Unyakuo kabla ya maafa ni nini? Ni nini mshindi anayekamilishwa kabla ya maafa?

13/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

“Kunyakuliwa” si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanaweza kufikiria; hiyo ni fikira potovu sana. “Kunyakuliwa” kunaashiria kujaaliwa Kwangu halafu kuchagua. Hii inawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale wote wataonyakuliwa ni watu waliopata hadhi ya wazaliwa wa kwanza, au wana, auwale ambao ni watu wa Mungu. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 104

Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!

…………

Leo Umefanya kamili makanisa yote—kanisa la Filadelfia—ambayo ni matunda ya miaka 6,000 ya mpango Wako wa usimamizi. Sasa watakatifu kwa unyenyekevu wanaweza kuwa watiifu mbele Yako; wao wameunganishwa pamoja katika roho na kuandama pamoja katika upendo. Wao wameunganishwa kwa chanzo cha chemchemi ya maji. Maji ya uhai ya maisha huenda bila mwisho na husafisha na kutakasa uchafu wote na taka katika kanisa, kwa mara nyingine tena yakitakasa hekalu Lako. Tumemjua Mungu wa ukweli wa vitendo, tumetembea ndani ya maneno Yake, tumetambua shughuli zetu na wajibu wetu wenyewe, na kufanya kila kitu tunachoweza kutumia kila rasilmali yetu kwa ajili ya kanisa. Tunapaswa kuchukua kila muda kuwa kimya mbele Yako na kutilia maanani kazi ya Roho Mtakatifu ili mapenzi Yako yasizuiwe ndani yetu. Miongoni mwa watakatifu kuna upendano, na nguvu za wengine zitafidia dosari za wengine. Tembea katika roho kila muda na upate nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu; fahamu ukweli na uuweke katika vitendo mara moja; kuwa sawa na nuru mpya na kufuata nyayo za Mungu.

…………

Shirikiana na Mungu kwa utendaji, tumikia kwa uratibu na kuwa moja, yakidhi mapenzi ya Mwenyezi Mungu, harakisha kuwa mwili mtakatifu wa kiroho, kanyaga Shetani, na kumaliza hatima yake. Kanisa la Filadelfia limechukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu na linajidhihirisha katika utukufu wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 2

Mungu Atakapokuja, watu wanapaswa kufurahia enzi Yake na hasira Yake, lakini haijalishi maneno Yake yalivyo makali, Anakuja kuokoa na kukamilisha binadamu. Kama viumbe, watu wanapaswa watekeleze wajibu ambao wanafaa kufanya, na kusimama shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji. Katika kila jaribio wanapaswa washikilie ushahidi ambao wanapaswa washuhudie, na kushuhudia ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Huyu ni mshindi. Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wa binadamu unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi. Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. Kazi inapotekelezwa katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vizuizi vya kupita kiasi, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa katika wakati ufaao: ndiyo maana, watu husafishwa kwa ajili ya neno la Mungu. Hiki pia ni kipengele cha mateso. Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

Mwanadamu atakamilishwa kabisa katika Enzi ya Ufalme. Baada ya kazi ya ushindi, mwanadamu atapitishwa kwenye mambo magumu ya kusafishwa na taabu. Wale ambao wanaweza kushinda na kushuhudia katika taabu hii ndio hatimaye watakaofanywa wakamilifu; wao ndio washindi. Katika taabu hii, mwanadamu anahitajika kukubali kusafishwa huku, na kusafishwa huku ndio tukio la mwisho la kazi ya Mungu. Itakuwa mara ya mwisho ambapo mwanadamu atasafishwa kabla ya hitimisho la kazi zote za usimamizi wa Mungu, na wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakubali jaribio hili la mwisho, lazima wakubali kusafishwa huku kwa mwisho. Wale ambao wamekabiliwa na taabu ni wale wasiokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na uelekezi wa Mungu, lakini wale ambao wameshindwa kwa kweli na wanatafuta mapenzi ya Mungu kwa kweli hatimaye watasimama imara; ndio wale ambao wana ubinadamu, na wanaompenda Mungu kwa kweli. Bila kujali Mungu hufanya nini, hawa washindi hawatapungukiwa na maono, na bado watauweka ukweli katika matendo bila kufeli katika ushuhuda wao. Wao ndio watakaosimama mwishowe kutoka kwenye taabu kubwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Nimesema hapo awali kuwa kikundi cha washindi wanapatwa kutoka Mashariki, washindi ambao wanatoka katika mashaka makubwa. Je maneno haya yana maana gani? Yanamaanisha kuwa watu hao ambao wamepatwa waliamini kwa kweli tu baada ya kupitia hukumu na kuadibu, na kushughulikiwa na kupogolewa, na aina yote ya usafishaji. Imani ya watu kama hao si isiyo dhahiri na dhahania, bali ni ya kweli. Hawajaona ishara na maajabu yoyote, ama miujiza yoyote; hawazungumzi kuhusu barua ngumu kueleweka na kanuni, ama mitazamo ya muhimu sana; badala yake, wana ukweli, na maneno ya Mungu, na maarifa ya kweli kuhusu ukweli wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Wale ambao Mungu atawaokoa wanarudishwa kwa makundi. Kundi la kwanza ni wale kutoka China bara; kundi la pili ni wale walio ng’ambo. Wale walio ng’ambo sasa wanaanza kumgeukia Mungu. Kundi la tatu ni wale ambao, baada ya maafa makubwa kufika, watagutuka na kurudi mbele za Mungu katikati ya maafa hayo. Wale ambao watanyakuliwa na kurudi mbele za Mungu kabla ya maafa ni wengi. Sasa hivi, kazi ya kunyakuliwa kabla ya maafa makubwa inafika tamati upesi. “Inafika tamati upesi” inamaanisha nini? Mbona niseme hivi? Ni kwa sababu maafa makubwa yanafika punde. Maafa makubwa yakifika katika miaka miwili, wale wanaomrudia Mungu katika miaka hii miwili pia watafikiriwa kama sehemu ya kundi linalonyakuliwa kabla ya maafa. Kuhusu wale wasiomrudia Mungu wakati wa miaka hii miwili, watu wengine wanaeneza injili kwao na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, lakini wanakana kabisa, “Hii si sahihi, haiwezekani! Sitaamini chochote ambacho sijaona mimi mwenyewe.” Bila kujali kile ambacho wengine wanaweza kusema, bado wanakataa kuikubali. Mungu atawaweka watu hawa katikati kabisa ya maafa. Atatumia maafa hayo kuwasafisha na kuwaadhibu, ili wawe wakilia na kusaga meno yao katikati ya maafa hayo, ndani ya giza.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

“Kwa nini unamwamini Mwenyezi Mungu; ni nini maana ya kumwamini Mwenyezi Mungu?” Hili ni muhimu kuelewa. Watu wengine hutafakari: “Mwanzoni nilimwamini Bwana Yesu. Sasa nimesikia ushuhuda wazi dhahiri wa ukweli wa Biblia kutoka kwa wainjilisti wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hasa, nimesikia matamshi ya Mwenyezi Mungu, ambayo yote ni ukweli na naweza kusikia ni sauti ya Mungu. Yametimiza kabisa kile ambacho kimeandikwa katika Ufunuo: ‘Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo 2:7). Baada ya kusikia matamshi yote ya Mwenyezi Mungu, nimedhibitisha jambo moja: Bwana Yesu amerudi, na Yeye ni Mwenyezi Mungu.” Sisi waumini wa Mwenyezi Mungu ni wa kundi la watu watakaonyakuliwa na Bwana. Hili limetimiza kabisa unabii wa Bwana Yesu katika Biblia: “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6), and “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). “Tazama, mimi nakuja kama mwizi. Amebarikiwa yeye anayekesha, na kuzihifadhi nguo zake, asije akatembea uchi, na wao waione haya yake(Ufunuo 16:15). Kwa kuwa unabii wa Bwana umetimizwa, sasa tunakula chajio na Bwana. Katika Biblia, Bwana Yesu alikiita “chajio cha harusi cha Mwanakondoo.” Ni nini maana ya “chajio cha harusi cha Mwanakondoo”? Kwa nini kinaitwa “chajio cha harusi cha Mwanakondoo”? “Mwanakondoo” ni Kristo, na harusi ya Mwanakondoo inamaanisha kwamba Kristo anakuja kukamilisha kundi la watu. Atawafanya kondoo Wake, wale ambao waliamuliwa kabla na Yeye kuwa washindi kabla ya maafa, kwa hiyo huku kunaitwa “kuhudhuria chajio.” “Harusi” ni kupata, na baada ya hapo tunakuwa familia. Kwa hiyo, maelezo mengine ya mahubiri haya yanamtaja Kristo kama bwana harusi, na kanisa kama bibi harusi. Hii inaitwa harusi, na ni kupata kitu. Kuzungumzia kupata, hii inahusu kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho, ambayo ni kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Kupitia kazi hii kunamaanisha kwanza kushindwa na Mungu, na baada ya hapo kutakaswa, kukamilishwa, kupatwa na kufanywa kuwa kamili; kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu ni kazi kama hiyo. Baada ya watu kupitia kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kulingana na Kristo, kazi ya Mungu kuanzia katika nyumba ya Mungu inafika mwisho basi. Punde linapokamilishwa, kundi la watu waliofanywa kamili ni kundi la washindi ambao wameundwa kabla ya maafa. Nafasi ya washindi katika ufalme wa Mungu ni ipi? Wao ndio nguzo za ufalme wa Kristo. Hawa washindi waliofanywa na Mungu kabla ya maafa watakuwa nguzo za ufalme wa Kristo. Hufikiri ni baraka kubwa mno? Hii ni baraka kubwa mno.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp