Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

Mlikuwa mnatafuta kutawala kama wafalme, na leo bado hamjaacha kabisa suala hili; bado mnatamani kutawala kama wafalme, kushikilia mbingu na kuhimili dunia. Sasa, fikiria kuhusu hilo: Je, unazo sifa kama hizo? Je, huoni unakuwa mtu mpumbavu? Je, mnachokitafuta na kujitolea umakini wenu kwacho ni cha uhalisi? Hamna hata hali ya kawaida ya ubinadamu—hilo si la kusikitisha? Hivyo, leo Nazungumzia tu juu ya kushindwa, kuwa na ushuhuda, kuendeleza ubora wa tabia yako, na kuingia katika njia ya kufanywa kuwa mkamilifu, na kutozungumzia kitu chochote kile. Watu wengine wanaonekana kuchoshwa na ukweli usiotiwa doa, na wanapoona mazungumzo haya yote ya ubinadamu wa kawaida na kuendeleza ubora wa tabia ya watu, wanakaidi. Wale ambao hawapendi ukweli sio rahisi kuwafanya wakamilifu. Ili mradi mnaingia leo, na kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, hatua kwa hatua, je, utaweza kuondolewa? Baada ya Mungu kufanya kazi nyingi sana katika eneo bara la Uchina—kazi ya kiwango kikubwa hivyo—na baada ya Yeye kuzungumza maneno mengi sana, je, Angesalimu amri Akiwa katikati? Je, angewapeleka watu kuzimu? Kitu ambacho ni cha msingi leo ni kwamba lazima mjue hulka ya mwanadamu, na lazima mjue ni nini mnapaswa kuingia kwacho; unapaswa kuzungumza juu ya kuingia katika maisha, na mabadiliko katika tabia, jinsi ya kushindwa kwa kweli, na jinsi ya kumtii Mungu kabisa, kuwa na ushuhuda wa Mungu wa mwisho, na kutimiza utii hata kifo. Unapaswa kulenga mambo haya, na kile ambacho si chenye uhalisi au muhimu kinapaswa kuwekwa pembeni na kisizingatiwe. Leo, unapaswa kuelewa namna ya kushindwa, na jinsi watu wanavyofanya baada ya kushindwa. Unaweza kusema umeshashindwa, lakini unaweza kutii hata kufa? Unapaswa uwe na uwezo wa kufuata hadi mwisho kabisa bila kujali kama kuna matumaini yoyote, na hupaswi kupoteza imani kwa Mungu bila kujali mazingira. Mwishowe, unapaswa kutimiza hali mbili za ushuhuda: ushuhuda wa Ayubu—utii hata kifo—na ushuhuda wa Petro—upendo mkuu wa Mungu. Kwa upande mmoja, unapaswa kuwa kama Ayubu: Hakuwa na mali hata kidogo, na alisumbuliwa na maumivu ya mwili, lakini hakulikana jina la Yehova. Huu ulikuwa ushuhuda wa Ayubu. Petro aliweza kumpenda Mungu hadi kifo. Alipokufa—alipoangikwa msalabani—bado alimpenda Mungu; hakufikiria juu ya matarajio yake mwenyewe au kufuatilia mambo yaliyo makuu au fikra za anasa, na alitafuta tu kumpenda Mungu, na kutii mipango yote ya Mungu. Hicho ndicho kiwango unachopaswa kutimiza kabla hujahesabiwa kuwa na ushuhuda, kabla hujawa mtu ambaye amefanywa mkamilifu baada ya kushindwa. Leo, ikiwa watu wangekuwa wanajua kabisa hulka na hadhi yao, je, bado wangetafuta matarajio yao na matumaini yao? Unachopaswa kujua ni hiki: Bila kujali kama Mungu atanifanya mkamilifu, ni lazima nimfuate Mungu; kila kitu anachofanya sasa ni chema na kinafanywa kwa ajili yangu, na ili tabia yetu iweze kubadilika na tuweze kuepukana na ushawishi wa Shetani, kuturuhusu kuzaliwa katika nchi ya uchafu na hata hivyo kuepukana na uchafu, kuondoa uchafu na ushawishi wa Shetani, kutuwezesha kuacha nyuma ushawishi wa Shetani. Bila shaka, hiki ndicho unachotakiwa kuwa nacho, lakini kwa Mungu ni ushindi tu, ili watu wawe na azimio la kutii, na waweze kutii mipango yote ya Mungu. Kwa njia hii, mambo yatakamilishwa. Leo, watu wengi tayari wamekwishashindwa, lakini ndani yao bado kuna mengi ambayo ni ya uasi na ukaidi. Kimo cha kweli cha watu bado ni kidogo sana, na wao huwa na nguvu kamili ikiwa kuna matumaini na matarajio, kama hayapo, wanakuwa na mitazamo hasi, na hata wanafikiria kuhusu kumwacha Mungu. Na watu hawana shauku kuu ya kutafuta kuishi kulingana na maisha ya ubinadamu wa kawaida. Hilo halitafaulu. Hivyo, bado lazima Nizungumze juu ya ushindi. Kwa kweli, ukamilifu hutokea wakati mmoja na ushindi: Unaposhindwa, matokeo ya kwanza ya kufanywa mkamilifu pia yanatimizwa. Panapokuwa na tofauti kati ya kushindwa na kufanywa mkamilifu, ni kulingana na kiwango cha mabadiliko kwa watu. Kushindwa ni hatua ya kwanza ya kufanywa mkamilifu, na haimaanishi kwamba wamefanywa wakamilifu kabisa, wala kuthibitisha kwamba wamepatwa na Mungu kabisa. Baada ya watu kushindwa, kunakuwa na mabadiliko fulani katika tabia yao, lakini mabadiliko hayo ni pungufu sana yakilinganishwa na mabadiliko ya watu ambao wamepatwa kabisa na Mungu. Leo, kile kinachofanywa ni kazi ya mwanzo ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu—kuwashinda—na kama huwezi kutimiza kushindwa, basi hutaweza kuwa na uwezo wa kufanywa mkamilifu na kupatwa kabisa na Mungu. Utapata tu maneno machache ya kuadibu na hukumu, lakini hayatakuwa na uwezo wa kuubadilisha kabisa moyo wako. Hivyo utakuwa mmoja wa wale ambao wameondolewa; haitakuwa tofauti na kutazama tu karamu ya gharama mezani lakini huli. Je, hilo si la huzuni? Na hivyo, ni lazima utafute mabadiliko: Kama ni kushindwa au kufanywa mkamilifu, yote yanahusiana na kama kuna mabadiliko ndani yako, na kama wewe ni mtii au la, na hili linaamua kama unaweza kupatwa na Mungu au la. Jua kwamba “kushindwa” na “kufanywa mkamilifu” yamejikita katika kiwango cha mabadiliko na utii, vilevile katika jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo. Kinachotakiwa leo ni kwamba uweze kufanywa mkamilifu kabisa, lakini mwanzoni ni lazima ushindwe—ni lazima uwe na ufahamu wa kutosha juu ya kuadibu na hukumu ya Mungu, lazima uwe na imani ya kufuata, na kuwa mtu ambaye anatafuta mabadiliko na matokeo kuweko. Wakati huo tu ndipo utakuwa mtu ambaye anatafuta kufanywa mkamilifu. Unapaswa kuelewa kwamba wakati wa kufanywa kuwa mkamilifu, mtashindwa, na wakati wa kushindwa mtafanywa kuwa wakamilifu. Leo, unaweza kutafuta kufanywa kuwa mkamilifu au kutafuta mabadiliko katika ubinadamu wako wa nje na maendeleo katika ubora wa tabia yako, lakini muhimu kabisa ni kwamba unaweza kuelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya leo kina maana na ni cha manufaa: Kinakuwezesha wewe ambaye unazaliwa katika nchi ya uchafu kuepuka uchafu na kuuondoa wote, kinakuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuacha nyuma ushawishi wa giza wa Shetani—na kwa kulenga vitu hivi, unakuwa umelindwa katika nchi hii ya uchafu. Mwishowe, utaambiwa utoe ushuhuda gani? Unazaliwa katika nchi ya uchafu lakini unaweza kuwa mtakatifu, usichafuliwe na najisi tena, unamilikiwa na Shetani, lakini unaachana na ushawishi wa Shetani, na humilikiwi au kunyanyaswa na Shetani, na unaishi mikononi mwa Mwenyezi. Huu ndio ushuhuda, na thibitisho la ushindi katika vita na Shetani. Unaweza kumwacha Shetani, hufichui tabia za kishetani tena katika kile unachoishi kwa kudhihirisha, lakini badala yake unaishi kwa kudhihirisha kile ambacho Mungu alitaka mwanadamu afikie Alipomuumba mwanadamu: ubinadamu wa kawaida, urazini wa kawaida, umaizi wa kawaida, azimio la kawaida la kumpenda Mungu, na utii kwa Mungu. Huo ndio ushuhuda ambao kiumbe wa Mungu huwa nao. Unasema, “Tunazaliwa katika nchi ya uchafu, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, kwa sababu ya uongozi Wake, na kwa sababu Ametushinda, tumejiondoa katika ushawishi wa Shetani. Kwamba tunaweza kutii leo pia ni matokeo ya kushindwa na Mungu, na sio kwa sababu sisi ni wema, au kwa sababu tunampenda Mungu kwa asili. Ni kwa sababu Mungu alituchagua, na kutujaalia, ndio tumeshindwa leo, tunaweza kuwa na ushuhuda Kwake, na tunaweza kumhudumia, kwa hiyo, pia, ni kwa sababu Alituchagua, na kutulinda, ndio tumechaguliwa na kutolewa katika miliki ya Shetani, na tunaweza kuachana na uchafu na kutakaswa katika nchi ya joka kuu jekundu.” Aidha, kile unachoishi kwa kudhihirisha nje kitaonyesha kwamba una ubinadamu wa kawaida, kuna maana katika kile unachosema, na unaishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Watu wengine wanapokuona, hupaswi kuwasababisha waseme, “Je, hii siyo sura ya joka kuu jekundu?” Matendo ya dada hayaonekani kuwa ni ya dada, matendo ya kaka hayaonekani kuwa ni ya kaka, na huna staha yoyote ya watakatifu. Kisha watu wanaweza kusema, “si ajabu Mungu alisema ni uzao wa Moabu, Alikuwa sahihi kabisa!” Ikiwa watu wanawatazama na kusema, “Ingawa Mungu alisema wewe ni uzao wa Moabu, kile unachokiishi kwa kudhihirisha kimethibitisha kwamba umeachana na ushawishi wa Shetani; ingawa mambo hayo bado yapo ndani yako, unaweza kuachana nayo,” basi hili linaonyesha kwamba umeshindwa kabisa, wewe ambaye umeshindwa na kuokolewa utasema, “Ni kweli kwamba sisi ni uzao wa Moabu, lakini tumeokolewa na Mungu, na ingawa uzao wa Moabu ulikataliwa na kulaaniwa, na kupelekwa uhamishoni na Waisraeli miongoni mwa Mataifa, leo Mungu ametuokoa. Ni kweli kwamba sisi ni wapotovu kuliko watu wote—hili lilitamkwa na Mungu, huu ni ukweli, na haupingwi na mtu yeyote. Lakini leo tumeukwepa ushawishi huo. Tunawachukia sana mababu zetu, tupo radhi kuwageuzia migongo mababu zetu, kuwatelekeza kabisa na kutii mipango yote ya Mungu, kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, na kutimiza matakwa Yake kwetu, na kufikia ridhaa ya mapenzi ya Mungu. Moabu alimsaliti Mungu, hakutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, na alichukiwa na Mungu. Lakini tunapaswa kujali moyo wa Mungu, na leo, kwa kuwa tunaelewa mapenzi ya Mungu, hatuwezi kumsaliti Mungu, na tunapaswa kuwakana mababu zetu wa kale!” Hapo awali Nilizungumza juu ya kumkana joka kuu jekundu—na leo, huko ni kukana hasa mababu wa kale. Huu ni ushuhuda mmoja wa ushindi wa watu, na bila kujali ni jinsi gani unaingia leo, ushuhuda wako katika eneo hili haupaswi kukosekana.

Ubora wa tabia ya watu ni duni sana, wanapungukiwa sana na ubinadamu wa kawaida, kupokea kwao ni kwa polepole sana, kwa uvivu, uharibifu wa Shetani umewaacha wakiwa wapumbavu, na ingawa hawawezi kubadilika kabisa kwa kipindi cha mwaka mmoja au miwili, ni lazima wawe na azimio la kushiriki. Inaweza kusemwa kuwa huu pia ni ushuhuda mbele ya Shetani. Ushuhuda wa leo ni matokeo yaliyotimizwa na kazi ya sasa ya ushindi, vilevile kama sampuli na mfano wa kuigwa na wafuasi wa baadaye. Hapo baadaye, utaenea katika mataifa yote; kile kinachofanyika Uchina kitaenea katika mataifa yote. Uzao wa Moabu ni watu duni sana kuliko watu wote duniani. Watu wengine huuliza, je, wafuasi wa Hamu sio duni kuliko wote? Kizazi cha joka kuu jekundu na uzao wa Hamu ni wenye umuhimu tofauti wakilishi, na uzao wa Hamu ni suala jingine. Bila kujali ni jinsi gani wamelaaniwa, bado ni uzao wa Nuhu; asili za Moabu, wakati ule ule, hazikuwa safi: Moabu alitoka katika uzinzi, na hii ndiyo tofauti. Ingawa wote walilaaniwa, hali zao hazikuwa sawa, na kwa hiyo uzao wa Moabu ni watu duni kabisa kuliko wote—hakuna ukweli unaoweza kushawishi kuliko kushindwa kwa watu duni kuliko watu wote. Kazi ya siku za mwisho inavunja kanuni zote, bila kujali kama umelaaniwa au kuadhibiwa, maadamu tu uisaidie kazi Yangu, na una manufaa kwa kazi ya ushindi ya leo, na bila kujali kama wewe ni uzao wa Moabu au kizazi cha joka kuu jekundu, maadamu tu unatekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katika hatua hii ya kazi, na kufanya kadri unavyoweza, basi matokeo yanayotarajiwa yatatimizwa. Wewe ni kizazi cha joka kuu jekundu, na ni uzao wa Moabu; kwa ujumla, wale wote walio wa mwili na damu ni viumbe wa Mungu, na waliumbwa na Muumba. Wewe ni kiumbe wa Mungu, hupaswi kuwa na chaguo lolote, na huu ndio wajibu wako. Bila shaka, leo kazi ya Muumba imeelekezwa kwa ulimwengu mzima. Bila kujali wewe ni uzao wa nani, zaidi ya yote, nyinyi ni mojawapo wa viumbe wa Mungu, ninyi—uzao wa Moabu—ni sehemu ya viumbe wa Mungu, ni vile tu nyinyi mna thamani ya chini. Kwa kuwa, leo, kazi ya Mungu inatekelezwa miongoni mwa viumbe wote, na imelenga ulimwengu mzima, Muumba yuko huru kuchagua watu, masuala, au vitu vyovyote ili viweze kufanya kazi Yake. Hajali wewe ni uzao wa nani; maadamu tu wewe ni mmoja wa viumbe wake, na maadamu una manufaa katika kazi Yake—kazi ya ushindi na ushuhuda—Ataifanya kazi Yake ndani yako bila haya yoyote. Hili linaharibu kabisa dhana za watu za kitamaduni, ambayo ni kwamba Mungu hatawahi kamwe kufanya kazi miongoni mwa Mataifa, hususan wale ambao wamelaaniwa na ambao ni duni; kwa maana wale ambao wamelaaniwa, uzao wao wa baadaye nao utaendelea kulaaniwa milele, hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mungu hatawahi kamwe kushuka na kufanya kazi katika nchi ya Mataifa, na Hatakanyaga mguu Wake katika nchi yenye uchafu, maana Yeye ni mtakatifu. Dhana hizi zote zimevunjwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Jua kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe vyote, ni mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote, na si Mungu wa watu wa Israeli pekee. Hivyo, kazi hii katika nchi ya Uchina ni ya umuhimu mkubwa, na unadhani haitaenea miongoni mwa mataifa yote? Ushuhuda mkubwa wa siku za usoni hautakomea Uchina tu; ikiwa Mungu angewashinda nyinyi tu, je, mapepo wangeshawishika? Hawaelewi maana ya kushindwa, au nguvu kubwa ya Mungu, na ni pale tu ambapo wateuliwa wa Mungu katika nchi yote watakapoona matokeo ya mwisho ya kazi hii ndipo viumbe wote watakuwa wameshindwa. Hakuna ambao wapo nyuma sana au waovu sana kuliko uzao wa Moabu. Iwapo tu watu hawa wataweza kushindwa—wale ambao ni waovu sana, ambao hawakumtambua Mungu au kuamini kwamba kuna Mungu wameshindwa, na kumtambua Mungu katika vinywa vyao, wakimtukuza, na wanaweza kumpenda—ndipo huu utakuwa ushuhuda wa ushindi. Ingawa wewe si Petro, mnaishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro, mnaweza kuwa na ushuhuda wa Petro, na ushuhuda wa Ayubu, na huu ni ushuhuda mkubwa sana. Hatimaye utasema: “Sisi sio Waisraeli, bali ni uzao wa Moabu uliotelekezwa, sisi sio Petro, ambaye hatuwezi kuwa na ubora wa tabia yake, wala sisi sio Ayubu, na hata hatuwezi kujilinganisha na azimio la Paulo la kuteseka kwa ajili ya Mungu na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, na sisi tupo nyuma sana, na hivyo, hatustahili kufurahia baraka za Mungu. Mungu bado Ametuinua leo; kwa hiyo tunapaswa kumridhisha Mungu, na ingawa tuna ubora wa tabia au sifa haba, tupo radhi kumridhisha Mungu—tuna azimio hili. Sisi ni uzao wa Moabu, na tulilaaniwa. Hili lilitangazwa na Mungu, na wala hatuwezi kuibadilisha, lakini kuishi kwetu kwa kudhihirisha na maarifa yetu yanaweza kubadilika, na tumeazimia kumridhisha Mungu.” Utakapokuwa na azimio hili, itathibitisha kwamba umeshuhudia kuwa umeshindwa.

Iliyotangulia: Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa

Inayofuata: Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp