Sura ya 18

Maneno yote ya Mungu yana sehemu fulani ya tabia Yake. Tabia ya Mungu haiwezi kuonyeshwa kikamilifu katika maneno, jambo ambalo linatosha kuonyesha ni kiasi gani cha utajiri kilicho ndani Yake. Kile ambacho watu wanaweza kuona na kugusa ni, finyu, hata hivyo, kama ulivyo uwezo wa watu. Ingawa maneno ya Mungu ni dhahiri, watu hawawezi kuyaelewa kikamilifu. Chukua maneno haya kwa mfano: “Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, mwanadamu amepata tena utakatifu aliokuwa nao wakati mmoja. Eh, dunia potovu ya zamani! Mwishowe, imeanguka na kutumbukia ndani ya maji machafu na, imezama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope!” Maneno yote ya Mungu yana nafsi Yake, na ingawa watu wote wanayajua maneno haya, hakuna ambaye amewahi kuelewa maana yake. Machoni pa Mungu, wote ambao humpinga ni adui Zake, yaani, wale ambao ni wa pepo wabaya ni wanyama. Kutokana na hili, mtu anaweza kuona hali ya kweli ya kanisa. Wanadamu wote wanaangaziwa na maneno ya Mungu, na katika mwanga huu, wanajichunguza bila kupitia karipio au kurudiwa au kupuuzwa moja kwa moja na wengine, bila kushurutishwa na njia zingine za kibinadamu za kufanya mambo, na bila wengine kutaja mambo. Kutoka katika “mtazamo wa hadubini”, wanaona waziwazi ni kiasi gani cha maradhi kilicho ndani yao kweli. Katika maneno ya Mungu, kila aina ya roho imeainishwa na kufichuliwa katika umbo lake la asili. Roho za malaika zinakuwa zenye nuru zaidi, na ndiyo maana ya maneno ya Mungu: “Mwanadamu amepata tena utakatifu aliokuwa nao wakati mmoja.” Maneno haya yametegemezwa kwa matokeo ya mwisho yaliyotimizwa na Mungu. Kwa sasa, bila shaka, matokeo haya hayawezi kutimizwa kikamilifu—ni jaribio tu la mwanzo, ambalo kwalo mapenzi ya Mungu yanaweza kuonekana. Maneno haya yanatosha kuonyesha kwamba idadi kubwa ya watu wataporomoka katika maneno ya Mungu na watashindwa katika mchakato wa hatua kwa hatua wa kutakaswa kwa watu wote. Hapa “kuyeyuka na kuwa tope” hakukinzani na Mungu kuuangamiza ulimwengu kwa moto, na “umeme” linarejelea ghadhabu ya Mungu. Mungu anapoachilia ghadhabu Yake kuu, ulimwengu mzima utapitia maafa ya kila aina kama matokeo, kama vile volkano kufoka. Ninaposimama juu kabisa ya angani, inaweza kuonekana kuwa duniani, maafa ya aina mbalimbali yanawakaribia wanadamu wote, yakikaribia kila siku. Nikiangalia chini kutoka juu, dunia inaonyesha mandhari mbalimbali kama yale yanayotangulia tetemeko la ardhi. Moto unaotiririka unasonga bila kupingwa, lava inatiririka kwa uhuru, milima inasonga, na mwanga wa baridi unametameta juu ya kila kitu. Dunia nzima imezama katika moto. Haya ndiyo mandhari ya Mungu akitoa ghadhabu Yake, na pia ndio wakati wa hukumu Yake. Wale wote ambao ni wa damu na nyama hawataweza kutoroka. Hivyo, vita kati ya nchi na migogoro kati ya watu havitahitajika kuharibu ulimwengu mzima; badala yake, dunia “itafurahia yenyewe kwa kufahamu” katika chanzo cha kuadibu kwa Mungu. Hakuna mtu atakayeweza kuiepuka; kila mtu atapitia katika mateso haya. Baada ya hapo, ulimwengu mzima utaanza tena kuangaza kwa miale takatifu na wanadamu wote wataanza tena maisha mapya. Na Mungu atakuwa Amepumzika juu ya ulimwengu na Atawabariki wanadamu wote kila siku. Mbingu haitakuwa na ukiwa usiovumilika, lakini itarudia nguvu ambayo haijawahi kuwa nayo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na kuja kwa “siku ya sita” itakuwa wakati Mungu ataanza maisha mapya. Mungu na wanadamu wote wataingia katika pumziko na ulimwengu hautakuwa tena mchafu au wenye najisi, lakini utafanywa upya tena. Ndiyo maana Mungu alisema: “Dunia si kimya cha mauti na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena.” Katika ufalme wa mbinguni, hakujakuwa na udhalimu au hisia za kibinadamu, au tabia yoyote potovu ya wanadamu, kwa sababu usumbufu wa Shetani haupo hapo. “Watu” wote wanaweza kuelewa maneno ya Mungu, na maisha mbinguni ni maisha yaliyojaa furaha. Wote walio mbinguni wana hekima na heshima ya Mungu. Kwa sababu ya tofauti iliyoko kati ya mbingu na dunia, raia wa mbinguni hawaitwi “watu”; badala yake, Mungu huwaita “roho”. Maneno haya mawili yana tofauti muhimu—wale wanaoitwa “watu” sasa wamepotoshwa na Shetani, wakati “roho” hazijapotoshwa. Mwishowe, Mungu atawabadilisha watu wa duniani wawe viumbe wenye sifa za roho wa mbinguni, na kisha hawatakuwa tena chini ya vurugu ya Shetani. Hii ndiyo maana halisi ya maneno, “utakatifu Wangu umeenea katika kila pembe ya ulimwengu.” “Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wa mwanadamu, kwa ajili ya kufanywa upya kwa mwanadamu, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu.” Hili linasemwa kuhusu watu walio na roho za malaika, na wakati huu, “malaika” watakuwa tena na uwezo wa kuishi pamoja kwa amani na kupata tena hali yao ya awali, hawatagawanywa tena na mwili kati ya falme za mbingu na dunia. “Malaika” walio duniani wataweza kuwasiliana na malaika walio mbinguni, watu walio duniani watajua siri za mbinguni, na malaika walio mbinguni watajua siri za ulimwengu wa binadamu. Mbingu na dunia zitaunganishwa, na hakutakuwa na umbali kati yao. Huu ni uzuri wa utambuzi wa ufalme. Ni kile ambacho Mungu atakamilisha, na ndicho kitu ambacho wanadamu wote na roho hutamani sana. Lakini wale walio katika ulimwengu wa kidini hawajui chochote kuhusu hili. Wao wanamngojea tu Yesu Mwokozi aje juu ya wingu jeupe na Azichukue roho zao, na kuacha “taka” zikitapakaa kila mahali duniani (taka inarejelera maiti). Je, hii si fikira ambayo wanadamu wote wanayo? Hii ndiyo maana Mungu alisema: “Eh, dunia ya dini! Ingekosaje kuangamizwa na mamlaka Yangu duniani?” Kwa sababu ya ukamilishaji wa watu wa Mungu ulimwenguni, ulimwengu wa kidini utapinduliwa. Hii ndiyo maana ya kweli ya “mamlaka” ambayo Mungu alizungumzia. Mungu alisema: “Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hulifedhehesha jina Langu? Watu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao.” Hili ndilo Alilosema juu ya matokeo ya uharibifu wa ulimwengu wa dini. Utatii kikamilifu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kwa sababu ya maneno Yake, na hawatasubiri tena wingu jeupe lishuke chini au watazame angani, lakini badala yake watashindwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ndiyo sababu ya maneno, “wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao”—haya yatakuwa matokeo kwa ulimwengu wa dini, ambao Mungu atakushinda kikamilifu. Hii ndiyo maana ya uweza wa Mungu—kuwaangusha chini watu wote wa dini, waasi wakuu kati ya wanadamu, ili kwamba wasiyashikilie tena mawazo yao wenyewe kwamba waweze kumjua Mungu.

Ingawa maneno ya Mungu yametabiri uzuri wa ufalme mara kwa mara, yamesema juu ya hali zake mbalimbali na kuzielezea kwa mitazamo tofauti, bado hayawezi kueleza kikamilifu kila hali ya Enzi ya Ufalme kwa sababu uwezo wa watu wa kupokea umepungukiwa sana. Maneno yote ya matamko Yake yamenenwa, lakini watu hawajayaangalia ndani kupitia kwa kipiga picha za ndani, X-ray na hivyo wamepungukiwa na mwanga na ufahamu na hata wamekanganywa. Hii ni kasoro kubwa zaidi ya mwili. Ingawa ndani ya mioyo yao, watu wanataka kumpenda Mungu, wanampinga kwa sababu ya usumbufu wa Shetani, kwa hiyo mara kwa mara Mungu amegusa mioyo ya watu yenye ganzi na isiyoelewa ili wapate kufufuliwa. Yote ambayo Mungu hufunua ni ubaya wa Shetani, kwa hivyo kadiri maneno Yake yalivyo makali zaidi, ndivyo Shetani huaibika zaidi, ndivyo mioyo ya watu inavyokuwa wazi zaidi, na ndivyo upendo wa watu unavyozidi kuamshwa. Hivi ndivyo Mungu anavyofanya kazi. Kwa sababu Shetani amefunuliwa na kwa sababu ametambuliwa, hathubutu tena kumiliki mioyo ya watu, na hivyo malaika hawachokozwi tena. Kwa njia hii, ndio wanampenda Mungu kwa moyo na akili zao zote. Ni wakati huu tu ndipo inakuwa wazi kuona kwamba, katika hali zao halisi, malaika ni wa Mungu na wanampenda Yeye. Ni kwa njia hii tu ndiyo mapenzi ya Mungu yanaweza kutimizwa. “Ndani ya nyoyo zao, sasa kuna nafasi kwa ajili Yangu. Sitakumbana tena na chuki na kukataliwa miongoni mwa wanadamu, kwani kazi Yangu kubwa imekwisha tekelezwa, na haizuiliwi tena.” Hii ndiyo maana ya yale yaliyoelezwa hapo juu. Kwa sababu ya uchokozi wa Shetani, watu hawawezi kupata wakati wa kumpenda Mungu na daima wao hutatizwa na mambo ya ulimwengu na wanahadaiwa na Shetani kiasi kwamba wao hutenda wakiwa wamechanganyikiwa. Hii ndiyo maana Mungu amesema kuwa wanadamu “wameyapitia matatizo mengi sana ya maisha, dhuluma nyingi za ulimwengu, mageuko mengi sana ya ulimwengu wa binadamu, lakini sasa huishi katika nuru Yangu. Je, ni nani asiyelia kwa ajili ya dhuluma za jana?” Wakati ambapo watu wamesikia maneno haya, wanahisi kama kwamba Mungu ni mwenzao katika taabu, Anasikitika nao, na wakati huo, Anashiriki nao malalamiko yao. Wanahisi ghafla maumivu ya ulimwengu wa binadamu na kufikiri: “Hiyo ni kweli kabisa—Sijawahi kufurahia chochote duniani. Tangu nitoke tumboni mwa mama yangu hadi sasa nimepitia maisha ya binadamu na sijawahi kupata kitu chochote, lakini nimeteseka sana. Yote ni tupu kweli! Na sasa nimepotoshwa sana na Shetani! Oh! Ikiwa si kwa ajili ya wokovu wa Mungu, wakati wa kifo changu unapokuja, je, sitakuwa nimeishi maisha yangu yote bila sababu? Je, Kuna maana yoyote kwa maisha ya binadamu? Si ajabu Mungu alisema kuwa kila kitu chini ya jua ni tupu. Kama Mungu hangenipa nuru leo, bado ningekuwa gizani. Jambo ovu lililoje!” Wakati huu, wanakuwa na shaka moyoni mwao: “Ikiwa siwezi kupata ahadi ya Mungu nitawezaje kuendelea kuwa na uzoefu wa maisha?” Kila mtu anayesoma maneno haya atalia akiomba. Hivyo ndivyo ilivyo roho ya mtu. Itakuwa vigumu kwa mtu kusoma hili na asiwe na mjibizo wowote, isipokuwa awe mwenye akili pungwani. Kila siku, hufichua hali za watu wa kila aina. Wakati mwingine, Yeye hutoa malalamiko kwa niaba yao. Wakati mwingine Huwasaidia watu kushinda na kupitia kwa ufanisi katika mazingira fulani. Wakati mwingine, Anawatajia watu “mabadiliko” yao. La sivyo, watu wasingejua kiasi ambacho wamekua katika maisha. Wakati mwingine, Mungu huonyesha uzoefu wa watu kwa uhalisi, na wakati mwingine Huonyesha upungufu na makosa yao. Wakati mwingine, Yeye hufanya matakwa mapya kwao, na wakati mwingine Huonyesha kiwango ambacho kwacho wao wanamwelewa Yeye. Hata hivyo, Mungu amesema pia: “Nimesikia maneno ya dhati yakinenwa na watu wengi, simulizi kutoka kwa watu wengi sana kuhusu matukio machungu ya mateso waliyopitia; Nimeona wengi sana, katika dhiki kubwa sana, wakinipa utiifu wao bila kukosa, na Nimewatazama wengi sana, wakitembea kwenye njia yenye mabonde, wakitafuta suluhisho.” Haya ni maelezo ya wahusika wa kujenga. Katika kila tukio la “tamthilia ya historia binadamu” sit u kwamba kumekuwa na wahusika chanya lakini kumekuwa na wahusika hasi pia. Kwa hivyo, Mungu anafichua ubaya wa wahusika hawa hasi. Hivyo, ni kupitia tu tofauti yao na “wasaliti” ndio uaminifu usiokubali kushindwa na ujasiri usio na hofu wa “wanadamu wenye haki” unafichuliwa. Katika maisha ya watu wote kuna vipengele hasi na pia, bila ubaguzi, vipengele vya kujenga. Mungu hutumia vyote kufichua ukweli juu ya watu wote, ili wasaliti wainamishe vichwa vyao na kukubali dhambi zao, na ili, kukiwa na himizo, watu wenye haki wataendelea kuwa waaminifu. Matokeo ya maneno ya Mungu ni ya kina kirefu sana. Wakati mwingine, watu huyasoma na kisha kuangua kichecko wakati mwingine, huinamisha tu vichwa vyao na kunyamaza. Wakati mwingine wanakumbuka, wakati mwingine wanalia kwa uchungu na kukiri dhambi zao, wakati mwingine wao hupapasa, na wakati mwingine wanatafuta. Kwa jumla, kuna mabadiliko katika mijibizo ya watu kwa sababu ya hali tofauti ambamo Mungu ananena. Mtu anaposoma maneno ya Mungu, wakati mwingine watazamaji wanaweza hata kuamini kwa makosa kwamba mtu huyo ni mgonjwa wa akili. Chukua maneno haya kwa mfano: “Na hivyo, migogoro yenye ubishi duniani haipo tena, na, kufuatia kutolewa kwa maneno Yangu, ‘silaha’ mbali mbali za enzi ya sasa zimeondolewa.” Neno “silaha” pekee linaweza kuibua kicheko cha siku nzima, na kila ambapo mtu kwa bahati anaweza kukumbuka neno “silaha”, atajichekea mwenyewe kwa nguvu. Si hivi ndivyo ilivyo? Unawezaje kukosa kucheka kwa ajili ya hili?

Unapocheka, usisahau kufahamu kile ambacho Mungu anataka kwa wanadamu, na usisahau kuona hali ya kweli ya kanisa: “Binadamu wote wamerudi katika hali ya kawaida na kuanza maisha mapya. Wakiishi katika mazingira mapya, idadi kubwa ya watu huangalia kandokando yao, wakihisi kana kwamba wameingia katika ulimwengu mpya kabisa, na kwa sababu ya hili, wanashindwa kubadilika mara moja katika mazingira yao ya sasa ama kuingia mara moja kwenye njia nyofu.” Hii ndiyo hali ya kweli ya kanisa sasa. Usiwe na hamu sana kuwafanya watu wote waingie mara moja kwenye njia sahihi. Punde kazi ya Roho Mtakatifu itakapokuwa imeendelea hadi hatua fulani, watu wote wataingia ndani yake bila kutambua. Unapofahamu kiini cha maneno ya Mungu, utajua Roho Wake amefanya kazi hadi kufikia hatua ipi. Mapenzi ya Mungu ni: “Mimi husimamia tu, kulingana na udhalimu wa mwanadamu, kipimo mwafaka cha ‘elimu,’ bora ili kumwezesha kila mtu kushika njia nyofu.” Hii ni mbinu ya Mungu ya kuzungumza na kufanya kazi, na pia ndiyo njia mahsusi ya kutenda kwa wanadamu. Baada ya hili, Aliwaashiria watu hali nyingine za binadamu: “Kama wanadamu hawataki kufurahia upeo wa furaha iliyo ndani Yangu, Ninaweza kukubaliana tu na kile ambacho mioyo yao inatamani kufanya na kuwatupa katika shimo lisilo na mwisho.” Mungu alinena kwa ukamilifu na kuwaacha watu bila fursa hata kidogo ya kulalamika. Hii hasa ndiyo tofauti iliyopo kati ya Mungu na mwanadamu. Daima Mungu huzungumza na mwanadamu waziwazi na kwa uhuru. Katika kila kitu ambacho Mungu anasema, mtu anaweza kuuona moyo Wake wa dhati, unaowasababisha watu waipime mioyo yao dhidi ya Wake na kuwawezesha kuifungua mioyo yao Kwake, ili Aweze kuona hali zao halisi hasa. Mungu hajawahi kusifu imani ya mtu au upendo wa mtu yeyote, lakini daima Ametoa matakwa kwa watu na kufunua upande wao mbaya. Hii inaonyesha “kimo” kidogo walicho nacho watu na jinsi “katiba” yao ilivyo na upungufu. Wanahitaji “mazoezi” zaidi ili kufidia mapungufu haya, ndiyo maana kila wakati Mungu “huwashushia watu” ghadhabu Yake. Siku moja, ambapo Mungu atafunua ukweli wote kuwahusu wanadamu, watu watakamilishwa, na Mungu atastarehe. Watu hawatamrarai Mungu tena, na Yeye “Hatawaelimisha” tena. Kuanzia hapo na kuendelea, watu wataweza “kuishi peke yao,” lakini sasa si wakati wa jambo hilo. Bado kuna mengi katika watu yanayoweza kuitwa “bandia”, na raundi kadhaa za uchunguzi zinahitajika, “vituo kadhaa zaidi vya ukaguzi” ambapo “ushuru” unaweza kulipwa vizuri. Ikiwa bado kuna bidhaa bandia, zitatwaliwa ili zisiuzwe, na kisha bechi hilo la bidhaa za magendo litaharibiwa. Je, hii siyo njia nzuri ya kufanya mambo?

Iliyotangulia: Sura ya 17

Inayofuata: Sura ya 19

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp