Sura ya 15

Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na mwanadamu ni kwamba maneno ya Mungu hulenga kiini cha jambo moja kwa moja, bila kuficha chochote. Hivyo, kipengele hiki cha tabia ya Mungu kinaweza kuonekana katika sentensi ya kwanza ya leo. Inafunua hali halisi za mwanadamu mara moja na kufichua tabia ya Mungu. Ni chanzo cha vipengele kadhaa vya uwezo wa maneno ya Mungu kufanikisha matokeo. Hata hivyo, watu hushindwa kufahamu hili; kila wakati wao huja kujijua kupitia katika maneno ya Mungu, bila ya “kumchambua” Mungu. Ni kana kwamba wanaogopa kumkosea Yeye au kwamba Atawaua kwa sababu ya “uangalifu” wao. Kwa kweli, watu wengi wanapokula na kunywa neno la Mungu, hufanya hivyo kutoka katika mtazamo hasi, sio ulio chanya. Inaweza kusemwa kuwa watu sasa wameanza “kuzingatia unyenyekevu na utiifu” chini ya mwongozo wa maneno Yake. Kutokana na hili, ni dhahiri kwamba watu wameanza kuzidi mipaka kwa namna nyingine—kutoka kwa kutokuwa makini na maneno Yake kuelekea kuyapa uzingativu usiostahili. Hata hivyo, hakuna mtu hata mmoja ambaye ameingia kutoka katika mtazamo chanya, wala hakuna mtu yeyote aliyewahi kujua kweli lengo la Mungu la kuwafanya wanadamu wazingatie maneno Yake. Inajulikana kutoka katika yale ambayo Mungu anasema kwamba Yeye hahitaji kupitia maisha ya kanisa binafsi ili kuweza kuelewa, kwa usahihi na bila makosa, hali halisi za watu wote waliyomo. Kwa sababu wamepata kuingia tu katika njia mpya, watu bado hawajaweza kuondokana kabisa na vipengele hasi; harufu za maiti bado zinaenea katika kanisa lote. Ni kana kwamba watu wamemeza dawa hivi punde na bado wametunduwazwa, ufahamu wao bado haujarejeshwa kikamilifu. Ni kana kwamba bado wanatishiwa na kifo, ili kwamba, wakiwa katikati ya hofu, hawawezi kuvuka mipaka wenyewe. “Wanadamu wote ni viumbe wasio na ufahamu kujihusu”: Namna ambavyo kauli hii inasemwa bado ina msingi katika ujenzi wa kanisa. Licha ya ukweli kwamba watu wote kanisani huzingatia maneno ya Mungu, asili zao zimekita mizizi kwa njia isiyochangulika. Hii ndiyo maana Mungu alizungumza jinsi alivyozungumza katika hatua iliyopita kuwahukumu watu, ili wapate kukubali kupigwa na maneno Yake katikati ya kiburi chao. Ingawa watu walipitia miezi mitano ya usafishaji kwenye shimo lisilo na mwisho, hali yao halisi bado ni ile ya kutomjua Mungu. Bado ni waovu; wanakuwa tu waliojilinda dhidi ya Mungu. Hatua hii ndiyo hatua ya kwanza inayofaa ambayo watu huchukua katika njia ya kuyajua maneno ya Mungu; hivyo, katika kuunganishwa na kiini cha maneno ya Mungu, si vigumu kuona kwamba sehemu ya hapo awali ya kazi iliandaa njia kwa ajili ya leo, na kwamba ni sasa tu ndiyo kila kitu kimefanywa kuwa kawaida. Udhaifu mbaya wa watu ni tabia yao ya kutenganisha Roho wa Mungu na nafsi Yake ya mwili ili kupata uhuru wa kibinafsi na kuepuka kizuizi cha kila wakati. Hii ndiyo sababu Mungu huwafafanua wanadamu kama ndege wadogo “wakirukaruka huku na kule kwa furaha.” Hii ndiyo hali halisi ya wanadamu wote. Hiyo ndiyo huwafanya watu wote wawe rahisi kuwashinda, na ndipo mahali ambapo wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupoteza njia yao. Ni dhahiri katika hili kwamba kazi ya Shetani kati ya wanadamu si zaidi ya kazi hii. Kadiri inavyofanywa zaidi na Shetani ndani ya watu, ndivyo mahitaji ya Mungu kwao yanavyozidi kuwa makali zaidi. Anawahitaji watu waweke mawazo yao katika maneno Yake, ilhali Shetani anafanya kazi kwa bidii kuivunja. Hata hivyo, Mungu daima huwakumbusha watu wazingatie zaidi maneno Yake; hiki ndicho kilele cha vita vinavyotanda katika ulimwengu wa kiroho. Inaweza kusemwa kwa njia hii: Kile ambacho Mungu anataka kufanya ndani ya mwanadamu ndicho ambacho Shetani anataka kuharibu hasa, na kile ambacho Shetani anataka kuharibu kinaonyeshwa kupitia katika mwanadamu, bila kufichwa hata kidogo. Kuna mifano ya wazi ya kile ambacho Mungu hufanya ndani ya watu: Hali zao zinaendelea kuwa bora zaidi na zaidi. Pia kuna maonyesho ya wazi ya uharibifu wa Shetani ndani ya wanadamu: Wanazidi kuwa wapotovu, na hali zao zinazidi kuzorota. Punde hali zinapokuwa duni kabisa, wanakuwa na uwezekano wa kutekwa na Shetani. Hii ndiyo hali halisi ya kanisa, kama ilivyoonyeshwa katika maneno ya Mungu, na pia ndiyo hali halisi ya ulimwengu wa kiroho. Ni onyesho la elimumwendo za ulimwengu wa kiroho. Ikiwa watu hawana imani ya kushirikiana na Mungu, basi wamo katika hatari ya kutekwa na Shetani. Huu ni ukweli. Ikiwa mtu anaweza kweli kuutoa moyo wake kikamilifu ili Mungu aumiliki, basi hivyo ni kama vile Mungu alivyosema: “... ambaye, wakati ako mbele Yangu, anaonekana kuwa katika kumbatio Langu, akionja joto lake.” Hili linaonyesha kuwa mahitaji ya Mungu kwa wanadamu si ya juu; Anawahitaji tu wainuke na kushirikiana na Yeye. Je, hili si jambo rahisi na la furaha? Je, hiki ndicho kitu kimoja ambacho kimemfadhaisha kila shujaa na mtu mkubwa? Ni kama kwamba majemadari walikuwa wamechukuliwa kutoka kwenye uwanja wa vita na walazimishwe kushona badala yake—“mashujaa” hawa wamelemazwa na ugumu, na hawajui la kufanya.

Kipengele chochote cha mahitaji ya Mungu kwa wanadamu kilicho kikubwa zaidi, hicho ndicho kipengele ambacho kwacho mashambulio ya Shetani kwa binadamu yatakuwa makali zaidi, na hivyo, hali za watu wote zinafunuliwa ipasavyo. “Ni yupi kati yenu mliosimama mbele Yangu atakuwa safi kama theluji na asiye na lawama kama jiwe la thamani?” Watu wote bado wanamrairai Mungu na kuficha vitu kutoka Kwake; bado wanatekeleza njama zao maalum. Hawajaweka mioyo yao kabisa mikononi mwa Mungu ili kumridhisha, lakini wanatamani kupata thawabu Zake kwa kuwa wenye shauku. Watu wanapokula chakula kitamu, wanamweka Mungu kando, wakimwacha Akisimama pale, akisubiri “kushughulikiwa”; watu wanapokuwa na mavazi mazuri, wao husimama hapo mbele ya kioo, wakifurahia uzuri wao wenyewe, na ndani ya mioyo yao, hawamridhishi Mungu. Wanapokuwa na hadhi, wanapokuwa na starehe za anasa, wao hukaa hapo juu ya hadhi zao na kuanza kufurahia, lakini hawajinyenyekezi kwa sababu ya kuinuliwa na Mungu. Badala yake, wao husimama katika maeneo yao ya juu, wakiongea maneno yao ya kifahari, na hawazingatii uwepo wa Mungu, wala hawatafuti kujua thamani Yake. Watu wanapokuwa na mungu mioyoni mwao, au mioyo yao inapokuwa imechukuliwa na mtu mwingine, inamaanisha kuwa tayari wamekataa uwepo wa Mungu, kana kwamba Yeye ni mdukizi mioyoni mwao. Wanaogopa kwamba Mungu ataiba upendo wa wengine kwao na kwamba baadaye watahisi upweke. Kusudi la asili la Mungu ni kwamba hakuna kitu duniani kinapaswa kuwafanya watu wampuuze, na ingawa kunaweza kuwa na upendo kati ya watu, bado Mungu hawezi kufukuzwa kutoka katika “upendo” huu. Vitu vyote vya kidunia ni tupu—hata hisia kati ya watu ambazo haziwezi kuonekana au kuguswa. Bila uwepo wa Mungu, viumbe vyote vitarudi kuwa bure. Duniani, watu wote wana vitu ambavyo wanapenda, lakini hakuna mtu ambaye amewahi kuyachukua maneno ya Mungu kama kitu anachopenda. Hii inaamua kiwango ambacho watu wanayaelewa maneno Yake. Ingawa maneno Yake ni makali, hakuna mtu anayejeruhiwa nayo, kwa maana watu hawayatilii maanani kwa kweli; badala yake, wanayachunguza kama wanavyolichunguza ua. Hawachukulii maneno Yake kama matunda ili waweze kuyaonja wenyewe, kwa hivyo hawajui kiini cha maneno ya Mungu. “Kama wanadamu wangeweza kweli kuona ukali wa upanga Wangu, wangekimbia kwa hofu hadi ndani ya mashimo kama panya.” Mtu aliye katika hali ya mtu wa kawaida, baada ya kusoma maneno ya Mungu, atakuwa mwenye kushangaa, aliyejaa aibu na asiyeweza kuonana na wengine. Hata hivyo, siku hizi, watu ni kinyume kabisa—wao huyatumia maneno ya Mungu kama silaha kuwapiga wengine. Kwa kweli hawana aibu!

Matamko ya Mungu yametuleta katika hali hii ya kuwepo: “Ndani ya ufalme, si tu kwamba matamko hutoka kinywani Mwangu, lakini miguu Yangu inatembea kwa heshima kila mahali katika nchi zote.” Katika vita kati ya Mungu na Shetani, Mungu anashinda kila hatua ya njia. Anapanua kazi Yake kwa kiwango kikubwa katika ulimwengu wote, na inaweza kusemwa kwamba kila mahali kuna nyayo za miguu Yake na ishara za ushindi Wake. Katika njama zake, Shetani anatumaini kuharibu usimamizi wa Mungu kwa kuzigawanya nchi, lakini Mungu amechukua fursa ya kusalimu amri huku kupanga upya ulimwengu mzima—ingawa si ili kuuangamiza wote. Mungu hufanya kitu kipya kila siku, lakini watu hawajatambua. Hawazingatii elimumwendo za ulimwengu wa kiroho, kwa hivyo hawawezi kuiona kazi mpya ya Mungu. “Ndani ya ulimwengu, kila kitu huangaza kama kipya katika mwangaza wa utukufu Wangu, kikitoa kipengele chenye kufurahisha ambacho hufurahisha akili na kuinua roho za watu, kana kwamba uko katika mbinguni iliyo zaidi ya mbingu, kama inavyodhaniwa katika fikira za binadamu, ambazo hazijanajisiwa na Shetani na zisizo na mashambulizi ya maadui wa nje.” Hii inatabiri tukio la kufurahisha la ufalme wa Kristo duniani, na pia inaijulisha hali ya mbingu ya tatu kwa wanadamu: Ni vitu hivyo vitakatifu pekee ambavyo ni vya Mungu ndivyo vipo huko, bila mashambulizi yoyote ya nguvu za Shetani. Lakini kilicho muhimu zaidi ni kuwaruhusu watu kuona hali za kazi hapa duniani kwa Mungu Mwenyewe: Mbingu ni mbingu mpya, na kuifuata, vivyo hivyo dunia inafanywa upya. Kwa sababu haya ni maisha chini ya mwongozo wa Mungu, watu wote wana furaha isiyo na kipimo. Katika ufahamu wao, Shetani ni “mfungwa” wa wanadamu, na hawaogopi au huogopa kwa sababu ya uwepo wake. Kwa sababu ya maagizo ya moja kwa moja na mwongozo kutoka kwa Mungu, njama zote za Shetani zimekuwa bure, na hili hata linatosha kuthibitisha kwamba Shetani hayupo tena, kwa kuwa ameangamizwa na kazi ya Mungu. Hiyo ndiyo maana inasemekana, “... uko katika mbinguni iliyo zaidi ya mbingu.” Mungu aliposema, “Hakuna usumbufu umewahi kutokea, wala ulimwengu haujawahi kugawanyika,” Alikuwa akimaanisha hali ya ulimwengu wa kiroho. Hili ni thibitisho kwamba Mungu anatangaza ushindi juu ya Shetani, na ni ishara ya ushindi wa mwisho wa Mungu. Hakuna mwanadamu anayeweza kubadilisha mawazo ya Mungu, wala hakuna anayeweza kuyajua. Ingawa watu wamesoma maneno ya Mungu na kuyachunguza kwa uzito, bado wanashindwa kuonyesha kiini chake. Kwa mfano, Mungu alisema, “Ninaruka kwa kupaa juu ya nyota, na jua linapotoa miali yake, Ninalizuia joto la miali hiyo, Nikituma chembe kubwa za theluji kiwango cha manyoya ya bata bukini yakielea kwenda chini kutoka katika mikono Yangu. Hata hivyo, Ninapobadili mawazo Yangu, theluji yote inayeyuka na kuwa mto, na papo hapo, majira ya kuchipua yameibuka kila mahali chini ya anga na zamaradi ya kijani imeyageuza mazingira yote juu ya dunia.” Ingawa watu wanaweza kufikiria maneno haya katika akili zao, kusudi la Mungu si rahisi sana. Wakati kila mtu aliye chini ya mbingu amepigwa na bumbuwazi, Mungu hutamka sauti ya wokovu, na hivyo kuiamsha mioyo ya watu. Hata hivyo, kwa sababu misiba ya kila aina inawapata, wanahisi hali ya ukiwa ya ulimwengu, kwa hivyo wote wanatafuta kifo na wanaishi katika mapango baridi yenye barafu. Wanagandizwa na baridi ya dhoruba kubwa ya theluji, kiasi kwamba hawawezi kuishi kwa sababu ya ukosefu wa joto duniani. Ni kwa sababu ya upotovu wa watu ndiyo wanauana kwa ukatili zaidi na zaidi. Na kanisani, watu wengi watamezwa kwa mmezo mmoja na joka kubwa jekundu. Baada ya majaribu yote kupita, usumbufu wa Shetani utaondolewa. Ulimwengu mzima, katikati ya mabadiliko, hivyo utapenyezwa na msimu wa kuchipua, joto litaifunika dunia, na dunia itajaa nguvu. Hizi zote ni hatua za mpango mzima wa usimamizi. “Usiku” ambao Mungu alizumngumzia unarejelea wakati ambapo wazimu wa Shetani atafika kilele chake, tukio ambalo litatokea usiku. Je, hilo silo linalofanyika hivi sasa? Ingawa watu wote huishi chini ya mwongozo wa nuru ya Mungu, wanapitishwa katika taabu za giza la usiku. Ikiwa hawawezi kuepuka pingu za Shetani, wataishi milele katikati ya usiku wenye giza. Tazama nchi za dunia: Kwa sababu ya hatua za kazi ya Mungu, nchi za dunia “zinakimbia huku na kule,” na kila moja “inatafuta hatima yake inayofaa.” Kwa sababu siku ya Mungu bado haijafika, kila kitu duniani kinabaki katika mchafuko wa matope. Wakati atakapoonekana wazi kwa ulimwengu wote, utukufu Wake utaujaza Mlima Sayuni, na vitu vyote vitakuwa taratibu na safi, kwa kuwa vitapangwa na mikono Yake. Maneno ya Mungu hayazungumzi kuhusu leo tu, lakini pia yanatabiri kesho. Leo ni msingi wa kesho, kwa hivyo, kama ilivyo leo, hakuna mtu anayeweza kuyaelewa maneno ya Mungu kikamilifu. Ni baada tu ya maneno Yake kutimizwa kikamilifu ndipo wanadamu wataweza kuyaelewa kikamilifu.

Roho wa Mungu anajaza nafasi yote katika ulimwengu, lakini Yeye pia hufanya kazi ndani ya watu wote. Hivyo, katika mioyo ya watu, ni kana kwamba umbo la Mungu liko kila mahali na kila mahali pana kazi ya Roho Wake. Kwa kweli, kusudi la kuonekana kwa Mungu katika mwili ni kuwashinda mifano hawa halisi wa Shetani na mwishowe kuwapata. Akiwa anafanya kazi katika mwili, hata hivyo, Roho pia anashirikiana na mwili kuwabadilisha watu hawa. Inaweza kusemwa kuwa matendo ya Mungu yanaenea katika ulimwengu mzima na kwamba Roho Wake anaujaza ulimwengu mzima, lakini kwa sababu ya hatua za kazi Yake, wale wanaofanya uovu hawajaadhibiwa, huku wale ambao hutenda mema hajatuzwa. Kwa hivyo, vitendo Vyake havijasifiwa na watu wote wa ulimwengu. Yeye yuko juu na ndani ya vitu vyote; aidha, Yeye yuko miongoni mwa watu wote. Hili linatosha kuonyesha kuwa Mungu hakika yupo. Kwa sababu hajawaonekania wanadamu wote waziwazi, wamekuwa na fikira za uwongo kama vile, “Kulingana na binadamu, Mimi kwa kweli nipo, lakini pia naonekana kutokuwepo.” Kati ya wale wote ambao sasa wanaamini katika Mungu, hakuna mtu aliye na uhakika kabisa, asilimia mia moja kwamba Mungu kwa kweli yupo; wote wanashuku asilimia sitini na kuamani asilimia arubaini. Hivi ndivyo wanadamu walivyo sasa. Watu wote siku hizi wako katika hali ifuatayo: Wanaamini kwamba kuna Mungu, lakini hawajamwona; au, hawaamini kuwa kuna Mungu, lakini wana shida nyingi ambazo wanadamu hawawezi kutatua. Inaonekana kila wakati kuna kitu ambacho kinawashikilia ambacho hawawezi kukikimbia. Hata ingawa wanamwamini Mungu, inaonekana kwamba kila wakati wao huhisi ukosefu wa uyakinifu. Hata hivyo, ikiwa hawaamini, wanaogopa kupoteza iwapo itatukia kwamba Yupo. Hii ndiyo hisia yao kinzani.

“Kwa ajili ya jina Langu, kwa ajili ya Roho Wangu, na kwa sababu ya mpango Wangu mzima wa usimamizi, ni nani anayeweza kutoa nguvu zake zote?” Mungu pia alisema, “Leo, wakati ambao ufalme upo katika ulimwengu wa wanadamu, ni wakati ambao Nimekuja binafsi miongoni mwa binadamu. Je, kuna yeyote ambaye anaweza kujitokeza aende kwenye uwanja wa vita kwa niaba Yangu bila hofu yoyote?” Kusudi la maneno ya Mungu ni hili: Isingekuwa kwa sababu ya Mungu mwenye mwili kufanya kazi Yake ya kiungu moja kwa moja, au Yeye asingekuwa mwenye mwili lakini badala yake Afanye kazi kupitia wahubiri, basi Mungu asingeweza kamwe kulishinda joka kubwa jekundu, wala Asingeweza kamwe kutawala kama Mfalme miongoni mwa wanadamu. Wanadamu wasingeweza kumjua Mungu Mwenyewe katika uhalisi, kwa hivyo huu bado ungekuwa utawala wa Shetani. Hivyo, hatua hii ya kazi lazima ifanywe na Mungu binafsi, kupitia katika mwili. Kama mwili ungebadilishwa, basi hatua hii ya mpango haingekamilika kamwe, kwa sababu umuhimu na kiini cha mwili ulio tofauti visingekuwa sawa. Watu wanaweza tu kuelewa maana halisi ya maneno haya, kwa sababu Mungu huelewa kiini. Mungu alisema, “Hata hivyo, baada ya yote, hakuna mtu anayeelewa ikiwa hii ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili. Itawachukua watu maisha yote kupitia jambo hili moja.” Watu wamepotoshwa na Shetani kwa miaka mingi sana, na walipoteza ufahamu wao wa mambo ya kiroho zamani. Kwa sababu hii, sentensi moja tu ya maneno ya Mungu ni kama karamu kwa macho ya watu. Kwa sababu ya umbali kati ya Roho na mapepo, wale wote wamwaminio Mungu wanahisi hisia ya kumtamani sana, na wote wako tayari kuwa karibu na Yeye na kumimina mioyo yao. Hata hivyo, hawathubutu kuwasiliana na Yeye, na badala yake wanabaki wakistahi. Hii ni nguvu ya kuvutia inayomilikiwa na Roho. Kwa sababu Mungu ni Mungu wa kupendwa na watu, na ndani Yake kuna vitu visivyo na mwisho vya wao kupenda, kila mtu anampenda na kila mtu anatamani kumwambia siri. Kwa kweli, kila mtu ana upendo kwa Mungu moyoni mwake—ni kwamba tu vurugu ya Shetani imewazuia watu wasiohisi, wapumbavu, wenye kuhurumiwa kumjua Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu alizungumza juu ya hisia za kweli ambazo wanadamu wanazo Kwake: “Wanadamu hawajawahi kunichukia ndani ya vina vya mioyo yao; badala yake, wananishikilia katika vina vya roho zao. … Uhalisi Wangu unawaacha wanadamu wasijue la kufanya, wakipigwa na butwaa na kukanganyikiwa, na bado wako tayari kuukubali.” Hii ndiyo hali halisi ndani kabisa ya mioyo ya wale wanaomwamini Mungu. Watu wanapomjua Mungu kweli, mtazamo wao Kwake hubadilika kwa kawaida, na wanaweza kutamka sifa kutoka ndani ya vina vya mioyo yao kwa sababu ya kazi ya roho zao. Mungu yuko ndani ya vina vya roho za watu wote, lakini kwa sababu ya upotoshaji wa Shetani, watu wamekanganyikiwa kujua tofauti kati ya Mungu na Shetani. Kazi ya Mungu leo inaanza na shida hii hasa, na katika ulimwengu wa kiroho, imekuwa lengo la vita tangu mwanzo hadi mwisho.

Iliyotangulia: Sura ya 14

Inayofuata: Sura ya 16

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp