Bibilia inasema: “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” (Warumi 10:10). Tunaamini kwamba Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wenye haki kupitia imani. Aidha, tunaamini kwamba mtu akiokolewa mara moja, basi ameokolewa milele, na Bwana atakaporudi tutanyakuliwa na tutaingia katika katika ufalme wa mbinguni. Hivyo kwa nini unashuhudia kuwa tunapaswa kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kabla ya kuweza kuokolewa na kuletwa katika ufalme wa mbinguni?

07/06/2019

Jibu:

Waumini wote katika Bwana hufikiria: Bwana Yesu alitukomboa Alipokufa msalabani, hivyo tayari tumeondolewa dhambi zote. Bwana hatuoni tena kama wenye dhambi. Tumekuwa wenye haki kupitia kwa imani yetu. Mradi tuvumilie hadi mwisho, tutaokolewa. Bwana atakaporudi tutanyakuliwa moja kwa moja kuingia katika ufalme wa mbinguni. Naam, huo ndio ukweli? Je, Mungu aliwahi kamwe kutoa ushahidi katika maneno Yake wa kuunga mkono madai haya? Kama mtazamo huu hauambatani na ukweli, matokeo yatakuwa ni yapi? Sisi ambao tunamwamini Bwana tunapaswa kutumia maneno Yake mwenyewe kama msingi wa mambo yote. Hili hasa ni kweli ikizingatiwa swali la jinsi ya kushughulikia kurudi kwa Bwana. Hatuwezi kushughulikia kurudi Kwake katika hali yoyote kulingana na fikra na mawazo ya mwanadamu. Matokeo ya tabia kama hiyo ni makali sana hata kuyafikiria. Ni sawa na wakati Mafarisayo walipomsulubisha Bwana Yesu msalabani huku wakimsubiri Masiha aje. Matokeo yangekuwa ni yapi? Bwana Yesu amekamilisha kazi ya kumkomboa mwanadamu. Hilo ni kweli, lakini je, kazi ya Mungu ya wokovu wa mwanadamu imekamilika? Je, hilo linamaanisha kuwa sisi wote waumini katika Bwana Yesu tuna sifa za kunyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni? Hakuna yeyote ajuaye jibu la swali hili. Mungu aliwahi kusema wakati mmoja mmoja, “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21), “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). Kulingana na maneno ya Mungu, tunaweza kuwa na uhakika kuwa wale wanaoingia katika ufalme wa mbinguni wamejiweka huru kutoka kwa dhambi na wametakaswa. Wao ndio hufanya mapenzi ya mungu, humtii Mungu, humpenda Mungu, na humheshimu. Kwa sababu Mungu ni mtakatifu na wale watakaoingia katika ufalme wa mbinguni wataishi pamoja na Yeye, ikiwa hatujatakaswa tunawezaje kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni! Kwa hivyo, dhana yetu kuwa sisi waumini tumeondolewa dhambi na tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni ni kutoelewa kabisa mapenzi ya Mungu. Ilitokana na mawazo ya wanadamu; ni fikra za kibinadamu. Bwana Yesu alituondolea dhambi; hilo ni kweli. Hata hivyo, Bwana Yesu hakuwahi kamwe kusema kuwa tumetakaswa kikamilifu kupitia kuondolewa huku kwa dhambi na sasa ni wenye kustahiki kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hakuna anayeweza kukataa ukweli huu. Basi ni kwa nini waumini wote hufikiri kuwa kila mmoja ambaye ameondolewa dhambi anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni? Wao hutumia nini kama ushahidi? Wao huungaje mkono madai haya? Watu wengi husema kuwa wao hutumia maneno ya Paulo na wanafunzi wengine kama msingi wa imani hii, kama ilivyoandikwa katika Biblia. Naam basi, hebu nikuulize, je, maneno ya Paulo na wanafunzi wengine yanawakilisha maneno ya Bwana Yesu? Je, yanawakilisha maneno ya Roho Mtakatifu? Maneno ya mwanadamu yanaweza kuwa katika Biblia, lakini, je, hili linaamnisha kuwa ni maneno ya Mungu? Kuna ukweli mmoja ambao tunaweza kuona wazi kutoka kwa Biblia: Watu ambao husifiwa na Mungu wanaweza kusikiliza sauti Yake na kutii kazi Yake. Wao ndio ambao hufuata njia Yake, ndio wenye kustahiki kuridhi kile ambacho Mungu aliahidi. Huu ni ukweli ambao hakuna yeyote anaweza kuukana. Sote tunajua kuwa hata ingawa dhambi zetu sisi waumini zimesamehewa, bado hatujatakaswa; bado tunatenda dhambi na kumpinga Mungu mara kwa mara. Mungu alituambia wazi, “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45), “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Kutokana na maneno ya Mungu, tunaweza kuwa na uhakika kuwa sio wote ambao dhambi zao zimesamehewa ni wenye kustahiki kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ni lazima watu watakaswe; ni lazima wawe watendaji wa mapenzi ya Mungu kabla ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Huu ni ukweli usioweza kukataliwa. Inaonekana kuwa kuelewa mapenzi ya Mungu sio rahisi kadri inavyoonekana. Hatutakaswi tu kwa sababu dhambi zetu zimesamehewa. Ni lazima kwanza tupokee uhalisi fulani wa ukweli na tupate sifa za Mungu. Basi tutakuwa wenye kutastahiki kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kama hatupendi ukweli na hakika umetuchosha na hata tunauchukia, ikiwa tutafuatilia tuzo na taji pekee lakini hatujali mapenzi ya Mungu, sembuse kusema kufanya mapenzi ya Mungu, je, hatufanyi maovu? Je, Bwana humsifu mtu wa aina hii? Ikiwa ni hivyo, sisi ni kama tu hao Mafarisayo wanafiki: Hata ingawa tumesamehewa dhambi, bado hatuwezi kuingia katika ufalme wa mbinguni. Huu ni ukweli usiopingika.

Bibilia inasema: “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” <span class=(Warumi 10:10). Tunaamini kwamba Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wenye haki kupitia imani. Aidha, tunaamini kwamba mtu akiokolewa mara moja, basi ameokolewa milele, na Bwana atakaporudi tutanyakuliwa na tutaingia katika katika ufalme wa mbinguni. Hivyo kwa nini unashuhudia kuwa tunapaswa kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kabla ya kuweza kuokolewa na kuletwa katika ufalme wa mbinguni?" width="615" height="346" class="aligncenter size-full wp-image-35427" />

Hebu tuendelee na ushirika. Bwana Yesu alituondolea dhambi zetu zote. Ni “dhambi” gani Alizotuondolea? Ni aina gani za dhambi ambazo tunakiri baada ya kuanza kumwamini Bwana? Dhambi kuu zinazorejelewa ni zile dhambi za jambo la hakika zinazosaliti sheria, amri, au maneno ya Mungu. Sisi wanadamu tulisaliti sheria na amri za Mungu na hivyo tutalaaniwa na kuadhibiwa na sheria Yake. Hiyo ndiyo maana Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake ya ukombozi. Hivyo, tunahitaji tu kuomba kwa Bwana Yesu na kukiri na kutubu dhambi zetu na Atatuondolea. Baada ya hapo, hatutalaaniwa na kuadhibiwa tena kulingana na sheria Yake. Mungu hatatushughulikia tena kama wenye dhambi. Hivyo tunaweza kuomba moja kwa moja kwa Mungu; tunaweza kumlilia Mungu na kushiriki neema na ukweli Wake tele. Hii ndiyo maana ya kweli ya “wokovu” ambayo mara nyingi tunazungumzia katika Enzi ya Neema. “Wokovu” huu hauhusiani hata kidogo na kutakaswa na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Unaweza kusema kuwa hayo ni mambo mawili tofauti, kwa sababu Bwana Yesu hakuwahi kamwe kusema kuwa wote ambao wameokolewa na kuondolewa dhambi wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hebu tusome baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, “Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)). “Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. … Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Maneno ya Mwenyezi Mungu yanajibu swali hili kwa uwazi sana. Punde tu tunapoyasikia, tunayaelewa. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya tu kazi Yake ya ukombozi ili kuwaondolea wanadamu dhambi, Akiwafanya kuwa wenye haki kupitia kwa imani na waliokolewa kupitia kwa imani. Hata hivyo, Bwana Yesu hakuwahi kamwe kusema kuwa kila mmoja ambaye amesamehewa dhambi anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hii ni kwa sababu Bwana Yesu anaweza kuwa Alituondolea dhambi zetu zote, lakini Hakuwahi kamwe kutuondolea asili zetu za kishetani. Kiburi chetu cha ndani, ubinafsi, udanganyifu, uovu n.k., yaani, tabia zetu mbovu, bado zipo. Mambo haya ni ya kina kuliko dhambi. Ni magumu zaidi kusuluhisha. Ikiwa asili za kishetani na tabia potovu, ambazo zinampinga Mungu sana, hazijasuluhishwa, hatuna budi ila kutenda dhambi nyingi. Tunaweza hata kutenda dhambi ambazo ni mbaya zaidi kushinda kuvunja sheria, yaani dhambi mbaya kupita kiasi. Ni kwa nini Mafarisayo waliweza kumlaani na kumpinga Bwana Yesu? Waliwezaje kumsulubisha msalabani? Hii inathibitisha kuwa ikiwa asili ya mwanadamu ya kishetani haijasuluhishwa mwanadamu anaweza kutenda dhambi bado, kumpinga Mungu, na kumsaliti Mungu.

Tumemwamini Bwana kwa hii miaka yote na kushuhudia kitu kimoja sisi wenyewe, kuwa, ingawa dhambi zetu zimeondolewa, bado hatuwezi kujizuia kufanya dhambi mara kwa mara. Bado tunadanganya, tunahadaa, kusema uwongo na kutumia hila ili kupata umaarufu na cheo. Hata tunakwepa majukumu na kuwatia watu wengine mashakani kwa ajili yetu wenyewe. Tunapokumbana na majanga ya asili na yanayosababishwa na mwanadamu, au majaribu na dhiki, tunamlaumu Mungu na kumsaliti. Wakati kazi ya Mungu haiambatani na fikra zetu wenyewe, tunamkana, kumhukumu, na kumpinga Mungu. Ingawa tunaamini katika jina la Mungu, badi tunaheshimu na kufuata wanadamu wengine. Ikiwa tuna vyeo, tunainua na kujishuhudia sisi wenyewe, kama tu makuhani wakuu waandishi, na Mafarisayo. Tunatenda kama sisi ni Mungu ili kujaribu na kuwafanya watu watuche na kututamani. Hata tunaiba na kujichukulia sadaka za Mungu. Tunakuwa na kiburi na kufuata mambo tunayopenda na mapenzi ya miili na hisia zetu. Tunasimamisha bendera zetu wenyewe, kuunda vikundi vyetu wenyewe na kuanzisha falme zetu ndogo wenyewe. Huu wote ni ukweli wazi. Tunaweza kuona kuwa ikiwa asili na tabia zetu za kishetani hazisuluhishwi, hatutaweza kustahiki kuingia katika ufalme wa mbinguni hata ingawa dhambi zetu zimesamehewa mara milioni. Ukweli kwamba bado tunaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu ni ishara kwamba bado tunamilikiwa na Shetani, ni adui wa Mungu, na bila shaka tutalaaniwa na kuadhibiwa na Yeye. Ni kama vile tu inavyosema katika Biblia, “Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi, lakini kuitafuta kwa hofu hukumu na uchungu mkali, ambao utawala maadui(Waebrania 10:26-27). Hebu tusome maneno zaidi ya Mwenyezi Mungu: “Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho). Kama unavyoona, tumekombolewa tu na Bwana Yesu lakini bado tunaishi katika tabia yetu ya kishetani, tukitenda dhambi na kumpinga Mungu mara kwa mara. Ni lazima tupitie hukumu na utakaso wa Mungu katika siku za mwisho ili tuwe huru kabisa kutoka kwa dhambi na tuupendeze moyo Wake. Kisha tutaweza kustahiki kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hakika, Bwana Yesu aliwahi kusema mara moja, “Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia(Yohana 14:2-3). Bwana alienda kutuandalia mahali na baada ya kutuandalia mahali, Atarudi kutupokea. Kwa kweli, huku “kutupokea” kunarejelea mipango Yake kwa ajili yetu ya kuzaliwa upya katika siku za mwisho. Bwana atakaporudi kufanya kazi Yake, Atatuleta mbele ya kiti Chake cha enzi ili tuhukumiwe, tutakaswe, na kufanywa kamili kwa maneno ya Mungu. Atatufanya washindi kabla ya majanga kufika. Mchakato wa kutupokea Kwake hakika ni jinsi Atatutakasa na kutufanya kamili. Sasa Bwana amekuja duniani kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Tumenyakuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi ili kuishi pamoja na Yeye. Je, hili si linatimiza kabisa unabii wa Bwana kuja kutupokea? Baada ya majanga makubwa kuisha, ufalme wa Kristo utaanzishwa duniani. Wale wote watakoendelea kuishi baada ya usafishaji wa majanga makubwa watakuwa na nafasi katika ufalme wa mbinguni.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ingawa dhambi zetu zimesamehewa kwa kumwamini Bwana, na tunahesabiwa kama waliookolewa, lakini kwa kweli, tunasalia wachafu na waliopotoshwa na hatujaepuka dhambi ili tupate usafi. Kusamehewa dhambi kunamaanisha tu kutohukumiwa na sheria. Hii ndiyo maana hasa ya “kuokolewa na neema.” Mungu anaweza kuwa amesamehe dhambi zetu na kutupa baraka nyingi, na kuturuhusu tufurahie amani na furaha ya kusamehewa dhambi zetu, na kutupa haki ya kumwomba Mungu na kuzungumza na kuwasiliana na Mungu, lakini kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu haiishii hapo. Kwa maneno mengine, kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu ni kuifungua tu njia ya kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Bila ukombozi wa Bwana Yesu, tusingestahili kumwomba Mungu na kupokea wokovu wa Mungu. Tunapaswa kujua hili. Inakuwaje kwamba hata baada ya dhambi zetu kusamehewa kwa kumwamini Bwana hatuwezi kujidhibiti na mara nyingi tunatenda dhambi, na hatuwezi kujinasua kutoka kwa kuishi kwa dhambi? Ni kwa sababu kupotoshwa kwetu na Shetani kumekolea sana, kwa kiasi kwamba sote tuna asili ya kishetani na tumejawa na tabia ya shetani. Ndiyo sababu hatuwezi kujizuia ila kutenda dhambi mara nyingi. Ikiwa hali hii ya kishetani haitatuliwa, bado tunaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu hata kama dhambi zetu zimesamehewa. Kwa njia hiyo, hatutaweza kamwe kufikia utangamano na Mungu. Ndiyo maana Bwana Yesu alisema lazima Arudi. Ni ili atekeleze kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho ili kuwatakasa kabisa na kuwaokoa wanadamu. Kama Mwenyezi Mungu anavyosema, “Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. … Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Maneno ya Mwenyezi Mungu ni wazi sana: Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya tu kazi Yake ya ukombozi. Dhambi za wanadamu zilisamehewa kwa kumwamini Bwana, lakini asili yao ya dhambi haijatatuliwa. Asili ya dhambi ya binadamu ni asili ya Shetani. Tayari imekita mizizi ndani ya mwanadamu, kuwa maisha ya mwanadamu. Ndiyo sababu mtu bado hana budi ila kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Mwanadamu kuwa na asili ya kishetani ni sababu ya msingi wa upinzani wake wa Mungu. Dhambi za mwanadamu zinaweza kusamehewa, lakini Mungu anaweza kusamehe asili yake ya kishetani? Asili ya kishetani inampinga Mungu na ukweli kwa uwazi. Mungu hawezi kamwe kuisamehe. Kwa hiyo, Mungu lazima awaokoe kabisa watu kutoka katika utumwa na udhibiti wa asili ya kishetani, na lazima awahukumu na awaadibu wanadamu. Hukumu na kuadibiwa na Mungu katika siku za mwisho ni kazi inayolenga asili na tabia ya Shetani ndani yetu. Watu wengine wanaweza kuuliza, Je, asili yetu ya kishetani inaweza tu kutatuliwa kwa hukumu na kuadibu? Je, hatuwezi, kwa kulipa gharama ya mateso, kushinda miili yetu, na kujizuia wenyewe kwa hiari, kutatua asili yetu ya kishetani? Hakika haiwezekani. Isingekuwa kwa ajili ya Mungu kuonyesha ukweli na kuhukumu na kufichua asili na kiini cha mwanadamu, hakuna mtu ambaye angeweza kujua ni nini hasa asili ya wanadamu wapotovu. Hebu tuangalie tena watakatifu wengi katika historia ambao wote walilipa gharama ya mateso na kushinda miili yao, ambao wote walitaka kuepuka utumwa na udhibiti wa dhambi, na kushinda mwili. Lakini ni nani kati yao aliyeweza kumshinda Shetani kuwa mtu ambaye anamtii Mungu kweli? Karibia hakuna. Hata kama kulikuwapo, walikuwa watu ambao Mungu aliwafanya kamilifu hasa. Lakini watu wangapi kama hao walikuwako? Ilikuwa kwa sababu hakuna hukumu na kuadibiwa na Mungu, hivyo tabia ya mwanadamu ya kishetani haikuweza kutakaswa. Tabia ya mwanadamu ya maisha basi haikuweza kubadilika. Ukweli huu unatosha kuthibitisha kwamba kutumia njia za kibinadamu hakuwezi kutatua tabia ya kishetani ya binadamu. Mwanadamu lazima apitie hukumu ya Mungu na kuadibiwa, kupogolewa na kushughulikiwa, na majaribio na kusafishwa, kabla ya kupata ukweli na uzima, kupokea njia ya uzima wa milele. Ni hivyo tu ndivyo tabia ya mwanadamu ya kishetani inaweza kutatuliwa kabisa. Ndiyo sababu, juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, Mwenyezi Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho, ili kuwaokoa kabisa wanadamu kutoka kwa utumwa na udhibiti wa asili ya kishetani, ili binadamu waweze kutakaswa ili wapate wokovu wa Mungu na kupatikana na Mungu. Kutokana na hili tunaweza kuona kuwa ni hukumu ya Mungu na kuadibiwa katika siku za mwisho ndiyo humsafisha kabisa na kumwokoa mwanadamu. Huu ni kweli.

Kwa nini Mungu anafanya kazi ya kuhukumu na kuadibu jamii ya wanadamu iliyopotoka katika siku za mwisho? Ili kuelewa jambo hili, lazima tujue kwamba Mungu haiokoi jamii ya wanadamu kikamilifu kwa hatua moja au mbili tu za kazi. Badala yake, linafanyika kupitia hatua tatu za kazi: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme. Ni hatua hizi tatu za kazi tu ndizo zinazoweza kuwaokoa wanadamu kabisa kutoka katika umiliki wa Shetani, na hizi tu ndizo zinazojumuisha kazi yote ya Mungu kuwaokoa binadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na amri ili kuongoza mwanadamu katika maisha yake duniani, na kupitia kwa hizi, wanadamu wangeweza kujua ni aina gani ya watu Mungu anawabariki, ni watu wa aina gani Mungu anawalaani, na vile vile kujua nini ni chenye haki na nini ni chenye dhambi. Hata hivyo, wakati wa hatua za baadaye za Enzi za Sheria, watu wote walikuwa wanaishi katika dhambi kwa sababu jamii ya wanadamu ilikuwa imepotoshwa zaidi na zaidi na Shetani. Hawakuweza kufuata sheria na walikabiliwa na hatari ya kutiwa hatiani na kulaaniwa na sheria hizi. Hiyo ndiyo sababu Bwana Yesu wa Enzi ya Neema alikuja kufanya kazi ya ukombozi akimruhusu mwanadamu kukiri dhambi zake, kutubu na kusamehewa dhambi hizo, hivyo kumwondoa mwanadamu kutokana na kuhukumiwa na kulaaniwa kupitia kwa sheria na kumruhusu awe na sifa zinazostahili kuja mbele ya Mungu na kuomba, kuwasiliana kwa karibu na Mungu, na kufurahia neema na ukweli Wake mwingi. Hii ndiyo maana ya kweli ya “kuokolewa.” Hata hivyo, Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu tu; Hakusamehe asili yetu ya dhambi au tabia yetu ya kishetani. Asili yetu ya kishetani bado ipo. Tuliendelea kuwepo katika mzunguko mbaya wa kutenda dhambi, kukiri na kisha kutenda dhambi tena bila njia ya kuwa huru kutoka katika vikwazo na udhibiti wa asili yetu ya dhambi. Tulimwita Mungu kwa uchungu, “Kwa kweli nateseka! Nawezaje kuwa huru kutoka katika vikwazo na udhibiti wa dhambi?” Hili ni tukio, kuelewa ambako sisi sote tunashiriki kama waumini katika Bwana. Hata hivyo, sisi hatuwezi kutatua asili yetu ya dhambi wenyewe. Hakuna binadamu anayeweza kufanya kazi ya kuokoa jamii ya wanadamu. Mungu Muumba ndiye anayeweza kuwaokoa wanadamu na kutukomboa kutoka kwa Shetani na dhambi. Yeye pekee ndiye anayeweza kutuokoa kutoka katika umiliki wa Shetani. Mwenyezi Mungu anasema: “Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu). Mungu ni mwaminifu. Kwa kuwa Mungu anamwokoa mwanadamu, Atafanya hili kikamilifu. Bila shaka Hataachia katikati. Hiyo ndiyo sababu Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu katika siku za mwisho ili kuwaokoa wanadamu kabisa. Anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu ili kutatua kabisa tatizo la asili ya kishetani na tabia ya kishetani ya wanadamu. Anafanya hili ili binadamu waweze kuwa huru kutoka katika dhambi, wapate wokovu, na wapatwe na Mungu. Kazi ya hukumu ambayo Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anaifanya ndiyo hasa wanayohitaji wanadamu waliopotoka, na pia ndiyo hatua muhimu ya kazi ambayo lazima itekelezwe na Mungu ili kuwaokoa wanadamu. Hii inatimiza unabii wa Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). “Roho wa ukweli” linamaanisha Mungu kupata mwili wa binadamu katika siku za mwisho, akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu. Kila tunachohitaji kufanya ni kukubali na kutii kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho ili tuweze kupata wokovu na kupatwa na Mungu. Hiki ni kitu ambacho wale wote ambao kweli wamepitia kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho wanaweza kuthibitisha.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp