222 Nimeona Uzuri wa Mungu

1

Nasikia sauti ninayoifahamu ikiniita kila wakati.

Nikiamshwa na kutazama ili nione, ni nani yuko hapo akizungumza.

Sauti Yake ni nyororo lakini kali, sura Yake nzuri!

Maneno hayo yalikuwa kama upanga mkali ukiuchoma moyo na roho yangu.

Yaliweka wazi ukweli wa upotovu wangu, sikuwa na mahali pa kujificha.

Najichukia, na majuto makubwa, nikifikiria nilichofanya.

Nikiwa nimepotoshwa sana na Shetani, nilikuwa mwovu sana.

Kwa kutiwa sumu na kulowezwa katika mawazo ya yule mwovu, nilikuwa nimepoteza ubinadamu wote.

Kwa ajili ya hadhi, nikishindana na Mungu, mimi siheshimiki.

Mungu bado ni Mungu, mwanadamu ni mwanadamu tu—mimi ni mpumbavu sana.

Mjinga sana na mwenye majivuno sana hata kutojijua.

Sikuwa na haya na kuaibika; moyo wangu unajaa na majuto.

Ukweli ulifichuliwa kuwa nilikuwa nimepotoka sana na sikuwa na mfanano wa binadamu.

Tabia iliyopotoka inanisumbua, utumishi wangu bado ni wa bure.

Bila kumjua Mungu, kujawa na dhana; ningekosa vipi kupinga?

Nashukuru hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa kunitakasa na kuniokoa.

2

Nimepigwa na napitia maumivu makali, lakini mkono wenye upendo upo ukinipapasa.

Mungu ananihukumu, kwa uasi wangu, na uovu wangu.

Ninajichukia, mfuasi wa muda mrefu wa Bwana ambaye hakumjua Mungu.

Kumwona Mungu kweli ni mwenye haki na mtakatifu, natii kabisa.

Hukumu na kuadibu ni upendo wa Mungu, baraka Zake.

Ni kwa sababu tu ya wokovu Wake kupitia kwa hukumu ndiyo ninayo siku hii.

Uhakika na uweza wa Mungu, umefichuliwa kabisa kwa mwanadamu.

Kuishi katika mwangaza, namjua Mungu na nimeona uzuri Wake.

Mungu ni mwenye kupendeza sana, nampenda Mungu kwa moyo wangu, nitamshuhudia milele.

Iliyotangulia: 221 Kuwa Mtu Mpya

Inayofuata: 223 Maisha ni ya Thamani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp