Sura ya 19

Katika mawazo ya watu, inaonekana Mungu ni wa fahari sana, naye ni Asiyeeleweka. Ni kana kwamba Mungu haishi miongoni mwa binadamu na kana kwamba anawadharau watu kwa sababu Yeye ni wa fahari sana. Mungu, hata hivyo, huziseta fikira za watu na kuzifuta zote, Akizizika katika “makaburi” ambamo zinageuka kuwa majivu. Mtazamo wa Mungu kwa fikira za binadamu ni sawa na mtazamo Wake kwa wafu, Akiwafafanua apendavyo. Inaonekana kana kwamba fikira hazina mjibizo; kwa hivyo, Mungi amekuwa akifanya kazi hii tangu uumbaji wa dunia hadi leo, na Hajaacha kamwe. Kwa sababu ya mwili, binadamu hupotoshwa na Shetani, na kwa sababu ya matendo ya Shetani duniani, binadamu huunda kila aina ya fikira katika harakati ya uzoefu wao. Huu unaitwa “muundo asilia.” Hii ndiyo hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani, kwa hiyo mbinu ya kazi Yake imefikia kilele chake, naye Anazidisha mafunzo Yake kwa binadamu ili waweze kufanywa wakamilifu katika kazi Yake ya mwisho, hatimaye wakiyaridhisha mapenzi ya Mungu. Awali, kulikuwa tu na kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu miongoni mwa binadamu, lakini hakuna maneno yaliyonenwa na Mungu Mwenyewe. Wakati ambapo Mungu alinena kwa sauti Yake Mwenyewe, kila mmoja alishangazwa, na maneno ya leo ni ya kushangaza zaidi. Maana ya maneno haya ni ngumu kutambua hata zaidi, na binadamu wanaoneka kuwa katika hali ya kuvutiwa sana, kwa sababu asilimia hamsini ya maneno Yake huja katikati ya alama za kudondoa. “Ninapozungumza, watu husikiliza sauti Yangu kwa makini sana; Ninaponyamaza kimya, hata hivyo, wao huanza ‘shughuli’ zao wenyewe.” Kifungu hicho kinajumuisha neno lililo katika alama ya kudondoa. Kadiri Mungu anavyozungumza kwa ucheshi zaidi, jinsi anavyofanya, ndivyo yanavyoweza kuwavutia zaidi watu kuyasoma. Watu wanaweza kukubali kushughulikiwa wakati ambapo wamepumzika. Kimsingi, hata hivyo, hili ni ili kuwazuia watu wengi kuvunjika moyo au kusikitika wakati ambapo hawajaelewa maneno ya Mungu. Hii ni mbinu ya vita vya Mungu dhidi ya Shetani. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu watasalia na kuvutiwa na maneno ya Mungu na waendelee kuyazingatia hata wanaposhindwa kufuata mkondo wa maneno hayo. Hata hivyo, kuna uzuri mwingi katika maneno Yake yote ambayo hayamo katika dondoo, na kwa hiyo yanatambulika zaidi na huwafanya watu kuyapenda maneno ya Mungu hata zaidi na kuhisi utamu wa maneno Yake ndani ya mioyo yao wenyewe. Kwa kuwa maneno ya Mungu huja katika miundo mingi mbalimbali, nayo ni mazuri na tofauti, na kwa kuwa hakuna urudiaji wa majina miongoni mwa maneno mengi ya Mungu, katika hisia yao ya tatu, watu huamini kuwa Mungu ni mpya daima na kamwe si mzee. Kwa mfano: “Siwataki watu wawe ‘wtumiaji’ tu; pia Nawataka wawe ‘wazalishaji’ wanaomshinda Shetani.” Maneno “watumiaji” na “wazalishaji” katika sentensi hiyo yana maana sawa na maneno mengine yaliyonenwa katika nyakati za awali, lakini Mungu si asiyebadilisha mawazo; badala yake, Huwafanya watu wafahamu upya Wake na hivyo kuthamini upendo wa Mungu. Ucheshi katika hotuba ya Mungu una hukumu Yake na madai Yake kwa binadamu. Kwa kuwa maneno yote ya Mungu yana malengo, kwa kuwa yote yana maana, ucheshi Wake haukusudiwi tu kuleta raha katika mazingira au kuwafanya watu waangue kicheko, wala si kwa ajili kulegeza misuli yao tu. Badala yake, ucheshi wa Mungu unanuiwa kumkomboa binadamu kutoka kwa kifungo cha miaka elfu tano, kamwe asifungwe tena, ili aweze kukubali maneno ya Mungu vizuri zaidi. Mbinu ya Mungu ni kutumia kijiko kimoja cha sukari kusaidia dawa iteremke; Huwa Hamlazimishi watu kumeza dawa chungu. Kuna uchungu ndani ya kilicho tamu, na pia utamu ndani ya kilicho chungu.

“Mwangaza hafifu unapoanza kuonekana Mashariki, watu wote ulimwenguni wanautilia maani zaidi kidogo. Bila kujawa na usingizi, binadamu wanasonga mbele kuchunguza chanzo cha mwangaza huu wa mashariki. Kwa sababu ya uwezo wao finyu, hakuna yeyote ambaye ameweza kuona mahali unapotokea mwangaza.” Hiki kinafanyika kila mahali ulimwenguni, sio tu miongoni mwa wana wa Mungu na watu Wake. Watu katika ulimwengu wa kidini na wasioamini wote huwa na mjibizo huu. Katika wakati ambapo nuru ya Mungu hung’aa, nyoyo zao zote hubadilika polepole, na wao huanza kugundua bila kujua kwamba maisha yao hayana maana, kwamba maisha ya binadamu hayana thamani. Binadamu hawafuatilii siku za baadaye, hawafikirii kuhusu kesho, au kuwa na wasiwasi kuhusu kesho; badala yake, wao hushikilia wazo kwamba wanapaswa kula na kunywa zaidi wakati bado ni “vijana,” na kwamba itakuwa imestahili mara tu siku ya mwisho itakapofika. Binadamu hawana hamu yoyote ya kuuongoza ulimwengu. Nguvu za upendo wa binadamu kwa ulimwengu ziliibwa kikamilifu na “ibilisi,” lakini hakuna ajuaye sababu ni gani. Kile wanachoweza kufanya ni kukimbia tu huku na kule, wakiarifiana, kwa kuwa siku ya Mungu bado haijafika. Siku moja, kila mtu ataona majibu kwa mafumbo yote yasiyoeleweka. Hiki ndicho ambacho Mungu alimaanisha hasa Aliposema, “Binadamu watazinduka kutoka usingizini na ndotoni, na ni hapo tu ndipo wanapotambua pole pole kwamba siku Yangu inawajia.” Wakati huo utakapofika, watu wote ambao ni wa Mungu watakuwa kama majani ya kijani kibichi “yakisubiri kufanya huduma yao Nikiwa duniani.” Watu wengi sana miongoni mwa watu wa Mungu Uchina bado hurudia hali mbaya baada ya Mungu kutamka sauti Yake, na kwa hiyo Mungu asema, “… ilhali, bila uwezo wa kubadilisha ukweli, hawana budi ila kunisubiri Nitoe hukumu.” Bado kutakuwa na wengine miongoni mwao wa kuondolewa—sio wote watabaki bila kubadilishwa. Badala yake, watu wanaweza tu kufikia viwango baada ya kujaribiwa, ambavyo kwavyo wanapewa “vyeti vya ubora”; la sivyo, watakuwa takataka juu ya rundo la takataka. Siku zote Mungu huonyesha hali halisi ya binadamu, kwa hiyo binadamu huendelea kuhisi usiri wa Mungu. “Kama Hangekuwa Mungu, Angewezaje kujua vizuri sana hali yetu halisi?” Hata hivyo, kwa ajili ya udhaifu wa watu, “[k]atika mioyo ya binadamu, Mimi daima si wa juu, wala duni. Kulingana na wao, haijalishi kama Nipo au la.” Je, hii hasa si hali ya watu wote inayolingana vizuri na uhalisi? Kulingana na wanadamu, Mungu yupo wakati ambapo wanamtafuta na hayupo wakati ambapo hawamtafuti. Kwa maneno mengine, Mungu yupo ndani ya mioyo ya binadamu punde tu wanapohitaji msaada Wake, lakini wakati hawamhitaji, Hayupo tena. Hiki ndicho kiko ndani ya mioyo ya watu. Kwa kweli, kila mtu duniani hufikiria hivi, ikiwemo “wakana Mungu” wote, na “fikira” yao kuhusu Mungu si dhahiri na ya isiyoonekana.

“Kwa hiyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu wa nchi tofauti mbali mbali, na hewa inapuliza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika nafasi zilizo juu ya dunia.” Hii ndiyo kazi ambayo Mungu alifanya wakati Alipokuwa Akiuumba ulimwengu. Kulitaja hili hapa kunawakanganya watu: Yawezekana kwamba Mungu anataka kuumba ulimwengu mwingine? Ni haki kusema hivi: Kila wakati Mungu anaponena, maneno Yake huwa na uumbaji, usimamizi, na uharibifu wa ulimwengu; ni kwamba tu wakati mwingine yako dhahiri, na wakati mwingine ni ya dhahania. Usimamizi wote wa Mungu unajumuishwa katika maneno Yake; ni kwamba tu wanadamu hawawezi kuyatofautisha. Baraka ambazo Mungu anawapa binadamu huifanya imani yao kukua mara mia moja. Kutoka nje, inaonekana kana kwamba Mungu anafanya ahadi kwao, lakini la muhimu ni kipimo cha matakwa ya Mungu kwa watu wa ufalme Wake. Wale wanaostahili kutumiwa watasalia, ilhali wale wasiotii watamezwa katika janga ambalo litaanguka kutoka mbinguni. “Radi, inayovingirika angani, itawaangusha binadamu; milima ya juu, inapoanguka, itawazika; wanyama pori kwa njaa yao watawala; na bahari, zinapobingirika, zitawagubika. Binadamu wanapojishughulisha na migogoro ya mauaji ya jamii, binadamu wote watatafuta maangamizo yao katika majanga yatokayo katikati yao.” Huku ni “kutendewa kwa njia ya pekee” kutakaotolewa kwa wale ambao hawafikii viwango vinavyohityajika na ambao baadaye hawataokolewa katika ufalme. Kadiri Mungu anavyosema mambo kama, “Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza,” ndivyo watu wanavyofahamu zaidi heshima yao wenyewe; hivyo, huwa na imani zaidi ya kutafuta maisha mapya. Mungu huwapa wanadamu jinsi wanavyomwomba. Punde Mungu anapowafichua kwa kiasi fulani, Yeye hubadilisha mtindo Wake wa kunena, Akitumia sauti ya kubariki ili kupata matokeo bora kabisa. Kuwawekea binadamu madai kwa njia hii hutoa matokeo zaidi ya kiutendaji. Kwa kuwa watu wote wako radhi kuzungumza kuhusu biashara na wenzi wao—wote ni watalaam katika biashara—hiki ndicho Anacholenga Mungu hasa katika kusema hivi. Kwa hiyo, “Sinimu” ni nini? Hapa, Mungu harejelei ufalme ulio duniani, ambao umepotoshwa na Shetani, badala yake kwakusanyiko la malaika wote waliotoka kwa Mungu. Maneno “simama imara na thabiti” yanadokeza kwamba malaika watapenyeza nguvu zote za Shetani, hiyo Sinimu katika ulimwengu mzima. Hivyo, maana halisi ya Sinimu ni kusanyiko la malaika wote duniani, na hapa inahusu wale walio duniani. Kwa hivyo, ufalme utakaokuwepo baadaye duniani utaitwa “Sinimu,” na sio “ufalme.” Hakuna maana halisi kwa “ufalme” ulio duniani; hususani, ni Sinimu. Hivyo, ni kwa kuunganisha tu kwa ufafanuzi wa Sinimu ndiyo mtu anaweza kujua maana halisi ya maneno “Hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.” Hili linaonyesha kupangwa katika madaraja kwa watu wote duniani katika siku za baadaye. Watu wote wa Sinim watakuwa wafalme wanaowaongoza watu wote duniani baada ya wao kupitia kuadibu. Kila kitu duniani kitatenda kazi kama kawaida kwa sababu ya usimamizi wa watu wa Sinim. Hiki ni kielelezo cha kukadiria tu hali hiyo. Watu wote watabaki ndani ya ufalme wa Mungu, kumaanisha kwamba wataachwa katika Sinim. Binadamu walio duniani wataweza kuwasiliana na malaika. Hivyo, mbingu na dunia zitaunganishwa; au, kwa maneno mengine, watu wote walio duniani watatii na kumpenda Mungu kama vile malaika mbinguni hufanya. Wakati huo, Mungu ataonekana waziwazi kwa watu wote duniani na Atawaruhusu wauone uso Wake halisi kwa macho yao, na Atajidhihirsha kwao wakati wowote.

Iliyotangulia: Sura ya 18

Inayofuata: Sura ya 20

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp