Sura ya 36

Inasemekana kwamba Mungu ameanza sasa kuwaadibu watu, lakini hakuna yeyote anayeweza kusema kwa hakika, hakuna yeyote anayeweza kutoa jibu dhahiri iwapo kusudi la asili la kuadibu huku limewafika wanadamu. Mungu asema, “Mwanadamu hajawahi kugundua chochote katika kuadibu Kwangu, kwani hafanyi chochote ila kushika nira inayozunguka shingo kwa mikono miwili, macho yake mawili yakiwa yamekodolewa Kwangu, kana kwamba anamwangalia adui kwa makini—na wakati huu tu ndio Nahisi vile amedhoofishwa. Ni kwa sababu ya hili ndio Nasema hakuna yeyote aliyewahi kusimama imara katikati ya majaribio.” Mungu humwambia mwanadamu kuhusu ukweli wa kuadibu ambao bado haujamfika, na Yeye hufanya hivyo kwa utondoti mkuu, bila kuacha chochote. Ni kana kwamba wameingia katika kuadibu na hawawezi kweli kusimama imara, Mungu anatoa picha dhahiri yenye kufanana na kiumbe chenye uhai ya uso mbaya wa mwanadamu. Hii ndiyo maana wanahisi kushurutishwa: Kwa vile Mungu asema kwamba mwanadamu hajawahi kamwe kusimama imara katikati ya majaribio, Ningekuwaje yule anayevunja rekodi ya dunia, kukubaliwa licha ya mila? Wakati huu, wao huanza kutafakari. Kwa kweli, ni kama tu asemavyo Mungu: “Je, Nimewaleta mpaka ukingoni?” Kwa kweli, Mungu amewafikisha watu wote ukingoni, na kwa hiyo, katika fahamu zao, watu daima huamini kwamba Mungu ni mkatili na asiye na huruma. Mungu amewavua watu wote kutoka kwa bahari la mateso ya dunia, baada ya hilo, “ili kuzuia ajali zozote, Niliwaua ‘samaki’ wote waliokuwa wamevuliwa, baada ya hilo samaki hao wakawa watiifu, na hawakuwa na malalamiko hata kidogo.” Je, huu si ukweli? Mungu amewavuta watu wote kutoka kwa bahari ya machungu ya kifo kuingia katika lindi kuu lingine la kifo, amewakokota wote kwa “jiwe kubwa la chakari,” Amewalazimisha kwenda ukingoni—mbona Hafanyi hili kwa wana na watu wengine wa Mungu? Kusudi Lake la kutekeleza kazi kama hii katika nchi ya joka kubwa jekundu ni lipi? Kwa nini mkono wa Mungu ni wenye “nia mbaya” hivyo? Si ajabu “Ninapomhitaji mwanadamu, daima huwa amejificha. Ni kana kwamba hajawahi kamwe kuona maonyesho ya kustaajabisha, kana kwamba alizaliwa mashambani na hajui chochote kuhusu mambo ya mjini.” Kwa kweli, ndani yao watu huuliza: “Mpango wa Mungu katika kufanya hili ni nini? Je, hatuui? Na ya nini? Kwa nini hatua za kazi Yake huja haraka na kwa wingi idadi kubwa, na kwa nini Yeye si mwenye huruma hata kidogo kwetu?” Lakini watu hawathubutu kusema hili, na kwa kuwa maneno ya Mungu huwafanya waache mawazo kama hayo, yakiwanyima nafasi ya kufikiria zaidi, hawana budi ila kuweka kando mawazo yoyote zaidi kama hayo. Ni vile tu Mungu hufichua dhana zote za mwanadamu, na kwa hivyo watu hulazimisha dhana zao kurudi, bila kuziruhusu kujitokeza. Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu. Mungu anapowalazimisha kufika ukingoni na kuwachinja, basi—bila shaka—roho ya joka kubwa jekundu haina nafasi zaidi ya kufanya kazi ndani yao. Kwa njia hii, watu wanapotembea hadi ukingoni ndio wakati ambapo joka kubwa jekundu hatimaye hufa pia. Inaweza kusemwa kwamba ni kutumia kifo kulipa “wema mkuu wa Mungu”—ambalo ni lengo la kazi ya Mungu katika taifa la joka kubwa jekundu. Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu, na hakuna anayeweza kuwashinda. Ni nini kingekuwa muhimu zaidi kuliko uzima? Hivyo, Shetani anakuwa hawezi kufanya chochote zaidi ndani ya watu, hakuna anachoweza kufanya na mwanadamu. Ingawa, katika ufafanuzi wa “mwili” inasemekana kwamba mwili hupotoshwa na Shetani, kama watu watajitoa kweli, na wasiendeshwe na Shetani, basi hakuna anayeweza kuwashinda—na wakati huu, mwili utatekeleza kazi yake nyingine, na kuanza kupokea rasmi mwongozo wa Roho wa Mungu. Huu ni mchakato wa lazima, lazima ufanyike hatua kwa hatua; la sivyo, Mungu hangekuwa na njia ya kufanya kazi ndani ya mwili mkaidi. Hiyo ndiyo hekima ya Mungu. Kwa njia hii, watu wote wameingia bila kufahamu katika hali za leo. Na je, si Mungu ambaye amewaongoza watu hadi “mwisho wa barabara”? Je, ingekuwa barabara mpya iliyofunguliwa na mwanadamu? Kwa kutazama uzoefu wenu, inaonekana kwamba ndani yenu, Mungu hutumia mbinu za ukatili mkuu zaidi, ambazo kwazo haki ya Mungu inaweza kuonekana. Mngekosaje kutoa sifa? Kile ambacho Mungu hufanya ndani yenu huwaruhusu watu kutazama tabia ya haki ya Mungu; hili halistahili uvutiwaji wenu kwa Mungu? Leo, katika njia panda wakati ambapo enzi ya zamani bado ipo na enzi mpya bado haijatokea, mnashuhudia vipi kwa Mungu? Suala la maana kama hili halistahili uzingatiaji wa kina? Je, bado mnazingatia mambo mengine, ya nje? Kwa nini Mungu asema “Ingawa wakati fulani watu walitangaza ‘Ufahamu udumu,’ hakuna yeyote ambaye ametumia muda mwingi kuchambua neno ‘ufahamu,’ kuonyesha kwamba watu hawana hamu ya kunipenda”? Kama Mungu hangesema mambo kama hayo, hamngeweza kujaribu kuuelewa moyo wa Mungu kwa hiari yenu wenyewe?

Ingawa, katika nyakati za hivi karibuni, watu wengine huenda wameweza kuja kujua kidogo malengo na wazo la kupata mwili kwa Mungu, Naweza kusema kwa hakika kwamba kama Mungu hangenena kwa wanadamu waziwazi, hakuna yeyote ambaye angeweza kukisia malengo na wazo la kupata mwili kwa Mungu. Hili ni kamili. Je, bado halieleweki kwenu? Kila kitu ambacho Mungu hufanya ndani ya watu ni sehemu ya mpango Wake wa usimamizi—lakini bado hawawezi kuelewa sawasawa mapenzi ya Mungu. Huu ni upungufu wa mwanadamu, lakini Mungu hahitaji kwamba watu wawe na uwezo wa kufanya chochote, Yeye hutaka tu wasikilize “maonyo ya daktari.” Haya ni matakwa ya Mungu. Yeye huwataka watu wote wajue maisha ya mwanadamu ya kweli, kwani “ndani ya mioyo yao, maneno ‘maisha ya mwanadamu’ hayapo, hawayajali, na huchoka tu na maneno Yangu, kana kwamba Nimekuwa bibi mzee mwenye kuparaganya.” Machoni pa watu, maneno ya Mungu ni kama chombo cha siku zote, hawayachukulii kuwa muhimu kabisa. Hivyo, watu hawawezi kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo—wamekuwa mafidhuli hafifu wanaofahamu ukweli lakini hawautii katika vitendo. Kosa hili la mwanadamu pekee kwa hivyo linatosha kusababisha chukizo ndani ya Mungu kwa kipindi cha muda, na kwa hiyo Asema mara nyingi kwamba watu hawatilii maanani maneno Yake. Lakini katika dhana zao, watu hufikiria yafuatayo: “Kila siku sisi husoma na kuchambua maneno ya Mungu, ingewezekanaje kusemwa hatuyatilii maanani? Je, huku si kutotutendea kwa haki?” Lakini wacha Niwachambulie kidogo—watu watakuwa na haya. Wanaposoma maneno ya Mungu, wao huitikia kwa vichwa vyao, wao hunyenyekea mno, kama mbwa wa pua na mdomo mfupi wenye kunyanzi akidorora kwa maneno ya bwana wake. Hivyo, wakati huu, watu huhisi wasiostahili, machozi hutiririka usoni mwao, ni kana kwamba wangependa kutubu na kuanza upya—lakini mara tu wakati huu umepita, kuona aibu kwao hutoweka mara moja, kubadilishwa na hali ya mbwa mwitu, wao huweka maneno ya Mungu upande mmoja, na daima huamini kwamba shughuli zao wenyewe hupewa umuhimu wa kwanza, kwamba mambo ya Mungu huja mwisho, na kwa sababu ya matendo haya yao, huwa hawawezi kamwe kutia maneno ya Mungu katika vitendo. Wakati ukweli unapowasili, wao hunyosha viwiko vyao nje[a]—huku ni kusaliti watu wao wenyewe—si ajabu Mungu asema, “‘wanakimbia kwenda upande mwingine’ ilhali ananitegemea kwa riziki.” Ni kutoka kwa hili pekee ndio inaweza kuonekana kwamba hakuna uwongo hata kidogo katika maneno ya Mungu, yote ni kweli, na hayana chuku hata kidogo, lakini yanaonekana kuwa yameshindwa kuelezwa kikamilifu kwa kiasi fulani, kwani kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hakina uwezo wa kuyakubali. Maneno ya Mungu tayari yametoa dhihirisho wazi kabisa la mambo ya mwanadamu, ndani na nje, wameyagandisha akilini kwa uwazi kabisa, wakifafanua mfano dhahiri ambao hasa ni sura ya asili ya Shetani. Ni vile tu katika hatua ya sasa, watu bado hawajaona kila kitu kwa dhahiri, na hivyo husemekana kwamba hawajajijua. Ni kwa sababu ya hili ndio Nasema somo hili lazima liendelee, haliwezi kukoma. Wakati ambapo watu watajijua utakuwa wakati ambapo Mungu atatukuzwa. Hili ni rahisi kuelewa—hakuna haja ya Mimi kuingia katika utondoti. Kunalo, hata hivyo, jambo moja ambalo Nitawakumbusha kuhusu, ingawa kwanza lazima maneno haya ya Mungu yasomwe: “Katika nyakati za leo, watu hawajawahi kunithamini, Sina nafasi ndani ya mioyo yao. Je, wataweza kuonyesha upendo wa kweli Kwangu katika siku zijazo za mateso?” Ni nini maana ya maneno haya? Mungu asema kwamba kuadibu bado hakujamfika mwanadamu, ambalo linaonyesha kwamba bado kuna maana ya ndani ya maneno “kujijua”—je, uliona hili? Bila kupitia taabu na kuadibu, watu wanawezaje kujijua? Haya si maneno matupu? Je, wewe kweli huamini yote yanayonenwa na Mungu? Je, waweza kutambua maneno ya Mungu? Ni kwa nini Mungu husema tena na tena mambo kama “Nionapo matendo ya mwanadamu, chaguo Langu la pekee ni kuondoka,” na pia asema “Ni wakati ambapo tu milima hupinduliwa na dunia kutenganishwa mbalimbali ndio watu hufikiria kuhusu maneno Yangu, wakati huo tu ndio wao huamshwa kutoka kwa ndoto zao, lakini wakati umefika tayari, wamemezwa katika mafuriko makuu, maiti yao yaelea juu ya maji”? Kwa nini Mungu asema, “watu hufikiria juu ya” na sio “watu hutii maneno Yangu”? Ni kweli kwamba milima hupinduliwa na dunia kutenganishwa mbalimbali? Watu hawatilii maanani maneno kama hayo, wao huyaacha yaponyoke, na kwa hiyo wao hupitia “taabu” nyingi katika maneno ya Mungu. Hili ni kwa sababu wao hawajali kabisa. Kwa sababu ya huku kushindwa kwa mwanadamu, Mungu asema “Mimi, ‘dubwasha’ huyu asiye na michirizi ya machozi, Nimelia machozi mengi kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu, hata hivyo, hajui lolote kuhusu hili.” Kwa kuwa watu hawatilii maanani maneno ya Mungu, Mungu hutumia njia hii kuwakumbusha na kupata “msaada” wao.

Kwa sasa, Sitatoa unabii kuhusu maendeleo ya ulimwengu, lakini Nitatabiri kitu fulani kuhusu majaliwa ya mwanadamu. Je, Sijataka kwamba watu wajijue? Hili linaweza kuelezwa vipi? Watu wanapaswa kujijua vipi? Mungu “anapowatesa” watu sana kiasi cha wao kukaribia kifo, wao huanza kuelewa jambo fulani kuhusu maana ya maisha ya mwanadamu, na wao huchukia maisha ya mwanadamu, wakiamini kwamba maisha yote ya mwanadamu ni ndoto tu. Wao huamini kwamba maisha ya mwanadamu ni ya uchungu, kwamba watakufa bila kuwahi kutimiza chochote, kwamba maisha yao hayana maana na hayana thamani. Maisha ya mwanadamu ni ndoto tu, ndoto ambayo kwayo huzuni na furaha huja na kuondoka. Leo, watu huishi kwa ajili ya Mungu, lakini kwa kuwa wanaishi katika ulimwengu wa mwanadamu, maisha yao ya kila siku hubaki matupu na bila thamani, kuwafanya watu wote wajue kwamba raha ya Mungu ni faraja ipitayo tu—lakini iwapo, wakati ambapo hawamfurahii Mungu, bado wao huishi ndani ya mwili hata kama wanamwamini Mungu, ya nini? Katika mwili, yote ni matupu kwa mwanadamu. Baada ya kupitia mabadiliko ya maisha ya mwanadamu, kwa majilio ya umri mzee nywele za mwanadamu hupata mvi, uso wake hujaa kunyanzi, mikono yake hufunikwa na sagamba. Ingawa amelipa gharama kubwa, hajapata chochote kwa kweli. Hivyo, maneno Yangu yanaenda hatua moja zaidi: Kila kitu ni kitupu kwa wanaoishi ndani ya mwili. Hili ni bila shaka, na hakuna haja ya wewe kulichunguza hili kwa utondoti. Hii ni sura ya asili ya maisha ya mwanadamu ambayo Mungu amezungumzia mara kwa mara. Mungu hakwepi maneno haya kutokana na udhaifu wa mwanadamu, lakini Hutenda tu kufuatana na mpango Wake wa asili. Labda, maneno mengine hutoa usaidizi na ufahamu kwa watu, na labda mengine hufanya kinyume kabisa, kwa makusudi kusababisha watu kuishi katika mazingira ya kifo—na ni kwa sababu ya hili kabisa ndio wao huteseka. Hivyo, labda Mungu hueleza kinagaubaga “mkakati wa mji mtupu”[b] ili kuwapotosha watu kimakusudi, lakini hawawezi kuona hili kabisa, wao hubaki gizani. Na bado, yote yako mikononi mwa Mungu, na ingawa watu hulijua hili, wangewezaje kujikinga dhidi ya hilo? Hivyo, hakuna yeyote awezaye kuepuka tishio la kuadibu—wangefanya nini? Wanaweza tu kutii mipango ya Mungu—na je, hilo si kwa sababu Mungu amewanyakua na hatawaachilia? Ni katika matishio ya Mungu tu ndiyo watu wote wanaweza kufuata hali ya asili ya maisha—je, hii si kweli? Kama sio mipango ya Mungu, watu wangewezaje kukubali kushindwa kwa hiari? Huo haungekuwa mzaha? Ingawa maisha ya mwanadamu ni matupu, nani yuko radhi, wakati ambapo maisha yake yana starehe, kuachana kimyakimya na ulimwengu wa mwanadamu na kujaribu kumridhisha Mungu? Watu hufa katikati ya kutojiweza—nani amewahi kufa katikati ya utele, wakati ambapo ana yote ambayo angeweza kutaka? Ni “nyota” iliyoshuka kutoka angani tu ingekuwa isiyofuata kawaida kwa jambo hili. Ikilinganishwa na maisha ya mbingu ya tatu iliyofurahia, maisha duniani yangekuwa sawa na kuishi jahanamu—ni katika hali kama hiyo tu ndiyo ingeweza kuwa radhi kufa. Lakini nani leo hii ni nyota mbinguni? Mimi, pia, “Sielewi” kuhusu hili. Hebu tutafute kila mahali tuone kama tunaweza kupata mmoja. Iwapo atapatikana, Naomba watu wanisaidie kuuliza iwapo yuko radhi kutenda kufuatana na maneno Yangu yaliyo hapo juu. Lakini Nina onyo kwa kila mmoja wenu: Hakuna kati yenu anatakiwa kujisingizia “shujaa” na kujitolea kufa, mnaelewa?

Tanbihi:

a. “Nyoosha kiwiko cha mtu nje” ni nahau ya Kichina, ambayo inamaanisha mtu anawasaidia wengine kwa gharama ya watu walio karibu na mtu huyo, kwa mfano wazazi, watoto, jamaa au ndugu.

b. “Mkakati wa jiji tupu” ni sehemu ya 32 ya Mikakati ya Thelathini na Sita ya China ya kale. Mkakati huu unajumuisha kuwasilisha taswira ya kujiamaini ili kuficha ukosefu wa kuwa tayari ili kumhadaa adui.

Iliyotangulia: Sura ya 35

Inayofuata: Sura ya 38

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp