Biblia ni kanuni ya Ukristo na wale wanaomwamini Bwana wamefanya hivyo kwa mujibu wa Biblia kwa miaka elfu mbili. Aidha, watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanaamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana, imani hiyo katika Bwana ni imani katika Biblia, na imani katika Biblia ni imani katika Bwana, na kwamba mtu akipotea kutoka kwa Biblia basi hawezi kuitwa muumini. Tafadhali hebu niulize kama kumwamini Bwana kwa njia hii au la kunakubaliana na mapenzi ya Bwana?
Jibu:
Wengi wanaamini kuwa Biblia inamwakilisha Bwana, inamwakilisha Mungu na kwamba imani katika Bwana inamaanisha imani katika Biblia, imani katika Biblia ni sawa na imani katika Bwana. Watu wanaweka hali sawa kwa Biblia kama wanavyofanya kwa Mungu. Kuna pia wale ambao wanatambua Biblia bila kumtambua Mungu. Wanaichukulia Biblia kama kuu, na hata kujitahidi kuifanya Biblia ichukue nafasi ya Mungu. Kuna hata viongozi wa kidini ambao wanatambua Biblia bila kumtambua Kristo, na kudai kuwa wale wanaohubiri kurejea kwa mara ya pili kwa Bwana kuwa waasi wa dini. Ni nini hasa ndio suala hapa? Ni dhahiri, dunia ya kidini imezama hadi kiwango cha kuitambua Biblia pekee na kukosa kuamini katika kurejea kwa Bwana—hakuna kuwaokoa wao. Kutoka hapa ni wazi, dunia ya kidini imekuwa kikundi cha wapinga Kristo, wakimpinga Mungu na kumchukua Mungu kama adui wao. Haiwezi kukataliwa kuwa viongozi wengi wa kidini ni Mafarisayo wanafiki. Hasa wale wanaodai kuwa “wale wanaohubiri kurudi kwa Bwana mara ya pili ni waasi wa dini,” wote ni wapinga Kristo na wasioamini. Inaonekana watu wengi hawajui imani hasa katika Bwana ni nini. Wanaita kuamini kwao katika Mungu asiye dhahiri kuwa imani halisi na hata kuamini katika Biblia badala ya Mungu. Hata wanamkataa na kumlaani Kristo mwenye mwili wa siku za mwisho. Wanapuuza na kuuacha ukweli wowote ambao Kristo anaeleza. Shida ni nini hapa? Ni swali la kina sana! Ni lenye kustahili kutafakari. Katika siku za awali wakati Yesu alifanya kazi Yake, je, Wayahudi hawakutenda katika njia hiyo hiyo? Kabla Kristo kutokea kuifanya kazi Yake, mwanadamu aliweka imani yake yote kwa Mungu katika Biblia. Hakuna ambaye angeweza kusema imani ya nani ni kweli na ya nani ni uongo, na kwa hakika hakuna angeweza kusema nani alikuwa anamtii Mungu kweli na nani aliyekuwa anampinga Yeye. Mbona ilikuwa kwamba wakati Bwana Yesu Kristo alikuwa mwili na kufanya kazi Yake, kila aina ya mwanadamu alifichuliwa? Hapa ndipo uenyezi wote na busara ya Mungu ipo. Wakati Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, Anatokea na kufanya kazi Yake, wanawali wenye busara wanasikia sauti Yake na kuona nyayo za Mungu; hivyo, kawaida, wanaletwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kuhusu wale wanawali wapumbavu, kwa sababu wanasisitiza kwa Biblia na kukosa kutambua kuwa Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho ni Mungu kwa kweli, basi wanafichuliwa na kutupwa mbali. Kwa sasa bado wanashikilia imara kile wanachoita imani yao, lakini majanga yatakapokuja, wataishia kulia na kusaga meno. Kutokana na hili tunaweza kuona, wale wanaoshikilia tu Biblia na kukosa kukubali ukweli, wale wanaoamini tu kwa Mungu aliye mbinguni lakini wanakosa kumkubali Kristo mwenye mwili wote ni wasioamini na kwa hakika wataondolewa na Mungu. Huu ni ukweli! Wacha tuone kile Mwenyezi Mungu anasema kuhusu haya.
Mwenyezi Mungu anasema, “Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)).
“Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?
Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo).
Inamaanisha nini kuamini katika Bwana? Inaanisha nini kuamini katika Biblia? Uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi? Ni kipi kilikuja kwanza, Biblia au Bwana? Basi nani anafanya kazi ya wokovu? Biblia inaweza kusimama katika nafasi ya Bwana kufanya kazi Yake? Je, Biblia inaweza kumwakilisha Bwana? Watu wakiweka imani pofu katika Biblia na kuabudu Biblia, je hii inamaanisha kuwa wanaamini na kumwabudu Mungu? Je, kushikilia Biblia ni sawa na kutenda na kupata uzoefu wa neno la Mungu? Je, kushikilia Biblia inamaanisha kuwa mtu anafuata njia ya Bwana? Kwa hivyo watu wakiweka Biblia kabla ya chochote kile, je, hii inamaanisha kuwa wanaabudu Bwana kama mkuu, kwamba wanamcha na kumtii Bwana? Hakuna anayeona ukweli wa masuala haya. Kwa maelfu ya miaka, watu wamekuwa wakiabudu kwa upofu Biblia na kuipa Biblia hali sawa na ile wanayompa Mungu. Wengine hata hutumia Biblia kuwa mbadala wa Bwana na kazi Yake, lakini hakuna anayemjua Bwana kwa kweli na kuwa mtiifu Kwake. Mafarisayo waliishikilia Biblia, ilhali walimpiga Bwana Yesu misumari msalabani. Suala lilikuwa nini? Je, kuelewa Biblia kunamaanisha kumjua Mungu? Je, kushikilia Biblia kunamaanisha kufuata njia ya Bwana? Mafarisayo walikuwa wataalam wa ufafanuzi wa kibiblia, lakini hawakumjua Mungu. Badala yake, walimpiga misumari msalabani Bwana Yesu ambaye alieleza ukweli na kufanya kazi ya ukombozi. Je, hakika tumeyasahau haya? Inamaanisha nini hasa kumjua Mungu? Je, kuweza tu kutafsiri Biblia na kuelewa maarifa ya Biblia kunastahili kuwa kumjua Mungu? Kama hiyo ndiyo hali, basi mbona Mafarisayo wamlaani na kumpinga Bwana Yesu hata walipokuwa wakiitafsiri Biblia? Msingi wa kama mtu anaweza kumjua na kumtii Mungu kweli ni kama anamjua ama hamjui na kumtii Kristo mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anawafichua binadamu wote, hili ni jambo ambalo watu wengi wanakosa kulitambua. Laana ya Bwana Yesu kwa Mafarisayo ni ushahidi kwa ukweli kuwa Mungu humtendea kila mmoja kwa haki. Kama ilivyo wazi, kama mtu hamtii na kumwabudu Bwana lakini tu anaamini na kuiabudu Biblia kwa upofu, hatapokea kibali cha Mungu. Kama imani ya mwanadamu inafuata kwa kipekee Biblia na moyo wake hauna nafasi ya Mungu, kama hawezi kumwabudu Bwana kama mkuu na kutenda maneno Yake, kama hana uwezo wa kukubali na kutii kazi na maelekezo ya Mungu, basi, kila mtu, hungesema kuwa mtu kama huyu ni Mfarisayo mnafiki? Je, mtu huyu sio adui wa Kristo, mwanadamu ambaye amefanya Kristo kuwa adui wake? Hivyo, mwanadamu akiishikilia tu Biblia, hii kwa hakika haimaanishi kuwa amepata ukweli na uzima. Ni makosa kuiabudu na kuifuata Biblia kwa upofu, kwa kufanya hivyo mtu kwa hakika hawezi kupokea kibali cha Mungu. Mungu amekuwa mwili na kueleza ukweli ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu, na kumwokoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani ili aweze kumtii Mungu, kumwabudu Mungu na kupatwa na Mungu hatimaye. Hili ndilo kusudi na maana ya Mungu mwenye mwili kufanya kazi Yake. Msingi wa imani yetu ni kutafuta ukweli, na kutenda na kupata uzoefu wa neno la Bwana. Kwa njia hii pekee ndiyo tutapokea kazi ya Roho Mtakatifu na kuja kumjua Bwana. Basi, tutaweza kumwogopa Bwana, na kumfanya Mungu kuwa mkuu mioyoni mwetu. Pia, tutakuwa na imani ya kweli na utii Kwake. Hii ndiyo maana ya kweli ya imani yetu katika Bwana. Kwa kutenda imani kwa njia hii pekee ndio tutapokea kibali cha Mungu. Kutokana na haya, kila mmoja anaweza kuona wazi kuwa imani katika Biblia sio sawa na imani katika Mungu. Kwa hivyo uhusiano kati ya Mungu na Biblia ni upi? Na kuhusu swali hili, Bwana Yesu alinena kwa uwazi sana. Tafadhali geukia Injili ya Yohana sura ya 5 msitari wa 39-40: “Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai.” Kutokana na maneno ya Bwana Yesu, ni wazi kabisa kwamba Biblia ni ushuhuda tu kwa Mungu, ni rekodi tu ya kazi ya Mungu ya zamani. Biblia haimwakilishi Mungu, kwa sababu Biblia ina maelezo machache ya kazi na maneno ya Mungu. Maelezo haya machache ya maneno na kazi ya Mungu yanawezaje kumwakilisha Mungu? Mungu ni Muumbaji ambaye Anajaza yote kwa yote, Yeye ni Bwana wa vitu vyote. Maisha ya Mungu hayana mkomo na hayamaliziki. Wingi wa Mungu, ukuu ambao mwanadamu hawezi kuuelewa. Na rekodi chache ya maneno na kazi ya Mungu inayopatikana katika Biblia ni tone la maji tu katika bahari kubwa ya maisha ya Mungu. Biblia inawezaje kumwakilisha Mungu? Biblia itakuwa vipi katika kiwango sawa na Mungu? Mungu anaweza kufanya kazi kumuokoa mwanadamu, je, Biblia inaweza kufanya kazi kuokoa mwanadamu? Mungu anaweza kueleza ukweli, Biblia inaweza kufanya hivyo? Mungu anaweza kutoa nuru, kutoa mwanga na kumwongoza mwanadamu katika wakati wowote, Biblia inaweza kufanya hilo? Bila shaka hapana! Kwa hivyo, Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu! Mwanadamu anaiweka Biblia katika kiwango sawa na Mungu na anafikiri kuwa Biblia inaweza kumwakilisha Mungu. Je, hii si kumdunisha na kumkufuru Mungu? Mwanadamu akitumia Biblia kwa nafasi ya kazi ya Mungu, hii ni kumkataa na kumsaliti Mungu. Mungu ni Mungu, Biblia ni Biblia. Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu, wala haiwezi kusimama mahali pa kazi ya Mungu. Biblia ni rekodi tu ya kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu katika Biblia ni ya kweli. Ni onyesho la tabia ya maisha ya Mungu, na yanaweza kuonyesha mapenzi ya Mungu. Lakini kila hatua ya kazi ya Mungu inawakilisha tu mahitaji na mapenzi ya Mungu kwa binadamu katika enzi hiyo. Haziwakilishi maneno na kazi ya Mungu katika enzi zingine. Je, wote mmeelewa haya sasa?
Kuhusu historia ya ndani ya Biblia, Nafikiri tunaweza kuangalia kifungu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. “Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (4)).
“Kabla ya hapo, watu wa Israeli walisoma tu Agano la Kale. Hiyo ni sawa na kusema, mwanzoni mwa Enzi ya Neema watu walisoma Agano la Kale. Agano Jipya lilionekana tu wakati wa Enzi ya Neema. Agano Jipya halikuwepo wakati wa kazi ya Yesu; watu waliandika kazi Yake baada ya kuwa amefufuka na kupaa mbinguni. Baada ya hapo kulikuwa na Injili Nne…. Inaweza kusemwa kuwa, kile walichorekodi kilikuwa ni kulingana na kiwango chao cha elimu na tabia. Kile walichokirekodi kilikuwa ni uzoefu wa wanadamu, na kila mmoja alikuwa na namna yake ya kurekodi na kuelewa, na kila rekodi ilikuwa tofauti. Hivyo, ikiwa unaiabudu Biblia kama Mungu wewe ni mjinga na mpumbavu wa kutupwa! Kwa nini usitafute kazi ya Mungu wa leo? Ni kazi ya Mungu tu ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu. Biblia haiwezi kuwaokoa wanadamu, wanaweza kuisoma kwa maelfu kadhaa ya miaka na bado hakutakuwa na mabadiliko hata kidogo ndani yao, na kama unaiabudu Biblia hutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (3)).
“Watu wanavyoichukulia Biblia ni shauku na imani, na hakuna anayeweza kufafanua kikamilifu kisa cha ndani au kiini cha Biblia. Kwa hivyo, leo watu bado wana hisia zisizoelezeka za kimiujiza linapokuja suala la Biblia, na hata wana shauku nayo zaidi, na wanaiamini hata zaidi. Leo, kila mtu anataka kutafuta unabii wa kazi ya siku za mwisho katika Biblia, wanataka kugundua ni kazi gani Mungu hufanya wakati wa siku za mwisho na kuna ishara gani ya siku za mwisho. Kwa njia hii, kuabudu kwao Biblia kunakuwa na maana sana, na kadri wanaposogelea siku za mwisho, ndivyo wanavyozidi kuonyesha imani pofu kwa unabii wa Biblia, hususani ule wa siku za mwisho. Kwa imani hiyo ya upofu katika Biblia, kwa imani hiyo katika Biblia, hawana shauku ya kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Katika dhana za watu, wanadhani kwamba ni Biblia pekee ndiyo inayoweza kuleta kazi ya Roho Mtakatifu; ni katika Biblia pekee ndimo wanamoweza kupata nyayo za Mungu; ni katika Biblia pekee ndimo kulimofichika siri za kazi ya Mungu; ni kwenye Biblia pekee—na sio katika vitabu vinginevyo au watu—wanaoweza kufafanua kila kitu cha Mungu na ujumla wa kazi Yake; Biblia inaweza kuleta kazi ya mbinguni duniani; na Biblia inaweza kuanzisha na kuhitimisha enzi. Kwa dhana hizi, watu hawana shauku kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo, licha ya kiasi gani Biblia ilikuwa ina msaada mkubwa kwa watu wa wakati wa nyuma, imekuwa ni kikwazo katika kazi ya Mungu ya hivi karibuni. Bila Biblia, watu wanaweza kutafuta nyayo za Mungu mahali kwingineko, bado leo, nyayo zake zimejumuishwa na Biblia, na kupanua kazi Yake ya hivi karibuni, imekuwa na ugumu mara mbili, na mapambano magumu. Hii yote ni kwa sababu ya sura na misemo maarufu kutoka katika Biblia, vilevile unabii mbalimbali wa Biblia. Biblia imekuwa sanamu katika akili za watu, limekuwa ni fumbo katika akili zao, na hawawezi kabisa kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi nje ya Biblia, hawawezi kuamini kwamba watu wanaweza kumpata Mungu nje ya Biblia, achilia mbali kuwa na uwezo wa kuamini kwamba Mungu angeweza kujitenga na Biblia wakati wa kazi ya mwisho na kuanza upya. Hili suala haliingii akilini mwa watu; hawawezi kuliamini, na wala hawawezi kulifikiria. Biblia imekuwa kikwazo kikubwa kwa watu kukubali kazi mpya ya Mungu, na imefanya kuwa vigumu kwa Mungu kuipanua kazi hii mpya” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)).
“Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Akafunika kichwa, Akavunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)).
Kutafuta na kuchunguza ukweli kuhusu swali la iwapo Biblia inaweza kumwakilisha Mungu na ni uhusiano upi uko kati ya Biblia na Mungu ni la muhimu zaidi. Kwanza lazima tujue: Mungu ni Mungu wa aina gani? Kama tunavyojua sote, Mungu ni Muumba wa vitu vyote, Mtawala wa vitu vyote. Mungu ni Yule Aliye, mwenye nguvu kubwa na busara. Mungu pekee ndiye Anayeweza kumwokoa Binadamu na kumwongoza Binadamu. Mungu pekee ndiye Anayeweza kuamua majaliwa ya binadamu. Huu ni ukweli unaotambulika kwa upana. Biblia ilitengenezwa vipi? Baada ya Mungu kumaliza kazi Yake, wanadamu waliotumiwa na Yeye waliandika chini ushuhuda na waliyoyapitia, na ushuhuda huu na matukio waliyopitia yalikusanywa baadaye kutengeneza Biblia. Huu ni ukweli! Kweli, hiyo ndio sababu tunaweza kusema kwa hakika kubwa kuwa Biblia ni rekodi tu ya kazi ya Mungu ya zamani, si chochote zaidi ya ushuhuda wa kazi ya Mungu. Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu, wala haiwezi kusimama mahali pa Mungu kufanya kazi ya kuokoa mwanadamu. Kama imani ya mwanadamu ina msingi katika Biblia pekee na sio kwa uzoefu wa kazi ya Mungu, hatawahi kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na kuokolewa. Kwa sababu kazi ya Mungu ya wokovu ni maendeleo yanayoendelea. Hivyo, mwanadamu hafai kushikilia hatua moja ama mbili za kazi ya Mungu. Lazima afuate nyayo za kazi ya Mungu hadi Mungu akamilishe kazi Yake ya kuokoa mwanadamu. Kwa jinsi hii pekee ndio mwanadamu ataweza kupokea wokovu kamili wa Mungu na kuingia katika mwisho wa safari unaopendeza kwa binadamu. Mpango wa usimamizi wa Mungu wa wokovu unajumuisha hatua tatu za kazi: kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Sasa kila mmoja anaelewa kuwa Enzi ya Sheria ilikuwa wakati ambapo Mungu alitumia sheria kuongoza maisha ya mwanadamu. Enzi ya Neema ilikuwa wakati Mungu alifanya kazi ya ukombozi kwa binadamu. Bwana Yesu alipigwa misumari msalabani ili kuokoa binadamu kutoka kwa mamlaka ya Shetani, wasamehe kutoka kwa dhambi zao, na kuwafanya wafae kuja mbele za Mungu, kumwomba Mungu, na kuwasiliana Naye. Kuhusu kazi ya hukumu katika Enzi ya Ufalme, hii ndiyo kazi ya kutakasa sana, kuokoa, na kukamilisha binadamu wote. Binadamu akipitia tu kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema lakini akose kukubali hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, hataokolewa kabisa na kupatwa na Mungu. Sote tunaweza kuona kuwa katika Enzi ya Neema kazi ya Bwana Yesu ilikuwa tu kukomboa binadamu. Katika enzi hii, kuamini katika Bwana kulituruhusu tu kusamehewa dhambi zetu, kustahili kumwomba Mungu, na kufurahia neema yote ya Mungu, lakini tulikosa kupata utakaso katika enzi hii. Kwa sababu tuna asili ya dhambi ndani yetu, na hutenda dhambi mara nyingi, humuasi na kumpinga Mungu, Bwana Yesu aliahidi kuwa Atarejea tena, na kueleza ukweli wote ambao unaokoa binadamu katika siku za mwisho kutakasa wale wote ambao wanasikia sauti ya Mungu na wanaletwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kama tu jinsi Bwana Yesu alivyotabiri: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13). Maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu ni utimizo kamili wa kifungu katika kitabu cha Yohana: “Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote.” Kwa hivyo Mwenyezi Mungu ni kurejea kwa Bwana Yesu. Mwenyezi Mungu kwa sasa anashiriki katika kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na anatakasa na kukamilisha wale wote ambao wamekuja mbele ya kiti Chake cha enzi, hivyo ni, kuwakamilisha wale wanawali wenye busara ambao wamerejea kuelekea Kwake baada ya kusikia sauti Yake ili wawe washindi ili kuwaleta katika ufalme wa Mungu. Ukweli wa Mungu kufanya hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu inaturuhusu sisi kuona kuwa Mungu amekuwa Akifanya kazi kila mara kuongoza na kuokoa binadamu. Kila hatua ya kazi ya Mungu imeinuliwa na ya maana zaidi kuliko wakati uliopita. Kuhusu Biblia, sio zaidi ya kitabu cha lazima kwa wafuasi wa Mungu. Biblia haiwezi kufanya kazi ya Mungu, kuwaongoza na kuwaokoa binadamu.
Biblia ni rekodi tu ya kazi ya Mungu. Mungu alipokuwa Amemaliza kazi, mwanadamu alinakili maneno na kazi Yake na kuyaweka pamoja kutengeneza Biblia. Ingawa Biblia ni muhimu kwa imani ya mwanadamu, kwa kupokea tu kazi ya Roho Mtakatifu ndipo mwanadamu ataelewa kweli Biblia na ukweli. Huu ni ukweli. Kwa hivyo, imani kwa Bwana inatuhitaji kufuata nyayo za Mwanakondoo kwa karibu, kukubali na kuiheshimu kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa jinsi hii pekee ndipo tutaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na wokovu wa Mungu. Tukisoma Biblia pekee lakini tukose kukubali maneno na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, hatuwezi kutakaswa na kuokolewa. Hakika, hata kama maneno yote ya Mungu yangerekodiwa katika Biblia, bila kazi ya Roho Mtakatifu, bado hatungeweza kulielewa na kulijua neno la Mungu. Kuuelewa ukweli, lazima tupate uzoefu na kuyatenda maneno ya Mungu, lazima tupokee nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Hapo tu ndipo tutaweza kuelewa neno la Mungu, kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli. Ukweli ni wa kutosha kuthibitisha, Kama muumini, kiini cha wokovu wetu ni nini? Kiini ni kazi ya Roho Mtakatifu, ukamilisho wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni nani? Je, Roho Mtakatifu si Mungu Mwenyewe tu? Biblia ni rekodi tu ya kazi ya Mungu zamani. Sasa ingeweza vipi kusimama kwa niaba ya Mungu Mwenyewe? Hivyo kama nilivyosema, Mungu pekee anaweza kumwokoa mwanadamu, Biblia haiwezi kumwokoa mwanadamu. Kama imani yetu inahusu tu kufuata Biblia na sio kukubali maneno na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, tusipofuata hatua za kazi ya Mungu, tutawachwa na kuondolewa. Katika Enzi ya Sheria, kuna wengi ambao walikosa kukubali kazi ya Bwana Yesu, na waliondolewa. Wale wanaoamini katika Bwana Yesu lakini wakosa kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho pia wataachwa na kuondolewa. Inaweza kusemekana kuwa watu hao ni vipofu na hawamjui Mungu. Kilichobaki kwao ni kuubeba mzigo mzito wa majanga yanayokuja, kulia na kusaga meno yao.
Kazi ya hukumu inayofanywa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kupitia kueleza ukweli ni kazi ya kiini katika mpango wa usimamizi wa Mungu kuwaokoa binadamu wote. Pia ni hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu kuwatakasa kabisa, kuwaokoa na kuwakamilisha binadamu. Kwa hivyo waumini wakishika tu hatua mbili za kwanza za kazi iliyoelezwa katika Biblia na wakose kukubali kazi ya utakaso na wokovu iliyofanywa na Kristo wa siku za mwisho, hawatawahi kuokolewa na kuingia katika ufalme wa Mungu. Haijalishi ni miaka mingapi watu hao wamekuwa na imani katika Bwana, yote itakuwa ya bure, kwa sababu wale wote wanaokataa wokovu wa wakati wa mwisho wa Mwenyezi Mungu ni wapinzani wa Mungu, wote ni Mafarisayo wanafiki. Hakuna swali hata moja kuihusu. Hata kama Mafarisayo walimkataa Bwana Yesu kwa msingi wa Biblia na katika siku za mwisho, wazee wa kanisa na wachungaji wanakataa kazi ya Mwenyezi Mungu kwa msingi wa Biblia, hoja zao hazina msingi. Kwa sababu hawaweki hoja zao kwa neno la Mungu, lakini kwa barua ya Biblia. Haijalishi ni sababu ngapi mmoja anazo, yeyote anayekosa kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni mpinzani na msaliti wa Mungu. Machoni mwa Mungu, wote ni watenda dhambi, Mungu hatawahi kuwatambua. Wapinga Kristo hao na wasioamini wanafichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho lazima waione adhabu ya majanga yanayokuja kwa kulia na kusaga meno. Wote wametupiliwa mbali na kuondolewa na Mungu milele, na hawataweza tena kuwa na nafasi ya kumwona Mungu na kupokea kibali Chake. Huu ni ukweli. Hapa, tunaweza kuja kuelewa ukweli: Biblia haiwezi tu kumwakilisha Mungu, na kwa hakika haiwezi kusimama kwa niaba ya kazi ya Mungu. Mungu ni Mungu, Biblia ni Biblia. Kwa sababu tunaamini katika Mungu, lazima tupate uzoefu wa kazi ya Mungu na kufuata kasi ya kazi ya Mungu, lazima tule na kunywa maneno ambayo Mungu anaeleza katika siku za mwisho, na lazima tukubali na kufuata ukweli wote ambao Mungu anaeleza. Hii ni maana ya kweli ya imani kwa Mungu. Kila wakati Mungu anapokuwa mwili ili Afanye kazi, Lazima Atupilie mbali na kuwaondoa wale ambao wanazingatia tu Biblia lakini wanakosa kujua na kumtii Mungu. Kwa hivyo, tunaweza kusema na ujasiri, “Imani kwa Mungu lazima iwe sambamba na Biblia, kushikilia Biblia ni imani ya kweli kwa Mungu, Biblia inamwakilisha Mungu,” kauli hizi ni udanganyifu kabisa. Yeyote anayetamka kauli za aina hii ni kipofu na hamjui Mungu. Kama mwanadamu angeweka Biblia juu ya kila kitu na kutumia Biblia kwa mahali pa Mungu, je, hangekuwa akitembea katika njia ya Mafarisayo? Mafarisayo walizingatia Biblia kwa kumpinga Mungu, kutokana na hilo walikutana na laana ya Mungu. Je, huu sio ukweli?
Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Ikiwa watu wanapata uzima kupitia imani yao katika Mungu hutegemea kama wanapata ukweli. Wakiupata, basi wamemjua Mungu kwa kweli; ni wale tu ambao wamefanya hivyo ndio wamepata uzima kwa kweli. Wale ambao hawamjui Mungu kwa kweli hawajapata ukweli; kwa hiyo, watu kama hao hawajapata uzima. Hili ni hakika, bila shaka yoyote. Hivyo inamaanisha nini hasa kuupata ukweli? Huku kunahitaji kuwa na maarifa ya Kristo, kwa sababu Yeye ni Mungu mwenye mwili miongoni mwa wanadamu, Mwenye Kuonyesha ukweli wote. Ukweli unatokana na uhai wa Mungu, na ni onyesho la Kristo kabisa, ambaye asili yake ni ukweli, njia, na uzima. Kristo tu ndiye anamiliki asili ya ukweli na uzima, hivyo kumjua na kumpata Yeye ndiyo njia halisi tu ya kupata ukweli. Kutoka kwa hili ni dhihiri kwamba miongoni mwa waaminifu, wale tu ambao wanamjua Kristo na wamempata Yeye ndio wamepata uzima kwa kweli, wamemjua Mungu, na kupata uzima wa milele. Hili linatimiza kamili lile liandikwalo katika Biblia: “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele: na yule asiyemwamini Mwana hatauona uzima; ila ghadhabu ya Mungu hukaa juu yake” (Yohana 3:36). Kumwamini Mwana bila shaka kunarejea kumfuata Kristo mwenye mwili. Kwa watu ambao wanamwamini Mungu, ni wale tu ambao wanamtambua Kristo kuwa ukweli, njia, na uzima, ndio wanaweza kumjua Mungu, kuokolewa, na kufanywa wakamilifu kwa kweli; hao tu ndio wataupokea utukufu wa Mungu. Yeyote ambaye anamwamini Mungu na bado anaweza kumkana, kumpinga, na kumtelekeza Kristo ni mtu ambaye ana imani lakini humpinga na kumsaliti Mungu. Kwa mfano, hataweza kufanikisha wokovu au ukamilifu. Mtu akimwamini Mungu lakini anaabudu tu na kuishuhudia Biblia bila kufikiri kwanza huku akipinga na kuhisi chuki juu ya Kristo, basi mtu huyo tayari ameingia katika njia ya mpinga Kristo na kuwa adui wa Mungu. Kuwa mpinga Kristo halisi, mtu kama huyo ataadhibiwa na kulaaniwa na Mungu, na atajipata katika mateso ya milele na kuangamia. Kwa waaminifu, huu ni ushinde na huzuni mbaya zaidi.
Kuna wengi ambao humwamini tu Mungu asiye dhahiri huko mbinguni kwa mujibu wa Biblia, lakini ambao hawaamini Mungu anaweza kuwa mwili, sembuse kumkubali Kristo kuwa Mungu mwenye Mwili, kuwa Mwokozi wa wanadamu wapotovu, au Mungu wa vitendo ambaye anawaokoa wanadamu. Watu kama hao hawajui kwamba Kristo ndiye ukweli, njia na uzima; isitoshe, hawawezi kuufanikisha uwiano na Kristo. Bila shaka ni aina ya watu ambao wanachoshwa na, kuhisi chuki juu ya ukweli. Sote tunaweza kusoma katika Biblia kwamba makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo walimwamini Mungu katika maisha yao yote lakini walikataa kumkubali Yesu aliyepata mwili, kufikia hali ambayo wangeweza hata kumsulibisha Yesu Kristo. Kama matokeo, walikuwa watu ambao walimpinga na kumsaliti Mungu, na kwa hiyo walipata adhabu na laana Zake. Licha ya imani yao ya maishani, walishindwa kupata baraka na ahadi ya Mungu. Ilikuwa ya kusikitisha na yenye huzuni jinsi gani! Hivyo, ikiwa watu wanafanikiwa katika imani yao hutegemea kama wanamjua na wamempata Kristo. Kiini cha jambo ni iwapo wameukubali ukweli wote unaoonyeshwa na Kristo, na kupata uzoefu wa kazi yote ya Mungu kwa utii; ni iwapo wanaweza kumtukuza Kristo na kumshuhudia hadi walingane na Yeye. Hili ndilo jambo muhimu ambalo linaamua kufanikiwa au kushindwa kwa imani yao katika Mungu. Hata hivyo, watu wengi hawakubaliani na hili; wanaiona Biblia kama iliyo muhimu kuliko vyote, na hata wameitumia kuchukua nafasi ya Mungu mioyoni mwao. Mungu mwenye mwili anapokuja kutenda kazi, watu hawa wanaweza kumkana, kumkataa, na kumpinga Kristo kwa kweli. Kama maneno na matendo ya Kristo hayakubaliani na sheria fulani za Biblia, hawa watu wanathubutu kumlaumu, kumkataa, na kumtelekeza Yeye. Badala ya kumwamini Mungu, ingekuwa sahihi zaidi kusema kwamba wao wanaiamini Biblia. Machoni pao, Biblia ni Bwana na Mungu wao. Inaonekana kwamba kwao Mungu, Bwana, yu ndani ya Biblia, nayo inamwakilisha Yeye. Hivyo, wanaamini kwamba ukweli ni chochote ambacho kinapatana kikamilifu na Biblia, wakati ambapo chochote ambacho hakikubaliani na Biblia hakiwezi kuwa ukweli. Wao wanaiona Biblia kama iliyo juu kuliko ukweli wote; kupotea kutoka kwa Biblia kungekuwa kupotea kutoka kwa ukweli, kwa kuwa kile tu kiandikwacho katika Biblia ndicho ukweli. Wao wanafikiria kazi na matamshi ya Mungu ni yale yaliyoorodheshwa ndani ya kurasa zake pekee; wanakataa kukikiri chochote ambacho huenda alikifanya au kukisema isipokuwa Biblia. Watu kama hao ni sawa na wale makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo, ambao waliitambua tu Biblia, lakini hawakumjua Mungu hata kidogo; na hata hawakuwa tayari kukubali kuweko kwa Kristo mwenye mwili. Hata wameifanya Biblia ipingane na Kristo, wakikosa maarifa kabisa kwamba Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima; badala yake, waliitukuza na kuishuhudia Biblia na walimsulibisha Kristo msalabani, kwa hiyo wakitenda dhambi mbaya sana ya kumpinga Mungu. Kwa njia hii, huenda walimwamini Mungu, lakini hawakuokolewa; badala yake, walikuwa maadui wa Mungu, na walitakiwa kupokea adhabu na laana Zake. Haya ndiyo matokeo ya moja kwa moja ya watu ambao walimwamini Mungu katika dini, ambao walidanganywa na kudhibitiwa na makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo, na kuingia kwenye njia ya mpinga Kristo. Inaonyesha kwamba lile alilolisema Bwana Yesu ni kweli: “Na kipofu akimwelekeza kipofu, wote wawili wataanguka ndani ya shimo” (Mathayo 15:14). Watu kama hao bila shaka hawawezi kuokolewa au kukamilishwa.
Biblia ina neno ambalo linaiwakilisha asili ya Kristo vizuri zaidi. Ilikuwa lile alilolisema Bwana Yesu, “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6). Kwa maneno haya, Bwana Yesu alilisema jambo lililo sahihi hasa, na kuifunua siri kubwa zaidi ya imani katika Mungu—ukweli kwamba watu wanaweza kuufanikisha wokovu tu kwa kumjua na kumpata Kristo. Hii ni kwa sababu ni wakati tu Mungu anapokuwa mwili Mwenyewe kama Kristo ndio Yeye anaweza kuwaokoa wanadamu kabisa. Kristo ndiye lango la pekee kwa kondoo Wake kuufikia ufalme wa mbinguni, na Kristo mwenye mwili tu ndiye Mungu wa vitendo ambaye anaweza kuleta wokovu kwa wanadamu. Wakimwamini Mungu, basi ni kwa kukubali na kumfuata Kristo tu ndiyo wanaweza kuingia njia ya wokovu na ukamilifu. Hii ndiyo njia tu wanaweza kuwa wale ambao wanafanya mapenzi ya Baba wa mbinguni, na kuingia katika ufalme wa mbinguni kwa zamu. Kutokana na hili, inaweza kuonekana kwamba wamwaminio Mungu lazima wakubali na kumtii Kristo mwenye mwili kabla ya wao kuweza kuokolewa na kukamilishwa ili kuupokea utukufu wa Mungu. Hii ndiyo njia ambayo kwayo Mungu amewajalia watu kumwamini Yeye na kuufanikisha wokovu. Hivyo, swali iwapo watu ambao wanamwamini Mungu wanamjua na wamempata Kristo kwa kweli ni muhimu sana, na lina uhusiano wa moja kwa moja na mwisho na matokeo yao.
Tunapokumbuka kazi aliyoifanya Bwana Yesu Alipokuja duniani kuianzisha Enzi ya Neema, tunaweza kuona kwamba hakuna kati ya waumini katika dini aliyemjua au kumfuata Yeye. Hii ilikuwa hasa kweli kuwahusu makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo wa Dini ya Kiyahudi, wote ambao walikataa kumtambua au kumkubali Kristo. Isitoshe, watu hawa walimkana, walimhukumu, na kumlaani Bwana Yesu kwa mujibu wa lile lililoandikwa katika Biblia. Hata walimsulibisha Yeye, hivyo wakitenda dhambi mbaya sana ya kumpinga Mungu na kuwa mifano kamili ya aina ya watu ambao wanamwamini Mungu lakini wanamkataa na kumsaliti Yeye kwa zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita, na kwa hiyo ambao wamepatwa na adhabu na laana za Mungu. Kwa kweli, mwanzoni, huku akihubiri, Bwana Yesu alikuwa ametambua tayari ukweli halisi kwamba dunia ya mambo ya dini ilikuwa, kimsingi, ikimpinga Mungu, na kwa usahihi mkubwa, Yeye alifichua moja kwa moja chanzo na kiini cha uhasama wa Mafarisayo dhidi ya Mungu: “Na hamna neno lake likiishi ndani yenu: kwani hammsadiki huyo ambaye amemtuma. Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai” (Yohana 5:38-40). Maneno ya Bwana Yesu yalifichua ukweli na kiini cha jumuia ya mambo ya dini ikimwamini lakini ikimpinga Mungu. Wakati huo huo, wao wanatoa habari mpya juu ya kiini cha uhusiano baina ya Biblia na Kristo. Bila shaka huu ni wokovu upitao kiasi kwa watu ambao wanamwamini Mungu. Hata hivyo, katika jumuia ya mambo ya dini ya siku hizi, bado watu wengi wanaamini bila kufikiri kwanza, wanaabudu, na kuishuhudia Biblia, wakiiona kuwa muhimu zaidi kuliko Kristo na kuiweka juu ya ushuhuda wa Kristo. Hii ni kweli hasa kuhusu viongozi wa mambo ya dini na wachungaji ambao, kama walivyofanya Mafarisayo, wanaendelea kumhukumu, kumlaani, na kumkufuru Kristo mwenye mwili katika siku za mwisho kwa mujibu wa Biblia, licha ya ukweli anaounyesha Yeye. Matendo yao yamesababisha sikitiko la mwisho wa kumsulibisha Kristo mara ya pili, na yaliamsha ghadhabu ya Mungu zamani. Matokeo ni yenye maafa, kwa kuwa mwanzoni Mwenyezi Mungu alionya, “Ole wao wale wamsulubishao Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa). Kwa hiyo, ni lazima kabisa kuuanzisha uhusiano wazi baina ya Biblia na Kristo ili kila mmoja aweze kuishughulikia Biblia kwa usahihi, amkubali Kristo, na kuitii kazi Yake ili kukipata kibali cha Mungu.
…………
Kuhusu maandiko matakatifu, wakati mmoja Bwana Yesu alisema, “nashuhudiwa na hayo.” Hapa neno la Mungu lilinenwa kwa uwazi mkubwa; Biblia ni mkusanyiko tu wa ushuhuda kumhusu Yeye. Sote tunafahamu kwamba Biblia ni kumbukumbu halisi ya hatua za kwanza mbili za kazi ya Mungu. Kwa maneno mengine, ni ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, ambazo zinahitimisha uongozi na ukombozi wa wanadamu baada ya kuumbwa kwa mbingu na dunia na vitu vyote, pamoja na wanadamu. Kutokana na kuisoma Biblia, kila mmoja anaweza kuona jinsi Mungu aliwaongoza wanadamu wakati wa Enzi ya Sheria na kuwafundisha kuishi mbele Zake na kumwabudu Yeye. Tunaweza kuona pia jinsi Mungu aliwakomboa wanadamu wakati wa Enzi ya Neema na kuwasamehe dhambi zao zote zilizopita huku akiwapa amani, furaha, na kila aina ya neema. Watu hawawezi tu kuona kwamba Mungu alikuwa amewaumba wanadamu, bali pia kwamba Yeye alikuwa amewaongoza kwa uthabiti na halafu akawakomboa. Wakati huo huo, Mungu amewakimu na kuwalinda wanadamu pia. Aidha, tunaweza kusoma kutoka kwa unabii wa Biblia kwamba siku za mwisho, maneno ya Mungu yatachoma kama moto ili kuwahukumu na kuwatakasa watu Wake. Yatawaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi zote na kutusaidia kuutoroka ushawishi wa giza la Shetani ili tuweze kumrudia Mungu kabisa na hatimaye kurithi baraka na ahadi Zake. Hili ndilo alilolimaanisha Mungu aliposema, “nashuhudiwa na hayo.” Kwa hiyo, yeyote ambaye ameisoma Biblia kwa makini anaweza kuona kiasi kidogo cha matendo ya Mungu na kutambua kuweko Kwake na uweza na hekima ambayo kwayo Yeye aliumba, Anatawala, na Hudhibiti kila kitu mbinguni na duniani. Hivyo, Biblia ni yenye maana sana kwa watu katika kumwamini Mungu, kumjua Mungu na kuingia njia ya imani—njia halisi ya uzima. Yeyote ambaye anamwamini Mungu kwa unyofu na anaupenda ukweli anaweza kupata lengo na mwelekeo katika maisha kwa kuisoma Biblia, na kujifunza kumwamini, kumtegemea, kumtii, na kumwabudu Yeye. Haya yote ni matokeo ya ushuhuda wa Biblia kwa Mungu; huu ni ukweli usiokanushika. Hata hivyo, Bwana Yesu pia alielezea wazo lililo muhimu zaidi Aliposema, “Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele” na “Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai.” Maneno haya ni muhimu sana! Kama watu ambao wanamwamini Mungu wanataka kupata ukweli na uzima, haitoshi kuutegemea tu ushuhuda wa Biblia; lazima pia wamjie Kristo ili kupata ukweli na uzima. Hii ni kwa sababu Yeye tu ndiye anaweza kuonyesha ukweli, kuwakomboa, na kuwaokoa wanadamu. Mungu ndiye Yule ambaye hutupa uzima. Biblia haiwezi kuchukua mahali pa uwezo Wake, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu, na haiwezi kutoa uzima kwa wanadamu kwa niaba ya Mungu. Ni kwa kumkubali na kumtii Kristo tu ndio tunaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na ukweli na uzima. Watu wakiiamini tu Biblia bila kumkubali Mungu wa vitendo mwenye Mwili, basi hawataweza kupata uzima, kwa sababu Biblia si Mungu; ni ushuhuda tu wa kazi ya Mungu. Kwa kumwamini Mungu, tunapaswa kufahamu kwamba kuna hatua kwa kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu; hatua tatu za kazi ni za lazima ili kuwaokoa wanadamu kabisa kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ili waweze kumrudia Mungu kwa kweli na Yeye awapate. Kwa hiyo, kila hatua ya kazi ya Mungu ambayo wanadamu wanaipitia inawaletea sehemu ya wokovu Wake. Ni kufuata tu kwa makini kasi ya kazi ya Roho Mtakatifu na kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu siku za mwisho ndio tunaweza kupokea wokovu wa Mungu tele na kamili. Kwa Mfano, katika kumwamini Bwana Mungu, Waisraeli wangeweza tu kufurahia ahadi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria. Kama hawakuukubali wokovu wa Yesu Kristo, hawangeweza kusamehewa dhambi zao, sembuse kufurahia amani, furaha, na neema tele itolewayo na Mungu; huu ni ukweli. Watu wakiukubali tu ukombozi wa Bwana Yesu ili wasamehewe dhambi zao, pamoja na neema nyingi zitolewazo na Mungu, lakini hawaikubali kazi Yake ya hukumu na ya kuadibu siku za mwisho, basi hawawezi kupata ukweli au uzima, wala hawataweza kuufanikisha mbadiliko katika tabia ya maisha yao. Kwa hiyo, hawatakuwa wenye sifa zinazostahili kuzirithi ahadi za Mungu na kuingia ufalme wa mbinguni. Kila hatua ya kazi ya Mungu huyazaa matunda yake. Kazi ya Mungu inajengwa juu ya hatua moja moja kwa zamu, na hatua hizi zote zinakamilishana moja kwa nyingine; hakuna hatua mojawapo inayoweza kuachwa. Hizo zinaelekea kwenye ukamilifu kwa taratibu. Kama mtu angekataa kukubali mojawapo ya hatua ya kazi ya Mungu, mtu huyo angeweza tu kupata sehemu ya wokovu Wake, sio wote. Huu, pia, ni ukweli. Watu wakiiamini tu Biblia bila kumkubali Kristo siku za mwisho, watakuwa wapinzani na wasaliti wa Mungu. Kama matokeo, watakuwa wamepoteza kijalizo kamili cha wokovu wa mwisho wa Mungu. Kwa maneno mengine, watu ambao wanamwamini tu Bwana Yesu na hawakubali wokovu unaoletwa na kurudi Kwake—Mungu Mwenyezi—siku za mwisho, basi imani yao itaharibiwa nusu njia, na yote yatakuwa bure. Lingesikitisha jinsi gani! Ni la kusikitisha jinsi gani! Kwa hiyo, kutomkubali Kristo mwenye mwili kunasababisha kutoweza kupata uzima. Kwa kuiamini Biblia tu, watu hawawezi kuokolewa au kupata uzima, na hawataweza kumjua Mungu, kwa sababu Biblia si Mungu; ni ushuhuda tu kwa Yeye. Hivyo, watu wakiiamini tu Biblia bila kumkubali Kristo, hawawezi kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Kama matokeo, hawawezi kuokolewa na Mungu; wanaweza tu kuuawa na Yeye. Hili halina shaka yoyote. Ni ukweli unaoweza kuonekana kwa kuisoma Biblia. Aidha, hii pia ndiyo sababu kubwa ya viongozi wa mambo ya dini na wachungaji ya kumwamini Mungu lakini wanampinga, ambayo yanasababisha kushindwa katika imani yao.
Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?