Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wenu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwamini Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa. Iwe ni maarifa au matendo halisi, watu wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo katika ufuatiliaji wao wa kale, wamegundua uzoefu wao wa juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu. Maarifa haya kwa upande wa watu ni aina ya maarifa ya kimtazamo; ili kufikia kiwango cha maarifa ya kimantiki kunahitaji ushughulikiaji wa kina na kuimarishwa kupitia uzoefu wa mtu. Kabla ya mwanadamu kumwelewa Mungu kikweli, inaweza kusemwa kwamba wanaamini kwa uwepo wa Mungu mioyoni mwao, lakini hawana ufahamu halisi wa maswali mahususi kama vile Yeye ni Mungu wa aina gani kwa hakika, mapenzi Yake ni nini, tabia Yake ni ipi, na mtazamo Wake halisi kwa binadamu ni upi. Hii inahatarisha sana imani ya watu katika Mungu—imani yao haiwezi kwa ufupi kufikia utakatifu au ukamilifu. Hata kama utakuwa uso kwa uso na neno la Mungu, au ukahisi kwamba umekutana na Mungu kupitia uzoefu wako, bado haiwezi kusemwa kwamba unamwelewa Yeye kabisa. Kwa sababu hujui fikira za Mungu, au kile Anachopenda na kile Anachochukia, kile kinachomfanya kuwa na ghadhabu na kile kinachomletea furaha, huna ufahamu wa kweli kumhusu. Imani yako imejengwa katika msingi wa hali isiyokuwa dhahiri na ile ya kufikirika, kulingana na matamanio yako binafsi. Bado iko mbali na imani ya kweli iko mbali na imani ya kweli, na wewe bado ungali mbali na kuwa mfuasi wa kweli. Fafanuzi za mifano kutoka kwenye hadithi hizi za Biblia zimemruhusu binadamu kuujua moyo wa Mungu, kujua ni nini Yeye Alichokuwa akifikiria katika kila hatua ya kazi Yake na kwa nini Aliifanya kazi hii, nia Yake ya awali ilikuwa ni nini na mpango Wake ulikuwa ni upi Alipoifanya, namna ambavyo Alifikia fikira Zake na namna Alivyojitayarisha na kuendeleza mpango Wake. Kupitia katika hadithi hizi, tunaweza kupata ufahamu mahususi wenye maelezo ya kina, ya kila nia mahususi ya Mungu na kila wazo halisi wakati wa kazi Yake ya usimamizi wa miaka elfu sita, na mtazamo Wake kwa binadamu katika nyakati tofauti na enzi tofauti. Kama watu wanaweza kuelewa kile ambacho Mungu alikuwa Anafikiria, mtazamo Wake ulikuwa ni upi na tabia Aliyoifichua alipokuwa Akikumbana na kila hali, kunaweza kumsaidia kila mtu kwa kina zaidi kuweza kutambua kuwepo Kwake kwa hakika, na kuhisi kwa kina zaidi ukweli na uhalisi Wake. Lengo Langu katika kusimulia hadithi hizi si kwamba watu waweze kuelewa historia ya kibiblia, wala si kuwasaidia kupata ufahamu wa vitabu vya Biblia au watu walio ndani yake, na hasa si kuwasaidia watu kuelewa maelezo zaidi kuhusu kile ambacho Mungu alifanya katika Enzi ya Sheria. Badala yake ni ili kuwasaidia watu kuelewa mapenzi ya Mungu, tabia Yake, na kila kitu Chake na kuongeza ufahamu na maarifa ya Mungu yenye uhalisi zaidi na usahihi zaidi. Kwa njia hii, mioyo ya watu inaweza, hatua kwa hatua, kufunguka kwa ajili ya Mungu na kuwa karibu zaidi na Mungu, na wanaweza kumwelewa Yeye zaidi, tabia Yake, kiini Chake, na kumjua vema zaidi Mungu wa kweli Mwenyewe.
Ufahamu wa tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho vinaweza kuwa na athari nzuri kwa binadamu. Vinaweza kuwasaidia kuwa na imani zaidi kwa Mungu, na kuwasaidia kufanikisha utiifu wa kweli na uchaji Kwake. Kisha, hawatamfuata tena kwa upofu au kumwabudu tu bila mpango. Mungu hawataki wapumbavu au wale wanaofuata umati kwa upofu, lakini Anataka kundi la watu ambao wana ufahamu na maarifa ya wazi katika mioyo yao kuhusu tabia ya Mungu na wanaweza kuchukua nafasi ya mashahidi wa Mungu, watu ambao hawawezi kamwe kumwacha Mungu kwa sababu ya uzuri Wake, kwa sababu ya kile Anacho na Alicho, na kwa sababu ya tabia Yake ya haki. Kama mfuasi wa Mungu, endapo katika moyo wako bado kuna ukosefu wa uwazi, au kuna utata au mkanganyo kuhusu kuwepo kwa kweli kwa Mungu, tabia Yake, kile Anacho na Alicho, na mpango Wake wa kumwokoa binadamu, basi imani yako haiwezi kupata sifa za Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii kumfuata Yeye, na pia Hapendi mtu wa aina hii akija mbele Zake. Kwa sababu mtu wa aina hii hamwelewi Mungu, hawezi kutoa moyo wake kwa Mungu—moyo wake umemfungwa Kwake, hivyo basi imani yake katika Mungu imejaa kasoro mbalimbali. Kumfuata kwake Mungu kunaweza tu kusemwa kuwa ni kwa kipumbavu. Watu wanaweza tu kupata imani ya kweli na kuwa wafuasi wa kweli kama watakuwa na ufahamu na maarifa ya kweli ya Mungu, jambo ambalo linaleta utiifu na uchaji wa kweli Kwake. Ni kwa njia hii tu ndiyo wanaweza kuitoa mioyo yao kwa Mungu, ili kumfungulia Yeye. Hili ndilo Mungu anataka, kwa sababu kila kitu wanachofanya na kufikiria, kinaweza kustahimili majaribu ya Mungu, na kinaweza kumshuhudia Mungu. Kila kitu Ninachowasiliana nanyi kuhusiana na tabia ya Mungu, au kuhusu kile Anacho na Alicho, au mapenzi Yake na fikira Zake katika kila kitu Anachofanya, na kutoka kwenye mtazamo wowote ule, kutoka kwa upande wowote ule Ninaozungumzia juu yake, yote haya ni kukusaidia kuwa na uhakika zaidi kuhusu uwepo wa kweli wa Mungu, na kuelewa na kufahamu zaidi kwa kweli upendo Wake kwa mwanadamu, na kuelewa na kufahamu vyema zaidi kwa kweli kile anachojali Mungu kuhusu binadamu, na tamanio Lake la dhati la kumsimamia na kumwokoa mwanadamu.
Uchambuzi wa Fikira, Mawazo na Matendo ya Mungu Tangu Uumbaji Wake wa Ulimwengu
Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza kisha kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeleo, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yaani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya ambapo hakukuwa na binadamu …
Mungu Mwenyewe Amuumba Mtu wa Kwanza Aliye Hai
Wakati Mungu aliinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisi, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwandani Wake wa kudumu. Mtu huyu angemsikiliza, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza, Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Mara tu Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, je, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi kufarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe wa aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—aliposimama mbele wa Mungu, aliyeumbwa kwa nyama na damu, aliye na mwili na umbo, na aliyeweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuihisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe huyu aliye hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia lilimgusa na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe huyu aliye hai aliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza Alipowahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambayo Hakuwahi kupata hapo awali. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa upendo Wake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na faraja ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, moyoni Mwake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali matakwa ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani kubwa kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.
Baada ya kuviumba vitu vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.
Mungu Afanya Msururu wa Kazi Zisizo na Kifani Katika Wakati wa Enzi ya Sheria
Kisha, si kipindi kirefu baada ya Mungu kuwaumba binadamu, tunaona kutoka katika Biblia ya kwamba kulikuwa na gharika kubwa kote ulimwenguni. Nuhu anatajwa kwenye rekodi ya gharika, na inaweza kusemwa kwamba Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kupokea mwito wa Mungu ili afanye kazi na Yeye ili kukamilisha kazi ya Mungu. Bila shaka, wakati huo ndio uliokuwa pia wa kwanza kwa Mungu kumwita mtu ulimwenguni kufanya kitu kulingana na agizo Lake. Mara tu Nuhu alipokamilisha kuijenga safina, Mungu alileta gharika katika nchi kwa mara ya kwanza. Mungu alipoiharibu nchi kwa gharika, ndiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu Alipowaumba wanadamu ambapo Alihisi kuzidiwa na chuki kwa binadamu; hili ndilo lililomlazimu Mungu kufanya uamuzi wa uchungu wa kuharibu kizazi hiki cha binadamu kupitia kwa gharika. Baada ya gharika kuiharibu dunia, Mungu alifanya agano Lake la kwanza na binadamu kwamba Hatawahi kufanya hivi tena. Ishara ya agano hili ilikuwa upinde wa mvua. Hili ndilo lililokuwa agano la kwanza la Mungu na binadamu, hivyo basi upinde wa mvua ndio uliokuwa ishara ya kwanza ya agano lililotolewa na Mungu; upinde huu wa mvua ni jambo halisi lililopo. Ni kule kuwepo kabisa kwa upinde huu wa mvua ambako humfanya Mungu mara nyingi ahisi huzuni kutokana na kizazi cha binadamu cha awali ambacho Alikipoteza, na huwa ni kumbusho la kila mara Kwake kuhusiana na kile kilichowafanyikia…. Mungu asingeweza kupunguza mwendo Wake—Alikuwa na hamu kubwa ya kuchukua hatua inayofuata katika usimamizi Wake. Hivyo basi, Mungu alimchagua Ibrahimu kama chaguo Lake la kwanza kwa kazi Yake katika Israeli nzima. Hii ndiyo iliyokuwa pia mara ya kwanza kwa Mungu kumchagua mteuliwa kama huyo. Mungu aliamua kuanza kutekeleza kazi Yake ya kumwokoa binadamu kupitia kwa mtu huyu, na kuendeleza kazi Yake miongoni mwa vizazi vya mtu huyu. Tunaweza kuona katika Biblia kwamba hivi ndivyo Mungu alivyomfanyia Ibrahimu. Basi Mungu akaifanya Israeli kuwa nchi ya kwanza iliyochaguliwa, na Akaianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria kupitia kwa watu Wake waliochaguliwa, Waisraeli. Tena kwa mara ya kwanza, Mungu aliwapa Waisraeli sheria na kanuni zilizo wazi ambazo mwanadamu anafaa kufuata, na Akazieleza kwa kina. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpatia binadamu sheria kama hizo mahususi na za kawaida kuhusu namna wanavyofaa kutoa dhabihu, jinsi wanavyofaa kuishi, kile wanachofaa kufanya na kutofanya, ni sikukuu na siku gani wanazofaa kutilia maanani, na kanuni za kufuata katika kila kitu walichofanya. Hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpa binadamu ufafanuzi kama huo, taratibu za kawaida na kanuni kwa ajili ya maisha yao.
Ninaposema “mara ya kwanza,” inamaanisha Mungu hakuwa Amewahi kukamilisha kazi kama hiyo hapo awali. Ni kitu ambacho hakikuwepo awali, na hata ingawa Mungu alikuwa Amemuumba binadamu na Alikuwa ameumba aina zote za viumbe na vitu vyenye uhai, Hakuwa amewahi kukamilisha kazi ya aina hiyo. Kazi hii yote ilihusisha usimamizi wa Mungu kwa binadamu; yote ilihusu binadamu na wokovu Wake na usimamizi wa binadamu. Baada ya Ibrahimu, Mungu alifanya chaguo tena kwa mara ya kwanza—Alimchagua Ayubu kuwa yule aliyeishi chini ya sheria na ambaye angeweza kustahimili majaribu ya Shetani huku akiendelea kumcha Mungu na kujiepusha na uovu na kuweza kumtolea Yeye ushuhuda. Hii pia ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumruhusu Shetani kumjaribu mtu na mara ya kwanza Alipoweka dau na Shetani. Mwishowe, kwa mara ya kwanza, Mungu alimpata mtu aliyekuwa na uwezo wa kusimama kama shahidi Wake huku akiwa amemkabili Shetani—mtu ambaye angeweza kumshuhudia Yeye na kumwaibisha kabisa Shetani. Tangu Mungu alipomuumba mwanadamu, huyu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza, aliyempata ambaye aliweza kumshuhudia Yeye. Mara tu Alipompata mwanadamu huyu, Mungu alikuwa na shauku zaidi ya kuendeleza usimamizi Wake na kuchukua hatua inayofuata katika kazi Yake, Akitayarisha chaguo Lake lifuatalo na mahali Pake pa kazi.
Baada ya kushiriki kuhusu haya yote, je, mnao ufahamu wa kweli wa mapenzi ya Mungu? Mungu anachukulia tukio hili la usimamizi Wake wa wanadamu, la wokovu Wake kwa wanadamu, kuwa ya muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Anafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, wa lengo, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi jinsi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi wanadamu ni wadhaifu kiasi gani, au uasi wa wanadamu ni wa kiasi gani, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake nyingi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kumsimamia na kumwokoa mwanadamu. Wakati Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha na kuachilia kwa wanadamu bila kuficha juhudi Zake nyingi, kile Anacho na Alicho, hekima na uweza, na kila kipengele cha tabia Yake. Anaachilia na kuonyesha haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya hapo awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipa gharama kubwa kwa ajili yao na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa kila mara na wao, Hakati tamaa juu yao na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …
Baada ya kusikia haya yote leo, mnaweza kuhisi kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni cha kawaida sana. Inaonekana kwamba binadamu siku zote wamehisi mapenzi fulani ya Mungu kwao kutokana na matamshi Yake na pia kazi Yake, lakini siku zote kuna umbali fulani kati ya hisia zao au maarifa yao na kile ambacho Mungu anafikiria. Kwa hivyo, Nafikiri ni muhimu kuwasiliana na watu wote kuhusu ni kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, na maelezo zaidi yanayoonyesha tamanio Lake la kuwapata watu aliokuwa Akitumainia. Ni muhimu kushiriki habari hii na kila mmoja, ili kila mmoja aweze kuwa wazi moyoni mwake. Kwa sababu kila fikira na wazo la Mungu, na kila awamu na kila kipindi cha kazi Yake vinafungamana ndani ya, na vyote hivi vimeunganishwa kwa karibu na, usimamizi Wake mzima wa kazi, unapoelewa fikira na mawazo ya Mungu, na mapenzi Yake katika kila hatua ya kazi Yake, ni sawa na ufahamu wa chanzo cha kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Ni katika msingi huu ndipo ufahamu wako wa Mungu unapoanza kuwa wa kina. Ingawa kila kitu ambacho Mungu alifanya Alipoumba kwanza ulimwengu ambacho Nilitaja hapo awali, kwa sasa inaonekana kuwa ni “taarifa” fulani tu, na inaonekana kwamba haina umuhimu sana katika utafutaji wa ukweli, katika kipindi cha uzoefu wako kutakuwa na siku ambapo hutafikiria kuwa ni jambo rahisi sana kama mkusanyiko tu wa taarifa, wala kwamba ni kitu rahisi sana kama mafumbo fulani. Kadri maisha yako yanavyoendelea, pale Mungu anapopata nafasi fulani katika moyo wako, au unapokuja kuelewa kwa uwazi na kwa kina mapenzi Yake, basi utaweza kuelewa kwa kweli faida na umuhimu wa kile Ninachokizungumzia leo. Haijalishi ni kwa kiwango kipi umeyakubali haya; ni muhimu kwamba uelewe na ujue mambo haya. Wakati Mungu anapofanya jambo, wakati Anapotekeleza kazi Yake, haijalishi kama amefanya kwa mawazo Yake au kwa mikono Yake, haijalishi kama ni mara ya kwanza ambapo Amelifanya au kama ni mara ya mwisho—mwishowe, Mungu anao mpango, na madhumuni Yake na fikira Zake vyote vimo katika kila kitu Anachokifanya. Madhumuni na fikira hizi vinawakilisha tabia ya Mungu, na vinaonyesha kile Anacho na Alicho. Vitu hivi viwili—tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho—lazima vieleweke na kila mmoja. Pale tu mtu anapoelewa tabia Yake na kile Anacho na Alicho, ataanza kuelewa kwa utaratibu ni kwa nini Mungu anafanya kile Anachofanya na kwa nini Anasema kile Anachosema. Kutokana na hayo, anaweza kuwa na imani zaidi ya kumfuata Mungu, kuufuatilia ukweli, na kufuatilia mabadiliko katika tabia. Hivyo ni kusema, ufahamu wa binadamu kuhusu Mungu na imani yake katika Mungu haviwezi kutenganishwa.
Ikiwa kile ambacho watu hupata ufahamu kuhusu au kupata kuelewa ni tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho, basi kile wanachopata kitakuwa ni uzima unaotoka kwa Mungu. Mara tu uzima huu unapofanyika ndani yako, uchaji wako kwa Mungu utaongezeka zaidi na zaidi, na kupata matokeo haya kunatokea kwa kawaida sana. Kama hutaki kuelewa au kujua kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake, kama hutaki hata kutafakari juu ya mambo haya au kuyazingatia, Naweza kukuambia kwa hakika kwamba hiyo njia unayoifuatilia katika imani yako kwa Mungu haitawahi kukuruhusu kuyaridhisha mapenzi Yake au kupata sifa Zake. Zaidi ya hayo, huwezi kamwe kufikia wokovu—haya ndio matokeo ya mwisho. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kumfungukia Yeye kwa kweli. Mara tu wanapomwelewa Mungu, wataanza kuthamini na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa shauku na imani. Unapothamini na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi jinsi ambavyo mabadilishano yako na Mungu yalivyokuwa ya aibu na dharau, madai yako kwa Mungu, na tamaa zako mwenyewe za kupita kiasi.. Moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna usaliti, hakuna udanganyifu, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kuna nuru na uadilifu tu; kuna haki na huruma. Kumejaa upendo na utunzaji, kumejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Ulimwengu huu usio na mwisho umejaa hekima za Mungu, na umejawa na nguvu Zake; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila kipengele cha kile ambacho Mungu Anacho na Alicho, kile kinachomletea Yeye furaha, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani anaweza kuona. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako ikiwa utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Anacho na Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile ambacho Anacho na Alicho kinastahili kuthaminiwa sana. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vitu na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna kitu chochote cha nje kitakachoweza kukuvuta tena, au kwamba kitu chochote cha nje kitakachowahi tena kuweza kukushawishi ukilipie gharama yoyote ile. Katika kunyenyekea kwa Mungu utaona ukuu Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya ambalo hapo awali uliliamini kuwa ni dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu sana, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokutokea katika maisha yako, na hata wale unaowapenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu ndiye unayethamini zaidi. Siku hiyo itakapowadia, Naamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkuu sana na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu ambacho Mungu Anacho na Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni kwa msingi gani ndipo uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengwa kwa msingi wa ufahamu wa binadamu wa tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni lengo la maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.
Mara ya Kwanza Mungu Kuwa Mwili Ili Afanye Kazi
Tumemaliza tu kuzungumzia kuhusu kazi zote ambazo Mungu alizikamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia ya Mungu Mwenyewe na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa zaidi kile ambacho Mungu anacho na alicho, hatuwezi tu kuishia katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, kwa mara nyingine tena Mungu Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza. Kazi katika enzi hii mpya kwa Mungu na hata kwa mwanadamu ilikuwa hatua mpya ya kuanzia. hatua hii mpya ya kuanzia ilikuwa tena kazi mpya ambayo Mungu alifanya kwa mara ya kwanza. Kazi hii mpya ilikuwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea hapo awali ambacho Mungu alitekeleza na hakikufikirika na binadamu na viumbe vyote. Ni kitu ambacho kwa sasa kinajulikana kwa watu wote—hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kugeuka kuwa mwanadamu, na kwa mara ya kwanza Alianza kazi mpya katika umbo la mwanadamu, akiwa na utambulisho wa mwanadamu. Kazi hii mpya ilionyesha kwamba Mungu alikuwa Amekamilisha kazi Yake katika Enzi ya Sheria, kwamba Asingefanya au kusema tena chochote chini ya sheria. Wala Asingewahi tena kuzungumza au kufanya chochote kwa mfumo wa sheria au kulingana na kanuni au masharti ya sheria. Yaani, kazi Yake yote inayotokana na sheria ilisitishwa milele na isingeendelezwa, kwa sababu Mungu alitaka kuanza kazi mpya na kufanya mambo mapya, na mpango Wake kwa mara nyingine tena ulikuwa na hatua mpya ya kuanzia. Hivyo basi, Mungu lazima Angemwongoza binadamu hadi katika enzi inayofuata.
Ikiwa hii ilikuwa habari ya furaha au ya kisirani kwa wanadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemwa kwamba hizi hazikuwa habari za furaha, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na kanuni, ambao walifuata tu mafundisho lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi ya zamani ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa mnyoofu na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwaminifu kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza kulikuwa ni habari zenye furaha sana. Kwani tangu kuwepo na binadamu, hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu kuonekana na kuishi miongoni mwa wanadamu katika umbo ambalo halikuwa Roho; badala yake, Alizaliwa na mwanadamu na kuishi miongoni mwa watu kama Mwana wa Adamu, na kufanya kazi katikati yao. Hii “mara ya kwanza” ilizivunja dhana za watu na pia ilikuwa zaidi ya matarajio yote. Aidha, wafuasi wote wa Mungu walipata manufaa yenye kuonekana. Mungu hakuikomesha tu enzi nzee, lakini pia Alikomesha mbinu Zake za kale za kufanya kazi pamoja na mitindo ya kufanya kazi. Hakuruhusu tena wajumbe Wake kuwasilisha mapenzi Yake, na Hakufichika tena katika mawingu na Hakuonekana tena au kuzungumza na wanadamu kwa kuamrisha kupitia radi. Tofauti na chochote kile cha awali, kupitia kwa mbinu ambayo haikufirika kwa binadamu ambayo pia ilikuwa ngumu kwa wao kuelewa na kukubali—kupata mwili—Aligeuka na kuwa Mwana wa Adamu ili kuendeleza kazi ya enzi hiyo. Kitendo hiki cha Mungu kiliwashtua wanadamu; kiliwafanya wawe na aibu, kwa sababu Mungu kwa mara nyingine alikuwa ameanza kazi mpya ambayo Hakuwa amewahi kufanya hapo awali. Leo, tutaangalia ni kazi gani mpya ambayo Mungu alikamilisha katika enzi mpya, na tutazingatia kile ambacho tunaweza kujifunza kutoka kwenye kazi hii mpya kulingana na tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho?
Yafuatayo ni maneno yaliyorekodiwa katika Agano Jipya la Biblia:
1. Yesu Avunja Masuke ya Nafaka ili Kula Siku ya Sabato
Mat 12:1 Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.
2. Mwana wa Adamu Ndiye Bwana wa Sabato
Mat 12:6-8 Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.
Hebu kwanza tuangalie kifungu hiki: “Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.”
Kwa nini Nimeichagua dondoo hii? Dondoo hii ina uhusiano upi na tabia ya Mungu? Katika maandiko haya kitu cha kwanza tunachojua ni kwamba ilikuwa ni siku ya Sabato, lakini Bwana Yesu alipita kule nje na kuwaongoza wanafunzi Wake katika mashamba ya nafaka. Lakini kilicho cha “hatari” zaidi ni kwamba waliweza hata “wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.” Katika Enzi ya Sheria, sheria ya Yehova Mungu ilisema kwamba watu hawangeweza kwenda nje au kushiriki shughuli za kawaida katika siku ya Sabato—kulikuwa na mambo mengi ambayo hayangefanywa siku ya Sabato. Hatua hii ya Bwana Yesu ilikuwa ya kuchanganya hasa kwa wale waliokuwa wameishi chini ya sheria kwa muda mrefu, na iliweza hata kuchochea upinzani mkubwa. Kuhusiana na mkanganyiko wao na jinsi walivyouzungumzia kile ambacho Yesu alifanya, tutaweka hilo pembeni kwa sasa na kuzungumzia kwanza kwa nini Bwana Yesu alichagua kufanya hivi katika siku ya Sabato, kati ya siku zote, na kile Alichotaka kuwasilisha kwa watu waliokuwa wakiishi katika enzi ya kale kupitia katika hatua hii. Huu ndio uhusiano kati ya dondoo hii na tabia ya Mungu ambayo Ningependa kuzungumzia.
Bwana Yesu alipokuja, Alitumia vitendo Vyake vya utendaji kuwambia watu: kwamba Mungu alikuwa ameiondoa Enzi ya Sheria na alikuwa ameanza kazi mpya, na kwamba kazi hii mpya haikuhitaji kuzingatiwa kwa Sabato. Mungu alipotoka katika mipaka ya siku ya Sabato, hicho kilikuwa ni kionjo tu cha mapema cha kazi Yake mpya, kazi haisi na kubwa ilikuwa bado inakuja. Bwana Yesu alipoanza kazi Yake, tayari Alikuwa ameacha nyuma zile pingu za Enzi ya Sheria, na alikuwa ametupilia mbali zile taratibu na kanuni zilizokuwa za enzi hiyo. Ndani Yake, hapakuwa na dalili ya kitu chochote kilichohusiana na sheria; Alikuwa ameitupilia mbali kabisa na hakuizingatia tena, na Hakuwahitaji tena mwanadamu kuifuata. Kwa hivyo hapa unaona kwamba Bwana Yesu alipita katika mashamba ya nafaka siku ya Sabato; kwamba Bwana hakupumzika, lakini Alikuwa akipita kule nje Akifanya kazi. Hiki kitendo Chake kilikuwa cha kushtua kwa dhana za watu na iliweza kuwawasilishia ujumbe kwamba Hakuishi tena chini ya sheria na kwamba Alikuwa ameacha ile mipaka ya Sabato na kujitokeza mbele ya mwanadamu na katikati yao katika taswira mpya, huku akiwa na njia mpya ya kufanya kazi. Hiki kitendo Chake kiliwaambia watu kwamba Alikuwa ameleta pamoja naye kazi mpya iliyoanza kwa kwenda nje ya sheria na kwenda nje ya Sabato. Wakati Mungu alitekeleza kazi Yake mpya, Hakushikilia tena ya kale, na Hakujali tena kuhusu taratibu za Enzi ya Sheria. Wala Hakuathiriwa na kazi Yake katika enzi iliyotangulia, lakini badala yake alifanya kazi siku ya Sabato kama vile Alivyofanya katika siku zingine, na wanafunzi Wake walipokuwa na njaa siku ya Sabato, wangeweza kuvunja masuke ya nafaka ili kula. Haya yote yalikuwa ya kawaida sana machoni pa Mungu. Mungu angeweza kuwa na mwanzo mpya kwa kazi nyingi ambazo Agetaka kufanya na mambo Anayotaka kusema. Mara tu Anapokuwa na mwanzo mpya, Hataji kazi Yake ya awali tena wala kuiendeleza. Kwani Mungu anazo kanuni Zake katika kazi Yake. Anapotaka kuanzisha kazi mpya, ndipo Anapotaka kumleta mwanadamu katika awamu mpya ya kazi Yake, na ndio wakati ambao kazi Yake imeingia katika awamu ya juu zaidi. Kama watu wanaendelea kutenda kulingana na misemo au taratibu za kale au kuendelea kuzishikilia, Hatakumbuka au kulisifu jambo hili. Hii ni kwa sababu tayari Ameileta kazi mpya, na ameingia katika awamu mpya ya kazi Yake. Anapoanzisha kazi mpya, Anaonekana kwa mwanadamu akiwa na taswira mpya kabisa, kutoka katika mtazamo mpya kabisa, na kwa njia mpya kabisa ili watu waweze kuona vipengele tofauti vya tabia Yake na kile ambacho Anacho na Alicho. Hii ni mojawapo ya malengo Yake katika kazi Yake mpya. Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia iliyotumiwa na wengi; Anapofanya kazi na kuzungumza, Yeye hawi na vizuizi kama watu wanavyofikiria. Kwa Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa, na hakuna vizuizi, hakuna mipaka —kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye yuko hai na ni mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi Yake yoyote. Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona au kutathmini kazi Yake mpya, Ataitekeleza kazi Yake bila wasiwasi. Hatajali kuhusu dhana za mtu yeyote au vidole vinavyonyooshwa katika kazi na maneno Yake, au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya. Hakuna yeyote kati ya viumbe vilivyoumbwa anayeweza kutumia akili ya kibinadamu, au mawazo ya kibinadamu, maarifa, au maadili ili kupima au kufafanua kile ambacho Mungu anafanya, au kudharau, kuvuruga au kuharibu kazi Yake. Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya; na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, tukio, au kitu, wala haitakatizwa na nguvu zozote za uadui. Kwa kadiri kazi Yake mpya inavyohusika, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za uadui na uzushi na dhana zote za wanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu. Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza, kwa hakika itaendelezwa na kupanuliwa katikati ya wanadamu, na kwa hakika itatekelezwa bila kuzuiliwa katika ulimwengu mzima mpaka pale ambapo kazi Yake kubwa itakapokuwa imekamilika imekamilika. Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake. Hivyo basi, Bwana Yesu angeweza kwenda nje waziwazi na kufanya kazi katika siku ya Sabato kwa sababu ndani ya moyo Wake hakukuwa na sheria zozote, na hakukuwa na maarifa au mafundisho yoyote yaliyotokana na wanadamu. Kile Alichokuwa nacho kilikuwa ni kazi mpya ya Mungu na njia Yake, na kazi Yake ndio iliyokuwa njia ya kumweka huru mwanadamu, kumwachilia, kumruhusu kuwepo katika nuru na kumruhusu kuishi. Na wale wanaoabudu sanamu au miungu ya uwongo wanaishi kila siku wakiwa wamefungwa na Shetani, wakiwa wamezuiliwa na aina zote za sheria na mila—leo kitu kimoja kinazuiliwa, kesho kingine—hakuna uhuru katika maisha yao. Wao ni sawa na wafungwa waliofungwa pingu, wanaishi maisha yasiyo na furaha ya kuzungumzia. “Kuzuiliwa” inawakilisha nini? Inawakilisha shurutisho, utumwa na uovu. Punde tu mtu anapoabudu sanamu, anaabudu mungu wa uwongo, akimwabudu roho wa uovu. Kuzuiliwa kunatokea wakati ambao shughuli kama hizo zinahusishwa. Huwezi kula hiki au kile, leo huwezi kwenda nje, kesho huwezi kuwasha jiko lako upike, siku inayofuata huwezi kuhamia katika nyumba mpya, siku fulani lazima zichaguliwe kwa minajili ya harusi na mazishi, na hata za wakati wa kujifungua mtoto. Haya yote yanaitwa nini? Haya yanaitwa kuzuiliwa; ni utumwa wa mwanadamu, na ndizo pingu za maisha za Shetani na pepo wabaya wanaowadhibiti, na wanaozuilia mioyo yao na miili yao. Je, vizuizi hivi vipo kwa Mungu? Tunapozungumzia utakatifu wa Mungu, unafaa kwanza kufikiria haya: Kwa Mungu hakuna vizuizi. Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake, lakini hakuna kuzuiliwa, kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.
Sasa hebu tuangalie dondoo ifuatayo: “Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya sabato” (Mat 12:6-8). Neno “hekalu” inarejelea nini hapa? Ili kuiweka kwa urahisi, inarejelea jengo refu la kupendeza, na katika Enzi ya Sheria, hekalu lilikuwa ni pahali pa makuhani kumwabudu Mungu. Bwana Yesu aliposema “mahali hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu,” je, “yupo aliye” ilikuwa inamrejelea nani? Ni wazi, “yupo aliye” ni Bwana Yesu katika mwili kwa sababu Yeye tu ndiye aliyekuwa mkuu kuliko hekalu. Na maneno hayo yaliwaambia watu nini? Yaliwaambia watu watoke hekaluni—Mungu alikuwa tayari ameshatoka nje na hakuwa tena akifanyia kazi ndani yake, hivyo basi watu wanafaa kutafuta nyayo za Mungu nje ya hekalu na kufuata nyayo Zake katika kazi Yake mpya. Usuli wa Bwana Yesu kusema haya ilikuwa kwamba chini ya sheria, watu walikuwa wamekuja kuona hekalu kama kitu kilichokuwa kikuu zaidi kuliko Mungu Mwenyewe. Yaani, watu waliliabudu hekalu badala ya kumwabudu Mungu, hivyo basi Bwana Yesu akawaonya kutoabudu sanamu, lakini kumwabudu Mungu kwa sababu Yeye ndiye Aliye mkuu zaidi. Hivyo basi, alisema: “Naitaka rehema, na siyo sadaka.” Ni wazi kwamba machoni pa Bwana Yesu, watu wengi sana walioishi chini ya sheria hawakumwabudu tena Yehova, lakini walikuwa tu wakipitia mchakato wa kutoa sadaka na Bwana Yesu aliamua kwamba mchakato huu ulikuwa ibada ya sanamu. Waabudu sanamu hawa waliliona hekalu kama kitu kikuu, cha juu zaidi kuliko Mungu. Ndani ya mioyo yao kulikuwa tu na hekalu, wala si Mungu, na kama wangelipoteza hekalu, wangepoteza mahali pao pa kukusanyika. Bila hekalu hawangekuwa na mahali popote pa kuabudu na wasingeweza kutoa sadaka zao. Mahali pao pa kukusanyika kama palivyojulikana ndipo walipofanyia shughuli zao kwa kisingizio cha kumwabudu Yehova Mungu, na hivyo basi wakaruhusiwa kuishi katika hekalu na kutekeleza shughuli zao binafsi. Ule utoaji wao wa dhabihu kama ulivyojulikana ulikuwa tu kutekeleza shughuli zao za kibinafsi za aibu wakisingizia kwamba walikuwa wanaendesha ibada yao katika hekalu. Hii ndiyo iliyokuwa sababu iliyowafanya watu wakati huo kuliona hekalu kuwa kuu kuliko Mungu. Bwana Yesu alisema haya ili kuwaonya watu, kwa sababu walilitumia hekalu kama maficho, na sadaka kama kisingizio cha kuwadanganya watu na kumdanganya Mungu. Kama mkitumia maneno haya kwa wakati wa sasa, yangali bado halali na yenye umuhimu sawa. Ingawa watu wa leo wameweza kupitia kazi tofauti za Mungu kuliko watu wa Enzi ya Sheria walivyowahi kupitia, kiini cha asili yao ni kile kile. Katika muktadha wa kazi ya leo, watu bado watafanya aina sawa ya mambo kama yale ya “hekalu kuwa kuu kuliko Mungu”. Kwa mfano, watu huona kutimiza wajibu wao kama kazi yao; wanaona kutoa ushuhuda kwa Mungu na kupigana na joka kuu jekundu kama harakati za kisiasa katika kulinda haki za kibinadamu, kwa ajili ya demokrasia na uhuru; wao hugeuza wajibu wao ili kutumia ujuzi wao kuwa ajira, lakini wanachukulia kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kuwa si kitu bali ni sehemu tu ya mafundisho ya kidini ya kufuatwa; na kadhalika. Je, tabia hizi kimsingi si zipo sawa na “hekalu kuwa kuu kuliko Mungu”? Isipokuwa tu kwamba, miaka elfu mbili iliyopita, watu walikuwa wakifanya shughuli zao za kibinafsi katika mahekalu yanayoonekana, lakini leo, watu wanafanya shughuli zao za kibinafsi katika mahekalu yasiyoonekana. Wale watu wanaothamini masharti huona masharti kuwa ni makuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda hadhi huona kuwa hadhi ni kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda ajira zao huziona ajira hizo kuwa kuu zaidi kuliko Mungu na kadhalika—maonyesho yao yote yananifanya Mimi kusema: “Watu humsifu Mungu kuwa ndiye mkuu zaidi kupitia kwa maneno yao, lakini machoni pao kila kitu ni kikuu zaidi kuliko Mungu.” Hii ni kwa sababu punde tu watu wanapopata fursa katika njia yao ya kumfuata Mungu ili kuonyesha vipaji vyao, au kuendelea na shughuli zao binafsi za kibiashara au ajira zao wenyewe, wanakuwa mbali na Mungu na kufanya kwa bidii ajira wanayoipenda. Kuhusiana na kile ambacho Mungu amewakabidhi, na mapenzi Yake, mambo hayo yote yametupiliwa mbali kitambo. Katika hali hii, ni nini tofauti baina ya watu hawa na wale wanaoendesha biashara zao katika hekalu miaka elfu mbili iliyopita?
Kisha, hebu tuangalie sentensi ya mwisho katika kifungu hiki cha maadiko: “Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya Sabato.” Je, kunao upande wa utendaji kwa sentensi hii? Je, unaweza kuona upande wa utendaji kwa sentensi hii? Kila kitu anachosema Mungu kinatoka moyoni Mwake, kwa hivyo kwa nini Alisema hivi? Unaielewa vipi sentensi hii? Unaweza kuelewa maana ya sentensi hii sasa, lakini wakati huo si watu wengi walikuwa wanaielewa kwa sababu binadamu alikuwa tu ametoka katika Enzi ya Sheria. Kwao, kutoka katika Sabato lilikuwa jambo gumu sana kufanya, sembuse kuelewa Sabato ya kweli ilikuwa ni nini.
Sentensi “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” inawaambia watu kwamba kila kitu kuhusu Mungu si cha asili ya kimwili, na ingawa Mungu anaweza kukupa mahitaji yako yote ya kimwili, mara tu mahitaji yako yote ya kimwili yametimizwa, je, kuridhika kutoka kwa vitu hivi kunaweza kuchukua nafasi ya ufuatiliaji wako wa ukweli? Kwa kweli hiyo haiwezekani! Tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, ambavyo tumeshiriki kuvihusu, vyote ni ukweli. Thamani yake haiwezi kupimwa kwa vitu vyovyote vinavyoonekana, haijalishi ni vya thamani kiasi gani, wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa pesa, kwa sababu si kitu kinachoonekana, na inatoa mahitaji ya moyo wa kila mtu. Kwa kila mmoja, thamani ya ukweli huu usioshikika inafaa kuwa kubwa zaidi kuliko thamani ya vitu vyovyote vya anasa unavyofikiria kuwa ni vizuri, sivyo? Kauli hii ni kitu mnachohitaji kukiwazia. Hoja kuu ya kile nilichosema ni kwamba kile ambacho Mungu anacho na alicho na kila kitu cha Mungu ndivyo vitu vya muhimu zaidi kwa kila mtu na haviwezi kubadilishwa na kitu chochote cha kimwili. Nitakupa mfano: Ukiwa na njaa, unahitaji chakula. Chakula hiki kinaweza kuwa kizuri kwa kiasi fulani au kinaweza kuwa kimekosa kitu fulani kwa kiasi fulani, lakini mradi tu umekula ukashiba, hisia ile isiyofurahisha ya kuwa na njaa haitakuwepo tena—itakuwa imeondoka. Unaweza kuketi pale kwa amani, na mwili wako utakuwa umetulia. Njaa ya watu inaweza kutatuliwa kwa chakula, lakini ukiwa unamfuata Mungu na kuhisi kwamba huna ufahamu wowote Kwake, unawezaje kutatua utupu huu katika moyo wako? Hali hii inaweza kusuluhishwa kwa chakula? Au unapomfuata Mungu na huelewi mapenzi Yake, ni nini unachoweza kutumia ili kufidia ile shauku katika moyo wako? Katika mchakato wa uzoefu wako wa wokovu kupitia kwa Mungu, wakati ukifuatilia mabadiliko katika tabia yako, kama huelewi mapenzi Yake au hujui ukweli ni nini, kama huelewi tabia ya Mungu, huhisi wasiwasi sana? Je, huhisi njaa kali na kiu katika moyo wako? Je, hizi hisia hazitakufanya ukose utulivu moyoni mwako? Kwa hivyo unawezaje kusuluhisha shauku hiyo moyoni mwako—je, kuna njia ya kutatua suala hilo? Baadhi ya watu wanaenda kufanya manunuzi, wengine wanawatafuta marafiki zao ili kuwaambia yaliyo moyoni, wengine wanalala mpaka watosheke, wengine wanasoma zaidi maneno ya Mungu, au wanaweka bidii zaidi na kutumia jitihada nyingi zaidi kukamilisha wajibu wao. Je, mambo haya yanaweza kutatua matatizo yako halisi? Nyinyi nyote mnaelewa kikamilifu aina hizi za mazoea. Unapohisi kuwa huna nguvu, unapohisi tamanio kubwa la kupata nuru kutoka kwa Mungu ili kukuruhusu kujua uhalisi wa ukweli na mapenzi Yake, je,ni nini unachohitaji zaidi? Kile unachohitaji si mlo kamili, na wala si maneno machache mema. Zaidi ya hayo, si faraja ya muda mfupi na kutosheka kwa mwili—kile unachohitaji ni Mungu kuweza kukueleza moja kwa moja, kwa uwazi kile unachofaa kufanya na namna unavyofaa kukifanya, kuweza kukuonyesha kwawazi ukweli ni nini. Baada ya kuelewa haya, hata kama utapata ufahamu mdogo tu, je, hutahisi kuwa umetosheka zaidi katika moyo wako kuliko vile ambavyo ungekuwa umekula mlo mzuri? Wakati moyo wakoumeridhika, je, moyo wako, na nafsi yako yote, havitapata utulivu wa kweli? Kutokana na mfano huu na uchambuzi, je, mnaelewa sasa ni kwa nini Nilitaka kushiriki na nyinyi kuhusu sentensi hii, “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato”? Maana yake ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu, kile Anacho na Alicho, na kila kitu kumhusu vyote ni vikuu zaidi kuliko kitu kingine chochote, kikiwemo kile kitu au yule mtu ambaye uliwahi kuamini kuwa unamthamini zaidi. Hivyo ni kusema, kama mtu hawezi kupata maneno kutoka katika kinywa cha Mungu au kama haelewi mapenzi Yake, hawezi kupata pumziko. Katika yale mtakayopitia katika siku zako za usoni, mtaelewa ni kwa nini Nilitaka nyinyi kuona dondoo hii leo—hii ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na uzima. Ukweli kwa wanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea utulivu moyoni mwako.
Je, ufahamu wenu wa ukweli umehusianishwa na hali zenu wenyewe? Katika maisha halisi, lazima kwanza ufikirie ukweli upi unahusiana na watu, matukio, na vitu ambavyo umekumbana navyo; ni katika ukweli huu ndimo unaweza kupata mapenzi ya Mungu na kuunganisha kile ulichokumbana nacho na mapenzi Yake. Iwapo hujui ni vipengele vipi vya ukweli vinavyohusiana na mambo ambayo umekumbana nayo lakini badala yake unaenda kwa njia ya moja kwa moja kutafuta mapenzi ya Mungu, huu ni mtazamo ambao hauna mwelekeo ambao hauwezi kufanikisha matokeo. Kama unataka kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu, kwanza unahitaji kuangalia ni mambo ya aina gani ambayo yametendeka kwako, ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mambo hayo yana uhusiano navyo, na kisha uutafute ukweli maalum katika neno la Mungu ambao unahusiana na kile ulichopitia. Kisha utafute njia ya utendaji ambayo ni sahihi kwako katika ukweli huo; kutokana na njia hii unaweza kupata ufahamu usio wa moja kwa moja kuhusu mapenzi ya Mungu. Kutafuta na kutenda ukweli si kufuata mafundisho au kufuata fomyula bila kufikiria. Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujafa—bali ni uzima wenyewe, ni kitu ambacho kina uhai, na ni kanuni ambayo lazima kiumbe kilichoumbwa kifuate katika Maisha na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima, kwa vyoyote vile, uelewe kupitia uzoefu. Haijalishi ni hatua gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile ambacho Mungu anacho na alicho yote yanaonyeshwa katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho mwenyewe ni ukweli kwa njia yake; ukweli ni udhihirisho halisi wa tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, ndani ya hayo, kuna ukweli; ukweli ni udhihirisho halisi wa tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho. Inafanya kile ambacho Mungu anacho na alicho kiwe halisi, na inaonyesha kwa uwazi kile ambacho Anacho na Alicho; inakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu anapenda, kile ambacho Hakipendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, ni watu gani Anaowadharau na ni watu gani Anaopendezwa nao. Katika ule ukweli ambao Mungu anawaonyesha watu, wanaweza kuona uzuri, hasira, huzuni, na furaha Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Mbali na kujua kile Mungu Anacho na alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kivitendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu wao umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kunatokea kutofautiana na vile ambavyo Mungu alivyo mwenyewe kwa kweli.
Kile tunachozungumzia sasa kimo ndani ya ule upana wa hadithi zilizorekodiwa katika Biblia. Kupitia katika hadithi hizi, na kupitia uchambuzi wa mambo haya yaliyofanyika, watu wanaweza kuelewa tabia Yake na kile Anacho na Alicho ambavyo Ameonyesha, na kuwaruhusu kujua kila kipengele cha Mungu kwa upana zaidi, kwa kina zaidi, kikamilifu, na kwa undani zaidi. Kwa hivyo, je, njia pekee ya kujua kila kipengele cha Mungu ni kupitia hadithi hizi? Hapana, siyo njia pekee! Kwani kile Mungu anachosema na kazi Anayofanya katika Enzi ya Ufalme kinaweza kuwasaidia watu kwa njia bora zaidi kujua tabia Yake, na kuijua kikamilifu. Hata hivyo, Nafikiri ni rahisi zaidi kujua tabia ya Mungu na kuelewa kile Anacho na Alicho kupitia baadhi ya mifano au hadithi zilizorekodiwa katika Biblia ambazo watu wanazifahamu. Nikichukua maneno ya hukumu na kuadibu na ukweli ambao Mungu anaonyesha leo ili kukufanya umjue Yeye neno kwa neno, utahisi kwamba haipendezi sana na inachosha mno, na baadhi ya watu hata watahisi kwamba maneno ya Mungu yanaonekana kuwa yanafuata fomyula fulani. Lakini tukichukulia hadithi hizi za Biblia kama mifano ya kuwasaidia watu kujua tabia ya Mungu, basi haitaonekana kuwa ya kuchosha. Unaweza kusema kwamba katika mkondo wa kuonyesha mifano hii, maelezo ya kile kilichokuwa moyoni mwa Mungu wakati huo—hali Yake ya moyo au hisia Zake za moyoni, au fikira na mawazo Yake—vimesimuliwa kwa watu katika lugha za kibinadamu, na lengo la haya yote ni kuwaruhusu kufahamu, kuhisi kwamba kile ambacho Mungu anacho na alicho sio fomula. Si hadithi ya kale, au kitu ambacho watu hawawezi kuona wala kugusa. Ni kitu ambacho kwa kweli kipo ambacho watu wanaweza kuhisi, na kufahamu. Hili ndilo lengo la msingi. Unaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika enzi hii wamebarikiwa. Wanaweza kuzitumia hadithi za Biblia kupata ufahamu mpana zaidi wa kazi za awali za Mungu; wanaweza kuiona tabia Yake kupitia katika kazi ambayo Amefanya. Na wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu kupitia kwa tabia hizi ambazo Ameonyesha, na kuelewa maonyesho halisi ya utakatifu Wake na utunzaji Wake kwa binadamu ili kuweza kufikia maelezo zaidi na maarifa ya kina zaidi kuhusu tabia ya Mungu. Naamini kwamba nyinyi nyote mnaweza kuhisi haya yote!
Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile ambacho Mungu anacho na alicho. Kipengele hiki kilionyeshwa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maonyesho ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na mawazo tofauti kuhusu Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yaani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele cha uungu wa Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika ulimwengu usioonekana, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkuu sana, na kwamba wasingeweza kusongea karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana na kisha Akapotea, na watu walihisi hata kwamba kila moja ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyafahamu. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa na umbali—kilikuwa na umbali kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana kuwa Alikuwa juu angani, na ilionekana kwamba Hakuwepo kabisa. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na fikira za Mungu au mawazo Yake yoyote kusingeweza kufikiwa, na hata ilikuwa nje ya uwezo wao kufikia. Ingawa Mungu alitenda kazi fulani halisi katika Enzi ya Sheria, na Akaweza kutoa pia maneno fulani na kuonyesha tabia fulani mahususi ili kuwaruhusu watu kufahamu na kuona maarifa fulani yaliyo halisi kumhusu, mwishowe bado, maonyesho hayo kuhusu kile ambacho Mungu anacho na alicho yalitoka katika ulimwengu usioonekana, na kile watu walichoelewa, kile walichokijua kilikuwa bado kinahusu kipengele cha uungu kuhusu kile ambacho Mungu anacho na alicho. Mwanadamu asingeweza kupata maana halisi kutoka kwa kile Anacho na Alicho, na ile picha waliyokuwa nayo kuhusu Mungu ilikuwa bado ndani ya mawanda ya “mwili wa kiroho ambao ni vigumu kuukaribia, unaoonekana na kupotea nje ya utambuzi.” Kwa sababu Mungu hakutumia kitu mahususi au taswira katika ulimwengu wa kimwili ili kuonekana kwa watu, bado wasingeweza kumfafanua Yeye kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Katika mioyo na akili za watu, siku zote walitaka kutumia lugha zao wenyewe ili kuweka kiwango kwa ajili ya Mungu, kumfanya Agusike na kumfanya Awe binadamu, kama vile Alikuwa mrefu kiasi gani, Alikuwa mkubwa kiasi gani, Alifanana vipi, Anapenda nini hasa na jinsi utu Wake ulivyo. Kwa kweli, moyoni Mwake Mungu alijua kwamba watu walifikiria hivyo. Alikuwa wazi sana kuhusu mahitaji ya watu, na bila shaka Alijua pia kile Alichofaa kufanya, hivyo basi Alitenda kazi Yake kwa njia tofauti katika Enzi ya Neema. Njia hii mpya ilikuwa ya kiungu na vilevile ya kibinadamu. Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuuona na kuugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile ambacho Anacho na Alicho, kuwa halisi na kupewa picha ya kibinadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Anacho na Alicho viliweza kabisa kuwakilisha utambulisho na hadhi ya Mungu Mwenyewe —kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Adamu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukutana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukuu Wake katikati ya unyenyekevu, pamoja na kupata ufahamu wa awali na ufafanuzi wa awali wa ukweli na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi Anazungumza kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.
Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.
3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
Mat 18:12-14 Mwaonaje? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.
Kifungu hiki ni mfano—je, ni hisia ya aina gani inayotoa kwa watu? Njia ya maelezo katika—mfano—huu uliotumika hapa ni tamathali za lugha katika lugha ya kibinadamu, na kwa hivyo ipo ndani ya upeo wa uelewa wa wanadamu. Kama Mungu angekuwa amesema kitu kinachofanana katika Enzi ya Sheria, watu wangehisi kwamba maneno kama hayo hayakulingana kabisa na utambulisho wa Mungu, lakini Mwana wa Adamu alipoonyesha kifungu hiki katika Enzi ya Neema, kilionekana cha kufariji, chenye uzuri, na kilicho karibu kwa watu. Mungu alipokuwa mwili, Alipoonekana katika umbo la mwanadamu, Alitumia mfano ufaao sana ambao ulitoka kwa ubinadamu Wake mwenyewe, ili kueleza sauti ya moyo Wake. Sauti hii iliwakilisha sauti ya Mungu mwenyewe na kazi Aliyotaka kufanya katika enzi hiyo. Pia iliwakilisha mtazamo ambao Mungu alikuwa nao kwa watu katika Enzi ya Neema. Tukiangalia kutoka kwa mtazamo wa mwelekeo wa Mungu kwa watu, Alimfananisha kila mtu na kondoo. Kama kondoo amepotea, Atafanya kila awezalo ili kumpata. Hii inawakilisha kanuni ya kazi ya Mungu miongoni mwa binadamu wakati huu katika mwili. Mungu aliutumia mfano huu kufafanua uamuzi na mtazamo Wake katika kazi hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa manufaa ya Mungu kuwa mwili: Angeweza kutumia vizuri maarifa ya binadamu na kutumia lugha ya binadamu kuongea na watu, kuonyesha mapenzi Yake. Aliwaelezea au “kuwatafsiria” binadamu lugha Yake ya kina sana, ya kiungu ambayo watu walipata ugumu kuielewa kupitia lugha ya binadamu, kwa njia ya kibinadamu. Hii iliwasaidia watu kuelewa mapenzi Yake na kujua kile Alichotaka kufanya. Aliweza pia kuwa na mazungumzo na watu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kwa kutumia lugha ya kibinadamu, na kuwasiliana na watu kwa njia waliyoelewa. Aliweza pia kuzungumza na kufanya kazi kwa kutumia lugha na maarifa ya kibinadamu ili watu waweze kuhisi wema na ukaribu wa Mungu, ili waweze kuona moyo Wake. Je, mnaona nini katika hili? Je, kuna vizuizi katika maneno na matendo ya Mungu? Jinsi watu wanavyoona ni kwamba, hakuna njia ambayo Mungu angeweza kutumia maarifa ya kibinadamu, lugha, au njia za kuongea ili kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu Mwenyewe alitaka kusema, kazi Aliyotaka kufanya, au kuonyesha mapenzi Yake mwenyewe; huku ni kufikiria ambako si sahihi. Mungu alitumia mfano wa aina hii ili watu waweze kuhisi uhalisi na uaminifu wa Mungu, na kuona mtazamo Wake kwa watu katika kipindi hicho cha wakati. Mfano huu uliwaamsha watu waliokuwa wakiishi chini ya sheria kwa muda mrefu kutoka katika ndoto, na vilevile uliweza kuhamasisha kizazi baada ya kizazi cha watu walioishi katika Enzi ya Neema. Kwa kukisoma kifungu cha mfano huu, watu wanajua uaminifu wa Mungu katika kuwaokoa binadamu na wanaelewa uzito na umuhimu unaotolewa kwa wanadamu katika moyo Wake.
Hebu tuangalie kwa mara nyingine sentensi ya mwisho katika kifungu hiki: “Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee." Je, maneno haya yalikuwa ya Bwana Yesu mwenyewe, au yalikuwa maneno ya Baba Yake aliye mbinguni? Kwa juujuu, inaonekana kuwa ni Bwana Yesu ambaye anazungumza, lakini mapenzi Yake yanawakilisha mapenzi ya Mungu Mwenyewe, na ndiyo maana Akasema: “Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.” Watu kwa wakati huo walimkubali tu Baba aliye mbinguni kama Mungu, na waliamini kwamba mtu huyu waliyemwona mbele ya macho yao alitumwa tu na Yeye, na hangeweza kumwakilisha Baba aliye mbinguni. Ndiyo maana Bwana Yesu alilazimika kuongeza sentensi hii mwishoni mwa mfano huu, ili watu waweze kuhisi kwa kweli mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, na kuhisi uhalisi na usahihi wa kile Alichosema. Hata ingawa jambo hili lilikuwa jepesi kusema, lilikuwa lenye utunzaji mwingi na lilifichua unyenyekevu na uficho wa Bwana Yesu. Bila kujali kama Mungu alikuwa mwili au Alifanya kazi katika ulimwengu wa kiroho, Aliujua moyo wa binadamu kwa njia bora zaidi, na Alielewa kwa njia bora zaidi kile watu walichohitaji, Alijua kile ambacho watu walikuwa na wasiwasi nacho, na kilichowachanganya, na ndiyo maana Aliongeza mstari huu. Mstari huu uliangazia tatizo lililofichika ndani ya mwanadamu: Watu hawakuamini kile ambacho Mwana wa Adamu alisema, hivi ni kusema kwamba, Bwana Yesu alipokuwa akiongea Alilazimika kuongeza: “Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.” Ni katika kauli hii tu ndiyo maneno Yake yangezaa matunda, kuwafanya watu kuamini kuwa yana usahihi na kuboresha kiwango cha kuaminika kwa maneno hayo. Hii inaonyesha kwamba Mungu alipokuwa Mwana wa Adamu wa kawaida, Mungu na mwanadamu walikuwa na uhusiano mgumu sana, na kwamba hali ya Mwana wa Adamu ilikuwa ya kuaibisha mno. Inaonyesha pia namna ambavyo hadhi ya Bwana Yesu ilivyokuwa isiyo na maana miongoni mwa binadamu wakati huo. Aliposema haya, kwa hakika ilikuwa ni kuwaambia watu: Mnaweza kuwa na uhakika kwamba—haya hayawakilishi yale yaliyo moyoni Mwangu mwenyewe, lakini ni mapenzi ya Mungu aliye mioyoni mwenu. Kwa mwanadamu, jambo hili halikuwa la kejeli? Ingawa Mungu kufanya kazi katika mwili kulikuwa na manufaa mengi ambayo Hakuwa nayo katika nafsi Yake, Alilazimika kustahimili mashaka yao na kukataliwa na wao pamoja na kutojali na upumbavu wao. Inaweza kusemwa kwamba mchakato wa kazi ya Mwana wa Adamu ulikuwa mchakato wa kupitia kukataliwa na wanadamu, na kupitia ushindani wao dhidi Yake. Zaidi ya hayo, ulikuwa ni mchakato wa kufanya kazi ili kuendelea kuishinda imani ya mwanadamu na kumshinda mwanadamu kupitia kile ambacho Anacho na Alicho, kupitia kiini Chake Mwenyewe. Haikuwa jambo kubwa sana kwamba Mungu mwenye mwili Alikuwa akipigana vita vikali dhidi ya Shetani; ilikuwa zaidi kwamba Mungu aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida na kuanzisha mapambano pamoja na wale wanaomfuata Yeye, na katika mapambano haya Mwana wa Adamu alikamilisha kazi Yake kwa unyenyekevu Wake, pamoja na kile ambacho Anacho na Alicho, na kwa upendo na hekima Yake. Aliwapata watu Aliowataka, Alipata utambulisho na hadhi Aliyostahili, na “kurudi” katika kiti Chake cha enzi.
Kifuatacho, hebu basi tuangalie vifungu viwili vifuatavyo katika maandiko.
4. Samehe Sabini Mara Saba
Mat 18:21-22 Kisha Petro akamjia, na kusema, Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba? Yesu akasema kwake, sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba.
5. Upendo wa Bwana
Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.
Kati ya vifungu hivi viwili, kimoja kinazungumzia juu ya msamaha na kingine kinazungumzia juu ya upendo. Mada hizi mbili zinaangazia kwa kweli kazi ambayo Bwana Yesu alitaka kutekeleza katika Enzi ya Neema.
Wakati Mungu Alipofanyika mwili, Alileta pamoja Naye hatua ya kazi Yake, ambayo ilikuwa kazi mahususi na tabia Aliyotaka kuonyesha katika enzi hii. Katika kipindi hicho, kila kitu ambacho Mwana wa Adamu alifanya kilikuwa ndani ya kazi ambayo Mungu alitaka kutekeleza katika enzi hii. Asingeweza kufanya zaidi au kufanya kidogo zaidi. Kila kitu Alichosema na kila aina ya kazi Aliyotekeleza vyote vilihusiana na enzi hii. Haijalishi kama Alionyesha kwa njia ya kibinadamu Akitumia lugha ya kibinadamu au kupitia kwa lugha ya kiungu—haijalishi ni njia gani, au kutoka kwa mtazamo gani—lengo Lake lilikuwa ni kuwasaidia watu kuelewa kile Alichotaka kufanya, mapenzi Yake yalikuwa nini, na mahitaji Yake yalikuwa yapi kutoka kwa watu. Anaweza kutumia mbinu mbalimbali kutoka mitazamo mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa na kujua mapenzi Yake, kuelewa kazi Yake ya kuwaokoa binadamu. Hivyo basi katika Enzi ya Neema tunamwona Bwana Yesu akitumia lugha ya kibinadamu wakati mwingi kuonyesha kile Alichotaka kuwasilisha kwa mwanadamu. Hata zaidi, tunamwona Yeye kutoka katika mtazamo wa uongozaji wa kawaida Akizungumza na watu, Akiwapa mahitaji yao, na Akiwasaidia na kile walichoomba. Njia hii ya kufanya kazi haikuonekana katika Enzi ya Sheria iliyokuja kabla ya Enzi ya Neema. Alikuwa karibu zaidi na mwenye huruma zaidi kwa binadamu, pamoja na kuweza kutimiza zaidi matokeo ya kivitendo katika umbo Lake na tabia Yake. Mfano wa kusamehe watu sabini mara saba unafafanua zaidi hoja hii. Kusudi lililotimizwa kupitia kwa nambari katika mfano huu ni ili kuwaruhusu watu kuelewa nia ya Bwana Yesu wakati huo aliposema hayo. Nia Yake ilikuwa kwamba watu wanafaa kuwasamehe wengine—si mara moja wala mara mbili na wala si hata mara saba, lakini sabini mara saba. Hili wazo la “sabini mara saba” ni la aina gani? Ni la kuwafanya watu kufanya msamaha kuwa wajibu wao wenyewe, kitu ambacho lazima wajifunze, na “njia” ambayo kwayo ni lazima waifuate. Hata ingawa huu ulikuwa ni mfano tu, lakini ulitumika kuwaangazia watu jambo muhimu. Uliwasaidia watu kufahamu kwa kina kile Alichokimaanisha na kupata njia bora za kufanyia mazoezi na kanuni na viwango vya utendaji. Mfano huu uliwasaidia watu kuelewa kwa uwazi na kuwapa maana sahihi-kwamba wanapaswa kujifunza kusamehe na wasamehe mara zote bila ya masharti na bila ya upungufu wowote, lakini kwa mtazamo wa uvumilivu na uelewa kwa wengine. Bwana Yesu aliposema haya, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Je, Alikuwa akifikiria kwa kweli kuhusu hesabu ya sabini mara saba? Hapana, Hakuwa akifikiria kuhusu hilo. Je, kuna hesabu ya mara kadhaa ambazo Mungu atawasamehe wanadamu? Kuna watu wengi walio na shauku katika “hesabu ya nambari” iliyotajwa, wanaotaka kwa kweli kuelewa asili na maana ya nambari hii. Wanataka kuelewa kwa nini nambari hii ilitoka kinywani mwa Bwana Yesu; wanaamini kwamba kuna maana ya ndani zaidi katika nambari hii. Kwa hakika, huu ulikuwa ni usemi tu wa Mungu katika ubinadamu. Tafsiri au maana yoyote lazima ichukuliwe pamoja na mahitaji ya Bwana Yesu kwa mwanadamu. Wakati Mungu alikuwa bado Hajafanyika mwili, watu hawakuelewa mengi kuhusu kile Alichosema, kwa sababu matamshi Yake yalitoka katika uungu kamili. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambao watu wasingeweza kuuona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, na Alitoka na kuvuka upeo wa ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya kiungu, mapenzi, na mtazamo wake kupitia mambo ambayo wanadamu wangeweza kuyafikiria, vitu ambavyo wangeweza kuviona na kukutana navyo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kuzikubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kufahamu, ili kuwaruhusu wanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Zake na viwango vyake vinavyohitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao, na kwa kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu katika ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa njia ya, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisi zaidi, na kwa utendaji ulipita ule wa Enzi ya Sheria.
Kisha, hebu tuzungumze kuhusu kumpenda Bwana na kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Je, hili ni jambo linaloelezewa moja kwa moja kupitia uungu? Bila shaka, sivyo! Haya yalikuwa mambo yote ambayo Mwana wa Adamu alizungumza katika ubinadamu; watu tu ndio wangeweza kusema kauli kama “Mpende jirani yako kama nafsi yako,” na “Wapende wengine kama vile unavyothamini maisha yako mwenyewe,” ni watu pekee ndio wangeweza kuongea kwa njia hii. Mungu hajawahi kuongea kwa njia kama hiyo. Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu hana aina hii ya lugha katika uungu Wake kwa sababu Hahitaji aina hii ya kanuni, “Mpende jirani yako kama nafsi yako” ili kudhibiti upendo Wake kwa mwanadamu, kwa sababu upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni ufunuo wa kiasili wa kile ambacho Anacho na Alicho. Je, ni lini mmewahi kusikia kwamba Mungu alisema kitu kama “Nampenda binadamu kama Ninavyojipenda”? Kwa sababu upendo umo katika kiini cha Mungu, na ndani ya kile Anacho na Alicho. Upendo wa Mungu kwa binadamu na jinsi Anavyowatendea watu na mtazamo Wake ni maonyesho ya kiasili na ufichuzi wa tabia Yake. Hahitaji kufanya hili kwa njia fulani ya uangalifu, au kufuata mbinu fulani au mfumo wa maadili kwa uangalifu ili kutimiza kumpenda jirani Yake kama Anavyojipenda—tayari Anamiliki aina hii ya kiini. Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Aacho na Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu ili waweze kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Anacho na Alicho, ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe. Hivyo ni kusema kwamba, Mwana wa Adamu katika mwili Alionyesha tabia ya asili na kiini cha Mungu Mwenyewe kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana na kwa usahihi zaidi unaowezekana. Sio tu kwamba ubinadamu wa Mwana wa Adamu haukuwa na kikwazo au kizuizi kwa mawasiliano na mwingiliano kati ya mwanadamu na Mungu mbinguni, lakini pia kwa kweli ilikuwa ndio njia pekee na daraja pekee la wanadamu kuunganishwa na Bwana wa uumbaji. Kwa wakati huu, je, hamhisi kwamba kuna mifanano mingi kati ya asili na mbinu za kazi zilizofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na awamu ya sasa ya kazi? Hatua ya sasa ya kazi inatumia pia lugha nyingi za kibinadamu kuelezea tabia ya Mungu, na inatumia lugha na mbinu nyingi kutoka katika maisha ya kila siku ya binadamu na maarifa ya kibinadamu ili kuonyesha mapenzi ya Mungu Mwenyewe. Mara tu Mungu anapofanyika mwili, haijalishi kama Anaongea kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu au mtazamo wa kiungu, lugha Zake nyingi na mbinu Zake za maonyesho yote ni kupitia katika njia ya lugha na mbinu za kibinadamu. Yaani, wakati Mungu anapokuwa mwili, hii ndiyo fursa nzuri zaidi kwako kuweza kuona nguvu za Mungu na hekima Yake, na kujua kila kipengele halisi cha Mungu. Mungu Alipopata mwili, wakati Alipokuwa Anakua, Alikuja kuelewa, kujifunza, na kufahamu sehemu ya maarifa ya wanadamu, akili ya kawaida, lugha, na mbinu za kujieleza katika ubinadamu. Mungu mwenye mwili Alimiliki vitu hivi ambavyo vilitoka kwa wanadamu Aliokuwa amewaumba. Waligeuka na kuwa zana za Mungu katika mwili za kueleza tabia Yake na uungu Wake, na wakamruhusu kuifanya kazi Yake ya kufaa zaidi, halisi zaidi, na sahihi zaidi Alipokuwa akifanya kazi katikati ya wanadamu, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu na kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Hii iliwezesha kazi Yake kufikiwa zaidi na kueleweka kwa urahisi zaidi na watu, hivyo basi kutimiza matokeo ya kile Mungu Alichotaka. Je, hii si ya kivitendo zaidi kwa Mungu kufanya kazi katika mwili kwa njia hii? Je, hii sio hekima ya Mungu? Wakati Mungu alipofanyika mwili, wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi Aliyotaka kutekeleza, ndipo Angeonyesha tabia Yake na kazi Yake kwa utendaji, na huu ndio wakati pia ambao Angeanza rasmi huduma Yake kama Mwana wa Adamu. Hii ilimaanisha kwamba hakungekuwepo tena na "umbali" kati ya Mungu na wanadamu, kwamba Mungu Angekomesha hivi karibuni kazi Yake ya kuwasiliana kupitia wajumbe, na kwamba Mungu Mwenyewe angeweza kuonyesha kibinafsi maneno na kazi zote Alizotaka katika mwili. Ilimaanisha pia kwamba watu ambao Mungu anawaokoa walikuwa karibu Naye, na kwamba kazi Yake ya usimamizi ilikuwa imeingia katika hatua mpya, na kwamba wanadamu wote walikuwa karibu kukabiliwa na enzi mpya.
Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi kati ya matukio hayo lilikuwa ni Yeye kuwindwa na mfalme wa mashetani, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka chini ya miwili katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi. Wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi miongoni mwa wanadamu, je, Alihisi vipi? Watu wanapaswa kuelewa hilo kwa kiwango fulani, sivyo? Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu alifurahia kwa sababu Angeanza kuendeleza kazi Yake mpya miongoni mwa wanadamu. Bwana Yesu alipobatizwa na kuanza rasmi kazi Yake ya kutimiza huduma Yake, moyo wa Mungu ulijawa na furaha kwa sababu baada ya miaka mingi sana ya kusubiri na matayarisho, hatimaye Angeweza kuuvaa mwili wa binadamu wa kawaida na kuanza kazi Yake mpya katika umbo la binadamu aliye na mwili na damu ambao watu wangeweza kuuona na kuugusa. Angeweza kuzungumza ana kwa ana na moyo kwa moyo na watu kupitia utambulisho wa mwanadamu. Mungu hatimaye angeweza kuwa ana kwa ana na mwanadamu katika lugha ya kibinadamu, kwa njia ya kibinadamu; Angeweza kumruzuku mwanadamu, kumwelimisha binadamu, na kumsaidia binadamu kwa kutumia lugha ya kibinadamu; angeweza kula kwenye meza moja na kuishi katika nafasi sawa na binadamu. Angeweza pia kuwaona binadamu, kuona vitu, na kuona kila kitu kwa jinsi ambavyo wanadamu waliviona na hata kupitia kwa macho yao wenyewe. Kwake Mungu, huu ulikuwa tayari ushindi Wake wa kwanza wa kazi Yake katika mwili. Inaweza pia kusemwa kwamba ilikuwa ni ufanikishaji wa kazi kubwa—hili bila shaka ndilo ambalo Mungu alilifurahia zaidi. Kuanzia hapo, Mungu alihisi kwa mara ya kwanza, aina ya faraja katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Matukio haya yote yalikuwa ya kivitendo sana na ya asili sana, na faraja ambayo Mungu alihisi ilikuwa ya kweli sana. Kwa mwanadamu, kila mara hatua mpya ya kazi ya Mungu inapokamilishwa, na kila mara Mungu anapohisi kuridhika, ndipo mwanadamu anapoweza kusogea karibu zaidi na Mungu, na ndipo watu wanapoweza kusogea karibu zaidi na wokovu. Kwa Mungu, huu pia ni uzinduzi wa kazi Yake mpya, wakati mpango Wake wa usimamizi unapoendelea hatua moja zaidi, na, vilevile, wakati mapenzi Yake yanapokaribia mafanikio kamili. Kwa mwanadamu, kuwasili kwa fursa kama hiyo ni bahati, na ni bora zaidi; kwa wale wote wanaosubiria wokovu wa Mungu, ni habari muhimu na zenye furaha. Mungu anapotekeleza hatua mpya ya kazi, basi Anao mwanzo mpya na wakati ambapo kazi hii mpya na mwanzo mpya vinazinduliwa na kufahamishwa miongoni mwa binadamu, ni wakati ambao matokeo ya hatua hii ya kazi tayari yameamuliwa, na kufanikishwa, naye Mungu tayari ameona matokeo na matunda yake ya mwisho. Huu pia ndio wakati ambapo athari hizi zinamfanya Mungu aridhike, na moyo Wake, bila shaka una furaha. Kwa sababu katika macho ya Mungu, tayari ameona na kuamua watu anaowatafuta, na tayari Amelipata kundi hili, kundi ambalo linaweza kufanya kazi Yake kufanikiwa na kumfanya Aridhike, Mungu anajihisi Akiwa ameondolewa mashaka, Anaweka pembeni wasiwasi Wake, na Anajihisi mwenye furaha. Kwa maneno mengine, wakati mwili wa Mungu unaweza kuanza kazi mpya miongoni mwa binadamu, na Anaanza kufanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kizuizi, na wakati Anapohisi kwamba yote yametimizwa, basi Kwake, tayari mwisho umeonekana. Na kwa sababu ya mwisho huu Anatosheka, na kuwa mwenye moyo wa furaha. Furaha ya Mungu inaonyeshwa vipi? Je, unaweza kufikiria jawabu litakuwa lipi? Je, Mungu anaweza kulia? Mungu Anaweza kutoa machozi? Je, Mungu anaweza kupiga makofi? Je, Mungu anaweza kucheza? Je, Mungu anaweza kuimba? Ikiwa ndivyo, je, wimbo huo ungekua ni upi? Bila shaka Mungu Angeweza kuimba wimbo mzuri, wa kusisimua, wimbo ambao unaweza kuonyesha shangwe na furaha katika moyo Wake. Angeweza kuwaimbia binadamu, kujiimbia Mwenyewe, na kuuimba kwa vitu vyote. Furaha ya Mungu inaweza kuonyeshwa kwa njia yoyote—yote haya ni ya kawaida kwa sababu Mungu ana furaha na huzuni, na hisia Zake mbalimbali zinaweza kuonyeshwa kwa njia mbalimbali. Hii ndiyo haki Yake na hakuna kitu kingekuwa cha kawaida zaidi na sahihi. Watu hawapaswi kufikiria kitu chochote kingine kuhusu hili. Hupaswi kujaribu kutumia “laana ya kukazwa na mshipi”[a] kwa Mungu, ukimwambia kwamba Yeye hafai kufanya hiki au kile, Hafai kutenda kwa njia hii au ile, kuwekea mipaka furaha Yake au hisia yoyote ile Aliyo nayo. Katika mioyo ya watu Mungu hawezi kuwa na furaha, Hawezi kutokwa na machozi, Hawezi kulia—Hawezi kuonyesha hisia zozote. Kupitia kwa yale tuliyoshiriki mara hizi mbili, Naamini hamtamwona tena Mungu kwa njia hii, lakini mtamruhusu Mungu kuwa na uhuru Fulani na kuachiliwa. Hiki ni kitu kizuri. Katika siku za usoni kama mtaweza kuhisi kwa kweli huzuni ya Mungu mnaposikia kwamba Yeye ana huzuni, na mnaweza kuhisi kwa kweli furaha Yake mnaposikia kuhusu Yeye kuwa na furaha—angalau, mnaweza kujua na kuelewa waziwazi kile kinachomfanya Mungu kuwa na furaha na kile kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni—unapoweza kuhisi huzuni kwa sababu Mungu ana huzuni na kuhisi furaha kwa sababu Mungu ana furaha, Atakuwa ameupata moyo wako na hakutakuwa tena na kizuizi chochotekati yako na Yeye. Hamtajaribu tena kumzuilia Mungu kwa mawazo, dhana, na maarifa ya kibinadamu. Wakati huo, Mungu atakuwa hai na dhahiri moyoni mwako. Atakuwa Mungu wa maisha yako na Bwana wa kila kitu chako. Je, mnalo tamanio kama hili? Je, mnayo imani kuwa mnaweza kutimiza haya?
Kisha, hebu tusome vifungu vifuatavyo.
6. Mahubiri ya Mlimani
Sifa na Heri (Mat 5:3-12)
Chumvi na Nuru (Mat 5:13-16)
Sheria (Mat 5:17-20)
Kuhusu Hasira (Mat 5:21-26)
Kuhusu Uzinzi (Mat 5:27-30)
Kuhusu Talaka (Mat 5:31-32)
Kuhusu Viapo (Mat 5:33-37)
Kuhusu Kulipiza Kisasi (Mat 5:38-42)
Upendo kwa Adui (Mat 5:43-48)
Kuhusu Utoaji Sadaka (Mat 6:1-4)
Kuhusu Maombi (Mat 6:5-8)
7. Mifano ya Bwana Yesu
Mfano wa Mpanzi (Mat 13:1-9)
Mfano wa Magugu katikati ya Ngano (Mat 13:24-30)
Mfano wa Punje ya Haradali (Mat 13:31-32)
Mfano wa Chachu (Mat 13:33)
Mfano wa Magugu Umeelezwa (Mat 13:36-43)
Mfano wa Hazina (Mat 13:44)
Mfano wa Lulu (Mat 13:45-46)
Mfano wa Wavu (Mat 13:47-50)
8. Amri
Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.
Hebu kwanza tuangalie katika kila kipengele cha “Mahubiri ya Mlimani.” Je, haya yote yanahusiana na nini? Inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba, haya yote ni ya juu zaidi, ni halisi zaidi, na yana ukaribu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.
Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Je, unapaswa kuelewa vipi kuhusu sifa na heri? Je, ni nini unapaswa kujua kuhusu sheria? Je! hasira inapaswa kufafanuliwaje? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Je, talaka inapaswa kuzungumziwa vipi, na je, kuna sheria za aina gani kuhusu talaka na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, vipi kuhusu viapo, kulipiza kisasi, kuwapenda maadui zako, na, maagizo kuhusu sadaka? Na kadhalika Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na kumfuata kwao Mungu. Baadhi ya vitendo hivi bado vinatumika leo, ingawa ni vya kiwango cha chini sana kuliko yale yanayohitajika kwa watu wa wakati huu—ni kweli za kimsingi ambazo watu hukutana nazo katika imani yao kwa Mungu. Tangu wakati ambao Bwana Yesu Alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari Ameanza kufanya kazi juu ya tabia ya maisha ya wanadamu, lakini vipengele hivi vya kazi Yake vilijengwa juu ya msingi wa sheria. Je, kanuni na mbinu za kuzungumza kuhusu mada hizi zilihusiana kwa vyovyote vile na ukweli? Bila shaka vilihusiana! Taratibu, na kanuni zote za awali, pamoja na mahubiri yote katika Enzi ya Neema, yalihusiana na tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, na bila shaka vilihusiana na ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, na haijalishi ni kwa njia gani Anakionyesha, au lugha Anayotumia, mambo ambayo Anayaonyesha yote yana msingi, asili, na mwanzo wake katika kanuni za tabia Yake na kile ambacho Anacho na Alicho. Hili halina shaka. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu kwa sasa, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Je, unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika mahubiri hayo hayaambatani na ukweli? La, huwezi kusema hivyo! Kila moja ya mambo hayo ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa wanadamu; yote yalikuwa ni kanuni na viwango vilivyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kutenda, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha kwa wakati huo, haya ndiyo mambo pekee ambayo waliweza kuyakubali na kuyaelewa. Kwa sababu dhambi za wanadamu zilikuwa bado hazijatatuliwa, haya ndiyo maneno pekee ambayo Bwana Yesu angeweza kuyatoa, na Angeweza tu kutumia mafundisho marahisi yaliyomo ndani ya upeo huu ili kuwaambia watu wa wakati huo jinsi wanavyopaswa kutenda, kile walichopaswa kufanya, ndani ya kanuni na upeo gani wanapaswa kufanya mambo, na jinsi wanavyopaswa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha wanadamu wa wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi chini ya sheria kukubali mafundisho haya, kwa hivyo kile ambacho Bwana Yesu alifundisha kilipaswa kubakia ndani ya upeo huu.
Kisha, hebu tuangalie ni nini kilicho katika “Mifano ya Bwana Yesu.”
Mfano wa kwanza ni mfano wa mpanzi. Huu ni mfano wa kuvutia sana; kupanda mbegu ni tukio la kawaida sana katika maisha ya watu. Mfano wa pili ni mfano wa magugu. Kulingana na jinsi magugu yalivyo, mtu yeyote ambaye amewahi kupanda mazao, na kwa hakika watu wazima wote, wanajua "magugu" ni nini. Wa tatu ni mfano wa punje ya haradali. Nyinyi nyote mnajua haradali ni nini, sivyo? Kama hujui, unaweza kuangalia katika Biblia. Nao mfano wa nne ni mfano wa chachu, watu wengi wanajua kwamba chachu inatumiwa katika kutia chachu; ni kitu ambacho watu wanatumia katika maisha yao ya kila siku. Mifano yote iliyotajwa hapa chini ukiwemo mfano wa sita, mfano wa hazina, mfano wa saba, mfano wa lulu, na wa nane mfano wa wavu; ni mifano iliyotolewa katika maisha ya watu; inatoka katika maisha halisi ya watu. Je, mifano hii inatoa picha ya aina gani? Hii ni taswira ya Mungu akigeuka kuwa mtu wa kawaida na kuishi pamoja na mwanadamu, Akitumia lugha ya kawaida yamaisha, Akitumia lugha ya mwanadamu ili kuwasiliana na binadamu na kuwapa kile wanachohitaji. Wakati Mungu alikuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa muda mrefu, baada ya kupitia na kushuhudia mitindo mbalimbali ya maisha ya watu, uzoefu huo ukawa nyenzo Yake ya kufundishia ambayo kwayo Alibadilisha lugha Yake ya kiungu kuwa lugha ya kibinadamu. Bila shaka, mambo haya Aliyoyaona na kuyasikia katika maisha yaliweza pia kuboresha uzoefu wa kibinadamu wa Mwana wa Adamu. Alipowataka watu waelewe ukweli fulani, ili kuwaelewesha mapenzi fulani ya Mungu, Angetumia mifano inayofanana na ile iliyotajwa hapo juu ili kuwaeleza watu kuhusu mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa binadamu. Mifano hii yote ilihusiana na maisha ya watu; hakukuwa na hata mmoja ambao haukuwa na uhusiano maisha ya binadamu. Bwana Yesu alipoishi na binadamu, Aliwaona wakulima wakilima mashamba yao; Alijua magugu yalikuwa ni nini na kutia chachu kulikuwa ni nini; Alielewa kwamba binadamu wanapenda hazina na hivyo basi Alitumia mfano wa hazina na hata lulu. katika maisha mara kwa mara Aliwaona wavuvi wakizirusha nyavu zao; Bwana Yesu aliliona hili na shughuli nyingine zinazohusiana na maisha ya wanadamu, na Yeye pia alipitia aina hiyo ya maisha. Kama tu binadamu mwingine wa kawaida, Alipitia taratibu za kila siku za binadamu na kula kwao milo mitatu kwa siku. Yeye binafsi alipitia maisha ya mtu wa kawaida, na Aliona maisha ya wengine. Aliposhuhudia na kupitia haya yote binafsi, kile Alichofikiria kilikuwa si namna ya kuwa na maisha mazuri au namna ambavyo Angeishi kwa uhuru zaidi au kwa raha zaidi. Badala yake, kutokana na uzoefu Wake wa maisha halisi ya binadamu, Bwana Yesu aliuona ugumu katika maisha ya watu, Aliuona ugumu, unyonge, na huzuni ya watu waliopotoshwa na Shetani, wakiishi katika utawala wa Shetani na walioishi katika dhambi. Wakati Akiyapitia maisha ya binadamu, Yeye binafsi aliweza pia kushuhudia namna ambavyo watu waliokuwa wakiishi ndani ya upotovu walivyokuwa wasioweza kujisaidia, na Akawaona kupitia ile hali duni ya wale walioishi katika dhambi, wale waliopotea katika mateso ya Shetani, ya mwovu. Bwana Yesu alipoyaona mambo haya, je,Aliyaona kwa uungu Wake au kwa ubinadamu Wake? Ubinadamu Wake ulikuwepo kwa kweli—ulikuwepo waziwazi—Angeweza kuyapitia na kuyaona haya yote na bila shaka Aliyaona katika kiini Chake halisi, katika uungu Wake. Yaani, Kristo Mwenyewe, Bwana Yesu ambaye Alikuwa mwanadamu Aliyaona haya na kila kitu Alichokiona kilimfanya kuhisi umuhimu na haja ya kazi Aliyokuwa Ameamua kuifanya wakati huu akiwa mwili. Hata ingawa Yeye Mwenyewe Alijua kwamba jukumu Alilohitaji kushughulikia Akiwa katika mwili lilikuwa kubwa mno, na namna ambavyo Angepitia maumivu ya kikatili, Alipomwona mwanadamu asiyejiweza ndani ya dhambi, Alipoona unyonge wa maisha yao na mapambano hafifu chini ya sheria, Alihuzunika zaidi na zaidi, na Akawa na hamu kubwa zaidi na zaidi ya kumwokoa binadamu kutoka dhambini. Haijalishi ni ugumu wa aina gani ambao Angepitia au ni aina gani ya maumivu Angehisi, Alizidi kuazimia zaidi na zaidi kuwakomboa wanadamu, ambao walikuwa wakiishi katika dhambi. Wakati wa mchakato huu, unaweza kusema kwamba Bwana Yesu alianza kuelewa waziwazi kazi Aliyohitajika kufanya na kile Alichokuwa Ameaminiwa kutekeleza. Alikuwa pia mwenye hamu kubwa zaidi ya kukamilisha kazi ambayo Alikuwa Aichukue—kuchukua dhambi zote za wanadamu, kuwafidia wanadamu ili wasiishi tena katika dhambi naye Mungu Angeweza kusahau dhambi za binadamu kwa sababu ya sadaka ya dhambi, na hivyo basi kumruhusu kuendeleza kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu. Yaweza kusemwa kwamba katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya wanadamu, kujitoa Mwenyewe. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani, na Alikuwa na hamu ya kukamilisha kazi hii. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja. Alipokuwa na hisia hii ya dharura, Alikuwa hafikirii namna ambavyo maumivu Yake mwenyewe yangekuwa makubwa, wala Hakuwa akifikiria zaidi kuhusu ni kiwango kipi cha udhalilishaji ambacho Angevumilia—Alishikilia azimio moja tu moyoni Mwake: Maadamu tu Angejitoa Mwenyewe, maadamu tu Angesulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi, mapenzi ya Mungu yangetendeka na Angeweza kuanza kazi mpya. Maisha ya wanadamu katika dhambi, hali yao ya kuwepo katika dhambi ingebadilika kabisa. Imani yake na kile Alichoamua kufanya vyote vilihusiana na kumwokoa binadamu, na Alikuwa na lengo moja tu: kufanya mapenzi ya Mungu ili Aweze kuanza kwa ufanisi hatua ambayo ingefuata katika kazi Yake. Haya ndiyo yaliyokuwa katika mawazo ya Bwana Yesu wakati huo.
Akiishi katika mwili, Mungu mwenye mwili Alikuwa na ubinadamu wa kawaida; Alikuwa na hisia na kule kuwaza kwa mtu wa kawaida. Alijua furaha ilikuwa ni nini, maumivu yalikuwa ni nini na Alipowaona wanadamu katika hali hii ya maisha, Alihisi kwa kina kwamba kuwapatia watu mafundisho Fulani tu, kuwapatia kitu au kuwafunza kitu kusingewaongoza kutoka katika dhambi. Wala kuwafanya kutii amri pia kusingewakomboa kutoka katika dhambi—ni pale tu Alipozichukua dhambi za binadamu na kuwa mfano wa mwili wenye dhambi ndipo Alipoweza kuubadilisha kwa ajili ya uhuru wa mwanadamu, na kuubadilisha kwa ajili ya msamaha wa Mungu kwa wanadamu. Kwa hivyo baada ya Bwana Yesu kupitia na kushuhudia maisha ya binadamu katika dhambi, kulikuwa na tamanio kuu lililojionyesha katika moyo Wake—kuwaruhusu wanadamu kujiweka huru kutoka katika maisha yao ya kupambana na dhambi. Tamanio hili lilimfanya kuhisi zaidi na zaidi kwamba lazima Aende msalabani na kuzichukua dhambi za binadamu haraka iwezekanavyo, kwa dharura. Hizi ndizo zilizokuwa fikira za Bwana Yesu kwa wakati huo, baada ya Yeye kuishi na watu na kuwaona, kuwasikia, na kuhisi taabu ya maisha yao ndani ya dhambi. Kwamba Mungu mwenye mwili Angekuwa na nia ya aina hii kwa wanadamu, kwamba Angeweza kueleza na kufichua tabia ya aina hii—je, hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida angekuwa nalo? Je, mtu wa kawaida angeona nini akiishi katika mazingira ya aina hii? Je, angefikiria nini? Kama mtu wa kawaida angekumbwa na haya yote, je, angeweza kutazama matatizo haya kwa mtazamo wa juu? Bila shaka hapana! Ingawa mwonekano wa nje wa Mungu mwenye mwili ni sawa kabisa na wa mwanadamu, na ingawa Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuzungumza lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine hata kueleza mawazo Yake kupitia mbinu au njia za kuzungumza za wanadamu, walakini, jinsi Anavyowaona wanadamu, na kuona kiini cha mambo, si sawa kabisa na jinsi watu wapotovu wanavyowaona wanadamu na kiini cha mambo. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni utoaji wa ukweli na uzima. Utolewaji huu sio kwa ajili ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadhaa ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake mwenyewe, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; lakini je, mawazo ya mtu mwenye huruma kama hayo yanaweza kwenda zaidi ya hapo? La hasha! Kwa sababu wanadamu, hata hivyo, ni wanadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha nafasi Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na mawazo ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa kibinadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za kibinadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya upeo wa kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Anacho na Alicho kama kipimo. Upeo huu unajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuyaona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu naMungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo. Je, unaona udhihirisho na ufunuo wa Mungu Mwenyewe ndani ya Bwana Yesu? Unaweza kusema kwamba kile ambacho Bwana Yesu alifanya na kusema kilihusiana na huduma Yake na kazi ya usimamizi ya Mungu binafsi, kwamba yote hayo yalikuwa ni udhihirisho na ufunuo wa kiini cha Mungu. Ingawa Alikuwa na udhihirisho wa kibinadamu, kiini Chake cha kiungu na ufichuzi Wake wa kiungu hauwezi kukataliwa. Je, udhihirisho huu wa kibinadamu ulikuwa udhihirisho wa kweli wa ubinadamu? Udhihirisho Wake wa ubinadamu ulikuwa, kwa kiini chake, tofauti kabisa na udhihirishaji wa ubinadamu wa watu waliopotoka. Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, na kama Angekuwa kweli mmojawapo wa wale wa kawaida, watu waliopotoka, je, Angeweza kuyaona maisha ya wanadamu ndani ya dhambi kutoka katika mtazamo wa kiungu? La hasha! Hii ndiyo tofauti kati ya Mwana wa Adamu na watu wa kawaida. Watu wote waliopotoka wanaishi ndani ya dhambi na wakati mtu yeyote anaiona dhambi, hana hisia zozote kuihusu hiyo dhambi; wako sawa tu, kama vile nguruwe anayeishi kwenye matope ambaye hahisi kero yoyote au uchafu-kinyume chake, anakula vizuri na kulala vizuri. Kama mtu anasafisha nyumba ya nguruwe, nguruwe kwa hakika hatahisi utulivu, na hatabakia akiwa msafi. Baada ya muda mfupi tu atakuwa tena akijigaragaza kwenye matope, akiwa amestarehe kabisa, kwa sababu yeye ni kiumbe mchafu. Wakati binadamu wanapomwona nguruwe wanahisi kwamba anao uchafu na ukimsafisha yule nguruwe hahisi vyema zaidi—ndio maana hakuna anayemfuga nguruwe ndani ya nyumba yake. Jinsi wanadamu wanavyowaona nguruwe itakuwa tofauti siku zote na namna ambavyo nguruwe wenyewe wanavyojihisi, kwa sababu wanadamu na nguruwe si wa aina moja. Na kwa sababu Mwana wa Adamu mwenye mwili si wa aina moja na wanadamu waliopotoka, Mungu mwenye mwili tu ndiye Anayeweza kusimama kutoka kwa mtazamo wa kiungu, na kusimama kutoka katika nafasi ya Mungu ili kuwaona wanadamu, ili kuona kila kitu.
Mungu anapokuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu, ni mateso yapi Anayopitia katika mwili? Je, kuna yeyote anayeelewa kwa kweli? Baadhi ya watu husema kwamba Mungu anateseka sana, na ingawa Yeye ni Mungu Mwenyewe, watu hawaelewi kiini Chake na siku zote wanamchukulia Yeye kama mtu, hali ambayo humfanya Yeye kuhisi huzuni na kuona kwamba Amekosewa—wanasema kwamba, kwa sababu hizi, mateso ya Mungu kwa kweli ni makubwa. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu hana hatia na hana dhambi, lakini Yeye huteseka sawa na wanavyoteseka wanadamu, na Yeye hupitia mateso, matusi, na kuvunjiwa heshima pamoja na wanadamu; wanasema Yeye pia huvumilia kutoelewana na kutotiiwa na wafuasi Wake—kuteseka kwa Mungu kwa kweli hakuwezi kupimwa. Yamkini humwelewi Mungu kwa kweli. Kwa hakika, mateso haya unayoyaongelea hayaonekani kuwa mateso ya kweli kwake Mungu, kwa sababu kunayo mateso makubwa zaidi ya haya. Basi mateso ya kweli kwa Mungu Mwenyewe ni yapi? Mateso ya kweli ya mwili wa Mungu ni yapi? Kwa Mungu, wanadamu kutomwelewa Yeye haihesabiki kuwa ni mateso, na vile vile watu wasio na ufahamu fulani wa Mungu na kwa kutomwona Yeye kama Mungu hakuhesabiki kuwa mateso. Hata hivyo, mara nyingi watu huhisi kwamba Mungu lazima alipitia dhuluma kubwa sana, kwamba wakati Mungu yumo katika mwili Hawezi kuionyesha nafsi Yake kwa wanadamu na kuwaruhusu kuuona ukuu Wake, na Mungu anajificha kwa unyenyekevu katika mwili duni na hivyo basi hali hii lazima ilikuwa ya kumpa Yeye maumivu makali. Watu hushikilia moyoni kile wanachoweza kuelewa na kile wanachoweza kuona kuhusu mateso ya Mungu, na kuweka kila aina ya huruma kwa Mungu na mara nyingi hata wataisifia kidogo hali hiyo. Katika hali halisi, kuna utofauti; kuna mgongano kati ya kile ambacho watu wanaelewa kuhusu mateso ya Mungu na kile Anachohisi kwa kweli. Nakwambia ukweli—kwa Mungu haijalishi kama ni Roho wa Mungu au mwili wa Mungu, mateso yaliyoelezwa hapo juu si mateso ya kweli. Basi ni nini hasa ambacho kwa kweli Mungu huteseka? Hebu tuzungumze kuhusu mateso ya Mungu kutoka katika mtazamo wa Mungu mwenye mwili pekee.
Wakati Mungu anapokuwa mwili, Akigeuka kuwa mtu wa kawaida, na wa kawaida kabisa Akiishi miongoni mwa wanadamu, miongoni mwa watu, je, Hawezi kuona na kuhisi mbinu za watu, sheria na falsafa zao za kuishi? Ni vipi ambavyo mbinu na sheria hizi zinamfanya Yeye kuhisi? Je, Anahisi kuwa na chuki katika moyo Wake? Kwa nini Ahisi chuki? Je, mbinu na sheria za wanadamu za kuishi ni zipi? Je, zimekita mizizi katika kanuni gani? Je, ziko katika msingi upi? Mbinu, sheria, na kadhalika, zinazohusiana na njia za kuishi kwa wanadamu—zote hizi zimeundwa kwa misingi ya mantiki, maarifa na falsafa za Shetani. Wanadamu wanaoishi chini ya aina hizi za sheria hawana ubinadamu, hawana ukweli—wote wanapinga ukweli nan i maadui wa Mungu. Tunapoangalia kiini cha Mungu, tunaona kwamba kiini Chake ni kinyume kabisa na mantiki, maarifa na falsafa za Shetani. Kiini Chake kimejaa haki, ukweli, na utakatifu na uhalisi wa mambo yote chanya. Mungu, akimiliki kiini hiki na Akiishi miongoni mwa wanadamu—Je, anahisi vipi katika moyo Wake? Je, haujajaa maumivu? Moyo Wake umo katika maumivu, na maumivu haya ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kuelewa wala kutambua. Kwa sababu kila kitu Anachokumbana nacho, kukabiliana nacho, kusikia, kuona na kupitia vyote ni upotovu wa wanadamu, uovu, na uasi wao dhidi ya, na upinzani wa ukweli. Kila kitu kinachotoka kwa wanadamu ndicho chanzo cha mateso Yake. Hivi ni kusema kwa sababu kiini Chake halisi si sawa na wanadamu waliopotoka, kupotoka kwa wanadamu kunakuwa ndiko chanzo cha mateso Yake makuu. Wakati Mungu anapokuwa mwili, Je, anaweza kupata mtu anayetumia lugha moja na Yeye? Hili haliwezi kupatikana miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayeweza kupatikana anayeweza kuwasiliana, anayeweza kuwa na mabadilishano haya na Mungu—je, unaweza kusema Mungu ana hisia za aina gani kuhusu hili? Yale mambo ambayo watu huzungumza ambayo wanapenda, ambayo wanafuatilia na kutamani yote yanahusu dhambi, na yana mielekeo ya uovu. Wakati Mungu anapokabiliana na haya yote, je, hayo si kama kisu katika moyo Wake? Akiwa Amekabiliwa na mambo haya, je, Anaweza kuwa na furaha katika moyo Wake? Je, Angeweza kupata faraja? Wale wanaoishi na Yeye ni wanadamu waliojaa uasi na uovu—je, moyo Wake utakosaje kuteseka? Mateso haya kwa kweli ni makubwa vipi, na ni nani anayeyajali? Ni nani anayeyasikiliza? Na ni nani anayeweza kuyatambua? Watu hawana njia yoyote ya kuuelewa moyo wa Mungu. Mateso Yake ni kitu ambacho watu hawawezi hasa kuyatambua, na ubaridi, na kutojua kwa binadamu kunayafanya mateso ya Mungu kuwa yenye kina zaidi.
Kuna baadhi ya watu ambao wanaonea huruma hali ya Kristo kwa sababukuna mstari katika Biblia unaosema: “Mbweha wana mapango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.” Wakati watu wanaposikia haya, wanayatia moyoni na kuamini kwamba haya ndiyo mateso makubwa zaidi ambayo Mungu huvumilia, na mateso makubwa zaidi ambayo Kristo huvumilia. Sasa, tukiangalia katika mtazamo wa ukweli, je, hivyo ndivyo ilivyo? Hapana? Mungu haamini kwamba ugumu huu ni mateso. Hajawahi kulia dhidi ya dhuluma hizi kwa ajili ya ugumu wa mwili, na Hajawahi kuwafanya wanadamu wamlipe au wampe thawabu kwa chochote. Hata hivyo, Anaposhuhudia kila kitu cha wanadamu, maisha yaliyopotoka na uovu wa wanadamu waliopotoka, Anaposhuhudia kwamba wanadamu wamo mikononi mwa Shetani na wamefungwa na Shetani na hawawezi kukwepa, kwamba watu wanaoishi katika dhambi hawajui ukweli ni nini—Hawezi kuvumilia dhambi hizi zote. Chuki Yake kwa binadamu huongezeka siku baada ya siku, lakini lazima Avumilie yote haya. Haya ni mateso makuu ya Mungu. Mungu hawezi kujieleza kikamilifu hata sauti ya moyo Wake au hisia Zake miongoni mwa wafuasi Wake, na hakuna yeyote miongoni mwa wafuasi Wake anayeweza kuelewa kwa kweli mateso Yake. Hakuna hata anayejaribu kuelewa au kuufariji moyo Wake—moyo Wake huvumilia mateso haya siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, mara kwa mara. Je, unaona nini katika haya yote? Mungu hahitaji chochote kutoka kwa wanadamu kama malipo kwa kile Alichokitoa, lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, Hawezi kuvumilia kamwe uovu, upotovu na dhambi za wanadamu, na badala yake Anahisi chukizo na chuki kupindukia, hali ambayo husababisha moyo wa Mungu na mwili Wake kuvumilia mateso yasiyoisha. Je, ungeyaona haya yote? Kuna uwezekano, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeyaona kwa sababu hakuna yeyote kati yenu anayeweza kumwelewa Mungu kwa kweli. Baada ya muda mnaweza kuyapitia haya wenyewe kwa utaratibu.
Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.
9. Yesu Atenda Miujiza
a. Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano. Naye Yesu akaichukua ile mikate, na baada ya kutoa shukrani, akaigawanya kwa wanafunzi, na wanafunzi wakawapa wale waliokuwa wameketi chini; na vivyo hivyo wale samaki kiasi walichotaka. Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.
b. Kufufuka kwa Lazaro Kwampa Mungu Utukufu
Yohana 11:43-44 Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje, akiwa amefungwa mkono na mguu na sanda: na uso wake ulikuwa umefungwa kwa kitambaa. Yesu akasema kwao, Mfungueni yeye, na mwache aondoke.
Kati ya miujiza iliyotendwa na Bwana Yesu, tumechagua tu hii miwili kwa sababu inatosha kuwaonyesha kile ambacho Ningependa kuzungumzia hapa. Miujiza hii miwili kwa kweli inashangaza, na inawakilisha hasa miujiza ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.
Kwanza, hebu tuangalie kifungu cha kwanza: Yesu Awalisha Watu Elfu Tano.
Ni nini tafsiri ya "mikate mitano na samaki wawili"?? Ni watu wangapi ambao mikate mitano na samaki wawili ingetosha kuwalisha kwa kawaida? Mkipima kulingana na hamu ya kula ya mtu wa kawaida, inaweza kutosha tu watu wawili. Hii ndiyo dhana ya kimsingi kabisa ya mikate mitano na samaki wawili. Hata hivyo, imeandikwa katika dondoo hii kwamba mikate mitano na samaki wawili iliwalisha watu wangapi? Imerekodiwa katika Maandiko kwamba: “Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano.” Tukilinganisha na mikate mitano na samaki wawili, je, watu elfu tano ni idadi kubwa? Ni ninikinachomaanisha kuwa idadi hii ni kubwa sana? Kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu, kugawanya mikate mitano na samaki wawili kati ya watu elfu tano haitawezekana, kwa sababu tofauti kati ya idadi hizi ni kubwa mno. Hata kama kila mtu angepata tu kipande kidogo cha kutafuna, bado mikate hiyo isingetosha watu hao elfu tano. Lakini hapa Bwana Yesu alitenda muujiza—Hakuhakikisha tu kwamba watu elfu tano wangeweza kula na kushiba, lakini kulikuwa na hata chakula kilichosalia. Maandiko yanasema kwamba: “Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee chochote. Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula.” Muujiza huu uliwaruhusu watu kutambua utambulisho na hadhi ya Bwana Yesu, na uliwaruhusu pia kuona kwamba hakuna kisichowezekana kwa Mungu—kwa njia hii, waliona ukweli wa uweza wa Mungu. Mikate mitano na samaki wawili viliweza kutosha kuwalisha watu elfu tano lakini kama kusingekuwa na chakula chochote, je,Mungu angeweza kuwalisha watu hao elfu tano? Bila shaka Angeweza! Huu ulikuwa muujiza, kwa hivyo bila shaka watu walihisi kuwa haueleweki na wakahisi kwamba haikuaminika na iliwashangaza lakini kwa Mungu kufanya kitu kama hicho haikuwa kitu. Kwa sababu hili lilikuwa jambo la kawaida kwa Mungu, ni kwa nini sasa imetengwa kwa ajili ya kufasiriwa? Kwa sababu kile kilichomo nyuma ya muujiza huu kimebeba mapenzi ya Bwana Yesu, ambayo hayajawahi kugunduliwa na wanadamu.
Kwanza, hebu tujaribu kuelewa watu hawa elfu tano walikuwa wa aina gani. Je, walikuwa wafuasi wa Bwana Yesu? Kutoka kwenye Maandiko, tunajua kwamba hawakuwa wafuasi Wake. Je, walijua Bwana Yesu alikuwa ni nani? Bila shaka hawakujua! Kwa kiwango cha chini sana, hawakujua yule mtu aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa Kristo, au pengine baadhi ya watu walijua tu jina Lake lilikuwa nani, na walijua kitu kumhusu Yeye au walikuwa wamesikia kitu kuhusu mambo aliyokuwa Ameyafanya. Udadisi wao kuhusu Bwana Yesu ulikuwa umechochewa tu walipokuwa wamesikia hadithi kumhusu, lakini bila shaka hamwezi kusema kwamba wao walimfuata Yeye, wala hata Kumwelewa. Bwana Yesu alipowaona watu hawa elfu tano, walikuwa na njaa na Angefikiria tu kuwalisha hadi washibe, na hivyo basi ilikuwa katika muktadha huu ndipo Bwana Yesu aliporidhisha matamanio yao. Baada ya kuyaridhisha matamanio yao, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Je, mtazamo Wake kwa watu hawa waliotaka tu kula hadi kushiba ulikuwa upi? Kwa wakati huu,mawazo ya Bwana Yesu na mtazamo Wake ulikuwa katika uhusiano na tabia na kiini cha Mungu. Kuwa mbele ya watu hawa elfu tano waliokuwa na njaa na ambao walitaka tu kula chakula hadi kushiba, kuwa mbele ya watu hawa waliojawa na udadisi na matumaini kumhusu, Bwana Yesu alifikiria tu kutumia muujiza huu ili kuwatolea neema. Hata hivyo, Hakujipa tumaini sana kwamba watakuwa wafuasi Wake, kwani Alijua kwamba walitaka tu kujiunga na furaha hiyo na kuweza kula hadi kushiba, hivyo basi Aliweza kutumia kwa njia bora zaidi kile Alichokuwa nacho hapo, na Akatumia mikate mitano na samaki wawili kuwalisha watu elfu tano. Aliwafumbua macho watu hawa waliofurahia kuona mambo ya kusisimua, waliotaka kushuhudia miujiza, na wakaona kwa macho yao mambo yale ambayo Mungu mwenye mwili Angeweza kukamilisha. Ingawa Bwana Yesu alitumia kitu kinachoweza kuonekana ili kuridhisha udadisi wao, tayari Alijua katika moyo Wake kwamba watu hawa elfu tano walitaka tu kuwa na mlo mzuri, hivyo basi Hakusema chochote kamwe au kuwahubiria kamwe—Aliwaacha tu kuuona muujiza ukifanyika. Bila shaka Asingeweza kuwatendea watu hawa kwa njia sawa ambayo Aliwatendea wanafunzi Wake ambao walimfuata Yeye kwa kweli, lakini katika moyo wa Mungu, viumbe vyote vilikuwa katika utawala Wake, na Angeviruhusu viumbe vyote katika macho Yake kufurahia neema ya Mungu kila ilipohitajika. Hata ingawa watu hawa hawakujua Yeye alikuwa ni nani au kumwelewa, au kuwa na picha yoyote kumhusu au kutoa shukrani Kwake hata baada ya kula mikate na samaki, hili halikuwa jambo ambalo Mungu Alijali kuhusu—Aliwapa watu hawa fursa nzuri ya kufurahia neema ya Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu ana kanuni katika kile Anachofanya, na kwamba Hawaangalii wala kuwalinda wale wasioamini, na Yeye hasa hawaruhusu kufurahia neema Yake. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa hakika? Machoni mwa Mungu, mradi tu viwe ni viumbe vyenye uhai ambavyo Yeye Mwenyewe aliviumba, Ataweza kuvisimamia na kuvitunza; Atavitendea, Atavipangia, na Atavitawala katika njia tofauti. Haya ndiyo mawazo na mtazamo wa Mungu kwa vitu vyote.
Ingawa watu hawa elfu tano walioila mikate hiyo na samaki hawakupanga kumfuata Bwana Yesu, Yeye hakuwa mkali kwao; baada ya wao kula hadi kushiba, je, mwajua kile Alichofanya Bwana Yesu? Je, Aliwahubiria chochote? Je, alienda wapi baada ya haya? Maandiko hayarekodi kwamba Bwana Yesu alisema chochote kwao; Alipokamilisha kutenda muujiza Wake Aliondoka kimya kimya. Kwa hivyo, je, Aliwawekea mahitaji yoyote watu hawa? Kulikuwa na chuki yoyote? Hakukuwepo na chochote kati ya haya—Yeye hakutaka tena kuwajali watu hawa ambao wasingeweza kumfuata, na kwa wakati huu moyo Wake ulikuwa katika maumivu. Kwa sababu alikuwa Ameuona upungufu wa wanadamu na Alikuwa amehisi namna ambavyo wanadamu walikuwa wamemkataa, na Alipowaona watu hawa au Alipokuwa na wao, upumbavu wa binadamu na kutojua kwao kulimfanya awe na huzuni sana na kukamwacha na maumivu katika moyo Wake, hivyo basi Alitaka tu kuwaacha watu hawa haraka iwezekanavyo. Bwana hakuwa na mahitaji yoyote kwao katika moyo Wake, Hakutaka kuwatilia maanani, Yeye hasa hakutaka kutumia nguvu Zake zozote kwao, na Alijua kwamba wasingeweza kumfuata—licha ya haya yote, mtazamo Wake kwao ulikuwa bado upo wazi kabisa. Alitaka tu kuwatendea wema, kuwapa neema, na kwa hakika huu ndio uliokuwa mtazamo wa Mungu kwa kila kiumbe kilicho katika utawala Wake: kwa kila kiumbe, Awatendee kwa huruma, Awatosheleze mahitaji yao, na kuwatunza. Sababu hasa ambayo Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, Aliweza kwa kawaida sana kufichua kiini cha Mungu mwenyewe na kuwatendea watu hawa kwa huruma. Aliwatendea kwa ukarimu na moyo wa huruma na uvumilivu. Haijalishi ni vipi watu hawa walimwona Bwana Yesu, na haikujalisha ni aina gani ya matokeo ambayo yangekuwepo, Alikitendea tu kila kiumbe kutokana na nafasi Yake kama Bwana wa uumbaji wote. Kila kitu Alichofichua kilikuwa, tabia ya Mungu, na kile ambacho Anacho na Alicho. Kwa hivyo Bwana Yesu alifanya kitu kimya kimya, kisha Akaondoka kimya kimya—je, hiki ni kipengele gani cha tabia ya Mungu? Je, unaweza kusema kwamba hizi ni fadhili zenye upendo wa Mungu? Je, unaweza kusema kwamba Mungu hana ubinafsi? Je, mtu wa kawaida anaweza kufanya hivi? Bila shaka hawezi! Katika kiini, wale watu elfu tano ambao Bwana Yesu aliwalisha kwa mikate mitano na samaki wawili walikuwa kina nani? Je, unaweza kusema kwamba walikuwa watu wanaolingana na Yeye? Je, unaweza kusema kwamba wote walikuwa na uadui kwa Mungu? Inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba hawakuwa kabisa wanaolingana na Bwana, na kiini chao halisi kilikuwa na uadui kabisa kwa Mungu. Lakini Mungu aliwashughulikia vipi? Alitumia mbinu ya kutuliza uadui wa watu kwa Mungu—mbinu hii inaitwa “huruma.” Yaani, ingawa Bwana Yesu aliwaona watu hawa kuwa watenda hawa kuwa watenda dhambi, machoni mwa Mungu walikuwa hata hivyo uumbaji Wake hivyo basi bado Aliwatendea wenye dhambi hawa kwa huruma. Huu ndio uvumilivu wa Mungu, na uvumilivu huu unaamuliwa na utambulisho na kiini cha Mungu binafsi. Hivyo basi, hili ni jambo ambalo hakuna mwanadamu aliyeumbwa na Mungu anayeweza kufanya—Mungu pekee ndiye anayeweza kufanya hivi.
Unapoweza kutambua kwa kweli fikira na mtazamo wa Mungu kwa wanadamu, wakati unapoweza kuelewa kwa kweli hisia na kujali kwa Mungu kwa kila kiumbe, utaweza kuelewa kule kujitola na upendo unaotumika kwa kila mmoja wa watu walioumbwa na Muumba. Haya yanapofanyika, utatumia maneno mawili kufafanua upendo wa Mungu—je, maneno hayo mawili ni yapi? Baadhi ya watu husema “usio na ubinafsi” na watu wengine husema "wenye fadhili." Kati ya kauli hizi mbili, “wenye fadhili” ndiyo kauli ambayo inafaa kwa kiasi kidogo zaidi kuufafanua upendo wa Mungu. Hii ni kauli ambayo watu huitumia kumwelezea mtu ambaye ni mkuu au mwenye mawazo mapana. Naichukia kweli kauli hii kwa sababu inarejelea ule utoaji wa msaada bila mpangilio na bila ubaguzi, bila kuzingatia kanuni zozote. Ni maelezo ya kihisia ambayo ni ya kawaida sana kwa watu wapumbavu na waliochanganyikiwa. Wakati neno hili linatumika kufafanua upendo wa Mungu, bila shaka kuna nia ya kumaanisha kukufuru. Nina maneno mawili ambayo yanafafanua kwa usahihi zaidi upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Neno la kwanza ni “kubwa.” Je, si neno hili huamsha na kuleta hisia? Neno la pili ni “pana.” Kuna maana halisi katika maneno haya mawili ambayo Nimeyatumia katika kufafanua upendo wa Mungu. Kama yatachukuliwa kwa njia ya moja kwa moja, “kubwa” inafafanua ukubwa au wingi wa kitu, lakini haijalishi kitu hicho kina ukubwa gani—ni kitu ambacho watu wanaweza kugusa na kuona. Hii ni kwa sababu ipo, si kitu cha kidhahania, bali ni kitu ambacho kinaweza kuwapa watu mawazo kwa njia sahihi na ya kivitendo. Haijalishi kama unautazama kwa mtazamo wa pande mbili au wa pande zote tatu; huhitajiki kufikiria uwepo wake, kwa sababu ni kitu ambacho kwa kweli kipo. Hata ingawa kwa kutumia “kubwa sana” kufafanua upendo wa Mungu kunaweza kuhisiwa kana kwamba tunataka kupima wingi wa upendo Wake, lakini hata hivyo inatoa hisia kwamba hauwezi kupimwa. Ninasema kwamba upendo wa Mungu unaweza kupimwa kwa sababu upendo Wake si aina fulani ya kitu kisichojulikana, na wala hautokani na hadithi zozote. Badala yake, ni kitu cha kutumiwa kwa pamoja na vitu vyote katika utawala wa Mungu, na ni kitu cha kufurahiwa na viumbe vyote kwa viwango tofauti-tofauti na kwa mitazamo tofauti. Ingawa watu hawawezi kuuona au kuugusa, upendo huu huleta utunzaji na uhai kwa vitu vyote jinsi unavyofichuliwa, kidogo kidogo, katika maisha yao, na wanahesabu na kutoa ushuhuda wa upendo wa Mungu ambao wanaufurahia katika kila wakati unaopita. Ninasema kwamba upendo wa Mungu hauwezi kupimwa kwa sababu fumbo la Mungu kutoa na kulisha vitu vyote ni jambo ambalo ni gumu kwa wanadamu kufahamu, kama vile fikira za Mungu kwa vitu vyote, na hasa zile kwa ajili ya wanadamu. Hivyo ni kusema hakuna anayejua damu na machozi ambayo Muumba ametoa kwa sababu ya wanadamu. Hakuna anayeweza kufahamu, hakuna anayeweza kuelewa undani au uzito wa upendo ambao Muumba anao kwa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Kufafanua upendo wa Mungu kama mkubwa sana ni ili kuwasaidia watu kutambua na kuelewa upana wake na ukweli wa uwepo wake. Iko hivyo ili watu waweze kufahamu kwa kina zaidi maana halisi ya neno “Muumba,” na ili watu waweze kupata ufahamu wa kina zaidi wa maana ya “kiumbe aliyeumbwa.” Neno “pana” kwa kawaida huwa inafafanua nini? Kwa ujumla inatumika kufafanua bahari au ulimwengu, kwa mfano: “ulimwengu mpana sana,” au “bahari pana.” Ule upana na kina cha siri cha ulimwengu upo nje ya ufahamu wa binadamu na ni kitu ambacho kinavutia fikra za binadamu, kitu ambacho wanahisi kupendezwa nacho sana. Fumbo lake na undani wake vyote vinaweza kuonekana, lakini haviwezi kufikika. Unapofikiria kuhusu bahari, unafikiria kuhusu upana wake—yaonekana isiyo na mipaka, na unaweza kuhisi maajabu yake na uwezo wake mkubwa wa kushikilia vitu. Hii ndiyo sababu Nimetumia neno “pana” kuufafanua upendo wa Mungu. Ni ili kuwasaidia watu waweze kuhisi jinsi ulivyo wa thamani, kuhisi uzuri wa kina wa upendo Wake, na kwamba nguvu za upendo wa Mungu haziishi na zimeenea. Nilitumia neno hili kwa ajili ya kuwasaidia kuhisi utakatifu wa upendo Wake, na heshima pamoja na hali ya kutoweza kukosewa ya Mungu ambayo inafichuliwa kupitia upendo Wake. Je, sasa unafikiri kwamba “pana” ni neno linalofaa kufafanua upendo wa Mungu? Je, upendo wa Mungu unaweza kufikia maana ya maneno haya mawili, “kubwa sana” na “pana”? Bila shaka! Katika lugha ya kibinadamu, maneno haya mawili tu ndiyo ambayo yanafaa kwa kiasi fulani, na kwa kiasi fulani yanakaribia kuufafanua upendo wa Mungu. Je, haufikirii hivyo? Kama Ningewauliza muufafanue upendo wa Mungu, je, mngetumia kauli hizi mbili? Kuna uwezekano mkubwa zaidi, msingeyatumia kwa sababu ufahamu na utambuzi wenu wa upendo wa Mungu umewekewa mipaka kwa upeo wa mtazamo wa pande mbili, na haujaongezeka kufikia kimo cha nafasi ya pande tatu. Hivyo basi kama Ningetaka mfafanue upendo wa Mungu, mngehisi kwamba mnakosa maneno; huenda pengine hata mtakosa kuongea kabisa. Maneno haya mawili ambayo Nimeyazungumzia leo yanaweza kuwa magumu kwako kuyaelewa, au unaweza usikubaliane nayo hata kidogo. Hii inaonyesha tu ukweli kwamba ufahamu na uelewa wako wa upendo wa Mungu ni wa juujuu tu na una mipaka ya upeo finyu. Nimesema hapo awali kwamba Mungu hana ubinafsi; je, unakumbuka neno hili, "kutokuwa na ubinafsi"? Je, inaweza kuwa kwamba upendo wa Mungu unaweza tu kuelezewa kuwa usio na ubinafsi? Je, huu si upeo finyu sana? Mnapaswa kutafakari suala hili zaidi, ili muweze kupata kitu kutoka kwalo.
Yale yaliyotajwa hapo juu ndiyo yale tuliyoyaona kuhusu tabia ya Mungu na kiini Chake kutoka katika muujiza wa kwanza. Hata ingawa ni hadithi ambayo watu wameisoma kwa maelfu kadhaa ya miaka, inao mtiririko mwepesi, na inawaruhusu watu kuweza kuona tukio lisilo la kawaida likitokea, ilhali katika mtiririko huu mwepesi tunaweza kuona kitu chenye thamani zaidi, hali ambayo ni tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho. Mambo haya Aliyo nayo na Aliyo yanamwakilisha Mungu Mwenyewe na ni onyesho la fikira za Mungu mwenyewe. Wakati Mungu anapoonyesha fikira Zake, ni udhihirisho wa sauti ya moyo Wake. Anatumai kwamba kutakuwa na watu wanaoweza kumwelewa Yeye, kumjua Yeye na wanafahamu mapenzi Yake, na Anatumai kutakuwa na watu wanaoweza kuisikia sauti ya moyo Wake na wataweza kushirikiana kwa bidii ili kuridhisha mapenzi Yake. Na mambo haya ambayo Bwana Yesu aliyafanya yalikuwa ni maonyesho ya Mungu ya kimyakimya.
Kisha, tuangalie kifungu kifuatacho: Ufufuo wa Lazaro Unamtukuza Mungu.
Je, mna maoni gani baada ya kusoma kifungu hiki? Umuhimu wa muujiza huu ambao Bwana Yesu aliutenda ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa awali kwa sababu hakuna muujiza ambao unastaajabisha zaidi kuliko ule wa kumfufua mtu aliyekufa kutoka kaburini. Bwana Yesu kufanya kitu kama hiki kulikuwa na umuhimu mkubwa mno katika enzi hiyo. Kwa sababu Mungu alifanyika mwili, watu wangeweza tu kuona sura Yake ya kimwili, upande Wake wa kivitendo, na kipengele Chake kisicho na umuhimu. Hata kama baadhi ya watu waliweza kuona na kuelewa kipengele fulani cha tabia Yake au uwezo fulani ambao Alionekana kuwa nao, hakuna aliyejua ni wapi Bwana Yesu alitoka, Yeye alikuwa ni nani kwa kweli katika kiini Chake, na ni mambo gani mengine ambayo kwa hakika alikuwa na uwezo wa kuyafanya. Yote haya hayakujulikana kwa wanadamu. Watu wengi sana walitaka kupata uthibitisho wa kujibu maswali haya kuhusu Bwana Yesu, na kuujua ukweli. Je, Mungu angeweza kufanya jambo fulani ili kuthibitisha utambulisho Wake Mwenyewe? Kwa Mungu, huu ulikuwa upepo mwanana—lilikuwa jambo rahisi sana. Angefanya kitu popote, wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho na kiini Chake, lakini Mungu alikuwa na njia Yake ya kufanya mambo—kwa mpango, na kwa hatua. Hakufanya vitu bila mpangilio; Alitafuta muda unaofaa, na fursa inayofaa kufanya kitu chenye maana zaidi kwa wanadamu kuweza kuona. Hili lilithibitisha mamlaka Yake na utambulisho Wake. Kwa hivyo, je, kufufuka kwa Lazaro kungeweza kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu? Hebu tuangalie kifungu hiki cha maandiko: “Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekuwa amekufa ….” Wakati Bwana Yesu alipofanya haya, Alisema tu jambo moja: “Lazaro, kuja nje.” Kisha Lazaro akatoka nje ya kaburi—hii ilitimizwa kwa sababu ya maneno machache tu yaliyotamkwa na Bwana. Kwa wakati huu, Bwana Yesu Hakuanzisha madhabahu, na Hakufanya vitendo vingine vyovyote. Alisema tu hili jambo moja. Je, hii inapaswa kuitwa muujiza au amri? Au ilikuwa ni aina fulani ya uchawi? Kwa juujuu, inaonekana inaweza kuitwa muujiza, na ukiangalia kutoka kwa mtazamo wa kisasa, bila shaka bado mnaweza kuuita muujiza. Hata hivyo, kwa hakika haikuweza kuchukuliwa kuwa ni uchawi wakuiita nafsi kurudi kutoka kwa wafu, na bila shaka si uchawi. Ni sahihi kusema kwamba muujiza huu ulikuwa ni udhihirisho wa kawaida, mdogo sana wa mamlaka ya Muumba. Haya ndiyo mamlaka, na uwezo wa Mungu. Mungu ana mamlaka ya kumfanya mtu afe, kuruhusu nafsi yake iondoke mwilini mwake na kurudi kuzimu au popote pale itakapoenda. Wakati wa kifo cha mtu, na mahali atakapokwenda baada ya kifo—haya yanaamuliwa na Mungu. Yeye anaweza kufanya haya wakati wowote na mahali popote. Yeye hazuiliwi na binadamu, matukio, vitu, nafasi, au jiografia. Akitaka kufanya hivyo, Anaweza kufanya hivyo, kwa sababu vitu vyote na viumbe hai viko chini ya utawala Wake, na vitu vyote vinaongezeka, vinaishi, na kupotea kwa neno Lake na mamlaka Yake. Anaweza kumfufua binadamu aliyekufa, na pia hiki ni kitu Anachoweza kufanya wakati wowote mahali popote. Haya ndiyo mamlaka ambayo Muumba pekee humiliki.
Wakati Bwana Yesu alipofanya jambo kama vile kumfufua Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa uthibitisho kwa wanadamu na kwa Shetani ili waweze kuona, na kuwafanya wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amefanyika mwili, daima, Alibakia katika kuuamuru ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu viko mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kuwafunza na kuwaelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua madhubuti ambayo kwayo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kutoa kwa ajili ya wanadamu. Ilikuwa ni njia, isiyo na matumizi ya maneno kwa ajili ya Muumba kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote. Ilikuwa ni mbinu Yake ya kuwaambia wanadamu kupitia hatua za kivitendo kwamba hakuna wokovu isipokuwa kupitia Kwake. Mbinu hii ya kimyakimya ambayo Aliitumia kuwaelekeza wanadamu inadumu milele, haitafutika, na iliweza kuleta mshtuko na nuru katika mioyo ya wanadamu ambayo kamwe haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hii ina athari kubwa kwa kila mmoja wa wafuasi wa Mungu. Inaweka kwa uthabiti ndani ya kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu. Ingawa Mungu ana aina hii ya mamlaka, na ingawa Aliutuma ujumbe kuhusu ukuu Wake juu maisha na kifo cha wanadamu kupitia kwa ufufuo wa Lazaro, hii haikuwa kazi Yake ya msingi. Kamwe Mungu hafanyi jambo lisilo na maana. Kila jambo Analolifanya lina thamani kubwa na hata linazidi kito kilicho ndani ya ghala la hazina. Bila shaka Yeye hangefanya “kumtoa mtu kutoka katika kaburi lake” kuwa sababu ya kimsingi au lengo au kipengele kikuu katika kazi Yake. Mungu hafanyi chochote ambacho hakina maana. Ufufuo wa Lazaro kama tukio la pekee unatosha kuonyesha mamlaka ya Mungu. Unatosha kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu hakurudia aina hii ya muujiza. Mungu hufanya mambo kulingana na kanuni Zake binafsi. Katika lugha ya kibinadamu, inaweza kusemwa kwamba Mungu anazingatia tu kazi muhimu. Yaani, Mungu anapofanya mambo, hatoki nje ya kusudi la kazi Yake. Anajua ni kazi gani Anayotaka kutekeleza katika hatua hii, kile Anachotaka kukamilisha, na Atafanya kazi mahususi kulingana na mpango Wake. Kama mtu aliyepotoka angekuwa na uwezo wa namna hiyo, angekuwa akifikiria tu kuhusu njia za kufichua uwezo wake ili wengine wajue namna alivyokuwa thabiti, ili wamsujudie, ili aweze kuwadhibiti na kuwameza. Huu ndio uovu unaotoka kwa Shetani—huu unaitwa upotovu. Mungu hana tabia kama hiyo, na Hana kiini kama hicho. Kusudi Lake katika kufanya mambo si kujionyesha Mwenyewe, lakini kuwapa wanadamu ufunuo na mwongozo zaidi, na hii ndiyo sababu watu wanaona mifano michache sana katika Biblia ya aina hii ya tukio. Hii haimaanishi kwamba uwezo wa Bwana Yesu ulikuwa finyu, au kwamba asingeweza kufanya jambo la aina hiyo. Ni kwamba Mungu hakutaka tu kulifanya jambo hilo, kwa sababu Bwana Yesu kumfufua Lazaro kulikuwa na umuhimu wa kivitendo kabisa, na pia kwa sababu kazi kuu ya Mungu kuwa mwili haikuwa ni kutenda miujiza, haikuwa kuwafufua watu kutoka kwa wafu, lakini ilikuwa ni kazi ya ukombozi wa wanadamu. Kwa hivyo, kazi nyingi ambazo Bwana Yesu alikamilisha zilikuwa ni kuwafunza watu, kuwatoshelezea haja zao, na kuwasaidia, na mambo kama vile kumfufua Lazaro yalikuwa tu sehemu ndogo ya huduma ambayo Bwana Yesu alitekeleza. Hata zaidi, mnaweza kusema kwamba “kujionyesha” si sehemu ya kiini cha Mungu, hivyo basi kutoonyesha miujiza zaidi hakukuwa kujizuia kwa kudhamiria, wala hakukuwa kwa sababu ya vizuizi vya kimazingira, na bila shaka hakukuwa kwa sababu ya ukosefu wa uwezo.
Bwana Yesu alipomfufua Lazaro kutoka kwa wafu, Alitumia maneno haya machache tu: “Lazaro, njoo huku nje.” Hakusema lolote mbali na hili. Kwa hivyo, je, maneno haya yanaonyesha nini? Yanaonyesha kwamba Mungu anaweza kutimiza jambo lolote kwa kunena, ikiwemo kumfufua mtu aliyekufa. Mungu alipoumba vitu vyote, Alipouumba ulimwengu, Alifanya hivyo kwa maneno—amri zilizotamkwa, maneno yaliyotamkwa kwa mamlaka, na hivyo tu vitu vyote viliumbwa. Yalikamilishwa hivyo. Mstari huu mmoja uliozungumzwa na Bwana Yesu ulikuwa sawa na maneno yaliyotamkwa na Mungu alipoziumba mbingu na vitu vyote; mstari huo pia uliweza kushikilia mamlaka ya Mungu, uwezo wa Muumba. Vitu vyote viliumbwa na vikasimama kwa sababu ya matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu, na vivyo hivyo, Lazaro alitembea kutoka katika kaburi lake kwa sababu ya matamshi kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu. Haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ya Mungu, yaliyoonyeshwa na kutambuliwa katika mwili Wake. Aina hii ya mamlaka na uwezo vinamilikiwa na Muumba, na kwa Mwana wa Adamu ambaye kwake Muumba alitambuliwa. Huu ndio ufahamu uliofunzwa kwa mwanadamu na Mungu kupitia kumfufua Lazaro kutoka kwa wafu. Hayo ndiyo yote katika mada hii. Kisha, hebu tuyasome maandiko.
10. Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu
Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.
11. Mafarisayo Kukemewa na Yesu
Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.
Mat 23:13-15 Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.
Kuna vifungu viwili tofauti hapo juu—hebu kwanza tuangalie kile cha kwanza: Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu.
Katika Biblia, tathmini ya Mafarisayo kwa Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “walisema, Amerukwa na akili,… Ana Beelzebuli, na kwa mkuu wa mapepo Anatoa mapepo” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Mafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa wao tu kuiga maneno ya watu wengine, na wala haikuwa dhana isiyo na msingi —ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho lao lilifanywa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele za watu ni kana kwamba ilikuwa na msingi mzuri, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kukizuia. Nguvu zao zilizochanganyikiwa za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua tamaa zao mbaya zisizo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na asili yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na tamaa zao mbaya zisizo na misingi, wivu, na asili yao mbaya na yenye nia mbaya ya uadui wao dhidi ya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, kwa upofu, bila subira, kwa wazimu, na kwa nia ya kudhuru, walishambulia na kudharau kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilifikia hata kiwango cha kumvunjia heshima Roho Wake kwa makusudi, yaani, Roho Mtakatifu ambaye ni Roho wa Mungu. Hivi ndivyo walivyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli,” na “mkuu wa mapepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa mapepo. Waliweza kuipatia sifa kazi ambayo Roho wa Mungu aliyepata mwili, ambaye Alikuwa amejivika mwili, kama iliyorukwa na akili. Hawakumkufuru Roho wa Mungu tu kama Beelzebuli na mkuu wa mapepo, bali pia waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upinzani wao na kumkufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kuwatumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na watumishi wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na majaribio yao kwa Mungu yasiyoisha. Kiini cha upinzani wao kwa Mungu na mtazamo wao wa uadui Kwake, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa kulingana na yale waliyoyasema na kuyafanya, na Mungu akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusamehewa katika ulimwengu huu na ule ulimwengu ujao, kama inavyofafanuliwa katika kifungu kifuatacho cha maandiko: “kwa kumkufuru Roho Mtakatifu wanadamu hawatasamehewa” na, “yeyote atakayenena neno baya juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” Leo, hebu tuzungumzie maana halisi ya maneno haya kutoka kwa Mungu “hatasamehewa, katika ulimwengu huu wa sasa, wala katika ule ujao.” Hivyo ni kusema, acha tuweke wazi namna ambavyo Mungu anatimiza maneno haya: “hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”
Kila kitu ambacho tumezungumzia kinahusiana na tabia ya Mungu na mtazamo Wake kuelekea watu, matukio, na vitu. Kwa kawaida, vifungu viwili vya hapo juu haviwezi kuachwa. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi mbili za maandiko? Baadhi ya watu husema wanaiona ghadhabu ya Mungu. Watu wengine watasema wanauona upande wa tabia ya Mungu ambao hauvumilii kosa la wanadamu, na kwamba watu wakifanya kitu ambacho kinamkufuru Mungu, hawatapata msamaha Wake. Licha ya ukweli kwamba watu wanaona na kutambua ghadhabu na kutovumilia makosa ya wanadamu kwa Mungu katika vifungu hivi viwili, bado hawaelewi kwa kweli mtazamo Wake. Vifungu hizi viwili vina ufafanuzi wa mwelekeo na mtazamo wa kweli wa Mungu kwa wale wanaomkufuru na kumghadhabisha Yeye. Dondoo hii katika maandiko inashikilia maana halisi ya mwelekeo na mtazamo Wake: “Yeyote atakayenena neno baya juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” Watu wanapomkufuru Mungu, wakati wanapomghadhabisha Yeye, Yeye hutoa hukumu, na hukumu hii ndiyo matokeo yaliyotolewa na Yeye. Hali hii inafafanuliwa hivi katika Biblia: “Kwa sababu hiyo nawaambia, kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, lakini kwa kumkufuru Roho Mtakatifu wanadamu hawatasamehewa” (Mat 12:31), na “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki!” (Mat 23:13). Hata hivyo, je, imerekodiwa katika Biblia ni matokeo yapi yalikuwepo kwa wale waandishi na Mafarisayo, pamoja na wale watu waliosema Alikuwa amerukwa na akili baada ya Bwana Yesu kuyasema mambo hayo? Je, imerekodiwa kama walipata adhabu yoyote? Kuna uhakika kwamba hakukuwa na adhabu: Kusema hapa kwamba “hakukuwa” si kwamba haikurekodiwa, lakini kwa hakika hakukuwa na matokeo yoyote ambayo yangeonekana kwa macho ya binadamu. Neno hili “haikurekodiwa” linaelezea suala, yaani, mtazamo na kanuni za Mungu katika kushughulikia mambo fulani. Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga, au hata wale wanaomkashifu—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mtazamo wa wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mtazamo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao. Hata hivyo, baada ya Mungu kusema mambo haya, bado watu wangeona kwa nadra ukweli wa namna ambavyo Mungu angewashughulikia watu hao, na wasingeelewa kanuni za matokeo na hukumu ambayo Mungu aliwapa. Hiyo ni kusema, wanadamu hawawezi kuona mtazamo na mbinu fulani za Mungu katika kuwashughulikia. Hali hii inahusiana na kanuni za Mungu za kufanya mambo. Mungu hutumia matukio ya kweli katika kushughulikia tabia ovu za baadhi ya watu. Yaani, Hatangazi dhambi zao na haamui matokeo yao, lakini Anatumia moja kwa moja matukio ya kweli ili kuwaruhusu waadhibiwe, ili wapate adhabu wanayostahili. Wakati matukio hayo ya kweli yamefanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia potovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuyaona, kama vile kuadhibiwa au kuuawa. Hii ni kwa sababu katika hali zile ambazo Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, kutoonyesha tena rehema au uvumilivu kwao, kutowapa fursa zaidi, mwelekeo Anaouchukua kwao ni kuwaweka pembeni. Ni nini maana ya “kuweka pembeni”? Maana ya msingi ya neon hili ni kuweka kitu kwa upande mmoja, kukipuuzia na kutokizingatia tena. Lakini hapa, wakati Mungu “anapomweka mtu pembeni,” kuna fafanuzi mbili tofauti kuhusu maana yake: Ufafanuzi wa kwanza ni kwamba Amempa Shetani kuyashughulikia maisha ya mtu huyo, na kila kitu cha mtu huyo. Mungu hatamwajibikia tena na Hataweza kumsimamia tena. Kama mtu huyo atarukwa na akili, au atakuwa mpumbavu, na kama atakuwa hai au atakufa, au kama atashushwa jehanamu ili kupata adhabu yake, hakuna hata moja kati ya haya ambayo yatakuwa na uhusiano wowote na Mungu. Hiyo ingemaanisha kwamba kiumbe hicho hakitakuwa na uhusiano wowote na Muumba. Ufafanuzi wa pili ni kwamba Mungu ameamua kwamba Yeye Mwenyewe anataka kufanya kitu na mtu huyu, kwa mikono Yake mwenyewe. Inawezekana kwamba Ataweza kutumia huduma ya mtu wa aina hii, au kwamba AtaMtumia mtu wa aina hii kama foili[b]. Inawezekana kwamba Atakuwa na njia maalum ya kushughulika na mtu wa aina hii, njia maalum ya kumshughulikia—kama tu Paulo. Hii ndio kanuni na mwelekeo katika moyo wa Mungu kuhusu namna Alivyoamua kumshughulikia mtu wa aina hii. Hivyo basi wakati watu wanapompinga Mungu, na kumkashifu na kumkufuru Yeye, kama wataendelea kusema ubaya kuhusu tabia Yake, au kama watapitiliza kiwango cha uvumilivu wa Mungu, athari zake hazifikiriki. Athari zile mbaya zaidi ni kwamba Mungu anayakabidhi maisha yao na kila kitu chao kwa Shetani, mara moja na milele. Hawatasamehewa daima dawamu. Hii inamaanisha kwamba mtu huyu amekuwa chakula katika kinywa cha Shetani, kitu cha kuchezea katika mikono yake, na kuanzia hapo, Mungu hahusiki naye. Mnaweza kufikiria ni aina gani ya masikitiko iliyokuweko wakati Shetani alipomjaribu Ayubu? Hata chini ya sharti kwamba Shetani hakuruhusiwa kudhuru uhai wa Ayubu, bado Ayubu aliteseka sana. Na, je, si vigumu hata zaidi kufikiria uharibifu ambao Shetani angesababisha juu ya mtu ambaye amekabidhiwa kabisa kwa Shetani, ambaye yumo mikononi mwa Shetani kabisa, ambaye amepoteza kabisa utunzaji na huruma za Mungu, ambaye hayuko tena katika utawala wa Muumba, ambaye amenyang’anywa haki ya kumwabudu Yeye, na haki ya kuwa kiumbe katika utawala wa Mungu, ambaye uhusiano wake na Bwana wa uumbaji umekatizwa kabisa? Kuteswa kwa Ayubu na Shetani kulikwa jambo ambalo lingeonekana kwa macho ya kibinadamu, lakini Mungu anapomkabidhi Shetani maisha ya mtu, athari zake zitakuwa jambo ambalo mtu hawezi kufikiria. Ni sawa tu na baadhi ya watu kuweza kuzaliwa tena wakiwa ng’ombe, au punda, au baadhi ya watu wakichukuliwa kabisa, na kupagawa na roho chafu, za uovu, na kadhalika. Haya ndiyo matokeo ya baadhi ya watu ambao Mungu anawakabidhi kwa Shetani. Kwa nje, yaonekana kwamba watu hao waliomdhihaki, waliomkashifu, kumshutumu, na kumkufuru Bwana Yesu hawakupata athari zozote. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Mungu Anao mwelekeo wa kushughulikia kila kitu. Huenda Asitumie lugha ya wazi kuwaambia watu matokeo ya namna Anavyowashughulikia kila aina ya watu. Wakati mwingine Hazungumzi kwa njia ya moja kwa moja, lakini badala yake Anatenda mambo kwa njia ya moja kwa moja. Kwamba Yeye haongelei jambo haimaanishi kwamba hakuna matokeo—kwa kweli, katika hali kama hiyo inawezekana kwamba matokeo ni mabaya zaidi. Kwa nje, inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna watu fulani ambao Mungu hasemi kwao kwa uwazi kuhusu mtazamo Wake, lakini kwa kweli, Mungu hajataka kuwaza juu yao kwa muda mrefu. Hataki kuwaona tena. Kwa sababu ya mambo ambayo wamefanya, tabia yao, kwa sababu ya asili yao na kiini chao, Mungu anawataka tu watoweke machoni Mwake, Anataka kuwakabidhi moja kwa moja kwa Shetani, kumpa Shetani roho zao, nafsi zao na miili yao, kumruhusu Shetani kufanya atakacho. Ipo wazi ni kwa kiwango gani Mungu anawachukia, na ni kwa kiwango gani Ameudhika nao. Kama mtu atamghadhabisha Mungu kufikia kiwango ambacho Mungu hataki kumwona tena, kwamba Atakata tamaa kabisa na yeye, hadi katika kiwango ambacho Mungu hataki tena kushughulika naye Yeye mwenyewe—kama itafikia kiwango hiki ambapo Atawakabidhi kwa Shetani ili aweze kufanya apendavyo, kumruhusu Shetani kumdhibiti, kumtumia, na kumtendea kwa njia yoyote—basi mtu huyu atakuwa amemalizika kabisa. Haki yake ya kuwa binadamu imebatilishwa kabisa, na haki yake ya kuwa kiumbe imefikia mwisho. Je, huoni kwamba hii ndiyo adhabu mbaya zaidi?
Yote hayo hapo juu ni maelezo kamili ya maneno haya: “Hatasamehewa, katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao,” na pia hutumika kama ufafanuzi rahisi juu ya vifungu hivi kutoka katika Maandiko. Naamini kwamba nyote mna uelewa wake sasa!
Sasa hebu tusome vifungu vifuatavyo kutoka kwenye maandiko hapa chini.
12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake
Yohana 20:26-29 Na kufuatia siku nane tena wanafunzi wake walikuwa ndani, naye Tomaso alikuwa nao: kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kusema, Amani iwe nanyi. Kisha akasema kwa Tomaso, nyoosha kidole chako hapa, na uitazame mikono yangu, nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani. Naye Tomaso akajibu na kumwambia, BWANA Wangu na Mungu wangu. Yesu akasema kwake, Tomaso, kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini.
Yohana 21:16-17 Akamwambia tena kwa mara ya pili, Simioni, mwana wa Yohana, unanipenda mimi? Akasema kwake, Ndiyo, Bwana, unajua kwamba mimi nakupenda. Akasema kwake, Walishe kondoo wangu. Akasema kwake mara ya tatu, Simioni, mwana wa Yohana, Unanipenda Mimi? Petro alisikitika kwa sababu alimwambia mara ya tatu, Unanipenda Mimi? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua vitu vyote, unajua kwamba mimi nakupenda. Yesu akamwambia, Walishe kondoo wangu.
Kile ambacho vifungu hivi vinasimulia ni baadhi ya mambo ambayo Bwana Yesu alifanya na kusema kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka Kwake. Kwanza, hebu tuangalie tofauti zozote zinazoweza kuwepo kwa Bwana Yesu kabla na baada ya kufufuka Kwake. Je, Alikuwa bado ni Bwana Yesu yule yule wa siku zilizopita? Maandiko yanao mstari ufuatao unaomfafanua Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake: “Kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kusema, Amani iwe nanyi.” Ni wazi sana kwamba Bwana Yesu wakati huo hakuwa tena mwili, lakini alikuwa katika umbo la kiroho. Hii ni kwa sababu Alikuwa amevuka ile mipaka ya mwili, na wakati ambapo mlango ulifungwa Aliweza bado kuja katikati ya watu na kuwaruhusu wao kumwona Yeye. Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu baada ya kufufuka na Bwana Yesu aliyeishi katika mwili kabla ya kufufuka. Hata ingawa hakukuwa na tofauti yoyote kati ya mwonekano wa mwili wa kiroho wa wakati huo na mwonekano wa Bwana Yesu hapo kabla, Bwana Yesu kwa wakati huo Alikuwa amekuwa mtu ambaye Alijihisi kama mgeni kwa watu, kwa sababu Alikuwa amekuwa mwili wa kiroho baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, na ikilinganishwa na mwili Wake wa awali, mwili huu wa kiroho ulikuwa wa kutatanisha na wa kuwachanganya watu zaidi. Hali hii iliunda umbali zaidi kati ya Bwana Yesu na watu, nao watu wakahisi katika mioyo yao kwamba Bwana Yesu wa wakati huo Alikuwa amekuwa wa ajabu zaidi. Ufahamu na hisia hizi kwa upande wa watu uliwarudisha ghafla katika enzi ya kuamini kwa Mungu ambaye hakuweza kuonekana wala kugusika. Hivyo basi, kitu cha kwanza ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake kilikuwa kumruhusu kila mmoja kuweza kumwona, kuthibitisha kuwa yupo, kuthibitisha ukweli wa kufufuka Kwake. Zaidi ya hayo, kitendo hiki kilirejesha uhusiano Wake na watu kama ulivyokuwa Alipokuwa akifanya kazi katika mwili, Alipokuwa Kristo ambaye wangeweza kumuona na kumgusa. Kwa njia hii, mojawapo ya matokeo ni kwamba watu hawakuwa na shaka kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka kutoka kwa kifo baada ya kusulubishwa msalabani, na hakukuwa na shaka katika kazi ya Bwana Yesu ya kuwakomboa wanadamu. Na matokeo mengine ni kwamba hoja ya Bwana Yesu kujitokeza kwa watu baada ya kufufuka Kwake na kuwaruhusu watu kuweza kumwona na kumgusa Yeye kwa uthabiti kuliweza kuwasalimisha wanadamu katika Enzi ya Neema. Kuanzia wakati huu, watu hawakuweza kurudi katika enzi ya awali, Enzi ya Sheria, kwa sababu ya “kutoweka” au “kuondoka bila neno” kwa Bwana Yesu lakini wangeendelea mbele, kufuata mafundisho ya Bwana Yesu na kazi Aliyokuwa amefanya. Hivyo basi, awamu mpya katika kazi ya Enzi ya Neema iliweza kufunguliwa rasmi na watu waliokuwa katika sheria walikuja rasmi kutoka katika sheria kuanzia hapo na kuendelea, na kuingia katika enzi mpya, katika mwanzo mpya. Hizi ndizo sababu mbalimbali za kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu baada ya kufufuka Kwake.
Kwa sababu Alikuwa mwili wa kiroho, watu wangewezaje kumgusa Yeye na kumwona Yeye? Swali hili linagusia juu ya umuhimu wa kuonekana kwa Bwana Yesu kwa wanadamu. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi za maandiko? Kwa ujumla miili ya kiroho haiwezi kuonekana wala kuguswa, na baada ya kufufuka, kazi ambayo Bwana Yesu alikuwa amechukua tayari ilikuwa imekamilika. Hivyo basi, kinadharia Hakuwa na haja kabisa ya kurudi katikati ya watu akiwa katika taswira Yake ya asili ili kukutana na wao, lakini kujitokeza kwa mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kwa watu kama vile Tomaso kulifanya umuhimu wa kuonekana Kwake kuwa thabiti zaidi, na hali hii iliweza kupenyeza zaidi kwa kina katika mioyo ya watu. Alipomjia Tomaso, alimwacha Tomaso aliyekuwa akishuku kumgusa mkono Wake na kumwambia maneno haya: “Nyoosha mkono wako hapa, na uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.” Maneno haya, na vitendo hivi vyote havikuwa vitu ambavyo Bwana Yesu alitaka kusema na kufanya tu baada ya Yeye kufufuka, lakini yalikuwa mambo Aliyotaka kuyafanya kabla ya kusulubishwa msalabani, kwa sababu mashaka ya Tomaso hayakuwa yameanza wakati huo tu, bali yalikuwa pamoja naye wakati wote alipokuwa akimfuata Bwana Yesu. Ni dhahiri kwamba, kabla ya Bwana Yesu kusulubishwa msalabani tayari alikuwa na ufahamu wa watu kama Tomaso. Hivyo basi, tunaweza kuona nini kutokana na haya? Alikuwa angali Bwana Yesu yule yule hata baada ya kufufuka Kwake. Kiini chake kilikuwa hakijabadilika. Hata hivyo, huyu alikuwa Bwana Yesu ambaye amefufuka kutoka kwa wafu na kurudi kutoka katika ulimwengu wa kiroho na akiwa na sura Yake ya asili, na tabia Yake ya asili, pamoja na uelewa Wake wa wanadamu tangu wakati Wake akiwa katika mwili, kwa hivyo Alimwendea Tomaso kwanza ili kumuacha Tomaso auguse ubavu Wake, kumfanya sio tu kuuona mwili Wake wa kiroho baada ya kufufuka, lakini pia kumruhusu auguse na kuuhisi uwepo wa mwili Wake wa kiroho, na kutupilia mbali kabisa mashaka yake. Kabla ya Bwana Yesu kusulubishwa msalabani, Tomaso siku zote alishuku kwamba Yeye ni Kristo, na hakuweza kuamini. Imani yake katika Mungu ilianzishwa tu kwa msingi wa kile ambacho angeweza kuona kwa macho yake, kile ambacho angeweza kugusa kwa mikono yake. Bwana Yesu alikuwa na ufahamu mzuri wa imani ya mtu wa aina hii. Waliamini tu katika Mungu wa mbinguni, na hawakuamini kamwe, na wasingekubali Yule Aliyetumwa na Mungu, au Kristo katika mwili. Ili kumfanya Tomaso aweze kukubali na kuamini katika uwepo wa Bwana Yesu na kwamba kweli Alikuwa Mungu mwenye mwili, Alimruhusu Tomaso kuunyosha mkono wake na kugusa ubavu Wake. Je, Tomaso alikuwa akishuku kwa njia tofauti kabla na baada ya kufufuka kwa Bwana Yesu? Alikuwa daima akishuku, na mbali na mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kumtokea yeye binafsi na kumruhusu Tomaso kugusa alama za misumari katika mwili Wake, hakuna aliyeweza kutatua mashaka yake, na hakuna mtu ambaye angemfanya kuziachilia. Hivyo basi, kuanzia muda ambao Bwana Yesu alimruhusu kuugusa ubavu Wake na kumwacha akihisi uwepo wa alama za misumari, mashaka ya Tomaso yakatoweka na akajua kwa kweli kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka na akatambua na kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Kristo wa kweli, na kuamini kwamba alikuwa Mungu mwenye mwili. Ingawa wakati huu Tomaso hakushuku tena, alikuwa amepoteza milele fursa ya kukutana na Kristo. Alikuwa amepoteza milele fursa ya kuwa pamoja na Yeye, kumfuata Yeye, na kumjua Yeye. Alikuwa amepoteza fursa ya Kristo kumfanya yeye kuwa mkamilifu. Kuonekana kwa Bwana Yesu na maneno Yake yalitoa hitimisho, na hukumu kuhusiana na imani ya wale ambao walijawa na kutoamini kwingi. Alitumia maneno na vitendo Vyake halisi kuwaambia wale waliokuwa wakishuku, kuwaambia wale ambao waliamini tu katika Mungu aliye juu mbinguni lakini hawakumwamini Kristo: Mungu hakuitukuza imani yao, wala Hakuupongeza ufuasi wao uliojawa na mashaka. Ile siku ambayo walimwamini Mungu na Kristo kikamilifu inaweza tu kuwa siku ambayo Mungu alikamilisha kazi Yake kubwa. Bila shaka, siku hiyo ndio ilikuwa pia siku ambayo hukumu ilitolewa juu ya mashaka yao. Mtazamo wao kwa Kristo uliamua hatima zao, na kushuku kwao kwa ukaidi kulimaanisha imani yao haikuwapatia matokeo yoyote, na ugumu wao ulimaanisha kwamba matumaini yao yaliambulia patupu. Kwa sababu imani yao katika Mungu aliye mbinguni ilisababishwa na njozi, na kushuku kwao katika Kristo kulikuwa kwa kweli mtazamo wao wa kweli kwa Mungu, hata ingawa walizigusa alama za misumari kwenye mwili wa Bwana Yesu, imani yao ilikuwa bado bure na matokeo yao yangeweza tu kufafanuliwa kama kuchota maji na kikapu cha mianzi—yote ni bure bilashi. Kile Bwana Yesu Alichomwambia Tomaso kilikuwa kikisema hivyo waziwazi kwa kila mtu: Yule Bwana Yesu aliyefufuka ndiye Bwana Yesu ambaye mwanzo alikuwa ametumia miaka thelathini na mitatu na nusu akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Ingawa alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia bonde la uvuli wa mauti, na ingawa amepitia kitendo cha kufufuka, Hakuwa amepitia mabadiliko yoyote katika kipengele chochote. Ingawa kwa sasa alikuwa na alama za misumari kwenye mwili Wake, na ingawa Alikuwa amefufuka na kutoka kaburini, tabia Yake, ufahamu Wake wa wanadamu na nia Zake kwa wanadamu bado zilikuwa hazijabadilika hata kidogo. Pia, Alikuwa akiwaambia watu kwamba Alikuwa ameshuka kutoka msalabani, Ameshinda dhambi, Ameshinda magumu, na Ameshinda kifo. Alama zile za misumari zilikuwa tu ushahidi wa ushindi wake dhidi ya Shetani, ushahidi wa kuwa sadaka ya dhambi ili kuweza kuwakomboa kwa ufanisi wanadamu wote. Alikuwa akiwaambia watu kwamba tayari Alikuwa amechukua dhambi za wanadamu na Alikuwa amekamilisha kazi Yake ya ukombozi. Aliporudi ili kuwaona wanafunzi Wake, Aliwaambia kwa kuonekana Kwake: “Mimi niko hai, bado Nipo; leo kwa kweli nasimama mbele yenu ili muweze kuniona na kunigusa Mimi. Siku zote nitakuwa nanyi.” Bwana Yesu alitaka pia kutumia mfano huo wa Tomaso kama onyo kwa watu wa siku za usoni: Ingawahuwezi kumwona wala kumgusa Bwana Yesu katika imani yako Kwake bado, unaweza kubarikiwa kutokana na imani yako ya kweli, na unaweza kumwona Bwana Yesu kupitia kwa imani yako ya kweli; na mtu wa aina hii amebarikiwa.
Maneno haya yaliyorekodiwa katika Biblia ambayo Bwana Yesu alizungumza Alipojitokeza kwa Tomaso ni msaada mkubwa kwa watu wote katika Enzi ya Neema. Kuonekana Kwake na maneno Yake kwa Tomaso yamekuwa na athari kubwa kwa vizazi vilivyofuata, na yatakuwa na umuhimu wa kudumu daima dawamu. Tomaso anawakilisha aina ya mtu anayemwamini Mungu ilhali anamshuku Mungu. Wana asili ya kushuku, wana mioyo isiyoeleweka, wao wenyewe ni wadanganyifu, na hawaamini mambo ambayo Mungu anaweza kukamilisha. Hawaamini katika uwezo wa Mungu na utawala Wake, na hawaamini katika Mungu mwenye mwili. Hata hivyo, kufufuka kwa Bwana Yesu kulikuwa ni sawa na kuzabwa kofi katika nyuso zao, na pia kuliwapa fursa ya kugundua mashaka yao wenyewe, kutambua kushuku kwao binafsi, na kuukubali usaliti wao binafsi na hivyo basi kuamini katika kuwepo na kufufuka kwa Bwana Yesu. Kile kilichomfanyikia Tomaso kilikuwa onyo na tahadhari kwa vizazi vijavyo ili watu wengi zaidi waweze kujitahadharisha na ili wasiwe wa kushuku kama Tomaso, na kama wangekuwa hivyo, wangezama katika giza. Ukimfuata Mungu, lakini kama Tomaso, siku zote unataka kuugusa ubavu wa Bwana na kuhisi alama Zake za msumari ili kuthibitisha, ili kuhakikisha, ili kukisia kama Mungu yupo au la, basi Mungu atakuacha. Hivyo basi, Bwana Yesu anawahitaji watu wasiwe kama Tomaso, kuamini tu kile wanachoweza kuona kwa macho yao wenyewe, lakini wawe watu safi, waaminifu, wasiwe na mashaka yoyote dhidi ya Mungu, lakini kumwamini tu na kumfuata Yeye. Mtu wa aina hii amebarikiwa. Hili ni hitaji dogo sana la Bwana Yesu kwa watu, na onyo kwa wafuasi Wake.
Huu ndio mtazamo wa Bwana Yesu kwa wale waliojaa mashaka. Hivyo basi ni nini ambacho Bwana Yesu aliwaambia, na ni nini Alichofanya kwa wale ambao wanaweza kuamini kwa uaminifu na kumfuata Yeye? Hiki ndicho tutakachokiangalia katika sehemu inayofuata, kuhusiana na kitu ambacho Bwana Yesu alimwambia Petro.
Katika mazungumzo haya, Bwana Yesu alimwuliza Petro mara kadhaa kuhusu jambo moja: “Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda?” Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi ambacho Bwana Yesu alihitaji kutoka kwa watu kama vile Petro baada ya kufufuka Kwake, watu wanaomwamini Kristo kwa kweli na kulenga kumpenda Bwana. Swali hili lilikuwa aina fulani ya uchunguzi, na aina fulani ya kuhoji, lakini hata zaidi lilikuwa hitaji na tarajio la watu kama Petro. Aliitumia mbinu hii ya kuuliza maswali ili watu waweze kujitafakari na kujiangalia katika maisha yao wenyewe: Je, mahitaji ya Bwana Yesu kwa watu ni yapi? Je, nampenda Bwana? Mimi ni mtu anayempenda Mungu? Nafaa vipi kumpenda Mungu? Hata ingawa Bwana Yesu aliuliza tu swali hili kwa Petro, ukweli ni kwamba katika moyo Wake, Alitaka kutumia fursa hii ya kumwuliza Petro ili kuuliza swali la aina hii kwa watu wengi zaidi wanaoutafuta kumpenda Mungu. Ni kwamba tu Petro alibarikiwa kuwa mwakilishi wa mtu wa aina hii, ili kupokea swali hilo kutoka kwa kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe.
Ikilinganishwa na maneno yafuatayo, ambayo Bwana Yesu alimwambia Tomaso baada ya kufufuka Kwake: “nyoosha mkono wako hapa, na uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye," na, Yeye kumwuliza Petro swali mara tatu: “Simioni, mwana wa Yohana, unanipenda mimi?” inawaruhusu watu kuweza kuhisi kwa njia bora zaidi ule uzito wa mtazamo wa Bwana Yesu na umuhimu Aliouhisi wakati huu wa kuuliza maswali hayo. Kuhusiana na Tomaso mwenye kushuku pamoja na asili yake ya udanganyifu, Bwana Yesu alimruhusu yeye kufikisha mkono wake na kuzigusa zile alama Zake za misumari, jambo ambalo lilimfanya yeye kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Mwana wa Adamu aliyefufuka na akatambua utambulisho wa Bwana Yesu kama Kristo. Na ingawa Bwana Yesu hakumkemea kwa ukali Tomaso, wala hakuonyesha kwa matamshi hukumu yoyote ilio wazi kwake, hata hivyo Alitumia njia ya vitendo ili kumjulisha Tomaso kwamba Alimwelewa, huku pia akionyesha mtazamo na uamuzi Wake kumwelekea mtu wa aina hiyo. Mahitaji na matarajio ya Bwana Yesu ya mtu wa aina hiyo hayawezi kuonekana kutokana na kile Alichosema. Kwa sababu watu kama Tomaso hawana katu imani ya ukweli. Mahitaji ya Bwana Yesu kwao yanafika mbali, lakini mtazamo Alioufichua kwa watu kama Petro ni tofauti kabisa. Hakuhitaji kwamba Petro aunyoshe mkono wake na kuzigusa hizo alama Zake za misumari, wala hakumwambia Petro: “usiwe asiyeamini, baliaaminiye.” Badala yake, Alimwuliza Petro kwa kurudia swali lilo hilo. Hili lilikuwa swali la kuchokonoa fikira, na lenye maana ambalo halina budi kumfanya kila mfuasi wa Kristo kuhisi majuto, na woga, lakini pia kuhisi ile hali ya moyo wa wasiwasi, na huzuni ya Bwana Yesu. Na wakati wakiwa katika maumivu na mateso makali, wanaweza kuelewa zaidi kujali kwa Bwana Yesu Kristo na utunzaji Wake; wanatambua mafundisho Yake ya dhati na mahitaji Yake madhubuti ya watu safi, na waaminifu. Swali la Bwana Yesu linawaruhusu watu kuhisi kwamba matarajio ya Bwana kwa watu yaliofichuliwa kupitia kwa maneno haya mepesi si ya kuamini tu na kumfuata Yeye, lakini kutimiza yote kwa kuwa na upendo, kumpenda Bwana wako, kumpenda Mungu wako. Upendo wa aina hii ni wa kujali na kujisalimisha. Ni wa wanadamu kuishi kwa ajili ya Mungu, kufa kwa ajili ya Mungu, kujitolea kila kitu chao kwa ajili ya Mungu, na kutumia na kutoa kila kitu chao kwa ajili ya Mungu. Upendo wa aina hii pia ni kumpa Mungu faraja, kumruhusu Yeye kufurahia ushuhuda, na kumruhusu Yeye kupumzika. Ni fidia ya wanadamu kwa Mungu, uwajibikaji wao, na wajibu wao, na ni njia ambayo wanadamu lazima wafuate kwa maisha yao yote. Haya maswali matatu yalikuwa mahitaji na ushawishi ambao Bwana Yesu alitoa kwa Petro na watu wote ambao wangefanywa kuwa wakamilifu. Maswali haya matatu ndiyo yaliyomwongoza na kumpa motisha Petro kukamilisha njia yake ya maisha, na yalikuwa maswali haya wakati ule wa Bwana Yesu kuondoka ambayo yalimfanya Petro kuanza njia yake ya kufanywa mkamilifu, na yaliyomwongoza, kwa sababu ya upendo wake kwa Bwana, kuujali moyo wa Bwana, kumtii Bwana, kumpa tulizo Bwana, na kuyatoa maisha yake yote na kila kitu chake chote kwa sababu ya upendo wake.
Katika Enzi ya Neema, kazi ya Mungu ilikuwa kimsingi ya aina mbili za watu. Wa kwanza alikuwa aina ya mtu aliyemwamini na kumfuata, ambaye angeweza kushika amri Zake na kuubeba msalaba, na ambaye angeweza kushikilia njia ya Enzi ya Neema. Mtu wa aina hii angepata baraka za Mungu na kufurahia neema ya Mungu. Mtu wa aina hii ya pili alikuwa kama Petro, mtu ambaye angeweza kufanywa kuwa mkamilifu. Hivyo basi, baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alifanya kwanza mambo haya mawili yenye umuhimu sana. La kwanza lilikuwa ni kwa Tomaso, na jingine lilikuwa kwa Petro. Mambo haya mawili yanawakilisha nini? Je, yanawakilisha nia za kweli za Mungu katika kuwaokoa binadamu? Je, yanawakilisha uaminifu wa Mungu kwa binadamu? Kazi Aliyoifanya na Tomaso ilikuwa ni kuwapa onyo watu wasiwe wanashuku, lakini kuamini tu. Kazi Aliyofanya na Petro ilikuwa ni kuipatia nguvu imani ya watu kama vile Petro, na kuweka wazi mahitaji ya aina hii ya watu, ili kuonyesha ni shabaha zipi wanafaa kuwa wakifuatilia.
Baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alionekana kwa watu Aliowaona kuwa muhimu, Akaongea na wao, na kuwapa wao mahitaji, huku akiacha nyuma nia Zake, na matarajio Yake kwa watu. Hivi ni kusema, Mungu mwenye mwili, kujali Kwake kwa wanadamu na matakwa Yake kwa watu hayakubadilika kamwe; haya yalibaki vilevile Alipokuwa katika mwili na Alipokuwa katika mwili Wake wa kiroho baada ya kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. Alijali kuwahusu wanafunzi hawa kabla ya kufika msalabani; ndani ya moyo Wake, Alikuwa wazi katika hali ya kila mmoja, Alielewa upungufu wa kila mmoja, na bila shaka ufahamu Wake wa kila mtu ulikuwa namna ile ile baada ya Yeye kufa, kufufuka, na kuwa mwili wa kiroho kama hali ilivyokuwa Alipokuwa katika mwili. Alijua kwamba watu hawakuwa na uhakika kabisa kuhusu utambulisho Wake kama Kristo, lakini katika kipindi Chake akiwa katika mwili Hakutoa matakwa makali kwa watu. Lakini baada ya kufufuka Alijitokeza kwao, na Akawafanya wawe na uhakika kabisa kwamba Bwana Yesu alikuwa amekuja kutoka kwa Mungu, kwamba Alikuwa Mungu mwenye mwili, na Alitumia ukweli wa kuonekana Kwake na kufufuka Kwake kama maono na motisha kubwa zaidi kwa muda mrefu katika ufuatiliaji wa wanadamu. Kufufuka kwake kutoka kwenye kifo hakukuwapa nguvu tu wale wote Waliomfuata, lakini pia kulitekeleza kikamilifu kazi Yake ya Enzi ya Neema miongoni mwa wanadamu, na hivyo injili ya wokovu wa Bwana Yesu katika Enzi ya Neema ilienea hatua kwa hatua katika kila pembe ya binadamu. Je, unaweza kusema kwamba kutokea kwa Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake kulikuwa na umuhimu wowote? Kama ungekuwa Tomaso au Petro wakati huo, na ukumbane na kitu hiki kimoja katika maisha yako ambacho kilikuwa na maana sana, ni athari ya aina gani ambayo kitu hicho kingekuwa nayo kwako? Je, ungeona hili kuwa ono bora na kuu zaidi la maisha yako katika kumwamini Mungu? Ungeona hali hii kama msukumo wako katika kumfuata Mungu, kujaribu kumridhisha Yeye, na kufuatilia kumpenda Mungu katika maisha yako yote? Je, ungeweza kutumia jitihada za maisha yako yote ili kueneza maono haya makubwa zaidi? Je, ungekubali kueneza wokovu wa Bwana Yesu kama agizo kutoka kwa Mungu? Ingawa hamjapitia haya, mifano miwili ya Tomaso na Petro tayari inatosha kwa watu wa sasa kupata ufahamu wa wazi kuhusu mapenzi ya Mungu na kumhusu Mungu. Inaweza kusemwa kwamba baada ya Mungu kuwa mwili, baada ya Yeye binafsi kupitia maisha miongoni mwa wanadamu na kupitia maisha ya wanadamu kibinafsi, na baada ya kuona upotovu wa wanadamu na hali ya maisha ya wanadamu kwa wakati huo, Mungu katika mwili alihisi kwa kina zaidi jinsi mwanadamu alikuwa asiyejiweza, mwenye masikitiko na wa kuonewa huruma. Mungu alipata huruma zaidi kwa hali ya binadamu kwa sababu ya ubinadamu Wake wakati akiishi katika mwili, kwa sababu ya silika Zake katika mwili. Hili lilimsababisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya wafuasi Wake. Haya pengine ni mambo ambayo huwezi kuyaelewa, lakini Naweza kufafanua wasiwasi na utunzaji wa Mungu katika mwili kwa kila mmoja wa wafuasi Wake kwa kutumia maneno mawili tu: “wasiwasi mkubwa. Hata ingawa neno hili linatokana na lugha ya binadamu, na hata ingawa ni ya kibinadamu sana, hata hivyo inaonyesha kwa kweli na kufafanua hisia za Mungu kwa wafuasi Wake. Na kuhusu wasiwasi mwingi wa Mungu kwa wanadamu, katika kipindi cha uzoefu wako utahisi hili polepole na kupata uelewa wake. Hata hivyo, hali hii inaweza kutimizwa tu kwa kuelewa kwa utaratibu tabia ya Mungu kwa msingi wa kufuatilia mabadiliko katika tabia yako wewe binafsi. Kuonekana kwa Bwana Yesu kulisababisha wasiwasi Wake mwingi kwa ajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na kubadilishwa na kupitishwa kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema, kwa uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kwa mara nyingine tena wapitie na kuhisi wasiwasi wa Mungu huku pia wakithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi. Kupitia kuonekana Kwake Aliimarisha imani ya watu wote, na kupitia kuonekana Kwake aliuthibitishia ulimwengu ukweli kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hali hii iliwapa wafuasi Wake uthibitisho wa milele, na kupitia kwa Kuonekana Kwake pia Aliweza kufungua awamu ya kazi Yake katika enzi mpya.
13. Yesu Ala Mkate na Kufafanua Maandiko Baada ya Kufufuka Kwake
Luka 24:30-32 Na ikatimia, alipokuwa akikaa na wao ili wale, aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa. Na macho yao yakafunguka, na wakamjua, na akatoweka wasimwone. Na wakaambiana, je, Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu sisi, wakati alipokuwa akituzungumzia njiani, na wakati alipotufungulia maandiko?
14. Wanafunzi Wampa Yesu Kipande cha Samaki wa Kuokwa Ale
Luka 24:36-43 Na wakati walipokuwa wakinena hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akasema kwao, Amani iwe kwenu ninyi. Lakini walikuwa na woga na hofu sana, na wakafikiri kwamba walikuwa wameona roho. Naye akawaambia, Mbona mnasumbuka? na mbona mashaka yanaibuka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe: Niguseni, na kuona; kwa sababu roho haina mwili na mifupa, jinsi mnavyoniona mimi nikiwa nayo. Na baada ya yeye kunena hayo, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. Na wakati walikuwa bado hawajaamini kwa furaha, na wakishangaa, akawaambia, Mnacho chakula chochote huku? Na wakampa kipande cha samaki wa kuokwa kwa asali. Na akakichukua, na kukila mbele yao.
Kisha, tutaangalia vifungu vya maandiko hapo juu. Kifungu cha kwanza ni simulizi ya Bwana Yesu akila mkate na kufafanua maandiko baada ya kufufuka kwake, na kifungu cha pili ni simulizi ya Bwana Yesu akila samaki wa kuokwa. Vifungu hivi viwili vinakusaidiaje kuijua tabia ya Mungu? Je, unaweza kuwaza ni picha ya aina gani unayopata kutoka katika ufafanuzi huu wa Bwana Yesu akila mkate na kisha kipande cha samaki aliyekaushwa? Je, unaweza kufikiria, kama Bwana Yesu angekuwa amesimama mbele yako akila mkate, unaweza kuhisi vipi? Au kama Angekuwa Akila pamoja nawe kwenye meza moja, huku Akila samaki kwa mkate na watu, ni hisia aina gani ambayo ungekuwa nayo wakati huo? Kama unahisi ungekuwa karibu sana na Bwana, kwamba yuko karibu sana na wewe, basi hisia yako ni sahihi. Haya ndiyo matokeo ambayo Bwana Yesu alitaka kuyaleta kwa kula mkate na samaki mbele ya watu waliokusanyika baada ya kufufuka Kwake. Kama Bwana Yesu angekuwa ameongea tu na watu baada ya kufufuka Kwake, kama wasingeweza kuhisi mwili na mifupa Yake, lakini badala yake wamhisi Yeye kuwa Roho asiyefikika, je, wangejisikiaje? Je, hawangekatishwa tamaa? Wakati wakiwa wamekata tamaa, je, watu hawangehisi wameachwa? Je, hawangehisi umbali kati yao na Bwana Yesu Kristo? Je, ni aina gani ya athari mbaya ambayo umbali huu ungeweza kujenga katika uhusiano wa watu na Mungu? Watu wangehisi woga bila shaka, kwamba wasingethubutu kumkaribia Yeye, na hivyo wangekuwa na mtazamo wa kumweka mbali kwa heshima. Kuanzia wakati huo na kuendelea, wangekatiza uhusiano wao wa karibu na Bwana Yesu Kristo, na kurudi katika uhusiano kati ya wanadamu na Mungu aliye juu mbinguni, kama ilivyokuwa kabla ya Enzi ya Neema. Mwili wa kiroho ambao watu wasingeweza kuugusa au kuuhisi ungesababisha ukomeshaji wa ukaribu wao na Mungu, na ungefanya ule uhusiano wa karibu—ulioanzishwa wakati Bwana Yesu Kristo akiwa katika mwili bila ya umbali wowote kati Yake yeye na binadamu—ukose kuwepo. Mambo pekee ambayo yalichochewa ndani ya watu na mwili wa kiroho yalikuwa ni hisia za woga, kukwepa, na kupigwa na butwaa. Hawangethubutu kumkaribia au kushiriki katika mazungumzo na Yeye, achilia mbali kumfuata, kumwamini, au kumtumainia Yeye. Mungu hakupenda kuiona hisia ya aina hii ambayo wanadamu walikuwa nayo kwake Yeye. Hakutaka kuwaona watu wakimwepuka Yeye au wakijiondoa Kwake yeye; Aliwataka tu watu kumwelewa Yeye, kumkaribia na kuwa familia Yake. Kama familia yako binafsi, watoto wako wangekuona lakini wasingekutambua wewe, na hawakuthubutu kukukaribia lakini siku zote walikuepuka wewe, kama usingeweza kupata ufahamu wao kwa kila kitu ulichokuwa umewafanyia, ungehisi vipi? Halingekuwa jambo la uchungu? Je, hungevunjika moyo? Hivyo hasa ndivyo Mungu anavyohisi wakati watu wanamwepuka. Hivyo basi, baada ya kufufuka Kwake, Bwana Yesu bado alijitokeza kwa watu katika umbo Lake la mwili na damu, na kula na kunywa pamoja nao. Mungu huwaona watu kama familia na Mungu pia anataka wanadamu wamwone kuwa Yeye ndiye aliye mpendwa zaidi kwao; ni kwa njia hii tu ndivyo Mungu anavyoweza kuwapata watu kwa kweli, na ndio watu wanavyoweza kumpenda na kumwabudu Mungu kwa kweli. Je, sasa mnaweza kuelewa nia Yangu katika kutoa vifungu hivi viwili kutoka katika maandiko pale ambapo Bwana Yesu anaula mkate na kuonyesha maandiko baada ya kufufuka Kwake, na wanafunzi wanampa kipande cha samaki aliyeokwa ili ale?
Inaweza kusemwa kwamba mfululizo wa mambo ambayo Bwana Yesu alisema na kufanya baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ya fikira njema, na kufanywa kwa nia njema. Mambo haya yalijaa huruma na hisia za kujali ambazo Mungu alikuwa nazo kwa wanadamu, na yamejaa pia upendo mkubwa na utunzaji wenye umakini Aliokuwa nao kwa ajili ya uhusiano wa karibu ambao Alikuwa Ameanzisha na wanadamu wakati Akiwa katika mwili. Hata zaidi, yalijawa na kumbukumbu zilizopita na shauku Aliyokuwa nayo kutokana na maisha Yake ya kula na kuishi miongoni mwa wafuasi Wake wakati akiwa katika mwili. Hivyo basi, Mungu hakuwataka watu kuhisi umbali kati ya Mungu na binadamu, wala Hakutaka wanadamu kuwa mbali na Mungu. Hata zaidi, Hakutaka wanadamu wahisi kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hakuwa tena Bwana ambaye alikuwa wa karibu na watu, kwamba Hakuwa pamoja tena na wanadamu kwa sababu Alirudi katika ulimwengu wa kiroho, alirudi kwa Baba ambaye watu wengi wasingeweza kumwona wala kumfikia. Hakutaka watu kuhisi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote katika hadhi kati Yake na wanadamu. Mungu anapowaona watu wanaotaka kumfuata lakini wanamweka katika umbali fulani, moyo Wake unapata maumivu kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba mioyo yao iko mbali sana na Yeye, inamaanisha kwamba itakuwa vigumu sana Kwake yeye kuweza kuipata mioyo yao. Hivyo basi kama angekuwa amejitokeza kwa watu kupitia kwa mwili wa kiroho ambao wasingeweza kuuona ama kuugusa, hali hii kwa mara nyingine tena ingeweza kumweka binadamu mbali na Mungu, na ingewasababisha wanadamu kumwona Kristo kimakosa baada ya kufufuka Kwake kuonekana kuwa Amegeuka kuwa Aliyetukuka, wa aina tofauti na wanadamu, na mtu ambaye asingeweza tena kushiriki mezani na kula pamoja na binadamu kwa sababu wanadamu ni wenye dhambi, wachafu, na hawawezi kumkaribia Mungu hata kidogo. Ili kuondoa kutoelewana huku kwa wanadamu, Bwana Yesu alifanya mambo kadha wa kadha ambayo mara kwa mara Alifanya katika mwili, kama ilivyorekodiwa katika Biblia, “aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaumega, na kuwapa.” Pia Aliwafafanulia maandiko, kama alivyokuwa akifanya hapo awali. Yote haya ambayo Bwana Yesu alifanya yalimfanya kila mmoja aliyemwona Yeye kuhisi kwamba Bwana hakuwa amebadililika, kwamba alikuwa bado ni Bwana Yesu yule yule. Hata ingawa Alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia kifo, Alikuwa amefufuka, na hakuwa amemwacha binadamu. Alikuwa amerudi kuwa miongoni mwa wanadamu, na kila kitu Chake hakikuwa kimebadilika. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele za watu alikuwa bado ni Bwana Yesu yule yule. Mwenendo Wake na mazungumzo Yake na watu yalikuwa ya kawaida sana. Alikuwa angali bado na huruma na upendo, neema, na uvumilivu—Alikuwa bado Bwana Yesu aliyewapenda wengine kama Alivyojipenda Mwenyewe, ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu mara sabini mara saba. Kama kawaida, Alikula na watu, Alijadili maandiko na wao, na hata muhimu zaidi, sawa tu na kama alivyofanya awali, Alifanywa kuwa mwili na damu na Aliweza kuguswa na kuonekana. Mwana wa Adamu katika njia hii aliwaruhusu watu kuhisi ukaribu, kuhisi kuwa watulivu, na kuhisi furaha ya kupata tena kitu ambacho kilikuwa kimepotea, na wao pia walihisi utulivu wa kutosha ya kuanza kumtegemea na kumtumainia Mwana huyu wa Adamu kwa ujasiri na kwa uhakika ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Walianza pia kuomba katika jina la Bwana Yesu bila ya kusita, kuomba ili kupokea neema Yake, baraka Zake, na kupokea amani na furaha kutoka Kwake, kupata utunzaji na ulinzi kutoka Kwake na wakaanza kuwaponya wagonjwa na kutoa mapepo kwa jina la Bwana Yesu.
Wakati ambao Bwana Yesu alifanya kazi katika mwili, wengi wa wafuasi Wake wasingeweza kuthibitisha kikamilifu utambulisho Wake na mambo Aliyoyasema. Wakati aliposulubishwa msalabani, mtazamo wa wafuasi Wake ulikuwa ule wa matarajio; kisha, tangu wakati Aliposulubishwa msalabani hadi Alipowekwa kaburini, mtazamo wa watu Kwake ulikuwa wa kukatishwa tamaa. Wakati huu, watu walikuwa tayari wameanza kubadili mioyo yao kutoka katika kushuku hadi kukataa mambo ambayo Bwana Yesu alikuwa amesema wakati Akiwa katika mwili. Na Alipotoka kaburini na kuwatokea watu mmoja baada ya mwingine, wengi wa watu ambao walikuwa wamemwona Yeye kwa macho yao au kusikia habari za kufufuka Kwake, walibadilika kwa utaratibu kutoka katika hali ya kumkana hadi ile ya nadharia ya kushuku. Kufikia muda ule ambao Bwana Yesu alimfanya Tomaso autie mkono wake ubavuni Mwake, na wakati Alipoumega mkate na kuula mbele ya umati wa watu baada ya kufufuka Kwake na kisha akala samaki wa kuokwa mbele yao, hapo tu ndipo walipokubali kwa kweli Bwana Yesu ni Kristo katika mwili. Mnaweza kusema kwamba ni kana kwamba mwili huu wa kiroho ulio na nyama na damu uliosimama mbele ya hao watu ulikuwa ukimuamsha kila mmoja wao kutoka katika ndoto. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Ndiye aliyekuwepo tangu miaka hiyo ya nyuma. Alikuwa na umbo, na mwili, na mifupa, na Alikuwa tayari ameishi na kula na wanadamu kwa muda mrefu…. Kwa wakati huu, watu walihisi kwamba uwepo Wake ulikuwa halisi, wa kushangaza sana; wote walichangamka na kufurahi mno, na wakati uo huo walijawa na hisia. Na kuonekana Kwake tena kuliwaruhusu watu waweze kuona kwa kweli unyenyekevu Wake, kuhisi ukaribu Wake na shauku Yake, upendo Wake kwa wanadamu. Muunganiko huu wa muda mfupi uliwafanya watu waliomwona Bwana Yesu kuhisi ni kana kwamba muda mrefu ulikuwa umepita. Mioyo yao iliyopotea, iliyochanganyikiwa, yenye hofu, yenye wasiwasi, yenye shauku na iliyokufa ganzi ilipata utulivu. Hawakuwa na shaka tena au kukata tamaa kwa sababu walihisi kwamba sasa kulikuwa na tumaini na kitu cha kutegemea. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Angekuwa nao milele, Angekuwa mnara wao thabiti, kimbilio lao la kila wakati.
Ingawa Bwana Yesu alifufuka, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi Alikuwa katika umbo gani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada. Bwana Yesu alitaka pia watu wajue kwamba, hawaishi peke yao katika ulimwengu huu. Mwanadamu ana utunzaji wa Mungu, Mungu yuko pamoja nao; watu siku zote wanaweza kumtegemea Mungu; Yeye ndiye familia ya kila mmoja wa wafuasi Wake. Akiwa na Mungu wa kumtegemea, mwanadamu hatawahi tena kuwa mpweke au bila usaidizi, na wale wanaomkubali kama sadaka yao ya dhambi hawatafungwa katika dhambi tena. Katika macho ya binadamu, sehemu hizi za kazi Zake ambazo Bwana Yesu alitekeleza baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ni mambo madogo sana lakini Ninavyoona Mimi, kila kitu kilikuwa na maana yenye thamani sana na zote zilikuwa zenye umuhimu na uzito.
Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa ukamilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu wanadamu kupitia kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa nyama na damu. Aliianza huduma Yake kwa kugeuka mwili na Alihitimisha huduma Yake kwa kujitokeza kwa wanadamu Akiwa katika umbo Lake la kimwili. Aliileta Enzi ya Neema, Aliianzisha Enzi ya Neema kupitia kwa utambulisho Wake kama Kristo. Kupitia utambulisho Wake kama Kristo, Alitekeleza kazi katika Enzi ya Neema na Aliimarisha na kuwaongoza wafuasi katika Enzi ya Neema. Inaweza kusemwa kuhusu kazi ya Mungu kwamba kwa kweli Anamaliza kile Anachokianzisha. Kuna hatua na mpango, na kazi imejaa hekima Yake, uweza Wake, matendo Yake ya ajabu, na pia imejaa upendo Wake na huruma Zake. Bila shaka, jambo kuu lililopo katika kazi yote ya Mungu ni utunzaji Wake kwa binadamu; umejawa na hisia Zake za kujali ambazo Hawezi kuweka pembeni. Katika aya hizi za Biblia, katika kila kitu ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake, kile kilichofichuliwa kilikuwa ni matumaini yasiyobadilika ya Mungu na kujali Kwake kwa wanadamu, pamoja na utunzaji wa Mungu wenye umakinifu na kuwathamini wanadamu. Hakuna hata moja kati ya haya ambayo yamewahi kubadilika hadi siku ya leo—je, unaweza kuona hili? Mnapoona hili, je, mioyo yenu haisogei karibu na Mungu bila kujua? Ikiwa uliishi katika enzi hiyo na Bwana Yesu akakutokea baada ya kufufuka Kwake katika umbo la kushikika ili uweze kumuona, na kama Angeketi mbele yako, Akala mkate na samaki na kukuchambulia wewe maandiko, Akaongea na wewe, basi ungehisi vipi? Ungehisi furaha? Je, ungehisi kuwa mwenye hatia? Hali za hapo awali za kutokumwelewa na kumuepuka Mungu, migongano na mashaka dhidi ya Mungu—hivi vyote havingetoweka tu? Je, unadhani kwamba uhusiano kati ya binadamu na Mungu ungekuwa bora zaidi?
Kupitia kwa ufasiri wa sura hizi chache za Biblia, je, umegundua kasoro zozote katika tabia ya Mungu? Je, umeona dosari yoyote katika upendo wa Mungu? Uliuona udanganyifu au uovu wowote katika uweza au hekima ya Mungu? Bila shaka la! Sasa unaweza kusema kwa uhakika kwamba Mungu ni mtakatifu? Je, unaweza kusema kwa uhakika kwamba hisia za Mungu zinafichua kiini Chake na tabia Yake kwa ujumla? Natumai kwamba baada ya kuyasoma maneno haya, kile ambacho umeelewa kutoka katika maneno haya kitakusaidia na kukunufaisha katika ufuatiliaji wako wa mabadiliko katika tabia na hali ya kumcha Mungu. Natumai pia kwamba maneno haya yataweza kukuzalia matunda ambayo yatakua kila siku, hivyo basi katika mchakato wa ufuatiliaji huu kukuleta karibu na Mungu zaidi na zaidi, wa kukuleta karibu na karibu zaidi na kiwango ambacho Mungu anahitaji, ili usichoke tena na ufuatiliaji wa ukweli na usihisi tena kwamba ufuataji wa ukweli na ule wa mabadiliko katika tabia ni usumbufu au jambo la ziada. Badala yake, ukichochewa na, udhihirisho wa tabia ya kweli ya Mungu na kiini kitakatifu cha Mungu ambayo yanakupa motisha kutamani mwangaza, kutamani haki, na kuazimia kufuatilia ukweli, kufuatilia kutimiza mapenzi ya Mungu, na kuwa binadamu anayepatwa na Mungu, na kuwa mtu halisi.
Leo tumezungumzia baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya katika Enzi ya Neema wakati ambapo Alikuwa mwili kwa mara ya kwanza. Kutoka kwa mambo haya, tumeona tabia ambayo Alionyesha na kuifichua katika mwili, pamoja na kila kipengele cha kile Anacho na Alicho. Vipengele hivi vyote vya kile ambacho Anacho na Alicho vinaonekana kuwa vya kibinadamu sana, lakini ukweli ni kwamba kiini cha kila Alichofichua na kuonyesha hakiwezi kutenganishwa na tabia Yake mwenyewe. Kila mbinu na kila kipengele cha Mungu mwenye mwili kinachoonyesha tabia Yake katika ubinadamu kimeunganishwa bila kutenganishwa katika kiini Chake Mwenyewe. Hivyo, ni muhimu sana kwamba Mungu alikuja kwa wanadamu kwa njia ya kuwa mwili na kazi aliyofanya katika mwili ni muhimu sana pia. Na, tabia Aliyoifichua na nia Alizozionyesha ni muhimu hata zaidi kwa kila mtu anayeishi katika mwili, kwa kila mtu anayeishi katika upotovu. Je, hili ni jambo ambalo unaweza kuelewa? Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, je, umefanya hitimisho lolote kuhusu jinsi unavyopaswa kumtendea? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili uufanye, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili ya Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anakufanyia, kile Anachopanga kwa ajili yako, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi. Hayo ndiyo yote ya kushiriki kwa siku ya leo.
Novemba 23, 2013
Tanbihi:
a. “Laana ya kukaza na mshipi” ni laana inayotumiwa na mtawa Tang Sanzang katika riwaya ya Kichina iitwayo Safari kwenda Magharibi. Anatumia laana hii kumdhibiti Sun Wukong kwa kukaza mshipi wa chuma kwenye kichwa chake, ukimpa maumivu makali ya kichwa, na hivyo kumdhibiti. Imekuwa istiara ya kuelezea kitu kinachomfunga mtu.
b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.