24. Hatimaye, Nimejifunza Jinsi ya Kutimiza Wajibu Wangu

Na Xincheng, Italia

Mwenyezi Mungu anasema, “Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu(Neno Laonekana katika Mwili). “Kufanya wajibu wako kwa shauku na kuweza kuaminika kunakuhitaji uteseke na ulipe gharama—kuzungumza tu juu yake hakutoshi. Usipofanya wajibu wako kwa shauku na badala yake, utake kila wakati kutumia nguvu za kimwili, basi bila shaka wajibu wako hautafanyika vizuri. Utaufanya tu kwa njia isiyo ya dhati na hutajua umefanya wajibu wako vizuri jinsi gani. Ukiufanya kwa shauku, utapata kuelewa ukweli polepole; usipofanya hivyo basi hutaelewa. Unapofanya wajibu wako na kufuatilia ukweli kwa shauku, utaweza kuelewa mapenzi ya Mungu polepole, kugundua upotovu wako na kasoro zako, na kujua hali zako mbalimbali. Usipotumia moyo wako kujichunguza bali uzingatie tu kutia juhudi za nje, basi hutaweza kugundua hali mbalimbali zinazotokea moyoni mwako na jinsi unavyoathiriwa na mazingira mbalimbali ya nje; usipotumia moyo wako kujichunguza, basi itakuwa vigumu kwako kutatua matatizo yaliyomo moyoni mwako(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kutoka katika maneno ya Mungu tunaweza kuona kwamba lazima tuwe waangalifu, waaminifu na tutafute ukweli ili tutimize wajibu wetu. Nilikuwa mzembe hapo zamani. Sikujitahidi sana katika lolote. Nilikuwa vivyo hivyo katika nyumba ya Mungu. Sikuwa nikifanya kazi kwa bidii sana. Kila nilipokabiliwa na jambo gumu lililohitaji bidii, nilikuwa mzembe na sikuaminika kwa hivyo nilikuwa nikifanya makosa kila wakati katika wajibu wangu. Baadaye, nilikuja kuelewa kidogo kuhusu tabia yangu mwenyewe potovu kutoka katika maneno ya Mungu na jinsi ya kutimiza wajibu wangu ili kuridhisha mapenzi ya Mungu, kisha nikaweza kutekeleza wajibu wangu kwa uaminifu na kwa uthabiti.

Wajibu wangu wakati huo ulikuwa kukagua tafsiri za Kiitaliano. Nilikuwa mwenye bidii mwanzoni na nilikuwa tayari kutatua matatizo yoyote yaliyotokea. Lakini muda ulipozidi kupita, nilikabiliwa na limbikizo la hati na nikaanza kuwa na wasiwasi kidogo, hasa nilipoona hati zilizokuwa na mihtasari iliyoandikwa kwa kila aina ya rangi na vituo vikuu, koma na alama nyingine nyingi za uandishi. Kila hati ilibidi ikaguliwe kwa ajili ya muundo na upangaji. Nilianza kuwa na wahaka. Niliwaza, “Je, nitalazimika kufikiria hili kwa kiasi gani? Hili linahitaji juhudi nyingi mno.” Kisha sikutaka kuzikagua kwa uangalifu tena, bali nilizikagua tu na kuhakikisha kwamba zilikuwa sahihi kwa kadiri. Wakati mwingine nilihitaji kutuliza mawazo yangu na kufikiria iwapo tafsiri hiyo ilikuwa sahihi, lakini nilipoona sentensi iliyokuwa na muundo changamano, nilifanya hesabu hizi za ubinafsi: “Kufikiria na kutafiti kila neno kunahitaji juhudi nyingi sana, na nisipofanikisha lolote, je, huko hakutakuwa kupoteza nguvu? Haidhuru, mtu mwingine ataishughulikia.” Na kwa njia hiyo tu, nilikuwa nikifanya wajibu wangu kwa namna isiyo ya dhati.

Baada ya muda, matatizo ya kawaida yalianza kutokea. Watu wengine walikuwa wakigundua makosa kadhaa ya kuandika kwa herufi kubwa na alama za uandishi katika hati nilizokuwa nimekagua na kulikuwa na maneno ambayo hayakutafsiriwa katika hati nyingine. Nilihisi vibaya sana nilipoona hayo. Mtu mwingine aliyaona matatizo hayo madogo mara moja lakini sikuwa nimeyaona yalipokuwa mbele yangu. Na kuliwezaje kuwa na makosa kama hayo ya wazi? Nilihisi vibaya zaidi nilipofikiria hilo. Siku moja baada ya chakula cha mchana nilipokea ujumbe uliosema kwamba kulikuwa na kosa la kimsingi sana la umoja na wingi katika hati ambayo nilikuwa nimekagua. Nilihisi kama kwamba kisu kiliuchoma moyo wangu. Nilikuwaje mzembe hivyo? Niliwezaje kupuuza kosa kama hilo la msingi? Sikuwa na hakika iwapo hati nyingine ambazo nilikuwa nimekagua zilikuwa na makosa kama hayo au la. Kazi yangu ilijaa makosa. Nilipaswa kufanya nini? Katika mateso yangu, nilikuja mbele za Mungu upesi na kuomba. Nilitafakari juu ya hali yangu na mtazamo wangu kwa wajibu wangu hivi karibuni.

Nilisoma kifungu fulani cha maneno ya Mungu: “Hata hivyo, usipouweka moyo wako katika wajibu wako na uwe holela, ukifanya tu vitu kwa njia rahisi zaidi uwezavyo, basi hii ni akili ya aina gani? Ni ile ya kufanya mambo kwa njia isiyo ya dhati tu, bila uaminifu kwa wajibu wako, bila hisia ya uwajibikaji, na bila hisia ya misheni. Kila unapofanya wajibu wako, unatumia tu nusu ya nguvu yako; unaufanya shingo upande, hufanyi kwa dhati, na unajaribu tu kuumaliza tu, bila kuwa mwangalifu hata kidogo. Unaufanya kwa njia ya utulivu sana kama kwamba unachezacheza tu. Je, hili halitasababisha shida? Hatimaye, watu watasema kwamba wewe ni mtu anayefanya wajibu wake vibaya, na kwamba unafanya tu kwa njia isiyo ya dhati. Na Mungu atasema nini kuhusu hili? Atasema kuwa hauaminiki. Ikiwa umeaminiwa na kazi na, iwe ni kazi ya jukumu la msingi au ya jukumu la kawaida, usipoifanya kwa dhati au ukose kutimiza jukumu lako, na ikiwa huioni kama misheni ambayo Mungu amekupa au jambo ambalo Mungu amekuaminia, au ulichukue kama wajibu na jukumu lako mwenyewe, basi hili litakuwa tatizo. ‘Huaminiki’—neno hili litafafanua jinsi unavyofanya wajibu wako, na Mungu atasema kwamba tabia yako haijafikia kiwango. Jambo likiaminiwa kwako, ilhali huu ndio mtazamo unaochukua katika jambo hilo na hivi ndivyo unavyolishughulikia, basi utapewa agizo la wajibu wowote zaidi katika siku zijazo? Je, unaweza kuaminiwa na kitu chochote muhimu? Pengine unaweza kuaminiwa nao, lakini itategemea jinsi ulivyotenda. Ndani kabisa, hata hivyo, Mungu daima Atakuwa na kutokuamini wewe, na vile vile kutoridhika. Hili litakuwa tatizo, sivyo?(“Ni Kupitia Kutafakari Mara kwa Mara Juu ya Ukweli Tu Ndipo Unaweza Kuwa na Suluhisho” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Mungu huchunguza mioyo ya wanadamu. Kila neno Lake lililenga kasoro yangu mbaya. Kisha nikagundua kwamba kufanya mambo kwa njia rahisi katika wajibu wetu ni mtazamo wa uzembe. Hakuna uangalifu katika hili, ni kupuuza tu mambo na kutowajibika hata kidogo. Ninapokumbuka utendaji wangu, kila wakati jambo lilipohitaji muda na juhudi, nilitumia njia ya mkato ya haraka zaidi na ambayo haikuhitaji juhudi nyingi kulimaliza. Nilifanya lolote lililokuwa rahisi zaidi, lililoniepusha na taabu zaidi au ambalo halikuchosha sana. Kulipokuwa na maneno mengi mapya au vipengele vigumu vya sarufi au miundo migumu ya sentensi, sikujitahidi sana kuvitafiti. Nilitumia njia rahisi ya kuvitia alama na kuuliza mtu mwingine. Nilipoona mihtasari changamani au nilipohitaji kukagua kwa uangalifu alama za uandishi, niliangalia tu kwa haraka na kisha sikutilia maanani matatizo mengine. Nilikuwa mzembe na nilikwepa jukumu langu katika wajibu wangu na agizo la Mungu. Nilifikiri tu juu ya kuepuka mateso ya mwili. Je, kulikuwa na nafasi hata ndogo ya Mungu moyoni mwangu?

Baadaye nilisoma maneno mengine zaidi ya Mungu ambayo yalisema: “Kwa watu walio na ubinadamu, kutekeleza wajibu wao vizuri kwa namna ile ile wakati ambapo hakuna anayeangalia kunapaswa kuwa rahisi; jambo hili linapaswa kujumuishwa katika mgawo wao wa majukumu. Kwa wale wasio na ubinadamu na ambao hawawezi kutegemewa, kutekeleza wajibu wao ni mchakato unaoelemea. Wengine lazima wawaonee wasiwasi, wawasimamie na kuulizia maendeleo yao kila wakati; vinginevyo, watasababisha madhara kila utakapowapa kazi ya kufanya. Kwa kifupi, watu wanahitaji kila mara kujitafakari wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao: ‘Je, nimetimiza wajibu huu kiasi cha kutosha? Je, niliufanya kwa shauku? Au niliumaliza tu kwa kubahatisha?’ Yoyote kati ya mambo hayo yakitokea, basi si vyema; ni hatari. Kwa kifupi, inamaanisha kwamba mtu kama huyo si wa kuaminika na watu hawawezi kumwamini. Kwa upana, iwapo mtu kama huyo hufanya tu wajibu wake kwa namna isiyo ya dhati kila mara, na akiendelea kuwa mzembe kwa Mungu, basi yeye yuko katika hatari kubwa! Je, matokeo ya kuwa mdanganyifu kwa makusudi ni yapi? Kwa muda mfupi, utakuwa na tabia potovu, utafanya dhambi za mara kwa mara bila kutubu na hutajifunza jinsi ya kutenda ukweli wala hutautia katika vitendo. Kwa muda mrefu, unapofanya mambo hayo siku zote, matokeo yako yatatoweka; jambo hili litakuingiza matatani. Hali hii inajulikana kama kutofanya makosa makubwa bali kufanya makosa madogo siku zote. Mwishowe jambo hili litakusababishia athari zisizorekebishika. Hilo litakuwa jambo baya sana!(“Uingiaji Katika Uzima Lazima Uanze na Uzoefu wa Kutenda Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilipoona Mungu akifichua asili na athari za uzembe wangu mbele yangu, sikuweza kujizuia kuogopa. Kufanya wajibu wetu kwa namna isiyo ya dhati ni kumdanganya Mungu na kuwadanganya wengine. Mtazamo huu hushutumiwa na Mungu. Nisingetubu, siku moja ningefanya kosa kubwa na kuondolewa. Kanisa lilipofanya mipango ya wajibu wangu, niliahidi kwa dhati kutekeleza wajibu wangu vizuri, lakini nilipohitajika kutia juhudi, nilizingatia tu mwili na niliogopa kuteseka. Nilikagua hati kwa haraka na kwa uzembe kwa hivyo nilikosa kuona hata makosa ya wazi kabisa. Je, huko hakukuwa kudanganya? Mawazo haya yalinijaza majuto, kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu! Sijakuwa mwaminifu katika wajibu wangu, bali nimekuwa nikijaribu kukudanganya. Jambo hili ni chukizo Kwako. Sijakuwa na dhamiri hata kidogo. Mungu, nataka kutubu. Tafadhali niongoze, nipe utashi wa kuvumilia dhiki na uwezo wa kuukana mwili na kutimiza wajibu wangu.”

Baadaye katika kila hati, nilikagua kila neno ambalo halikuwa sahihi kabisa. Niliwauliza washiriki wengine au mtafsiri mtaalamu wakati ambapo sikuwa na hakika hadi nilipoelewa kabisa. Kuhusiana na hati zilizokuwa ngumu na ndefu, sikuthubutu kuzikagua kwa namna isiyo ya dhati na kwa kubahatisha tu, bali nilizingatia kwa uangalifu kila sentensi tena na tena na kwa utondoti, nikijaribu kadiri niwezavyo kuboresha tafsiri. Nilipokuwa nikikamilisha hati, niliorodhesha kila kitu nilichohitaji kukagua na nikajikumbusha kila wakati kwamba kila hatua ilihitaji kuzingatiwa kikamilifu. Nilikagua kila kitu nilipokamilisha na nikafanya liwezekanalo kupunguza idadi ya makosa mwishoni. Baada ya muda fulani, nilikuwa bila shaka nikipata matokeo mazuri zaidi katika wajibu wangu na kiasi changu cha makosa kilipungua pia.

Baadaye, dada mwingine, ambaye alisaidia kusanifisha muundo wa tafsiri zilizokamilika, alijiunga na timu. Aliniuliza mara kwa mara, “Je, alama hii ya uandishi ni sahihi? Je, kuna habari gani kuhusu alama hiyo ya uandishi?” Alipouliza maswali mengi, niliwaza, “Kueleza kila kitu kunataabisha. Fuata tu hati iliyokamilishwa." Kwa hivyo nilimhadaa tu na kusema: “Hii ni hati iliyokamilishwa. Hamna matatizo yoyote ya alama ya uandishi. Alama za uandishi katika Kiitaliano na Kiingereza kimsingi ni sawa. Alama nyingi zinaweza kushughulikiwa kama za Kiingereza, lakini si zote. Lazima uzingatie maana.” Kisha akaniuliza, “Vitabu vyetu vya marejeo vya sasa ni vile ambavyo wataalamu huvitumia. Sielewi sehemu nyingine. Je, tuna hati zozote rahisi zaidi zinazohusu alama za uandishi za Kiitaliano?” Nilisema kwamba hatukuwa nazo bado. Baadaye, nilifikiri kwamba nilipaswa kubuni hati ambayo washiriki wapya wangeitumia, lakini kulikuwa na alama nyingi sana za uandishi. Hiyo ilimaanisha kwamba ningehitaji kuangalia kwa makini vitabu vya marejeo na ingekuwa vigumu sana. Niliahirisha jambo hilo kwa muda. Nilidhani kwamba huo ulikuwa mwisho wa suala hilo, lakini aliposhughulikia alama za uandishi wa Kiitaliano kama wa Kiingereza katika muundo kama nilivyomwambia, alifuta nafasi zote kabla na baada ya vistari virefu kwenye hati ya maneno 150,000. Nilishangaa sana nilipogundua. Katika Kiitaliano, lazima uache nafasi kabla na baada ya kistari kirefu ili kuepuka kuchanganya vistari virefu na vifupi na ni tofauti na Kiingereza. Lakini sikumwambia kuhusu hayo. Hakukuwa na lingine. Ilibidi apitie tena na kurekebisha kila alama. Nilihisi vibaya na nikajuta sana. Nilijichukia na nikawaza, “Kwa nini sikutia tu juhudi kidogo mara ya kwanza ili kutunga hati ya marejeo? Kwa nini nilifikiria mwili na kuogopa sana kutaabika kila wakati? Alilazimika kuipitia tena kwa sababu tu ya uzembe wangu. Ilibidi ithibitishwe tena pia. Hiyo ilihitaji bidii, na jambo kuu ni kwamba ilichelewesha maendeleo yetu ya kazi. Je, huko hakukuwa kuharibu kazi ya nyumba ya Mungu?” Nilijawa na hisia hizo za kuwa na deni, kujilaumu na kujuta tena. Nilitaka tu kujizaba kofi usoni. Kwa nini ninamudu tu kwa kubahatisha tena? Je, nina tatizo gani?

Wakati mmoja katika ibada zangu, nilipata kifungu kimoja cha maneno ya Mungu: “Je, kushughulikia mambo kwa mzaha na pasipo uaminifu si jambo lililo ndani ya tabia potovu? Jambo lipi? Ni uovu; katika masuala yote, wao husema ‘hiyo imekaribia kuwa sawa’ na ‘imekaribia kutosha’; ni mtazamo wa ‘pengine,’ ‘labda,’ na ‘nne kati ya tano’; wao hufanya mambo kwa uzembe, wao huridhishwa na kufanya kazi ya kiwango cha chini zaidi na wanaridhishwa na kubananga mambo kadiri wawezavyo; hawaoni sababu ya kuchukulia mambo kwa makini au kujitahidi kufikia usahihi na hawaoni sababu ya kutafuta kanuni. Je, hili si jambo lililo ndani ya tabia potovu? Je, ni dhihirisho la ubinadamu wa kawaida? Kuliita kiburi ni sahihi, na kuliita upotovu pia kunafaa kabisa—lakini ili kulieleza kikamilifu, neno pekee ambalo litaeleza vizuri ni ‘uovu.’ Uovu kama huu upo katika ubinadamu wa watu wengi sana; katika mambo yote, wao hutaka kujitahidi kwa kiasi kidogo kabisa kadiri iwezekanavyo, ili waone jinsi wanavyoweza kufanikiwa bila kugunduliwa, na kuna kidokezo cha udanganyifu katika kila kitu wanachofanya. Wao huwadanganya wengine wanapoweza, wao hutumia njia za mkato wanapoweza na huchukia kutumia muda mwingi au mawazo kufikiri kuhusu jambo. Almradi waweze kukwepa kufichuliwa, na wasisababishe matatizo yoyote, na wasiitwe wajieleze, wao hufikiri kwamba mambo yote ni mazuri, na hivyo wao husonga mbele kwa kubahatisha. Kwao, kufanya kazi vizuri kunasumbua zaidi kuliko jinsi inavyostahili. Watu kama hawa hawajifunzi lolote hadi wawe stadi na hawatii bidii katika masomo yao. Wao hutaka tu kupata muhtasari wa jumla wa mada fulani na kisha hujiita stadi wa mada hiyo, na kisha wao hutegemea hili kumaliza kazi zao kwa kubahatisha. Je, huu sio mtazamo ambao watu wanao kwa mambo? Je, ni matazamo mzuri? Mtazamo wa aina hii ambao watu kama hao huwa nao kwa watu, matukio na mambo, kwa maneno machache, ni, ‘kumaliza mambo kwa kubahatisha’, na uovu kama huu upo ndani ya wanadamu wote wapotovu(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalionyesha waziwazi chanzo cha ukosefu wangu wa bidii katika wajibu wangu. Uovu wangu ulikuwa mbaya sana. Nilifanya kila kitu kwa mtazamo wa uzembe na udanganyifu. Dada yule aliponiuliza juu ya matumizi sahihi ya alama za uandishi, sikutaka kutaabika. Sikuchukulia suali hilo kwa uzito na sikutaka maswali mengi sana, kwa hivyo nilimdanganya tu kwa kumwambia afuate kanuni rahisi. Na aliponiuliza kuhusu hati ya marejeo, ningeweza kumtungia, lakini nilipofikiri juu ya gharama ya kuteseka kwangu mwenyewe, niliamua kutojisumbua. Nilikuwa na wasiwasi juu ya makosa kutokea, lakini bado niliamua kudanyanga. Ingekuwa vyema iwapo ningetia juhudi na mambo yangekwenda vizuri. Kila nilipofanya mambo bila kutia juhudi, nilikuwa nikitegemea bahati. Nilikuwa nikitegemea kutumia juhudi ndogo kabisa kumudu. Sikuwa nikitia juhudi za kweli katika kutimiza wajibu wangu kwa kuzingatia kila kila kitu na kufanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba hakukuwa na makosa. Ilionekana kana kwamba nilikuwa nikifanya kazi na nilikuwa nikiyajibu maswali, lakini kwa kweli, nilikuwa nikimdanganya tu huyo dada na nilikuwa mjanja. Kama matokeo, aliamini majibu yangu na alifanya makosa makubwa na akijichosha kwa kazi ya bure. Alilazimika kurudia kazi nyingi na kuchelewesha kila kitu, jambo ambalo liliiletea hasara kazi ya kanisa. Kanuni iliyosababisha matendo yangu, kufanya jambo rahisi zaidi na lisilo na taabu zaidi, ilikuwa kanuni ya kuwadhuru watu. Nilikuwa nikitumia ujanja mdogo kutumia juhudi kidogo kwa muda mfupi. Sikuwa nimeteseka kimwili lakini makosa yangu katika wajibu wangu hayakuwa na kikomo na yalivuruga kazi ya nyumba ya Mungu. Nilikuwa nikimdhuru kila mtu. Nilipewa kazi muhimu sana, lakini niliichukulia kwa wepesi na nilikuwa mzembe, asiyewajibika, mdanganyifu na mvivu na nilipuuza athari. Sikuwa na dhamiri hata kidogo. Wakati huo tu ndipo nilipoona jinsi uovu wangu ulivyokuwa mbaya, jinsi uadilifu wangu ulivyokuwa duni na jinsi ambavyo sikuwa na thamani.

Baadaye, nilitazama video ya usomaji wa maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? … Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna nia zenye uovu kunihusu na hamnipendi kwa dhati. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa hata kidogo? Mnawezaje kuchukuliwa kama kiumbe aliyeumbwa? Je, hamjui wazi mnachopaswa kuonyesha nakuishi kwa kudhihirisha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno Yangu na kazi Yangu, kundi lenu litakuwa la kuadhibiwa. Kamwe hamtapata neema, na hamtakuwa na baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu). Maneno ya Mungu yasema, “Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna nia zenye uovu kunihusu na hamnipendi kwa dhati. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee.” Maneno haya yaliuchoma moyo wangu. Mungu alinipa nafasi ya kutekeleza wajibu wangu ili niweze kutafuta na kupata ukweli kupitia wajibu wangu, kuondoa tabia yangu potovu na kuokolewa na Mungu. Lakini badala ya kutafuta ukweli, niliujali tu mwili, nikimlaghai na kumhadaa Mungu. Nilikumbuka jinsi Mungu alivyopata mwili ili Awaokoe wanadamu, Akavumilia fedheha kubwa na maumivu makubwa, Akasakwa na kuteswa na serikali, Akashutumiwa na kukataliwa na watu, lakini Yeye huonyesha ukweli kila wakati na hufanya kazi ya kuwaokoa watu. Ubora wetu wa tabia ni duni kwa hivyo sisi huelewa ukweli polepole. Mbali na Mungu kutotuacha, pia Yeye hufanya ushirika nasi kwa makini kutoka kila pembe. Yeye hueleza ukweli wote kwa utondoti mkuu. Yeye husimulia hadithi, hutoa mifano na hutumia sitiari ili kutusaidia tuelewe. Baadhi ya ukweli una utata na unagusia mambo mengi, kwa hivyo Mungu huuainisha na kutupa muhtasari. Yeye hutuongoza kwa uvumilivu na utaratibu ili tuelewe ukweli kupitia ushirika. Tunaweza kuona kwamba Mungu huwajibikia sana maisha yetu. Lakini hata hivyo, nilichukuliaje wajibu wangu mwenyewe? Nilidhani kwamba kujitahidi sana na kufikiri sana hakukufaa. Sikuwa makini au mwaminifu katika kazi yangu. Nilitumia mbinu rahisi zaidi bila kuangalia matokeo au athari. Nilikuwa nikichukulia agizo la Mungu kwa wepesi, nikilifanya kwa njia rahisi. Dhamiri yangu ilikuwa wapi? Nilistahili adhabu ya Mungu. Lakini Mungu hakuacha kuniokoa. Alitumia maneno Yake kunipa nuru na kuniongoza, kunisaidia nijijue na nielewe mapenzi ya Mungu. Iwapo ningeendelea kuzembea na kufanya wajibu wangu kwa namna isiyo ya dhati, nisingestahili kuishi au kuitwa mwanadamu. Kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu! Uovu wangu ni mbaya sana. Siko tayari kuendelea kuishi kwa njia hii ya aibu na isiyofaa. Tafadhali nipe nguvu ya kutenda ukweli ili niweze kuishi kwa kudhihirisha mfano halisi wa binadamu na kutimiza wajibu wa kiumbe.”

Baadaye, nilisoma maneno ya Mungu: “Kama mwanadamu, ili kukubali agizo la Mungu, lazima mtu ajitolee. Mtu lazima ajitolee kikamilifu kwa Mungu na hapaswi kuwa mtu wa shingo upande, kushindwa kuwajibika, au kutenda kulingana na masilahi yake mwenyewe au mihemko; huku si kujitolea. Kujitolea kunamaanisha nini? Kunamaanisha kwamba unapokuwa ukitimiza wajibu wako, huathiriwi wala kuzuiwa na mihemko, mazingira, watu, mambo au vitu. ‘Nimepokea agizo hili kutoka kwa Mungu; Amenipa. Hili ndilo ninalopaswa kufanya. Kwa hivyo, nitalifanya nikilichukulia kama shughuli yangu mwenyewe, kwa njia yoyote itakayoleta matokeo mazuri na nikitilia maanani kumridhisha Mungu.’ Unapokuwa na hali hii, mbali na kudhibitiwa na dhamiri yako, pia kujitolea kunahusishwa vilevile. Iwapo wewe huridhika tu na kumaliza kulifanya, bila kutamani kuwa na ufanisi na kupata matokeo, na uhisi kwamba kujitahidi kidogo tu kunatosha, basi hiki ni kiwango tu cha dhamiri na huku hakuwezi kuhesabiwa kama kujitolea. Unapojitolea kwa Mungu, kiwango hiki ni cha juu zaidi kidogo kuliko kiwango cha dhamiri. Basi, hili tena si suala la kujitahidi kidogo; lazima pia uwe na shauku kabisa. Lazima kila wakati uchukulie wajibu wako kama kazi yako unayopaswa kufanya, uibebe mizigo ya kazi hii, ukubali lawama ukifanya kosa dogo kabisa au ukizembea hata kidogo, lazima uhisi kwamba hupaswi kuwa mtu wa aina hii kwa sababu hilo litakufanya usiwe mwenye kustahili kwa Mungu kabisa. Watu ambao kwa kweli wana akili hutimiza wajibu wao kana kwamba ni kazi zao wenyewe wanazopaswa kufanya, bila kujali iwapo kuna mtu anayesimamia. Iwapo Mungu anafurahishwa nao au la na bila kujali jinsi Anavyowatendea, wao kila wakati hujishurutisha kutimiza wajibu wao na kutimiza agizo ambalo Mungu amewaaminia. Huku kunaitwa kujitolea(“Ni kwa Kuwa Mtu Mwaminifu tu Ndiyo Mtu Anaweza Kuwa na Furaha Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinionyesha njia ya kutenda. Hatuwezi kufuata mhemko na upendeleo wetu katika wajibu wetu huku tukifanya lolote tutakalo. Hatuwezi tu kumaliza jambo kwa kubahatisha wakati ambapo linahitaji bidii, bali tunapaswa kuchukulia wajibu wetu kama agizo la Mungu, kama wajibu wetu sisi wenyewe. Tunapaswa kutumia mawazo na bidii ili tupate matokeo bora. Bila kujali ni mgumu jinsi gani, iwe kwamba tunasimamiwa au la, tunapaswa kutekeleza wajibu wetu kila wakati kwa nguvu zetu zote. Nilipogundua haya, nilimwomba Mungu, nikiwa tayari kutubu na kutenda kulingana na maneno ya Mungu. Baadaye, nilitafuta wakati wa kutunga hati juu ya matumizi ya alama za uandishi katika Kiitaliano ili washiriki wapya waitumie. Baadaye, nilifanya muhtasari wa matatizo ya kawaida ambayo hutokea katika tafsiri na nikaorodhesha kila kitu kilichohitaji kuzingatiwa. Niliangalia mambo haya wakati wa kukagua hati ili kusiwe na kosa lolote. Na ndugu yeyote alipouliza swali juu ya wajibu wake, sikuangalia tu kwa haraka wala kutumia mawazo yangu kujibu, bali nilizingatia swali lake kwa uangalifu, nilitumia kanuni na kutafuta maarifa ya kitaalamu ambayo ningeweza kutumia kumjibu. Wakati ambapo sikuelewa jambo fulani, nililielewa polepole kupitia juhudi halisi pamoja na nuru na mwongozo kutoka kwa Mungu. Pia nilitafakari sana juu ya nia yangu kosefu katika wajibu wangu. Kila nilipokabiliwa na matatizo na kutaka kutumia mbinu rahisi, nilimwomba Mungu anipe nguvu ili niweze kutatua matatizo hayo kwa kiwango halisi cha juhudi zilizohitajika. Mtazamo wangu katika wajibu wangu ulirekebishika polepole na nilizembea kidogo zaidi. Niliweza kutekeleza wajibu wangu kwa njia thabiti. Mabadiliko haya yaliyotokea ndani yangu yalikuwa matokeo ya kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu. Shukrani kwa Mungu!

Iliyotangulia: 23. Hatimaye Naelewa Maana ya Kutimiza Wajibu Wangu

Inayofuata: 25. Kumpa Mungu Moyo Wangu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

45. Kuishi Mbele za Mungu

Na Yongsui, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp