Unashuhudia kwamba Bwana Yesu amekwisha kurudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, ambaye huonyesha ukweli wote ambao humtakasa na kumwokoa wanadamu na ambaye hufanya kazi ya hukumu akianzia na familia ya Mungu, hivyo tunafaa kutambuaje sauti ya Mungu na tunafaa kuthibitishaje kwamba Mwenyezi Mungu ndiye hasa Yesu aliyerudi?

09/06/2019

Jibu:

Swali ni la umuhimu mkubwa sana. Kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kutazama kuonekana kwa Mungu, lazima tujue jinsi ya kutambua sauti ya Mungu. Kwa Kweli, kutambua sauti ya Mungu kumaanisha kufahamu maneno na matamshi ya Mungu, na kufahamu zile sifa bainifu za maneno ya Muumba. Bila kujali kama maneno ya Mungu aliyepata mwili, au matamshi ya Roho wa Mungu, yote ni maneno yaliyonenwa na Mungu kwa mwanadamu kutoka juu sana. Sauti na sifa bainifu ya maneno ya Mungu ni namna hiyo. Hapa, mamlaka na utambulisho ya Mungu vimebainishwa kwa dhahiri. Hii, inaweza kusemwa, ni njia ya pekee ambayo Muumba hunena. Matamshi ya Mungu kila wakati Yeye huwa mwili bila shaka hufikia maeneo mengi. Kimsingi yanahusiana na mahitaji ya Mungu na maonyo kwa mwanadamu, maneno ya maagizo ya utawala na amri za Mungu, maneno Yake ya hukumu na kuadibu, na ufunuo Wake wa binadamu wapotovu. Vivyo hivyo, pia, kuna maneno ya unabii na ahadi za Mungu kwa mwanadamu, na kadhalika. Maneno haya yote ni maonyesho ya ukweli, njia na uzima. Yote ni ufunuo wa kiini cha maisha ya Mungu. Yanawakilisha tabia ya Mungu, na vyote Mungu anacho na alicho. Na hivyo, tunaweza kumwona kutoka kwa maneno yanayoonyeshwa na Mungu kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, na yana mamlaka, na nguvu. Hivyo, kama unatamani kuamua kama maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni sauti ya Mungu, unaweza kuangalia maneno ya Bwana Yesu na maneno ya Mwenyezi Mungu. Unaweza kuyalinganisha, na kuona kama ni maneno yanayoonyeshwa na Roho mmoja, na kama ni kazi ifanywayo na Mungu mmoja. Kama chanzo chao ni kimoja, basi hili linathibitisha kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni matamshi ya Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Mungu. Hebu tuangalie maneno yaliyonenwa na Yehova wakati wa Enzi ya Sheria, na maneno ya Yesu katika Enzi ya Neema. Yote mawili yalikuwa maonyesho ya Roho Mtakatifu moja kwa moja, na yalikuwa kazi ya Mungu mmoja. Hili linathibitisha kwamba Bwana Yesu Alikuwa kuonekana kwa Yehova, na kuonekana kwa Muumba. Wale ambao wamesoma Biblia wote wanajua kwamba ndani ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu wakati wa Enzi ya Neema, kulikuwa na maneno ya maonyo, maneno ya mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, na maneno ambayo yaliguzia amri za utawala za Mungu. Hivyo, pia, kulikuwa na maneno ya unabii na ahadi nyingi, na kadhalika. Haya yalikuwa hatua moja kamilifu ya kazi iliyotekelezwa na Mungu wakati wa Enzi ya Neema.

Kondoo wa Mungu husikia sauti Yake. Ijapo kwa jinsi ya kutambua sauti ya Mungu hasa, yote yatakuwa dhahiri tukiangalia maneno ya Bwana Yesu. Kwanza, tutaangalia mahitaji ya Bwana yesu na maonyo kwa mwanadamu. Kwa mfano, Bwana Yesu Alisema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). “Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda. Katika amri hizi mbili kumetundikwa torati yote na manabii(Mathayo 22:37-40). Bwana Yesu pia Alisema, “Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao. … Wamebarikiwa wale walio na njaa na kiu ya haki: kwa kuwa watapewa shibe” (Mathayo 5:3-6). “Wamebarikiwa wale wanaoteswa kwa sababu ya haki; kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao. Mmebarikiwa ninyi wakati wanadamu watakapowalaani, na kuwatesa, na kusema kila aina ya uovu dhidi yenu kwa udanganyifu. Shangilieni kwa sababu yangu, na kuweni na furaha nyingi: kwani thawabu yenu mbinguni ni kubwa(Mathayo 5:10-12).

Hebu tuangalie ni nini Bwana Yesu alisema kuhusu amri za utawala. Mathayo 12:31-32, Bwana Yesu alisema, “Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Vile vile, Mathayo 5:22 Bwana Yesu alisema: “Lakini mimi nawaambieni, Kwamba yeyote amkasirikiaye ndugu yake bila sababu atakuwa katika hatari ya kuhukumiwa: na yeyote atakayemwita ndugu yake mpumbavu, ana hatari ya kuikabili baraza: na yeyote atakayesema, Wewe mjinga, atakuwa na hatari ya kukumbana na moto wa kuzimu.

Kuongezea kwa maneno haya ya amri za utawala, kuna pia maneno ya Bwana Yesu yakiwahukumu na kuweka wazi Mafarisayo. Bwana Yesu Alisema, “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie(Mathayo 23:13). “Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko(Mathayo 23:15).

Bwana Yesu pia Alinena unabii mbalimbali na ahadi kwa mwanadamu. Katika Yohana 14:2-3, Bwana Yesu Alisema, “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia.” Kuna pia Yohana 12:47-48, Bwana Yesu pia Alisema, “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho.” Basi, pia, kuna Ufunuo 21:3-4: “Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita.

Kutoka kwa ukweli kadhaa ulioonyeshwa na Bwana Yesu katika kipindi cha Enzi ya Neema, tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu Alikuwa kuonekana kwa Mwokozi, na kwamba maneno ya Bwana Yesu yalikuwa matamshi ya Mungu kwa wanadamu wote. Yeye Alionyesha moja kwa moja tabia ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu, kumwongoza mwanadamu, na kumkimu mwanadamu, na kumkomboa mwanadamu Yeye binafsi. Jambo hili kabisa linawakilisha utambulisho na mamlaka ya Mungu Mwenyewe. Kuyasoma mara moja hutufanya tuhisi kwamba maneno haya ni ukweli, na yanamiliki mamlaka na nguvu. Maneno haya ni sauti ya Mungu, ni matamshi ya Mungu kwa mwanadamu. Wakati wa siku za mwisho, Bwana Yesu amerudi: Mwenyezi Mungu amekuja kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Ameanzisha Enzi ya Ufalme, na Amemaliza Enzi ya Neema. Kwa msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, Mwenyezi Mungu amefanya hatua ya kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu, na Ameonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa mwanadamu, Maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yana nema maudhui, na ni pana kabisa. Kama vile Mwenyezi Mungu Anasema, “Ni haki kusema kwamba hii ilikuwa mara ya kwanza tangu uumbaji kwa Mungu kuwahutubia wanadamu wote. Mungu hakuwa amewahi kuzungumza kwa wanadamu walioumbwa kinaganaga hivyo na kwa utaratibu sana. Bila shaka, hiyo pia ilikuwa mara ya kwanza Alipozungumza mengi hivyo, na kwa muda mrefu sana, kwa wanadamu wote. Ilikuwa ya kipekee kabisa. Na zaidi, matamshi haya yalikuwa maneno halisi ya kwanza yaliyoonyeshwa na Mungu miongoni mwa wanadamu ambapo Aliwafichua watu, akawaongoza, akawahukumu, na kuzungumza nao wazi wazi na kwa hiyo, pia, yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo kwayo Mungu aliwaruhusu watu wajue nyayo Zake, mahali Anapokaa, tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, mawazo ya Mungu, na sikitiko Lake kwa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba haya yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo Mungu alikuwa amezungumza kwa wanadamu kutoka mbingu ya tatu tangu uumbaji, na mara ya kwanza ambapo Mungu alikuwa ametumia utambulisho Wake wa asili kuonekana na kuonyesha sauti Yake kwa wanadamu katikati ya maneno(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Utangulizi). Sasa ni siku za mwisho, maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu huenea kotekote na yana ufahari usiolinganishwa. Ndani yao, hasa kuna hukumu, ufunuo wa mwanadamu, na maagizo ya utawala na amri za Enzi ya Ufalme, pamoja na maonyo, mahitaji na ahadi za Mungu kuelekea kwa mwanadamu, unabii, na kadhalika. Kisha, hebu kwanza tusome mafungu kadhaa ya maneno ya Mungu kuhusu maonyo ya Mungu na mahitaji Yake kwa mwanadamu pamoja na kazi Yake.

Mwenyezi Mungu anasema, “Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 19).

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Watu wakibaki katika Enzi ya Neema, basi hawatawahi kujiweka huru kutokana na tabia zao za upotovu, sembuse kujua tabia ya asili ya Mungu. Wanadamu wakiishi daima katika wingi wa neema ila hawana njia ya maisha inayowaruhusu kumjua Mungu na kumridhisha Mungu, basi kamwe hawataweza kumpata Mungu kwa kweli hata ingawa wanaamini Kwake. Hiyo ni aina ya imani ya kutia huruma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu).

Mwanadamu ameendelea kwa makumi ya maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia alipo leo. Hata hivyo, mwanadamu wa uumbaji Wangu wa asili kwa muda mrefu uliopita amezama katika upotovu. Tayari amecha kuwa kile Ninachotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, hawastahili tena jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, ambao Shetani amewateka nyara, maiti zilizooza zinazotembea ambamo Shetani huishi na huvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuja Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki kwa kweli katika furaha na huzuni za maisha pamoja na Mimi. Kwa vile wanadamu huniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, kuleta namna ya kujidekeza kwa yule aliye na madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, sembuse mapenzi Yangu kwa wakati wa sasa. Nitakuwa wazi na nyinyi nyote: Siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote ambaye huniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yenu Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—na hivyo, siku ya moto ikifika, kuteseka kwenu kutakuwa kali zaidi kuliko kule kwa Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kuliko kule kwa wale viongozi 250 waliompinga Musa, na kuliko kule kwa Sodoma chini ya moto mkali wa uharibifu wake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi).

Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Maangamizo ya mwisho ya wale wana wa uasi pia yatafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).

Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho).

Ni lazima ujue aina ya watu ambao Ninataka; wale walio najisi hawakubaliki kuingia katika ufalme, wale walio najisi hawakubaliki kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na umefanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mwovu kupindukia—hakuvumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba wewe unataka kuingia katika ufalme wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijatoa njia rahisi ya kuingilia ufalme Wangu kwa wale wenye neema Yangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja. Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe tu unatazamia tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea).

Kuhusu kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika kipindi cha Enzi ya Ufalme, hebu tusome mafungu kadhaa ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu).

Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. … Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Hebu tusome fungu la amri za utawala zilizotolewa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme.

Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii

1. Mwanadamu hapaswi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.

2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupaswi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.

3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu. Sadaka hizi hazifai kufurahiwa na binadamu yeyote ila kasisi na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu pekee ndiye Anayeweza kumgawia kasisi sadaka hizi, na hakuna mwingine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi. Sadaka zote zinazotolewa na mwanadamu (ikiwemo pesa na vitu vinavyoweza kufurahiwa) vinapewa Mungu, na sio kwa mwanadamu. Na hivyo, vitu hivi havipaswi kufurahiwa na mwanadamu; iwapo mwanadamu angevifurahia vitu hivi, basi angekuwa anaiba sadaka. Yeyote yule atakayefanya hili ni msaliti kama Yuda, kwa kuwa, zaidi ya Yuda kuwa msaliti. Yuda alijitwalia vilivyokuwa katika mfuko wa hela.

4. Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu bila kuwepo na mtu mwingine. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili.

5. Hupaswi kumhukumu Mungu, au kujadili kwa kawaida mambo yanayomuhusu Mungu. Unapaswa kutenda vile mwanadamu anavyopaswa kutenda, na kuzungumza jinsi mwanadamu anapasa kuzungumza, na hupaswi kuvuka upeo wako wala kuvuka mipaka yako. Uchunge ulimi wako na uwe mwangalifu na hatua zako. Yote haya yatakuzuia kufanya jambo lolote linaloweza kukosea tabia ya Mungu.

6. Unapaswa kufanya yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu, na kutenda wajibu wako, na kutimiza majukumu yako, na kushikilia jukumu lako. Kwa sababu unaamini katika Mungu, unapasa kutoa mchango wako kwa kazi ya Mungu; kama huwezi, basi wewe hufai kula na kunywa maneno ya Mungu, na hufai kuishi katika nyumba ya Mungu.

7. Katika kazi na mambo yanayohusiana na kanisa, kando na kumtii Mungu, katika kila kitu unapaswa kufuata maagizo ya mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata kosa lolote hata liwe dogo kivipi halikubaliwi. Lazima uwe mkamilifu katika kutii kwako, na hupaswi kuchunguza kati ya mazuri na mabaya; yaliyo mazuri au mabaya hayakuhusu. Unapaswa kujishughulisha tu na utiifu kamili.

8. Watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumtii na kumwabudu. Hupaswi kusifu au kumwabudu mtu yeyote; hupaswi kumpa Mungu nafasi ya kwanza, binadamu unayemheshimu nafasi ya pili, kisha wewe mwenyewe nafasi ya tatu. Mtu yeyote asishikilie nafasi yoyote moyoni mwako, na hufai kuzingatia watu—hasa wale unaowaenzi—kuwa katika kiwango sawa na Mungu, kuwa sawa na Yeye. Mungu hawezi kustahimili hili.

9. Mawazo yako yanapasa kuwa ya kazi ya kanisa. Unapaswa kuweka kando matarajio ya mwili wako, uwe na msimamo thabiti kuhusu mambo ya kifamilia, na ujitoe kwa moyo wako wote kwa kazi ya Mungu, na uiweke kazi ya Mungu kwanza kisha maisha yako katika nafasi ya pili. Huu ndio mwenendo mwema wa utakatifu.

10. Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani. Amri hii inaelekezwa kwa kila mwanadamu. Kuhusu hili jambo mnapaswa kuchunguza, mfuatilie na mkumbushane, na hakuna anayepasa kukiuka amri hii. Hata jamaa wako wasio wa imani yako wanapoingia kanisani shingo upande, hawapaswi kupatiwa jina jipya wala kupewa vitabu vya kanisa; watu kama hao si wa kaya ya Mungu, na kuingia kwao kanisani kunapaswa kukomeshwa kwa udi na uvumba. Iwapo matatizo yataletwa kanisani kwa sababu ya uvamizi wa mapepo, basi wewe mwenyewe utafukuzwa au kuwekewa vikwazo. Kwa ufupi, kila mmoja analo jukumu katika hili jambo, lakini pia hupasi kuwa asiyejali, wala kutumia jambo hili kulipiza kisasi cha kibinafsi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu Katika Enzi ya Ufalme Wazitii).

“Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Tutasoma vifungu vingine zaidi vya unabii wa Mwenyezi Mungu na ahadi Yake kwa mwanadamu: “Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hizi ni kazi Zangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20).

Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).

Sasa tumeyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu, tumeona kwamba Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni kitu kimoja Wote wawili ni Mungu mwenye mwili Akisimama juu na akinena kwa mwanadamu. Wanachofichua wote wawili ni tabia ya Mungu na kiini Chake takatifu. Na katika jambo hili, wanaonyesha kabisa mamlaka na utambulisho wa Mungu. Kutoka kwa maneno ya Bwana Yesu ya hukumu na ufunuo wa Mafarisayo na maneno ya Mwenyezi Mungu ya hukumu na ufunuo wa wanadamu wapotovu, tunaona kwamba Mungu huchukia dhambi, na hudharau upotovu wa mwanadamu. Tunaona tabia ya Mungu yenye haki na takatifu, na zaidi ya hayo, kwamba Mungu kwa makini huangalia ndani kabisa wa moyo wa mwanadamu. Upotovu wetu unajulikana sana Kwake kama kiganja cha mkono Wake. Kutoka kwa maonyo ya Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu na mahitaji ya mwanadamu, tunaona matarajio ya Mungu kwa mwanadamu, Mungu hupenda wale ambao ni waaminifu, na Yeye hubariki wale ambao hujitoa kwa kweli Kwake. Jambo hili hutuonyesha kujali kwa Mungu kwa, na wokovu wa mwanadamu. Kutoka kwa ahadi za Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu, tunaona upendo wa Mungu kwa mwanadamu, na, zaidi ya hayo, tunaona mamlaka na nguvu ambayo Mungu hutumia kuamuru jaala ya mwanadamu na hutawala vitu vyote. Matamshi ya Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu yanafanana kwa sauti na jinsi ya kuongea, yote ni maonyesho ya tabia ya Mungu Hili linadhibitisha kabisa utambulisho wa na kiini cha Mungu. Hebu tufikiri: Ni nani, mbali na Muumba, angeweza kuonyesha maneno kwa wanadamu wote? Ni nani angeweza kuonyesha mapenzi ya Mungu moja kwa moja, na afanye madai kwa mwanadamu? Ni nani angeamua mwisho wa mwanadamu? Ni nani angedhibiti iwapo wangeishi au kufa? Ni nani angethibiti nyota ulimwenguni, na kutawala vitu vyote? Mbali na Mungu, ni nani angebaini kiini cha upotovu wa mwanadamu? Na nani angefichua asili ya kishetani iliyofichwa ndani ya kina cha mioyo yetu? Ni nani angetimiza kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho na kutuokoa kabisa kutoka kwa ushawishi wa Shetani? Muumba pekee ndiye Amemiliki mamlaka na nguvu kama hizi! Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaonyesha kabisa mamlaka na utambulisho wake wa pekee. Baada ya kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu, sote tunahisi ule uthibitisho kama huo ndani ya mioyo yetu: Maneno haya yote yanaonyeshwa na Mungu, yote ni sauti ya Mungu. Yote ni ukweli ulioonyeshwa na Muumba wakati wa kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Ndani ya mioyo yetu, mara moja kunazaliwa uchaji wa kweli wa Mungu. Baada ya kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu, je, mna hisia ile ile? Jambo hili lathibitisha vya kutosha kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Bwana Yesu yanatoka katika chanzo kimoja. Yote ni maonyesho ya Roho mmoja. Ni matamshi ya Mungu mmoja kuelekea kwa wanadamu katika enzi tofauti. Wakati wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu hufanya kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu kwa msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli wote kwa ajili ya wokovu na utakaso wa mwanadamu, na Hufichua mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na hutuambia kwa dhahiri kuhusu kiini cha vipengele mbalimbali vya ukweli. Yanafungua macho yetu, na yanatushawishi kabisa. Neno la Mwenyezi Mungu na kazi Yake vimetimiza na kumaliza unabii wote wa Bwana Yesu. Katika maneno yote yaliyooyeshwa na Mwenyezi Mungu kwa kazi ya hukumu ya siku za mwisho, tunatambua sauti ya Mungu, na kuhakikisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu, Mungu mmoja pekee wa kweli Aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote, huja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Yeye huja kumaliza utawala wa Shetani duniani, enzi ya uovu na giza, na kukaribisha utawala wa Mungu duniani, Enzi ya Ufalme wa Milenia. Na hili huleta kweli matamanio yetu mazuri ya kuingia katika ufalme wa Mbinguni.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tutasikiaje sauti ya Mungu? Ubora wa sifa zetu au kadiri ya uzoefu wetu haujalishi katika jambo hili. Tukimuamini Bwana Yesu, tunasikia nini tunaposikia mengi ya maneno yake? Ingawa hatuna uzoefu na ujuzi wa maneno ya Bwana, wakati tunapoisikia tunasikia kuwa ni kweli, kwamba yana uweza na mamlaka. Hisia hii inatokeaje? Je, inazalishwa kutokana na uzoefu wetu? Ni athari ya msukumo na uelewa. Hii inatosha kuthibitisha kuwa watu wenye moyo na roho wote wanaweza kuhisi kwamba maneno ya Mungu yana nguvu na mamlaka; hii ni kusikia sauti ya Mungu. Hivyo kweli ndivyo ilivyo. Zaidi ya hayo, tofauti kubwa kati ya sauti ya Mungu na ya mtu ni kwamba sauti ya Mungu ni kweli na ina nguvu na mamlaka; tunaweza kuihisi mara tu tunapoyasikia. Kama tunaweza kuiweka katika maneno au la, hisia hiyo ni wazi. Ni rahisi kutambua sauti ya mtu au ya Shetani; papo hapo tunapoisikia ndipo tunahisi ni uwazaji wa kimantiki wa binadamu, dhana ya binadamu ambayo inaweza kufahamika na kueleweka. Hatujisiki nguvu hata kidogo au mamlaka katika maneno ya mwanadamu, na hata hatuwezi kuthibitisha kuwa ni kweli. Hii ni tofauti kubwa kati ya maneno ya Mungu na maneno ya mwanadamu. Kwa mfano, tunaona kwamba maneno ya Bwana Yesu yana nguvu na mamlaka; mara tu tunapoyasikia tunaweza kuthibitisha kuwa ni kweli, ni makubwa, ya ajabu, na zaidi ya kipimo cha mwanadamu. Hebu tuangalie maneno ya mitume katika Biblia. Haya hayafikii kabisa kiwango cha maneno ya Bwana Yesu. Hata ingawa yanayosema pia ni sawa, hata hivyo, hayana nguvu au mamlaka; ni mema tu na ya manufaa kwa mwanadamu. Je, si hii ndiyo tofauti kati ya maneno ya mitume na maneno ya Bwana Yesu? Je, mtu yeyote anaweza kusema maneno ambayo Bwana Yesu alisema? Hakuna mtu anayeweza. Hii inathibitisha maneno ya Bwana Yesu kuwa sauti ya Mungu. Je, mtu yeyote anayeamini katika Bwana Yesu anaweza kunena maneno ambayo mitume walinena? Kuna baadhi ambayo sisi pia tunaweza kuyanena. Je, si hilo linayatofautisha? Je, si ni rahisi kutofautisha kati ya sauti ya Mungu na ile ya mwanadamu?

Hebu tusome baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na kuona kama ni ukweli na sauti ya Mungu, sawa? Mwenyezi Mungu asema, “Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu, kana kwamba mtoto mchanga amezaliwa hivi karibuni. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye ‘Mlima wa Mizeituni’ wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni ‘mtoto mchanga’ Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni).

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.

…Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikiweka vitu vyote vilivyo na maumbo pamoja na mifano zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu—utapata uhuru wako Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele kali na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa majaaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimami dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, sisi sote tuna hisia sawa; tunaweza wote kuhisi kwamba huyu ni Mungu akizungumza na wanadamu. Mbali na Mungu, ni nani anayeweza kuzungumza na wanadamu wote? Nani anayeweza kuwaonyesha wanadamu nia ya Mungu ya kuokoa wanadamu? Nani anaweza kutangaza waziwazi kabisa kwa watu wote mpango wa Mungu kwa kazi Yake ya siku za mwisho na matokeo ya wanadamu na wanakoelekea? Ni nani anayeweza kutangaza kwa ulimwengu kwa amri za utawala? Mbali na Mungu, hakuna mtu aliyeweza. Mwenyezi Mungu anaongea na watu wote na kumruhusu mwanadamu kuhisi nguvu na mamlaka ya maneno ya Mungu; maneno ya Mwenyezi Mungu ni onyesho la moja kwa moja la Mungu, ni sauti ya Mungu! Maneno yote yaliyotamkwa na Mwenyezi Mungu ni kama kwamba Mungu amesimama juu ya mbingu ya tatu na anaongea na wanadamu wote; hapa Mwenyezi Mungu anasema kama Muumba kwa wanadamu, akiwaonyesha wanadamu tabia yake isiyoweza kukosewa ya haki na utukufu. Wakati ambapo kondoo wa Mungu wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu, ingawa hawaelewi ukweli wao mwanzoni, na ingawa hawana uzoefu wa maneno hayo, wanahisi kwamba kila neno la Mwenyezi Mungu lina nguvu na mamlaka na wanaweza kuthibitisha kuwa ni sauti ya Mungu na matamshi ya Roho wa Mungu. Wateule wa Mungu wanahitaji tu kusikia maneno ya Mungu ili kuthibitisha kuwa ni sauti Yake. Kwa nini wale wachungaji na wazee wa kanisa katika duru za dini wanamdhihaki Mwenyezi Mungu? Kwa wale wapinga Kristo mbalimbali ambao hawatambui mwili wa Mungu, na hawakubali kwamba Mungu anaweza kusema ukweli, ingawa wanaona ukweli wote ambao Mungu husema na kuhisi kwamba maneno Yake yana nguvu na mamlaka, bado hawaamini kwamba Mungu anaweza kusema kwa njia hii na hawakubali kwamba kila kitu ambacho Mungu anasema ni kweli. Nini suala hapa? Je, unaweza kujua? Mwenyezi Mungu aliyepata mwili katika siku za mwisho anaongea na watu wote, lakini wangapi kati yetu tunaweza kusikia sauti ya Mungu? Sasa hivi kuna wengi katika duru za kidini ambao wanaona Mwenyezi Mungu akizungumza, lakini hawawezi kutambua katika kusikia kwamba ni sauti ya Mungu; wao hata huchukulia maneno ambayo Mungu huongea kama maneno ya mwanadamu, na hata kufikia kiwango cha kutumia mawazo ya mwanadamu kumhukumu, kumtukana na kumshutumu. Je, watu hawa wana moyo unaoogopa Mungu? Je, si wao ni sawa na Mafarisayo wa zamani? Wote huchukia ukweli na kumhukumu Mungu. Maneno ya Mungu yana mamlaka makuu sana, nguvu nyingi, na hawasikii hata kidogo kwamba maneno haya ni sauti ya Mungu. Watu hao wanaweza kuwa kondoo wa Mungu? Mioyo yao imepofushwa; ingawa wanasikia, hawajui, na ingawa wanaona, wanashindwa kuelewa. Watu hao wanawezaje hata kustahili kunyakuliwa? Mungu aliyepata mwili katika siku za mwisho amesema ukweli, na kuwafichua watu katika duru za dini: Waumini wa kweli na wale wa uongo, wapendao ukweli na wale wanaouchukia, wanawali wenye hekima na wale wajinga. Watu wote kwa kawaida wamegawanyika, kila mmoja katika aina yake. Kama asemavyo Mwenyezi Mungu, “Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili). Hivyo, wale ambao wanaweza kusikia sauti ya Mungu wamekutana na kuja kwa mara ya pili kwa Bwana, na wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na wanahudhuria karamu ya ndoa ya Mwanakondoo. Watu hawa ni wanawali wenye busara, na walio na bahati zaidi kati ya wanadamu.

Ili kusikia sauti ya Mungu tunapaswa kusikiliza kwa moyo na roho. Akili zinazofanana zinaweza kuelewana kwa urahisi. Maneno ya Mungu ni ya kweli, yana uwezo na mamlaka; wale wenye moyo na roho wanaweza kuihisi kwa uhakika. Watu wengi, baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu kwa siku chache tu, wanaweza kuthibitisha kuwa ni sauti ya Mungu na maneno yake. Kila wakati Mungu anapopata mwili Anakuja kufanya hatua ya kazi; tofauti na manabii ambao, kwa maagizo ya Mungu, wanatumia maneno machache tu katika muktadha fulani. Wakati ambapo Mungu anapata mwili na kufanya hatua ya kazi Anapaswa kusema maneno mengi; Lazima atasema kweli nyingi, yataangaza siri na kusema unabii. Hii inahitaji miaka au hata miongo kukamilisha. Kwa mfano, katika kufanya kazi ya ukombozi, Bwana Yesu alihubiri kwanza “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17), na kumfundisha mwanadamu jinsi ya kukiri, jinsi ya kutubu, kusamehe, kuvumilia na jinsi ya kuteseka na kubeba msalaba wake, na vyote vinginevyo vinavyotengeneza njia ya mwanadamu katika Enzi ya Neema vinapaswa kufuata. Alionyesha tabia ya Mungu ya upendo na huruma, na kufunuliwa pia siri za ufalme wa mbinguni, na masharti ambayo kwayo tunaingia; Ilikuwa tu kwa kusulubiwa kwake, ufufuo wake na kupaa kwake mbinguni kwamba kazi ya Mungu ya ukombozi ilikamilishwa. Maneno yaliyosemwa na Bwana Yesu ni ukweli wote ambao Mungu amewapa watu katika kazi yake ya ukombozi. Katika siku za mwisho Mwenyezi Mungu amekuja, na akaeleza ukweli wote unaotakasa na kuwaokoa wanadamu. Amefanya kazi ya hukumu kuanzia na nyumba ya Mungu, na amefunulia kwa wanadamu hali yake ya haki na utukufu kama msingi wake. Amefunua siri zote za mpango wake wa usimamizi wa miaka sita elfu; Amefungua Enzi ya Ufalme na kumalizia Enzi ya Neema. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni matukio ya asili ya kiini cha maisha ya Mungu na onyesho la hali yake; hii ni hatua nzima ya kazi ya neno Mungu anafanya katika siku za mwisho ili kusafisha kabisa na kuokoa wanadamu. Hebu tusome baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na kusikia kama ni ukweli na yana uweza na mamlaka.

Mwenyezi Mungu asema, “Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. … Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, je, si sisi sote tumeelewa kwa uwazi zaidi kuhusu jinsi Mungu anavyofanya kazi yake ya hukumu katika siku za mwisho? Kama Mungu hangefunua na kusema jambo hili kwa wazi, tungewezaje kuwa na ufahamu wowote? Katika siku za mwisho Mwenyezi Mungu husema ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu. Maneno yake yanafunua kiini na hali halisi ya ufisadi mkubwa wa wanadamu; wao wanaangaza kabisa kila dhihirisho ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu na uharibifu wa mwanadamu na tabia ya shetani, na wanawaonyesha wanadamu tabia ya Mungu isiyoweza kukosewa ya utakatifu na uadilifu. Kwa hiyo watu wameona kuonekana na kazi ya Mungu, na wamegeukia kwa Mungu moja kwa moja, na wamekubali wokovu wa Mungu.

…………

Tumetambua kutokana na hukumu ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na asili ya Shetani ndani yetu ambayo inakataa na kumsaliti Mungu, na tumeona tamaa yetu, kiburi chetu na udanganyifu wetu na kwamba kwa kila namna tunasaliti tabia yetu ya kishetani. Ingawa huenda tukajitumia wenyewe, kuvumilia shida, na kujitolea kwa Mungu, tunamtumia Mungu na kufanya biashara na Yeye ili kupata tuzo na uingiaji katika ufalme wa mbinguni; sisi humtendea Mungu bila dhamiri au mantiki, bila upendo au utiifu hata kidogo. Je, tunafanana na wanadamu tunapoishi kwa namna hii? Tumekuwa tu mazimwi yaliyo hai, wanyama; tumeona ubaya wetu wa hawinde, na mioyo yetu ina maumivu makali kwa ajili ya hilo na imejawa na aibu. Katika ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu, tunaona kwamba Mungu anaona kila kitu, na tunaogopa na kutetemeka ndani ya mioyo yetu tunapohisi utakatifu wake mkubwa, utakatifu na kwamba tabia yake haiwezi kuwa na kosa. Tunahisi kuwa ingawa tuna tabia ya kishetani, tuna aibu kumwona Mungu, hatustahili kuishi mbele Yake, basi tunaanguka chini, kulia kwa toba, hata kujikemea wenyewe, na kupiga nyuso zetu wenyewe. tukiomba kwamba Mungu atatuhukumu kwa ukali zaidi, Atatutakasa na kutubadilisha; hatutaki tena kuishi na tabia ya Shetani. Tunaanza kutenda ukweli, na kufuatilia ukweli. Bila sisi kujua tumepitia mambo mengi, na tumeelewa ukweli fulani, na tumepata maarifa fulani ya kweli kumhusu Mungu. Badiliko katika njia yetu ya kuangalia mambo linatokea. Mabadiliko yanaanza kutokea katika tabia yetu ya maisha, na ndani ya moyo wetu kunadhihirika uchaji na utiifu wa kweli kwa Mungu; hatujaribu tena kufanya biashara na Mungu, tunaweza kufanya wajibu wa kulipa upendo wa Mungu kwa uaminifu na kuanza kuishi kama binadamu halisi. Baada ya kusafiri katika njia hii, tunahisi kwa kweli kuwa isingekuwa kwa sababu ya hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, Isingekuwa kwa ajili ya hukumu na adhabu ya maneno ya Mungu, hatungeweza kamwe kuona picha ya kweli ya ufisadi wetu wa kishetani, hatungeweza kamwe kujua chanzo cha dhambi zetu dhidi na kumpinga Mungu, sembuse kujua jinsi ya kujitenga na pingu za dhambi na utawala wake juu yetu katika kuwa watiifu kweli kwa Mungu. Isingekuwa kwa hukumu kali ya maneno ya Mungu, hatungeweza kujua tabia yake ya haki, ya heshima na isiyo na kosa; wala hatungeweza kukuza moyo unaoogopa Mungu, wala hatungeweza kuwa mtu anayeogopa Mungu na anaondokea uovu. Huu ni ukweli. Ikiwa Mungu hakupata mwili, ni nani aliyeweza kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Nani angeweza kumwonyesha mwanadamu tabia ya Mungu iliyo takatifu, yenye haki, na isiyo na kosa? Mungu asingepata mwili, maneno yake yangekuwa na nguvu na mamlaka kama hayo ya kuweza kutuhukumu, kututakasa, na kutuokoa kutoka katika ufisadi wetu mkubwa kwa dhambi? Ni maneno ya Mungu tu yana mamlaka na nguvu. yanaonyesha kabisa hali Yake na utambulisho kama Mungu, na kumwonyesha kuwa Muumba, na kuonekana kwa Mungu mmoja wa kweli! Tumetambua sauti ya Mungu katika maneno ya Mwenyezi Mungu, na kuona kuonekana kwa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp