1 Wimbo wa Ufalme
(I) Ufalme Unashuka Duniani

Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli. Ufalme unashuka katika dunia ya wanadamu.

1 Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo Vyangu. Ufalme unashuka katika dunia ya wanadamu, nafsi Yangu ni ya fahari na yenye neema. Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa ajili furaha? Ee Sayuni! Inua bendera yako ya ushindi unisherehekee! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina Langu takatifu!

2 Viumbe wote hadi miisho ya dunia! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka Kwangu! Nyota juu mbinguni! Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu Yangu kuu katika anga! Nazisikiliza sauti za watu duniani, wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yangu kwa nyimbo! Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Nashuka katika dunia ya wanadamu. Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha! Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka, ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena kamwe!

3 Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Ninaposhuka duniani Naleta moto, Naleta ghadhabu, Naleta maafa ya aina yote. Falme za dunia sasa ni ufalme Wangu! Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi; chini ya anga, maziwa na mito inatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha. Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao, na watu wote ambao wamelala wanaamshwa na Mimi. Siku ambayo watu wengi wameingojea hatimaye imefika! Wananiimbia nyimbo nzuri sana!

Umetoholewa kutoka katika “Wimbo wa Ufalme” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: Dibaji

Inayofuata: 2 Wimbo Wa Ufalme
(II) Mungu Amekuja, Mungu Ni Mfalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp