Sura ya 14

Mwanadamu hajawahi kamwe kujifunza chochote kutoka kwa neno la Mungu. Badala yake, mwanadamu huthamini tu umbo la nje la neno la Mungu, lakini kutojua maana yake halisi. Kwa hivyo, ingawa wengi wa watu wanapenda neno la Mungu, Mungu asema kwamba hawalithamini kwa kweli. Hili ni kwa sababu katika maoni ya Mungu, hata ingawa neno Lake ni kitu cha thamani, watu hawajaonja utamu wake halisi. Kwa hivyo, wanaweza tu “kukata kiu chao na mawazo ya matunda kama zambarau,” na hivyo kutuliza mioyo yao yenye tamaa. Roho wa Mungu hafanyi tu kazi miongoni mwa watu wote, pia kuna kupata nuru kwa neno la Mungu. Ni vile tu watu hawajali sana kiasi kwamba hawawezi kuthamini kweli kiini chake. Katika akili ya mwanadamu, sasa ndiyo enzi ya ufalme inatambuliwa kabisa, lakini kwa kweli huu si ukweli. Ingawa kile ambacho Mungu hutabiri ni kile ambacho Amefanikisha, ufalme halisi bado haujawasili duniani kabisa. Badala yake, pamoja na mabadiliko katika wanadamu, pamoja na maendeleo katika kazi, na pamoja na umeme unaotoka Mashariki, yaani, pamoja na kuzidi kwa neno la Mungu, ufalme utajitokeza polepole duniani, utakuja duniani polepole lakini kwa ukamilifu. Mchakato wa kuwasili kwa ufalme pia ni mchakato wa kazi takatifu duniani. Wakati huo huo, kotekote ulimwenguni, Mungu ameanza kazi ambayo haijafanywa katika enzi zote katika historia nzima: Kuupanga ulimwengu mzima upya. Kwa mfano, mabadiliko makubwa mno yanaonekana kotekote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika Taifa la Israeli, mapinduzi ya serikali Marekani, mabadiliko katika Misri, mabadiliko katika Mwungano wa Baraza la Kirusi, na kuangushwa kwa Uchina. Wakati ambapo ulimwengu wote utakuwa umetulia na utakuwa umerudishwa kuwa kawaida, huo ndio wakati ambapo kazi ya Mungu duniani itakamilishwa; huo ndio wakati ambapo ufalme utakuja duniani. Hii ni maana ya kweli ya maneno “Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima.” Mungu hawafichi wanadamu chochote, Amewaambia watu siku zote kuhusu utajiri Wake wote, lakini hawawezi kuelewa maana Yake, wao hukubali tu neno Lake kama wapumbavu. Katika hatua hii ya kazi, wanadamu wamejifunza kutoeleweka kwa Mungu, na zaidi ya hayo, wanaweza kutambua vyema ugumu wa kazi ya kumfahamu; kwa sababu hii, wamehisi kwamba siku hizi, kumwamini Mungu ni jambo gumu zaidi kufanya, sawa na kumfundisha nguruwe kuimba. Hawana uwezo kabisa kama panya aliyekwama ndani ya mtego. Kwa kweli, haijalishi mtu ana nguvu kiasi gani au jinsi ujuzi wa mtu ulivyo stadi, au kama mtu ana uwezo usio na kikomo ndani yake, inapohusu neno la Mungu mambo haya hayana maana yoyote. Ni kana kwamba wanadamu ni rundo la jivu la karatasi lililoteketea machoni pa Mungu, bila thamani yoyote kabisa, sembuse matumizi yoyote. Hiki ni kielezo kamili cha maana ya kweli ya maneno “Nimekuwa, kwa maoni yao, Nimefichwa zaidi na zaidi kutoka kwake na Nikazidi kutoeleweka na wao.” Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba kazi ya Mungu hufuata uendeleaji wa kawaida na hutekelezwa kutegemea kile ambacho ogani za wanadamu za utambuzi zinaweza kuelewa. Wakati ambapo asili ya wanadamu ni imara na thabiti, maneno anenayo Mungu hupatana kabisa na dhana zao na huonekana kana kwamba dhana za Mungu na za wanadamu ni kitu kimoja, bila tofauti yoyote kabisa. Hili huwafanya watu waujue uhalisi wa Mungu kwa kiasi fulani, lakini hili silo lengo kuu la Mungu. Mungu anawaruhusu watu kutulia kabla ya kuanza rasmi kazi Yake ya kweli duniani. Kwa hivyo, wakati wa mwanzo huu ambao ni wa kuwatatanisha wanadamu, wanadamu wanatambua kwamba mawazo yao ya awali hayakuwa sahihi na kwamba Mungu na mwanadamu wanatofautiana kama mbingu na dunia na hawafanani kabisa. Kwa sababu maneno ya Mungu hayawezi tena kutathminiwa kutegemea dhana za wanadamu, mwanadamu mara moja anaanza kumfahamu Mungu vinginevyo, na kwa sababu hii anaanza kumkazia Mungu macho kwa mshangao, kana kwamba Mungu wa vitendo ni mkali kama Mungu asiyeonekana na Asiyegusika, kana kwamba mwili wa Mungu uko nje pekee na hauna kiini Chake. Licha ya ukweli kwamba Roho wa Mungu amepata mwili, Anaweza kujigeuza kuwa umbo la Roho na kutoweka kwa kuelea wakati wowote; watu wamekuza mtazamo wa hadhari kwa kiasi fulani. Mungu anapotajwa, watu humvisha mavazi na dhana zao, wakisema Anaweza kupanda juu ya mawingu na ukungu, Anaweza kutembea juu ya maji, Anaweza kuonekana na kutoweka ghafla miongoni mwa wanadamu, na wengine hata wana fafanuzi zaidi za kutoa wasifu. Kwa sababu ya kutojua kwa wanadamu na kukosa umaizi, Mungu alisema “wakati wameamini wamenipinga ama kukosea amri Zangu za kitawala, Nafunga macho.”

Wakati ambapo Mungu hufichua upande mbaya na ulimwengu wa ndani wa wanadamu, Yeye daima huwa sahihi kabisa, bila mkengeuko hata kidogo. Hata inaweza kusemwa kwamba hakuna kosa kwa vyovyote vile. Hili ni thibitisho linalowaridhisha watu kabisa. Kwa sababu ya kanuni ya kazi ya Mungu, mengi ya maneno Yake na matendo huacha alama ambayo haiwezi kufutwa, na watu huonekana kuwa na hata ufahamu mkubwa zaidi kumhusu Yeye, kana kwamba wanagundua mambo ambayo ni ya thamani zaidi ndani Yake. “Kwa kumbukumbu zao, mimi ni Mungu anayeonyesha huruma kwa wanadamu badala ya kuwarudi, ama Mimi ni Mungu Mwenyewe asiyemaanisha Anachokisema. Haya yote ni mawazo yanayotokana na fikira za wanadamu na sio kwa mujibu na ukweli.” Ingawa wanadamu hawajawahi kamwe kutilia maanani uso halisi wa Mungu, wanajua “upande wa kando wa tabia Yake” vizuri sana; wao daima hutafuta makosa katika maneno na matendo ya Mungu. Hili ni kwa sababu wanadamu huwa radhi kila mara kuzingatia vitu hasi, na kupuuza vitu vya hakika, wakidunisha tu matendo ya Mungu. Kadri Mungu anavyosema kwamba Yeye hujificha kwa unyenyekevu katika makao Yake, ndivyo binadamu wanavyomwekea Yeye madai mengi zaidi. Wanasema, “Ikiwa Mungu mwenye mwili anatazama kila kitendo cha binadamu na kupitia maisha ya binadamu, kwa nini kwamba wakati mwingi Mungu hajui kuhusu hali zetu halisi? Je, lina maana kwamba Mungu amejificha kweli?” Ingawa Mungu hutazama ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu, Yeye bado hufanya kazi kufuatana na hali halisi za wanadamu, bila kuwa asiye yakini wala wa mwujiza. Ili kuondoa kabisa tabia ya zamani ndani ya wanadamu, Mungu ametumia kila juhudi kunena kutokana na mitazamo mbalimbali: Akifunua asili yao halisi, Akitamka hukumu kwa uasi wao; wakati mmoja Akisema Atashughulikia watu wote, na wakati mwingine Akisema Ataokoa kundi la watu; ama Akiwapa wanadamu masharti au Anawaonya; kwa zamu Akichangua sehemu yao ya ndani, kwa zamu Akitoa matibabu. Hivyo, chini ya uongozi wa neno la Mungu, ni kana kwamba wanadamu walikuwa wamesafiri kwenda kwa kila pembe ya dunia na wakaingia katika bustani karimu ambapo kila ua linashindana kuwa zuri kupita yote. Chochote asemacho Mungu wanadamu wataingia katika neno Lake, kana kwamba Mungu ni sumaku na chochote chenye chuma kitavutiwa kwake. Wanapoona maneno “Binadamu hawanitambui, hivyo nami pia Siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora?” inaonekana watu wote wa Mungu wameangushwa kuzimu tena, au kugongwa tena katika sehemu zao za uhai, wakiwachwa wameshtuka kabisa. Hivyo, wao wanaingia tena katika mbinu. Wanatatanishwa hasa kuhusiana na maneno “Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wako, utachukiwa na kukataliwa na Mimi!” Watu wengi sana wamesababishwa kuwa na machozi ya kuhuzunisha sana: “Nilikuwa na wakati mgumu kujiondoa kuzimu, kwa hiyo Singekuwa na tumaini kabisa ikiwa Ningeanguka ndani yake tena. Sijapata chochote katika ulimwengu wa wanadamu, nikipitia kila aina ya taabu na matatizo katika maisha yangu. Hasa, baada ya kuingia katika imani, nilipitia hali ya kuachwa na wapendwa, mateso kutoka kwa familia, kashfa kutoka kwa watu wa dunia, na sikufurahia raha ya ulimwengu. Nikianguka tena kuzimu, maisha yangu hayatakuwa bure hata zaidi?” (Kadri mwanadamu anavyofikiria kuhusu hili ndivyo anavyohisi huzuni zaidi.) “Matumaini yangu yote yamekabidhiwa mikononi mwa Mungu. Mungu akiniacha, heri nife sasa…. Kwa hakika, yote yamejaaliwa na Mungu, sasa naweza tu kutaka kumpenda Mungu, mengine yote ni ya baadaye. Ni nani alifanya hili kuwa majaaliwa yangu?” Kadri mwanadamu anavyofikiria, ndivyo anavyokuwa karibu zaidi na viwango vya Mungu na kusudi la maneno Yake. Kwa njia hii lengo la maneno Yake linatimizwa. Baada ya wanadamu kuyaona maneno ya Mungu wote huwa na mapambano ya itikadi ndani yao. Chaguo lao pekee ni kutii masharti ya majaaliwa, na kwa njia hii lengo la Mungu hutimizwa. Kadri maneno ya Mungu yalivyo makali, ndivyo ulimwengu wa ndani wa wanadamu unavyokuwa mgumu zaidi kufahamika kutokana na hilo. Huku ni kama kugusa kidonda; kadri kinavyoguswa kwa nguvu ndivyo kinavyouma zaidi, kiasi kwamba wanakaribia kifo na hata kukata tamaa ya kuendelea kuishi. Kwa njia hii, wakati ambapo wanadamu huteseka zaidi tu na wakiwa wamezama katika kutaka tamaa ndipo wanaweza kutoa mioyo yao halisi kwa Mungu. Asili ya wanadamu ni kwamba hata chembe ya tumaini ikibaki hawatamwendea Mungu kupata msaada, lakini watachukua mbinu za kujitosheleza za kuendelea kudumu kwa kawaida. Hili ni kwa sababu asili ya wanadamu ni ya kujidai, na wao humdharau kila mtu. Kwa hivyo, Mungu alisema: “hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake.” Hili kweli ni la kusikitisha: Mungu aliwaumba wanadamu, lakini Anapokuja kwa ulimwengu wa wanadamu, watu hutaka kumpinga na humfukuza kutoka kwa eneo lao, kana kwamba Yeye ni yatima fulani tu, akielea duniani, au kama mtu wa dunia asiye na nchi. Hakuna mtu anayehisi kumpenda Mungu sana, hakuna mtu anayempenda kweli, hakuna mtu ambaye amekaribisha kuja kwake. Badala Yake, wanapoona kuja kwa Mungu, kufumba na kufumbua nyuso zao za furaha huwa na huzuni, kana kwamba dhoruba ya ghafula inakaribia, kana kwamba Mungu angeondoa raha ya familia zao, kana kwamba Mungu hakuwahi kamwe kuwabariki wanadamu, lakini badala yake Alikuwa Amewapa wanadamu taabu. Kwa hivyo, katika akili za wanadamu, Mungu si mwandani kwao, lakini Yule ambaye daima huwalaani; kwa hivyo, wanadamu hawamtilii maanani, hawamkaribishi, kila mara wao huwa hasimu Kwake, na hili halijawahi kubadilika kamwe. Kwa sababu wanadamu wana mambo haya katika mioyo yao, Mungu asema wanadamu hawana akili na ni waovu, na kwamba hata hisia ambazo wanadamu kwa kuwazia wamejizatiti nazo haziwezi kuonekana ndani yao. Wanadamu hawadhihirishi fikira yoyote kwa hisia za Mungu, lakini hutumia kinachoitwa “haki” kumshughulikia Mungu. Wanadamu wamekuwa hivi kwa miaka mingi na kwa sababu hii Mungu amesema tabia yao haijabadilika. Hili linaonyesha wazi kwamba hawana dutu linalozidi manyoya machache. Inaweza kusemwa kwamba wanadamu ni wanyonge wasio na thamani kwa sababu hawajithamini. Kama hata hawajipendi, bali hujikandamiza, hili halionyeshi kwamba hawana thamani? Wanadamu ni kama mwanamke mwovu ambaye hujihadaa na ambaye hujitoa kwa wengine kwa hiari kuingiliwa bila heshima. Lakini hata hivyo, bado hawajui vile walivyo duni. Wao hufurahia kuwatumikia wengine, au kuzungumza na wengine, kujiweka chini ya utawala wa wengine; huu kweli si uchafu wa wanadamu? Ingawa Sijapitia maisha miongoni mwa wanadamu, kwa vile Sijapitia kweli maisha ya binadamu, Nina ufahamu kamili wa kila mwendo, kila hatua, kila neno, na kila kitendo cha mwanadamu. Naweza hata kuwaweka wanadamu wazi mpaka waaibike kabisa, kiasi cha kutoweza tena kuthubutu kuonyesha hila zao na kutoweza tena kuthubutu kujiachilia kwa tamaa zao. Kama konokono ambaye hurudi ndani ya kombe lake, hawathubutu tena kuonyesha hali zao mbaya. Kwa sababu wanadamu hawajijui, dosari yao kubwa sana ni kuonyesha kwa hiari haiba yao mbele ya wengine, wakionyesha sura yao mbaya; Hiki ni kitu ambacho Mungu hukichukia zaidi. Kwa sababu mahusiano kati ya watu si ya kawaida, na hakuna mahusiano ya kawaida ya mtu mmoja na mwingine kati ya watu, sembuse uhusiano wa kawaida kati yao na Mungu. Mungu amesema mengi sana, na kwa kufanya hivyo lengo Lake kuu ni kumiliki nafasi ndani ya mioyo ya wanadamu, kuwafanya watu waondoe sanamu zote ndani ya mioyo yao, ili Mungu aweze kuwatawala wanadamu wote na Atimize lengo Lake la kuwa duniani.

Iliyotangulia: Sura ya 13

Inayofuata: Sura ya 15

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp