221 Kuwa Mtu Mpya

1

Nikikumbuka imani yangu katika Mungu zamani, moyo wangu unahisi kuwa na deni sana.

Kwa kuwa sikufuatilia ukweli, naachwa na majuto mengi sana.

Mungu aliniinua kutenda wajibu wangu, lakini sikujua kujali mapenzi Yake.

Nilifanya kazi na kuhubiri ili kujilinganisha na watu wengine tu.

Nilifurahia kuheshimiwa na kuthaminiwa na wengine.

Nilimtumikia Mungu kwa jina, lakini kwa kweli nilikuwa najikuza.

Mungu alinikumbusha na kunionya mara nyingi sana lakini sikujali.

Nisiyepindika, nilishughulika tu ili kupata tuzo, kwa ajili ya taji.

Nilijitahidi ili kupata heshima na hadhi, ni machukizo sana kwa Mungu.

2

Mungu alificha uso Wake nami nikaanguka gizani bila mahali pa kugeukia.

Kama maiti itembeayo siku zangu zilikuwa kama miaka.

Katika majaribu, nilichunguza vitendo na tabia yangu mwenyewe.

Nilifurahia upendo mwingi sana wa Mungu lakini sikufikiria kumlipiza.

Nilitumia fursa kufanya wajibu wangu kujionyesha.

Asili yangu, kama ile ya malaika mkuu, inapaswa kulaaniwa na Mungu.

Nikitetemeka kwa hofu, nilianguka mbele za Mungu kwa majuto mengi.

Nikiwa mwasi na mpinzani sana kwa Mungu, ninawezaje kustahili kuitwa mwanadamu?

Natamani kukubali hukumu ya Mungu na kufikia mabadiliko ya tabia.

3

Kwa kupitia hukumu ya Mungu, nilikuja kuijua tabia ya Mungu kuwa ya haki.

Moyoni mwangu namcha na kumtii Mungu na ninaishi kwa kudhihirisha mfano kiasi wa binadamu.

Ni sasa tu ndipo najua kuwa bila mabadiliko ya tabia, sistahili kumtumikia Mungu.

Nashukuru hukumu ya Mungu ya wakati ufaao ambayo ilinileta katika ulinzi Wake.

Sasa nimeonja upendo wa Mungu, na ni wa kweli na halisi sana.

Ee Mungu, sitakuasi tena wala kusababishia huzuni.

Natamani tu kuthamini wakati huu wa mwisho na kuwa mtu mpya,

sio kutafuta heshima ya wengine, bali kuridhisha tu mapenzi Yako,

kuishi kwa kufuata maneno Yako na kukutukuza na kukushuhudia katika kila kitu.

Iliyotangulia: 220 Ningechukia Kurudi Katika Njia Zangu za Zamani na Kumwumiza Mungu Tena

Inayofuata: 222 Nimeona Uzuri wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp