na kutokuwa radhi kukata tamaa na kumwacha mtu au kitu; unamaanisha huruma ya Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Ingawa Mungu alitumia neno hili, ambalo huzungumzwa kwa kawaida na wanadamu, matumizi ya neno hili yanaweka wazi sauti ya moyo wa Mungu na mtazamo Wake kwa mwanadamu.

Ingawa mji wa Ninawi ulikuwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo ambao ulitofautiana kabisa na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na ya dhati katika mambo yote, Mungu kwa mara nyingine tena alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa. Kile ambacho Mungu huwapa binadamu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kuiga, na haiwezekani kwa mtu yeyote kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Je, yupo yeyote unayemwona kuwa mwanamume au mwanamke mkuu, au hata mwanadamu mkuu zaidi, ambaye angeweza, kutoka katika mtazamo mkuu, kuongea kama mwanamume au mwanamke mkuu au kwenye sehemu ya mamlaka ya juu, kutoa aina hii ya kauli kwa mwanadamu au viumbe? Ni nani miongoni mwa wanadamu anayeweza kujua hali za maisha ya binadamu kama viganja vya mikono yao? Ni nani anayeweza kubeba mzigo na jukumu la uwepo wa mwanadamu? Nani aliye na sifa ya kutangaza kuangamizwa kwa mji? Na ni nani aliye na sifa ya kuusamehe mji? Ni nani anayeweza kusema kwamba anauthamini uumbaji Wake wote? Ni Muumba pekee! Muumba pekee ndiye Anayethamini jamii hii ya wanadamu. Muumba pekee ndiye Anaewaonyesha wanadamu hawa huruma na upendo. Ni Muumba pekee ndiye aliye na upendo wa kweli, usioweza kutenganishwa kwa wanadamu hawa. Vivyo hivyo, ni Muumba pekee ndiye Anayeweza kuwahurumia wanadamu hawa, na kuvithamini viumbe Vyake vyote. Moyo Wake unavutwa na kuumizwa kwa kila kitendo cha mwanadamu: Anagadhibishwa, Anahuzunishwa na kuumizwa kwa uovu na upotovu wa mwanadamu; Anakuwa radhi, Anafurahishwa, Anasamehe na kushangilia kutokana na toba na imani ya mwanadamu; kila moja ya mawazo Yake na fikira Zake vipo kwa ajili ya wanadamu na yanawazunguka wanadamu; kile Alicho na Anacho kinaonyeshwa kikamilifu kwa ajili ya wanadamu; hisia Zake zote zinahusiana sana na uwepo wa wanadamu. Kwa ajili ya wanadamu, Anasafiri na kukimbia huku na kule; Anatoa kwa ukimya kila sehemu ya maisha Yake; na Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua jinsi ya kuyathamini maisha Yake Mwenyewe, lakini daima Amewatunza wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe…. Anatoa kila Alichonacho kwa wanadamu hawa…. Anatoa rehema na uvumilivu Wake bila masharti na bila kutarajia malipo. Anafanya hivi tu ili kwamba wanadamu waweze kuendelea kuishi mbele ya macho Yake, wakipokea utoaji Wake wa maisha. Anafanya hivi tu ili kwamba wanadamu waweze siku moja kujisalimisha mbele Zake na kutambua kwamba Yeye ndiye Anayetosheleza maisha ya wanadamu na kutoa uhai wa viumbe vyote.

Muumba Aonyesha Hisia Zake za Kweli Kwa Binadamu

Mazungumzo haya kati ya Yehova Mungu na Yona bila shaka ni onyesho la hisia za kweli za Muumba juu ya binadamu. Kwa upande mmoja yanafahamisha watu kuhusu ufahamu wa Muumba wa viumbe vyote chini ya ukuu Wake; kama vile Yehova Mungu alivyosema, “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Kwa maneno mengine, ni kwamba ufahamu wa Mungu juu ya mji wa Ninawi si wa kukadiria. Sio kwamba anajua tu idadi ya viumbe vilivyo hai ndani ya mji (wakiwemo watu na mifugo), bali Alijua pia ni wangapi wasioweza kutambua kati ya mikono yao ya kulia na kushoto—yaani, ni watoto na vijana wangapi waliokuwepo. Huu ni uthibitisho kamili wa ufahamu mpana wa Mungu juu ya wanadamu. Kwa upande mwingine mazungumzo haya yanafahamisha watu kuhusu mtazamo wa Muumba kwa binadamu, yaani, umuhimu wa wanadamu katika moyo wa Muumba. Ni vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu…?” Maneno haya yalisemwa na Yehova Mungu dhidi ya Yona, lakini yote yalikuwa kweli.

Ingawaje Yona alikuwa ameaminiwa kutangaza matamshi ya Yehova Mungu kwa watu wa Ninawi, hakuelewa nia za Yehova Mungu, wala hakuelewa wasiwasi na matarajio Yake kwa watu wa mji huu. Kupitia kwa kemeo hili Mungu alinuia kumwambia kwamba binadamu walikuwa ni zao la mikono Yake mwenyewe, na kwamba Mungu alikuwa ametia jitihada za dhati kwa kila mtu; kwamba Mungu ameweka matarajio Yake kwa kila mtu, kwamba kila mtu anafurahia maisha yanayotolewa na Mungu, na kwamba kwa kila mtu, Mungu alikuwa amelipa gharama ya dhati. Kemeo hili lilimfahamisha Yona kwamba Mungu aliwahurumia wanadamu, ambao walikuwa ni kazi ya mikono Yake mwenyewe, kama vile tu ambavyo Yona mwenyewe aliuhurumia ule mtango. Mungu kwa vyovyote vile asingewaacha kwa urahisi kabla ya ule muda wa mwisho unaowezekana; vilevile, kulikuwa na watoto wengi na mifugo isiyo na hatia ndani ya mji. Wakati wa kushughulikia wanadamu hawa wenye umri mdogo walio zao la uumbaji wa Mungu, ambao bado hawawezi hata kutofautisha kati ya mikono yao ya kushoto na ile ya kulia, na walio katika umri wa ujinga, Mungu asingeweza hata zaidi kukatisha maisha yao kwa urahisi na kuamua mwisho wao kwa haraka hivyo. Mungu alitumai kuwaona wakikua; Alitumai kwamba wasingetembea njia ile ile kama wakubwa wao, kwamba wasingeweza kusikia tena onyo la Yehova Mungu, na kwamba wangeshuhudia mambo ya kale ya Ninawi. Na hata zaidi Mungu alitumai kuiona Ninawi baada ya kuweza kutubu, kuuona mustakabali wa Ninawi kufuatia kutubu kwake, na muhimu zaidi, kuiona Ninawi ikiishi katika huruma za Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa hivyo, machoni pa Mungu, wale wanadamu walioumbwa ambao bado hawakuweza kutofautisha kati ya mikono yao ya kulia na kushoto walikuwa mustakabali wa Ninawi. Wangeweza kubeba na kusimulia hadithi ya kale ya Ninawi iliyostahili dharau, na pia wangebeba wajibu muhimu wa kushuhudia wakati uliopita na ule ujao wa Ninawi chini ya uongozi wa Yehova Mungu. Katika tangazo hili la hisia Zake za kweli, Yehova Mungu aliwasilisha huruma ya Muumba kuhusu binadamu kwa ujumla wake. Lilionyesha binadamu kwamba “ile huruma ya Muumba” si kauli tupu tu, wala si ahadi isiyotimizika; ilikuwa na kanuni, mbinu na malengo madhubuti. Mungu ni wa kweli na halisi, na hatumii uwongo au utapeli wowote, na kwa njia hii hii huruma Yake hutolewa bila kikomo kwa wanadamu katika kila wakati na enzi. Hata hivyo, hadi siku hii, mabadilishano ya mazungumzo ya Muumba na Yona ndiyo kauli moja, na ya kipekee ya matamshi yanayoelezea ni kwa nini Anaonyesha huruma kwa binadamu, jinsi Anavyoonyesha huruma kwa binadamu, ni vipi Alivyo na uvumilivu kwa binadamu na hisia Zake za kweli kuhusu binadamu. Mazungumzo haya ya Yehova Mungu kwa ufupi na uwazi yanaonyesha fikira Zake kamili kuhusu binadamu; ni maonyesho ya kweli ya mtazamo wa moyo Wake kwa binadamu, na pia ni uthibitisho kamili wa utoaji Wake wa huruma nyingi juu ya binadamu. Huruma yake haitolewi tu kwa vizazi vya wazee wa binadamu, lakini pia hutolewa kwa washiriki wachanga wa binadamu, kama vile tu ambavyo imekuwa siku zote, kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ingawa ghadhabu ya Mungu mara kwa mara hushuka kwenye pembe fulani na enzi fulani za binadamu, huruma za Mungu hazijawahi kukoma. Kupitia kwa huruma Yake, Yeye huongoza na kuelekeza kizazi kimoja cha uumbaji Wake hadi kingine, huruzuku na kukimu kizazi kimoja cha uumbaji hadi kingine, kwa sababu hisia Zake za kweli kwa binadamu hazitawahi kubadilika. Kama vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma…?” Siku zote amefurahia uumbaji Wake mwenyewe. Hii ndiyo huruma ya tabia ya haki ya Muumba, na ndio pia upekee usio na kasoro wa Muumba!

Aina Tano za Watu

Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika makundi kadhaa, kulingana na ufahamu wao wa Mungu, pamoja na ufahamu na uzoefu wao kuhusu tabia Yake ya haki, ili uweze kujua hatua uliyomo kwa sasa, pamoja na kimo chako cha sasa. Kuhusiana na maarifa ya watu juu ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, hatua na vimo tofauti ambavyo watu wanashikilia kwa ujumla vinaweza kugawanywa katika aina tano. Mada hii imeelezewa kwa msingi wa kumjua Mungu wa kipekee na tabia Yake ya haki; kwa hivyo, unaposoma maudhui yafuatayo, unafaa kujaribu kwa makini kuchambua ni kiwango kipi haswa cha ufahamu na maarifa ulichonacho kuhusiana na upekee wa Mungu na tabia Yake ya haki, na kisha utumie hayo kujua ni hatua gani ambayo kwa kweli unapatikana ndani, kimo chako ni kikubwa vipi kwa kweli, na wewe ni mtu wa aina gani kwa kweli.

Aina ya Kwanza: Hatua ya Mtoto Mchanga Aliyevikwa Nguo za Kitoto

Mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto ni nani? Mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto ni mtoto mchanga ambaye ndio amekuja tu katika ulimwengu huu, amezaliwa. Huu ndio wakati ambao watu wako katika awamu ndogo zaidi na isiyo na ukomavu.

Watu katika awamu hii kimsingi hawamiliki utambuzi au ufahamu wowote wa masuala ya imani katika Mungu. Wamechanganyikiwa na hawajui kila kitu. Watu hawa huenda wamemsadiki Mungu kwa muda mrefu au kwa muda usiokuwa mrefu, lakini hali yao ya kuchakanganywa na kutojua kimo chao halisi kinawaweka kwenye awamu ya mtoto mchanga ambaye amevikwa kwa nguo za kitoto. Ufafanuzi sahihi wa hali hii ya mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto ni kama vile: Haijalishi ni kwa muda gani mtu wa aina hii amemwamini Mungu, siku zote atakuwa mpumbavu, atachanganyikiwa na atakosa busara; hajui ni kwa nini anamwamini Mungu, wala hamjui Mungu ni nani au Mungu ni nini. Ingawa wanamfuata Mungu, hakuna ufafanuzi sahihi wa Mungu ndani ya mioyo yao, na hawawezi kuamua kama Yule wanayemfuata ni Mungu, achilia mbali kama kweli wanafaa kumwamini Mungu na kumfuata. Hii ndiyo hali halisi ya mtu wa aina hii. Fikira za watu hawa zimezingirwa na ukungu, na kama nitasema wazi, imani yao ni ile ya mkanganyo. Siku zote wanakuwa katika hali ya kutokuelewa na utupu; wanakuwa wapumbavu, wanachanganyikiwa, na wanakosa busara, hivi ndivyo vitu vinavyofanya muhtasari wa hali zao. Hawajawahi kuona wala kuhisi uwepo wa Mungu, na hivyo basi, kuzungumza nao kuhusu kumjua Mungu ni sawa tu na kuwafanya wasome kitabu kilichoandikwa kwa maandishi ama ishara zisizoeleweka; hawataelewa wala kuyakubali. Kwao, kumjua Mungu ni sawa na kusikia hadithi ya ajabu. Huku mawazo yao yakiwa yamejaa ukungu, wanaamini kwa hakika kwamba kumjua Mungu ni kupoteza muda na jitihada. Huyu ndiye mtu wa aina ya kwanza: mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto.

Aina ya Pili: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayenyonya

Akilinganishwa na mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto, mtu wa aina hii amepata maendeleo fulani. Kwa bahati mbaya, bado hawana ufahamu wowote wa Mungu. Bado hawana ufahamu wazi wa Mungu na utambuzi wa Mungu, na hawaelewi vizuri sana ni kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, lakini katika mioyo yao wana madhumuni yao wenyewe na mawazo yaliyo wazi. Hawajishughulishi katika suala la ikiwa ni sahihi kumwamini Mungu. Lengo na madhumuni wanayotafuta kupitia imani katikaMungu ni kufurahia neema Yake, kuwa na furaha na amani, kuishi maisha yenye utulivu, kuwa na utunzaji na ulinzi wa Mungu na kuishi katika baraka za Mungu. Hawajali kiwango ambacho wanamjua Mungu; hawana msukumo wa kutafuta kuelewa kuhusu Mungu, wala hawashughuliki na kile ambacho Mungu anafanya au kile ambacho Angependa kufanya. Wanatafuta tu bila mwelekeo kufurahia neema Yake na kupata baraka Zake nyingi; wanatafuta kupokea baraka mara mia moja katika wakati wa sasa, na uzima wa milele katika wakati ujao. Mawazo yao, kiasi wanachojitumia wao wenyewe kujitolea kwao, pamoja na kuteseka kwao, vyote vinalo lengo moja: kupokea neema na baraka za Mungu. Hawana shughuli na kitu kingine chochote. Mtu wa aina hii ana uhakika tu kwamba Mungu anaweza kuwalinda wakawa salama na kuwapa neema Yake. Mtu anaweza kusema kwamba hawapendezwi na wala hawana uelewa sana kuhusiana na kwa nini Mungu angependa kumwokoa binadamu au matokeo ambayo Mungu angependa kupata kutokana na matamshi na kazi Yake. Hawajawahi kutia jitihada za kujua kiini cha Mungu na tabia Yake ya haki, wala hawawezi kujipa moyo na kuwa na nia ya kufanya hivyo. Hawana mwelekeo wa kuzingatia mambo haya, na, wala hawapendi kuyajua. Hawapendi hata kuulizia kuhusu kazi ya Mungu, mahitaji ya Mungu kwa binadamu, mapenzi ya Mungu au kitu kingine chochote kinachohusiana na Mungu; wala hawawezi kuwa na msukumo wa kuulizia mambo haya. Hii ni kwa sababu wanaamini kwamba mambo haya hayahusiani na kufurahia kwao neema ya Mungu; wanajali tu Mungu anayeweza kuwapa neema na ambaye ana uhusiano na masilahi yao ya kibinafsi. Kamwe hawana haja na kitu kingine chochote, na kwa hivyo hawawezi kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, licha ya miaka mingapi ambayo wamemwamini Mungu. Bila kuwepo mtu yeyote wa kuwanywesha mara kwa mara au kuwalisha, ni vigumu kwao kuendelea na njia ya imani katika Mungu. Kama hawawezi kufurahia furaha yao na amani ya awali au kufurahia neema ya Mungu, basi wana uwezekano mkubwa wa kujiondoa. Huyu ndiye mtu wa aina ya pili: mtu anayekuwepo kwenye awamu ya mtoto mchanga wa kunyonya.

Aina ya Tatu: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayeachishwa Kunyonya, au Hatua ya Mtoto Mdogo

Kundi hili la watu humiliki ufahamu fulani wenye uwazi. Watu hawa wanao ufahamu kwamba kufurahia neema ya Mungu hakumaanishi kwamba wao wenyewe wanamiliki uzoefu wa kweli; na wanafahamu kwamba hata kama hawatachoka kamwe kutafuta furaha na amani, kutafuta neema, au kama wanaweza kutoa ushuhuda kwa kushiriki uzoefu wao katika kufurahia neema ya Mungu au kwa kumsifu Mungu kwa baraka Alizowapa, mambo haya hayamaanishi kwamba wana uzima, wala hayamaanishi kwamba wanao uhalisi wa ukweli. Tukianzia katika ufahamu wao, wanaacha kuwa na matumaini yasiyo na mipaka kwamba wataandamana tu na neema ya Mungu; badala yake, wakati wanapofurahia neema ya Mungu, wanapenda wakati uo huo kufanya kitu kwa ajili ya Mungu; wako radhi kutekeleza wajibu wao, kuvumilia ugumu kidogo na uchovu, kuwa na kiwango fulani cha ushirikiano na Mungu. Hata hivyo, kwa sababu ufuatiliaji wao wa imani yao katika Mungu umepotoka sana, kwa sababu nia za kibinafsi na matamanio waliyo nayo ni yenye nguvu sana, kwa sababu tabia yao ni yenye kiburi kupita kiasi, ni vigumu sana kwao kutosheleza nia zaMungu au kuwa watiifu kwa Mungu; hivyo basi, wao mara nyingi hawawezi kutambua matamanio yao ya kibinafsi au kuheshimu ahadi zao kwa Mungu. Mara nyingi wanajikuta katika hali zinazopingana: Wanatamani sana kumridhisha Mungu kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana, ilhali wanatumia uwezo wao wote kumpinga Yeye; mara nyingi wanaweka nadhiri kwa Mungu lakini kwa haraka sana wanaishia kuzivunja nadhiri zao. Hata mara nyingi zaidi wanajikuta katika hali zingine zinazopingana: Wanamwamini Mungu kwa dhati, ilhali wanamkana Yeye na kila kitu kinachotoka Kwake; wanatumai kwa hamu kwamba Mungu atawapa nuru, atawaongoza, atawaruzuku na kuwasaidia, ilhali bado wanatafuta njia yao wenyewe ya kutokea. Wanatamani kumwelewa na kumjua Mungu, ilhali hawako radhi kuwa na uhusiano wa karibu na Yeye. Badala yake, siku zote wanamwepuka Mungu; mioyo yao haiko wazi kumkaribisha. Ingawa wana ufahamu wa juu juu na uzoefu wa maana halisi ya matamshi ya Mungu na ya ukweli, na dhana ya juujuu ya Mungu na ukweli, bila kujua bado hawawezi kuthibitisha au kubainisha kama Mungu ndiye ukweli, wala hawawezi kuthibitisha kama Mungu kweli ni mwenye haki. Pia hawawezi kubainisha uhalisi wa tabia na kiini cha Mungu, achilia mbali uwepo Wake wa kweli. Imani yao katika Mungu siku zote ina mashaka na kutokuelewa kwingi, na pia ina mawazo na dhana. Wanapofurahia neema ya Mungu, pia kwa kusita wanapitia au kutenda baadhi ya ukweli ambao wanaona kuwa unaweza kutekelezeka ili kuimarisha imani yao, kuongeza uzoefu wao katika kumwamini Mungu, kuthibitisha uelewa wao wa kumwamini Mungu, na kutosheleza ubatili wao kwa kutembea juu ya njia ya uzima ambayo wao wenyewe waliianzisha na kutimiza vitendo vya haki vya wanadamu. Wakati huo huo, wao pia hufanya mambo haya ili kukidhi matamanio yao wenyewe ya kupata baraka, ambayo ni sehemu ya dau wanalofanya kwa matumaini ya kupokea baraka kubwa zaidi za binadamu, na ili kutimiza matamanio yao makubwa na hamu ya maisha yao yoteya kutopumzika mpaka pale ambapo wamempata Mungu. Watu hawa kwa nadra sana wanaweza kupokea nuru ya Mungu, kwani tamanio lao na nia yao ya kufaidi baraka ni muhimu sana kwao. Hawana tamanio la kuacha na hawawezi kuvumilia kutupilia mbali hili. Wanaogopa kwamba bila ya tamanio la kupata baraka, bila ya matamanio ya muda mrefu ya kutopumzika hadi wampate Mungu, wataweza kupoteza msukumo wa kumwamini Mungu. Kwa hivyo, hawapendi kukabiliana na uhalisi. Hawapendi kukabiliana na matamshi ya Mungu au kazi ya Mungu. Hawapendi kukabiliana na tabia au kiini cha Mungu, sembuse kuzungumzia hata mada ya kumjua Mungu. Hii ni kwa sababu mara tu Mungu, kiini Chake na tabia Yake ya haki vinapobadilisha maono yao, ndoto zao zitatoweka hivyo bila kuonekana; imani yao inayodhaniwa kuwa safi na “sifa njema” zilizokusanywa baada ya miaka ya kazi ngumu zitatoweka zote na kutokuwa na manufaa yoyote; “eneo” lao ambalo wameshinda kupitia kwa jasho na damu yao kwa miaka mingi litakuwa karibu kusambaratika. Hii itamaanisha kwamba miaka yao mingi ya kazi ngumu na jutihada vyote vimekuwa bure, na kwamba lazima waanze tena bila ya kuwa na chochote. Haya ndiyo maumivu makali sana kwao kuyavumlia katika mioyo yao, na ni matokeo ambayo hawangetamani kuyaona hata kidogo; hivyo basi, siku zote wamefungwa katika kizuizi cha aina hii, wakikataakurudi nyuma. Huyu ndiye mtu wa aina ya tatu: mtu anayekuwa katika awamu hii ya mtoto mchanga aliyeachishwa kunyonya.

Aina tatu za watu waliofafanuliwa hapo juu—kwa maneno mengine, watu wanaopatikana katika hatua hizi tatu—hawamiliki imani yoyote ya kweli katika utambulisho na hadhi ya Mungu au katika tabia Yake ya haki, na wala hawana utambuzi wowote wa wazi, wa uhakika au uthibitisho wa mambo haya. Kwa hivyo, ni vigumu sana kwa aina hizi tatu za watu kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, na ni vigumu pia kwa wao kupokea huruma, ufahamu au mwangaza wa Mungu kwa sababu ya namna ambavyo wanamwamini Mungu na mtazamo wao potofu kwa Mungu unamfanya Yeye kutoweza kutekeleza kazi yoyote ndani ya mioyo yao. Mashaka yao, dhana zao potofu na mawazo yao juu ya Mungu yanazidi imani yao na ufahamu wao juu ya Mungu. Hizi ni aina tatu za watu walio katika hatari kubwa, na ni hatua tatu hatari sana. Wakati mtu anapoendeleza mtazamo wa shaka kwa Mungu, kiini cha Mungu, utambulisho wa Mungu, kwa suala la iwapo Mungu ndiye ukweli na uhalisi wa kuwepo Kwake, na wakati ambapo mtu hawezi kuwa na uhakika katika mambo haya, ni vipi ambavyo mtu anaweza kukubali kila kitu kinachotoka kwa Mungu? Mtu anawezaje kukubali ukweli kwamba Mungu ndiye ukweli, njia na uzima? Mtu anawezaje kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu? Mtu anawezaje kukubali wokovu wa Mungu? Ni vipi ambavyo mtu wa aina hii anaweza kupokea mwongozo na ruzuku ya kweli kutoka kwa Mungu? Wale ambao wanapatikana katika awamu hizi tatu wanaweza kumpinga Mungu, kupitisha hukumu kwa Mungu, kumkufuru Mungu au kumsaliti Mungu wakati wowote. Wanaweza kuacha njia ya kweli na kumwacha Mungu wakati wowote. Mtu anaweza kusema kwamba watu katika hatua hizi tatu wapo katika kipindi cha hatari sana, kwani hawajaingia kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu.

Aina ya Nne: Hatua ya Mtoto Anayekomaa, au Kipindi cha Utoto

Baada ya mtu kuachishwa kunyonya—yaani, baada ya wao kufurahia kiasi cha kutosha cha neema—wanaanza kuchunguza ni nini maana ya kumwamini Mungu, wanaanza kutamani kuelewa maswali tofauti, kama vile kwa nini binadamu anaishi, binadamu anafaa kuishi vipi, na kwa nini Mungu hutekeleza kazi Yake kwa binadamu. Wakati ambapo mawazo haya yasiyo wazi na mawazo yaliyokanganyikiwa hujitokeza ndani yao, na kuwepo ndani yao, wanaendelea kupokea kunyunyizwa, na wao wanaweza pia kutekeleza wajibu wao. Kwenye kipindi hiki, hawana tena shaka kuhusiana na ukweli wa uwepo wa Mungu, na wanao ufahamu sahihi wa ni nini maana ya kumwamini Mungu. Kwenye msingi huu wao hupata maarifa ya Mungu hatua kwa hatua, na polepole wanapata baadhi ya majibu ya mawazo yao yasiyo wazi na mawazo yaliyokanganyika kuhusiana na tabia ya Mungu na kiini Chake. Kwa upande wa mabadiliko yao katika tabia pamoja na maarifa yao kuhusu Mungu, watu katika awamu hii huanza kushika njia sahihi na kuingia kwenye kipindi cha mabadiliko. Ni katika awamu hii ambapo watu huanza kuwa na maisha. Dalili za wazi za kumiliki uzima ni utatuzi wa taratibu wa maswali mbalimbali yanayohusiana na kumjua Mungu ambayo watu wanakuwa nayo katika mioyo yao—kama vile kutoelewana, mawazo, fikira, na ufafanuzi usio wazi wa Mungu—na sio tu kwamba wanakuja kweli kuamini na kutambua uhalisi wa uwepo wa Mungu, lakini pia wanakuja kumiliki ufafanuzi sahihi wa Mungu na kuwa na nafasi sahihi ya Mungu katika mioyo yao, na kumfuata Mungu kwa kweli kunachukua nafasi ya imani yao isiyo dhahiri. Katika hatua hii, watu wanaanza hatua kwa hatua kujua dhana zao potofu kwa Mungu, mambo yasiyo sahihi waliyofuatilia na njia za imani zisizo sahihi. Wanaanza kutamani ukweli, kutamani kupitia hukumu ya Mungu, kurudiwa na nidhamu, kutamani mabadiliko katika tabia yao. Kwa utaratibu wanaanza kuacha aina zote za dhana na fikira kuhusu Mungu katika hatua hii; wakati uo huo wanabadilisha na kurekebisha maarifa yasiyo sahihi kuhusu Mungu na kupata baadhi ya maarifa muhimu na sahihi kuhusu Mungu. Ingawa sehemu ya maarifa inayomilikiwa na watu katika awamu hii si mahususi au sahihi sana, kwa kiwango cha chini zaidi wanaanza kwa utaratibu kuacha dhana zao, maarifa ya kimakosa na kutoelewa mambo kuhusu Mungu; hawaendelezi tena dhana zao binafsi na fikira zao kuhusu Mungu. Wanaanza kujifunza namna ya kuacha—kuacha mambo yanayopatikana miongoni mwa dhana zao binafsi, kutoka kwa maarifa yao na kutoka kwa Shetani; wanaanza kuwa radhi kutii mambo sahihi na mazuri, hata kwa mambo yanayotoka kwenye matamshi ya Mungu na yanayopatana na ukweli. Wanaanza pia kujaribu kupata matamshi ya Mungu, kujua kibinafsi na kutekeleza matamshi Yake, kukubali matamshi Yake kama kanuni za matendo yao na kama msingi wa kubadilisha tabia yao. Kwenye kipindi hiki, watu bila kufahamu wanakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanakubali bila fahamu matamshi ya Mungu kuwa maisha yao. Huku wakikubali hukumu ya Mungu, kuadibu kwa Mungu, na kukubali matamshi ya Mungu, wanaendelea kupata ufahamu zaidi na kuweza kuhisi kwamba Mungu wanayemwamini ndani ya mioyo yao yuko kweli. Katika maneno ya Mungu, katika uzoefu wao na maisha yao, wanazidi kuhisi kwamba Mungu siku zote amesimamia hatima ya binadamu, kumwongoza binadamu na kumruzuku binadamu. Kupitia kwa ushirikiano wao na Mungu, wanaanza kwa utaratibu kuthibitisha uwepo wa Mungu. Kwa hivyo, kabla ya wao kutambua hilo, tayari wameidhinisha bila kujua na kuanza kuamini kwa dhati katika kazi ya Mungu, na wameidhinisha matamshi ya Mungu. Baada ya watu kuidhinisha matamshi ya Mungu, na kuidhinisha kazi ya Mungu, daima wao watajikana wenyewe, watakana dhana zao wenyewe, watakana maarifa yao wenyewe, watakana fikira zao wenyewe, na wakati huo huo pia bila kukoma watatafuta ukweli ni nini na mapenzi ya Mungu ni nini. Maarifa ya watu kuhusu Mungu ni ya juujuu sana kwenye kipindi hiki cha maendeleo—hawawezi hata kufafanua kwa uwazi maarifa haya kwa kutumia matamshi, wala hawawezi hata kufafanua kimahususi—na wanao tu ufahamu unaotegemea mtazamo; hata hivyo, wakati hatua hii inawekwa sambamba na zile awamu tatu zilizotangulia, maisha ya watu wasiokomaa katika kipindi hiki tayari yameanza kupokea unyunyiziaji na utolewaji wa matamshi ya Mungu, na hivyo tayari yameanza kuchipua. Maisha yao ni kama mbegu iliyofukiwa ardhini; baada ya kupokea unyevunyevu na virutubisho, lazima itapenyeza kupitia kwenye udongo; kuota kwake kunawakilisha kuzaliwa kwa maisha mapya. Kuzaliwa huku kwa maisha mapya kunaruhusu mtu kuona viashiria vya maisha. Kupitia kwa maisha, watu wataweza kukua. Kwa hivyo, juu ya misingi hii—hatua kwa hatua wataingia kwenye njia sahihi ya kuamini katika Mungu, wakiacha dhana zao wenyewe, wakipata mwongozo wa Mungu—maisha ya watu yataweza kukua bila shaka hatua kwa hatua. Ni katika msingi gani ndipo ukuaji huu unapimwa? Unapimwa kulingana na uzoefu wao na maneno ya Mungu na ufahamu wao wa kweli kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Ingawa wanaona ni vigumu sana kutumia maneno yao wenyewe ili kufafanua kwa usahihi maarifa yao kuhusu Mungu na kiini Chake katika kipindi hiki cha ukuaji, kundi hili la watu haliko radhi tena kufuatilia kimsingi furaha kupitia kwa kufurahia neema ya Mungu, au kuamini katika Mungu ili kufuata kusudi lao la kupokea neema Yake. Badala yake, wako radhi kutafuta kuishi kwa neno la Mungu, ili kuwa walengwa wa wokovu wa Mungu. Vilevile, wanamiliki ujasiri na wako tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Hii ndiyo alama ya mtu aliye katika hatua ya ukuaji.

Ingawa watu katika hatua hii wanayo maarifa fulani kuhusu tabia ya haki ya Mungu, maarifa yao si dhahiri na hayana uwazi. Huku wakiwa hawawezi kufafanua wazi hali hii, wanahisi kwamba tayari wamefaidi kitu fulani ndani kwa ndani, kwani wamepata kiasi fulani cha maarifa na ufahamu wa tabia ya haki ya Mungu kupitia kwa kuadibu kwa Mungu na hukumu yake; hata hivyo yote haya ni kana kwamba ni ya juujuu, na bado yapo katika hatua ya msingi. Kundi hili la watu lina mtazamo mahususi kuhusiana na neema ya Mungu. Mtazamo huu mahususi unaelezewa kupitia kwenye mabadiliko ya malengo wanayoyatafuta na njia ambayo wanayatafutia. Tayari wameona—katika maneno na kazi ya Mungu, katika kila aina ya mahitaji Yake kwa mwanadamu na katika ufunuo Wake kwa mwanadamu —kwamba kama bado hawatafuatilia ukweli, kama bado hawatafuti kuingia kwenye uhalisia, kama bado hawatafuti kumridhisha na kumjua Mungu wanapopitia maneno Yake, basi watapoteza umuhimu wa kuamini katika Mungu. Wanaona kwamba haijalishi ni kiwango kipi ambacho wanafurahia neema ya Mungu, hawawezi kubadilisha tabia zao, kumridhisha Mungu na kumjua Mungu, na kwamba kama watu wataendelea kuishi chini ya neema ya Mungu, basi hawatawahi kupata ukuaji, kupata uzima au kuweza kupokea wokovu. Kwa muhtasari, kama mtu hawezi kupitia maneno ya Mungu kwa njia ya kweli na hawezi kumjua Mungu kupitia kwa maneno Yake, mtu huyo daima dawamu atabakia katika awamu ile ya mtoto mchanga na hatawahi kupiga hatua yoyote mbele kwenye ukuaji wa maisha yake. Iwapo siku zote utabakia kwenye hatua ya mtoto mchanga, kama kamwe huingii kwenye uhalisi wa neno la Mungu, kama kamwe huna neno la Mungu kama maisha yako, kama kamwe huna imani na maarifa ya kweli kuhusu Mungu, je, kunao uwezekano wowote kwako wewe kufanywa kuwa kamili na Mungu? Hivyo basi, yeyote anayeingia katika uhalisi wa neno la Mungu, yeyote anayekubali neno la Mungu kuwa maisha yake, yeyote anayeanza kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, yeyote ambaye tabia yake potovu inaanza kubadilika, na yeyote aliye na moyo unaotamani ukweli, analo tamanio la kumjua Mungu, analo tamanio la kukubali wokovu wa Mungu—watu hawa ndio wale wanaomiliki uzima kwa kweli. Hii kwa kweli ndiyo aina ya nne ya mtu, ile ya mtoto anayekomaa, mtu aliye katika hatua ya utoto.

Aina ya Tano: Hatua ya Maisha Yaliyokomaa, au Hatua ya Mtu Mzima

Baada ya kupitia hatua ya utoto, hatua hii ya ukuaji imejaa misukosuko ya kujirudia rudia, maisha ya watu tayari yameimarishwa, hatua zao za kusonga mbele hazisimami tena, wala hakuna yeyote anayeweza kuwazuia. Ingawanjia iliyo mbele ingali na mabonde na misukosuko, si wanyonge tena au wenye woga; hawayumbiyumbi tena huko mbele au kupoteza mwelekeo wao. Misingi yao imekita mizizi ndani ya uzoefu halisi wa neno la Mungu. Mioyo yao imevutwa na hadhi na ukuu wa Mungu. Wanatamani kufuata nyayo za Mungu, kujua kiini cha Mungu, kumjua Mungu kwa ukamilifu Wake wote.

Watu katika hatua hii tayari wanajua waziwazi ni nani wanayemwamini, na wanajua wazi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu na maana ya maisha yao wenyewe, na pia wanajua wazi kwamba kila kitu ambacho Mungu anaeleza ni ukweli. Katika uzoefu wao wa miaka mingi, wametambua kwamba bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, mtu hataweza kamwe kumridhisha au kumjua Mungu, na kamwe hawezi kuja mbele za Mungu kwa kweli. Ndani ya mioyo ya watu hawa kuna shauku kubwa ya kujaribiwa na Mungu, ili waweze kuona tabia ya haki ya Mungu wanapojaribiwa, na kufikia upendo safi zaidi, na wakati huo huo waweze kumwelewa na kumjua Mungu kwa njia ya kweli zaidi. Watu katika hatua hii tayari wameaga kabisa hatua ya mtoto mchanga, na hatua ya kufurahia neema ya Mungu na kula mkate na kushiba. Hawaweki tena matumaini mengi ya kupita kiasi juu ya kumfanya Mungu awavumilie na kuwaonea huruma; badala yake, wanao ujasiri wa kupokea na kutumai kupata kuadibu na hukumu ya Mungu isiyokoma, ili waweze kujitenga na tabia zao potovu na kumridhisha Mungu. Maarifa yao kwa Mungu, kufuatilia kwao au malengo yao ya mwisho ya ufuatiliaji wao: mambo haya yote yako wazi kabisa katika mioyo yao. Kwa hivyo, watu katika hatua ya watu wazima tayari wameaga kwaheri kabisa hatua ya imani isiyo dhahiri, hatua ambayo wanategemea neema kupata wokovu, kwenye hatua ya maisha yasiyo na ukomavu unaoweza kustahimili majaribu, kwenye hatua ya kutokuwa na uhakika, kwenye hatua ya kupapasa, kwenye hatua ya kukosa njia ya kutembea mara kwa mara, kwenye kipindi kisichokuwa thabiti cha kubadilisha kati ya joto na baridi kwa ghafla, na kwenye hatua ambayo mtu anamfuata Mungu huku akiwa ameyafumba macho yake. Mtu wa aina hii hupokea nuru na mwangaza wa Mungu mara kwa mara, na pia mara kwa mara hujihusisha katika ushirikiano na mawasiliano ya kweli na Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika hatua hii tayari wameng’amua sehemu ya mapenzi ya Mungu; wanaweza kupata kanuni za ukweli katika kila kitu wanachofanya; wanajua namna ya kutosheleza tamanio la Mungu. Isitoshe, wamepata pia njia ya kumjua Mungu na wameanza kutoaushuhuda wa maarifa yao kwa Mungu. Wakati wa mchakato huu wa ukuaji wa taratibu, wanapata ufahamu wa taratibu na maarifa ya nia za Mungu: ya nia za Mungu katika kumuumba mwandamu, na nia za Mungu katika kumsimamia mwanadamu. Pia hatua kwa hatua wanapata ufahamu na maarifa ya tabia ya haki ya Mungu katika suala la kiini. Hakuna dhana za kibinadamu au mawazo yanayoweza kubadilisha maarifa haya. Ingawa mtu hawezi kusema kwamba katika hatua ya tano maisha ya mtu yamekomaa kabisa au kumwita mtu huyu mwenye haki au mkamilifu, mtu wa aina hii hata hivyo tayari amepiga hatua kuelekea kwenye hatua ya ukomavu katika maisha; mtu huyu tayari anaweza kuja mbele za Mungu, kusimama ana kwa ana na neno la Mungu na kuwa ana kwa ana na Mungu. Kwa sababu mtu wa aina hii tayari amepitia maneno mengi ya Mungu, amepitia majaribu yasiyohesabika na amepitia matukio yasiyohesabika ya nidhamu, hukumu na kuadibu kutoka kwa Mungu, unyenyekevu wake kwa Mungu si wa kutegemea chochote bali ni kamili. Maarifa yao juu ya Mungu yamebadilika kutoka katika hali ya kutokufahamu hadi kwenye maarifa yaliyo wazi na sahihi, kutoka yale ya juujuu hadi yale ya kina, kutoka kwenye hali ya utata na kutokuwa bainifu hadi hali ya umakinifu na thabiti, na wamebadilika kutoka kwenye kutafutatafuta kwa kupapasa na kutafuta kwa ulegevu hadi katika hali ya kuwa na maarifa kwa hakika na kushuhudia ukweli kwa vitendo. Inaweza kusemwa kwamba watu katika awamu hii wamemiliki uhalisi wa ukweli wa neno la Mungu, kwamba wamepitia kwenye njia ya kukamilishwa kama vile Petro alivyopita. Huyu ndiye mtu wa aina ya tano, yule anayeishi katika hali ya kuwa mkomavu—awamu ya kuwa mtu mzima.

Desemba 14, 2013

Iliyotangulia: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp