Ingawa Mungu Amejificha Kutoka kwa Mwanadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

01/03/2021

Ingawa Mungu Amejificha Kutoka kwa Mwanadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, na sembuse yeye kuipitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliokuwa nao wakati wa majaribu unashuhudiwa na kila mmoja, na unapendwa, unafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wanayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na hata zaidi ya hayo, wanaimba sifa zao. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo mbalimbali ya maisha yake isiyo ya ajabu, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu kuliko mtu yeyote mwingine. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakuwa sanasana yenye ushupavu, wala, aidha, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole na unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea, haki, na iliyopenda mambo chanya—hakuna kati ya mambo haya yanayomilikiwa na watu wengi wa kawaida. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwangalifu sana katika kufikiria kwake. Hivyo, wakati wake usio wa ajabu duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na aliuona ukubwa, utakatifu, na kuwa na haki kwa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na aliuona utukufu na mamlaka ya Mungu mkuu zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu aweze kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa kwamba alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu na mtimilifu, na wa kuwa mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na aliyejiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuatilia mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawa alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo kwazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawa alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuza binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawa miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu kutokuwa wa ajabu kwa maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Machoni pake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Hakuwa amemwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa ajabu duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu havikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala havikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi, katika maisha yake ya kila siku, wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye Amejificha miongoni mwa mambo yote. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti ya moyo wa Mungu na maneno ya Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote lakini anaonyesha sauti ya moyo Wake na maneno kwa kutawala sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule ufahamu na maarifa sawa kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu hakuwa amemwonekania Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kumwonekania au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote yanatosha kwa mwanadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo, nguvu na mamlaka ya Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu yanatosha kumfanya mwanadamu afuate njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu mwanadamu wa kawaida kama vile Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi kila mtu wa kawaida anayemfuata Mungu anafaa pia kuweza kufanya hivyo. Ingawa maneno haya yanaweza kusikika kana kwamba ni hitimisho la kimantiki, hili halikiuki sheria ya mambo. Bado ukweli haujalingana na matarajio: Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, kunaweza kuonekana, ni hifadhi ya Ayubu na Ayubu pekee. Kwa kutaja “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu,” watu hufikiri kwamba hii inafaa tu kufanywa na Ayubu, ni kana kwamba njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ilikuwa imebandikwa jina la Ayubu na haikuhusiana na watu wengine. Sababu ya hili ni wazi: Kwa sababu Ayubu tu ndiye aliyemiliki hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na iliyopenda kutopendelea na haki na mambo yaliyokuwa mazuri, hivyo ni Ayubu tu ambaye angeweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima nyinyi nyote muwe mmeelewa matokeo hapa—kwa sababu hakuna yule anayemiliki ubinadamu ulio na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na ule ambao unapenda kutopendelea na haki na ule ambao ni mzuri, hakuna mtu anayeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na hivyo watu hawawezi kamwe kupata furaha ya Mungu au kusimama imara katikati ya majaribu. Hii pia inamaanisha kwamba, bila kujumuisha Ayubu, watu wote wangali wamefungwa na kutegwa na Shetani; wote wanashtakiwa, wanashambuliwa, na kudhulumiwa na yeye. Wao ndio wale ambao Shetani anajaribu kumeza, na wote hawana uhuru, ni wafungwa ambao wametekwa nyara na Shetani.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Ayubu (Sehemu 1)

Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe,...

Kuhusu Ayubu (Sehemu 2)

Urazini wa Ayubu Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp