2. Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:

Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu Yeye ni mwanadamu na, hata zaidi, Yeye ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kuifanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, Ana uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kwa kutoa ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na Ana uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kwa kuweza kumpata mwanadamu kikamilifu. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa wanadamu unamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani atii kikamilifu chini ya utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amepata mwili ndio maana Anaweza kumshinda Shetani na Anaweza kumwokoa binadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda binadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kutoa ushuhuda Kwake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unatoa ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko uangamizaji wa Shetani wa moja kwa moja na Roho wa Mungu. Mungu katika mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kutoa ushuhuda Kwake Mwenyewe miongoni mwa viumbe Vyake vilivyoumbwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba, Anaweza kuacha maneno na mawaidha sahihi, na mapenzi Yake mahususi kwa ajili ya wanadamu kwa wale wanaomfuata, ili baadaye wafuasi Wake waweze kwa usahihi zaidi na kwa uthabiti zaidi kupitisha kazi Yake yote katika mwili, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote, kwa wale wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili Anahitimisha enzi ambapo ni mgongo wa Yehova pekee ndio ulioonekana kwa wanadamu, na pia Anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Hasa, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya kivitendo zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la muhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida, ambaye ni Mwenye haki na mtakatifu, ambaye Anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kufafanua mafumbo na hatima ya wanadamu, ambaye Aliwaumba wanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye Amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili kwa niaba ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili Wake, wale wanaomfuata wanakuwa hawatafuti tena na kupapasa vitu hivyo vinavyoonekana kuwa vipo na ambavyo havipo, na wanaacha kukisia mapenzi ya Mungu asiyeonekana. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yanayosikiwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa ni mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona binafsi, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao kupitia huo Anaeneza kazi, na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, injili Yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali tu kwa fikira za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Roho hagusiki na mwanadamu, na wala Hawezi kuonekana na mwanadamu, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia bora zaidi ya Mungu kuonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho, ila kwa ule wa kawaida sana. Zaidi ya hayo, ni mwili wa kupata mwili kwa Mungu mara ya pili, na pia ni mwili ambao Mungu anarudi kupitia kwao tena. Ni mwili wa kawaida sana. Ukimwangalia, huwezi kuona chochote kinachomfanya aonekane tofauti na wengine, lakini unaweza kupata kutoka Kwake ukweli ambao haujawahi kusikika hapo awali. Mwili huu tu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya Mungu ya ukweli, uletao kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na maonyesho ambayo kwayo mwanadamu anaielewa tabia nzima ya Mungu. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakwambia hizi siri zote—siri ambazo hakuna mwanadamu yeyote amewahi kuweza kukuambia—na pia Atakwambia ukweli ambao huelewi. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile ambacho mwanadamu anaona wakati huu ni Mungu ambaye ni sawa na mwanadamu, Mungu mwenye pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu sana, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba kama mtu huyu hangekuwepo, mbingu na dunia zingepitia mabadiliko makubwa; kama mtu huyu hangekuwepo, mbingu zingefifia, dunia ingetumbukia katika machafuko, na wanadamu wote wangeishi katikati ya njaa na tauni. Atawaonyesha kwamba iwapo Mungu aliyefanyika mwili wa siku za mwisho hangekuja kuwaokoa, basi Mungu angekuwa amewaangamiza wanadamu wote jahanamu zamani; iwapo mwili huu haungekuwepo, basi ninyi mngekuwa wenye dhambi kubwa milele, na mngekuwa maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba iwapo mwili huu haungekuwepo, isingewezekana kwa wanadamu wote kuepuka janga kuu, na isingewezekana kwao kuepuka adhabu kali zaidi ambayo Mungu huwapa wanadamu katika siku za mwisho. Kama mwili huu wa kawaida haungezaliwa, nyote mngekuwa katika hali ambayo mnaomba uzima bila kuweza kuishi na kuomba kifo bila kuweza kufa; kama mwili huu haungekuwepo, basi hamngeweza kupata ukweli na kuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu leo, bali, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu za kusikitisha. Je, mnajua kwamba isingekuwa kwa ajili ya kurudi kwa Mungu katika mwili, kusingekuwa na nafasi ya wokovu kwa yeyote; na kama mwili huu haungekuja, Mungu angekuwa ameshakomesha enzi ya zamani? Hali ikiwa hivi, je, bado mtakataa kupata mwili kwa Mungu mara ya pili? Kwa kuwa mnaweza kupata faida kubwa namna hii kutoka kwa mtu huyu wa kawaida, kwa nini msimkubali kwa furaha?

Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa. Hata hivyo, lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo. Kwa hivyo, bila kujali, hii gharama iliyolipwa na Mungu yote imekuwa katika maandalizi ya kazi ya kupata mwili Kwake katika siku za mwisho. Ukweli kwamba mmefika siku ya leo ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu, kwa sababu ni ukweli, uzima, na njia Aliyoleta ndivyo vilivyowaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya mwanadamu na Mungu, ikafupisha umbali kati yao, na kufungua kiungo kati ya mawazo ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi upendo wenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?

Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wenye mzaha mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba wale ambao hawamkubali Kristo wa siku za mwisho watachukiwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, na hakuna ambaye anaweza kumpita Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unamwamini Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kulitii neno Lake. Usifikiri tu kuhusu kupata baraka huku ukikosa kuweza kupokea ukweli na ruzuku ya uzima. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili Aweze kuwatolea uzima wale wote ambao wanamwamini kwa dhati. Kazi hii ipo kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuiingia enzi mpya, na kazi hii ndiyo njia ambayo lazima ifuatwe na wale wote ambao wataingia katika enzi mpya. Kama humtambui Kristo, na zaidi ya hayo umhukumu, umkufuru au kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Hii ni kwa sababu Kristo huyu Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani, na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unamkufuru Roho Mtakatifu.Adhabu inayostahili kwa wale wanaomkufuru Roho Mtakatifu ni dhahiri kwa wote. Pia nakuambia hili: Ukimpinga Kristo wa siku za mwisho, ukimkataa Kristo wa siku za mwisho, basi hakuna mtu mwingine anayeweza kubeba matokeo ya hili kwa niaba yako. Zaidi ya hayo, kuanzia wakati huo na kuendelea hutawahi kuwa na nafasi ya kupata kibali cha Mungu kamwe; hata ukitaka kujikomboa, hutaweza kuutazama uso wa Mungu tena. Hii ni kwa sababu unayempinga si mwanadamu, unayemkataa si mtu asiye na maana, bali ni Kristo. Je, unajua matokeo ya hili ni yapi? Hufanyi kosa dogo, bali unatenda dhambi mbaya sana. Na kwa hivyo namshauri kila mtu asitoe kucha na meno au kutoa maoni kiholela mbele ya ukweli, kwa maana ukweli pekee ndio unaoweza kukuletea uzima, na hakuna chochote isipokuwa ukweli kinachoweza kukuwezesha kuzaliwa upya na kuutazama uso wa Mungu tena.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Iliyotangulia: 1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Inayofuata: 3. Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu Mwenye Mwili na Kazi ya Roho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp