Tunaamini kwamba kurudi kwa Bwana kutamaanisha kwamba waumini wanainuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni, kwa maana imeandikwa katika Biblia: “Baada ya hayo sisi ambao tuko hai na kusalia tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa: na hivyo tutakuwa naye Bwana daima” (1 Wathesalonike 4:17). Unashuhudia kuwa Bwana Yesu amerejea, hivyo ni kwa nini sisi sasa tuko duniani na bado hatujanyakuliwa?

07/06/2019

Jibu:

Tunapaswa kutarajia kurudi kwa Bwana kulingana na unabii ambao Yeye Mwenyewe aliuzungumza. Hiyo ndiyo njia ya kawaida kabisa ya kusubiri kurudi kwa Bwana. Unamnukuu nani, kwa hakika? Je, unanukuu maneno ya Bwana au maneno ya wanadamu? “Baada ya hayo sisi ambao tuko hai na kusalia tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa,” ni nani aliyasema hayo? Je, hayo ni maneno ya Bwana Yesu? Bwana Yesu hajawahi kamwe kusema kitu chochote kama hicho. Roho Mtakatifu hakuwahi kamwe kusema hilo, pia. Maneno unayoamini na unayonukuu ni maneno ya Paulo. Je, maneno ya Paulo yanawakilisha maneno ya Bwana Yesu? Je, anaweza kumwakilisha Mungu? Ni Mungu pekee anayejua jibu la fumbo hili. Ikiwa sisi wanadamu waovu tunaweza kuthubutu kufanya ufasili na hukumu bila kufikiria namna hii, hilo ni tatizo kubwa. Paulo hakuwa Kristo. Alikuwa tu mtu mwovu wa kawaida Maandishi yake yamejawa na mawazo na fikra za mwanadamu. Maneno yake si ukweli, hivyo hatuwezi kuyatumia kama uthibitisho. Uthibitisho wote unapaswa kuzingatia maneno ya Mungu katika Biblia. Hilo linaambatana na ukweli. Si sawa kuchunguza kunyakuliwa na kuingia katika ufalme wa mbinguni kwa kuzingatia maneno ya watu kwenye Biblia, hasa Paulo, na sio kwa kuzingatia maneno ya Bwana Yesu kwa sababu maneno ya Bwana Yesu pekee ndiyo ukweli; maneno Yake pekee ndiyo yenye mamlaka. Bwana Yesu pekee ndiye Kristo, Mfalme wa ufalme wa mbinguni. Kwa nini usitafute ukweli na mapenzi ya Mungu katika maneno ya Bwana Yesu? Ni kwa nini badala yake unatumia maneno ya wanadamau kama msingi wa upekuzi wako? Je, hili linaambatana na mapenzi ya Bwana? Hili linaweza kukufanya umfuate mwanadamu na utembee katika njia yako mwenyewe. Mungu alimuumba mwanadamu kutokana na udongo wa ardhi. Aliwapa kazi ya kufanya jukumu lao duniani, ambalo ni kusimamia wale viumbe Wake wengine duniani. Aliwaagiza wamtii, wamwabudu, na kumuheshimu wakiwa duniani, na kuamuru kuwa hatima yao ilikuwa duniani, wala sio mbinguni. Zaidi ya hayo, Mungu alituambia zamani kuwa Ataanzisha ufalme Wake duniani. Ataishi nasi wanadamu duniani na falme za dunia ni lazima zibadilishwe kuwa falme zinazotawalwa na Kristo. Kwa hivyo, ufalme wa Mungu hatimaye utaanzishwa duniani, wala si mbinguni. Watu wengi kila wakati wanatazamia kuinuliwa kuingia mbinguni. Hayo ni mawazo na fikra zao, shauku yao wenyewe ya kubuni. Haliambatani hata kidogo na ukweli au ukweli wa kazi ya Mungu.

Hebu tuone kile ambacho Bwana Yesu alisema: “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni(Mathayo 6:9-10). Bwana Yesu alituambia wazi kuwa ufalme wa Mungu uko duniani, na sio mbinguni. Mapenzi ya Mungu yatatimizwa duniani kama huko mbinguni. Hebu tusome kutoka kwa Ufunuo 21:2-3: “Na mimi Yohana nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukija chini kutoka kwa Mungu mbinguni…. Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao.” Hebu tufungue Ufunuo 11:15, “Falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele.” Unabii huu ulitaja, “Hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu,” “… Yerusalemu mpya, ukija chini kutoka kwa Mungu mbinguni,” “Falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake.” Hili linathibitisha kuwa Mungu atajenga ufalme Wake duniani, na ataishi duniani pamoja na wanadamu. Falme zote za ulimwengu zitakuwa falme za Kristo, na zitadumu milele. Ikiwa tunaamini ufalme wa mbinguni uko mbinguni kulingana na fikra na mawazo yetu wenyewe, tunaamini kuwa Bwana atakaporudi atatuchukua juu kuingia mbinguni, je, maneno Yake ya awali si yatakuwa ya bure? Ndiyo. Kwa kweli, matokeo ya mpango wa Mungu wa usimamizi wa kuokoa wanadamu ni kuanzishwa kwa ufalme wa Mungu duniani. Mwenyezi Mungu—Kristo wa siku za mwisho—hufanya kazi Yake ya kuhukumu na kutakasa binadamu ili kufanya kikundi cha washindi duniani. Wale wanaopokea wokovu wa Mungu, hufanywa kuwa kamili na kuwa washindi ndio wanaweza kutenda maneno ya Mungu na kufuata njia Yake duniani. Wao ndio watu wa ufalme Wake. Baada ya washindi hawa kufanywa, mapenzi ya Mungu yatatimizwa duniani. Kisha ufalme wa Kristo utaanzishwa duniani, na Mungu atapata utukufu kamili. Mwishowe, Atatimiza unabii ulioko katika Kitabu cha Ufunuo. Je, bado hatuelewi ukweli huu kwa waziwazi? Ni mahali gani ambapo tumetayarishiwa na Bwana Yesu? Aliamuru kuwa tungezaliwa katika siku za mwisho, tukutane na Yeye duniani Atakaporudi, tukubali utakaso wa Mungu na tufanywe kamili, na tuwe washindi ili tufanye mapenzi ya Mungu, na falme zote duniani zitafanywa kuwa falme za Kristo. Hayo ni mapenzi ya Mungu. Mungu anakuja duniani lakini tunajaribu kwenda juu mbinguni. Kwa kufanya hivi, je, si tunakwenda kinyume cha kazi ya Mungu na mapenzi Yake? Akituinua juu angani, naam, humo hamna chakula na hakuna mahali pa kuishi, tutaishi vipi? Je, hizo zote si ni fikra na mawazo yetu tu? Je, Bwana angefanya kitu kama hicho? Ukweli kuwa tunaweza kufikiria hivyo, inaonyesha kuwa hakika tuna utoto. Hatuna uhalisia bali ni kama tu tunaota!

Ufalme wa Mungu utajengwa duniani katika siku za mwisho. Hatima ya mwisho ya mwanadamu itakuwa duniani, sio mbinguni. Hili limeamuriwa na Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi ndani ya mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuwaongoza binadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. Mungu hataishi tena miongoni mwa binadamu, na mwanadamu pia hataweza kuishi na Mungu katika hitimisho la Mungu. Mungu na mwanadamu hawawezi kuishi ndani ya ulimwengu sawa; badala yake, wote wawili wana njia zao binafsi za kuishi. Mungu ndiye anayeongoza binadamu wote, wakati binadamu wote ni matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Ni binadamu wanaoongozwa; kuhusu kiini, binadamu si sawa na Mungu. Kuingia rahani kunamaanisha kurudi pahali pa awali pa mtu. Kwa hivyo, Mungu aingiapo rahani, kunamaanisha kwamba Mungu amerudi pahali Pake pa awali. Mungu hataishi tena duniani ama kushiriki kwa furaha na mateso ya binadamu wakati yupo miongoni mwa binadamu. Binadamu wanapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; binadamu watamwabudu Mungu wakiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na binadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Wakati binadamu wanamwabudu Mungu katika pumziko, wataishi duniani, na wakati Mungu anaongoza sehemu iliyobaki ya binadamu katika pumziko, Atawaongoza kutoka mbinguni, sio kutoka duniani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). Mwenyezi Mungu ametuambia waziwazi kuwa kazi Yake ya usimamizi itakapoisha, Mungu na mwanadamu wataingia mapumzikoni. Mahali pa Mungu pa mapumziko ni mbinguni, na mahali petu wanadamu pa pumziko bado ni duniani. Lakini basi, Mungu atawaongoza watu waliobaki kuishi duniani. Hii ndiyo hatima nzuri ambayo Mungu ametutayarishia sisi wanadamu. Ndio ufalme wa Mungu pia uliotimizwa duniani. Tukimwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini bado hatuwezi kuona hili, je, hiyo haimaanishi kuwa hatuelewi ukweli au maneno ya Bwana?

Naam, kunyakuliwa hakika ni nini? Watu wengi hawaelewi hilo vizuri. Fumbo la kunyakuliwa kwa watakatifu lilifichuliwa tu Mwenyezi Mungu alipowasili. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Kunyakuliwa’ si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanaweza kufikiria; hiyo ni fikira potovu sana. ‘Kunyakuliwa’ kunaashiria kujaaliwa Kwangu halafu kuchagua. Hii inawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale wote wataonyakuliwa ni watu waliopata hadhi ya wazaliwa wa kwanza, au wana, auwale ambao ni watu wa Mungu. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 104). Maneno ya Mwenyezi Mungu ni wazi sana. “Kunyakuliwa” sio kile ambacho tunafikiria—kuinuliwa angani kutoka ardhini na kumlaki Bwana mawinguni. Wala sio kuinuliwa kuingia mbinguni. Kunamaanisha kuwa Mungu atakaporudi duniani kuzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake, tutasikia sauti ya Mungu na tutaweza kumfuata na kutii kazi Yake katika siku za mwisho. Hii ndiyo maana ya kweli ya kunyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Wote ambao wanaweza kutofautisha sauti ya Bwana, kupata ukweli katika maneno ya Mwenyezi Mungu, kukubali ukweli, na kurudi kwa Mwenyezi Mungu ndio wananawali werevu. Wao ndio dhahabu, fedha na mawe yenye thamani ambayo “yameibwa” na Bwana na kurudishwa kwa nyumba Yake kwa sababu wote ni wa kipimo kizuri cha tabia na wanaweza kuelewa na kukubali ukweli. Wanaweza kuelewa sauti ya Bwana. Wao ndio ambao hakika wamepokea kunyakuliwa. Wao ndio washindi ambao watafanywa wakati Mungu atakapofanya kazi Yake Atakaposhuka kisiri duniani katika siku za mwisho. Tangu Mwenyezi Mungu aanze kazi Yake ya siku za mwisho, watu wengi zaidi na zaidi ambao wana kiu ya kuonekana kwa Bwana wametambua sauti Yake katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Mmoja baada ya mwingine, wamekubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ili kumlaki uso kwa uso na wamekubali kunyunyiziwa na kulishwa na maneno Yake. Wamepata ufahamu wa kweli wa Mungu. Tabia zao potovu zimetakaswa na wameweza kudhihirisha uhalisi wa ukweli katika maneno ya Mungu. Tayari wamepokea wokovu tele wa Mungu. Watu hawa tayari wamefanywa washindi kabla ya majanga makubwa kuwasili. Wamepatwa na Mungu kama malimbuko. Wale wanaoshikilia fikra na mawazo yao wenyewe na wanaosubiri bila kufikiria kurudi kwa Bwana ili Awachukue juu kuingia mbinguni, wao ambao hukataa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ndio wanawali wajinga. Wao ndio ambao watatelekezwa na Mungu. Hatima yao ni kuteseka katika majanga; watalia na kusaga meno yao. Huu ni ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tunapaswa kuelewaje “unyakuo”? Tunatumia unyakuo kuelezea jinsi Mungu humwokoa mwanadamu kutoka kwa hali hili na chini ya utawala huu na kumweka katika hali hiyo na chini ya utawala huo. Hata hivyo, wakati wowote watu hufikiri kuhusu “unyakuo”, wanaiona tu kama kubebwa juu hewani. Je hili si kosa? Iwapo, kwa mfano, ulizaliwa katika kijiji chenye maendeleo kidogo mno, cha mbali na kufuatia hilo ulipewa kazi katika mji mkubwa, tunapaswa kueleza hili katika lugha ya binadamu kama kuwa umepandishwa cheo kutoka kwa kijiji cha mbali kufanya kazi na kuishi katika mji mkubwa, Je, hii si maana ya “kupandishwa cheo”? Je kupandishwa cheo huku ni tofauti na kuinuliwa hewani kama mwanadamu anavyodhani? Je, lipi kati ya haya ni uhalisi? Hiyo ndiyo maana tunasema kwamba “unyakuo” inamaanisha kuinuliwa kutoka kwa aina moja ya hali hadi katika aina nyingine ya hali—huku ni kupandishwa cheo! Kupandishwa cheo huku sio kuinuliwa kutoka kwa ardhi, ama kuinuliwa kutoka kwa ardhi hadi angani, hakumaanishi hivyo. Badala yake, kunamaanisha kuinuliwa juu katika cheo cha juu zaidi, hadi kwa nafasi ya juu zaidi, hata nafasi ya tabaka la juu zaidi. Huku ni kupandishwa cheo. Kwa mfano, kwa asili tulikuwa wakulima wadogo na wafanyikazi kutoka kwa kiwango cha chini zaidi cha wanadamu wapotovu, bila hadhi yoyote katika jamii, tulioangaliwa kwa dharau na wengine, tukipitia ukandamizaji na unyonyaji, bila haki ya kuongea, na sasa kwa mkupuo tunainuliwa kaka watu wa Enzi ya Ufalme, je nafasi hii siyo kupandishwa cheo? Kwa asili, tulikuwa wanadamu wapotovu, wanadamu wa kiwango cha chini zaidi katika dunia ya giza, ovu, na sasa ghafla tunainuliwa katika kunyakuliwa kuwa watu wa ufalme wa Mungu, watu ambao ni wananchi wa Enzi ya Ufalme. Iwapo tunainuliwa kuwa watu wa Enzi ya Ufalme, je huku si kunyakuliwa? Huku ni kunyakuliwa hakika. Haya, wengine husema: “Je, siishi hapo bado? Sifanyi kazi hiyo bado? Si kile ninachokula na kuvaa hakijabadilika hata kidogo bado? Ni vipi sihisi niko juu sana?” Iwapo umeinuliwa katika kunyakuliwa au la haiwezi kuamuliwa na jinsi unavyohisi kuwa juu au chini. Siku itakapokuja ambapo ukweli huu utafichuliwa, yule unayemwamini kuwa wa juu atang’olewa, na ingawa unaweza kufikiri hujapata chochote, utaendelea kuishi; Utaelezaje hilo? Maana hii ya watu wa ufalme ni kweli, siyo? Siku moja itafika ambapo ukweli huu utathibitishwa. Wakati huo utasema: “Aa, kwa kweli nimeinuliwa katika kunyakuliwa, lakini sina ufahamu wa hilo, kazi ya Mungu ni ya ajabu sana.” Iwapo hawana ukweli, watu hawatafahamu kunyakuliwa huku, wataishi katika neema bila kujua neema. Hii ndiyo maana ya vitendo ya kunyakuliwa; unapaswa kuelewa hilo. Mungu hukulinda na hakuna maafa yatakayokufikia; je, hili halielezi kwamba sasa tayari umeinuliwa juu katika kunyakuliwa, kwamba ninyi ni wateule wa Mungu, watu wa Enzi ya Ufalme? Je, unaweza kueleza swali hili? Siku moja utakubali kwamba “Huu ni ukweli, hadhi yangu hakika ni tofauti. Ingawa watu katika dunia hunichukulia kama bado mfanyikazi ama mkulima mdogo, machoni pa Mungu mimi ni mtu wa Enzi ya Ufalme; kwa hivyo kwa kweli nimeinuliwa juu katika kunyakuliwa na tayari ninafurahia neema ya kunyakuliwa.” Hii ndiyo maana ya utendaji ya unyakuo. Iwapo huelewi ile inayoitwa unyakuo na ukitegemea fikira zako mwenyewe unaamini kwamba unyakuo ni kuinuliwa hewani, hivyo, wewe subiri tu kuinuliwa juu hewani basi.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp