Sura ya 13

Mungu anachukia urithi wote wa joka kubwa jekundu, na Hulichukia joka kubwa jekundu hata zaidi. Huu ni mzizi wa ghadhabu iliyo ndani ya moyo wa Mungu. Inaonekana kwamba Mungu anataka kutupa vitu vyote ambavyo ni mali ya joka kubwa jekundu ndani ya ziwa la moto wa jahanamu kuviteketeza kabisa. Kuna nyakati ambazo hata inaonekana kwamba Mungu anataka kuunyosha mkono Wake kuliangamiza binafsi—hilo tu ndilo lingeweza kufuta chuki iliyo ndani ya moyo Wake. Kila mtu katika nyumba ya joka kubwa jekundu ni mnyama anayekosa ubinadamu, ndiyo maana Mungu alizuia kwa nguvu hasira Yake ili kusema yafuatayo: “Miongoni mwa watu Wangu Wote, na miongoni mwa Wanangu wote, yaani, miongoni mwa wale Niliowachagua kutoka kwa wanadamu wote, unapatikana katika kundi la chini zaidi. …” Mungu ameanza vita vya kuamua mshindi na mshinde dhidi ya joka kubwa jekundu katika nchi yake, na wakati ambapo mpango wake utafaulu Ataliangamiza, Hataliruhusu tena kuwapotosha wanadamu au kuharibu nafsi zao. Hakuna siku ipitayo bila Mungu kuwaita watu Wake ambao wanasinzia ili awaokoe, ilhali wote wameduwaa kana kwamba wamemeza dawa ya usingizi. Asipowaamsha hata kwa dakika moja wanarudi kwa hali yao ya usingizi, bila ufahamu. Inaonekana kwamba watu Wake wote wamepooza kwa thuluthi tatu. Hawajui mahitaji yao wenyewe au kasoro zao wenyewe, au hata wanachopaswa kuvaa au wanachopaswa kula. Inaonyesha kwamba joka kubwa jekundu limetumia kiasi kikubwa cha jitihada kuwapotosha watu. Ubaya wake unafikia kotekote katika kila mkoa wa Uchina. Hata limewafanya watu kuchukizwa na kutokuwa radhi kuishi tena katika nchi hii ya kuharibika, isiyo na adabu. Kile ambacho Mungu huchukia zaidi ni kiini cha joka kubwa jekundu, ndiyo maana Huwakumbusha watu katika ghadhabu Yake kila siku, na watu huishi chini ya ulinzi wa ghadhabu Yake kila siku. Hata hivyo, wengi sana wa watu bado hawajui kumtafuta Mungu, lakini wao huketi tu wakitazama na kungoja kulishwa kwa mkono. Hata kama wangekuwa wana njaa kabisa hawangekuwa radhi kwenda kutafuta chakula chao wenyewe. Dhamiri za watu zilipotoshwa na Shetani kitambo sana na zikabadilika kwa hali kuwa zisizo na huruma. Si ajabu Mungu alisema: “Kama Mimi Singewazindua, bado usingeamka, lakini, mngeendelea kuwa kama mlioganda, na tena, katika hali ya kubumbwaa.” Ni kana kwamba watu walikuwa kama wanyama ndani ya bumbwaa waliokuwa wakipitisha majira ya baridi na hawakutaka kula au kunywa; hii hasa ni hali ya sasa ya watu wa Mungu, ndiyo maana Mungu huwataka tu watu wamjue Mungu mwenye mwili Mwenyewe katika nuru. Hawashurutishi watu wabadilike kiasi kikubwa au wao kuwa na ukuaji mkubwa katika maisha yao. Hilo lingetosha kulishinda joka kubwa jekundu chafu, lenye kutia kinyaa, hivyo kudhihirisha vizuri zaidi nguvu kuu za Mungu.

Watu wanaposoma maneno ya Mungu wanayoweza kufahamu tu ni maana halisi lakini hawawezi kufahamu umuhimu wa kiroho wa maneno hayo. Maneno mawili “mawimbi mabaya” yamemshinda kila shujaa. Ghadhabu ya Mungu inapodhihirishwa, je, maneno Yake, matendo Yake, na tabia Yake si mawimbi yanayopanda na kushuka? Mungu anapowahukumu wanadamu wote, huu si ufichuaji wa ghadhabu Yake? Huu si wakati ambapo mawimbi hayo yanayopanda na kushuka hufanya kazi? Ni nani huyo asiyeishi katikati ya mawimbi yanayopanda na kushuka kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu? Yaani, ni nani asiyeishi katikati ya ghadhabu ya Mungu? Wakati ambapo Mungu anataka kugawa msiba mkuu kwa wanadamu, je, kile ambacho watu huona si “dhoruba na mawingu meusi”? Miongoni mwa wanadamu, ni nani asiyeukimbia msiba mkuu? Ghadhabu ya Mungu inamiminika juu ya watu kama mvua nzito na kuwapeperusha kama upepo mkali. Watu wote wanatakaswa kupitia kwa maneno ya Mungu kana kwamba walikuwa wamekumbana na dhoruba ya theluji izungukayo upesi. Ni maneno ya Mungu ambayo hayatambulikani sana kwa wanadamu. Aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno Yake na pia Anawaongoza na kuwatakasa wanadamu wote kwa kutumia maneno Yake. Na mwisho, Atarudisha tena utakatifu wa ulimwengu wote kwa kutumia maneno Yake. Inaweza kuonekana katika kila sehemu ya maneno Yake kwamba kuweko kwa Roho wa Mungu si uwongo. Watu wanaweza kuona sehemu ya njia ya kuendelea kuishi ndani ya maneno ya Mungu pekee. Watu wote wanaweza kuthamini maneno Yake kwa sababu yana riziki ya maisha. Kadri mwanadamu anavyolenga maneno Yake, ndivyo Atamkabidhi mwanadamu hoja zaidi—hili humfanya kuchanganyikiwa kabisa na akakosa wakati wa kujibu. Maswali ya mfululizo kutoka kwa Mungu pekee yanatosha kwa watu kutafakari mambo kwa muda fulani, sembuse maneno Yake mengine. Ndani ya Mungu, yote ni kamili na tele na hakuna kinachokosekana. Hata hivyo, watu hawana uwezo wa kufurahia mengi ya hayo; wanajua tu upande wa juujuu wa maneno Yake kana kwamba yote ambayo wangeweza kuona ni ngozi ya kuku lakini hawangeweza kula nyama ya kuku. Hili linamaanisha kwamba watu wana uhaba wa bahati kiasi kwamba hawawezi kumfurahia ndani ya Mungu. Katika fikira za watu kila mmoja wao anashikilia Mungu fulani ndani ya moyo wake, ndiyo maana hakuna anayejua Mungu asiye dhahiri ni nini, au sura ya Shetani ni nini. Kwa hiyo Mungu aliposema “kwa sababu unachokiamini ni sura ya Shetani tu na hakihusiani na Mungu kwa njia yoyote. ” watu wote walipigwa bumbuazi kwamba walikuwa wameamini kwa miaka mingi sana, lakini bado hawakuwa wametambua kwamba kile walichokuwa wameamini ni Shetani na si Mungu Mwenyewe. Walihisi uwazi wa ghafula lakini hawakujua la kusema. Wakati huo walianza kuchanganyikiwa tena. Ni kwa kufanya kazi hivi tu ndiyo watu wanaweza kukubali vizuri zaidi nuru mpya na hivyo kukana mambo ya kale. Haijalishi yanavyoonekana kuwa mazuri, hayatakuwa na maana. Ni la manufaa zaidi kwa watu ni kumfahamu Mungu Mwenyewe wa vitendo; hili linawawezesha kujiondolea mioyoni mwao hali ambayo fikira za watu hushikilia humo ndani, na kumruhusu Mungu Mwenyewe awamiliki watu. Ni kwa njia hii tu ndio umuhimu wa kupata mwili unaweza kutimizwa na watu wanaweza kumjua Mungu Mwenyewe wa vitendo kwa macho yao ya mwili.

Mungu amewaambia watu mara nyingi kuhusu hali za ulimwengu wa kiroho. “Shetani anapokuja mbele Yangu, sitetemeki kwa kuuogopa ukali wake, wala kumuogopa kwa sababu ya ubaya wa sura yake: Ninampuuza tu.” Walichoelewa watu kutokana na hili ni hali tu kwa kweli; hawajui ukweli katika ulimwengu wa kiroho. Kwa kuwa Mungu amepata mwili, Shetani ametumia kila aina za mbinu za shutuma, akitaka kumshambulia Mungu kwa njia hii. Hata hivyo, Mungu harudi nyuma kwa sababu ya hili—Anazungumza tu na kufanya kazi miongoni mwa wanadamu na Anawaruhusu watu kumjua kupitia mwili Wake. Shetani amejawa ghadhabu na ametumia kiasi kikubwa cha juhudi kwa watu wa Mungu kuwafanya wawe hasi, warudi nyuma, na hata wapotee njia. Lakini kwa sababu ya athari ya maneno ya Mungu Shetani ameshindwa kabisa, hivyo kuongeza kiwango cha ukali wake. Kwa hivyo, Mungu anamkumbusha kila mtu, “Katika maisha yako, ipo siku itakuja ambayo utakumbana na hali kama hii: Je, utakubali bila kusita kushikwa mateka na Shetani, au utaniruhusu Nikuokoe?” Ingawa watu hawajui mambo yanayotokea katika ulimwengu wa kiroho, punde wasikiapo aina hizi za maneno kutoka kwa Mungu wao hutahadhari na kuogopa—hili hushinda mashambulizi ya Shetani, ambalo linatosha kuonyesha utukufu wa Mungu. Ingawa waliingia katika mbinu mpya ya kufanya kazi zamani sana, watu bado hawana ubayana kuhusu maisha katika ufalme—hata kama wanaelewa, wanakosa ubayana. Kwa hiyo baada ya Mungu kutoa onyo kwa watu, Aliwasilisha kwao kiini cha maisha katika ufalme: “Maisha katika ufalme ni maisha ya watu na Mungu Mwenyewe.” Kwa vile Mungu Mwenyewe amekuwa mwili, maisha ya mbingu ya tatu yametimizwa hapa duniani. Huu si mpango wa Mungu tu, lakini pia unafanikishwa na Mungu. Muda unapoendelea watu huja kumjua Mungu Mwenyewe zaidi na zaidi na hivyo wanaweza zaidi kuonja maisha yaliyo mbinguni, kwa kuwa wamehisi kweli kwamba Mungu yuko duniani, kwamba Yeye si Mungu asiye dhahiri aliye mbinguni. Kwa hiyo, maisha duniani ni sawa na yale yaliyo mbinguni. Ukweli ni kwamba Mungu anakuwa mwili na Anaonja uchungu wa ulimwengu wa binadamu, na kadri Anavyoweza kuonja uchungu huo katika mwili, ndivyo inavyothibitisha zaidi kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe wa vitendo. Hii ndiyo maana maneno yafuatayo yanatosha kuthibitisha utendaji wa Mungu wa leo: “Katika makao Yangu, ambayo ni sehemu Nilipojificha, hata hivyo, katika haya makao Yangu, Nimewashinda maadui Wangu wote; katika makao Yangu, Nimepata uzoefu wa kuishi duniani; katika makao Yangu, Ninalichunguza kila neno na tendo la mwanadamu, na kuchungulia na kuongoza wanadamu wote.” Kuishi katika mwili kwa kweli, kupitia maisha ya mwanadamu katika mwili kwa kweli, kufahamu binadamu wote kutoka ndani ya mwili kwa kweli, kuwashinda wanadamu katika mwili kwa kweli, kupigana vita vya kuamua mshindi na mshinde na joka kubwa jekundu katika mwili kwa kweli, na kufanya kazi yote ya Mungu katika mwili—je, huku hasa si kuweko kwa Mungu Mwenyewe wa vitendo? Ilhali, ni nadra sana kuwapata watu wanaoweza kuona ustadi katika maneno haya ya kawaida yaliyonenwa na Mungu. Wao huyapitiapitia tu, na hawahisi thamani au uadimifu wa maneno ya Mungu.

Maneno ya Mungu hugeuka vizuri sana—msemo “Mwanadamu akiwa kwenye usingizi mzito” unageuza ufafanuzi wa Mungu Mwenyewe kuwa ufafanuzi wa hali ya wanadamu wote. Hapa, “milipuko ya mwanga baridi” hayawakilishi umeme wa Mashariki, lakini ni maneno ya Mungu, yaani, mbinu Yake mpya ya kufanya kazi. Hivyo, katika hili aina zote za nguvu za watu zinaweza kuonekana: Baada ya kuingia katika mbinu mpya, wote wanapoteza mwelekeo wao, wasijue wanakotoka wala wanakoenda. “Watu wengi hufumwa na mwanga huu” yanahusu watu waliotolewa kupitia mbinu mpya, wale wasioweza kuhimili majaribio au kustahamili usafishaji wa mateso na hivyo wanatupwa kuzimu mara nyingine. Neno la Mungu huwafichua wanadamu kwa kiwango fulani—inaonekana kwamba watu huogopa wanapoyaona maneno ya Mungu, na hawathubutu kusema lolote kana kwamba tu wameona mtutu wa bunduki umeelekezwa moja kwa moja kwa mioyo yao. Hata hivyo, wao pia wanahisi kwamba kuna mambo mazuri katika maneno ya Mungu. Mioyo yao imezozana sana na hawajui wanachopaswa kufanya, lakini kwa sababu ya imani yao, yote wafanyayo ni kujizatiti na kutafuta zaidi katika maneno Yake wakihofu kwamba Mungu atawaacha. Kama tu alivyosema Mungu: “ni nani miongoni mwa wanadamu hayumo katika hali sawa na hii? Ni nani hayumo katika mwangaza Wangu? Hata kama wewe ni mwenye nguvu, au hata kama wewe ni mnyonge, ni vipi waweza kuepuka ujio wa mwanga Wangu?” Mungu akimtumia mtu, hata kama ni mnyonge, Mungu bado Atamwangaza na kumpa nuru katika kuadibu Kwake, kwa hivyo kadri watu wanavyosoma maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomfahamu zaidi, ndivyo wanavyomcha zaidi, na ndivyo wanavyopunguza kuthubutu kuwa wazembe. Kwamba watu wamefika hapa leo ni kwa sababu tu ya nguvu kuu za Mungu. Ni kwa sababu ya mamlaka ya maneno Yake, yaani, ni kwa ajili ya Roho aliye ndani ya maneno Yake ndiyo watu wanamcha Mungu. Kadri Mungu anavyofichua sura halisi ya wanadamu, ndivyo wanavyomheshimu zaidi, hivyo ndivyo wanavyokuwa na hakika zaidi kuhusu uhalisi wa kuwepo Kwake. Huu ni mnara wa Mungu ulio njiani kwa wanadamu kumfahamu Mungu; huu ni ujia ambao Mungu amewapa kuufuata. Mkifirikia kwa makini kulihusu, je sivyo?

Je, yaliyosemekana hapo juu si mnara ulio njiani mbele ya wanadamu?

Iliyotangulia: Sura ya 12

Inayofuata: Sura ya 14

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp