Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa

Kazi ya watendaji huduma ilikuwa hatua ya kwanza katika kazi ya ushindi. Leo ndiyo hatua ya pili katika kazi ya ushindi. Kwa nini kukamilishwa kunatajwa pia katika kazi ya ushindi? Ni ili kujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye. Leo ndiyo hatua ya mwisho ya kazi ya ushindi; wakati wa kupitia dhiki kuu, ambao utaashiria mwanzo rasmi wa kuwakamilisha wanadamu, utafuata. Swala kuu sasa ni ushindi, lakini sasa pia ndio wakati wa hatua ya kwanza katika mchakato wa kukamilishwa. Kile ambacho hatua hii ya kwanza inahitaji ni kukamilisha maarifa na utii wa watu, ambavyo bila shaka vinaunda msingi wa kazi ya ushindi. Ili uweze kukamilishwa, basi lazima uwe na uwezo wa kusimama imara katikati ya dhiki ya siku za baadaye na kujitolea kabisa ili ueneze hatua inayofuata ya kazi; hii ndiyo maana ya kukamilishwa, na wakati kama huo pia ndio wakati ambapo watu wanapatwa kabisa na Mungu. Leo tunazungumza kuhusu kushindwa, ambako ni sawa na kuzungumza kuhusu kukamilishwa. Lakini kazi ambayo inafanywa leo ndiyo msingi wa kukamilishwa katika siku za baadaye; ili kukamilishwa, lazima watu wapitie dhiki, na uzoefu huu wa dhiki lazima uwe na msingi wake katika kushindwa. Ikiwa watu hawana msingi wa leo—ikiwa hawajashindwa kabisa—basi itakuwa vigumu kwao kusimama imara wakati wa hatua inayofuata ya kazi. Kushindwa pekee si kusudi la msingi. Lakini ni hatua moja tu ya ushuhuda kwa ajili ya Mungu wanapokabiliwa na Shetani. Kukamilishwa ndilo kusudi la msingi, na usipokamilishwa, basi unaweza pia kuchukuliwa kama kitu kisicho na thamani tena. Wakati tu unapokabiliwa na dhiki katika siku za baadaye ndipo kimo chako cha kweli kitakapoonekana; ambako ni kusema, ni wakati huo tu ndipo kiwango cha utakatifu wa upendo wako kwa Mungu kitakapokuwa dhahiri. Kile ambacho watu wanasema leo ni hiki: “Lazima tumtii Mungu bila kujali Anachofanya. Kwa hiyo tuko tayari kuwa foili[a] ambao wanaweza kudhihirisha nguvu kuu za Mungu na tabia ya Mungu. Iwe Mungu ni mwema kwetu au Yeye hutulaani, au iwe Yeye hutuhukumu, bado tunamshukuru Mungu.” Kwamba unasema hivi kunaonyesha tu kuwa una ufahamu kidogo, lakini kama ufahamu kama huo unaweza kutumika kwa kweli kunategemea kama ufahamu huu ni halisi au la. Kwamba watu wanao utambuzi na ufahamu kama huu leo ni matokeo ya kazi ya ushindi. Kama unaweza kukamilishwa au la kunaweza kuonekana tu unapokabiliwa na dhiki, na wakati huo itaonekana kama unampenda Mungu kwa kweli kwa dhati. Ikiwa upendo wako ni safi kwa kweli, basi utasema: “Sisi ni foili, sisi ni viumbe walio mikononi mwa Mungu.” Unapoieneza injili kwa watu wa mataifa, utasema, “Ninafanya huduma tu. Kwa kutumia tabia potovu zilizo ndani mwetu, Mungu amesema mambo haya yote ili Atuonyeshe tabia Yake yenye haki; Asingesema mambo kama haya, hatungeweza kumwona Mungu, wala kuelewa hekima Yake, wala kupokea wokovu mkubwa kama huu na baraka kubwa kama hizi.” Ikiwa kwa kweli una utambuzi kama huo, basi hii inatosha. Hata hivyo, hujali mambo mengi unayosema leo, nawe unaongea maneno matupu tu kwa sauti kubwa: “Sisi ni foili, watendaji huduma, tunatamani kushindwa, kuwa na ushuhuda mkubwa sana wa Mungu….” Haitoshi kusema kwa sauti tu—kusema kwa sauti hakuthibitishi kuwa una kimo; lazima uwe na ufahamu wa kweli, na lazima ufahamu wako ujaribiwe.

Kumbuka yale ambayo umepitia katika kipindi hiki cha wakati, na angalia tena maneno ambayo Nimeonyesha katika wakati huu, na uyalinganishe na yale ambayo umefanya. Ni kweli kabisa kuwa wewe ni foili kabisa! Je, kiwango cha ufahamu wako ni kipi leo? Fikira zako, mawazo yako, tabia yako, maneno na matendo yako—si kila kitu unachoonyesha katika namna unavyoishi ni foili kwa haki na utakatifu wa Mungu? Si kile kinachofunuliwa katika maneno ya leo ni tabia potovu ya mwanadamu? Fikira zako, motisha yako—yote ambayo yamefunuliwa ndani yako yanaonyesha tabia ya Mungu yenye haki na utakatifu Wake. Mungu pia Alizaliwa katika nchi ya uchafu, lakini Anabaki kutopakwa matope na uchafu. Anaishi katika ulimwengu huo huo mchafu kama wewe, lakini Anayo mantiki na utambuzi, naye huchukia uchafu. Huenda usiweze hata kugundua kitu chochote kilicho kichafu katika maneno na vitendo vyako, lakini Yeye anaweza, na Yeye hukuonyesha kitu hicho. Mambo hayo yako ya zamani—ukosefu wako wa ukuzaji, utambuzi, na akili, na njia zako za kuishi za kuelekea nyuma—sasa vimedhihirishwa na ufunuo wa leo; ni kwa Mungu kuja duniani kufanya kazi tu ndipo watu wanaona utakatifu Wake na tabia Yake yenye haki. Yeye hukuhukumu na kukuadibu, Akikusababisha upate ufahamu; wakati mwingine, asili yako ya kishetani inadhihirishwa, na Yeye hukuonyesha asili hiyo. Anajua kiini cha mwanadamu vyema sana. Yeye huishi kama unavyoishi, Yeye hula chakula kile kile kama wewe, naye Anaishi katika nyumba ileile—lakini Yeye anajua zaidi. Hakuna kitu Yeye hudharau zaidi ya falsafa za kuishi na udanganyifu na usaliti wa mwanadamu; Yeye anadharau mambo haya na hataki kuyatilia maanani hata kidogo. Anachukia hasa maingiliano ya kimwili ya mwanadamu. Huenda Asijue baadhi ya mazoea ya maingiliano ya binadamu, lakini Anajua kabisa watu wanapofichua tabia potovu. Yeye hufanya kazi ili kuongea na kumfundisha mwanadamu kupitia mambo haya, Yeye hutumia mambo haya ili Awahukumu watu, na kuonyesha tabia Yake mwenyewe yenye haki na takatifu. Hivyo, watu wanakuwa foili kwa kazi Yake. Ni Mungu mwenye mwili tu ndiye Anayeweza kuweka wazi tabia potovu za mwanadamu na sura zote mbaya za Shetani. Kwa kufanya hivi, Yeye hakuadhibu, lakini badala yake Anakutumia tu kama foili kwa ajili ya utakatifu Wake, na huwezi kusimama imara, kwa sababu wewe ni mchafu sana. Yeye huzungumza Akitumia mambo hayo ambayo yamefunuliwa ndani ya mwanadamu, na ni wakati ambapo mambo haya yanawekwa wazi tu ndipo watu wanajua jinsi Mungu alivyo mtakatifu. Yeye hapuuzi uchafu hata kidogo ndani ya watu, hata mawazo machafu yaliyo mioyoni mwao; ikiwa maneno na matendo ya watu hayapatani na mapenzi Yake, basi Yeye hawasamehei. Katika maneno Yake, hakuna nafasi ya uchafu wa wanadamu au kitu kingine chochote—lazima yote yafunuliwe. Ni wakati huo tu ndipo utakapoona kuwa kweli Yeye ni tofauti na mwanadamu. Ikiwa kuna uchafu kidogo sana ndani ya watu, basi Yeye huwachukia kabisa. Hata kuna nyakati ambapo watu hawawezi kuelewa, na wanasema, “Mungu, mbona Umekasirika sana? Mbona Wewe huzingatii udhaifu wa mwanadamu? Mbona Usiwasamehe watu kidogo? Mbona Wewe humfikirii mwanadamu hata kidogo? Ni wazi kwamba Unajua ni kwa kiwango gani ambacho watu wamepotoshwa, basi mbona bado Unawatendea hivi?” Yeye hudharau dhambi, Anachukizwa nayo, naye Anachukizwa hasa ikiwa kuna dalili yoyote ya kutotii ndani yako. Unapoonyesha tabia ya uasi, Yeye huiona naye Anachukizwa kwa kina—Anachukizwa kwa njia isiyo ya kawaida. Ni kupitia kwa mambo haya ndipo tabia Yake na kile Mungu alicho vinaonyeshwa. Ukilinganisha tabia ya Mungu na kile Mungu alicho na wewe binafsi, ulinganishi huu unaonyesha kuwa ingawa Yeye hula chakula sawa na mwanadamu, huvaa nguo sawa, hufurahia vitu anavyofurahia mwanadamu, na huishi na kukaa pamoja nao, bado Yeye ni tofauti na mwanadamu. Je, huu sio umuhimu wa foili? Ni kupitia mambo haya ya kibinadamu ndipo nguvu za Mungu zinaonyeshwa; ni giza ambalo huanzisha uwepo wa thamani wa nuru.

Bila shaka, Mungu hawafanyi muwe foili bila sababu. Badala yake, ni wakati tu kazi hii inapozaa matunda ndipo inapodhihirika kwamba uasi wa mwanadamu ni foili kwa tabia ya Mungu yenye haki, na ni kwa sababu tu ninyi ni foili ndiyo mna fursa ya kujua onyesho asili la tabia ya Mungu yenye haki. Mnahukumiwa na kuadibiwa kwa sababu ya uasi wenu, lakini ni uasi wenu pia unaowafanya muwe foili, na ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo mnapokea neema kubwa ambayo Mungu huwapa. Uasi wenu ni foili kwa kudura na hekima ya Mungu, na pia ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo mmepata wokovu na baraka nyingi kama hizo. Ingawa mmehukumiwa nami mara kwa mara, mmepokea baraka nyingi sana ambazo hazijawahi kupokelewa na mwanadamu. Kazi hii ni ya muhimu sana kwenu. Kuwa “foili” pia ni yenye thamani sana kwenu: Mmekombolewa na kuokolewa kwa sababu ninyi ni foili, kwa hiyo foili kama huyo si wa thamani kubwa sana? Je, si mwenye umuhimu mkubwa sana? Ni kwa sababu ninyi mnaishi katika ulimwengu uleule, nchi hiyo hiyo chafu, sawa na Mungu, kwamba ninyi ni foili na mnapokea wokovu mkubwa zaidi. Mungu asingekuwa mwili, ni nani angekuwa na huruma kwenu, na ni nani angewatunza, watu duni kama ninyi? Nani angewajali? Mungu asingekuwa mwili ili Afanye kazi miongoni mwenu, mngepokea lini wokovu huu ambao wale waliokuwa kabla yenu hawakuwahi kuupata? Nisingekuwa mwili ili Niwajali, Nihukumu dhambi zenu, je, si mngelikuwa mmeanguka kuzimu kitambo? Nisingekuwa mwili na kujinyenyekeza miongoni mwenu, mngewezaje kustahili kuwa foili kwa tabia ya Mungu yenye haki? Je, ninyi si foili kwa sababu Nilichukua umbo la binadamu na kuja miongoni mwenu ili kuwawezesha kupata wokovu mkubwa zaidi? Je, hampokei wokovu huu kwa sababu Nimekuwa mwili? Mungu asingekuwa mwili ili Aishi nanyi, je, bado mngegundua kuwa mnaishi maisha ya mateso hapa duniani, ambayo ni mabaya kuliko mbwa na nguruwe? Je, hamjaadibiwa na kuhukumiwa kwa sababu ninyi ni foili kwa kazi Yangu katika mwili? Hakuna kazi inayofaa zaidi kwenu kuliko kazi ya foili, kwa kuwa ni kwa sababu ninyi ni foili ndiyo mnaokolewa katikati ya hukumu. Je, hamhisi kuwa kustahilishwa kutenda kama foili ni baraka yenu kubwa zaidi ya maisha? Ninyi hufanya kazi ya foili tu, lakini mnapokea wokovu kiasi ambacho hamjawahi kuwa nacho au hata kufikiria. Leo, jukumu lenu ni kuwa foili, na thawabu yenu ya haki ni kupokea baraka za milele katika siku za baadaye. Wokovu mnaoupata si ufahamu wa muda mfupi au ufahamu fulani wa muda kwa ajili ya wakati huu, lakini baraka kubwa zaidi: mwendelezo wa milele wa maisha. Ingawa Nimetumia “foili” kuwashinda, mnapaswa kujua kwamba wokovu na baraka hii imetolewa ili kuwapata; ni kwa ajili ya ushindi, lakini pia ni ili Niweze kuwaokoa vyema zaidi. “Foili” ni ukweli, lakini sababu ambayo ninyi ni foili ni kwa sababu ya uasi wenu, na ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mmepata baraka ambazo hakuna mtu amewahi kupata. Leo mnasababishwa kuona na kusikia; kesho mtapokea, na zaidi ya hayo, mtabarikiwa sana. Kwa hiyo, foili si wenye thamani kubwa sana? Athari za kazi ya leo ya ushindi zinatimizwa kupitia tabia zenu zenye uasi mkitenda kama foili. Yaani, kilele cha kuadibu na hukumu ya mara ya pili ni kutumia uchafu na uasi wenu kama foili, kukiwasababisha kuona tabia ya Mungu yenye haki. Mnapokuwa watiifu tena katika hukumu na kuadibu kwa mara ya pili, basi tabia nzima ya Mungu yenye haki inaonyeshwa wazi kwenu. Hii ni kusema kwamba wakati ambapo kukubali kwenu kazi ya ushindi kunakamilika, huu pia ndio wakati ambapo mnamaliza kutekeleza jukumu la foili. Si nia Yangu kuwapachika majina. Badala yake, Ninatumia jukumu lenu kama watendaji huduma ili kutekeleza kazi ya ushindi ya mara ya kwanza, Nikionyesha tabia ya Mungu yenye haki na isiyokosewa. Kupitia tofauti yenu, kupitia uasi wenu mkitenda kama foili, athari za kazi ya ushindi ya mara ya pili zinatimizwa, zikiwaonyesha kikamilifu tabia ya Mungu yenye haki, ambayo haikuwa imeonyeshwa kikamilifu mara ya kwanza, na zikiwaonyesha tabia yote ya Mungu yenye haki, yote Aliyo, ambayo yanajumuisha hekima, maajabu na utakatifu wa asili wa kazi Yake. Athari ya kazi kama hiyo inatimizwa kupitia ushindi katika vipindi tofauti, na kupitia hukumu za viwango tofauti. Kadri hukumu inavyofikia kilele chake, ndivyo inavyofichua zaidi tabia za uasi za watu, na ndivyo ushindi unavyokuwa wenye kufaa zaidi. Tabia nzima ya Mungu yenye haki imewekwa wazi wakati wa kazi hii ya ushindi. Kazi ya ushindi imegawanywa katika hatua mbili, nayo ina hatua na viwango tofauti, na hivyo bila shaka, athari ambazo zinatimizwa pia ni tofauti. Hii ni kusema kwamba kiwango cha utii wa watu kinazidi kuwa kikubwa hata zaidi. Ni baada ya hii tu ndiyo watu wanaweza kuletwa kikamilifu kwenye njia sahihi ya ukamilifu; ni baada tu ya kazi yote ya ushindi kukamilishwa (wakati hukumu ya mara ya pili imetimiza athari yake ya mwisho) ndipo watu hawahukumiwi tena lakini wanaruhusiwa kuingia kwenye njia sahihi ya kupitia maisha. Kwa maana hukumu ni ishara ya ushindi, na ushindi huchukua umbo la hukumu na kuadibu.

Mungu alipata mwili katika mahali palipokuwa nyuma kimaendeleo na pachafu zaidi, na ni kwa njia hii tu ndiyo Mungu anaweza kuonyesha wazi tabia Yake yote iliyo takatifu na yenye haki. Na tabia Yake yenye haki inaonyeshwa kupitia nini? Inaonyeshwa Anapozihukumu dhambi za mwanadamu, Anapomhukumu Shetani, Anapochukia dhambi sana, na Anapowadharau maadui wanaompinga na kuasi dhidi Yake. Maneno Ninayonena leo ni kwa ajili ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, kuhukumu udhalimu wa mwanadamu, kulaani uasi wa mwanadamu. Upotovu na udanganyifu wa mwanadamu, maneno na vitendo vya mwanadamu—yote ambayo hayapatani na mapenzi ya Mungu lazima yatapitia hukumu, na uasi wa mwanadamu kushutumiwa kama dhambi. Maneno Yake yanahusu kanuni za hukumu; Yeye hutumia hukumu ya udhalimu wa mwanadamu, laana ya uasi wa mwanadamu, na mfichuo wa asili mbaya za mwanadamu ili kudhihirisha tabia Yake mwenyewe yenye haki. Utakatifu ni kielelezo cha tabia Yake yenye haki, na kwa kweli utakatifu wa Mungu ni tabia Yake yenye haki. Tabia zenu potovu ni muktadha wa maneno ya leo—Ninazitumia kunena na kuhukumu, na kutekeleza kazi ya ushindi. Hii pekee ndiyo kazi halisi, na hii pekee inadhihirisha kabisa utakatifu wa Mungu. Ikiwa hakuna dalili ya tabia potovu ndani yako, basi Mungu hatakuhukumu, wala hatakuonyesha tabia Yake yenye haki. Kwa kuwa unayo tabia potovu, Mungu hatakusamehe, na ni kwa njia hii ndiyo utakatifu Wake unaonyeshwa. Mungu angaliona kuwa uchafu na uasi wa mwanadamu vilikuwa vikubwa sana lakini Asinene au kukuhukumu, wala kukuadibu kwa ajili ya udhalimu wako, basi hii ingethibitisha kwamba Yeye si Mungu, kwa maana Asingeichukia dhambi; Angelikuwa mchafu sawasawa na mwanadamu. Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na ndiyo Ninawaachia huru hasira Yangu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu. Mungu angelikuwa mtu na kufuata mfano wa mwanadamu na kugaagaa na wanadamu katika matope machafu, basi kusingelikuwa na chochote kitakatifu kumhusu, na Asingelikuwa na tabia yenye haki, na kwa hiyo Asingelikuwa na haki ya kuhukumu uovu wa mwanadamu, wala Asingelikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya mwanadamu. Mtu angelimhukumu mtu mwingine, haingekuwa kana kwamba anajipiga kofi usoni? Watu ambao wote ni wachafu kwa kiwango sawa wanastahili vipi kuwahukumu wale ambao ni sawa na wao? Ni Mungu mtakatifu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu. Mwanadamu angewezaje kuhukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na mwanadamu angewezaje kuwa na sifa za kulaani dhambi hizi? Mungu Asingelikuwa na sifa ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki Mwenyewe? Tabia potovu za watu zinapofichuliwa, Mungu hunena ili Awahukumu watu, na ni hapo tu ndipo watu wanapoona kuwa Yeye ni mtakatifu. Anapomhukumu na kumwadibu mwanadamu kwa ajili ya dhambi zake, wakati huo wote Akizifichua dhambi za mwanadamu, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuepuka hukumu hii; mambo yote ambayo ni machafu yanahukumiwa na Yeye, na ni kwa sababu hiyo tu ndiyo tabia Yake inaweza kusemwa kuwa yenye haki. Kama ingekuwa vinginevyo, ingewezaje kusemwa kwamba ninyi ni foili kwa jina na kwa kweli?

Kuna tofauti kubwa kati ya kazi iliyofanywa Israeli na kazi ya leo. Yehova aliyaongoza maisha ya Waisraeli, na hakukuwa na kuadibu na hukumu nyingi, kwa sababu wakati huo, watu walielewa kidogo sana kuhusu ulimwengu na walikuwa na tabia chache zilizokuwa potovu. Hapo zamani, Waisraeli walimtii Yehova kabisa. Alipowaambia wajenge madhabahu, walijenga madhabahu haraka; Alipowaambia wavae mavazi rasmi ya makuhani, walitii. Katika siku hizo, Yehova alikuwa kama mchungaji akilichunga kundi la kondoo, na kondoo wakifuata mwongozo wa mchungaji na kula nyasi katika malisho; Yehova aliyaongoza maisha yao, Akiwaongoza katika jinsi walivyokula, kuvalia, kuishi, na kusafiri. Huo haukuwa wakati wa kuweka wazi tabia ya Mungu, kwa kuwa wanadamu wa wakati huo walikuwa waliozaliwa karibuni; kulikuwa na wachache waliokuwa waasi na wapinzani, hakukuwa na uchafu mwingi kati ya wanadamu, na kwa hivyo watu hawangeweza kutenda kama foili kwa tabia ya Mungu. Ni kupitia watu ambao wanatoka katika nchi ya uchafu ndipo utakatifu wa Mungu unaonyeshwa; leo, Yeye hutumia uchafu ulioonyeshwa katika watu hawa wa nchi ya uchafu, naye Anahukumu, na kwa kufanya hivyo, kile Alicho kinafichuliwa katika hukumu Yake. Kwa nini Anahukumu? Anaweza kunena maneno ya hukumu kwa sababu Anadharau dhambi; Je, Angewezaje kukasirika sana hivyo ikiwa hakuchukia uasi wa wanadamu? Kusingekuwa na karaha ndani Yake, kusingekuwa na machukio, Asingejali uasi wa watu, basi hiyo ingethibitisha Yeye kuwa mchafu kama mwanadamu. Kwamba Yeye anaweza kumhukumu na kumwadibu mwanadamu ni kwa sababu Yeye huchukia uchafu, na Anachokichukia hakimo ndani Yake. Kama pia kungekuwa na upinzani na uasi ndani Yake, Asingewadharau wale ambao ni wapinzani na waasi. Kazi ya siku za mwisho ingekuwa ikifanywa Israeli, hakungekuwa na maana yoyote kwayo. Mbona kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali paovu na palipo nyuma kabisa kimaendeleo kuliko sehemu zote? Ni ili kuonyesha utakatifu na haki Yake. Kwa kifupi, kadri mahali palivyo paovu, ndivyo utakatifu wa Mungu unavyoweza kuonyeshwa wazi zaidi. Kwa kweli, yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Ni leo tu ndipo mnatambua kuwa Mungu ameshuka kutoka mbinguni ili Asimame kati yenu, Ameonyeshwa kupitia uchafu na uasi wenu, na ni wakati huu tu ndipo mnamjua Mungu. Je, hii siyo sifa kubwa zaidi? Kwa kweli, ninyi ni kikundi cha watu nchini China waliochaguliwa. Na kwa sababu mlichaguliwa na mmefurahia neema ya Mungu, na kwa sababu hamfai kufurahia neema kubwa kama hiyo, hii inathibitisha kwamba haya yote ni kuwapa sifa kubwa kabisa. Mungu amewatokea, na kuwaonyesha tabia Yake nzima iliyo takatifu, na Amewapa yote hayo, na kuwasababisha mfurahie baraka zote ambazo mnaweza kufurahia. Hamjaionja tu tabia ya Mungu yenye haki, lakini, zaidi ya hayo, mmeuonja wokovu wa Mungu, ukombozi wa Mungu na upendo wa Mungu usio na kikomo. Ninyi, wachafu zaidi ya wote, mmefurahia neema kubwa kama hii—je, hamjabarikiwa? Je, huku si Mungu kuwainua? Ninyi ni wa chini zaidi ya wote, kwa asili hamstahili kufurahia baraka kubwa kama hiyo, lakini Mungu anang’ang’ania kukuinua. Je, huoni aibu? Ikiwa huwezi kutekeleza wajibu wako, basi mwishowe utaaibika, nawe utajiadhibu. Leo, hufundishwi nidhamu, wala huadhibiwi; mwili wako uko salama salimini—lakini mwishowe, maneno haya yatakuaibisha. Hadi leo, bado Sijamwadibu mtu yeyote waziwazi; maneno Yangu yanaweza kuwa makali, lakini Ninawatendeaje watu? Ninawafariji, na kuwashawishi, na kuwakumbusha. Ninafanya hivi ili kuwaokoa tu. Je, kwa kweli hamwelewi mapenzi Yangu? Mnapaswa kuelewa Ninachosema, na kutiwa moyo nacho. Ni sasa tu ndipo kunao watu wengi wanaoelewa. Je, hii si baraka ya kuwa foili? Je, kuwa foili si jambo la kubarikiwa zaidi? Mwishowe, mnapoenda kueneza injili, mtasema hivi: “Sisi ni foili wa kawaida.” Watawauliza, “Inamaanisha nini kwamba ninyi ni foili wa kawaida?” Nanyi mtasema: “Sisi ni foili kwa kazi ya Mungu, na kwa nguvu Zake kuu. Tabia nzima ya Mungu yenye haki imefunuliwa kupitia uasi wetu; sisi ni vyombo vya kutumikia kwa kazi ya Mungu ya siku za mwisho, sisi ni viambatisho vya kazi Yake, na pia vifaa vya kazi hiyo.” Wanaposikia hivyo, watavutiwa sana. Baadaye, utasema: “Sisi ni vielelezo na mifano ya Mungu kukamilisha kazi ya ulimwengu wote, na ya ushindi Wake wa wanadamu wote. Iwe sisi ni watakatifu au wachafu, kwa jumla, bado tumebarikiwa zaidi kuliko ninyi, kwa maana tumemwona Mungu, na kupitia fursa ya Yeye kutushinda, nguvu kuu za Mungu zimeonyeshwa; ni kwa sababu tu sisi ni wachafu na waovu ndiyo tabia Yake yenye haki imetokea. Je, hivyo mnaweza kuishuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Hamstahili! Hii ni Mungu kutuinua tu! Ingawa tunaweza kukosa kuwa wenye kiburi, tunaweza kumsifu Mungu kwa kujivunia, kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kurithi ahadi kubwa kama hiyo, na hakuna mtu anayeweza kufurahia baraka kubwa kama hiyo. Tunashukuru sana kwamba sisi, ambao ni wachafu sana, tunaweza kufanya kazi kama foili wakati wa usimamizi wa Mungu.” Na wanapouliza, “Vielelezo na mifano ni nini?” unasema, “Sisi ni wanadamu waasi zaidi na wachafu zaidi; tumepotoshwa kwa kina kabisa na Shetani, nasi ni viumbe tulio nyuma kimaendeleo na duni zaidi kimwili. Sisi ni mifano bora ya wale ambao wametumiwa na Shetani. Leo, tumechaguliwa na Mungu kama wa kwanza kati ya wanadamu walioshindwa, na tumeona tabia ya Mungu yenye haki na kurithi ahadi Yake; tunatumiwa kuwashinda watu zaidi, kwa hiyo sisi ndio vielelezo na mifano ya wale wanaoshindwa kati ya wanadamu.” Hakuna ushuhuda bora zaidi kuliko maneno haya, na huu ndio uzoefu wako bora kabisa.

Tanbihi:

a. Foili: Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?

Inayofuata: Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp