Utangulizi

Mnamo Februari 11, mwaka wa 1991, Mungu alitoa tamko Lake la kwanza katika kanisa, na tamko hili lilikuwa na athari isiyo ya kawaida kwa kila mmoja wa watu walioishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu wakati huo. Tamko hili lilitaja yafuatayo: “Makazi ya Mungu yameonekana” na “Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa.” Kwa maneno haya ya maana sana, watu hawa wote waliletwa katika ulimwengu mpya. Wale wote waliosoma tamko hili walihisi maelezo ya kazi mpya, kazi kuu ambayo Mungu alikuwa karibu kuianzisha. Lilikuwa ni tamko hili zuri, tamu, na lenye habari nyingi katika maelezo machache liliwaleta binadamu wote katika kazi mpya ya Mungu na katika enzi mpya, na ambalo liliweka msingi na kuanzisha kazi ya Mungu katika kupata mwili huku. Mtu anaweza kusema kwamba tamko ambalo Mungu alitoa wakati huu ni lile ambalo linaunganisha enzi; kwamba ni wakati wa kwanza tangu mwanzo wa Enzi ya Neema ambapo Mungu amezungumza wazi kwa jamii ya binadamu; zaidi, kwamba ni wakati wa kwanza ambapo Amezungumza baada ya kujificha kwa miaka elfu mbili; na, zaidi ya hayo, kwamba ni utangulizi, sehemu muhimu ya kuanzia, kwa ajili ya kazi ambayo Mungu yuko karibu kuanza kufanya katika Enzi ya Ufalme.

Mara ya kwanza Mungu alipotoa tamko, Alifanya hivyo kwa njia ya sifa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu, kwa lugha ambayo mara moja ilikuwa ya sanaa na ya ustaarabu na wazi na ya nyumbani, na vile vile ruzuku ya maisha ambayo ilieleweka kwa urahisi na bila shida. Akiwa na hili, Alilichukua kundi hili dogo la watu, waliojua tu jinsi ya kufurahia neema Yake wakingoja kwa hamu kurudi kwa Bwana Yesu, na kuwaleta kwa kimya katika hatua nyingine ya kazi katika mpango wa Mungu wa usimamizi. Katika hali hizi, binadamu hawakujua, sembuse kuthubutu kufikiri, ni aina gani ya kazi Mungu angeifanya hatimaye, ama yale ambayo yangetokea mbeleni. Baadaye, Mungu aliendelea kutoa matamko zaidi ili kuwaleta binadamu katika enzi mpya hatua kwa hatua. La kushangaza, kila tamko la Mungu ni tofauti katika maudhui na aidha hutumia aina tofauti za sifa na njia za maonyesho. Matamko haya, yaliyo sawa kwa sauti lakini ya namna mbalimbali katika maudhui, yamejazwa kila wakati na hisia za Mungu za utunzaji na kujali, na karibu kila moja lina ruzuku za maisha na maudhui tofauti na vile vile maneno ya kukumbusha, kushawishi, na kufariji kutoka kwa Mungu hadi kwa mwanadamu. Katika matamko haya, mafungu kama hili yanaonekana mara kwa mara: “Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote”; “Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu”; “Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake”; na kadhalika. Ujumbe unawasilishwa katika mafungu haya, ama mtu anaweza kusema kwamba mafungu haya yanawasilisha ujumbe kwa jamii ya binadamu: Mungu tayari Amekuja katika dunia ya binadamu, Mungu ataanzisha kazi kubwa hata zaidi, ufalme wa Mungu tayari umeshuka katika kundi fulani la watu, na Mungu tayari Amepata utukufu na kuwashinda maadui Wake wengi. Kila mwanadamu anaelewa kila tamko la Mungu. Wanadamu wote wanamsubiri Mungu ayape sauti maneno mengi mapya hata zaidi, kwa sababu kila wakati Mungu anaponena, Yeye huutikisa moyo wa binadamu hadi katika kiini chake, na zaidi Anatawala na kuruzuku sawa kila mwendo na kila hisia ya mwanadamu, ili kwamba binadamu waanze kuyategemea na, na zaidi kuyaheshimu maneno ya Mungu hata zaidi kuvutiwa na maneno ya Mungu…. Kwa njia hii, pasipo kujua, kimsingi watu wengi sana walikuwa wameisahau Biblia, na hata waliyasikiliza shingo upande mahubiri ya kale na maandishi ya watu wa kiroho, kwa sababu hawakuweza kupata msingi wowote wa maneno haya ya Mungu katika maandishi ya zamani, wala hawakuweza kugundua mahali popote kusudi la Mungu katika kutoa matamko haya. Kwa sababu hiyo, iliwapasa binadamu kukiri kwa kiasi gani zaidi kwamba matamko haya ni sauti ya Mungu ambayo hayajaonwa wala kusikika tangu mwanzo wa wakati, kwamba yako mbali ya uwezo wa mtu yeyote anayemwamini Mungu, na kwamba yanapita chochote kilichosemwa na mtu yeyote wa kiroho katika enzi za zamani au matamko ya Mungu ya zamani. Wakihimizwa na kila moja ya matamko haya, binadamu waliingia katika hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu bila kujua, katika maisha kwa safu ya mbele ya enzi mpya. Wakihimizwa na maneno ya Mungu, binadamu, wakiwa wamejawa na matarajio, walionja utamu wa kuongozwa binafsi na maneno ya Mungu. Naamini muda huu mfupi kuwa wakati ambapo kila binadamu ataangalia nyuma kwa kumbukumbu ya kuvumilia, wakati ambapo kwa kweli kile ambacho binadamu walifurahia wakati huu hakikuwa zaidi ya hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, au mtu anaweza kukiita ladha tamu ya sukari ambayo inaifunika dawa iliyo chini yake. Hii ni kwa sababu, kutoka wakati huu na kuendelea, bado chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, bado katika hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, binadamu waliongozwa katika awamu nyingine ya maneno ya Mungu pasipo kujua, ambayo ilikuwa hatua ya kwanza iliyohemshwa na tamko la Mungu katika Enzi ya Ufalme—jaribio la watendaji huduma.

Maneno yaliyotamkwa kabla ya jaribio la watendaji huduma yalikuwa hasa kwa njia ya maagizo, ushawishi, lawama, na kufundisha nidhamu, na katika sehemu nyingine yalitumia mtindo mzee wa mawasiliano uliotumiwa katika Enzi ya Neema—kutumia “Wanangu” kwa wale waliomfuata Mungu ili kufanya iwe rahisi kwa binadamu kumkaribia Mungu, au ili binadamu waweze kuchukulia uhusiano wao na Mungu kuwa wa karibu. Kwa njia hii, hukumu yoyote ambayo Mungu alitoa kwa kujiona, majivuno na tabia nyingine potovu za binadamu, mwanadamu angeweza kuishughulikia na kuikubali katika utambulisho wake wa “mwana,” bila kuwa na uhasama kwa matamko ya “Mungu Baba,” zaidi ya hayo ahadi ambayo “Mungu Baba” alitoa kwa “wana” Wake haikuwa ya shaka kamwe. Katika kipindi hiki, binadamu wote walifurahia uwepo ulio huru kutokana na taabu kama ule wa mtoto mchanga, na hili lilitimiza kusudi la Mungu, yaani, walipoingia katika utu uzima, Angeanza kutekeleza hukumu kwao. Hili pia liliweka msingi wa kazi ya kuihukumu jamii ya binadamu ambayo Mungu anaanzisha rasmi katika Enzi ya Ufalme. Kwa sababu kazi ya Mungu katika kupata mwili huku hasa ni kuihukumu na kuishinda jamii nzima ya binadamu, punde mwanadamu alipochukua msimamo thabiti, Mungu aliingia katika mtindo wa kazi Yake mara moja—katika kazi ambayo Anamhukumu mwanadamu na kumwadibu. Kwa uwazi, matamko yote kabla ya jaribio la watendaji huduma yalitolewa kwa ajili ya kupitia mageuzi, lengo la kweli likiwa tofauti na lile lilioonekana kuwa. Nia ya Mungu yenye hamu ilikuwa kwamba Aweze kuzindua rasmi kazi Yake katika Enzi ya Ufalme punde iwezekanavyo. Kwa vyovyote vile, Hakutaka kuendelea kuwabembeleza binadamu kuelekea mbele kwa kuwapa vidonge vya dawa iliyopakwa sukari; badala yake, Alikuwa na hamu ya kuuona uso wa kweli wa kila mwanadamu mbele ya kiti Chake cha hukumu, na hata Alitaka kuona kwa hamu zaidi mtazamo wa kweli ambao binadamu wote wangekuwa nao kumwelekea baada ya kupoteza neema Yake. Alitaka tu kuona matokeo, si mchakato. Lakini wakati huo, hakukuwa na mtu aliyeelewa nia ya Mungu yenye hamu, kwa sababu moyo wa binadamu ulishughulika tu na hatima yake na matarajio yake ya baadaye. Si ajabu kwamba mara kwa mara, hukumu ya Mungu ilikuwa imeelekezwa kwa jamii nzima ya binadamu. Ilikuwa tu wakati binadamu walipoanza kuishi maisha ya kawaida ya binadamu, chini ya mwongozo wa Mungu, ndipo mtazamo wa Mungu kwa binadamu ulipobadilika.

Mwaka wa 1991 haukuwa wa kawaida: hebu tuuite mwaka huu “mwaka wa ustawi.” Mungu alianzisha kazi mpya ya Enzi ya Ufalme na kuelekeza matamshi Yake kwa jamii yote ya binadamu. Wakati huo huo, binadamu walifurahia wema wa pekee na, hata zaidi, kupitia uchungu unaoifuata hukumu ya Mungu ya pekee kwa mwanadamu. Jamii ya binadamu iliuonja utamu usiojulikana, hukumu na hali ya kutupwa isiyojulikana, kana kwamba ilikuwa imempata Mungu na tena kana kwamba ilikuwa imempoteza Mungu. Kuteseka katika umiliki na kuteseka katika ufukara—hisia hizi zinajulikana tu na wale wanaozipitia binafsi; hisia hizi ni kitu ambacho mwanadamu hana uwezo wala njia ya kueleza. Majeraha ya aina hii ni yale Mungu alimpa kila mtu kama aina ya uzoefu na mali isiyoshikika. Maudhui ya matamko ambayo Mungu aliyatoa katika mwaka huu kweli yamo katika sehemu mbili kuu: Ya kwanza ni sehemu ambapo Mungu alishuka katika dunia ya wanadamu ili kuwaalika binadamu waje mbele ya kiti Chake cha enzi kama wageni; ya pili, sehemu ambapo baada ya binadamu kula na kunywa hadi wakashiba, walitumiwa na Mungu kama watendaji huduma. Bila shaka ni dhahiri kwamba sehemu ya kwanza ni matakwa ya binadamu yenye thamani zaidi na ari zaidi, hasa kwa kuwa tangu zamani wanadamu wamezoea kufanya kufurahia kila kitu cha Mungu kuwa lengo la imani yao Kwake. Hii ndiyo maana, punde Mungu alipoanza kuyapa sauti matamko Yake, binadamu wote walikuwa tayari kuingia katika ufalme nao walisubiri hapo ili Mungu awape thawabu tofauti. Katika hali hizi watu hawakulipa gharama ya kufaa kabisa kwa kubadilisha tabia zao, kutafuta kumridhisha Mungu, kuyafikiria mapenzi ya Mungu na kadhalika. Kwa mtazamo wa haraka wa juu juu, wanadamu walionekana kushughulika huku na kule siku zote huku wakijitumia na kumfanyia Mungu kazi, wakati kwa kweli walikuwa wakifanya hesabu, katika mahala pa siri zaidi pa vina vya mioyo yao, hatua ifuatayo wanayopaswa kuchukua ili wapate baraka au kutawala kama wafalme. Mtu anaweza kusema kwamba, wakati moyo wa mwanadamu ulipokuwa ukimfurahia Mungu, ulikuwa ukifanyia Mungu hila wakati huo huo. Katika hali hii binadamu hukutana na chuki na karaha ya Mungu yenye kina zaidi; tabia ya Mungu haivumilii binadamu yeyote kumdanganya au kumtumia. Lakini hekima ya Mungu haifikiki na mwanadamu yeyote. Ilikuwa katikati ya kuvumilia mateso haya yote ambapo Alinena sehemu ya kwanza ya matamko Yake. Hakuna mwanadamu anayeweza kuwaza kuhusu kiasi cha mateso ambayo Mungu alivumilia, na kiasi cha kujali na fikira Alivyotumia wakati huu. Lengo la sehemu ya kwanza ya haya matamko ni kufichua aina tofauti za ubaya ambao mwanadamu huonyesha anapokabiliwa na cheo na faida, na kufichua ulafi na kustahili dharau kwa mwanadamu. Hata ingawa, katika kusema, Mungu huyafuma maneno Yake kwa sauti ya kweli na yenye ari ya mama anayependa, ghadhabu iliyo ndani kabisa mwa moyo Wake huchoma kama jua la mchana, kana kwamba limeelekezwa dhidi ya adui Zake. Kwa hali yoyote ile, Mungu hataki kuzungumza kwa kundi la watu ambao wamepungukiwa na usawa wa kawaida wa jamii ya binadamu, na hivyo, wakati wowote Anapozungumza, Anaizuia ghadhabu iliyo ndani ya moyo Wake ilhali wakati huo huo Akijizuia ili kutoa maonyesho kwa tamko Lake. Zaidi ya hayo Anazungumza kwa jamii ya binadamu isiyo na ubinadamu wa kawaida, isiyo na mantiki, iliyo potovu kabisa, yenye ulafi uliogeuka na kuwa asili ya pili, na isiyotii na inayomwasi Mungu kabisa. Vina ambavyo jamii ya mwanadamu imeanguka na kadiri ya chuki na karaha ya Mungu kwa jamii ya mwanadamu inaweza kufikiriwa kwa urahisi; jambo gumu kwa jamii ya binadamu kufikiri ni maumivu waliyompa Mungu—ambayo hayawezi kuelezwa kwa maneno. Lakini ilikuwa katika usuli huu hasa—ambapo hakuna mtu aliweza kugundua jinsi moyo wa Mungu unavyoteseka, na aidha hakuna mtu aliyegundua jinsi jamii ya binadamu isivyo na busara na isivyorekebishika—kwamba kila mtu, bila aibu yoyote au haya hata kidogo, alilichukulia kuwa jambo la kawaida kwamba alikuwa na haki kama wana wa Mungu kupokea thawabu zote ambazo Alikuwa amemtayarishia mwanadamu, hata kufikia kiwango cha kugombana, mtu yeyote asitake kubaki nyuma na wote wakiogopa sana kupoteza. Kufikia sasa unapaswa kujua ni nafasi ya aina gani ambayo watu walioishi wakati huo walimiliki machoni pa Mungu. Jamii ya wanadamu kama hii inawezaje kupata thawabu za Mungu? Lakini kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa Mungu ni hazina ya thamani sana nyakati zote, na kinyume chake kile ambacho Mungu hupokea kutoka kwa mwanadamu ni uchungu mkubwa kabisa. Tangu mwanzoni mwa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, hiki ndicho mwanadamu amepokea daima kutoka kwa Mungu na kile ambacho amempa Mungu daima kama malipo.

Ingawa Mungu alijawa na wasiwasi, Alipoiona jamii hii ya binadamu, iliyo potovu kabisa, Hakuwa na budi kuitupa ndani ya jahanamu ili iweze kusafishwa. Hii ni sehemu ya pili ya tamko la Mungu, ambapo Mungu aliwatumia binadamu kama watendaji huduma Wake. Katika sehemu hii, Mungu alibadilika kutoka kuwa mpole hadi kuwa mkali, na kutoka machache hadi mengi, kuhusu mbinu na urefu, Akitumia nafasi ya “nafsi ya Mungu” kama ubembe ili kuifichua asili potovu ya mwanadamu na wakati huo huo Akiviweka mbele vikundi tofauti vya[a] watendaji huduma, watu, na wana kwa watu ambao wangeweza kuchagua. Bila shaka, kama vile Mungu alivyokuwa Ametabiri, hakuna mtu aliyechagua kuwa mtendaji huduma kwa ajili ya Mungu, na badala yake wote walijitahidi kuwa nafsi ya Mungu. Hata ingawa, katika kipindi hiki, ukali ambao Mungu alitumia kuzungumza kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwahi kutarajia na sembuse kusikia, hata hivyo, kujali sana kuhusu hadhi, na juu ya hili, kushughulika kwa msisimko mkubwa na kupata baraka, hawakuwa na wakati wa kuunda fikira kuhusu sauti ya kuzungumza ya Mungu na njia Yake ya kuzungumza, lakini badala yake hali yao wenyewe na kile ambacho siku za usoni zinaweza kuwa nayo, kilajaa akilini mwao. Kwa njia hii, bila kujua, binadamu waliingizwa katika “matata” kwa matamshi ya Mungu aliyokuwa Amewawekea. Wakiwa wameshawishiwa, bila hiari, na mvuto wa siku za mbele na kudura yao, binadamu walijijua kuwa hawafai kuwa nafsi ya Mungu, na bado walikuwa wakisita kutenda kama watendaji huduma Wake. Wakiwa wameshindwa kuchagua kati ya fikira hizi zinazopingana, bila kujijua walikubali hukumu na kuadibu kwa pekee ambako Mungu alikuwa Amewapa binadamu. Kwa kawaida, aina hii ya hukumu na usafishaji kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwa tayari kukubali hata kidogo. Hata hivyo, Mungu tu ndiye Aliye na hekima, na ni Yeye tu Aliye na uwezo, kuhitaji utii mpole kutoka kwa jamii hii potovu ya wanadamu, ili kwamba, watake au wasitake, wote walikubali mwishowe. Binadamu hawakuwa na njia badala ambazo wangeweza kuchagua. Ni Mungu tu ndiye Aliye na uamuzi wa mwisho, na ni Mungu tu ndiye Anayeweza kutumia mbinu kama hii kumpa mwanadamu ukweli na uhai na kumwonyesha mwelekeo. Mbinu hii ni kutoepukika kwa kazi ya Mungu kwa mwanadamu, na pia, bila shaka au ugomvi, ni jambo la lazima kwa mwanadamu. Mungu hutumia mbinu kama hii kwa ajili ya kunena na kufanya kazi ili kuwasilisha ukweli huu kwa binadamu: Katika kuwaokoa binadamu, Mungu hufanya hivyo kutokana na upendo na huruma Yake na kwa ajili ya usimamizi Wake; katika kupokea wokovu wa Mungu, jamii ya binadamu hufanya hivyo kwa sababu imeanguka hadi kiwango ambapo Mungu huzungumza binafsi tu. Mwanadamu anapoupokea wokovu wa Mungu, hii ndiyo neema kuu zaidi, na pia ni fadhila ya pekee, yaani, isingekuwa Mungu kulipa sauti tamko Lake mwenyewe, majaliwa ya jamii ya binadamu yangekuwa ni kufa. Wakati huo huo ambapo Anaikirihi jamii ya binadamu, bado Mungu yuko tayari na mwenye radhi kulipa gharama yoyote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Wakati ule ule, mwanadamu anapozungumza kwa kurudiarudia kuhusu upendo wake kwa Mungu na jinsi anavyoweka yote wakfu kwa Mungu, anaasi dhidi ya Mungu na kupokonya kila aina ya neema kutoka kwa Mungu, huku akimwumiza Mungu na kuutia moyo Wake uchungu mbaya sana. Hivyo ndivyo ilivyo tofauti dhahiri baina ya asiye na ubinafsi na aliye na ubinafsi kati ya Mungu na mwanadamu!

Katika kufanya kazi na kuzungumza, Mungu halazimiki kufuata mbinu yoyote maalum, ila Yeye husababisha kufikia matokeo katika upande Wake. Kwa sababu hii, katika sehemu hii ya matamko Yake, Mungu amehakikisha kutoonyesha utambulisho Wake mwenyewe kwa dhahiri, ila tu kufichua maneno machache kama vile “Kristo wa siku za mwisho,” “Mkuu wa ulimwengu,” na kadhalika. Hili haliathiri huduma ya Kristo au ufahamu wa binadamu kumhusu Mungu hata kidogo, hasa kwa kuwa katika siku hizo za awali binadamu hawakujua kabisa kuhusu dhana ya “Kristo” na “kupata mwili,” kiasi kwamba Mungu alilazimika kujinyenyekeza ili awe mtu aliye na “kazi maalum” ili kuonyesha tamko Lake. Huu ni mfano wa nia yenye juhudi ya Mungu, kwa sababu watu walioishi wakati huo wangeweza tu kukubali aina hii ya mtindo wa mawasiliano. Bila kujali aina ya mtindo wa mawasiliano ambao Mungu hutumia, matokeo ya kazi Yake hayaathiriwi, kwa sababu katika yote anayoyafanya, Mungu hunuia kumwezesha mwanadamu kubadilika, kumwezesha mwanadamu kupata wokovu wa Mungu. Bila kujali Anachokifanya, daima Mungu huyafikiria mahitaji ya mwanadamu. Hii ndiyo nia ya Mungu katika kufanya kazi na kuzungumza. Hata ingawa Mungu yuko mwangalifu kabisa katika kufikiria vipengele vyote vya binadamu, na ni mwenye busara kamili katika yote Anayoyafanya, Ningeweza kusema hili: Kama Mungu hangejishuhudia binafsi, hakungekuwa na yeyote miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa ambaye anaweza kumtambua Mungu Mwenyewe au kusimama kumshuhudia Mungu Mwenyewe. Kama Mungu angeendelea kutumia “mtu aliye na kazi maalum” kama mtindo wa mawasiliano katika kazi Yake, hakungekuwa na binadamu hata mmoja ambaye angemchukulia Mungu kama Mungu—hii ni huzuni ya binadamu. Yaani, miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa hakuna ambaye anaweza kumjua Mungu, sembuse kuwepo na yeyote wa kumpenda Mungu, kumjali Mungu na kumkaribia Mungu. Imani ya mwanadamu ni kwa ajili ya kupata baraka pekee. Utambulisho wa Mungu kama mtu aliye na kazi maalum imetoa dokezo kwa kila binadamu: Binadamu wanaona ikiwa rahisi kumchukulia Mungu kama mmoja miongoni mwa jamii ya wanadamu walioumbwa; uchungu na fedheha kuu kabisa ambayo binadamu wanamwumiza Mungu nayo ni hiyo hasa, Anapoonekana na kufanya kazi waziwazi, bado Mungu anakataliwa na mwanadamu na hata kusahaulika naye. Mungu huvumilia fedheha kuu zaidi ili Aweze kuiokoa jamii ya binadamu; katika kutoa kila kitu, lengo Lake ni kuwaokoa binadamu, ili Aweze kutambuliwa na binadamu. Gharama ambayo Mungu amelipa kwa ajili ya haya yote ni kitu ambacho kila mtu aliye na dhamiri anapaswa kuweza kuthamini sana. Jamii ya binadamu imepata kuzungumza na kufanya kazi kwa Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Hata hivyo, hakuna mtu ambaye amefikiria kuuliza jambo hili: Na ni nini ambacho Mungu amepata kutoka kwa binadamu? Kutoka katika kila tamko la Mungu, binadamu wameupata ukweli, wamefanikiwa kubadilika, wamepata mwelekeo katika maisha; lakini kile ambacho Mungu amekipata si zaidi ya maneno binadamu anayotumia kuonyesha kumdai kwake Mungu na minong’ono dhaifu ya sifa. Hakika hii si fidia ambayo Mungu anadai kutoka kwa mwanadamu?

Ingawa matamko mengi ya Mungu sasa yameonyeshwa, watu wengi sana bado wamesita katika hatua inayowakilishwa na maneno ya Mungu mwanzoni katika ufahamu na maarifa yao kumhusu Mungu, ambapo kwayo hawajaendelea mbele—hili kweli ni swala la kuhuzunisha. Sehemu hii ya “Matamko ya Kristo Mwanzoni” ni ufunguo tu wa kuufungua moyo wa binadamu; kusita hapa ni kutotimiza nia ya Mungu kabisa. Lengo la Mungu katika kunena sehemu hii ya matamko Yake ni kumleta binadamu kutoka kwa Enzi ya Neema hadi katika Enzi ya Ufalme tu; Hataki kamwe binadamu wabaki wakiwa wamesimama katika sehemu hii ya matamko Yake au hata kuchukua sehemu hii ya matamko Yake kama mwongozo, vinginevyo matamko ya baadaye ya Mungu hayatakuwa muhimu au ya maana. Iwapo kuna yeyote ambaye bado hawezi kuingia katika kile ambacho Mungu anadai kwamba mwanadamu anapaswa apate katika sehemu hii ya matamko Yake, basi kuingia kwa mtu huyo kunabaki kitu kisichojulikana. Sehemu hii ya matamko ya Mungu inajumuisha mahitaji ya msingi zaidi ambayo Mungu hutaka kutoka kwa mwanadamu katika Enzi ya Ufalme, na ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo binadamu wataingia katika njia sahihi. Iwapo wewe ni mtu asiyeelewa chochote, basi ni bora uanze kwa kusoma maneno katika sehemu hii!

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “vikundi tofauti vya.”

Iliyotangulia: Dibaji

Inayofuata: Sura ya 1

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp