Jinsi ya Kufuatilia Ukweli (3)

Utendaji wa Kwanza wa Kuufuatilia Ukweli: Kuachilia

Kuachilia Vizuizi Kati ya Mtu na Mungu na Uhasama wa Mtu kwa Mungu

I. Kuachilia Dhana na Mawazo ya Kufikirika ya Mtu Kumhusu Mungu: Kuachilia Dhana na Mawazo ya Kufikirika ya Mtu Kuhusu Kazi ya Mungu

Kwa muda sasa, tumekuwa tukifanya ushirika juu ya mada ya kuufuatilia ukweli. Maudhui yanayohusika katika mada hii ni mapana sana, lakini haijalishi jinsi maudhui yalivyo mapana, hayawezi kutenganishwa na baadhi ya masuala ambayo watu hukumbana nayo katika maisha yao ya kila siku yanayohusiana na jinsi wanavyowachukulia watu na mambo, na jinsi wanavyojiendesha na wanavyotenda, sivyo? (Ndiyo.) Haya ni masuala halisi katika maisha ya watu. Ingawa yanagusa maudhui mbalimbali, na maudhui haya ni mapana sana, masuala haya hayatengani na maisha ya kila siku ya watu, wala hayatengani na ubinadamu wao wa kawaida. Masuala haya yanajumuisha jinsi wanavyowachukulia watu na mambo, mitazamo na maoni yao kuelekea mambo mbalimbali, na vilevile mambo makubwa ya kila aina wanayokumbana nayo katika uwepo wao na katika safari zao za maisha. Maudhui ya ushirika wetu uliopita yalihusu kipengele kimoja cha utendaji ndani ya "kuachilia" katika "Jinsi ya Kuufuatilia Ukweli"—kuachilia vizuizi kati ya mtu na Mungu na uhasama wa mtu kwa Mungu. Kipengele hiki cha utendaji kinahusisha kitu gani? Kinahusisha uhusiano kati ya watu na Mungu, sivyo? (Ndivyo.) Maudhui ya vipindi vichache vya ushirika vilivyopita yalihusu jinsi mtu anavyopaswa kuchukulia watu wa kila na mambo ya kila aina kulingana na kanuni na viwango anavyotaka Mungu, na jinsi anavyopaswa kushughulikia watu wa kila aina na mambo ya kila aina. Maudhui ya ushirika wetu uliopita yalihusu uhusiano kati ya watu na Mungu, na yaliwafahamisha watu jinsi wanavyopaswa kuachilia dhana na mawazo mbalimbali ya kufikirika ambayo hayalingani na nia za Mungu, hayalingani na matakwa ya Mungu, na hayalingani na kanuni za ukweli. Haya ndiyo matatizo halisi yaliyopo kati ya watu na Mungu katika safari ya kumwamini Mungu na katika mchakato wa kuwepo. Tuligawanya mada hii kuu ya "kuachilia vizuizi kati ya mtu na Mungu na uhasama wa mtu kwa Mungu" katika vipengele vinne: Cha kwanza ni dhana na mawazo ya kufikirika, cha pili ni matakwa yasiyo na busara, cha tatu ni kujihadhari na kuwa na mashaka, na cha nne ni kuchunguza na kudadisi. Tulianza ushirika wetu na dhana na mawazo ya kufikirika. Jambo la kwanza ndani ya dhana na mawazo ya kufikirika linahusu kazi ya Mungu—yaani, ni dhana na mawazo gani ya kufikirika ambayo watu wanayo kuhusu kazi ya Mungu. Tulifanya ushirika kiasi kuhusu jambo hili. Ushirika wetu kuhusu jambo hili ulihusu jinsi watu wanavyoichukulia kazi ya Mungu, na ni mikengeuko, dhana, na mawazo gani ya kufikirika ambayo watu wanayo katika maarifa na mawazo yao kuhusu kazi ya Mungu; dhana na mawazo haya ya kufikirika ni mambo ambayo watu wanapaswa kuyaachilia. Ikiwa watu wataachilia dhana na mawazo haya kufikirika na watautafuta ukweli, wataweza kuijua kazi ya Mungu na kuwa na ufahamu safi wa maneno ya Mungu. Wakati ambapo kazi ya Mungu hailingani na dhana na mawazo ya kufikirika ya watu, wanapaswa kujitafakari na kujaribu kujijua, na wanapaswa pia kuachilia dhana na mawazo yao wenyewe ya kufikirika, badala ya kuvitegemea ili kupima jinsi kazi ya Mungu inavyopaswa kuwa, au ni matokeo gani ambayo Mungu anakusudia kufikia ndani ya watu kupitia kazi Yake. Dhana na mawazo ya kufikirika ya watu kuihusu kazi ya Mungu yana athari ya moja kwa moja juu ya kuingia kwa watu katika uzima na mtazamo wao kwa Mungu, kwa hivyo dhana na mawazo haya ya kufikirika pia ni mambo ambayo watu lazima wayaachilie. Kwa mfano, tulishiriki kwamba Mungu habadilishi ubora wa tabia wa asili wa watu, haiba zao, silika zao, na kadhalika, kwamba sifa za asili ambazo watu huzaliwa nazo na silika za mwili wao si malengo ya kazi ya Mungu, na kwamba kazi Yake inalenga tabia potovu za watu, mambo yaliyo ndani ya watu ambayo hayapatani na Mungu, na mambo yaliyo ndani ya watu ambayo yanaasi dhidi ya Mungu. Ikiwa watu wanawazia kwamba kazi ya Mungu inalenga kubadilisha ubora wao wa tabia, silika zao, na hata haiba yao, mazoea yao, mitindo yao ya maisha, na kadhalika, basi kila kipengele cha utendaji wao katika maisha ya kila siku kitashawishiwa na kitayumbishwa na dhana na mawazo yao wenyewe ya kufikirika, na bila shaka kutakuwa na sehemu nyingi potofu au mambo ya kupita kiasi. Sehemu hizi potofu na mambo ya kupita kiasi hayaendani na kanuni za ukweli na yatasababisha watu kukengeuka kutoka kwenye dhamiri na busara ya ubinadamu wa kawaida, na kujitenga na mkondo wa ubinadamu wa kawaida. Tuseme, kwa mfano, kwamba katika dhana na mawazo yako ya kufikirika, unaamini kwamba Mungu anataka kubadilisha ubora wa tabia wa watu, uwezo wao, na hata silika zao; ukifikiri kwamba haya ndiyo mambo ambayo Mungu anataka kubadilisha, utakuwa na ufuatiliaji wa aina gani? Utakuwa na ufuatiliaji potofu na wa kung’ang’ania—utataka kufuatilia ubora wa tabia wa hali ya juu, na utalenga kujifunza aina mbalimbali za ustadi na kumudu aina mbalimbali za maarifa ili uje kuwa na ubora wa tabia wa hali ya juu na uwezo wa hali ya juu, na umaizi wa hali ya juu na kujikuza kwa hali ya juu, na hata uwezo fulani ambao ni wa hali ya juu kuliko ule wa watu wa kawaida—kwa namna hii, utatilia maanani karama, uwezo na talanta za juu juu. Basi, je, matokeo ya ufuatiliaji kama huo kwa watu ni yapi? Si tu kwamba watashindwa kuingia kwenye njia ya kuufuatilia ukweli, lakini badala yake watachukua njia ya Mafarisayo. Watashindana wao kwa wao ili kuona ni nani aliye na ubora wa tabia wa hali ya juu, ni nani aliye na karama za hali ya juu, ni nani aliye na maarifa ya hali ya juu, ni nani aliye na uwezo mkubwa zaidi, ni nani aliye na vipaji zaidi, ni nani aliye na hadhi ya juu zaidi miongoni mwa watu na anayeenziwa na anayeheshimiwa na wengine. Kwa namna hii, si tu kwamba hawataweza kutenda ukweli na kutenda kulingana na kanuni za ukweli, bali badala yake wataelekea kwenye njia inayowaongoza mbali na ukweli.

F. Kazi ya Mungu Haibadilishi Hali za Asili za Watu; Inalenga Kubadilisha Tabia Zao Potovu
1. Kazi ya Mungu Haibadilishi Hali za Asili za Watu

Kazi ya Mungu ni kuzibadilisha tabia potovu za watu, na fikira na mitazamo yao mbalimbali potofu inayokiuka ukweli, ndani ya upeo wa ubinadamu wao wa kawaida, ili kwamba dhamiri na busara zao ziweze kurejeshwa na kuboreshwa. Yaani, kadiri unavyoelewa ukweli zaidi, ndivyo dhamiri yako na busara yako vitakavyokuwa vya kawaida zaidi, na pia zitaendelea kukua katika mwelekeo wa manufaa; hili si jambo la kupita maumbile hata kidogo. Ninamaanisha kitu gani kwa neno hili "kawaida"? Ikiwa watu wana utambuzi wa dhamiri na hisia ya haki, watakuwa wema—kwa kutumia maneno ya mwanadamu, watakuwa wenye kuelewa, wanyoofu, wenye busara, na wasio wakaidi na wenye mwelekeo wa upotofu. Haya ndiyo matokeo ambayo Mungu anakusudia kufikia kuhusiana na ubinadamu wa watu. Kadiri watu wanavyoelewa ukweli zaidi na zaidi, tokeo moja la pembeni ni kwamba ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi. Hata hivyo, ikiwa watu wanafuatilia kulingana na dhana na mawazo yao wenyewe ya kufikirika, dhana hizi na mawazo haya ya kufikirika yatakuwa na ushawishi mkubwa hasi na mwongozo hasi juu ya ufuatiliaji wao, na yatawaongoza kwenye njia za kila aina zilizo potofu na zinazofuatwa kwa ukaidi, zenye kupita kiasi, na zenye upotofu. Kwa mfano, katika dhana na mawazo ya kufikirika ya watu, wao wanaamini kwamba kazi ya Mungu inakusudia kuinua ubinadamu wa watu, na kuwawezesha watu kuvuka silika za binadamu, ubora wa tabia wa binadamu, na hata umri na jinsia ya binadamu. Watu wanapokuwa na dhana kama hizi, watafuatilia, watajitahidi, na watapapasa katika mwelekeo huu. Basi, ni mambo gani watakayolenga? Kwa upande mmoja, watalenga maarifa, uwezo, ustadi, karama, na talanta; kwa upande mwingine, watalenga mambo ya kupita maumbile. Je, mnajua udhihirisho wa mambo ya kupita maumbile ni upi? (Je, inamaanisha kwamba, katika baadhi ya mambo, watu watapitia mabadiliko ya ubora moja kwa moja bila kulipa gharama?) Ni kama wakati ambapo mtu hasomi maneno ya Mungu kwa kawaida, lakini jambo linapomtokea, na maneno ya Mungu yanatokea ghafla akilini mwake, au wakati ambapo mtu hajawahi kuweza kuimba wala kucheza dansi, lakini baada ya kupata msukumo ghafla anaweza kuimba na kucheza dansi, na hata kucheza dansi vizuri sana, au ambapo wakati mtu hajawahi kujifunza lugha ya kigeni, lakini ghafla anaweza kuzungumza lugha ya kigeni. Je, mambo haya ni ya kupita maumbile? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme kwamba unapaswa kwenda nje kwa jambo la dharura, lakini hujui jinsi ya kuendesha gari, na katika hali ya kukata tamaa unaomba, na mara moja unahisi msisimko mkubwa, na ghafla unajua jinsi ya kuendesha gari, na hata unaendesha kwa utulivu kama dereva mwenye uzoefu. Mtu anakuuliza, "Unaendeshaje vizuri hivi?" Unasema, "Mimi mwenyewe pia sijui. Haya yote yanafanywa na Mungu; niliguswa na Roho Mtakatifu. Tazama, mikono yangu hii si mikono yangu mwenyewe tena; inashikiliwa na Roho Mtakatifu!" Kwa kweli, Roho Mtakatifu hafanyi hili; badala yake, roho nyingine ya aina fulani imeingia ndani yako na inakutawala kwa hila, kiasi kwamba umekuwa mtu tofauti na huwezi kujidhibiti. Je, huku si kuvuka uwezo wa asili wa mtu? Hili ni jambo la kupita maumbile, sivyo? (Ndiyo.) Jambo la kupita maumbile linamaanisha nini? Je, hili ni jambo zuri? (Hapana, hili humfanya mtu asiwe wa kawaida.) Ikiwa unaweza ghafla kujua lugha fulani, kuwa na ustadi fulani, au kuelewa maarifa fulani bila kusoma kwa kipindi fulani au kuongozwa na mtaalamu yeyote, hilo ni jambo la kupita maumbile. Ikiwa tabia ya uzima ya mtu imebadilika bila yeye kuhitaji kuufuatilia ukweli, kutafuta, kusubiri, au kupitia mambo, je, hili si jambo la kutisha? (Ndiyo.) Ikiwa bado kuna mambo mengi ya dhana na mawazo ya kufikirika akilini mwako na katika ufahamu wako uliofichika, basi unapaswa kuyaachilia na usiyafuatilie, kwa sababu si maarifa ya kweli kuhusu kazi ya Mungu, na hayaendani na mbinu na kanuni za kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu kwa hakika haitavuka ubinadamu wako wa kawaida, na matokeo yanayofikiwa na kazi ya Mungu ndani yako kwa hakika si yale ya kuubadilisha ubinadamu wako wa kawaida uwe ubinadamu ulioinuliwa, wa kupita maumbile. Zaidi ya hayo, Mungu asingekubadilisha kutoka kuwa mtu wa kawaida kuwa mtu asiye wa kawaida. Tuseme kwamba, katika mchakato wa kupitia kazi ya Mungu, dhamiri yako inazidi kuwa nyeti, na unakuza hisia kubwa zaidi ya aibu. Unakuwa mwema, unayeweza kujali nia za Mungu, na unayeweza kulinda kazi ya kanisa na masilahi ya nyumba ya Mungu. Zaidi ya hayo, maneno na matendo yako hayaendi kinyume na dhamiri na busara yako, na hatua kwa hatua unakuwa na uwezo wa kutenda kulingana na kanuni za ukweli; unaweza kutoa hukumu kuhusu watu, matukio, na vitu vya kila aina, na kutambua watu, matukio, na vitu vya kila aina kulingana na maneno ya Mungu. Hili linathibitisha kwamba njia unayoitembea katika imani yako katika Mungu ni sahihi. Lakini tuseme kwamba bado unalenga kuisikiliza sauti fulani unapoomba, na unasubiri msukumo fulani, mwako wa nuru, au ufunuo wa kupita maumbile unapotafuta kutoka kwa Mungu na unapomsihi Mungu. Zaidi ya hayo, dhamiri na busara zako hazijarejeshwa wa hazijarekebishwa kwa namna yoyote, na hujakuja kuwa na hisia ya haki wala kumtii Mungu. Hili linathibitisha kwamba kuna matatizo na ufuatiliaji wako na njia unayoitembea, na inaweza pia kusemwa kwamba hujaingia kwenye njia ya kuufuatilia ukweli hata kidogo. Wewe pia mara nyingi hutafuta bila kujitambua kuwa mtu wa kupita maumbile, na mara nyingi unahisi kwamba unapaswa kuuvuka mwili—kutohisi njaa usipokula, na kutohisi uchovu au usingizi usipolala au usipopumzika kwa siku kadhaa—na hata unatafuta kuelewa na kumudu ghafla mambo usiyoyaelewa au ambayo hujajifunza katika mchakato wa kutekeleza wajibu wako unapoyahitaji kwa dharura. Mawazo haya ya kufikirika kuhusu mambo ya kupita maumbile yote yanatokana na dhana na mawazo ya kufikirika ya binadamu. Kwa sababu watu hawajapitia kazi ya Mungu, kwa kawaida wamejaa mawazo ya kufikirika kuhusu kazi Yake. Kwa kweli, kazi ya Mungu ndiyo halisi na ya vitendo kabisa kati ya mambo yote. Mungu kamwe hatendi kulingana na dhana na mawazo ya kufikirika ya watu; Hafanyi kamwe kazi ya aina hii juu ya watu. Yeye hufanya tu kazi kidogo ya kupita maumbile chini ya hali maalum sana na kwa watu wachache sana, lakini kazi hii ni ya muda tu na ni kitu kinachohitajika katika hali maalum—si mbinu ya kazi ambayo mara nyingi hudhihirishwa ndani ya watu katika wokovu wa Mungu. Katika kazi Yake ya usimamizi, Mungu anakusudia kuwaokoa watu, kuwawezesha kuvua tabia zao potovu na kufikia wokovu, na mbinu ya msingi ambayo kwayo Mungu hufanya kazi ni kuwapa watu ukweli, ili kwamba waweze kutenda kulingana na kanuni za ukweli baada ya kuelewa ukweli. Kwa hivyo, haijalishi una dhana na mawazo gani ya kufikirika akilini mwako na katika ufahamu uliofichika, haijalishi dhana zako na mawazo yako ya kufikirika yana mantiki kiasi gani au yanakidhi mahitaji yako ya kiroho kwa kiasi gani—haijalishi sababu ni zipi, daima yatakuwa dhana na mawazo, na unapaswa kuyaachilia na usiyang’ang’anie. Haijalishi kazi ya Mungu imefanywa kwa kiwango gani, na haijalishi inaendelea kwa muda gani, watu daima watakuwa watu na kamwe hawatakuwa malaika. Hata ukigeuka mweupe kuanzia kichwani hadi miguuni, ukiwa na nywele nyeupe, uso uliopakwa rangi nyeupe, na shati jeupe na suruali nyeupe, na pia unavaa mabawa mawili, huwezi kuwa malaika—watu daima watakuwa watu. Zaidi ya hayo, "watu" hapa inarejelea watu walio na dhamiri na busara ya ubinadamu wa kawaida, si watu wasio wa kawaida, na sembuse watu wasio wa kawaida. Watu hawa si wa kupita maumbile hata kidogo, lakini ni tofauti waziwazi na watu wasioamini ambao hawamwamini Mungu, kwa kuwa hawatendi maovu, wanaweza kuutia ukweli katika vitendo mara tu wanapouelewa, na wanaelewa jinsi ya kuchukulia watu na mambo, na kujiendesha na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, na kulingana na matakwa ya Mungu na kanuni za ukweli, badala ya kuishi kwa tabia zao potovu na kwa fikira na mitazamo mbalimbali ambayo Shetani huingiza ndani ya watu. Haijalishi watu wamefuatilia kwa muda gani kulingana na dhana na mawazo yao wenyewe ya kufikirika katika mchakato wa kumwamini Mungu, na haijalishi wanahisi kwamba wamepata kiasi gani, hayo hayahesabiki machoni pa Mungu, na Mungu hayakumbuki hata kidogo. Ninarejelea kitu gani Ninaposema hivi? Yaani kwamba ikiwa wewe, kulingana na dhana zako na mawazo yako ya kufikirika, unazuia mahitaji yote mbalimbali ya kawaida ya mwili wako, au unajitahidi sana kubadilisha silika zako, ubora wako wa tabia, uwezo wako, haiba yako, mitindo yako ya maisha, na mazoea yako ya maisha, basi haijalishi unajitahidi kiasi gani kuzuia na kubadilisha mambo haya, hata ikiwa unaweza kupata matokeo fulani, haimaanishi kwamba tayari umepata chochote kwenye njia ya kutenda ukweli, na hata zaidi, haimaanishi kwamba tayari wewe ni mtu anayeufuatilia ukweli—Mungu hayakumbuki mambo haya. Je, umeelewa? (Ndiyo.)

Ingawa dhana na mawazo ya kufikirika ya watu hayaonekani na kwa nje hayaonekani kuwalazimisha watu kusema wala kufanya chochote, wala kuitembea njia ya aina yoyote, yanadhibiti kwa nguvu fikira na nafsi za ndani za watu, ndani kabisa ya mioyo yao na katika ufahamu wao uliofichika. Kwa nini hali iko hivi? Ni kwa sababu mambo ambayo watu wanayapenda na wanayafuatilia yanalingana na dhana na mawazo yao ya kufikirika vizuri sana, na mambo haya pia yanaendekeza mahitaji ya mwili wa binadamu na yanatosheleza matamanio na udadisi wa kila aina wa binadamu. Kwa mfano, katika dhana na mawazo ya kufikirika ya watu, wanaamini kwamba kazi ya Mungu inakusudia kuwabadilisha wawe viumbe wasio wa kawaida ambao ni tofauti na watu wa kawaida, na kwamba, wanapoguswa na Roho Mtakatifu, wataweza kuzungumza lugha kadhaa. Hili kwa wazi linavuka uwezo wa asili wa watu na upeo wa ubinadamu wa kawaida, lakini kwa kiwango kikubwa sana linatosheleza ubatilifu, udadisi, na ushindani wao. Yaani, kabla ya watu kuupata ukweli, wanapenda baadhi ya mambo ya kupita maumbile, na mambo haya huwafanya wahisi kuwa muhimu, bora kuliko watu wa kawaida, na tofauti nao—hili ndilo hasa jambo ambalo binadamu wapotovu wanalipenda na wanalitamani. Kila mtu anatumaini kuwa mtu wa kipekee miongoni mwa jamii ya binadamu, kuwa tofauti na kila mtu mwingine, kuwa asiye na kifani na wa aina yake, na kuenziwa na kuvutiwa na wengine. Kwa mfano, kuna jambo miongoni mwa binadamu wapotovu kwamba ikiwa bidhaa moja tu ya kitu itatengenezwa, wale watu ambao ndio matajiri na mashuhuri watashindana kwa hamu kubwa ili kuinunua. Watafanya jambo hili kwa kiwango gani? Kwa kiwango ambacho bidhaa hii huishia kuuzwa kwa bei ambayo ni mara kadhaa au hata zaidi ya mara kumi ya bei yake ya awali. Mtu anayefaulu kuinunua anafikiri, "Tazama, nimefanikiwa kupata kitu hiki ambacho ni cha pekee duniani. Kwa kweli nina uwezo mkubwa sana, sivyo? Mimi ni bora kuliko wengine, sivyo? Hakuna mtu mwingine aliye na uwezo kama wangu!" Katika akili yake mwenyewe anahisi kujifurahia, na wanahisi kwamba yeye ni maalum, asiye wa kawaida, na mwenye uwezo. Hii ni tabia ya aina gani? (Kiburi.) Hili linasababishwa na tabia ya kiburi. Baadhi ya watu huhisi vibaya wanapovaa vazi sawa na mtu mwingine. Wakivaa vazi ambalo watu wengine hawawezi kumudu na ambalo hawajawahi kuliona hapo awali, na kila mtu anayeliona anaona wivu, wanahisije? (Hujifurahia.) Wanajifurahia zaidi, na wanafikiri kwamba wao hawafanani na mtu mwingine yeyote na wako daraja la juu kuliko wengine. Ni tabia ya aina gani inayosababisha hili? (Kiburi.) Hili pia linasababishwa na tabia ya kiburi. Unaona, karibu asilimia 100 ya watu wana fikira hizi: Ikiwa wamemudu ustadi wa kiufundi au wa kitaaluma, wanafikiri kwamba wao ni bora kuliko wengine na kwamba hakuna mtu aliye hodari kama wao. Ikiwa mtu mwingine pia atamudu ustadi uleule wa kiufundi au wa kitaaluma, watamwonea wivu mtu huyo na watatamani sana kwamba kusiwe na mtu anayeweza kulingana nao. Kwa nini wana fikira kama hizi? (Wanataka kuwa wasiofanana na mtu mwingine yeyote.) Ikiwa wao ndio pekee wanaomudu ustadi huu wa kitaaluma, basi, katika kundi lao, wao ni wa kipekee na bora kuliko mtu wa kawaida. Wakiwa na maarifa ya ustadi huu wa kiufundi au wa kitaaluma, wanaogopa kwamba wengine watajifunza kutoka kwao. Wengine wakitafuta msaada kutoka kwao, je, watawafundisha? (Hapana, hawatawafundisha.) Watakufundisha tu mambo fulani rahisi; kuhusu mambo muhimu na ya msingi kabisa, hawatamfundisha mtu yeyote mambo hayo, na watakuacha uyatambue wewe mwenyewe. Kwa kweli wanafikiri nini? "Nikikufundisha, basi ninawezaje kujitokeza kuwa wa pekee? Ikiwa kila mtu angeweza kufanya jambo hilo, basi nisingekuwa tu mtu wa kawaida? Ikiwa hakuna yeyote kati yenu anayejua jinsi ya kufanya jambo hili, basi mimi ndiye mtu bora zaidi hapa, na ninyi nyote mnapaswa kujipendekeza kwangu—kwa namna hiyo ninapata kuhisi kuwa muhimu, sivyo? Je, mimi si ndiye mwenye hadhi ya juu kabisa na mwenye uwezo mkubwa kabisa miongoni mwenu? Mimi ndiye mtu wa juu kabisa miongoni mwenu, sivyo?" Wakiwa na maarifa fulani ya ustadi wa kitaaluma au wa kiufundi, wanaogopa sana kwamba wengine watajifunza kutoka kwao, na hawataki wengine wawe sawa na wao. Wataudhika ikiwa mtu yeyote atakuwa na ustadi uleule wa kitaaluma au wa kiufundi au utaalamu kama wao, kwa hivyo daima wanafikiria njia za kujifunza kitu ili wawapite wengine. Wanataka kuwa bora kuliko wengine na daima wanataka kuwazidi wengine ili wahisi kuwa muhimu. Je, huu ndio ufuatiliaji sahihi? (Hapana.) Hasa kwa sababu binadamu wapotovu wana matamanio na ufuatiliaji kama huo, kwa kawaida wanakuza dhana na mawazo ya kufikirika ya kila aina kuhusu kazi ya Mungu, na wanatafuta kuwa daraja la juu kuliko watu wengine, kuwa na hadhi na heshima, kuhisi kuwa muhimu, kuwa wasiofanana na mtu mwingine yeyote, na hata kuwa watu wanaopita uwezo wa binadamu au wasio wa kawaida machoni pa wengine. Kwa hivyo, watu wanapaswa kuachilia dhana na mawazo haya ya kufikirika kuhusu kazi ya Mungu. Kwa upande wa mambo mahususi, hili linapaswa kutendwaje? Msifuatilie karama wala talanta za hali ya juu, na msifuatilie kubadilisha ubora wenu wenyewe wa tabia au silika zenu wenyewe, bali, chini ya hali zenu za asili—kama vile ubora wa tabia, uwezo, na silika—fanyeni wajibu wenu kulingana na matakwa ya Mungu, na mfanye kila jambo kulingana na kile ambacho Mungu anataka. Mungu hataki ufanye mambo yaliyo nje ya uwezo au ubora wako wa tabia—hupaswi kujifanyia mambo kuwa magumu pia. Ni sawa ikiwa utafanya tu kadiri ya uwezo wako kulingana na kile unachoelewa na kile unachoweza kufikia, na utatenda kulingana na kile ambacho hali zako mwenyewe zinaruhusu. Kwa mfano, ikiwa ubora wako wa tabia na talanta zako vinakuruhusu tu kufaa kwa jukumu la kiongozi wa timu, basi fanya kazi nzuri kama kiongozi wa timu, ukiainisha kazi zozote na ustadi wowote wa kitaaluma ulio ndani ya upeo wa jukumu hili, ukivishughulikia kimoja baada ya kingine, na ukivitekeleza kulingana na mbinu na kanuni ambazo Mungu amekufundisha—kwa namna hii, utakuja kumridhisha Mungu. Tuseme kwamba unaongozwa na dhana na mawazo yako ya kufikirika, na unafikiri, "Kwa kuwa ninaweza kuwa kiongozi wa timu, nikijitahidi zaidi kufanya vizuri zaidi, kuvumilia dhiki kidogo na kulipa gharama kidogo na Roho Mtakatifu anafanya kazi kubwa juu yangu, basi je, sitaweza kuwa kiongozi wa kanisa au kiongozi wa kikundi cha kufanya maamuzi? Watu wanaweza kufikiri kwamba sina uwezo huo ndani yangu, lakini nitamsihi Mungu—hakuna jambo lililo gumu kwa Mungu kulitimiza! Sitaki kuwa kiongozi wa timu. Nitamwomba Mungu, nikimsihi Yeye aniruhusu niibebe kazi kubwa zaidi, aniruhusu niwe kiongozi au mfanyakazi." Je, ufuatiliaji wa aina hii ni sahihi? (Hapana, si sahihi.) Kwa nini mnasema kwamba si sahihi? (Watu kama hao daima wanataka kufanya mambo yaliyo nje ya ubora wao wa tabia na uwezo wao wenyewe, na hawawezi kuendelea kufanya kazi yao wenyewe kulingana na ubora wao wa tabia na talanta zao wenyewe, wakibaki katika nafasi yao ipasayo.) Haifai kutaka daima kuwa mtu anayepita uwezo wa binadamu; hili si jambo ambalo mtu wa kawaida anapaswa kufuatilia.

Baadhi ya watu mara nyingi husema, "Hakuna jambo lililo gumu kwa Mungu"; msemo huu ni ukweli, na kila mtu anaweza kuelewa hilo. Lakini baadhi ya watu wana ufahamu potofu, wanaamini kwamba jambo lolote ambalo haliwezekani kwa watu kulifanya linaweza kutimizwa kwa ajili yao na Mungu ikiwa tu watamwomba Yeye, na kwamba kwa kumtegemea Mungu kwa namna hii, watu wanaweza kuvuka silika zao wenyewe na kuwa wanaopita uwezo wa binadamu. Je, ndivyo ilivyo kweli? (Sivyo.) Msemo "Hakuna jambo lililo gumu kwa Mungu" kwa wazi unarejelea nguvu na kiini cha Mungu, uweza yote wa Mungu, na pia utawala wa Mungu juu ya vitu vyote—hakuna jambo ambalo Mungu hawezi kutimiza. Hata hivyo, hili halimaanishi kwamba watu lazima wavuke ubinadamu wa kawaida na wawe wa kupita maumbile; haijalishi Mungu ana uweza wa yote kiasi gani, kazi Anayofanya juu watu inategemea ubinadamu wao wa kawaida na inafanywa ndani ya upeo wa ubinadamu wa kawaida. Mungu hupanga na huendesha vitu vyote, Huendesha watu, matukio, na vitu, ili kwamba vihudumu kwa utimizaji Wake wa mambo ya kila aina, akitimiza mambo halisi ambayo Yuko karibu kutimiza. Katika kipindi ambacho Mungu anatimiza mambo ya kila aina, watu bado wako katika ubinadamu wa kawaida—hakuna kilichobadilika kuwahusu, na bado ni watu. Haijalishi Mungu ana uweza wa yote kiasi gani, na haijalishi ni mbinu gani Mungu anatumia kutawala juu ya jambo fulani au kutimiza jambo fulani, binadamu walioumbwa daima ni binadamu walioumbwa; bado wanaishi katika ubinadamu wa kawaida na si wa kupita maumbile kwa namna yoyote. Je, ninyi nyote mngesema kwamba haya ni mambo ya kweli? (Ndiyo.) "Si wa kupita maumbile" inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba, Mungu anapopanga watu, matukio, na vitu, watu hawawezi kujizuia kuishi, kuendelea kuishi, kufanya kila jambo, na kuishi katika wakati wa sasa chini ya mpango wa Mungu. Lakini unapoishi katika wakati wa sasa, je, ufahamu wako huwa hauko wazi? (Hapana.) Bado una akili timamu. Kwa hivyo, je, ubora wako wa tabia umeboreshwa au umebadilika mara moja? (Hapana.) Unabaki vilevile kama ulivyokuwa hapo awali. Je, silika zako zimebadilika mara moja, basi? Hapana, hazijabadilika pia. Chini ya utawala, mipango, na mipangilio ya Mungu, haijalishi unapitia mambo mangapi, hakuna mabadiliko yoyote katika haiba yako, mazoea yako, mitindo yako ya maisha, na katika ubora wako wa tabia, uwezo wako, na dhima mbalimbali za ubinadamu wako wa kawaida. Ni kwamba tu, watu wanapopitia kazi ya Mungu, wanapitia mambo na watu wa kila aina katika mazingira yao husika, na matokeo yake yakiwa kwamba, katika mchakato wa kupitia kazi ya Mungu, wanapata umaizi na wanajifunza baadhi ya mafunzo. Ikiwa ni watu wanaoufuatilia ukweli, basi wanaweza kupata mavuno kuhusiana na ukweli na kumjua Mungu. Katika mchakato wa kupitia kazi ya Mungu, kufikiri kwa watu ni kwa kawaida, ufahamu wao uko wazi, na ubora wao wa tabia, uwezo wao, na silika zao vinabaki vilevile kama vilivyokuwa hapo awali, bila mabadiliko yoyote. Kwa hivyo, "Hakuna jambo lililo gumu kwa Mungu" inarejelea uweza yote wa Mungu na mpango wa Mungu wa vitu vyote. Hairejelei kuwafanya watu kuwa wa kupita maumbile au kubadilisha kiini cha binadamu walioumbwa. Mungu habadilishi kiini cha watu; binadamu bado ni binadamu, na haijalishi kama wewe ni mwanamume au mwanamke, hakuna mabadiliko yoyote katika suala hili. Mungu hupanga kila kitu, na Mungu ni mweza wa yote; hiki ndicho kile Mungu anacho na alicho, na hiki ndicho anachomiliki Mungu. "Hakuna jambo lililo gumu kwa Mungu" haimaanishi kwamba watu wamekuwa wa kupita maumbile, wala haimaanishi kwamba watu wana uweza wa yote. Hata ikiwa baadhi ya watu wanaweza wakati mwingine kufikia mambo fulani yaliyo inje ya ubora wao wa tabia au yaliyo inje ya silika zao za kimwili, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni Mungu ambaye amewapa karama hii; si kwamba walizaliwa na uwezo huu. Hii ni kwa sababu binadamu walioumbwa hawana uwezo wa kubadilisha haya yote ambayo Mungu ameamuru. Nitatoa mfano rahisi kuhusu suala la silika ya binadamu. Watu wanapoisikia sauti ya kutisha, kwa mfano, watahisi hofu na watajikunyata kisilika. Haijalishi una umri gani, umekuwa hivi tangu utotoni, na bado utakuwa hivi hadi utakapokutana na kifo chako—hii ndiyo silika. "Silika" inamaanisha nini? Ni dhima ya asili ya mwili wa nyama na haitabadilika kamwe. Ni kwa kumiliki tu silika za asili ndipo mtu wa kawaida anaweza kudumisha maisha na kuendelea kuishi katika ubinadamu wa kawaida, kwa hivyo silika za binadamu si jambo ambalo Mungu anakusudia kubadilisha. Je, umeelewa hili? (Ndiyo.) "Mungu ni mweza wa yote" inarejelea nini? (Inarejelea mamlaka ya Mungu Mwenyewe na uweza yote wa Mungu.) Je, ina uhusiano wowote na watu? (Haina uhusiano wowote na watu, na haimaanishi kwamba watu wanaweza kufanya mambo ya kupita maumbile.) Haimaanishi kwamba chini ya udhibiti wa Mungu, watu wana uweza wa yote; hata wakati watu wako chini ya udhibiti wa Mungu, hawawezi kufikia uweza wa yote. Kwa nini iko hivyo? (Kwa sababu watu si Mungu; watu ni viumbe walioumbwa tu, ilhali Mungu ni wa kipekee.) Hiyo ni kweli, hivyo ndivyo ilivyo. Watu daima watakuwa watu. Hawatakuwa spishi nyingine, na, bila shaka, hata zaidi hawatakuwa Mungu; sifa za watu hazitabadilika. Sifa za watu hazitabadilika, kwa hivyo je, silika zao zitabadilika? (Hapana, hazitabadilika.) Silika za watu hazitabadilika, wala mazoea yao ya maisha na mitindo yao ya maisha, au haiba zao za asili ambazo wamepewa na Mungu. Chukua mitindo ya maisha, kwa mfano. Binadamu, kama viumbe wengi, hufanya kazi baada ya jua kuchomoza na hupumzika baada ya jua kutua. Wanapoamka asubuhi, na akili zao zimepumzika vya kutosha na miili yao inahisi vizuri, wanaanza kufanya kazi; usiku, miili yao inapoanza kuchoka, na wanapiga miayo na akili zao zimechoka, wanaanza kuingia katika hali ya kupumzika—huu ni mtindo wa maisha wa kawaida sana. Hii ndio sifa ya kawaida ya binadamu, na pia ndio silika ya binadamu, na bila shaka pia ndio mtindo wa maisha ambao Mungu ameuweka kwa ajili ya binadamu. Mtindo huu huamuliwa kulingana na mzunguko wa jua, mwezi, na nyota, na kuchomoza na kutua kwa jua. Ukivunja mtindo huu wa maisha, kwa muda mfupi huenda kusiwe na matatizo yoyote makubwa—unapohisi uchovu mara kwa mara na unapotaka kulala, unaweza kujizuia na kunywa chai au kahawa kidogo, na uchovu wako wa kimwili utapungua kiasi—lakini kwa muda mrefu, mwili wako utapata matatizo. Kwa nini utapata matatizo? Kwa sababu umekiuka mtindo wa maisha ambao Mungu ameuweka kwa ajili ya watu. Mwili wako unapopata matatizo na uende kumwona daktari, atasema, "Lazima ulale mapema usiku, upumzike ifikapo saa nne usiku, na uamke saa kumi au kumi na moja asubuhi; baada ya miezi michache, utakuwa mzima tena." Baada ya miezi mitatu ya kufuata ushauri wa daktari, dalili zako zote za usumbufu wa kimwili kimsingi zitatoweka, kwa hivyo utafikiri moyoni mwako, "Kumbe matatizo ya mwili wangu hayakutokana na ugonjwa fulani mbaya, bali yalisababishwa na mimi kutofuata mtindo huu wa kawaida katika maisha yangu." Unaona, je, usingesema kwamba mitindo ya maisha ya watu haiwezi kuvunjwa? (Ndiyo.) Mtindo huu wa maisha wa binadamu ni sawa na ule wa viumbe wengine; wote hufanya kazi baada ya jua kuchomoza na hupumzika baada ya jua kutua. Bila shaka, kuna baadhi ya viumbe, kama bundi, ambao hupumzika mchana na hutoka inje na kuchangamka usiku; mtindo wao wa maisha ni tofauti na ule wa binadmu na viumbe wengine, lakini ikiwa ungetaka kuvunja mtindo wao huu, hilo lisingewezekana. Zaidi ya hayo, baadhi ya viumbe hulala usingizi wa majira ya baridi. Je, binadamu wana mtindo huu? (Hapana.) Hapana, binadamu hawahitaji kulala usingizi wa majira ya baridi. Maisha ya binadamu yana mtindo—wanapumzika kwa siku moja au mbili kwa wiki, wanafanya kazi baada ya jua kuchomoza na wanapumzika baada ya jua kutua, na wanadumisha daima mtindo huu wa kawaida wa kazi na kupumzika, na kwa namna hii maisha yao yanaweza kulindwa na kuendelea kwao kuishi kunaweza kudumishwa. Binadamu wana mitindo yao wenyewe ya maisha, na mitindo hii ya maisha iliwekwa na Mungu. Yote ina maana na yote ni kwa madhumuni ya kudumisha maisha ya kawaida na kuendelea kuishi kwa binadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu kwa hakika haitavunja mitindo ya maisha ya binadamu na kuendelea kuishi kama watu wanavyowazia kwamba itafanya, na unapaswa pia kuachilia dhana na wazo hili la kufikirika. Ikiwa binadamu wangevunja kwa nguvu mitindo hii ambayo Mungu ameiweka kwa ajili yao, au ikiwa binadamu wangetaka daima kuibadilisha kwa sababu ya kutawaliwa na mawazo fulani kuhusu mambo ya kupita maumbile, basi huo ungekuwa upumbavu. Ukifikiri kwamba kuibadilisha kutainua maisha yako na kuboresha ubinadamu wako, basi jaribu kuibadilisha na uone ni muda gani utaweza kuishi, uone jinsi mambo yatakavyobadilika katika siku zinazofuata, na ikiwa ubinadamu wako wa kawaida utainuliwa, na ikiwa utakuwa mtu anayepita uwezo wa binadamu, au malaika. Ukiamini kwamba kazi ya Mungu inapaswa kuwa na kipengele cha kupita maumbile ndani yake, na kwamba inapaswa kubadilisha mitindo yako ya maisha, na pia unataka kuibadilisha kwa nguvu ili kujifanya uvuke mipaka ya binadamu, basi unaweza kujaribu. Inaweza kuwa kwamba baada ya kujaribu kwa miaka kadhaa, kwa kweli unabadilisha mitindo ya maisha yako na kuendelea kwako kuishi. Kuna hali moja tu ambapo hili linaweza kutokea, ambayo ni kwamba mwili wako wa nyama hautakuwepo tena, ambapo kweli utakuwa wa kupita maumbile na kugeuka kuwa wingu la moshi, na utageuka kuwa "kiumbe cha mbinguni" na kuwa asiyekufa. Ukitaka kuuweka mwili wako wa nyama katika hali ya kawaida na wenye afya, na uweze kukubali kazi ya Mungu na maneno Yake huku ukiwa katika hali ya kawaida, basi hupaswi kutafuta kuwa yule anayeitwa mtu anayepita uwezo wa binadamu au kufuatilia kile kinachoitwa ubinadamu ulioinuliwa kulingana na dhana na mawazo yako mwenyewe ya kufikirika; badala yake, unapaswa kuishi katika ubinadamu wa kawaida, kudumisha mtindo wa maisha na kuendelea kuishi kwa ubinadamu wako wa kawaida, na pia kudumisha silika za ubinadamu wako wa kawaida. Usitoe matakwa yasiyo na busara kwa Mungu; matakwa haya yasiyo na busara yote yanatokana na mawazo yako ya kufikrika na dhana zako. Silika zako, mitindo yako ya maisha, na kadhalika si mambo ambayo Mungu anakusudia kubadilisha, wala si mambo Anayokusudia kubadilisha kupitia kazi Yake. Mtu aliyeokolewa hakika si mtu aliyejawa na dhana na mawazo ya kufikirika, na sembuse kuwa mtu anayepita uwezo wa binadamu au mtu asiye wa kawaida. Badala yake, yeye ni mtu aliye na ubinadamu wa kawaida, na dhamiri na busara, mtu ambaye anaweza kutii maneno ya Mungu, na kuchukulia watu na mambo, na kujiendesha na kutenda kulingana na kanuni za ukweli; ni mtu anayeweza kumtii Mungu katika mambo yote, ambaye si wa kupita maumbile hata kidogo, na ambaye ubinadamu wake ni wa kawaida na wa vitendo hasa.

Watu wanaoishi katika ubinadamu wa kawaida pia huzuiliwa na silika nyingi za kimwili na mahitaji ya kimwili. Kwa mfano, wakati mwingine watu wanaweza kuchelewesha kufanya wajibu wao kwa siku kadhaa kwa sababu wamechoka sana au ni wagonjwa na wanahitaji kupumzika; wakati mwingine, kwa sababu ya mazingira yenye mvutano, wanaweza kuhisi hofu na kushindwa kutulia ili kufanya wajibu wao; au mara nyingi wanaweza kuhisi wana deni na huzuni mioyoni mwao kwa sababu, kutokana na ubora wao wa tabia na uwezo wao wenye kikomo, hawawezi kumudu aina fulani ya kazi au wajibu—haya yote ni madhihirisho ya kawaida yaliyo ndani ya mipaka ya ubinadamu wa kawaida. Wakati mwingine watu wanaweza kubanwa na hisia au kubanwa na mahitaji ya kimwili, na wakati mwingine wanaweza kuwa chini ya na vizuizi vya silika za kimwili, au vizuizi vya wakati na haiba—hili ni jambo la kawaida na la asili. Kwa mfano, watu wengine wamekuwa wasiojichanganya kabisa na watu tangu utotoni; hawapendi kuzungumza na wanatatizika kutangamana na wengine. Hata wakiwa watu wazima katika miaka yao ya thelathini au arobaini, bado hawawezi kushinda haiba hii: Bado wao si stadi wa kuongea wala hodari wa kuzungumza, wala si stadi wa kutangamana na wengine. Baada ya kuwa viongozi, sifa hii ya haiba huwekea mipaka na huzuia kazi yao kwa kiwango fulani, na hili mara nyingi huwasababishia dhiki na kufadhaika, na kuwafanya wahisi kubanwa sana. Kutojichanganya na watu na kutopenda kuzungumza ni madhihirisho ya ubinadamu wa kawaida. Kwa kuwa ni madhihirisho ya ubinadamu wa kawaida, je, yanachukuliwa kuwa makosa kwa Mungu? Hapana, si makosa, na Mungu atayashughulikia kwa usahihi. Bila kujali matatizo, kasoro, au dosari zako, hakuna hata moja ya mambo haya ambalo ni tatizo machoni pa Mungu. Mungu hutazama tu jinsi unavyoutafuta ukweli, unavyotenda ukweli, unavyotenda kulingana na kanuni za ukweli, unavyotenda kulingana na maneno ya Mungu, na unavyoifuata njia ya Mungu, chini ya hali za asili za ubinadamu wa kawaida—haya ndiyo mambo ambayo Mungu hutazama. Kwa hivyo, katika mambo yanayohusiana na kanuni za ukweli, usiruhusu hali za msingi, kama vile ubora wa tabia, silika, haiba, mazoea, na mitindo ya maisha ya ubinadamu wa kawaida, zikuzuie. Bila shaka, usitumie nguvu na muda wako katika kujaribu kushinda hali hizi za msingi pia, wala usijaribu kuzibadilisha. Kwa mfano, ikiwa una haiba ya kutojichanganya na watu, na hupendi kuzungumza, na wewe si hodari wa kuzungumza, na wewe si stadi wa kutangamana na kuhusiana na watu, hayo si matatizo. Ingawa watu wanaojichanganya na watu wanapenda kuzungumza, si kila kitu wanachosema ni cha manufaa au kinalingana na ukweli, kwa hivyo kuwa mtu asiyejichanganya na watu si tatizo na huhitaji kujaribu kuibadilisha. Unaweza kusema, "Ikiwa ningekuwa mfuasi wa kawaida, lisingekuwa tatizo kwangu kuwa na haiba ya kutojichanganya na watu; lakini sasa mimi ni kiongozi, kwa hivyo si lazima nibadilishe haiba yangu ya kutojichanganya na watu?" Ikiwa kweli unataka kuibadilisha, unaweza kujaribu kujifunza jinsi ya kutangamana na wengine, au kuweka sheria kuhusu kiasi cha mambo unayosema, idadi ya mambo unayoshughulikia, na aina za watu unaoshughulika nao kwa siku moja. Ikiwa kweli una uwezo wa kubadilisha haiba yako ya asili, basi bila shaka, hili si lazima liwe jambo baya katika suala la wewe kufanya kazi ya kanisa. Hata hivyo, ikiwa ulizaliwa na haiba ya kutojichanganya na watu na wewe si hodari wa kuzungumza, na si stadi wa kutangamana na watu, na hujui jinsi ya kuzungumza wala kutangamana na wengine, basi hakuna anayeweza kubadilisha hili. Baadhi ya watu wana haiba ya kutojichanganya na watu, hawako tayari kutangamana wala kuzungumza na wengine, na zaidi ya hayo, hawana mengi ya kusema. Daima wanahisi kwamba ni sawa tu kusema jambo la manufaa, na kwamba hakuna haja ya kusema mambo yasiyo ya lazima, kwa hivyo hawako tayari kusema mengi. Kwa baadhi ya watu, inaweza kuwa kwa sababu wao ni wachanga sana na hawana uzoefu wa maisha na wanakosa maneno; kwa baadhi ya watu, inaweza kuwa kwamba wao si wachanga tena na tayari wana uzoefu wa maisha, lakini bado wana haiba hii ya kutojichanganya na watu. Ukijaribu kubadilisha haiba ya aina hii na kutumia mbinu ya kila aina ili kuibadilisha, basi acha Nikuambie, hutaweza kamwe kuibadilisha katika maisha yako yote, kwa sababu Mungu hafanyi kazi ya aina hii. Haijalishi kama uso au sura yako inafanana na ya baba yako, mama yako au jamaa mwingine yeyote, sura hii haitabadilika, na hata zaidi, haiba yako hasa haitabadilika. Baadhi ya watu husema, "Ni vigumu kubadilisha haiba ya kutojichanganya na watu, kwa hivyo je, ni rahisi kubadilisha ile ya kujichanganya na watu?" Ni vigumu vilevile kubadilisha haiba ya kujichanganya na watu. Watu wanaojichanganya na watu wanapenda kuzungumza na wana mengi ambayo wanataka kusema; ukiwataka wasizungumze au wazungumze kidogo, hawawezi kujidhibiti, na mtu yeyote akiwazuia kuzungumza, ni kama kuwanyang'anya uhai wao. Ikiwa mtu asiyejichanganya na watu atalazimishwa kutangamana na mtu anayejichanganya na watu, je, watashawishiana? Wanaweza kushawishiana kwa kiasi fulani mwanzoni; kwa ajili ya kudumisha heshima, watu hao wawili watachukuliana na kuvumiliana, au watakuwa wenye ustahimilivu na uelewa wao kwa wao. Lakini baada ya muda, watajuana na watapata wazo la wazi la haiba ya kila mmoja wao, na hakutakuwa na haja ya kutenda kwa ustahimilivu na uelewa sana wao kwa wao, kwa hivyo watarudi upesi katika hali zao za asili. Ikiwa hapo awali ulikuwa na haiba ya kutojichanganya na watu, bado wewe ni mtu asiyejichanganya na watu sasa; unapozungumza na unapoongea, unatamka tu maneno au sentensi chache, na huna jambo lingine la kusema. Mtu akiuliza, "Je, ulienda nje?" unajibu, "Nilienda." Kisha akiuliza, "Ulirudi lini?" unajibu, "Sasa hivi." Husemi kilichotokea, na husemi kile ambacho mtu huyo anataka kusikia. Kinyume chake, watu wanaojichanganya na watu hutoa maneno bila kukoma, kama mashinegani, na hata ukiwakatiza, baada ya muda wataendelea kuzungumza. Je, ni rahisi kwa haiba ya mtu kubadilika? (Hapana, si rahisi.) Hili ni jambo ambalo kila mwanadamu aliyeumbwa huzaliwa nalo. Halina uhusiano wowote na tabia potovu au kiini cha ubinadamu wa mtu. Haiba inarejelea kitu gani? Inarejelea tu hali ya nafsi ambayo watu wanaweza kuona kwa nje, na njia ambayo kwayo mtu huchukulia watu, matukio, na vitu. Baadhi ya watu ni hodari wa kujieleza, ilhali wengine si hodari; baadhi wanapenda kufafanua mambo, huku wengine hawapendi; baadhi wanapenda kujiwekea fikira zao, huku baadhi hawapendi kuweka fikira zao ndani, bali wanataka kuyaeleza kwa sauti ili kwamba kila mtu aweze kuyasikia, na ni hapo tu ndipo wanapohisi furaha. Hizi ndizo njia tofauti ambazo watu hushughulikia maisha na watu, matukio, na vitu; hizi ndizo haiba za watu. Haiba yako ni kitu ulichozaliwa nacho. Ikiwa umeshindwa kuibadilisha hata baada ya majaribio mengi, basi acha Nikuambie, unaweza kupumzika sasa; hakuna haja ya kujichosha sana. Haiwezi kubadilishwa, kwa hivyo usijaribu kuibadilisha. Haiba yoyote ya asili uliyo nayo, hiyo ndiyo inabaki kuwa haiba yako. Usijaribu kubadilisha haiba yako kwa ajili ya kufikia wokovu; hili ni wazo potofu—haiba yoyote uliyo nayo, huo ni ukweli halisi, na huwezi kuibadilisha. Kwa upande wa sababu halisi za hili, matokeo ambayo Mungu anataka kutimiza katika kazi Yake hayana uhusiano wowote na haiba yako. Suala la ikiwa unaweza kufikia wokovu pia halihusiani na haiba yako. Zaidi ya hayo, suala la ikiwa wewe ni mtu anayetenda ukweli na aliye na uhalisi wa ukweli halihusiani na haiba yako. Kwa hivyo, usijaribu kubadilisha haiba yako kwa sababu unafanya wajibu fulani au unahudumu kama msimamizi wa kipengele fulani cha kazi—hili ni wazo lenye makosa. Basi, unapaswa kufanya nini? Bila kujali haiba yako au hali zako za asili, unapaswa kushikilia na kutenda kanuni za ukweli. Hatimaye, Mungu hapimi ikiwa unaifuata njia Yake au unaweza kufikia wokovu kulingana na haiba yako, au kulingana na ubora wa tabia wa asili, ustadi, karama, au talanta ulizo nazo, na bila shaka Yeye hatazami ni kwa kiasi gani umezuia silika na mahitaji yako ya kimwili pia. Badala yake, Mungu hutazama ikiwa unatenda na unapitia maneno Yake, ni maneno Yake mangapi ambayo umetenda, ikiwa una nia na azimio la kuufuatilia ukweli, na ikiwa hatimaye umefikia kutenda ukweli na kuifuata njia ya Mungu, katika mchakato wa kumfuata Mungu na kufanya wajibu wako. Hili ndilo jambo ambalo Mungu hutazama. Je, mnaelewa hili? (Ndiyo, tunaelewa.)

Baadhi ya wanawake wanapotenda, wanafanya mambo kwa kasi kubwa, huwa wepesi na wenye nguvu kama radi, na wanafanya maamuzi ya haraka na thabiti; haiba yao ni kama ile ya mwanamume. Ni neno gani maarufu linalotumiwa kuwaelezea siku hizi? Wanawake wenye tabia za kiume. "Wanawake wenye tabia za kiume" si tena wale wajinga, wakubwa, na wazembe ambao watu walizoea kuwarejelea kwa neno hili. Si neno la kudharau; badala yake, ni la kusifu. Lakini Mungu analichukuliaje neno hili la kusifu? Wewe ni mwepesi na mwenye nguvu kama radi, na jasiri na mwenye maamuzi thabiti katika matendo yako, lakini kanuni za utendaji wako na msingi wa matendo yako ni nini? Je, ni ukweli? Je, ni maneno ya Mungu? Hili ndilo jambo la msingi. Ikiwa mwanamume ni wa polepole na mwangalifu sana katika matendo yake, basi katika maneno ya watu wasioamini, yeye ni kama mwanamke aliyefungwa miguu—wengine hata hutumia neno la kudharau, wakisema kwamba yeye ni "wa kike kidogo"—lakini Mungu humtazamaje? Bila kujali kama mtu ni mwepesi na mwenye nguvu kama radi na jasiri na mwenye maamuzi thabiti katika kufanya mambo, au anatenda kama mwanamke aliyefungwa miguu na anaonekana kuwa wa kike kidogo katika matendo yake, je, mojawapo ya mambo haya ni tatizo? (Hapana.) Je, kuwa mwepesi na mwenye nguvu kama radi, na jasiri na mwenye maamuzi thabiti ni sifa nzuri? (Hapana, si lazima.) Kwa hivyo je, ni udhaifu kutenda kama mwanamke aliyefungwa miguu? (Vivyo hivyo hapana, si lazima.) Ingawa moja ya maneno haya mawili "wanawake wenye tabia za kiume" na "wa kike kidogo" ni la kusifu na lingine ni la kudharau, kiini cha aina hizi mbili za mienendo au namna za kufanya mambo hakipaswi kuhukumiwa kulingana na maana zake za moja kwa moja. Ni nini kinachopaswa kutumiwa kuhukumu hili? (Ikiwa kile ambacho mtu anatenda ni neno la Mungu au la.) Msingi wa matendo yake, na pia matokeo ambayo anakusudia kufikia, vinapaswa kutumiwa kuhukumu hili. Ikiwa msingi wa matendo yake ni neno la Mungu na kanuni za ukweli, basi kimsingi kuna uhakika wa asilimia 90 kwamba hafanyi kosa lolote. Ikiwa si tu kwamba anafanya mambo kulingana na kanuni za ukweli, bali zaidi ya hayo, matokeo anayokusudia kufikia ni yale ya kulinda ushuhuda wa Mungu na masilahi ya nyumba ya Mungu, na ya kuwaimarisha ndugu na dada wengi zaidi, basi tunaweza kuwa na uhakika kwa asilimia 100 kwamba hafanyi kosa lolote. Haijalishi kama anatenda kwa ujasiri na kwa uthabiti au kama mwanamke aliyefungwa miguu—haijalishi jinsi anavyotenda kwa nje—hilo si muhimu. Kile ambacho ni muhimu ni ikiwa kanuni za ukweli ndizo msingi wa matendo yake au la, na kama lengo la matendo yake na matokeo anayokusudia kufikia kupitia matendo yake ni yale ya kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu na kazi ya kanisa, na ya kuwaimarisha watu zaidi au la. Kwa hivyo je, namna ya matendo yao ni muhimu? (Hapana, si muhimu.) Bila kujali kama wewe ni mwanamke mwenye tabia za kiume au kama mwanamke aliyefungwa miguu, hili si jambo ambalo Mungu hulitazama; hiki si kigezo ambacho Mungu hutumia kuwatathmini watu. Kwa hivyo, ikiwa mwanamke anaonekana kama mwanamke mwenye tabia za kiume, na katika matendo yake, yeye ni mwepesi na mwenye nguvu kama radi, na jasiri na mwenye maamuzi thabiti, je, hili linastahili sifa na heshima? (Hapana, halistahili.) Je, kuwa mwepesi na mwenye nguvu kama radi, na jasiri na mwenye maamuzi thabiti ni kanuni ya kufanya mambo? (Hapana.) Bila kujali kama wewe ni mwanamume au mwanamke, kuwa jasiri na mwenye maamuzi thabiti na mwepesi na mwenye nguvu kama radi si kanuni ya kufanya mambo. Basi, kanuni ya kufanya mambo ni nini? (Mtu lazima afanye mambo kulingana na kanuni za ukweli, na matokeo ambayo mtu anakusudia kufikia lazima yawe kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu na kuwaimarisha watu wengi zaidi—hii ndiyo kanuni.) Hii ni kanuni mahususi. Ukitenda kulingana na kanuni hii, basi unatenda ukweli; usipotenda kulingana na kanuni hii, basi machoni Pangu, onyesho linalokufafanua vyema kabisa kuwa jasiri na mwenye maamuzi thabiti, mwepesi na mwenye nguvu kama radi ni "kufanya maovu kiholela." Ni wazi kwamba kufanya maovu kiholela si kutenda kulingana na kanuni za ukweli; ingawa unaonekana kufanya maamuzi kwa thabiti na bila kusitasita katika matendo yako, na unaonekana kuwa na mwonekano wa kiongozi au mfalme, kwa kweli unafanya maovu kiholela. Matokeo ya kufanya maovu kiholela ni yapi? Jambo hili husababisha vurugu na usumbufu, na huhujumu kazi ya kanisa. Kwa hivyo, je, Mungu atakumbuka jambo hili? (Hapana.) Si tu kwamba Mungu hatakumbuka jambo hili, bali pia Atalilaani. Kwa hivyo, unasema kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia za kiume, na kwamba katika matendo yako wewe ni mwepesi na mwenye nguvu kama radi, na jasiri na mwenye maamuzi thabiti, lakini je, hilo lina manufaa? (Hapana, halina manufaa.) Ni kuutafuta ukweli na kutenda kulingana na kanuni za ukweli pekee ndiko kunaweza kuitwa uwezo wa kweli; huku tu ndiko kutenda ukweli na kufuatilia ukweli, na jambo hili tu ndilo ambalo watu walio na ubinadamu wa kawaida wanapaswa kulifanya. Tuseme unasema, "Hii ni haiba yangu tu na haiwezi kubadilika, kwa hivyo ninapaswa kufanya nini?" Kuna suluhisho rahisi. Iwe wewe ni mtu mwenye mwendo wa haraka au una tabia ya polepole, hilo si tatizo; usibanwe na jambo hili. Pia hakuna haja kwako kujitahidi kubadilisha mbinu yako ya kufanya mambo kwa sababu unataka kutenda kulingana na kanuni. Bila kujali mbinu yako, ikiwa msingi wa matendo yako ni kanuni za ukweli, na matokeo unayofikia ni yale ya kulinda ushuhuda wa Mungu, masilahi ya Mungu, na kazi ya nyumba ya Mungu, basi haya ndiyo matendo mema, na yatakumbukwa na Mungu. Kinyume chake, bila kujali kama wewe kwa nje ni mwoga na mwenye kusitasita kama mwanamke aliyefungwa miguu, au ni mwepesi na mwenye nguvu kama radi kama kiongozi au mfalme—bila kujali umbo la nje la matendo yako—ikiwa hutendi kulingana na kanuni za ukweli, basi unasababisha vurugu na usumbufu, na haya ni matendo maovu, na yatalaaniwa na Mungu, na hayatakumbukwa na Mungu. Hii ndiyo kanuni ya kuhukumu ikiwa mtu ni mwema au mwovu. Je, mnaelewa? (Ndiyo.) Kwa hivyo, sasa kwa kuwa tumemaliza kufanya ushirika kuhusu mambo haya, je, mna uelewa fulani kuhusu ni dhana na mawazo gani ya kufikirika ambayo watu huwa nayo kuhusu kazi ya Mungu? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mnayaelewa, je, mnajua baadhi ya mikengeuko ambayo watu huwa nayo katika mchakato wao wa kumwamini Mungu na kuufuatilia ukweli? Je, pia mko wazi kuhusu jinsi mnavyopaswa kutenda? (Ndiyo, tuko wazi.)

Kusudi la kuelewa dhana na mawazo ya kufikirika ya watu, kwa upande mmoja, ni kuwazuia watu kuishi kulingana na dhana na mawazo haya ya kufikirika na kutembea katika njia isiyo sahihi ya maisha. Kwa upande mwingine, ni kuwawezesha watu—huku wakiachilia dhana na mawazo haya ya kufikirika—kuishi ndani ya ubinadamu wa kawaida kwa urahisi na furaha, kutimiza majukumu na wajibu wao, na kutojilazimisha kufanya mambo wasiyoweza. Ikiwa kuna jambo ambalo unaweza kulifikia na ambalo unapaswa kulifanya, basi jitahidi kadiri uwezavyo kulifanya; ikiwa jambo liko nje ya ubora wako wa tabia na uwezo wako, basi tafuta mtu wa kushirikiana na yeye kulihusu au uombe msaada kutoka kwa ndugu na dada wengine, na ulifanye kwa uwezo wako wote—hizi ndizo kanuni. Kwa muhtasari, kile ambacho watu wanapaswa kuelewa kuhusu jambo hili ni kwamba, katika kipindi ambacho Mungu anafanya kazi, ubinadamu wa kila mtu unakua hatua kwa hatua kuelekea upande mzuri katika mchakato wa kukubali maneno ya Mungu, na ndani ya mipaka ya hali za msingi za asili za ubinadamu wao, badala ya kuwa uliopotoka, wa kupita maumbile, au usio wa kawaida. Kwa hivyo, ikiwa wajibu unaofanya unahusisha ustadi wa kiufundi au wa kitaaluma, basi ili kufanya wajibu huo vizuri, na kufikia matokeo bora zaidi katika wajibu huo, unapaswa kujitahidi ili kujifunza kwa bidii na kuchunguza kwa kina ustadi huo wa kiufundi au wa kitaaluma. Hupaswi kungoja kwa upofu Mungu atende kulingana na fikira na mitazamo kama vile "Mungu ni mwenye uweza wa yote, na jambo lolote ambalo haliwezekani kwa watu kulifanya linaweza kutimizwa na Mungu ikiwa tu tutamwomba Yeye" na mawazo ya kufikirika kuhusu mambo ya kupita maumbile, bila kujitahidi ili kujifunza ustadi huo wewe mwenyewe. Unapaswa kuuweka moyo wako wote, nguvu zako zote, na akili yako yote katika kufanya kile kilicho ndani ya mipaka ya kile ambacho ubora wako wa tabia unaweza kufikia, na linapokuja suala la yale yaliyo nje ya ubora wako wa tabia na uwezo wako, usijifanyie mambo kuwa magumu, usijilemee, usijitwike mzigo, wala usijiwekee shinikizo la aina yoyote, badala yake chukulia mambo kwa urahisi. Kwa mfano, chukulia kujifunza ustadi wa kutumia kompyuta. Tuseme kwamba umri wako umeenda kiasi, na kulingana na umri wako, ubora wako wa tabia, na hali zako za sasa, kujifunza tu kupiga chapa tayari ni mafanikio makubwa kwako. Ikiwa unaweza pia kujifunza kuwasiliana na ndugu na dada na kufanya kazi mtandaoni, hilo tayari ni jambo zuri sana. Hata hivyo, hutosheki kamwe na bado una tamaa ya mengi zaidi—unataka kujifunza jinsi ya kuandika programu na kuweka mtandao salama, ukifanya kazi fulani ambayo wahandisi wa mtandao na wafanyakazi wa teknolojia ya hali ya juu pekee ndio wanaoweza kufanya. Je, huo si upumbavu? (Ndiyo.) Huwezi kumudu mambo haya, kwa hivyo unakuwa hasi na unamlalamikia Mungu: "Mungu, kwa nini Ulinipa ubora wa tabia wa aina hii? Kwa nini siwezi kumudu mambo haya? Mimi ni mzee sana—kwa nini Huwezi kunifanya kijana tena? Je, Mungu si mwenye uweza wa yote?" Ni makosa kwako kuwa na fikira kama hizo na kutoa matakwa kama hayo. Inamaanisha nini "kufanya chochote kilicho ndani ya uwezo wa mtu, na kutovuka ubora wa mtu wa tabia, uwezo wake, na silika zake"? Chochote ambacho ubora wako wa tabia na uwezo wako vinakuruhusu kufikia, hicho ndicho Mungu anataka kutoka kwako. Chochote kilicho nje ya uwezo wako, Mungu hakitaki kutoka kwako, na huhitaji kujiwekea matakwa hayo pia. Ikiwa huwezi kufanya jambo fulani, kuna wengine wanaoweza kulifanya; Mungu hataki kwamba wewe uwe ndiye wa kulifanya. Unasema, "Mimi ni mzee—sijui jinsi ya kupakia video, sijui jinsi ya kuweka mtandao salama pia, na sembuse kujua jinsi ya kuandika programu," na bado unasisitiza kujifunza mambo haya—je, umeuliza iwapo nyumba ya Mungu inakuhitaji ufanye kazi hii? Je, umefanya kazi yako mwenyewe ipasavyo? Je, umefanya kazi ambayo ubora wako wa tabia unakuruhusu kufikia ipasavyo? Ikiwa hujaifanya ipasavyo, na bado unasisitiza kujaribu kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wako na uelewa wako, na ambayo hata hutaweza kamwe kujifunza katika maisha yako yote, je, unafikiri kwamba nafsi yako mwenyewe au unapambana na Mungu? Je, hili si la kusumbua sana? (Ndiyo.) Daima unataka kujipita na kuwa mtu anayepita uwezo wa binadamu, lakini Mungu hajakutaka ufanye hivyo. Kunaweza tu kuwa na sababu moja kwa nini unataka kuwa mtu anayepita uwezo wa binadamu, ambayo ni kwamba unataka kujionyesha na hutakubali kushindwa wala kukubali uzee. Si kwa ajili ya kufanya wajibu wako vizuri kwamba unavumilia dhiki na kulipa gharama; hufanyi wajibu wako kulingana na kanuni ya kujiendesha kwa namna ya nidhamu na kushikilia kwa uthabiti nafasi yako ipasayo. Unataka kuthibitisha kwamba wewe si mzee kwa kuzipa changamoto ubora wako wa tabia na uwezo wako. "Bado nina uwezo," unafikiri. "Mimi ni hodari kama wengine, ninaweza kufanya chochote ambacho watu wengine wanaweza kufanya!" Je, jambo hili lina maana? (Hapana.) Halina maana. Jitihada hizi zote unazoweka ni za bure na hazina thamani. Ikiwa utaweka moyo wako wote, akili yako yote, na nguvu zako zote katika kufanya ipasavyo yale ambayo hali zako mwenyewe zinakuruhusu kufikia, basi Mungu ataridhika. Usijipe changamoto, wala usitafute kuvuka mipaka yako. Mungu anajua jinsi ubora wako wa tabia na uwezo wako ulivyo. Ubora wa tabia ambao Mungu amekupa na talanta ambazo Mungu amekupa vimekwishaamuliwa na Yeye tangu zamani. Kutaka daima kuvipita hivi ni kuwa na kiburi na kujikadiria kupita kiasi; ni kutafuta shida na bila shaka kutaishia katika kushindwa. Je, watu kama hao hawapuuzi kazi zao zinazofaa? (Ndiyo.) Hawajiendeshi kwa namna ya kutii sheria, na hawashikilii kwa uthabiti nafasi zao zinazofaa ili kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa—hawafuati kanuni hizi katika matendo yao, bali badala yake daima hujaribu kujionyesha. Kuna msemo wa sehemu mbili: "Bibi kizee anapaka rangi ya midomo—ili kukupa kitu cha kutazama." Kwa madhumuni gani "bibi kizee" angefanya hili? (Ili kujionyesha.) Bibi kizee anataka kukuonyesha: "Mimi, kama bibi kizee, si wa kawaida—nitakuonyesha kitu maalum." Hataki kudharauliwa, bali badala yake anataka kuenziwa na kuheshimiwa sana; anataka kutoa changamoto kwa mipaka yake na kujipita. Je, huku si kuwa na asili ya kiburi? (Ndiyo.) Ikiwa una asili ya kiburi, basi hubaki ndani ya mipaka yako, hutaki kujiendesha kwa namna inayofaa hadhi yako. Daima unataka kujipa changamoto. Chochote ambacho wengine wanaweza kufanya, unataka kuweza kukifanya pia. Wengine wanapofanya mambo yanayowafanya wajitokeze, wafikie matokeo, au watoe michango, na wapokee sifa za kila mtu, unahisi vibaya, wivu, na kutoridhika. Kisha unataka kuacha kazi zako za sasa ili kufanya kazi inayokuruhusu kung'aa, ukitamani kuenziwa sana pia. Lakini huwezi kufanya kazi inayokuruhusu kujitokeza, kwa hivyo je, huku si kupoteza muda? Je, huku si kupuuza kazi zako zinazofaa? (Ndiyo.) Usipuuze kazi zinazofaa, kwa maana kuzipuuza hakutaishia vizuri. Si tu kwamba kunachelewesha mambo na kupoteza muda, bali pia kunamfanya Mungu akuchukie na kuwafanya wengine wakudharau, na mwishowe, unajitesa na kuwa hasi kabisa. Bila kujali umri wa mtu—iwe yeye ni kijana, wa makamo au mzee—ana mipaka katika suala la ubora wake wa tabia na talanta zake; hakuna mtu aliye mkamilifu. Sahau kuhusu kuwa mtu mkamilifu, sahau kuhusu kujua jinsi ya kufanya kila kitu, kuweza kufanya kila kitu, na kuelewa kila kitu—ni jambo la kusumbua ikiwa una tabia ya aina hii.

Katika kazi ya Mungu, Anaponena na watu wa kila aina kuhusu mada yoyote au suala la aina yoyote, daima Hushughulikia hali mbalimbali—kwa nini Yeye hunena tena na tena kuhusu jambo lilelile akishughulikia hali na mazingira tofauti? Wale wanaokosa ufahamu wa kiroho wanafikiri, "Kuzungumza kwa njia hii kuna maelezo mengi mno na ni kurefusha maneno; tayari tumeelewa." Huenda wewe tayari umeelewa, lakini wengine huenda hawajaelewa; na hata kama unaelewa, je, unaweza kutatua matatizo yanayotokana na hali mbalimbali? Ikiwa huwezi, inamaanisha kwamba bado huelewi kikamilifu, kwa hivyo usijifanye kwamba unaelewa. Hali za watu zote ni tofauti. Ni pale tu ambapo hali zote za mtu wa kila aina zimezungumziwa, na hali mbalimbali zote zimeshughulikiwa—yaani, mara tu hali za watu wa kila aina ndani ya suala fulani kuu zimejadiliwa zote, na kila mtu anaelewa kipengele hiki cha ukweli—ndipo suala hili limeelezwa waziwazi. Ninamaanisha nini kwa hili? Ni kwamba kila mtu hukumbana na matatizo tofauti huku akiishi chini ya hali zake mwenyewe; matatizo ya kila mtu ni tofauti, haiba na nguvu za kila mtu ni tofauti pia, na mambo ambayo yeye ni hodari kwayo pia ni tofauti. Kwa hivyo, kila mtu ana hali zake binafsi, matatizo yake mwenyewe, na fikira na mitazamo yake tofauti. Hata hivyo, haijalishi hali za watu wenyewe ni tofauti kiasi gani, na haijalishi uwezo wao, ubora wao wa tabia, mipaka yao ya maono, haiba yao, na mazoea yao ni tofauti kiasi gani, tabia potovu na kiini cha asili cha binadamu ni sawa. Yaani, haijalishi hali mbalimbali za ubinadamu wa watu ni tofauti kiasi gani, watu wana sifa za pamoja. Kwa nini binadamu wana sifa zilezile za pamoja? Kwa sababu kiini cha tabia ambacho binadamu hukitegemea ili kuendelea kuishi ni sawa. Kwa hivyo, baada ya hali na matatizo ya watu wa kila aina kufichuliwa, kile ambacho binadamu wanahitaji kufanya ni kutenda kulingana na ukweli na kanuni ambazo Mungu anataka, na kisha matatizo ya pamoja ya binadamu yatatatuliwa. Haijalishi haiba yako wala ubora wako wa tabia, haijalishi una uwezo kiasi gani, na haijalishi ikiwa wewe ni mwanamume au mwanamke, au ikiwa ulizaliwa Magharibi au Mashariki, au ikiwa unatoka Kusini au Kaskazini, mradi tu tabia zako potovu zinatatuliwa kupitia kuukubali ukweli, kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kupitia kutenda ukweli, matatizo yako yatatatuliwa. Hili linamaanisha kwamba hali mbalimbali zote zinazotokea ndani ya watu katika muktadha wa matatizo ya pamoja ya binadamu zinaweza pia kutatuliwa. Kwa nini hali mbalimbali hutokea ndani ya watu? Ni kwa sababu hali za asili za ubinadamu ambazo kila mtu anazo ni tofauti. Kwa mfano, ikiwa unaishi Kusini, na una baadhi ya mazoea na mitindo ya maisha vya watu wa kusini, na pia unakuza baadhi ya sifa za haiba na mtindo wa maisha ambazo ni maalum kwa watu wa kusini, basi ukiwa na usuli wa aina hii, utakuza dhana na mawazo fulani maalum ya kufikirika, fikira na mitazamo fulani maalum, na hali fulani maalum. Ikiwa ulizaliwa Kaskazini, ungekuwa na haiba na mazoea ya maisha ya watu wa kaskazini, au baadhi ya hali zinazotokana na desturi, usuli wa kitamaduni, mbinu za elimu, na mambo mengine kama hayo ambayo ni ya asili kwa watu wa kaskazini. Kwa namna hii, hali zinazotokea ndani ya watu wanaoishi Kusini na Kaskazini ni tofauti. Hata hivyo, chanzo na kiini cha hali zinazotokana na tatizo moja ni sawa, kwa hivyo zote zinaweza kutatuliwa kwa ukweli uleule. Kwa kuwa hali iko hivi, haijalishi ikiwa unatoka Kaskazini au Kusini, au unatoka Mashariki au Magharibi; mradi tu wewe ni mwanadamu aliyeumbwa, matatizo yako yote yanaweza kutatuliwa kwa ukweli. Je, umeelewa? Je, suala hili ni ni lenye utata? (Sasa kwa kuwa nimesikia likielezwa, ninahisi kwamba si lenye utata tena.) Kwa nini unasema kwamba suala hili si lenye utata? (Ingawa hali, usuli, na haiba za watu wenyewe ni tofauti, na hili kiasili husababisha hali tofauti, chanzo cha hali hizi tofauti ni sawa, na kiini potovu cha watu ni sawa. Haijalishi watu wanafunua tabia potovu kiasi gani, inaweza kutatuliwa kwa ukweli uleule; kwa hivyo, ukweli unaweza kutatua matatizo ya kila mtu.) Bila kujali kama watu wanatoka Kusini, Kaskazini, Mashariki, au Magharibi, bila kujali kama wao ni wanaume au wanawake, vijana au wazee, na bila kujali hali zao wenyewe ni zipi, tabia zao potovu ni sawa, na hali mbalimbali, fikira na mitazamo, na mielekeo kuelekea ukweli ambao tabia hizi potovu husababisha vina sifa ya pamoja. Sifa hii ya pamoja ni ipi? Kila kitu kinachotokana na tabia hizi potovu ni cha Shetani na hakilingani na ukweli; bila shaka, kwa kuwa mahususi zaidi, inaweza kusemwa kwamba ni kinyume na ukweli. Kwa hivyo, haijalishi kuna tofauti gani kati ya jamii, dini, au tamaduni za binadamu wapotovu, na haijalishi ikiwa watu wana ngozi ya njano, nyeupe, kahawia, au nyeusi, wote ni binadamu wapotovu, na binadamu wote wana kiini sawa cha kumpinga Mungu. Hili ni jambo ambalo wanalo kwa pamoja. Kwa hivyo, bila kujali watu wanatoka nchi gani au wao ni wa jamii gani, kwa ujumla wanarejelewa kama binadamu wapotovu. Yaani, bila kujali kama jamii hizi za watu ni bora au duni, maskini au tajiri katika suala la rangi yao ya ngozi, sura yao, mazoea yao ya maisha, au utamaduni wao wa kijamii, na bila kujali wamepokea elimu gani, kwa vyovyote vile, kanuni ambazo wanazitegemea kwa ajili ya kuendelea kwao kuishi zinatoka kwa Shetani, hazipatani na ukweli, na zinampinga Mungu. Hata kama watu ni wa jamii tajiri na yenye hadhi ya juu, yenye usuli wa kidini ulio wa kiwango cha juu, kiini chao bado ni kile cha binadamu wapotovu, bado wao ni wa aina ya Shetani inayompinga Mungu, bado wao ni binadamu wapotovu, wote wanampinga Mungu, wote ni wale wanaohukumiwa na wanaoadibiwa ndani ya kazi ya Mungu, na wale miongoni mwao wanaoweza kuukubali ukweli ndio wale ambao Mungu anakusudia kuwaokoa. Hili linamaanisha nini? Ni kwamba haijalishi wewe ni wa nchi gani wala jamii gani, kabla ya kufikia wokovu, unaweza kumpinga Mungu, na kiini chako kina uhasama kwa Mungu na hakipatani na Mungu. Haijalishi usuli wako wa kitamaduni ni wa kiwango cha juu kiasi gani, usuli wako wa elimu ni wa kiwango cha juu kiasi gani, usuli wako wa kidini ni wa kiwango cha juu kiasi gani, kiini chako kinabaki bila kubadilika—bado ni kile cha kumpinga Mungu. Kwa hivyo, kiini cha binadamu hakitabadilika kwa sababu ya rangi yao ya ngozi, dini yao, nchi yao ya kuzaliwa, au usuli wao wa elimu au usuli wao wa kitamaduni. Vivyo hivyo, haijalishi mtu ni wa jamii gani, hatakuwa kabaila au duni machoni pa Mungu kwa sababu ya hali zake mwenyewe. Basi machoni pa Mungu, kigezo cha kutathmini iwapo watu ni wa hali ya juu au duni ni kipi? Kuna kigezo kimoja tu, na hicho ni iwapo unaukubali ukweli au la. Ukiukubali ukweli, basi haijalishi jamii yako au rangi ya ngozi yako, wewe ni kabaila. Usipoukubali ukweli, basi hata ukisema, "Nina ngozi nyeupe, nywele za kimanjano, na macho ya bluu, na familia yangu imekuwa ya kifalme kwa vizazi," hakuna manufaa katika hilo! Hata kama wewe ni kabaila miongoni mwa binadamu, usipoukubali ukweli, basi machoni pa Mungu bado wewe ni mwanadamu mpotovu, wewe ni sawa na mwanadamu mwingine yeyote mpotovu—hakuna tofauti. Haijalishi ni washiriki wangapi wa jamii ya binadamu wanaokuenzi, wanaokuheshima, na wanaokutolea matoleo, hilo halina manufaa na halitabadilisha hadhi, utambulisho, na kiini chako machoni pa Mungu. Kigezo cha Mungu cha kutathmini binadamu—ambacho bila shaka pia ni kigezo na kipimo cha juu cha kutathmini binadamu ambacho ni cha asili kwa Mungu—ni kuwatathmini kwa ukweli. Ikiwa unapenda ukweli na unatenda ukweli, basi wewe ni kabaila; ikiwa hutendi ukweli, basi mwili wako huu wa zamani ni mwanadamu mpotovu; hauna thamani ya senti moja, na hata hauna thamani kama chungu aliye chini. Isipokuwa vijiumbe vidogo sana ambavyo watu hawawezi kuviona, chungu ni wadogo kiasi miongoni mwa viumbe wote walio hai. Mitindo yao ya maisha, kanuni zao za kuendelea kuishi, na silika zao hufuata kikamilifu sheria zilizowekwa na Mungu. Ratiba yao ya kufanya kazi na kupumzika hubadilika kulingana na hali ya hewa na mabadiliko ya halijoto ya majira manne, na hawatawahi kubadilisha mitindo na kanuni hizi kwa hiari. Lakini binadamu ni tofauti. Binadamu daima wanataka kubadilisha hali ilivyo na dunia, daima wana tamaa ya makuu, na wanajihusisha daima na usaliti na uasi. Ingawa chungu hawana uwezo wa kuukubali ukweli, wala uwezo wa kuufahamu ukweli, angalau hawampingi Mungu. Binadamu ni tofauti; watajitokeza kwa hiari kumshambulia na kumpinga Mungu. Kwa hivyo, machoni pa Mungu, binadamu ambao hawajaupata ukweli na hawajaokolewa hawana thamani yoyote. Je, huu si ukweli? (Ndiyo.) Kuwatathmini na kuwaainisha watu kulingana na ukweli huu kunalingana kikamilifu na kanuni za ukweli. Kupitia kufanya ushirika kuyahusu masuala haya, watu wanapaswa kuwa na mtazamo na ufahamu sahihi kuhusu kiini cha binadamu na matokeo ambayo kazi ya Mungu inakusudia kufikia. Baada ya kuelewa kipengele hiki cha ukweli, je, hutabanwa sana unapowahubiria watu injili au unapotangamana na kufanya ushirika nao, haijalishi wao ni watu wa aina gani—bila kujali kama wana usuli wa kidini au la, kama wana cheo na hadhi katika jamii au hadhi duni ya kijamii, na kama wao ni weupe au watu wa rangi? (Ndiyo.) Ikiwa huuelewi ukweli huu, daima utaelekea kuwaona watu wa jamii nyingine kuwa bora, au kuhisi kwamba huwezi kuwaelewa, na hujui jinsi ya kufanya ushirika au kutangamana nao. Je, kuuelewa ukweli huu hakuwasaidii kutangamana na watu hao? Kutawasaidia kuitazama jamii yote ya binadamu kutoka katika msimamo sahihi na kutoka katika mtazamo sahihi. Haya ndiyo manufaa ya kuuelewa ukweli. Unapouelewa ukweli, mtazamo wako kuyahusu mambo utakuwa sahihi na pia utakuwa wenye fikira pana kiasi, na si wenye fikira finyu sana. Vinginevyo, daima utakosa ujasiri kama kiongozi au mfanyakazi. Kwanza, utahisi kwamba unakosa uzoefu wa maisha. Pili, utahisi kwamba hujapitia mambo ya kutosha. Tatu, utahisi kwamba wewe si hodari wa kuzungumza na huwezi kung'amua hali za watu wengi kabisa; hasa, unapowaona watu wazee, utaogopa na kuwa na wasiwasi, na hutathubutu kuzungumza. Baadhi ya watu husema, "Hasa ninapoona kwamba waumini wa kidini wa muda mrefu wana maarifa fulani kuhusu Biblia, sijui jinsi ya kuwahubiria injili, nami huogopa na hujihisi duni mbele yao." Unaelewa ukweli mwingi sana, kwa hivyo ni kitu gani unachoogopa? Je, huku si kushindwa kung'amua mambo? Mara tu watu wanapouelewa ukweli, wanapaswa kuweza kutatua mambo na matatizo haya, na hawatabanwa tena na mambo haya.

Ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mmeelewa kupitia mada ambazo tumefanya ushirika kuzihusu leo? Je, mko wazi kuhusu kazi ya Mungu, na jinsi Mungu anavyowaokoa watu, mbinu za Mungu za kuwaokoa watu, na vipengele vya watu ambavyo Mungu hubadilisha? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mko wazi kuyahusu mambo haya, je, hamhisi hata zaidi umuhimu wa kutenda ukweli na wa kutathmini kila kitu kwa ukweli? (Ndiyo.) Je, hamfikirii hata zaidi kwamba ni muhimu sana kuufuatilia na kuuelewa ukweli? Ikiwa mtu hauelewi ukweli, basi hawezi kung'amua jambo lolote, hawezi kung'amua watu wa aina zote, na hawezi kung'amua watu kutoka nchi na makabila yote, na kwa hivyo yeye ni mpumbavu, mjinga. Baadhi ya watu wanapowaona watu wanaovaa miwani, wanadhani kwamba wao ni maprofesa au wasomi, na kwa hivyo wanahisi kubanwa na hawathubutu kuzungumza, na kila wanapowaona watu warefu na wenye sura nzuri, wanahisi duni mbele yao. Baada ya kuelewa ukweli, je, watu kimsingi hawataathiriwa na mambo haya? Kwa upande mmoja, hawatajibana; kwa upande mwingine, wataboresha—kwa kiwango fulani—mtazamo na maoni yao kuhusiana na kushughulika na watu na mambo, na pia watakuwa na umaizi fulani kuyahusu. Hili litakuwa na manufaa kwa utekelezaji wa wajibu wao, hasa linapokuja suala la viongozi na wafanyakazi katika viwango vyote kutekeleza kazi.

2. Jinsi ya Kushughulikia kwa Usahihi Hali za Asili za Mtu Mwenyewe

Baada ya watu kuelewa walengwa na umuhimu wa kweli wa kazi ya Mungu, je, wanapaswa kutendaje ili kushughulikia hali zao wenyewe za asili kwa usahihi? Kuna kanuni ngapi? (Zile ninazoweza kufikiria ni kwamba watu wanapaswa kutazama haiba yao wenyewe, ubora wao wenyewe wa tabia, na hali zingine kwa usahihi, waache kufuatilia mambo ya kupita maumbile na waache kutafuta kuwa wanaopita uwezo wa binadamu, wafanye chochote wanachoweza kufanya kwa kadiri ya uwezo wao, na wasijilazimishe kufikia kile kilicho nje ya uwezo wao. Kwa namna hiyo, maisha yao yatakuwa huru zaidi, na ubinadamu wao utakuwa wa kawaida zaidi na zaidi.) Kwanza kabisa, ukitaka kuepuka kufanya mambo ya kipumbavu au ya kijinga, lazima kwanza uelewe hali zako mwenyewe: ubora wako wa tabia ukoje, ubora wako ni upi, wewe ni hodari katika mambo gani, na wewe si hodari katika mambo gani, na vilevile mambo gani unayoweza na usiyoweza kufanya kulingana na umri wako, jinsia yako, maarifa uliyo nayo, na umaizi na uzoefu wako wa maisha. Yaani, unapaswa kuwa wazi kuhusu mambo unayofanya vizuri na udhaifu wako katika wajibu unaotekeleza na kazi unayofanya, na kuhusu mapungufu na sifa nzuri za haiba yako mwenyewe. Mara tu unapokuwa wazi kuhusu hali zako mwenyewe, sifa zako mwenyewe nzuri, na mapungufu yako mwenyewe, unapaswa kisha kuangalia ni sifa gani nzuri na mambo gani unayofanya vizuri unayopaswa kudumishwa, ni mapungufu yapi na dosari zipi zinazoweza kurekebishwa kwa kiwango fulani, ni mapungufu yapi na dosari zipi zinazoweza kushindwa ndani ya muda mfupi au chini ya hali maalum, na ni zipi ambazo haziwezi kushindwa kabisa—lazima uwe wazi kuhusu mambo haya. Ili kufikia uwazi huu, kwa upande mmoja, unapaswa kuutafuta ukweli, kutafakari na kupata maarifa kuhusu mambo haya kwa kulinganisha maneno ya Mungu na hali yako halisi, na, wakati huohuo, kumwomba Mungu afunue mambo haya. Kwa upande mwingine, unaweza pia kuwauliza ndugu na dada walio karibu na wewe na kuwaomba wakupe vidokezo na mwongozo. Kwa namna hiyo, utakuwa na uelewa wa kina zaidi kujihusu, na utakuwa na mawazo na vidokezo zaidi linapokuja suala la kujijua. Kuna baadhi ya matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa na watu. Kwa mfano, unaweza kuwa na mwelekeo wa kupata wasiwasi unapozungumza na wengine; unapokabiliwa na hali mbalimbali, unaweza kuwa na mawazo na mitazamo yako mwenyewe lakini usiweze kueleza mambo hayo waziwazi. Unahisi wasiwasi hasa kunapokuwa na watu wengi; unazungumza kwa namna isiyoeleweka na kinywa chako kinatetemeka. Baadhi ya watu hata hugugumiza; kwa wengine, ikiwa kuna watu wa jinsia tofauti, hawaeleweki hata zaidi, hawajui kabisa la kusema wala la kufanya. Je, jambo hili ni rahisi kulishinda? (Hapana.) Angalau kwa muda mfupi, si rahisi kwako kushinda dosari hii kwa sababu ni sehemu ya hali zako za asili. Ikiwa baada ya miezi kadhaa ya kufanya mazoezi bado una wasiwasi, wasiwasi huo utageuka kuwa shinikizo, ambalo litakuathiri vibaya kwa kukufanya uogope kuzungumza, kukutana na watu, kuhudhuria mikutano, au kutoa mahubiri, na hofu hizi zitakulemea. Kwa hivyo unapaswa kufanya nini? Unaweza kutafakari suala hili na kulizungumzia na wengine; uone wengine huwa na fikira gani wanapokumbana na tatizo hili, na jinsi wanavyolitatua, na kisha unapaswa pia kutenda kwa njia hii wewe mwenyewe. Tuseme kwamba wakati wa mkutano wa leo uko katika hali nzuri kiasi; uko katika hali ya uchangamfu, na zaidi ya hayo, unaguswa pia na kusoma maneno ya Mungu, na unahisi hamu ya pekee ya kujieleza. Inatokea tu kwamba ni mkutano wa kikundi kidogo wenye watu wachache tu, kwa hivyo unajaribu kushiriki maneno machache na unahisi vizuri kiasi kuyahusu, na huna wasiwasi. Katika hali hii, wakati huna shinikizo lolote na hujajitayarisha hata kidogo, unajieleza kwa uhuru vizuri sana, na kila mtu anaguswa na anajengwa sana na hilo. Je, haya si maendeleo? Anza tu kufanya mazoezi ya kuzungumza na kufanya ushirika katika mikutano ya vikundi vidogo, ambapo kuna watu wachache, na hatua kwa hatua utaweza kuzungumza kwa kawaida, na wasiwasi wako utapungua kidogo kidogo. Kutenda kwa namna hii kutafikia matokeo bora kabisa. Kwanza, chagua mkutano wa kikundi kidogo ambapo kuna watu wachache au mazingira yasiyo rasmi ili kufanya mazoezi ya hili, ukizungumza na ukifanya ushirika kwa namna ya papo hapo, kana kwamba unapiga gumzo, ili kushinda dosari hii yako. Wakati mwingine, baada ya kuzungumza kwa dakika moja unaweza kuhisi wasiwasi kidogo, unaweza kuhisi kupoteza ujasiri kadiri unavyozidi kuzungumza, na unaweza kuwa na machache ya kusema kadiri unavyoendelea; katika hali kama hizo, usizungumze tena—malizia haraka na unyamaze. Wakati mwingine, baada ya kuzungumza kwa muda, kila mtu anaweza kuwa tayari kusikiliza na kuhisi amefunguka sana; katika hali kama hizo, wasiwasi na shinikizo lako vitaondoka bila wewe kutambua. Ni chini ya hali kama hizo tu ndipo dosari hii yako inaweza kuboreshwa hatua kwa hatua—lakini haitashindwa. Ikiwa unahisi kwamba baada ya kufanya mazoezi kwa mwezi mmoja, hali yako haijaimarika sana, na hata shinikizo la aina fulani linatokea moyoni mwako, likikufanya uwe na wasiwasi zaidi na zaidi, jambo ambalo linaathiri kazi yako ya kawaida, maisha yako, na utendaji wako wa wajibu, basi huhitaji kuendelea kufanya mazoezi. Inatosha ikiwa unaweza kufanya wajibu wako kwa njia ya kawaida. Lenga tu kufanya wajibu wako vizuri—hili ndilo jambo sahihi. Weka kasoro hiyo, dosari hiyo, moyoni mwako, umwombe Mungu kimyakimya, na kisha utafute nyakati zinazofaa za za kufanya mazoezi ya kuzungumza na kutangamana na watu, ukieleza kile unachotaka kusema kwa kutamka kila neno waziwazi, ukizungumza kwa mpangilio na uwazi. Kwa namna hii, kasoro yako, dosari hii, itaboreka hatua kwa hatua. Inawezekana kwamba baada ya mwaka mmoja au miwili, unaweza kuwa mkomavu kadiri umri unavyoongezeka na kuwazoea zaidi watu walio karibu na wewe, na macho yao, maoni yao, na hali inayojitokeza wakati kila mtu yuko pamoja huenda visiwe tena chanzo cha shinikizo, kifungo, wala kizuizi kwako—kisha dosari yako inaweza kuondolewa na kutatuliwa unapotangamana na watu hawa. Huyu ndiye mtu aliye na dosari hii iliyo kali kabisa; anaweza tu kuiondoa kupitia kufinyangwa na kuzoezwa kwa muda mrefu katika mazingira kama hayo. Bila shaka, pia kuna watu ambao hatua kwa hatua hutatua dosari hii katika kipindi kifupi cha miezi mitatu hadi mitano. Hawana wasiwasi wanapotangamana na wanapozungumza na wengine katika hali za kawaida, isipokuwa wanapokabiliwa na matukio makubwa. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kushinda kasoro hii, dosari hii, kwa muda mfupi, basi fanya hivyo. Ikiwa ni vigumu kuishinda, basi usijisumbue nayo, usipambane nayo, na usijitie changamoto. Bila shaka, ikiwa huwezi kuishinda, hupaswi kuhisi hasi. Hata ikiwa huwezi kamwe kuishinda katika maisha yako yote, Mungu hatakuhukumu, kwa maana hii si tabia yako potovu. Hofu yako ya kuzungumza mbele ya watu, wasiwasi wako, na woga wako—madhihirisho haya hayaonyeshi tabia yako potovu; yawe ya asili au yamesababishwa na mazingira baadaye maishani, kwa kiwango cha juu kabisa, ni kasoro, dosari ya ubinadamu wako. Ikiwa huwezi kuibadilisha kwa muda mrefu, au hata katika maisha yako yote, usijishughulishe nayo kupita kiasi, usiiruhusu ikubane, wala hupaswi kuwa hasi kwa sababu yake, kwa maana hii si tabia yako potovu; hakuna manufaa yoyote kujaribu kuibadilisha wala kupambana nayo. Ikiwa huwezi kuibadilisha, basi ikubali, iruhusu iwepo, na uichukulie kwa usahihi, kwa sababu unaweza kuishi pamoja na kasoro hii, dosari hii—kuwa nayo hakuathiri kumfuata kwako Mungu na kufanya wajibu wako. Mradi tu unaweza kuukubali ukweli na kufanya wajibu wako kwa kadiri ya uwezo wako, bado unaweza kuokolewa; hakuathiri kukubali kwako ukweli na hakuathiri kufikia kwako wokovu. Kwa hivyo, hupaswi kubanwa mara nyingi na kasoro au dosari fulani katika ubinadamu wako, wala hupaswi kuwa hasi na kuvunjika moyo mara nyingi, au hata kuacha wajibu wako na kuacha kuufuatilia ukweli, ukikosa fursa ya kuokolewa, kwa sababu hiyo hiyo. Hilo halifai kabisa; hivyo ndivyo mtu mpumbavu, mjinga angefanya.

Baadhi ya watu wanaweza tu kufikia noti za kati wanapoimba na hawawezi kufikia noti za juu haijalishi wanajizoeza kiasi gani. Kwa hivyo, jambo gani linaweza kufanywa kuhusu hili? Imba tu noti zilizo katika viwango vya kati na vya chini; ni sawa kuimba tu noti hizo vizuri. Ukitaka kila mara kujitia changamoto, ukisema, "Mimi ni hodari kwa kuimba noti za kati. Ninataka kujitia changamoto kufikia noti za juu," basi hata ukifanikiwa katika changamoto hii, haitakuwa na maana, na haitamaanisha kwamba umeupata ukweli. Kwa kiwango cha juu kabisa, itamaanisha tu kwamba umepata ustadi wa ziada, unaweza kufanya wajibu wa ziada, unaweza kuimba nyimbo chache zaidi, na unaweza kujitokeza mbele ya watu zaidi kidogo. Lakini jambo hilo lina maana gani? Je, kujitokeza mbele ya watu zaidi kunamaanisha kwamba unatenda ukweli zaidi? Je, kuna uhusiano kati ya mambo haya mawili? (Hapana.) Ikiwa unaweza kuimba noti za kati, basi ziimbe vizuri. Ikiwa huwezi kuimba noti za juu vizuri, lakini unasisitiza kujilazimisha kuziimba, na unaishia kutoweza kuziimba kwa usahihi, na pia unajifanya mgonjwa kwa uchovu, Mungu hatakumbuka jambo hili. Haijalishi ikiwa unaweza kuimba noti za juu au noti za kati, mradi tu unaweza kuimba vizuri, na kujitoa na kutoa yote uwezayo katika wajibu wako, bila kufanya mambo kwa kijuujuu tu, au kuwa mjanja na kulegeza kamba, au kutenda maovu kwa uzembe, au kusema maneno matupu ya kujidai, na unajitahidi—iwe ni kwa upande wa mbinu, hisia, ubora wa sauti, na noti—kuimba kwa namna inayofikia kiwango kinachostahili, iliyo nzuri inayogusa moyo, na kuimba kwa namna inayoweza kuwagusa watu, kutuliza mioyo ya watu mbele za Mungu, na kuwajenga watu wanapokusikiliza, basi huku ni kufanya wajibu wako kwa namna inayofikia kiwango kinachostahili. Ikiwa unataka daima kujitia changamoto ya kuvuka mipaka yako, na daima unataka kufanya mafanikio mapya ya kibinafsi na kujipita mwenyewe, huku ni kufunua tabia yako potovu ya kishetani, na si kufanya wajibu wako. Baada ya kufanya kazi yako mwenyewe ipasavyo, na kufanya kile unachoweza kufikia ipasavyo, ni sawa kwako kujifunza jambo la manufaa kwa wajibu wako katika wakati wako wa ziada, lakini hili si jambo ambalo Mungu anataka. Tuseme kwamba unaimba noti za kati vizuri, na katika wakati wako wa ziada unafanya mazoezi ya kuimba noti za juu. Baada ya kipindi cha muda, unapata mafanikio mapya, na baada ya miaka miwili hadi mitatu ya kufanya kazi kwa bidii unaweza pia kuimba noti za juu vizuri. Unaweza kuimba noti za kati na za juu, na kutimiza majukumu haya yote mawili; unaweza kufanya majukumu haya yote mawili kulingana na kanuni za ukweli, na kuimba kwa moyo wako wote, bila kufanya mambo kwa kijuujuu tu, kuwa mjanja au kulegeza kamba, au kusema maneno matupu ya kujidai. Hili ni bora hata zaidi, ni tendo jema, na Mungu atalikumbuka. Lakini tuseme kwamba huwezi kufikia jambo hili, na bado unafikiri daima, "Mungu ana matarajio makubwa kwangu, je, si kwamba ninakuwa mjanja na ninalegeza kamba ikiwa ninaimba tu noti za kati? Mungu haridhiki!" Hilo ni wazo lako mwenyewe la kufikirika. Unamkisia Mungu, na unajihusisha katika utendaji wa "kumpima mtu kabaila kwa mawazo finyu ya mtu duni." Mungu hajaweka matakwa kama hayo kwako. Kile ambacho Mungu anataka kutoka kwako ni wewe kufanya vizuri yale unayopaswa kufanya ndani ya mipaka ya ubora wako wa tabia na uwezo wako wa asili, na ikiwa unayafanya vizuri kulingana na kanuni zinazohitajika na Mungu, basi Mungu atakuwa tayari amekupa alama kamili. Lakini ikiwa hujaribu kufanya vizuri yale unayoweza kufikia, na huyafanyi kulingana na kanuni, na daima unakuwa mjanja na unalegeza kamba na daima unataka kusema maneno matupu ya kujidai, na hufanyi mazoezi ya mbinu mbalimbali za uimbaji, lakini bado unataka kujitia changamoto ya kuvuka mipaka yako, basi kutenda kwako hivi ni kukosa busara, ni udhihirisho wa kiburi na ujinga, na Mungu hatapendezwa. Hatasema kamwe, "Mtu huyu anaweza kuimba noti za kati na anajaribu kuimba noti za juu pia. Ingawa hawezi kuimba noti za juu vizuri, hilo linaonyesha kwamba anajituma sana, na hiyo inatosha." Mungu hatakutazama kwa namna hiyo, kwa hivyo usijione kuwa unafanya vizuri. Mungu hutazama tu iwapo unajiendesha kwa namna inayofaa nafasi yako, na ikiwa wewe ni mtu anayefanya wajibu wa kiumbe aliyeumbwa vizuri. Hutazama iwapo, katika utekelezaji wako wa wajibu wako, unaweka moyo wako wote na nguvu zako zote ndani yake chini ya hali za asili ambazo Mungu amekupa, na iwapo unatenda kulingana na kanuni za ukweli na kufikia matokeo ambayo Mungu anataka. Ikiwa unaweza kutimiza mambo haya yote, Mungu anakupa alama kamili. Tuseme kwamba hufanyi mambo kulingana na matakwa ya Mungu, na hata kama unajitahidi na unaweka bidii, yote unayofanya ni kujionyesha na kujigamba tu, na hutendi kulingana na kanuni za ukweli au huutoi moyo wako wote na nguvu zako zote ili kumridhisha Mungu katika utekelezaji wa wajibu wako. Katika hali hiyo, madhihirisho na mienendo yako vinachukiza kwa Mungu. Kwa nini Mungu anavichukia? Mungu anasema kwamba hulengi kazi ipasayo, hujaweka moyo wako wote, nguvu yako yote, au akili yako yote katika utekelezaji wa wajibu wako, na hutembei katika njia sahihi. Ubora wa tabia, karama, na talanta ambazo Mungu amekupa tayari vinatosha—ni kwamba tu hutosheki, hujitoi kwa wajibu wako, hujui nafasi yako kamwe, daima unataka kusema maneno matupu ya kujidai na kujionyesha, na hatimaye unaharibu wajibu wako. Hujatumia ubora wa tabia, karama, na talanta zilizotolewa kwako na Mungu, hujajitahidi kikamilifu, na hujafikia matokeo yoyote. Ingawa unaweza kuwa na shughuli nyingi, Mungu anasema kwamba wewe ni kama mchekeshaji, si mtu anayejua nafasi yake na anayelenga kazi zake zinazofaa. Mungu hapendi watu kama hao. Kwa hivyo, haijalishi mipango na malengo yako ni yapi, ikiwa hatimaye huji kufanya wajibu wako kulingana na kanuni zinazohitajika na Mungu kwa moyo wako wote, akili yako yote, na kwa nguvu zako zote, kwa msingi wa ubora wa tabia, karama, talanta, uwezo, na hali zingine za asili ambazo Mungu amekupa, basi Mungu hatakumbuka yale uliyofanya, na hutakuwa ukifanya wajibu wako, bali, utakuwa ukitenda maovu.

Je, umeelewa kanuni ya utendaji ya jinsi ya kushughulikia kwa usahihi hali zako za asili—yaani, hali zako mwenyewe, sifa zako mwenyewe nzuri, na mapungufu yako mwenyewe? (Ndiyo.) Hatua ya kwanza ni ipi? Kwanza, tumia kikamilifu karama, uwezo, na ubora wa asili na uliopo ambao Mungu amekupa, pamoja na ustadi wa kiufundi au wa kitaaluma ambao unaweza kuupata na kuufikia, na usijizuie. Ikiwa umekuja kumridhisha Mungu katika mambo haya yote na unahisi kwamba bado unaweza kufikia viwango vya juu zaidi, basi angalia ni ustadi upi wa kiufundi au wa kitaaluma unaoweza kuboresha au kupata mafanikio mapya katika kuumudu, ndani ya mipaka ya kile ambacho ubora wako wa tabia unaweza kufikia. Unaweza kuendelea kujifunza na kuboresha kulingana na kile unachoweza kupata kwa ubora wako mwenyewe wa tabia. Kwa hivyo, mtu anapaswa kutendaje kuachilia dhana na mawazo yake ya kufikirika kuhusu kazi ya Mungu? Kwanza kabisa, lazima uelewe hali zako za asili ni zipi, kile ambacho Mungu amekupa ni nini, jinsi unavyopaswa kutumia mambo haya, na jinsi ya kudhihirisha uwezo wa mambo hayo kikamilifu, na kuyatumia kikamilifu, na jinsi ya kuyafanya kuwa hali za msingi—badala ya vizuizi—kwa wewe kuja kufanya wajibu wako kwa kujitoa. Kwanza, jielewe mwenyewe. Elewa sifa zako mwenyewe nzuri, na uzidhihirishe. Elewa dosari na kasoro zako mwenyewe na ikiwa unaweza kuzibadilisha ndani ya kipindi kifupi, fanya hivyo; ikiwa si rahisi kuzibadilisha, usiziache ziwe vikwazo wala vizuizi katika mchakato wa kufanya wajibu wako, usibanwe wala usishawishiwe nayo, na usifungwe mikono na miguu navyo. Tuseme, kwa mfano, kwamba ulizaliwa na afya mbaya na mwili dhaifu, na daima unataka kushinda hili, na unataka kuweza kula, kunywa, na kukesha usiku kama mtu wa kawaida, lakini Mungu hajakupa uwezo huo. Basi unapaswa kuishi kila siku kulingana na hali zako mwenyewe, na kufanya mambo kulingana na kanuni zinazohitajika na Mungu. Usijitie changamoto, na usiruhusu dosari na kasoro zako mwenyewe ziwe vikwazo na vizuizi kwenye njia yako ya kumfuata Mungu, kufanya wajibu wako, na kuufuatilia ukweli; usiziruhusu ziwe kichocheo cha wewe kuwa hasi, na hata zaidi, usiache kuufuatilia ukweli wala kufanya wajibu wako, au kuhisi wivu na chuki kwa wengine kwa sababu tu una kasoro, dosari, na mapungufu fulani—hupaswi kufanya lolote kati ya haya. Lazima uzichukulie kasoro na dosari zako mwenyewe kwa usahihi; ikiwa huwezi kuzibadilisha, unapaswa kuziruhusu ziwepo, na kisha uutafute ukweli ili kuelewa nia za Mungu, na uweze kuzishughulikia kwa usahihi, na usibanwe nazo. Kwa nini unapaswa kufanya hivyo? Hii ndiyo busara ambayo ubinadamu wa kawaida unapaswa kuwa nayo. Ikiwa busara ya ubinadamu wako ni ya kawaida, unapaswa kukabiliana na kasoro na dosari zako kwa namna sahihi; unapaswa kuzikiri na kuzikubali. Hili lina manufaa kwako. Kuzikubali hakumaanishi kubanwa nazo, wala hakumaanishi kuwa hasi mara nyingi kwa sababu ya dosari na kasoro hizo, bali kunamaanisha kutobanwa nazo, kutambua kwamba wewe ni mshiriki wa kawaida tu wa binadamu wapotovu, ukiwa na dosari na kasoro zako mwenyewe, bila chochote cha kujisifia, kwamba ni Mungu anayewainua watu kufanya wajibu wao, na kwamba Mungu anakusudia kufanya neno na uzima Wake viingie ndani yao, akiwawezesha kufikia wokovu na kuepuka ushawishi wa Shetani—kwamba huku ndiko Mungu kuwainua watu kikamilifu. Kila mtu ana dosari na kasoro. Unapaswa kuziruhusu dosari na kasoro zako ziwepo pamoja na wewe; usiziepuke wala uzifiche, na usihisi kukandamizwa ndani yako mara nyingi au hata kujihisi duni daima kwa sababu ya dosari na kasoro hizo. Wewe si duni; ikiwa unaweza kufanya wajibu wako kwa moyo wako wote, nguvu zako zote, na akili yako yote, kwa kadiri ya uwezo wako, na una moyo wa dhati, basi wewe ni wa thamani kama dhahabu mbele za Mungu. Ikiwa huwezi kulipa gharama na unakosa uaminifu katika kufanya wajibu wako, basi hata ikiwa hali zako za asili ni bora kuliko zile za mtu wa kawaida, wewe si wa thamani mbele za Mungu, hata huna thamani ya chembe ya mchanga. Je, umeelewa? (Ndiyo.) Iwe ni sura yako ya asili, ubora wako wa tabia na talanta zako za asili, au kasoro na mapungufu ya kipengele fulani cha ubinadamu wako, usiviruhusu vikubane, usiviiache vizuie utekelezaji wako wa wajibu wako na viathiri uaminifu na utii wako kwa Mungu, usivirusuhu viathiri ufuatiliaji wako wa ukweli, na bila shaka, hata zaidi usiviruhusu viathiri jambo kuu la wokovu wako. Unapaswa kushughulikia kasoro na mapungufu yako kwa usahihi na kuyaruhusu yawepo pamoja na wewe, ikimaanisha kwamba hupaswi tena kujaribu kuyabadilisha, kwa sababu hayataathiri hata kidogo utendaji wako wa wajibu wako kwa moyo wako wote na nguvu zako zote, na bila shaka, pia hayataathiri utekelezaji wako wa wajibu wako kulingana na kanuni, na hata kidogo hayataathiri ufuatiliaji wako wa maisha yote wa ukweli katika imani yako katika Mungu, wala hayataathiri jinsi unavyotazama watu na mambo, na unavyojiendesha na unavyotenda, kulingana na kanuni za ukweli katika mchakato wa kuufuatilia ukweli. Bila shaka, hupaswi daima kujiwekea matakwa, ukifikiri, "Usionyeshe dosari hii, usiwaruhusu wengine waone kasoro zangu, na usiwaruhusu wengine wanidharau!" Ukifanya hivyo, basi utaishi maisha ya kuchosha sana. Ukiruhusu kasoro na dosari zako ziwepo pamoja na wewe, basi ziruhusu ziwepo, na hata ikiwa wengine wanaona kasoro zako, hili linaweza hata kuwa na manufaa kwako, na pia ulinzi, ambao utakuzuia kuwa mwenye kiburi na majivuno. Bila shaka, kwa watu wengi inahitaji ujasiri kwao kufunua kasoro na dosari zao wenyewe. Baadhi ya watu husema, "Kila mtu hufunua mambo yao wenyewe wanayofanya vizuri na sifa zao wenyewe nzuri. Ni nani angefunua kwa makusudi udhaifu na kasoro zake mwenyewe?" Si kwamba unazifunua kwa makusudi, bali kwamba unaziruhusu zifunuliwe. Kwa mfano, ikiwa wewe ni mwoga na mara nyingi unahisi wasiwasi kuzungumza wakati kuna watu wengi karibu, unaweza kuchukua hatua ya kwanza kuwaambia wengine, "Mimi hupata wasiwasi kwa urahisi ninapozungumza; ninaomba tu kwamba kila mtu anielewe na asinitafutie makosa." Unachukua hatua ya kwanza kufunua kasoro na dosari zako kwa kila mtu, ili kwamba waweze kuwa wenye kuelewa na kukuvumilia, na ili kwamba kila mtu apate kukujua. Kadiri kila mtu anavyozidi kukujua, ndivyo moyo wako utakavyokuwa na utulivu zaidi, na ndivyo utakavyozidi kutobanwa na kasoro na dosari zako. Hili kwa kweli litakuwa na manufaa na msaada kwako. Daima kuficha kasoro na dosari zako kunathibitisha kwamba hutaki kuishi pamoja nazo. Ukizuruhusu ziwepo pamoja na wewe, lazima uzifunue; usihisi aibu wala kuvunjika moyo, na usijihisi duni kuliko wengine, wala usifikiri kwamba hufai na huna tumaini la kuokolewa. Mradi tu unaweza kuufuatilia ukweli, na unaweza kufanya wajibu wako kwa moyo wako wote, nguvu zako zote, na akili yako yote kulingana na kanuni, na moyo wako ni wa dhati, na humfanyii Mungu mambo kwa kijuujuu tu, basi una tumaini la kuokolewa. Ikiwa mtu anasema, "Tazama jinsi ulivyo asiyefaa na mwoga. Unapata wasiwasi mwingi kwa kuzungumza tu maneno machache, na uso wako wote unakuwa mwekundu," basi unapaswa kusema, "Nina ubora duni wa tabia na mimi si hodari wa kuzungumza. Mkinitia moyo, basi nitakuwa na ujasiri wa kufanya mazoezi ya kuzungumza." Usifikiri kwamba hufai, au kwamba wewe ni mtu wa aibu. Kwa kuwa unajua kwamba hizi ni kasoro na matatizo ya ubinadamu wako, unapaswa kukabiliana nazo na kuzikubali. Usiathiriwe nazo kwa namna yoyote. Kuhusu ni lini kasoro na dosari hizi zitabadilika, usijisumbue na hilo. Lenga tu kuishi na kufanya wajibu wako kwa kawaida kwa namna hii. Lazima ukumbuke tu: Kasoro na dosari hizi za ubinadamu si mambo hasi wala tabia potovu, na mradi tu si tabia potovu, hazitaathiri utekelezaji wako wa wajibu wako wala ufuatiliaji wako wa ukweli, na hata kidogo hazitaathiri kufikia kwako wokovu; bila shaka, jambo muhimu hata zaidi ni kwamba hazitaathiri jinsi Mungu anavyokutazama. Je, hilo halikupi utulivu moyoni mwako? (Ndiyo.) Ikiwa bado una wasiwasi kuhusu kudharauliwa na watu wengine, hilo ni tatizo la tabia yako ya kiburi, na lazima utatue tabia hii ya kiburi. Hii ndiyo njia ya utendaji ya kushughulikia kasoro na dosari zako mwenyewe kwa usahihi. Je, kutenda kwa namna hii hakufanyi iwe rahisi kwako kuachilia mambo haya na kutobanwa nayo tena? (Ndiyo.)

Je, utekelezaji wa kawaida wa wajibu wa mtu na kasoro na dosari za ubinadamu wake vitaathiriana? (Kupitia ushirika wa Mungu, sasa ninaelewa kwamba kasoro na dosari za ubinadamu si tabia potovu, na kwamba hazitaathiri utekelezaji wa kawaida wa watu wa wajibu wao. Mradi tu watu wanafanya wajibu wao kulingana na kanuni za ukweli, watapata matokeo mazuri. Kuhusu kasoro na mapungufu ya ubinadamu, ikiwa tunaweza kuyashinda, basi tunaweza kufanya hivyo. Ikiwa hatuwezi kuyashinda katika kipindi kifupi, basi tunapaswa kuyaruhusu yawepo na kuyashughulikia kwa usahihi.) Ikiwa una kiwango duni cha elimu, lakini unahitaji kutumia maarifa ya kitaaluma katika wajibu wako, je, jambo hili si aina ya upungufu? (Ndiyo.) Basi ugumu huu unaweza kutatuliwaje? (Ninaweza kufanya wajibu unaonifaa badala yake kulingana na kiwango changu cha elimu. Au, ikiwa wajibu huu unanifaa, lakini unahitaji kiasi fulani cha maarifa ya kitaaluma, ninaweza kuwatafuta baadhi ya ndugu na dada walioelimika ili kushirikiana na mimi—tunaweza kutumia ubora wa kila mmoja wetu kufidia udhaifu wetu, na kutimiza wajibu huu pamoja.) Je, ukweli unaweza kufidia kiwango duni cha elimu? (Unaweza, kwa sababu wakati mtu ana ukweli, anaweza kung'amua mambo.) Elimu ni jambo lililo katika kiwango cha maarifa. Haijalishi una maarifa kiasi gani, ikiwa huelewi ukweli, basi unapozungumza au unapoyaandika makala, utaweza tu kutumia sarufi sahihi, hutaweza kueleza waziwazi wala kutatua masuala yanayohusiana na ukweli. Kwa hivyo, elimu si muhimu; ukweli ni muhimu zaidi kuliko elimu. Bila shaka, ikiwa huna msingi wa elimu, na ikiwa wajibu unaofanya unahusisha maarifa ya kitaaluma, hutakuwa na na ustadi wa kuufanya. Hata hivyo, ikiwa unaelewa ukweli, unaweza kuwaongoza watu wengine—unaweza kufanya uhakiki kwa kuzingatia kanuni za ukweli. Ikiwa una kiwango duni cha elimu na unakosa uwezo wa kujieleza, na unataka kuhubiri mahubiri au kufanya ushirika kuhusu ukweli, unaweza kumtafuta mtu aliyeelimika akusaidie kupanga rasimu zako. Kisha itakuwa rahisi kwako kufikia matokeo unapofanya ushirika au unapohubiri. Hata hivyo, angalau, lazima uelewe ukweli. Ikiwa huelewi ukweli, na pia huna elimu, hutaweza kufanya wajibu unaohusisha maarifa ya kitaaluma, na kwa hivyo unapaswa kufanya wajibu unaofaa kiwango chako cha elimu. Je, jambo hili halitatui tatizo? (Linatatua.) Kwa hivyo, kuufuatilia ukweli ndilo jambo muhimu kabisa, haijalishi unalitazama kutoka kwa mtazamo upi. Unaweza kuepuka kasoro na mapungufu ya ubinadamu, lakini huwezi kamwe kukwepa njia ya kuufuatilia ukweli. Bila kujali jinsi ubinadamu wako unavyoweza kuwa mkamilifu au wenye heshima, au kama unaweza kuwa na dosari na kasoro chache, na una ubora mwingi zaidi, kuliko watu wengine, hili halimaanishi kwamba unaelewa ukweli, wala haliwezi kusimama katika nafasi ya ufuatiliaji wako wa ukweli. Kinyume chake, ikiwa unaufuatilia ukweli, unaelewa ukweli mwingi, na unakuwa na uelewa wa kina na wa vitendo wa kutosha kuuhusu, hili litafidia kasoro na matatizo mengi katika ubinadamu wako. Kwa mfano, tuseme kwamba wewe ni mwoga na mtu asiyejichanganya na watu, unagugumiza, na huna elimu nzuri sana—yaani, una kasoro na mapungufu mengi—lakini una uzoefu wa vitendo, na ingawa unagugumiza unapozungumza, unaweza kushiriki ukweli waziwazi, na ushirika huu unamjenga kila mtu anapousikia, unatatua matatizo, unawawezesha watu kuibuka kutoka katika hali hasi, na unaondoa malalamiko yao na dhana zao potofu kumhusu Mungu. Unaona, ingawa unagugumiza maneno yako, yanaweza kutatua matatizo—jinsi maneno haya yalivyo muhimu! Watu wa kawaida wanapoyasikia, wanasema kwamba wewe ni mtu asiye na elimu, na hufuati sheria za sarufi unapozungumza, na wakati mwingine maneno unayotumia hayafai kabisa pia. Inaweza kuwa kwamba unatumia lugha ya eneo, au lugha ya kila siku, na kwamba maneno yako yanakosa hadhi na mtindo wa yale ya watu walioelimika sana ambao huzungumza kwa ufasaha mkubwa. Hata hivyo, ushirika wako una uhalisi wa ukweli, unaweza kutatua matatizo ya watu, na baada ya watu kuusikia, mawingu yote meusi yanayowazunguka yanatoweka, na matatizo yao yote yanatatuliwa. Unaona, je, kuelewa ukweli si muhimu? (Ni muhimu.) Tuseme kwamba huelewi ukweli, na ingawa una maarifa fulani ya kitaaluma na unazungumza kwa ufasaha, kila mtu anapokusikia ukizungumza, anafikiri, "Maneno yako ni mafundisho tu, hakuna hata chembe ya uhalisi wa ukweli ndani yake, na hayawezi kutatua matatizo halisi hata kidogo, kwa hivyo je, maneno yako haya yote si matupu? Huelewi ukweli. Je, wewe si Mfarisayo tu?" Ingawa ulizungumza mafundisho mengi, matatizo yanabaki bila kutatuliwa, na unafikiri moyoni mwako, "Nilikuwa nikizungumza kwa dhati na kwa bidii sana. Kwa nini hamjaelewa kile nilichosema?" Ulizungumza mafundisho mengi sana, lakini wale waliokuwa hasi wanabaki hasi, na wale waliokuwa na dhana potofu kumhusu Mungu bado wana dhana hizo potofu, na hakuna hata moja ya matatizo yaliyopo katika utekelezaji wao wa wajibu wao ambayo yametatuliwa—hili linamaanisha kwamba maneno uliyozungumza yalikuwa upuuzi tu. Haijalishi kuna kasoro na dosari ngapi katika ubinadamu wako, ikiwa maneno unayozungumza yana uhalisi wa ukweli, basi ushirika wako unaweza kutatua matatizo; ikiwa maneno unayozungumza ni mafundisho, na hayana hata chembe ya maarifa ya vitendo, basi haijalishi unazungumza kiasi gani, hutaweza kutatua matatizo halisi ya watu. Haijalishi watu wanakuonaje, mradi tu mambo unayosema hayalingani na ukweli, na hayawezi kushughulikia hali za watu, wala kutatua matatizo ya watu, basi watu hawatataka kuyasikiliza. Kwa hivyo, ni kipi muhimu zaidi: ukweli au hali za watu wenyewe? (Ukweli ni muhimu zaidi.) Kuufuatilia ukweli na kuelewa ukweli ndiyo mambo muhimu zaidi. Kwa hivyo, haijalishi una kasoro gani katika suala la ubinadamu wako au hali zako za asili, hupaswi kubanwa nazo. Badala yake, unapaswa kuufuatilia ukweli, na kufidia kasoro zako mbalimbali kwa kuelewa ukweli, na ukigundua mapungufu fulani ndani yako, unapaswa kuharakisha kuyarekebisha. Baadhi ya watu hawalengi kuufuatilia ukweli, na badala yake daima wanalenga kutatua matatizo, dosari, na kasoro katika ubinadamu wao, na kurekebisha matatizo ya ubinadamu wao, na inatokea kwamba wanajitahidi kwa miaka kadhaa bila kupata matokeo wazi, na kwa sababu hiyo wanahisi kukatishwa tamaa na wao wenyewe, na wanafikiri kwamba ubinadamu wao ni duni sana na kwamba hawawezi kukombolewa. Je, jambo hili si la kipumbavu sana?

3. Ili Kupata Ukweli na Uzima Lazima Mtu Afuatilie Ukweli na Atatue Tabia Zake Potovu

Baadhi ya watu huonekana wapole, wavumilivu, na wastahimilivu; huzungumza kwa ustaarabu na hutekeleza kazi kwa haraka na kwa nguvu kama radi na kwa mwonekano wenye mamlaka. Ubinadamu wao unaonekana mkamilifu kabisa, na wana mwenendo wa kawaida wa kiongozi. Hata hivyo, hawaelewi ukweli wowote ule, wanajaribu kutumia mafundisho kutatua tatizo la kila aina, na hawawezi kufanya kazi yoyote ya maana wala kutekeleza mipango ya kazi. Je, hawa si watu wasio na manufaa yoyote? Hawa ndio Mafarisayo wa kawaida. Kwa nje, Mafarisayo wanavalia vizuri sana, wana hadhi, na ni watulivu; wameelimika, wanafahamu adabu vizuri, ni wenye heshima, wenye upendo, ni wavumilivu, na wastahimilivu. Maneno, matendo, na mienendo yao ni sahihi kupita kiasi, na wanazungumza kwa upole wa kipekee, na wanatenda kwa kiasi na unyenyekevu wa kipekee. Huwezi kuona dosari, nyufa, au kasoro zozote ndani yao. Kwa kuangalia ubinadamu wao, wanaonekana kuwa wa kutegemewa, wenye umaizi, wastaarabu, na wenye madaha sana, kama tu waungwana walioelimika na wa kifahari wanaozungumziwa na watu wa China. Ubinadamu wao unaonekana mkamilifu, na kwa nje, hakuna kosa linaloweza kupatikana kwao, lakini je, wanaelewa nia za Mungu? Je, wanaelewa kanuni za kufanya mambo ya kila aina? Watu hawa wanaweza kuzungumza kwa saa nyingi katika kila mkutano, na wale wasioelewa ukweli husujudu kwa kuvutiwa, wakifikiri kwamba wanazungumza kwa ufasaha sana, na wanajieleza kwa namna iliyo wazi sana na yenye mantiki. Lakini wale wanaoelewa ukweli wanajua baada ya kuwasikiliza watu hawa kwamba yale wanayozungumza yote ni mafundisho, na kwamba hayatatui matatizo halisi ya watu kwa kulenga shida zao. Watu hawa hupuuza matatizo halisi ya watu ni yapi hasa, na wanajua tu jinsi ya kuhubiri mafundisho matupu na kuzungumza bila kikomo kuhusu nadharia za juu na tupu. Baada ya kuzungumza, hata wanajisikia fahari kabisa, wakifikiri wanaelewa ukweli na wana uhalisi wa ukweli. Kwa kweli, kile wanachotafuta ni kuficha tu mwonekano wa nje wa ubinadamu wao ili kuufanya uonekane mkamilifu na wenye madaha, na kuufanya uonekane wa juu na wa kifahari. Hata hivyo, kiini chao na tabia zao potovu zinazompinga Mungu hazijabadilika hata kidogo. Dhana zao kumhusu Mungu, uasi wao dhidi Yake, kutoelewa kwao, kujihami kwao, na mashaka yao kumhusu Mungu, na hasa matakwa yao yasiyo na busara na matamanio ya kupita kiasi kuelekea kwa Mungu vinajaza akili zao zote. Hawafuatilii ukweli hata kidogo, wala hawakubali ukweli hata kidogo. Kwa hivyo, ili kuelezea ubinadamu wao kuwa "mkamilifu" ni kutumia "mkamilifu" kwa maana ya kudharau, kwa sababu hakuna ubinadamu ulio mkamilifu; "ukamilifu" wao ni mwonekano wa kujifanya na kujificha tu. Ubinadamu usio na kasoro haupo; ni mwonekano wa kujifanya, usiwaamini. Kadiri mtu anavyoonekana mkamilifu zaidi kwa nje, ndivyo l azima ujilinde dhidi yake, umtazame, na umtambue. Unamtambuaje? Tangamana na yeye zaidi, zungumza na yeye zaidi, na uone ikiwa anajielewa. Tuseme kwamba anasema, "Mimi ni ibilisi, mimi ni Shetani, ninampinga Mungu, mimi ni mpotovu! Mimi ni mwenye dhambi, mwenye dhambi mkuu, Mungu hapendezwi na mimi, Mungu ananichukia!" au, "Mimi ni kipofu na mpumbavu, maskini na mwenye kusikitisha! Mimi ni mchafu, mimi ni najisi!" Je, kuna ukweli wowote halisi katika maneno haya? Je, kuna uelewa wowote wa maana? (Hapana.) Hana uelewa wowote ule wa tabia zake mwenyewe potovu; hata hakiri ukweli kwamba ana tabia potovu. Anajifunza tu kuzungumza maneno fulani matupu na nadharia fulani. Maneno haya matupu na nadharia hizi si uelewa unaotokana na kile ambacho amehisi au amepitia ndani kabisa ya moyo wake; ni maneno tu yanayosikika vizuri, yote ni mwonekano wa kujifanya anaouonyesha. Kisha ukimwomba azungumze kuhusu uzoefu wake mwenyewe, jinsi alivyokuja kuelewa tabia zake mwenyewe potovu, na ni upogoaji gani ambao amepitia na ni maneno yapi ya Mungu ambayo amesoma baadaye ili kutatua tabia zake potovu, anatenda kana kwamba hakukusikia, na tena anazungumza lundo la maneno yasiyo na maana: "Ubora wangu wa tabia ni duni, nilizaliwa mwenye dhambi, mimi ni mtu duni katika lundo la kinyesi, sistahili wokovu wa Mungu! Nina tabia potovu, na siwezi kutoa ushuhuda kwa Mungu popote nilipo; ninapenda tu kuwa na hadhi." Ukimwuliza jinsi ambavyo amejaribu kutatua hili, bado atakupa jibu lisilohusiana kama itikio: "Watu hawapaswi kuwa na hadhi; mara tu watu wanapokuwa na hadhi, wamekwisha. Kufuatilia hadhi ni tamanio la kupita kiasi. Jaribu tu kuwa mtu asiye muhimu kabisa, na haijalishi unaenda wapi, keti kwenye kiti cha chini kabisa, keti mahali pasipoonekana kabisa. Watu lazima wawe wanyenyekevu; huu ndio unaoitwa unyenyekevu." Je, amepitia mabadiliko yoyote ya maana? Je, amekuwa na uzoefu wowote wa kweli? (Hapana.) Hakuna kati ya mambo haya ambayo yametokea. Je, ana ufahamu wowote wa tabia zake potovu? (Hapana.) Hana uelewa wowote kuzihusu. Kwa hivyo, je, anakubali ukweli au maneno ya Mungu? (Hapana.) Watu ambao hawakiri kwamba wana tabia potovu hawakubali ukweli kamwe. Ikiwa wangeukubali ukweli, wangelinganisha kila neno na tendo lao na ufunuo wao wa upotovu na maneno ya Mungu. Walipofunua upotovu, wangejitafakari, wakiuliza, "Kwa nini, ndani ya muktadha fulani, nilifunua upotovu? Nilikuwa nikifikiri na nilikuwa nikitawaliwa na kitu gani wakati huo?" Kupitia ufichuzi wa maneno ya Mungu na kufanya ulinganisho, wangegundua kwamba hii ni tabia potovu, na kwamba wao si watakatifu au safi kama walivyowazia, kwamba kumbe wao pia wana udanganyifu, nia za ubinafsi, tamaa ya makuu, na matamanio, na kwamba wao si watu walio na uhalisi wa ukweli hata kidogo. Je, wamekuwa na uzoefu kama huo? Hapana. Wamesema maneno mengi, lakini hakuna hata ukweli mmoja unaothibitisha wanakiri kwamba wana tabia potovu. Wamemwamini Mungu kwa miaka mingi sana, lakini hawana uzoefu wowote ule wa ukweli. Wanazungumza tu mafundisho, wanatafakari tu jinsi ya kuweka mwonekano wa kujifanya na kujipamba ili kuficha dosari na kasoro za ubinadamu wao. Wanajipamba kwa mienendo ya inje, matendo ya inje, mionekano ya uso ya inje, mkao wa inje, na mwenendo wa inje wa hali ya kiroho ya uongo, huku wakiendelea kufungia tabia zao potovu ndani yao kwa nguvu, kwa uthabiti, na kwa usalama. Hawakubali hata kidogo masuala yoyote mbalimbali ya tabia potovu za mwanadamu ambayo Mungu anayafichua, wala kauli mbalimbali ambazo Mungu anazitumia kufichua tabia hizi, wala hawazizingatii wala hawaziweki moyoni; wanatia tu bidii katika mwonekano wa nje wa ubinadamu wao. Kisha ukiwaomba wazungumze kuhusu uelewa wao wa maneno ya Mungu, ikiwa wana ufahamu au uthamini wowote wa kweli wa maneno Yake ya kuadibu na hukumu, maneno Yake yanayofichua tabia potovu za binadamu, au maneno Yake kuhusu tabia ya Mungu, wanaepuka mada hizi za vitendo na tena wanatoa mkondo wa nadharia za kiroho: "Mungu ndiye Muumba, Mungu anatawala juu ya vitu vyote, matendo ya Mungu ni ya ajabu! Mungu anastahili kusifiwa na kutukuzwa, Mungu ni wa kipekee, mamlaka na nguvu za Mungu ni kuu!" Watu husema, "Basi zungumza kuhusu uzoefu wako mwenyewe. Ni katika jambo gani uliona tabia ya Mungu na utakatifu wa Mungu?" Wanajibu, "Mungu ni mkuu sana, mwanadamu ni duni sana, mwanadamu hastahili! Machoni pa Mungu, mwanadamu ni duni hata kuliko mchwa ardhini. Mungu anamwinua mwanadamu!" Je, wana uelewa wowote wa aina hii? (Hapana.) Hawana uelewa wa aina hii hata kidogo. Huyu ni mtu wa aina gani? (Mfarisayo mnafiki.) Huyu ni Mfarisayo mnafiki. Hawaukubali ukweli hata kidogo; maneno ya Mungu na ukweli ni kaulimbiu na mafundisho tu machoni pao. Kwa kawaida wao husoma maneno ya Mungu, huandika dondoo za ibada ya kiroho, na huhudhuria mikutano na husoma kwa kuomba maneno ya Mungu—hutekeleza taratibu hizi zote bila kukosa hata moja au kuacha yoyote. Kwa hivyo, wamejifunza kitu gani kutokana na kusoma maneno haya ya Mungu? Wamepata kitu gani? Hawasomi maneno ya Mungu ili kuelewa ukweli, sembuse kulinganisha maneno Yake na tabia zao potovu, dhana na mawazo yao ya kufikirika, au fikira na mitazamo yao potofu, ili kwamba waweze kutatua matatizo yao, na kuja kuwa na njia ya kufuata katika utendaji wao. Wanasoma maneno ya Mungu ili kujizatiti kwa mafundisho ili kwamba waweze kutoa hotuba na kuwafundisha wengine mafunzo kwenye mikutano. Kile wanachosema hutofautiana kila wakati, na wanaweza kuzungumza bila kukoma kwa muda mrefu, wakichagua maneno tofauti ya Mungu kushiriki na watu tofauti, wakilenga kuwafanya wengine wawaenzi na wawaabudu. Baadhi ya watu ni stadi hasa katika kujificha—wanaweza hata kuwa wenye kudharauliwa kiasi gani? Wanaposikiliza maneno ambayo Nimenena na wanayaona kuwa yanafaa, huyakariri, na kisha hutafuta fursa za kujionyesha wakati wa mikutano. Hasa, wanapokuwa miongoni mwa makundi ya waumini wapya—watu ambao hawajasikia mahubiri mengi, na ambao hawawezi kukumbuka maneno ya Mungu hata kama wamesoma kiasi—wanatumia fursa hii na kuanza kujionyesha na kujigamba miongoni mwa waumini hao wapya. Baada ya kuwasikiliza, kila mtu hufikiri, "Mtu huyu ametiwa nuru na Roho Mtakatifu, yeye ni mtu wa kiroho." Kutumia mbinu kama hizo kujigamba ili kupata enzi na heshima ya wengine—je, hili si jambo la kudharauliwa? Je, huku si kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Huku ni kuwapotosha watu.

Ikiwa, katika maisha yako yote, unatafuta kanuni za ukweli na unatafuta maneno ya Mungu kuwa msingi wa kutatua tabia zako potovu na mambo yaliyo ndani yako ambayo hayapatani na ukweli, basi mwishowe hakika utakuwa mtu anayefikia wokovu. Lakini tuseme kwamba, katika maisha yako yote, unaelekeza jitihada zako na unatafuta njia za kutatua dosari na kasoro za ubinadamu wako, ukibuni mbinu za kila aina ili kujiondolea dosari na kasoro zozote, ili kwamba uweze kuwa mtu aliye tofauti na wengine, mkamilifu, na asiye na kosa. Baadhi ya watu hata husema, "Ninataka kuwa mtu safi, mtu wa hali ya juu na mwenye ukuu, mtu anayevuka ubinadamu wote wa kawaida." Acha Nikuambie: Kwa kufanya hivi, umeshindwa! Haijalishi ni dosari wala kasoro gani ya ubinadamu wako unayojaribu kutatua, haina uhusiano wowote na wokovu wako, kwa sababu huufuatilii ukweli ili kutatua tabia zako potovu. Ukitatua kasoro na dosari za ubinadamu wako, basi kwa kiwango cha juu kabisa hili linamaanisha tu kwamba hakuna dosari za ubinadamu zinazoweza kuonekana ndani yako kwa nje, na unaonekana kuwa mkamilifu na mstaarabu kwa juu juu. Sahau kuhusu ukweli kwamba dosari na kasoro za ubinadamu wako kimsingi haziwezekani kubadilika; hata ikiwa zingebadilishwa, dosari na kasoro zako kubwa zaidi—tabia zako potovu—bado zimefichika ndani yako! Kadiri unavyozidi kujifanya na kufuatilia ubinadamu mkamilifu ambao hauna kasoro zozote, ndivyo tabia zako potovu zitakavyozidi kukunasa na kukufunga kwa kina na kwa nguvu kabisa, zikikufanya uwe mwenye kiburi, mdanganyifu, mwovu, na mkaidi hata zaidi. Na matokeo ya hili ni nini? Linakufanya ukengeuke mbali zaidi na ukweli na kutoka kwenye njia ya kufuatilia ukweli. Mwishowe, kuondolewa kutakuwa matokeo yako, na utakuwa umekwisha. Hakuna uwezekano kwamba Mungu atafanya upekee na kukuokoa kwa sababu tu wewe ni mkamilifu kwa nje au unaonekana kuwa mtu safi. Kinyume chake, kadiri unavyofuatilia ubinadamu mkamilifu usio na dosari zozote, ndivyo Mungu atakavyokuchukia zaidi na hatafanya kazi juu yako. Hata hivyo, baadhi ya watu mara nyingi huhisi majuto na huzuni kwa sababu wanafunua tabia potovu. Huku wakihisi majuto, wanakuza azimio la kuufuatilia ukweli, wanaweza kuvumilia dhiki na kulipa gharama ili kuupata ukweli, wanadumu katika kusoma maneno ya Mungu kila siku, na kumwomba Mungu na kuutafuta ukweli katika mambo yote. Kwa namna hii, wanazidi kuwa wazi kuhusu ukweli, hatua kwa hatua wakifikia uingiaji fulani, mafanikio fulani, na kuishi kwa kudhihirisha halisi kuhusiana na vipengele vyote vya ukweli. Mwishowe, wanapokabiliwa na watu, matukio, na vitu vya kila aina, wanakuwa na kanuni za ukweli zinazolingana za kutenda na kufanya tathmini nazo. Baada ya miaka mingi ya uzoefu, kupitia kuadibu kwa Mungu na hukumu Yake, upogoaji Wake, na pia kupitia gharama ambayo wamelipa katika kuufuatilia ukweli, hatua kwa hatua wanakuja kuwa na ukweli kama uzima wao ndani yao. Tumaini lao la wokovu linazidi kuwa kubwa zaidi, na uwezekano wa wao kuasi dhidi ya Mungu na kumsaliti Yeye unazidi kuwa mdogo zaidi. Ingawa kasoro na dosari za ubinadamu wao na hali zao za asili kimsingi zinabaki bila kubadilika, tabia zao potovu zinapungua hatua kwa hatua, wanampinga Mungu na kuasi dhidi Yake mara chache zaidi, wanazidi kupendwa na Mungu, wanazidi kuwa wenye kujenga kwa wengine, na wanazidi kuwa wanaofaa kutumiwa. Ikiwa watu kama hawa wataendelea katika njia hii, basi hakika watakuwa wale wanaofikia wokovu; hawa ndio wale ambao kazi ya Mungu inakusudia kuwaokoa. Watazameni watu walio karibu nanyi. Angalieni ni nani ambaye daima huendelea kujitahidi katika mionekano, katika dosari, kasoro, na udhaifu wa ubinadamu wake, akifanya kila awezalo kujificha na kujifanya ili kupata sifa, uvutiwaji, na heshima ya wengine, na kuwa na hadhi mioyoni mwa watu—watu wa aina hii ndio Mafarisayo. Mafarisayo wana tokeo moja tu la mwisho: kuangamia pamoja na panya. Kwa hivyo Ninasema kwamba watu wa aina hii wamekwisha na wameondolewa.

Kuanzia mwanzo hadi mwisho, kazi anayofanya Mungu si kubadilisha kasoro na dosari katika ubinadamu wa watu, ni kurejesha tu dhamiri na busara ya ubinadamu wa kawaida. Kile ambacho Mungu anataka kubadilisha ni tabia potovu za watu. Bila shaka, Mungu pia mara nyingi hunena kuhusu kuondoa tabia potovu za watu na hivyo kuwawezesha kufikia wokovu. Kwa hivyo, urejesho wa ubinadamu wa kawaida umejengwa juu ya msingi gani? Umejengwa juu ya msingi wa watu kuwa wamevua tabia zao potovu. Ubinadamu wa kawaida wa watu kurejeshwa hatua kwa hatua kunamaanisha kwamba dhamiri yao inapata hisia, busara yao inazidi kuwa ya kawaida, na wanaweza kufanya mambo sahihi na kusema maneno sahihi kutoka katika mtazamo wa ubinadamu wa kawaida; hawasababishi vurugu wala usumbufu, wana busara hasa, maneno na matendo yao si ya msukumo, ya upofu, au ya pupa, bali yanaligana kabisa na kanuni za maneno ya Mungu, busara yao ni ya kawaida hasa, na ubinadamu wao ni mnyoofu na mwema hasa. Kwa hivyo, ni kwa msingi gani mambo haya yanaweza kufikiwa, na kiwango hiki cha urejesho kinaweza kufikiwa? Yanafikiwa kwa msingi wa tabia potovu za watu kubadilishwa, kwa watu kuvua tabia zao potovu kupitia kutenda ukweli na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Ikiwa tabia zako potovu hazijabadilishwa na hazijavuliwa, hata ikiwa ubinadamu wako ni mzuri kiasi na una dhamiri na busara kiasi, maisha yako hayawezi kutawaliwa na dhamiri na busara ya ubinadamu wa kawaida. Wakati hujavua tabia zako potovu, maisha yako ni maisha ya tabia za kishetani, badala ya ukweli kuwa uzima wako. Kwa hivyo, hata ikiwa una dhamiri na busara kiasi, bado utashawishiwa, utachochewa, na utasukumwa mara kwa mara na tabia zako potovu kufanya mambo yanayoenda kinyume na dhamiri na busara. Kwa hivyo, hata ikiwa una hisia ya haki kiasi, ni aina tu ya matamanio na azimio. Una ubinadamu mwema kiasi tu, lakini kwa sababu tabia zako potovu ndizo uzima wako na zinakudhibiti kutoka ndani, kile unachoweza kufikia ni kutotenda maovu tu na kutochukua hatua ya kwanza kuwadanganya na kuwadhuru wengine, jambo ambalo tayari ni kufanya vizuri kabisa. Yaani, unaweza tu kuhakikisha kwamba hutendi maovu wakati masilahi yako binafsi hayaathiriwi, na mara tu masilahi yako binafsi yanapoathiriwa, tabia zako potovu zitaibuka na zitakandamiza dhamiri na busara yako, zikikufanya utetee masilahi na haki zako mwenyewe, na hivyo itakuwa vigumu sana kwako kuruhusu dhamiri na busara kuchukua usukani. Kwa nini iwe hivyo? Ni kwa sababu uzima wako si ule wa ukweli kuwa ndio uzima wako, bali ni ule wa tabia za kishetani kuwa ndizo uzima wako. Kwa hivyo, unaweza tu kufunua dhamiri na busara kiasi ya ubinadamu wa kawaida chini ya sharti la masilahi yako kutodhuriwa. Mara tu jambo linapotokea ambalo lingesababisha masilahi yako kupata hasara au kutishia maisha yako, tabia zako potovu zitachukua usukani na zitanyakua mamlaka mara moja. Dhamiri na busara zako zitatoweka baadaye, na utafanya mambo yanayoenda kinyume na dhamiri na busara, kinyume na maadili, na kinyume na haki ya kimaadili; hata utaweza kutenda uovu wa aina yoyote. Bila shaka, inaweza kusemwa kwamba matendo haya yote yanaenda kinyume na ukweli; jambo hili haliepukiki. Kwa hivyo, kile ambacho mtu anaishi kwa kudhihirisha hakitegemei hali za ubinadamu wake, bali kinategemea kiini cha uzima wake wa ndani ni nini. Ikiwa kwa kweli ana ukweli kama uzima wake, basi uzima wake una ukweli, maneno ya Mungu, na njia ya kumcha Mungu na kuepuka uovu. Kisha dhamiri na busara zake za ubinadamu wa kawaida zitabaki katika hali bora na zitaweza kufanya kazi, zikimwezesha kutenda ukweli na kutenda kulingana na kanuni. Hata hivyo, ikiwa kiini cha uzima cha mtu ni tabia zake potovu, basi dhamiri na busara zake zinashushwa hadi kiwango cha chini kabisa, yaani, hashuki tu chini ya mpaka wa chini kabisa wa ubinadamu. Mpaka huu wa chini kabisa ni upi? "Sitashambulia isipokuwa nishambuliwe; nikishambuliwa, hakika nitalipiza kisasi"; "Jino kwa jino, jicho kwa jicho"; "Wape wengine kionjo cha dawa yao wenyewe." Nini kingine? "Ni afadhali kuwa mhalifu wa kweli kuliko mwungwana wa uongo." Huu ndio mpaka wa chini kabisa wa jinsi watu wengi wasioamini wanavyojiendesha. Kwa mtu asiyeamini, kuweza kutenda kwa namna hii tayari ni kufanya vizuri kiasi. Mmeelewa nini kutokana na hili? Usipoufuatilia ukweli, tabia zako potovu hazitavuliwa, kiini cha uzima wako hakitabadilika, na ikiwa kiini cha uzima wako hakitabadilika, basi dhamiri na busara zako za ubinadamu wa kawaida hazitarejeshwa kimsingi, na kwa umbo tu, hazitashuka chini ya mpaka wa chini kabisa wa ubinadamu. Hata hivyo, ikiwa tabia zako potovu zimevuliwa na kiini cha uzima wako kimebadilika, basi dhamiri na busara ya ubinadamu wako wa kawaida, kwa kiwango fulani, zitaboreshwa na zitainuliwa. "Kuboreshwa" na "kuinuliwa" kunarejelea nini hapa? Inamaanisha kwamba dhamiri na busara zako zinaanza kufanya kazi kwa kawaida—si kweli kwamba hazivuki tu mpaka wa chini kabisa, badala yake zinafikia kiwango cha kutenda ukweli. Wale wanaoitwa watu wema miongoni mwa watu wasioamini huonyesha tu dhamiri na busara kiasi, hawatendi matendo maovu yaliyo wazi, na hawavuki mpaka wa chini kabisa wa haki ya kimaadili. Hili tayari ni kufanya vizuri kabisa; wanaweza kuchukuliwa kuwa watu wema sana. Hata hivyo, watu mbao wana ukweli kama uzima wao huenda zaidi ya kiwango hili; wana uwezo wa kutambua jambo lililo sahihi na lisilo sahihi, na wanaweza kutambua aina mbalimbali za mambo yaliyo sahihi na yasiyo sahihi, na kuwatambua watu aina mbalimbali. Kwa hivyo msingi wao ni upi? Ni kanuni za ukweli. Wana kanuni za ukweli—je, hiki si kiwango cha juu zaidi kuliko kiwango cha dhamiri na busara? (Ndiyo.) Kwa sababu wanaelewa ukweli na wana ukweli kama uzima wao, na msingi wanaotumia kutambua mambo mbalimbali ni wa juu zaidi kuliko kiwango cha watu wapotovu wa kawaida, watadumu katika kutenda kulingana na kanuni za ukweli wanapokabili mambo magumu. Baada ya kufahamu kanuni za ukweli, akili zao hazitachanganyikiwa na fikira zao zitakuwa wazi. Wazi inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa na busara. Haijalishi mambo wanayokumbana nayo ni magumu kiasi gani, kanuni za ukweli za utendaji zimekita mizizi mioyoni mwao; wameelewa ukweli kwa usahihi na kikamilifu, na tayari umekuwa uzima wao. Wanapokabiliwa na watu, matukio, na vitu vya kila aina vigumu, wana kigezo cha msingi, nacho ni kushikamana na kanuni za ukweli. Kanuni hizi za ukweli zinawawezesha kung’amua kiini cha mambo mbalimbali magumu na uhalisi wa suala hilo ni nini; wanaweza kuyatambua mambo haya. Hii ndiyo busara yao. Je, busara hii si ya juu zaidi kuliko ile ya watu wa kawaida? (Ndiyo.) Basi, baada ya kufikia kiwango hiki, je, busara yao haijainuliwa na haijaboreshwa? (Ndiyo.) Ubinadamu wa kawaida wa aina hii ndio ambao Mungu anautaka; Mungu hataki watu waliochanganyikiwa. Baadhi ya watu husema, "Mimi sina hila na ni mwoga, na mimi daima ninaonewa," huku wengine wakisema, "Ubora wangu wa tabia ni duni sana, na sina uwezo wala talanta yoyote." Mungu anasema kwamba mambo haya si muhimu, na kwamba jambo muhimu ni ikiwa unaelewa kanuni za ukweli. Ikiwa unaelewa kanuni za ukweli, na unazungumza na unatenda kulingana na viwango na kanuni za kuwa mtu mwaminifu, basi hata ikiwa watu wasioamini wanakudhihaki kuwa mpumbavu, huo si upumbavu wa kweli. Kwa nini? Ni kwa sababu, mara tu unapoelewa kanuni za ukweli, busara yako inakuwa timamu na inaboreshwa, ya juu zaidi kuliko ile ya watu wa kawaida. Unapokumbana na jambo lolote, huchanganyikiwi; una kanuni, msimamo, na malengo sahihi kama msingi wa kulishughulikia. Akili yako iko wazi na fikira zako ziko wazi. Unatenda, ukijitahidi kufikia kanuni na viwango hivyo, na hakika huendi kinyume na nia za Mungu; hakika unatenda kulingana na nia Zake. Baada ya kushughulikia jambo hilo, bila kujali kama watu waliling’amua wakati huo, mara tu muda wa kutosha unapopita na watu wanapoelewa, wote watasadikika kabisa, na watajua kwamba jinsi ulivyolishughulikia lilikuwa na manufaa makubwa. Kwa hivyo, chanzo kikuu cha kufikia matokeo kama hayo ni nini? Ni kwamba una ukweli kama uzima wako. Ni hapo tu ndipo busara yako inaweza kukuwezesha kuwa na hukumu sahihi, uainishaji sahihi, na mahitimisho sahihi kuhusu mtu yeyote na jambo lolote, na vilevile kanuni sahihi za utendaji, na bila shaka, kanuni sahihi za kuwasaidia na kuwaongoza watu. Je, busara yako haijainuliwa na haijaboreshwa basi? Ubinadamu wa kawaida hupata busara kama hiyo kutoka wapi? (Ukweli.) Watu walio na ukweli kama uzima wao ndio binadamu ambao Mungu anawataka. Huenda wewe ni mpumbavu, huna hila, ni mwoga, na huna uwezo, labda hupendwi na watu na unaonewa na watu duniani, lakini hakuna lolote kati ya mambo haya ambalo ni muhimu; haya si mambo ambayo Mungu huangalia. Huenda una uwezo mkubwa duniani, stadi hasa katika kuwasoma watu, kutambua mienendo, na kubadili mwelekeo kulingana na upepo unaovuma, lakini jambo hili pia halina maana; halimaanishi kwamba busara yako ni timamu. Ni pale tu ambapo umeukubali ukweli, umeelewa ukweli, na umeelewa, umetenda, na umepata uzoefu wa ukweli wote, na ukweli umekuwa uzima wako, ndipo utambuzi, hukumu, na maamuzi yako kuhusu mambo mbalimbali yanaweza kuwa sahihi.

Kuhusu dhamiri—tumesema hapo awali inarejelea nini? Ni hisia ya haki na wema wa ubinadamu wa kawaida. Mtu lazima awe mnyoofu na mwema ili asemwe kuwa ana dhamiri. Kwa hivyo, unyoofu na wema wa ubinadamu wa kawaida vinawezaje kuboreshwa na kuinuliwa baada ya mtu kuja kumwamini Mungu? Hili lazima lijengwe juu ya msingi wa kuelewa ukweli. Yaani, baada ya mtu kuuelewa ukweli, vigezo anavyotumia katika kujiendesha na kutenda vitakuwa lengo chanya, ambalo litakuwa na athari chanya, thamani chanya, na maana chanya kwake mwenyewe na kwa kila mtu mwingine. Mara tu anapoelewa ukweli, atatazama na atashughulikia kila kitu kulingana na kanuni za ukweli zinazofundishwa na Mungu. Machoni pa wengine, mtu kama huyo ni mnyoofu kabisa. Unyoofu unamaanisha nini? Unyoofu unamaanisha kutopendelea upande wa kushoto au wa kulia, kutoegemea kuelekea kushika moto, hisia, masilahi au mahusiano ya kibinafsi, au nia za kibinafsi, bali ni kutenda kuelekea lengo lililo sahihi kabisa, linalofaa kabisa, lile linalostahili kabisa heshima, uvutiwaji, na kuthaminiwa sana na watu—au, inaweza kusemwa, kutenda kuelekea lengo ambalo Mungu analiona kuwa jema na analikubali. Je, huu si bora kuliko "unyoofu" kama unavyotazamwa na binadamu wapotovu wa kawaida? (Ndiyo.) Unyoofu huu unamaanisha nini? Unalingana kikamilifu na kanuni za ukweli, unategemea kabisa maneno ya Mungu, na umejengwa juu ya msingi wa dhamiri. Mtu anapoelewa ukweli, huwa na njia na kanuni za kutatua matatizo na kushughulikia mambo, kwa hivyo je, dhamiri ya mtu huyu si kamilifu kabisa? Je, haijaboreshwa? (Ndiyo.) Basi je, mtu wa kweli, kiumbe wa kweli aliyeumbwa, hapaswi kuwa na dhamiri kama hiyo? Je, hapaswi kuwa na unyoofu katika maana hii? (Ndiyo.) Mtu wa kweli anapaswa kuwa na unyoofu katika maana hii unaolingana na ukweli, badala ya ule ambao watu huzungumzia—kuwa mnyoofu na asiye na upendeleo kwa uthabiti, wazi na mwadilifu, au "mwanamume wa kweli hafichi chochote na daima husimamia matendo yake." Huko ni kushika moto, hakuna maudhui yoyote halisi, na ni jambo ambalo watu hujifanya kuwa nalo kabisa. Unyoofu una ukweli kama msingi wake; kuna matendo halisi ya kuishi kwa kudhihirisha ndani yake. Inamaanisha kwamba mtu aliye na ubinadamu wa kawaida ana ukweli kama chanzo na kianzio chake, na anaweza kuchukulia na kushughulikia mambo mbalimbali kulingana na maneno ya Mungu—huu ndio unaitwa unyoofu. Wema, hata zaidi, hauna haja ya kusemwa; angalau, unazidi kiwango cha dhamiri na busara. Ndani ya wema, hakuna unafiki, sembuse ukatili. Ni kutenda kabisa kulingana na njia ambazo zina manufaa na zinawajenga watu, na ambazo wakati huohuo zinalingana na matakwa ya Mungu; ni kutenda kabisa kulingana na lengo na vigezo vya kumcha Mungu na kuepuka uovu, kumridhisha Mungu, na kuifuata njia ya Mungu. Hili ndilo jambo jema kabisa, zuri sana chini ya mbingu, katika ulimwengu mzima. Mtu ambaye ana maneno ya Mungu au ukweli kama uzima wake hakika ana moyo mwema kabisa, kwa sababu anaweza kuukubali ukweli, na jambo hili linafikia kikamilifu kiwango ambacho Mungu anawataka watu wafikie. Kwa kuwa ana ubinadamu wa aina hii, inafaa kusema kwamba yeye ni mnyoofu, na inafaa pia kusema kwamba yeye ni mwema. Hii ni kwa sababu anaweza kukubali na kutenda ukweli, na haongozwi na hisia zake wala hana tamaa ya makuu wala matamanio katika utekelezaji wa wajibu wake, na hana ndani yake sumu za utamaduni wa kimapokeo, na kiwango chake cha kupima maadili na ubinadamu hakijachanganywa na falsafa, fikira, wala mitazamo yoyote ya Shetani—kinalingana kikamilifu na ukweli. Basi Niambie, je, ubinadamu ulio na dhamiri na busara kama hizo tayari haujaboreshwa sana? (Ndiyo.) Kwa sababu mtu wa aina hii ana ukweli, na kwa sababu kiini cha maisha anayoishi kwa kudhihirisha ni ukweli, ubinadamu wake ulio na kiini kama hicho cha uzima ni mkamilifu. Ikiwa hampendi kusikia neno "mkamilifu," basi Ninaweza pia kuliita "lililoboreshwa." Angalau, machoni pa Mungu, ameboreshwa na anapendwa na Mungu. Mungu anatumia ufahamu kidogo wa dhamiri, busara, na hisia ya aibu ambao watu wanao kufinyanga maneno Yake na ukweli ndani yao. Ukweli wa maneno ya Mungu unapofinyangwa ndani yako, si tu kwamba dhamiri na busara zako hazidhoofishwi wala hazifichwi, bali badala yake zinakuwa za kawaida zaidi na zilizoboreshwa zaidi. Hao ndio binadamu ambao Mungu anawataka. Tuseme si wakamilifu, tuseme walioboreshwa. Kwa nini tusiseme wakamilifu? Nikisema wakamilifu, baadhi ya watu wasiokuwa na ufahamu wa kiroho watasema, "Je, si Ulisema kwamba tusiwe watu wakamilifu?" Kwa hivyo inabidi Niepuke neno hili, endapo watu wengine wataelewa vibaya. Kwa kweli, ikiwa kitu kimeboreshwa machoni pa Mungu, basi miongoni mwa binadamu walioumbwa kinaweza kusemwa kuwa kikamilifu. Ukamilifu huu si ukamilifu katika mawazo ya kufikirika ya watu, bali ni jambo zuri na jema, nguvu ya haki, na pia jambo chanya, linachostahili sifa, hamu, uthamini, heshima, na utunzaji wa watu. Kwa hivyo, ukitaka dhamiri yako isikwame tu katika kutovuka mpaka wa chini kabisa wa ubinadamu katika mwenendo wako wa kibinafsi, bali unataka kuifanya dhamiri yako iwe nyeti zaidi, yenye ufahamu zaidi, na kuifanya busara yako ifikie matakwa ya Mungu, basi una njia moja tu. Njia hii si kushinda dosari na kasoro mbalimbali za ubinadamu, bali ni kuufuatilia ukweli, kuweka jitihada katika ukweli mbalimbali ambao Mungu huwafundisha watu, na kuelewa viwango ambavyo Mungu anataka kwako ni vipi linapokuja suala la watu, matukio, na vitu mbalimbali, na jinsi unavyopaswa kutazama, kuchukulia, na kushughulikia watu, matukio, na vitu hivi. Mungu ana kanuni na viwango vinavyohitajika kwa vipengele hivi vyote. Kazi yako ni ipi? Ni kutenda kuelekea upande huu, lengo hili, kulingana na viwango hivi. Kwanza, tafuta na uelewe viwango vya kutenda ukweli ni vipi. Kisha, jiwekee matakwa kulingana na viwango ambavyo Mungu anataka, huku wakati huohuo ukiachilia fikira, mitazamo, sheria, taratibu, visanduku mbalimbali, na kadhalika katika dhana na mawazo yako ya kufikirika ambayo hayaendani na maneno ya Mungu wala ukweli. Kisha, yaruhusu maneno ya Mungu hatua kwa hatua yawe kanuni zako za utendaji. Huku ukijifunza kuachilia, usisahau: Kusudi la kuachilia si kukufanya uwe mtu asiye na kitu chochote ndani ya moyo wake; Mungu anataka maisha yako yawe na maudhui. Maudhui haya yanarejelea nini? Yanarejelea kanuni ambazo Mungu anataka kwa mambo mbalimbali. Bila shaka, Mungu hataki watu wageuze kanuni mbalimbali za utendaji kuwa nadharia tupu, wakizizungumzia tu lakini bila kuziweka katika utendaji. Badala yake, Anatumaini kwamba watu wanaweza kugeuza kanuni hizi za ukweli kwa uthabiti kuwa sehemu ya maisha yao, na kuyaleta maneno ya Mungu katika maisha yao halisi. Chukua kufanya wajibu, kwa mfano—Mungu anataka kiwango gani kutoka kwa watu katika suala hili? Ni wao kujiendesha kwa namna ya uhalisi na kulingana na nafasi yao inayofaa. Yaani, katika kufanya wajibu wako, lazima uwe mwenye uhalisi, lazima usiwe wa kufanya mambo kwa kijuujuu tu wala kwa haraka haraka, lazima usifanye mambo kwa mazoea tu, au kuutekeleza ili wengine waone, na pia lazima usijionyeshe; bila shaka, lililo muhimu hata zaidi ni kwamba lazima utende kulingana na kanuni za ukweli. Unapaswa kutenda kwa njia ambayo Mungu anakuambia utende, na unapaswa kujizuia kufanya mambo ambayo Mungu anakuambia usiyafanye. Ikiwa huwezi kujizuia kabisa kufanya mambo hayo, basi anza kwa kuyafanya mara chache zaidi, uasi dhidi ya matamanio yako mwenyewe na mapendeleo yako mwenyewe, na hatua kwa hatua uje kujizuia kuyafanya kabisa—je, hili si rahisi kufikia? (Ndiyo.) Katika mchakato wa kufuatilia wokovu, unapaswa kutatua na kuachilia tabia mbalimbali potovu zinazofichuliwa na maneno ya Mungu. Bila shaka, kuachilia tabia hizi potovu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni, kwa sharti la kuachilia tabia hizi potovu, kukubali maneno ya Mungu na matakwa ya Mungu. Kuyakubali si kwa ajili ya kubadilisha hali yako, wala si kwa ajili ya kukuwezesha kuishi kwa heshima; ni kwa ajili ya kuvua tabia zako potovu. Hili ndilo lengo la mwisho, kwa maana unaweza tu kufikia wokovu baada ya kuvua tabia zako potovu.

Kikwazo kikubwa kabisa kwa watu kufikia wokovu ni tabia zao potovu. Elimu yako duni, uzee wako, au namna yako ya kuzungumza isiyo ya ustadi na ukosefu wako wa uwezo wa kujieleza—hakuna hata kimoja kati ya hivi ambacho ni kikwazo kikubwa kabisa kwa wokovu. Ustadi wako duni wa kitaaluma katika wajibu wako na kutoweza kwako kuumudu— hiki pia si kikwazo kikubwa kabisa kwa wokovu wako. Basi kikwazo kikubwa kabisa kwa wokovu ni nini? Ni tabia zako potovu. Bila shaka, tabia mbalimbali potovu za mwanadamu ambazo zinafichuliwa katika maneno ya Mungu si rahisi kwa watu kuzitatua. Hii si kwa sababu watu hawako tayari kuachilia tabia zao potovu, wala si kwa sababu fikira na mitazamo yao imepitwa na wakati, na, bila shaka, si hasa kwa sababu ya kasoro au dosari katika ubinadamu wao, wala si kwa sababu watu ni wajinga, wazito kuitikia, na kadhalika—hakuna hata kimoja kati ya hivi ambacho ni chanzo cha tatizo. Basi ni kwa nini? Ni kwa sababu tu tabia potovu za watu zimekita mizizi mioyoni mwao, watu hawawezi kuzivua kwa sababu tu wanataka, na hivyo tabia zao potovu mara nyingi hujitokeza na kusababisha usumbufu na kuleta shida huku wakifanya wajibu wao. Kwa mfano, tuseme wewe ni kiongozi wa kanisa, na ulifanya jambo fulani baya na ukapogolewa. Katika hali hiyo, unapaswa kukubali hilo, kukiri kwamba ulifanya jambo baya, kuwa tayari kutubu, na kubadili mbinu hiyo usiyo sahihi na kutenda kulingana na kanuni za ukweli. Hili ni jambo rahisi sana, lakini huwezi kulifanya. Unatafakari, "Je, nilipogolewa hivi kwa sababu wananiona kuwa sipendezi na wanataka kunivua wadhifa?" Malalamiko na kutoelewa huibuka moyoni mwako, na hata unajaribu kubishana na Mungu, "Kwa kuwa Unaniona kuwa sipendezi na Unataka kunivua wadhifa na kuniondosha, basi sawa, hebu tuweke hili wazi. Nilianza kumwamini Mungu nikiwa na miaka kumi na minane, nimekuwa kiongozi miaka hii yote, nikitelekeza familia na kazi, nikiacha ndoa na familia—haya yatahesabiwaje?" Kadiri unavyozidi kufanya hesabu, ndivyo unavyozidi kukasirika. Je, huku ni kutoweza tu kuachilia? Hapana. Kwa nini huwezi kuyaachilia mambo haya? Kuna tatizo la msingi hapa. Unapopogolewa, unahisi umetendewa isivyo haki, unalalamika na unahisi ukaidi moyoni mwako, na pia unajaribu kubishana na kujitetea, na hata kuwaomba wengine wakutetee. Kwa nini unatenda hivi? (Kwa sababu tuna tabia potovu.) Kuna sababu moja tu, chanzo kimoja: Una tabia potovu ambazo hujazitatua. Baadhi yenu mtasema, "Je, ni kwa sababu ubora wangu wa tabia wa asili na uwezo wangu havitoshi na siwezi kufanya kazi hiyo?" Inawezekana kwamba, kwa baadhi yenu, hii ni mojawapo ya sababu; kwa sababu ya ubora duni wa tabia hamna uwezo wa kufanya kazi hiyo, na pia hamwelewi ukweli, kwa hivyo mnafanya mambo yanayosababisha vurugu na usumbufu. Je, hili ni kwa sababu tu ubora wako wa tabia ni duni? Hicho ni kipengele kimoja tu. Tatizo la msingi ni kwamba kuna suala katika dhamiri yako. Suala hili la dhamiri yako linahusiana moja kwa moja na tabia zako potovu. Ulifanya mambo yaliyosababisha vurugu na usumbufu na ukapogolewa—unapaswa kulichukuliaje hili? Unachukuliaje jambo la wewe kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo? Ikiwa unaweza kutenda ukweli, haya si matatizo, na unaweza kuyachukulia kwa usahihi. Lakini watu wengi hujiendeshaje wanapokumbana na mambo haya? Wanajaribu kubishana, wanalalamika, wanakuwa hasi, na hata wanazungumza kwa kushika moto, "Je, si ni kwa sababu tu unafikiri kwamba ubora wangu wa tabia ni duni na sina uwezo? Je, si Mungu ndiye aliyenipa ubora huu wa tabia? Lakini unalalamika kwamba siwezi kufanya kazi hiyo! Kama unaniona kuwa sipendezi, ungesema hivyo mapema!" Ikiwa maneno makali kiasi yanatumiwa huku wakipogolewa, wanafikiri, "Je, tumaini langu la kupata baraka limetoweka? Hadhi yangu katika maisha haya iko hatarini, na labda sina tumaini katika dunia ijayo pia." Je, wana nia yoyote ya kuutafuta ukweli? Je, wanaweza kutii mioyoni mwao? Si rahisi kwao kutii. Madhihirisho haya yote, mwishowe, ni kwa sababu watu wana tabia potovu. Ubora wako wa tabia ni duni na huna uwezo wa kufanya kazi hiyo—hiyo ni mojawapo tu ya dosari au kasoro za asili za ubinadamu; hilo si tatizo. Hata ikiwa dosari na kasoro zako za asili ni kubwa na huna uwezo wa kufanya kazi hiyo, Mungu hahisi kutokupendezwa wala kuchukizwa na wewe hata kidogo. Lakini, mbali na kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo, hutambui matatizo yako mwenyewe, na pia unalalamika, unahisi upinzani, na mwishowe unakuwa hasi na unaiacha kazi yako—hili ni nini? Hizi ni tabia potovu. Hizi ndizo unazohitaji kuzitatua. Sivyo? (Ndiyo.) Baada ya tabia zako potovu kutatuliwa, utafaa kutumiwa katika kazi ambayo ubora wako wa tabia na hali za ubinadamu wako vinakuwezesha kufanya. Lakini, usipotatua tabia zako potovu, na usipoweza kutenda kulingana na ukweli, usipoweza kutii upogoaji, au kutii kufichuliwa, basi haijalishi ubora wako wa tabia ni mzuri kiasi gani, hali za ubinadamu wako ni bora kiasi gani, hutafaa kutumiwa. Umeelewa? (Nimeelewa.) Niambie, kiini cha yale tuliyofanya ushirika kuyahusu hivi punde kilikuwa nini? (Katika kumwamini Mungu, jambo muhimu kabisa ni kujua tabia potovu za mtu mwenyewe. Mkazo unapaswa kuwa katika kutatua tabia potovu za mtu, si kasoro au mapungufu ya nje ya ubinadamu wake. Tunapokumbana na hali mbalimbali, sisi daima hunaswa katika mambo ya nje, kimsingi hatuwezi kutatua matatizo ya msingi, na pia hatuwezi kufikia utii kwa upogoaji au utii kwa mazingira ambayo Mungu huandaa.) Ikiwa tabia zako potovu zimetatuliwa, na katika mambo unayokumbana nayo, unaweza kuelewa kanuni za ukweli, na unajua jinsi ya kuyashughulikia kulingana na kanuni, basi utafaa kutumiwa katika kufanya wajibu wako. Bila kujali kama ubora wako wa tabia ni wa juu au duni na bila kujali una talanta kiasi gani, ikiwa tabia zako potovu hazijatatuliwa, basi haijalishi unawekwa katika nafasi gani, hutafaa kutumiwa. Kinyume chake, ikiwa ubora wako wa tabia na uwezo wako vina ukomo, lakini unaelewa kanuni mbalimbali za ukweli, ikiwa ni pamoja na kanuni za ukweli unazopaswa kuelewa na kufahamu ndani ya upeo wa kazi yako, na tabia zako potovu zimetatuliwa, basi utakuwa mtu anayefaa kutumiwa. Mmeelewa? Huenda mkahitaji kutafakari maneno haya kwa muda ili kuyaelewa kikamilifu.

Kwa sasa, watu wengi kabisa bado wanategemea karama na wanafuata taratibu katika kufanya wajibu wao. Mradi tu hawatendi dhambi wala hawatendi maovu, wanaamini kwamba wametimiza wajibu wao. Hawalengi kuufuatilia ukweli na kujitafakari ili kutatua tabia zao potovu. Watu wengi kabisa hunaswa na hukwama tu katika mbinu na matendo, lakini hawalengi kuutafuta ukweli na kutenda kulingana na kanuni. Wanatosheka tu na kufanya yale wanayoweza, wakijaribu kutosababisha vurugu wala usumbufu, au kuharibu mambo, na ni hivyo. Watu wengi kabisa bado hawajakumbana na upogoaji au ufichuzi, wala hawajapitia kuadibu na hukumu, sembuse hatua ya majaribu makali, kwa hivyo tabia potovu za watu wengi kabisa hazijaanza kubadilika. Hizi si habari njema, lakini ni ukweli. Nitatoa mfano, na kisha mtajua kinachoendelea. Unaona, watu wengi kabisa wanaofanya wajibu sasa ni wafuasi wa kawaida; hawana hadhi, na hawajafikia hatua ambapo wanatekeleza kipengele fulani cha kazi huku wakiwa na hadhi na mamlaka. Kanuni ya msingi ambayo watu wengi kabisa hutenda ni kuwa wasikivu na watiifu. Wanafikiri kwamba, kwa vyovyote vile, viongozi wanafanya ushirika kulingana na mipango ya kazi ya Aliye juu, kwa hivyo wanafanya tu kile ambacho viongozi wanaomba, kwa namna ambayo viongozi wanawaomba wakifanye, na wanafikiri kwamba hakuna haja ya kutambua lililo sahihi au lisilo sahihi au kuchunguza ikiwa jambo hilo jambo hilo linalingana na ukweli, na kwamba mradi tu hawafanyi makosa, ni sawa. Je, huku ndiko kuwa na kanuni za ukweli kama uzima wa mtu? (Hapana.) Basi ni chini ya hali gani inaweza kuthibitishwa ikiwa una ukweli kama uzima wako? Ni wakati unapochaguliwa kuwa kiongozi wa kufanya kazi ya kanisa; hili huwafunua watu zaidi kabisa. Ikiwa una kanuni katika kushughulikia mambo na ni kiasi gani cha tabia zako potovu unachofunua kunaweza kuthibitisha ikiwa una uhalisi wa ukweli, na ikiwa unafaa kuwa kiongozi au mfanyakazi. Ukifunua tabia potovu, unapaswa kulichukuliaje hili? Je, unapaswa kuufungua moyo wako na kufanya ushirika kuhusu ukweli, au kujificha na kujifanya? Huu pia ndio wakati ambapo watu hufunuliwa kabisa. Watu wengi kabisa kanisani hawawezi kutazama mambo kulingana na kanuni za ukweli; badala yake, wanatazama na wanatoa maoni kuhusu mambo kulingana na dhana na mawazo yao wenyewe ya kufikirika, na kulingana na mapendeleo yao. Watu wengi kabisa hufikiri, "Mradi tu sifanyi makosa makubwa katika wajibu wangu, na ninaendeleza kazi hivi, hiyo inatosha. Nikifanya kosa kubwa na nitengwe kwa ajili ya kujitafakari au nihamishiwe kwenda kundi B, basi hiyo ni bahati yangu mbaya tu." Hali hii inadhihirisha nini? Ingawa unaweza kuwa msikivu na mtiifu katika mchakato wa kufanya wajibu wako, ukifanya chochote unachoombwa kufanya, hili halimaanishi kwamba una ukweli kama uzima wako, na halimaanishi kwamba wewe ni mtu anayemtii Mungu. Unapochaguliwa kuwa kiongozi na unapopata hadhi hiyo, utafunuliwa. Kwa nini? Mara tu unapokuwa na hadhi, utafanya chochote upendacho, utasimamia kila kitu, utadai utawala kamili, na utaanzisha ufalme huru; utatenda kulingana na kushika moto, kulingana na tabia zako mwenyewe potovu, na kulingana na matamanio na tamaa yako mwenyewe ya makuu. Kwa hivyo, bado hufai kutumiwa. Hadi sasa, inaweza kusemwa kwamba asilimia tisini na tisa ya watu wako katika hali na mazingira ya aina hii. Ingawa watu wengi kabisa wamefanya wajibu wao kwa miaka mingi na kwa nje wamekuwa watiifu na wenye mwenendo mzuri kiasi, je, hili linamaanisha hawana tena tabia potovu? (Hapana.) Mwenendo wao si mpotovu tena, kwa nje wana mwenendo mzuri, na wanaonekana kuwa na kiasi fulani cha ya adabu mtakatifu, lakini tabia zao potovu hazijabadilika hata kidogo kwa sababu hawautafuti ukweli kikamilifu ili kutatua tabia zao wenyewe potovu. Matatizo yanapotokea katika kazi yao, iwe wanapogolewa na viongozi au Aliye juu, wanachofikiri kabisa ni, "Sawa, wakiniambia nirekebishe jambo hilo, nitalirekebisha. Nitavumilia tu dhiki kidogo zaidi, nitatumia muda kidogo zaidi, na nitaharakisha kulifanya upya." Wana tu mtazamo na fikira za aina hii. Hizi haziwakilishi utii kwa ukweli, na haziwakilishi utii wa kweli. Fikira hizi zinatoka wapi? Zinatokana na ukweli kwamba, katika imani yao katika Mungu, watu wana hamu chanya, wakitamani kuwa watu wema, wakitamani kuwa viumbe walioumbwa wanaofikia kiwango kinachostahili. Tamaa hii huleta fikira za aina hii katika maisha ya kila siku ya watu na katika utekelezaji wa wajibu wao; kwa maneno ya kibinadamu, ni: "Usisababishe shida, hebu sote tuwe na mwenendo mzuri." "Kuwa na mwenendo mzuri" kunarejelea nini? Je, hii ni kanuni ya ukweli? Hili linakufanya tu utii, ufuate sheria, na usisababishe shida. Hili ndilo hitaji la chini kabisa kwa watu, na halifikii kiwango cha kuwa kanuni ya ukweli. Basi kanuni ya ukweli ni nini? Ni kwamba lazima utafute nia ya Mungu kikamilifu. Unapofunua tabia potovu, unapokuwa na matamanio ya ubinafsi au unapofunua kushika moto, tabia potovu zinaposababisha hali fulani kuibuka ndani yako, lazima ulinganishe madhihirisho haya na maneno ya Mungu kikamilifu. Kwa nuru na mwongozo wa Mungu, na kwa msaada na utegemezo wa Mungu, na hata hukumu kali na kuadibu kwa maneno ya Mungu, hatua kwa hatua, unabadilisha mtazamo wako kuelekea maneno ya Mungu, kiwango chako cha kuyakubali maneno ya Mungu kinazidi kuwa cha juu zaidi na zaidi, na unazidi kuyakiri na kusema Amina kwa maneno ya Mungu. Kisha unayakubali maneno ya Mungu ndani yako, unaachilia fikira na mitazamo potofu, na hushikilii tena urithi wa mwanadamu; unaweza kuukubali ukweli, na unaweza kushughulikia watu, matukio, na vitu vilivyo karibu na wewe, na kubadilisha mtazamo, msimamo, na maoni yako kuelekea watu, matukio, na vitu, kulingana na maneno ya Mungu na kanuni za ukweli. Hii ndiyo njia ya kutatua tabia zako potovu. Basi je, sasa mna utendaji wa aina hii wa kuchukua hatua wenyewe? Ninafikiri kwamba asilimia tisini na tisa ya watu hawana. Makala za ushuhuda wa upitiaji za watu wengi kabisa zinahusu kupitia mazingira yaliyowalazimisha kutenda kwa njia fulani na kufikia "utii kwa Mungu" katika matendo yao. Wanahisi kuridhika sana na nafsi zao, wakifikiri kwamba wana uhalisi wa ukweli. Ingawa uliandika makala ya ushuhuda, kwa kweli inahusu kujisifu, kujishuhudia, na kujiimarisha: "Tazama, nina ushuhuda. Sikumwangusha Mungu. Nilishikilia wajibu wangu katika mazingira haya!" Makala za ushuhuda wa upitiaji za baadhi ya watu wengine zinahusu jinsi, baada ya kupogolewa, wanavyotafakari na wanavyofikia utambuzi, wakitambua kwamba walikuwa wa kijuujuu tu na hawakumridhisha Mungu, na sasa wako tayari kutubu. Hata ingawa kuna kipindi cha kuonyesha toba, ambapo inaonekana hawafanyi tena mambo kwa kijuujuu tu, je, tabia zao potovu zimebadilika? Hapana. Kwa siri, bado ni wenye kiburi sana na bado wanajiona kuwa bora kuliko wengine. Msimamo, mtazamo, na maoni ambayo wanatumia kutazama na kushughulikia watu na vitu hayalingani na maneno ya Mungu hata kidogo. Kwa hivyo tabia zao potovu hazijaanza kubadilika hata kidogo! Basi, mabadiliko unayozungumzia ni yapi? Ni mabadiliko tu katika mwenendo, mtindo wa maisha, na pengine sauti, namna ya kujieleza, na mtindo ambao unatumia unapotangamana na wengine na unapoyashughulikia mambo. Imani yako pia imeimarika; unaweza kuutafuta ukweli baada ya kupitia matukio mengi ya kupogolewa katika mazingira mbalimbali, na sasa unaelewa ukweli mwingi, na azimio lako la kumfuata Mungu ni thabiti zaidi kuliko awali—vipengele hivi vyote vimebadilika. Mabadiliko haya huwafanya watu wawe na ujasiri zaidi katika kupata wokovu, wawe tayari zaidi kuufuatilia ukweli, na wawe na matumaini na matarajio mema zaidi kuhusu kumfuata Mungu. Majaribu au dhiki zozote zile zinazowajia, hawatakuwa hasi sana kiasi cha kuacha imani yao. Hata hivyo, haya ni mabadiliko tu katika yale yanayoishiwa kwa kudhihirisha kwa nje katika ubinadamu wa kawaida. Fikira na mitazamo hii chanya na yenye jitihada hatua kwa hatua huchukua nafasi mioyoni mwa watu. Mabadiliko haya ni ishara kwamba mioyo yao inaamshwa na inahuishwa. Yaani, watu wanakuwa wenye bidii na matamanio zaidi, na wanatamani zaidi mambo chanya, wakizidi kuwa na ujasiri katika kufuatilia maneno ya Mungu, kazi Yake, na matakwa Yake. Kiasili, pia wana dhana iliyo wazi zaidi kuhusu kazi muhimu kabisa anayofanya Mungu—kazi ya kuwaokoa watu. Kulingana na hali hizi, watu wengi hufanya wajibu wao kwa njia ya uhalisi zaidi, kwa namna ya kufuata sheria zaidi, na ya utiifu zaidi kuliko awali. Ufanisi wa wajibu wao unaboreka, hasa katika kazi ya kiufundi, ambayo inaendelea kwa kasi zaidi sasa. Wao si wazito kama walivyokuwa awali, wakati kazi ambazo zilipaswa kuchukua siku chache zingechukua wiki moja au zaidi—sasa kuna matokeo katika siku chache tu. Bila shaka, hizi ni habari njema. Lakini habari mbaya ni zipi? Ni kwamba kile mnachofunua na mnachoonyesha ni mabadiliko tu katika mwenendo, wazo, na fikira, na baadhi ya ishara za vipengele chanya, vya bidii, na vya matumaini kiasi katika katika akili zenu za ndani vinavyoamshwa. Hata hivyo, ishara hizi hazimaanishi kwamba tabia zenu potovu zimeanza kubadilika. Habari hizi si nzuri sana, sivyo? (Hapana, si nzuri.) Ingawa si nzuri sana, huu ni mchakato usioepukika kwa binadamu wapotovu kufikia wokovu. Watu ni wa kusikitisha na maskini hivi, hawajakomaa hivi, na kasi ya uingiaji wao katika uzima na kuvua tabia potovu ni ya polepole hivi. Sababu ya kimsingi ya kasi hii ya polepole ni kwamba binadamu kama hao wanakosa uwezo wa kuukubali ukweli, na kwamba wao ni wazito hivi kuitikia ukweli, mambo chanya, na chochote kinachotoka kwa Mungu.

Baadhi ya watu wamemwamini Mungu kwa zaidi ya miaka kumi, ishirini, au thelathini, lakini ni sasa tu ndipo wanatambua kwamba baada ya miaka hii yote, wamebadilika tu kiasi katika mienendo yao ya nje na wamepitia mwamko mdogo mioyoni mwao, lakini hakujawa na mabadiliko ya kimsingi katika tabia zao potovu. Baadhi, wakiona mabadiliko fulani ya mienendo ndani yao, hufikiri kwamba haya ni mabadiliko katika tabia ya uzima na hata kujisifu kwa wengine, "Tazama, je, tabia yangu ya uzima haijabadilika?" Kwa kweli, umebadilika tu katika mwenendo; huna madhihirisho halisi ya mabadiliko ya tabia na hujaishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Basi, mtu anawezaje kujua ikiwa kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako? Huku si kusoma nyuso za watu; mtu hawezi kujua kwa kutazama mwonekano wako wa nje, wala kwa kusikiliza kile unachosema, sembuse kwa kukusikiliza ukieleza maazimio na matamanio yako—maazimio na matamanio ni mambo matupu kabisa. Basi, mtu anawezaje kujua? Mtu anaweza kujua kwa kuangalia ikiwa, bila mtu yeyote kukuhimiza, kukusimamia, au hata kukutegemeza na kukusaidia, una njia na uwezo wa kuchukulia na kushughulikia kila jambo kulingana na maneno ya Mungu, na ikiwa una maneno ya Mungu kama uzima wako ndani ya moyo wako ili yakuzuie katika kila jambo unalofanya. Ikiwa hujafikia kiwango hiki, basi tuzungumze kuhusu kile cha chini zaidi: ikiwa una ufahamu wa kutumia maneno ya Mungu kama kanuni kwa kila jambo unalofanya na unalosema. Ikiwa huwezi kufikia hili, basi kwa bahati mbaya, huna ukweli kama uzima wako. Tabia zako potovu bado ndizo uzima wako; bado zinaweza kukudhibiti wakati wowote, mahali popote, zikitawala ufahamu wako na fikira zako na mitazamo yako. Wakati wowote, mahali popote, utatendea na utashughulikia mtu, tukio, au kitu chochote kulingana na hisia zako, hali yako mwenyewe ya moyo, matakwa yako, hukumu yako, mtazamo wako, na mapendeleo yako mwenyewe. Bado uko katika hatari kubwa; bado huwezi kutimiza wajibu wako kwa kujitegemea, na huwezi kuishi kwa kujitegemea—lazima daima uwategemee wengine, na bila tegemezo la wengine, utaanguka. Hili linamaanisha kwamba kimo chako ni kidogo sana; linathibitisha kwamba hujapata ukweli kama uzima wako. Inamaanisha nini kutopata ukweli kama uzima? Inamaanisha kwamba una kanuni moja au mbili tu zinazokuzuia kufanya mambo mabaya au kufanya makosa makubwa. Yaani, wakati busara yako ni ya kawaida, na hakuna mtu anayekuchochea au anayekushawishi, hakika hutamkufuru Mungu, hutamlaani Mungu, au kuivuruga na kuisumbua kazi ya kanisa kwa makusudi. Hata hivyo, ukweli kwamba hutafanya hivyo kwa makusudi haimaanishi kwamba huwezi kufanya hivyo; huenda usifanye hivyo kwa hiari, lakini bado unaweza kufanya hivyo bila kukusudia. Bila kukusudia kunarejelea nini hapa? Kunamaanisha kwamba tabia zako potovu zinaweza kuibuka wakati wowote ili kukudhibiti na kukufanya useme na ufanye chochote, na zinaweza kukusababisha uchukulie mtu au jambo kwa mitazamo potofu wakati wowote, na kisha utumie tabia zako potovu kushughulikia jambo au kushughulika na mtu wa aina fulani. Kwa mfano, tuseme kwamba umefanya jambo baya na unafikiri kwamba huwezi kumruhusu Aliye juu, viongozi, au mtu mwingine yeyote ajue jambo hilo. Bila kujali sababu ya hili, kwa vyovyote vile, una mawazo yako mwenyewe ya kishetani, kwa hivyo unalificha jambo hilo na husemi chochote. Je, ni tabia zako potovu ndizo zinazotawala hapa, au ni ukweli ndio unaotawala? Ni wazi kwamba, ni tabia zako potovu ndizo zinazotawala. Tabia zako potovu zinakutawala, zikikufanya ulifiche jambo hilo na usiseme chochote, na huwezi kujinasua. Kutoweza kujinasua kunamaanisha nini? Kunamaanisha kwamba ingawa uko tayari kutenda ukweli unaouelewa, unakosa nguvu ya kufanya hivyo; huwezi kabisa kushinda tabia zako potovu. Hili linamaanisha kwamba uko taabani; huwezi kutenda ukweli. Ukitaka kuficha mambo na kuwadanganya wengine, hakika unaweza kutenda vitendo vya maficho na udanganyifu, hasa kwa Aliye juu, ukiripoti habari njema tu lakini si mbaya, hata ukiwadanganya walio juu na ukiwaficha mambo walio chini. Unasema, "Ninaupenda ukweli sana, na mimi ni mtu anayetenda ukweli. Mimi huandika dondoo kwa makini, hutafakari, na hufupisha kila ukweli ambao Mungu ananena, na kisha huufanyia mazoezi katika maisha halisi." Unafikiri hivi, una tamanio hili, lakini halimaanishi kwamba umetenda ukweli. Kwa nini? Kwa sababu una fikira na mitazamo mingi potofu ndani yako ambayo tayari imeutawala moyo wako. Kwa sababu hiyo, tabia potovu zimekuwa uzima wako. Tabia zako potovu ndizo zinazotawala, zikitawala fikira na matendo yako. Hata ikiwa unataka kutenda ukweli, ni bure; unashindwa kabisa kufanya hivyo. Kwa hivyo, ikiwa tabia zako potovu hazitatatuliwa, hata ikiwa unafanya wajibu wako, haiwezekani kwako kuja kutenda kulingana na kanuni—tayari ni vizuri sana ikiwa unaweza kujizuia kuhukumu, kupinga, au kumkufuru Mungu kwa makusudi na kwa wazi. Hata hivyo, huku tabia potovu zikitawala moyoni mwako, huwezi kujizuia kumwasi na kumpinga Mungu. Pengine unafikiri kwamba unajaribu tu kudanganya na kuficha mambo kwa Aliye juu na kumdanganya Mungu katika hali ya kutawaliwa au katika nyakati za kukata tamaa, na kwamba unawakandamiza watu tu au unafunua hali yako ya kushika moto katika nyakati za kukata tamaa. Je, kweli ni kwa sababu ya nyakati za muda za kukata tamaa? Hapana, ni matokeo ya tabia zako potovu zilizokita mizizi zinazotawala. Hili haliepukiki. Kwa nini haliepukiki? Kwa sababu ukweli unaouelewa ni utayari wa aina fulani tu, imani ya aina fulani tu kwako; bado haujakuwa uzima wako. Haijalishi ikiwa una maarifa au ikiwa ubora wako wa tabia ni wa juu au duni, angalau, ukweli haujakuwa uzima wako. Yaani, ukweli hautawali ndani yako; kile kinachotawala ndani yako ni tabia za kishetani na falsafa za Shetani. Unapotawaliwa na tabia za kishetani, unaishi kwa kutegemea tabia za kishetani, na bado unaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Wakati masilahi na kiburi chako havijadhuriwa, wakati hadhi, umaarufu, na faida yako havihusiki, uko tayari kutenda kwa kiasi fulani. Lakini mara tu umaarufu, faida, hadhi, au hatima yako vinapohusika, tabia zako potovu zinakunasa na zinakudhibiti kwa uthabiti na kwa nguvu. Bado huna utii wa kweli kwa Mungu; bado una uwezekano wa asilimia mia moja wa kumsaliti Mungu na ukweli. Kwa kuangalia matukio haya, je, tabia zako potovu zimetatuliwa? Je, zimevuliwa? Je, ukweli umekuwa uzima wako? Jambo linapotokea, ikiwa ukweli unaouelewa hauwezi kushinda tabia zako potovu, hauwezi kushinda chaguzi na matakwa yako, hauwezi kushinda matamanio, tamaa ya makuu, hadhi, na sifa yako, basi ukweli unaouelewa si uzima wako. Ukweli unapokuwa uzima wako, kiasili unaweza kushinda tabia hizi potovu. Ikiwa huwezi kushinda tabia zako potovu, inaonyesha kwamba ukweli bado hautawali ndani yako, na kwamba bado haujakuwa uzima wako. Unasema kwamba unaupenda ukweli, lakini hili ni tamanio na takwa lako tu; haliwakilishi uzima wako. Watu wenye ubinadamu wa kawaida wote wana matamanio chanya. Je, kutamani kuwa mtu mwema kunamaanisha kwamba wewe ni mtu mwema? (Hapana.) Je, kuupenda ukweli, usawa, na haki kunamaanisha kwamba una ukweli, usawa, na haki? Hapana—huna mambo haya, unayatamani tu. Kutamani kunarejelea nini? (Takwa zuri la mtu.) Sahihi, ni takwa tu. Halina uhusiano wowote na jinsi unavyojiendesha kwa kweli, sivyo? (Hapana.)

Je, sasa ninyi mna ukweli kama uzima wenu? (Hapana.) Mtu anawezaje kujua ikiwa una ukweli kama uzima wako? Mtu anaweza kujua kwa kuangalia ikiwa ukweli unaouelewa unaweza kushinda tabia zako potovu wakati masilahi yako yanapokinzana na ukweli, wakati masilahi yako yanapokaribia kupata hasara au kutishiwa. Ikiwa ukweli unaouelewa unaweza kufanya hivyo, basi wewe ni mtu aliye na ukweli kama uzima wako. Ikiwa hauwezi kufanya hivyo, inathibitisha kwamba kimo chako ni kidogo sana. Kidogo kiasi gani? Huna ukweli kama uzima wako. Huu ndio uhalisi. Baadhi ya watu husema, "Ikiwa hatuna ukweli kama uzima wetu, basi kwa nini bado tunaweza kutelekeza kila kitu ili kufanya wajibu wetu katika nyumba ya Mungu? Kwa nini bado tunaweza kuteseka na kulipa gharama kwa ajili ya Mungu?" Baadhi hata husema, "Tayari nina kujitoa kiasi; tayari nimefanywa mshindi." Kwa kweli, kauli kama hizo zimechanganywa na dhana na mawazo ya kufikirika ya watu. Si kosa kwa watu kuwa na maazimio na matamanio makuu. Kutamani kwa watu nuru, haki, na pia kutamani kwao kufuatilia ukweli, kufikia wokovu, na kadhalika—matakwa haya mazuri yanaweza kubadilisha baadhi ya ufahamu wao, mwelekeo wa njia wanayotembea, na bila shaka, baadhi ya mienendo yao, na kwa nje, baadhi ya vipengele vya mwenendo wao na namna yao ya kuishi. Mabadiliko yanarejelea nini hapa? Kwa mfano, tuseme kwamba sasa hivi una imani, hali yako ni nzuri sana, wewe si hasi, na wajibu wako unaendelea vizuri hasa. Kwa sababu hiyo, unahisi kwamba wewe ni mwaminifu hasa, na kwamba una tumaini la kutimiza takwa lako la kufikia wokovu, na uko tayari kuvumilia dhiki yoyote. Lakini nyakati nzuri hazidumu. Katika mchakato wa kufanya wajibu wako, unakumbana na vikwazo na kushindwa fulani, unapogolewa, unapitia njia nyingi za mzunguko, na hata unapotoshwa na unakandamizwa na wapinga Kristo, ukiteseka kwa dhuluma nyingi. Kisha unahisi usumbufu moyoni mwako. Huelewi ukweli, na hujui kwa nini mambo haya yalitokea, kwa hivyo unahisi kufadhaika, na hupati majibu yoyote unapomwomba Mungu. Kwa kiwango kikubwa, kutokea kwa mambo haya kunasababisha pigo na uharibifu fulani juu ya azimio lako la kutamani ukweli na nuru. Baada ya kuteseka na uharibifu huu, hutaki tena kufanya wajibu wako, ukihisi kwamba hakuna maana. Kuna nini kinaendelea hapa? Ulibadilikaje haraka hivyo? Kwa nini wewe ni kama mtu tofauti kabisa na hapo awali? Ikiwa ungekuwa na kimo, na ungekuwa na ukweli kama uzima wako, kujitoa kwako kusingebadilika. Lakini kwa sababu huna ukweli kama uzima wako, hali, fikira, na msukumo wako wa ndani wa kumwamini Mungu na kujitumia daima havina uthabiti na hubadilika-badilika kati ya joto na baridi. Katika vipindi ambavyo kila kitu kinaendelea vizuri na uko katika hali nzuri ya moyo, unakuwa na msukumo, una mengi ya kusema wakati wa maombi, uko tayari kusoma maneno ya Mungu, unajitahidi sana katika wajibu wako, na uko tayari kuwa na shughuli nyingi au kuchoka, na kuvumilia dhiki yoyote. Lakini mara tu mambo yanapokuwa mabaya kidogo, unakuwa hasi na dhaifu, ukipoteza msukumo wa kufanya wajibu wako. Unapokosa mlo mmoja au unapolala kwa muda mfupi kidogo, unahisi kwamba ni dhiki kubwa, na malalamiko yanaibuka moyoni mwako: "Kwa nini niteseke? Sipati hata pesa kwa kufanya wajibu wangu, hailipi!" Tazama, fikira zako ni tofauti kabisa. Kwa nini mabadiliko makubwa kama haya yametokea? Ni kwa sababu huna ukweli kama uzima wako, na tabia zako potovu bado zipo ndani yako. Watu wanapokuwa na shauku, wanahisi kwamba hawana tamaa ya makuu au matamanio, au matakwa kwa Mungu. Kwa kweli, tabia zao potovu bado ndizo zinazotawala ndani yao; mambo haya yanabaki bila kubadilika. Watu wanapokuwa chanya, wanakuwa na shauku sana na msukumo wa pekee, na hakuna anayeweza kuwazuia. Wanapokuwa hasi, wanakuwa kama madimbwi ya tope, wasioweza kuvutwa juu na yeyote. Daima huwa na misimamo mikali, na hawana uthabiti kabisa. Hili linaonyesha kwamba wanakosa kitu fulani katika ubinadamu wao wa kawaida. Wanakosa kitu gani? Wanakosa ukweli kama uzima wao—hivyo ndivyo ilivyo. Hali yako inabadilika-badilika kati ya joto na baridi, hasi wakati mmoja na chanya wakati unaofuata. Ni kitu gani kinasababisha hili? Ni tabia zako potovu zinazosababisha shida. Leo zinakufanya ufikirie jambo moja, kesho jambo jingine; kwa vyovyote vile, fikira hizi daima zinaendana na matakwa yako, kuwa kwako mwenye kushika moto, na hali yako ya sasa, hali yako ya sasa ya moyo, na hisia zako za sasa. Lakini ni tofauti wakati watu wana ukweli ndani yao. Ikiwa ukweli unakuwa uzima wako, daima utakuwezesha kuwa na ufafanuzi sahihi na wa kweli wa kile unachofanya, na hili halitabadilika kamwe. Hutabadilika-badilika kati ya joto na baridi, na hutakuwa hasi na hutakwama katika hali ya kushuka moyo kwa sababu ya kushindwa na kuanguka mara moja, au kwa sababu ya upogoaji kidogo au kikwazo kidogo. Wala hutakuwa chanya sana kiasi cha kutenda kama kijana mwenye bidii, ukikesha kwa siku tatu mchana na usiku. Badala yake, utakuwa na busara ya kawaida. Sivyo? (Ndivyo.) Mara tu watu wanapoelewa ukweli na ukweli unakuwa uzima wao, wanakuwa wazi kuhusu maono. Wanajua kwa nini wanahitaji kumfuata Mungu, kwa nini wanahitaji kufanya wajibu wao, ni matokeo gani ambayo wanapaswa kufikia katika utekelezaji wa wajibu wao, na kusudi, umuhimu, na thamani ya kuvumilia dhiki hizi. Wanaelewa kanuni hizi zote za ukweli kikamilifu mioyoni mwao, bila mkanganyiko au ukungu. Na hivyo, wanateseka kwa hiari na bila malalamiko, wana sheria na kanuni katika kila kitu wanachofanya, na hawapotezi kamwe imani katika Mungu; wanapohisi hasi, hawamlalamikii Mungu wala hawamwachii Yeye, na wanapohisi chanya, hawana matakwa ya ziada kwa Mungu, na hali yao ni ya kawaida sana. Je, ninyi mko hivi sasa? (Hapana.) Basi nini kifanyike? (Kuanzia sasa na kuendelea, tunapaswa kuzingatia kuufuatilia ukweli ili kutatua tabia zetu potovu; hakuna njia nyingine.) Hakuna njia nyingine isipokuwa kuufuatilia ukweli. Acha Nikuambie: Usipoufuatilia ukweli, na tabia potovu daima zinabaki kutawala kama uzima wako, basi hutakuwa na hatima njema; mwishowe, utaishia kuwa mtendaji huduma. Lakini ukiufuatilia ukweli, tumaini lako la kufikia wokovu litakuwa kubwa, na baraka utakazopokea mwishowe pia zitakuwa kubwa. Ukiufuatilia ukweli, utakuwa huru kutokana na utumwa wa tabia potovu, tabia potovu hazitakuwa tena uzima wako, na kwa sababu hiyo utaona kweli tumaini la kufikia wokovu. Usipoufuatilia ukweli, na tabia zako potovu zinabaki bila kutatuliwa, na unataka kutegemea tu kujizuia na nguvu ya utashi kufanya mambo mema na kutotenda maovu, basi ni vigumu kusema ikiwa unaweza hata kufika mwisho wa njia. Mmeelewa? (Tumeelewa.) Ni tatizo gani kubwa kabisa ambalo watu wanahitaji kutatua katika kumwamini Mungu? (Tabia potovu.) Kutatua tabia potovu ndilo jambo muhimu kabisa. Usifikiri, "Sasa ninafanya wajibu wakati wote katika nyumba ya Mungu, nikijitumia wakati wote, kwa hivyo mimi ni mshindi!" Mungu ananena kuhusu kufanya kundi la washindi—washindi inamaanisha nini? “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo.” (Ufunuo 14:4). Hawa ndio washindi katika maana rahisi ya neno hili. Mtu hawezi kuridhika kwa kuwa mshindi tu. Kuwa mshindi katika maana hii rahisi hakumaanishi kwamba tabia potovu za mtu zimevuliwa, na hakumaanishi kwamba mtu ana ukweli kama uzima wako. Wale ambao mwishowe wanaokolewa si washindi tu—jambo hili si rahisi hivyo. Washindi ni wale tu wanaoshinda dunia isiyoamini, Shetani, mienendo mibovu, na tawala mbovu—hivi ndivyo washindi walivyo. Ikiwa unaelewa tu baadhi ya kanuni za ukweli, na unaweza kwa muda kushinda mwili na hisia, au hubanwi na uvumi mbalimbali usio na msingi, au husumbuliwi na watu waovu au wasioamini, jambo hili bado halifikii kikamilifu kiwango cha mshindi. Kuwa na uzoefu huu mchache na mdogo tu hakuna thamani kubwa. Ni kitu gani chenye thamani? Kuwa na ukweli kama uzima wa mtu ndilo jambo lenye thamani kabisa. Mtu anawezaje kufanya ukweli kuwa uzima wake? Kuna njia moja tu: Lazima usome maneno ya Mungu zaidi, na utende na upitie maneno ya Mungu zaidi. Ni kwa namna hii tu ndipo unaweza kupata ukweli kutoka katika maneno ya Mungu na kuja kuwa na ukweli kama uzima wako. Ukitumia ukweli kuongoza maisha yako yote, maisha yako ya kila siku, na kanuni ambazo kwazo unatenda na unajiendesha—ukitenda kwa namna hii—utakuwa na uhalisi wa ukweli. Unapokuwa na uhalisi wa ukweli, tabia zako za zamani za kishetani zitawekwa kando. Kabla ya kuamua jinsi ya kutenda, kwanza tafakari, "Kile ninachofikiri hakiwakilishi kanuni za ukweli. Lazima nione kile ambacho maneno ya Mungu yanasema." Ukitafakari kwa namna hii kila wakati, na ukizungumza na ukitenda kulingana na maneno ya Mungu kila wakati, je, ukweli hautakuja kuingia katika uzima wako kidogo kidogo? Haba na haba hujaza kibaba. Uruhusu ukweli uingie moyoni mwako kidogo kidogo ili kubadilisha maisha yako ya kila siku, kubadilisha mitazamo yako, kubadilisha hali yako ya sasa ya kuwepo, na kubadilisha hali yako. Kadiri hali yako inavyobadilika hatua kwa hatua na inavyokuwa katika mwelekeo mzuri, ndivyo uwezekano wa wewe kutenda maovu na kusababisha vurugu na usumbufu utakavyoendelea kupungua, madhihirisho ya wewe kujionyesha yataendelea kupungua, huku shuhuda zako za kutenda kulingana na kanuni za ukweli zikiendelea kuongezeka. Mambo muhimu kuhusu mema na mabaya yanapoibuka, kanuni za ukweli zinashinda tabia zako potovu za kishetani, na matakwa, mapendeleo, na mipango yako binafsi. Ni hapo tu ndipo utakuwa mshindi wa kweli, mtu aliye na ukweli kama uzima wake, na mtu anayeweza kufikia wokovu. Vinginevyo, ikiwa unatenda tu kulingana na mapendeleo yako, ukifikiri, "Kutenda kwa namna hii ni vizuri, ninafanya mambo haya kwa furaha na kwa hiari na sina malalamiko," jambo hilo lina manufaa gani? Huna malalamiko, lakini kanuni za utendaji wako ni zipi? Utendaji wako unatokana kabisa na mapendeleo ya tabia zako potovu, unatokana na fikira na mitazamo vipotofu, unatokana na nia za ubinafsi, unatokana na tamaa ya makuu na matamanio, unatokana na hisia, na unatokana na kuwa mwenye kushika moto—unaongozwa kabisa na tabia zako potovu. Haya ndiyo maisha yanayofunua tabia potovu, si maisha yanayofunua ukweli. Mungu si tu kwamba hayakumbuki, bali pia Atayahukumu. Lazima ujaribu kila uwezalo ili kuhakikisha kwamba kile unachoishi kwa kudhihirisha, maneno unayozungumza na mambo unayofanya, na fikira na mitazamo unayofunua vyote vinalingana na ukweli; ili kuhakikisha kwamba fikira na mitazamo hiyo potofu inayozalishwa na tabia potovu inazidi kupungua moyoni mwako; na ili kuhakikisha kwamba kile unachofikiri moyoni mwako na mitazamo yako kuhusu mambo vyote vinahusiana na ukweli, na vyote vinalingana na ukweli. Lazima ufuatilie na ulenge kipengele hiki, na kisha kutakuwa na mabadiliko zaidi na zaidi ndani yako, na hali yako itazidi kuwa nzuri. Siku hizi, watu wengi wanaweza kuzungumza maneno na mafundisho, wakiyafafanua kwa uwazi na kwa mantiki, lakini inapokuja suala la kuzungumza kuhusu uhalisi wa ukweli, hawana la kusema, na hawawezi kueleza hata ufahamu kidogo wa vitendo. Kuna nini kinaendelea hapa? (Hatuna ukweli.) Maisha yako bado ni maisha ya tabia potovu, maisha ya Shetani, na si maisha ya ukweli.

Mmeelewa kile ambacho tumeshiriki hivi punde? Ikiwa ninyi mnatambua kweli kwamba tabia zenu potovu hazijavuliwa bado na kwamba bado mnaishi kwa kutegemea tabia potovu, je, mtakuwa hasi? (Hivi punde, nilipomsikia Mungu akisema kwamba tabia zetu potovu hazijabadilika, nilihisi kukatishwa tamaa sana moyoni mwangu, nikifikiri kwamba nimekuwa nikila na nikinywa maneno ya Mungu kila mara miaka hii yote, na nimelenga kutenda ukweli katika hali fulani—kwa hivyo imekuwaje kwamba tabia zangu potovu bado hazijabadilika? Nilihisi kukatishwa tamaa kidogo na kuwa hasi. Lakini kupitia Mungu kutoa mwongozo na kufanya ushirika kidogo kidogo, nilielewa kwamba ninaonyesha tu baadhi ya mienendo mizuri ya nje, lakini tabia zangu potovu bado zinatawala ndani yangu; kwa kweli hakujawa na mabadiliko yoyote. Mungu alisema kwamba wanapofanya mambo, watu lazima kwanza watafakari, na kwamba haijalishi mawazo yao ni mazuri kiasi gani, hayawakilishi kanuni za ukweli, na kwamba lazima waone kile ambacho ukweli katika maneno ya Mungu unasema, na wajifunze kuutafuta ukweli na kutenda kulingana na maneno ya Mungu kila wakati wanapofanya jambo, na ndipo hali yao itabadilika polepole. Baada ya kusikiliza ushirika wa Mungu, nilionekana kuona tumaini tena, na nilihisi kwamba kuna njia, na sikuwa tena hasi.) Kuwa hasi ni kosa; hupaswi kuwa hasi chini ya hali yoyote. Kuvua tabia potovu ni jambo kuu la kufikia wokovu. Kadiri jambo fulani linavyokuwa tabia potovu, ndivyo lazima ulenge zaidi kulitatua. Lazima ujitahidi kwa uwezo wako wote na uelekeze umakini wako wote katika jambo hilo. Huwezi kuwa hasi, wala huwezi kukata tamaa. Ingawa ninyi sasa mnaanza kulenga kuufuatilia ukweli, wakati mwingine bado hamjui jinsi ya kutenda. Kunena nanyi sasa kuhusu njia ya utendaji kuna manufaa zaidi kwa kuingia kwenu katika uzima, na wakati huo huo, kunaweza kusababisha hisia ya hatari kuibuka ndani yenu, na kuwawezesha kulenga ukweli, na kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo. Msijiridhishe, na msiridhike na hali yenu ya sasa. Ninyi mmekuwa watiifu na wenye mwenendo mzuri tu, na mna busara kidogo zaidi kuliko hapo awali, lakini bado mko mbali na kuvua tabia zenu potovu! Ukweli uko wazi kuonekana, kwa hivyo kuna manufaa gani katika kuwa hasi? Kuwa hasi hakuwezi kutatua matatizo halisi. Mnapaswa kutafuta chanzo cha tatizo kiko wapi na kuanza kujaribu kulitatua kuanzia hapo. Bado hamjachelewa kuanza sasa. Ni lini itakuwa imechelewa sana? Itakuwa imechelewa sana wakati kazi ya Mungu itakapokwisha. Je, ninyi mna azimio la kuingia katika uhalisi wa ukweli na kuja kuupata ukweli kama uzima wenu? (Sasa tuna azimio hili.) Kwa kweli, kuingia katika uhalisi wa ukweli si jambo gumu. Fikirieni kuhusu jambo hilo, maneno mengi ya ushirika kuhusu ukweli yamenenwa, na ni ya kina sana na mahususi. Inaonekana kwamba kuna maudhui mengi, lakini kanuni hazibadiliki, na njia ya utendaji haibadiliki. Unapofunua tabia potovu, tambua kwa makusudi wazo au fikira hiyo, na utafakari moyoni mwako, "Hii ndiyo tabia potovu, kwa hivyo ninapaswa kuitatuaje? Sijawahi kuitatuwa hapo awali. Nimemwamini Mungu kwa miaka mingi sana, lakini nimelenga tu matendo ya nje na kujionyesha, na sijawahi kutafakari juu ya ukweli kwamba bado nina tabia potovu. Leo nimegundua ghafla kwamba nina fikira kama hiyo ndani yangu. Fikira hii ilitoka wapi? Ilitokana na tabia potovu. Basi tabia hii potovu inapaswa kutatuliwaje?" Mwombe Mungu na utafute ukweli, na pia uwaulize watu walio karibu na wewe ambao wamekuwa na uzoefu; watakuongoza kuutafuta ukweli na kutatua tatizo. Wakati kila mtu yuko pamoja, lazima mtegemezane na msaidiane, na muwe wenye kuelewana. Kimo cha kila mtu ni sawa, na hakuna anayepaswa kumstahi au kumdharau mtu mwingine yeyote. Ikiwa kila mtu anasaidia na anategemeza mwingine hivi, na kimo cha kila mtu kinakua hatua kwa hatua, na mwishowe, nyote mnafikia wokovu na mnaingia katika ufalme pamoja, je, hilo lisingekuwa zuri? (Ndiyo.) Sawa, tuhitimishe ushirika wetu hapa kwa leo. Kwaheri!

Tarehe 9 Septemba 2023

Inayofuata: 

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp