10 Ufalme Wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu

1

Mwenyezi Mungu mwenye mwili Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,

kama tu vile jua la haki likichomoza;

mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.

Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma

Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,

Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.

Mwenyezi Mungu yuko uso kwa uso nasi.

Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;

Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.

Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,

Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.

Ufalme wa Kristo unapatikana duniani.

2

Mungu uliyekuwa na kiu naye, Mungu niliyemngoja ameonekana.

Tuliutafuta ukweli, tulitamani sana haki;

ukweli na haki vimekuja miongoni mwa wanadamu.

Unampenda Mungu, nampenda Mungu; mwanadamu amejaa sana matumaini mapya.

Watu wanatii, mataifa yanamwabudu Mungu mwenye mwili wa utendaji.

Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli na kuleta hukumu,

Akifichua tabia ya Mungu yenye haki.

Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;

Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.

Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,

Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.

Ufalme wa Kristo unapatikana miongoni mwa wanadamu.

3

Kwa hukumu, kuadibu na majaribu ya maneno,

Anashinda na kukamilisha kikundi cha washindi.

Maneno ya Mungu, ya gadhabu na uadhama,

yanahukumu na kuutakasa uovu wa mwanadamu,

yakiharibu kabisa enzi ya giza.

Ukweli na haki vinatawala duniani.

Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;

Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.

Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,

Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.

Ufalme wa Kristo unapatikana miongoni mwa wanadamu.

Iliyotangulia: 9 Ufalme Wenye Haki wa Kristo Umetimia

Inayofuata: 11 Ufalme wa Mungu Umekuja Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp