Sura ya 3

Leo si tena Enzi ya Neema, wala enzi ya rehema, bali ni Enzi ya Ufalme ambamo watu wa Mungu wanafichuliwa, enzi ambayo kwayo Mungu hufanya mambo moja kwa moja kwa njia ya uungu. Hivyo, katika sura hii cha maneno ya Mungu, Mungu huongoza wale wote ambao wanayakubali maneno Yake katika ulimwengu wa kiroho. Katika aya ya ufunguzi, Anatangulia kufanya maandalizi haya, na ikiwa mtu ana maarifa ya maneno ya Mungu, atafuata nyuki ili apate asali, na ataelewa moja kwa moja kile ambacho Mungu Anatamani kutimiza kwa watu Wake. Hapo kabla, watu walikuwa wanapimwa kupitia cheo cha “wafanya huduma,” na leo, baada ya wao kuathiriwa na majaribu, mafunzo yao huanza rasmi. Aidha, watu lazima wawe na ufahamu mkubwa juu ya kazi ya Mungu katika msingi wa maneno ya wakati uliopita, na wanapaswa kuyaangalia maneno na mtu, na Roho na mtu, kama kitu kimoja kamili kisichoachana—kama kinywa kimoja, moyo mmoja, tendo moja, na chanzo kimoja. Matakwa haya ni matakwa ya kiwango cha juu sana ambayo Mungu Ameyafanya kwa mwanadamu tokea uumbaji. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba Mungu anatamani kutumia sehemu ya jitihada Zake kwa watu Wake, kwamba Anatamani kuonyesha ishara na maajabu kadhaa ndani yao, na, muhimu zaidi, kwamba Anatamani kuwafanya watu wote kutii kazi na maneno yote ya Mungu kikamilifu. Kwa upande mmoja, Mungu Mwenyewe Anashikilia ushuhuda Wake, na kwa upande mwingine, Ameweka matakwa kwa watu Wake, na moja kwa moja Ametoa kwa umma amri ya Mungu ya kiusimamizi: Hivyo, kwa kuwa mnaitwa watu Wangu, mambo hayapo kama yalivyokuwa; mnapaswa kusikiliza na kutii matamshi ya Roho Wangu, fuateni kwa karibu kazi Yangu, na msitenganishe Roho Wangu na mwili Wangu, maana kwa asili Sisi ni wamoja, na Hatujatengana. Katika hili, ili kuwazuia watu wasimpuuze Mungu mwenye mwili, mara nyingine tena msisitizo unawekwa kwa “maana kwa asili Sisi ni wamoja, na Hatujatengana”; kwa sababu kupuuzia huko ni kuanguka kwa mwanadamu, hii kwa mara nyingine tena imeorodheshwa katika amri za Mungu za kiusimamizi. Kisha, Mungu huwataarifu watu juu ya athari za kukosea amri za Mungu za kiusimamizi, bila kuficha kitu chochote, kwa kusema “watapata hasara, na wataweza tu kunywa kutoka kwenye kikombe chao chungu.” Kwa sababu mwanadamu ni dhaifu, baada ya kuyasikia maneno haya hana budi ila kuwa macho dhidi ya Mungu moyoni mwake maana “kikombe chungu” kinatosha kuwafanya watu watafakari kwa muda. Watu wana tafsiri nyingi za hiki “kikombe chungu” ambapo Mungu Anazungumza: kuhukumiwa na maneno au kufukuzwa kutoka katika ufalme, au kutengwa kwa muda fulani, au mwili wa mtu kuharibiwa na Shetani na kuingiwa na pepo wabaya, au kutelekezwa na Roho wa Mungu, au mwili wa mtu kukomeshwa na kupelekwa Kuzimu. Tafsiri hizi ndizo akili za watu zinaweza kutimizwa, na hivyo katika mawazo yao, watu hawawezi kuzizidi. Lakini mawazo ya Mungu si kama ya mwanadamu; ni sawa na kusema “kikombe chungu” hakirejelei chochote kati ya hayo hapo juu, bali ni kwa kiwango cha ufahamu wa watu juu ya Mungu baada ya kushughulikiwa na Mungu. Kulifanya hili lieleweke vizuri zaidi, mtu anapotenga kiholela Roho wa Mungu na maneno Yake, au anatenganisha maneno na mtu, au Roho na mwili ambao Yeye Mwenyewe huuvaa, mtu huyu si kwamba hawezi tu kumjua Mungu katika maneno ya Mungu, lakini pia anapokuwa na shaka kidogo na Mungu—atakuwa na upofu mara kwa mara. Si kama watu wanavyodhani kwamba wameondolewa moja kwa moja; badala yake, pole pole wanaanguka katika adabu ya Mungu—ambayo ni sawa na kusema, wanatumbukia kwenye janga kubwa sana, na hakuna anayeweza kulingana nao, kana kwamba wameingiwa na pepo wabaya, na kana kwamba wao ni nzi wasiokuwa na kichwa, wakigonga vitu kila wanapokwenda. Licha ya hili, bado hawawezi kuondoka. Katika mioyo yao, mambo ni magumu kiasi kisichoelezeka, kana kwamba kuna mateso yasiyoelezeka mioyoni mwao—lakini hawawezi kufungua vinywa vyao, na wanashinda siku nzima wakiwa wamezubaa, wakiwa hawawezi kumhisi Mungu. Ni katika mazingira haya ndipo amri za Mungu za kiusimamizi zinawatisha, kiasi kwamba hawawezi kuliacha kanisa licha ya kutokuwa na furaha—hiki ndicho kile kinachoitwa “mashambulizi ya ndani na ya nje,” na ni vigumu sana watu kuvumilia. Kile kilichosemwa hapa ni tofauti na dhana za watu—na hiyo ni kwa sababu, kwa hali ilivyo, bado wanajua kumtafuta Mungu, na hii hutokea pale ambapo Mungu Anawakwepa, na kitu ambacho ni muhimu zaidi ni kwamba, kama tu mtu asiye muumini, hawawezi kabisa kumhisi Mungu. Mungu hawaokoi moja kwa moja watu kama hao; wakati vikombe vyao chungu vitakapomwagika, hapo ndipo wakati ambapo siku yao ya mwisho itakuwa imewasili. Lakini kwa wakati huu, bado wanatafuta mapenzi ya Mungu, wakitamani kufurahi zaidi kidogo tu—lakini wakati huu ni tofauti na zamani, isipokuwa kama kuna hali mahususi.

Kufuatia hili, Mungu pia Anaelezea kipengele chema kwa wote na hivyo kwa mara nyingine tena wanapata maisha—kwa kuwa, katika nyakati za zamani, Mungu alisema kwamba wafanya huduma hawakuwa na maisha, lakini leo kwa ghafula Mungu huzungumzia juu ya “maisha yaliyomo ndani.” Ni kwa mazungumzo tu ya maisha ndipo watu wanajua kwamba bado kunaweza kuwa na maisha ya Mungu ndani yao. Kwa namna hii, upendo wao kwa Mungu huongezeka mara kadhaa, na wanapata maarifa makubwa zaidi ya upendo na rehema ya Mungu. Hivyo, baada ya kuyaangalia maneno haya, watu wote hutubu makosa yao ya nyuma, na kwa siri wanatokwa na machozi ya toba. Wengi pia, kimyakimya wanaamua kwamba ni lazima wamridhishe Mungu. Wakati mwingine, maneno ya Mungu yanachoma ndani kabisa kwenye mioyo ya watu, na kufanya kuwa vigumu kwa watu kuyakubali, na vigumu kwa watu kuwa na amani. Wakati mwingine, maneno ya Mungu ni ya kweli na ya dhati, na huwafurahisha watu, kiasi kwamba baada ya watu kuwa wameyasoma, ni kama wakati ambapo mwanakondoo anamwona mama yake baada ya miaka mingi ya kupotea. Machozi yanajaa machoni mwao, wanaelemewa na hisia, na wana shauku ya kujirusha kwenye kumbatio la Mungu, wakiwa wamejawa na kikweukweu, wakiondoa maumivu yasiyoelezeka ambayo yamekuwa mioyoni mwao kwa miaka mingi ili kuonyesha utiifu wao kwa Mungu. Kwa sababu ya majaribio ya miezi kadhaa, wamekuwa wepesi kuhisi zaidi kiasi, mfano wa mtu ambaye ana shambulio la neva, kama mtu asiyejiweza ambaye amekaa kitandani kwa miaka mingi. Kuwafanya kuwa wagumu katika imani yao kwa maneno ya Mungu, mara nyingi Mungu anasisitiza yafuatayo: “Ili kwamba hatua inayofuata ya kazi Yangu iweze kuendelea taratibu na bila kizuizi, Ninatumia usafishaji wa maneno kuwajaribu wale wote ambao wapo katika nyumba Yangu.” Hapa, Mungu anasema “kuwajaribu wale wote ambao wapo katika nyumba Yangu”; usomaji wa makini wa maneno haya hutuambia kwamba watu wanapofanya kazi kama watoa huduma, bado ni watu ndani ya nyumba ya Mungu. Aidha, maneno haya husisitiza hali ya ukweli ya Mungu kwa cheo cha “watu wa Mungu,” yakiwaleta watu kipimo cha unafuu katika mioyo yao. Na hivyo kwa nini Mungu huonyesha kwa kurudiarudia ufunuo mwingi kwa watu baada ya wao kusoma maneno ya Mungu, au wakati ambapo neno “watu wa Mungu” halijafichuliwa bado? Ni kuonyesha tu kwamba Mungu ni Mungu ambaye anaangalia ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu? Hii ni sehemu tu ya sababu—na hapa, ni umuhimu tu wa pili. Mungu hufanya hivyo ili kuwafanya watu wote kushawishika kabisa, ili kwamba kila mtu, kutoka kwa maneno ya Mungu, aweze kuelewa udhaifu wake mwenyewe, na kujua mapungufu yake ya wakati uliopita kuhusiana na maisha, na, muhimu zaidi, ili kuweka msingi kwa ajili ya hatua ya kazi inayofuata. Watu wanaweza kujitahidi tu kumjua Mungu na kutaka kumuiga Mungu tu kwa msingi wa kujijua wenyewe. Kwa sababu ya maneno haya, watu hubadilika kutoka kuwa watu hasi na wa kutoonyesha hisia na kuwa na mtazamo mwema na wa kufanya vitendo, na hii huweka mizizi ya sehemu ya pili ya kazi ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, kwa hatua hii ya kazi kama msingi, sehemu ya pili ya kazi ya Mungu inakuwa rahisi, ikihitaji jitihada kidogo tu. Hivyo, wakati watu huondoa huzuni mioyoni mwao na kuwa wenye mtazamo mwema na wa kufanya vitendo, Mungu huitumia vizuri fursa hii ili kufanya matakwa mengine kwa watu Wake: “Maneno Yangu yanatolewa na kuonyeshwa wakati wowote au mahali popote, na hivyo, nyinyi pia, mnapaswa kujijua wenyewe mbele Yangu wakati wote. Kwani leo ni, hata hivyo, tofauti na kile kilichokuja kabla, na hamwezi tena kutimiza chochote mnachotamani. Badala yake, kwa kuongozwa na maneno Yangu, mnapaswa kuweza kuidhibiti miili yenu, mnapaswa kutumia maneno Yangu kama nguzo, na hampaswi kutenda kizembe.” Katika hili, Mungu kimsingi husisitiza “maneno Yangu”; wakati uliopita, pia, Alirejelea “maneno Yangu” mara nyingi, na hivyo, kila mtu hana budi ila kuelekeza uangalifu wake fulani katika hili. Ndivyo kiini cha hatua inayofuata ya kazi ya Mungu kinaonyeshwa: Watu wote watalazimika kuelekeza uangalifu wao kwa maneno ya Mungu, na wasiwe na upendo wowote mwingine. Wote wanapaswa kuyathamini maneno yote yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na si kuyachezea, na hivyo hali iliopita itakuwa imekomeshwa kanisani, wakati mtu angesoma maneno ya Mungu na wengi wangesema amina na kuwa watiifu. Wakati huo, watu hawakujua maneno ya Mungu, lakini waliyachukua kama silaha ya kujilinda wenyewe. Kubadilisha hili, Mungu duniani hufanya matakwa mapya na ya juu kwa mwanadamu. Kuwazuia watu wasiwe hasi na watu wasio wa kuonyesha hisia baada ya kuona viwango vya juu vya Mungu na matakwa magumu, Mungu huwatia moyo watu mara nyingi kwa kusema: “Kwa kuwa mambo yamefikia hali ilivyo leo, hamhitaji kujihisi kutiwa uchungu na kujuta kuhusu matendo yenu ya zamani. Ukarimu Wangu hauna mipaka kama ilivyo bahari na anga—uwezo na ufahamu wa mwanadamu kunihusu Mimi unawezaje kukosa kujulikana Kwangu kama kiganja Changu?” Maneno haya ya kweli na ya dhati ghafula yanafungua akili za watu, na mara moja yanawaondoa katika hali ya kukata tamaa hadi kuwa na upendo kwa Mungu, kuwa wenye mtazamo mwema na wa kufanya vitendo, maana Mungu huzungumza kwa kukamata udhaifu ndani ya mioyo ya watu. Bila kutambua, watu siku zote wanaona haya mbele ya Mungu kwa sababu ya matendo yao ya zamani, na wao huonyesha majuto tena na tena. Hivyo, Mungu hufichua maneno haya hususan kwa uhalisia na kwa kawaida, ili kwamba watu wasihisi kwamba maneno ya Mungu ni magumu na hayana maisha, bali ni makali na laini, na ni dhahiri na kama yenye maisha.

Kuanzia uumbaji hadi leo, Mungu Amepanga kila kitu kwa ajili ya mwanadamu kimyakimya kuanzia ulimwengu wa kiroho, na kamwe hajaelezea ukweli wa ulimwengu wa kiroho kwa mwanadamu. Lakini, leo, ghafula Mungu anaelezea kwa muhtasari vita ambavyo vinaendelea vikali ndani yake, ambavyo kwa asili huwaacha watu wakikuna vichwa vyao, hukuza ufahamu wao kwamba Mungu ni wa maana sana na hawezi kueleweka, na hufanya iwe vigumu zaidi kwao kutambua chanzo cha maneno ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba hali ya kujihami ya ulimwengu wa kiroho huwaleta watu wote katika roho. Hii ni sehemu ya kwanza muhimu ya kazi ya baadaye, na ni dokezo tu ambalo kwalo watu wanaweza kuingia katika ulimwengu wa kiroho. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba hatua inayofuata ya kazi ya Mungu imelengwa hasa roho, lengo la msingi ambalo ni kuwapa watu wote ufahamu mkubwa zaidi wa matendo ya kimiujiza ya Roho wa Mungu ndani ya mwili, hivyo kuwapa wale wote ambao ni watiifu kwa Mungu ufahamu mkubwa wa ujinga wa Shetani na asili ya Shetani. Ingawa hawakuzaliwa katika ulimwengu wa kiroho, wanahisi kana kwamba wamemtazama Shetani, na mara wanapokuwa na hisia hii, Mungu mara moja Anabadilisha kwenda kwa njia nyingine ya kuzungumza—na mara watu wanapokuwa wamepata njia hii ya kufikiri, Mungu huuliza: “Kwa nini Ninawafundisha kwa hali hiyo ya dharura? Kwa nini Ninawaelezea ukweli wa ulimwengu wa kiroho? Kwa nini Ninawakumbusha na kuwaonya mara kwa mara?” Na kadhalika—mfululizo kamili wa maswali yanayoamsha maswali mengi katika akili za watu: Kwa nini Mungu huzungumza katika toni hii? Kwa nini Huzungumza masuala ya ulimwengu wa kiroho, na si matakwa Yake kwa watu katika kipindi cha kujenga kanisa? Kwa nini Mungu hagongi kwenye dhana za watu kwa kufichua siri? Kwa kutafakari kidogo zaidi tu, watu wanapata ufahamu mdogo wa hatua za kazi ya Mungu, na hivyo, wanapokumbana na majaribu hapo baadaye, ndani yao kunazaliwa maana halisi ya kumchukia Shetani. Na hata wanapokabiliana na majaribu hapo baadaye, bado wanaweza kumjua Mungu na kumchukia Shetani kwa kina zaidi, na hivyo kumlaani Shetani.

Mwishoni, mapenzi ya Mungu yote yanafichuliwa kwa mwanadamu: “kuruhusu kila maneno Yangu kukita mzizi kustawi na kuzaa matunda ndani ya roho zenu, na muhimu zaidi kuzaa matunda zaidi. Hiyo ni kwa sababu kile ninachokiomba si maua angavu yaliyostawi sana, bali matunda mengi—matunda, zaidi ya hayo, ambayo hayaharibiki.” Kati ya matakwa ya mara kwa mara ya Mungu kwa watu Wake hili ndilo pana zaidi kwa yote, ni hoja kuu, na limepelekwa mbele kwa njia iliyo ya moja kwa moja. Nimebadilika kutoka kufanya kazi katika ubinadamu wa kawaida hadi kufanya kazi katika uungu kamili; hivyo, katika wakati uliopita, katika maneno Yangu yaliyosemwa waziwazi, hakukuwa na haja Kwangu kuongeza ufafanuzi zaidi, na watu wengi sana waliweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Matokeo yalikuwa ni kwamba, hapo nyuma, yale yote ambayo yalikuwa yanahitajika ni watu kuyajua maneno Yangu na waweze kuzungumza juu ya uhalisia. Hata hivyo, hatua hii, ni tofauti kwa kiasi kikubwa. Uungu Wangu unafanya kazi kabisa, na haujaacha nafasi kwa ubinadamu kuwa mshirika. Hivyo, ikiwa wale miongoni mwa watu Wangu wanatamani kuelewa maana ya kweli ya maneno Yangu, wana shida kubwa sana. Ni kupitia tu matamshi Yangu, ndipo wanaweza kupata mwanga na nuru, na ikiwa si kupitia njia hii, mawazo yoyote ya kuelewa malengo ya maneno Yangu ni ndoto tu bure za mchana. Watu wote watakapokuwa na ufahamu mkubwa zaidi kuhusu Mimi baada ya kukubali matamshi Yangu ni wakati ambapo watu Wangu kuishi kulingana na Mimi, ni wakati ambapo kazi Yangu katika mwili imekamilika, na wakati ambapo uungu Wangu unaishi kwa kudhihirishwa kabisa katika mwili. Wakati huu, watu wote watanitambua Mimi katika mwili, na kweli wataweza kusema kwamba Mungu huonekana katika mwili, na hili litakuwa ndilo tunda. Huu ni ushahidi zaidi kwamba Mungu amechoshwa na ujenzi wa kanisa—yaani, “Ingawa maua katika nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea ni yasiyohesabika kama nyota, na huwavuta watalii wote, mara yanaponyauka yanakuwa mabovu mabovu kama hila danganyifu za Shetani, na hakuna mtu anayevutiwa nayo.” Ingawa Mungu Mwenyewe pia Alifanya kazi wakati wa kipindi cha ujenzi wa kanisa, kwa kuwa Yeye ni Mungu ambaye siku zote ni mpya, na kamwe si mzee, Hana hamu ya mambo yaliyopita. Kuwazuia watu kukumbuka nyakati za nyuma, Alitumia maneno “yanakuwa mabovu mabovu kama hila danganyifu za Shetani,” kitu kinachoonyesha kwamba Mungu hatii mafundisho ya dini. Baadhi ya watu wanaweza kufasiri vibaya mapenzi ya Mungu, na kuuliza: Kama ni kazi iliyofanywa na Mungu, kwa nini Alisema “mara yanaponyauka, hakuna mtu anayevutiwa nayo”? Maneno haya huwapatia watu ufunuo. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba huwafanya watu wote kuwa na mwanzo mpya na sahihi, na baada ya hapo tu ndipo wataweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hatimaye, watu wa Mungu wataweza kumpatia Mungu sifa ambayo ni ya kweli, si ya kulazimishwa, na ambayo inatoka mioyoni mwao. Hiki ndicho kipo katika kiini cha mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000. Yaani, ni udhihirisho wa mpango huu wa usimamizi wa miaka 6,000: kuwafanya watu wote kujua umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu—kuwafanya kumjua Mungu kupata mwili kwa vitendo, ambayo ni kusema, matendo ya Mungu katika mwili—ili kwamba wamkane Mungu asiye yakini, na kumjua Mungu ambaye ni wa leo na pia wa jana, na zaidi ya hilo, Mungu wa kesho, ambaye kwa kweli Ameishi toka milele hadi milele. Ni baada ya hapo tu, ndipo Mungu ataingia pumzikoni!

Iliyotangulia: Sura ya 1

Inayofuata: Sura ya 4

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp