Biblia ni ushahidi wa kazi ya Mungu; ni kwa kusoma Biblia pekee ndiyo wale wanaomwamini Bwana wanaweza kutambua kwamba Mungu aliumba mbingu na dunia na vitu vyote na kuona matendo ya ajabu ya Mungu, ukuu Wake na uweza. Katika Biblia kuna maneno mengi ya Mungu na ushuhuda mwingi wa uzoefu wa mwanadamu; inaweza kuyakimu maisha ya mwanadamu na kuwa na manufaa sana kwa mwanadamu, hivyo kile ninachopenda kufuatilia ni, kwa kweli tunaweza kupata uzima wa milele kwa kusoma Biblia? Kweli hakuna njia ya uzima wa milele katika Biblia?

08/06/2019

Jibu:

Kupitia kusoma Biblia tunakuja kuelewa kuwa Mungu ni Muumba wa vitu vyote na tunaanza kutambua matendo Yake ya ajabu. Hii ni kwa sababu Biblia ni ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu. Ni rekodi ya maneno na kazi ya Mungu na ushuhuda wa mwanadamu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kwa hivyo, Biblia ni muhimu sana kwa imani yetu. Fikiria kuihusu, kama sio Biblia, mwanadamu angewezaje kuelewa neno la Bwana na kumjua Bwana? Ni kwa njia nyingine ipi ndiyo mwanadamu angeshuhudia matendo ya Mungu na kuanza kukuza imani ya kweli kwa Mungu? Mwanadamu asiposoma Biblia, ni kwa njia nyingine ipi ataweza kushuhudia ushuhuda wa kweli wa watakatifu wote katika enzi zote wakimtii Mungu? Kwa hivyo, kusoma Biblia ni muhimu kwa utendaji wa imani, na muumini yeyote wa Mungu hafai kupotoka kutoka kwa Biblia. Unaweza kusema, yeyote anayepotoka kutoka kwa Biblia hawezi kuamini katika Bwana. Hii imethibitishwa kwa matukio ya watakatifu katika enzi zote. Hakuna anayethubutu kukataa thamani na maana ya kusoma Biblia katika utendaji wa imani. watakatifu katika enzi zote na waumini wote wanaona kusoma Biblia kama suala la maana. Wengine wangeenda mbali hata kiasi cha kusema kuwa, kusoma Biblia na maombi ni muhimu kama miguu yetu miwili ilivyo muhimu kwa kutembea, bila mguu mmoja hatuwezi kusonga mbele. Lakini Bwana Yesu amesema, “Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai(Yohana 5:39-40). Watu wengine wamechanganyikiwa. Wanafikiri, kwa sababu Biblia ni rekodi ya neno la Mungu na ushuhuda wa mwanadamu, kusoma Biblia kunafaa kumpa mwanadamu uzima wa milele! Basi mbona Bwana Yesu alisema hakuna uzima wa milele katika Biblia? Kweli, hili sio wazo ngumu sana. Ili mradi tuelewe hadithi ya ndani na kiini cha maneno na kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema na pia matokeo yanayofikiwa kwa kuyapitia, basi tutakuja kugundua kawaida ni kwa nini mtu hawezi kupokea uzima wa milele kwa kupitia kusoma Biblia. Katika Enzi ya Sheria, Yehova alijishughulisha sana na kutunga sheria, amri na maagizo ya kufuatwa na mwanadamu. Maneno Yake yalikuwa mara nyingi aina ya mwongozo kwa binadamu, ambayo bado ilikuwa utotoni mwao, kuishi duniani. Maneno haya hayakuhusisha kubadilisha tabia ya maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo maneno ya Mungu katika Enzi ya Sheria yote yalilengwa kwa kufanya watu kufuata sheria na amri. Ingawa maneno haya yalikuwa ukweli, yanawakilisha ukweli wa mwanzo kabisa. Katika Enzi ya Neema, Maneno na kazi ya Bwana Yesu yalilengwa kwa kazi ya ukombozi. Maneno Aliyotoa ni kuhusu ukweli wa ukombozi na yaliwafunza watu kuwa wanafaa kukiri dhambi zao na kutubu na kujiepusha kutokana na kufanya dhambi na kufanya uovu. Maneno haya pia yaliwafunza watu njia inayofaa ya kumuomba Bwana na kuhitaji kuwa mwanadamu lazima ampende Bwana na moyo na roho yao yote, wapende jirani wao kama wanavyojipenda wawe wastahimilivu na wavumilivu, na kusamehe wengine sabini mara saba, na kadhalika. Haya yote yamejumlishwa katika njia ya toba. Kwa hivyo, kupitia kusoma Biblia, tunaweza kuelewa tu kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Tunakuja kutambua kuwa vitu vyote vimeumbwa na Mungu na kujifunza jinsi ya kuishi duniani na jinsi ya kumwabudu Mungu. Tunaelewa dhambi ni nini, waliobarikiwa na Mungu ni nani na wale waliolaaniwa na Mungu ni nani. Tunakuja kujua jinsi ya kukiri dhambi zetu na kutubu kwa Mungu. Tunajifunza unyenyekevu, uvumilivu na msamaha, na kujua tunafaa kuchukua msalaba kumfuata Bwana. Tunajionea rehema isiyo na kikomo na huruma ya Bwana Yesu, na kutambua kuwa kwa kuja mbele ya Bwana Yesu kwa imani ndipo tutafurahia neema Yake nyingi na ukweli. Maneno na kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema ilivyorekodiwa katika Biblia yalikuwa ukweli ulionenwa na Mungu kulingana na mpango wa kumwokoa binadamu na mahitaji ya binadamu katika wakati huo. Ukweli huu haungeweza kabisa kutatua kiini cha utendaji dhambi wa mwanadamu, ukibadilisha tabia ya maisha ya mwanadamu, na kuruhusu mwanadamu kupata utakaso, wokovu na ukamilishaji. Hivyo, maneno yaliyotolewa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema yanaweza tu kuitwa njia ya toba, lakini sio njia ya uzima wa milele.

Basi njia ya uzima wa milele ni gani? Njia ya uzima wa milele ni njia ya ukweli inayomruhusu mwanadamu kuishi milele, ambayo ni kusema, ni njia inayomruhusu mwanadamu kutupa pingu na vizuizi vya asili yake ya utendaji dhambi, kubadilisha tabia ya maisha yake, na inamruhusu kupata ukweli kama maisha, kujitoa kabisa kwa ushawishi wa Shetani na kulingana na Kristo. Inamruhusu mwanadamu kujua, kutii na kuheshimu Mungu ili wasitende tena dhambi kumpinga ama kumsaliti Mungu. Njia inayoweza kufikia tokeo hili tu ndiyo inaweza kuitwa njia ya uzima wa milele. Mwanadamu, hufa kama tokeo la dhambi. Mwanadamu akipata ukweli kama maisha na kutatua dhambi yote inayomsumbua, Mungu atambariki na uzima wa milele. Kwa hiyo, kwa kupokea wokovu wa Mungu tu katika siku za mwisho ndipo tutaweza kufurahia njia ya uzima wa milele ambayo Mungu anawaridhia wanadamu. Bwana Yesu alisema, “Mimi ndiye ufufuo, na uzima: yeye ambaye ananiamini, ingawa alikuwa amekufa, bado ataishi: Na yeyote ambaye anaishi na kuniamini hatakufa kamwe(Yohana 11:25-26). Hii inaonyesha kwamba maisha na kifo cha mwanadamu viko mikononi mwa Mungu. Haya ni mamlaka ya Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadili majaliwa yake mwenyewe. Ni wale tu wanaoufanikisha wokovu kwa kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kuupata ukweli kama uzima wao ndio wanaoweza kupata uzima wa milele. Hii ni ya hakika kabisa. Kwa hiyo, baada ya Bwana Yesu kuikamilisha kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, Aliahidi kwamba Atarudi, na wakati huo Alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Ukweli unaoonyeshwa na Bwana Yesu aliyerudi ndiyo njia pekee ya uzima wa milele, na hii inaonyesha kwamba Kristo ndiye kweli, njia, na uzima. Kwa nini Biblia haina njia ya uzima wa milele? Ni kwa sababu hasa Biblia inasimulia hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, lakini haina ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Kwa hiyo, Biblia haina njia ya uzima wa milele. Hii, hata hivyo, haipunguzi Biblia kama ushuhuda kwa Mungu au matokeo yake kwa wasomaji wake. Ni kwa sababu hasa ushahidi wa Mungu katika Biblia ni kweli, kwa sababu uumbaji wa Mungu wa mbingu, dunia na vitu vyote ni kweli, na kwa sababu ushuhuda wa utiifu na uaminifu kwa Mungu na vizazi vya watakatifu ni kweli, ndipo nafasi ya Biblia katika moyo wa mwanadamu haijawahi kuyumbayumba. Mtu anaweza kusema kwamba vizazi vya watakatifu vilikua na kukomaa kwa sababu ya ujenzi wa maadili waliyopokea kutoka kwa Biblia. Licha ya ukweli kwamba tabia potovu ya wanadamu iliendelea kuwepo ndani yao, asili zao za kishetani bado zilikuwepo, na hawakuwa wametakaswa kwa kweli, hata hivyo imani ya watakatifu katika Mungu na uaminifu wao vilikuwa imara. Wengi walikuwa wafiadini kwa ajili ya Bwana, na wote walionyesha ushuhuda mzuri na ulioenea pote Kwake. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Ni dhahiri kwetu sote kwamba wale wenye imani katika Bwana ni wengi sana, na hata kama hawajatakaswa, tabia yao ya maisha haijabadilika, na hawana ufahamu wa kweli kumhusu Mungu, hata hivyo imani yao ni ya kweli. Mungu hajawaacha watu hawa, lakini badala yake Anasubiri kurudi kwa Bwana katika siku za mwisho, wakati ambapo watainuliwa mbele Yake, kutakaswa, na kukamilishwa. Kwa njia hii, wote ambao wana imani ya kweli katika Bwana na wanaopenda ukweli watapata njia ya uzima wa milele iliyotolewa na Mungu katika siku za mwisho. Sasa tunalielewa swala la kwa nini Biblia haiwezi kuridhia uzima wa milele, siyo?

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp