Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Nisingeokolewa na Mungu

Nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,

nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.

Nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,

kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.

Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma kwangu, maneno Yake yananiita.

Huniruhusu niisikie sauti Yake na kuniinua mbele ya kiti Chake cha enzi.

Kila siku nakula na kunywa maneno ya Mungu, nafurahia kazi ya Roho Mtakatifu.

Naona kwamba upotovu wa binadamu ni wa kina sana, kwamba tunahitaji wokovu wa Mungu.

Ukweli wa Mungu hunitakasa na kuniokoa.

Nahukumiwa na kusafishwa mara nyingi, na tabia yangu ya kishetani inatakaswa.

Kujua kwamba Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, nakuja kuelewa uzuri Wake.

Naweza kumwogopa Mungu na kuepuka uovu, na tabia ya maisha yangu inabadilika.

Nimemwona Mungu uso kwa uso, nimeonja upendo Wake wa kweli.

Naona kwamba ukweli ni wa thamani sana, kwamba ni maisha ya milele ambayo Mungu humpa mwanadamu. 

Namtii Mungu na kutimiza wajibu wangu; moyo wangu una utulivu na unapata amani, ninaridhika.

Baada ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, napokea wokovu Wake wa siku za mwisho.

Natembea katika njia inayong’aa ya maisha, maisha yangu yana maana.

Napokea wokovu mkuu zaidi wa Mungu, na moyo wangu umejaa shukrani isiyo na mwisho.

Mungu yuko karibu sana, mwenye kupendeza sana, niko tayari kumpa Yeye mwili na roho yangu.

Nitamtii Yeye na kumpenda katika maisha yangu yote, nitalipiza upendo Wake kwa uaminifu wangu.

Iliyotangulia:Katika Familia Ya Mungu, tunakutana na kila mmoja

Inayofuata:Mwanadamu Anafaa Kuishi kwa Ajili Ya Nani

Maudhui Yanayohusiana

 • Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani

  Ⅰ Nimerejea katika familia ya Mungu, nikiwa mwenye msisimko na furaha. Nina bahati ya kukujua Wewe Mwenyezi Mungu, nimekupa moyo wangu. Ingawa nimepi…

 • Tilia Maanani Majaliwa ya Binadamu

  Ⅰ Mungu anawahimiza watu wa makabila yote, nchi zote na hata nyanja: Sikilizeni sauti ya Mungu na kuona kazi Yake; tilia maanani jaala ya binadamu; mf…

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  Ⅰ Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwe…