607 Kiwango cha Chini Zaidi cha Kuwa Mtu Anayemtumikia Mungu

1 Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu amewaamulia kabla watu wengi kumhudumia, wakiwemo watu kutoka kila tabaka la maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni inatimia kwa urahisi. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia. Kila mtu anayemhudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na kudura ya Mungu, na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni.

2 Mungu kwa kweli anakuja ulimwenguni kufanya kazi Yake, kuwasiliana na watu, ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, kundi hili la watu lina bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa utendaji. Hii ni baraka isiyopimika kwenu. Kwa kweli ni Mungu anayewainua. Katika kumteua mtu ili amhudumie, Mungu siku zote huwa na kanuni Zake binafsi. Kumhudumia Mungu hakika, kama vile watu wanavyofikiria, si suala tu la kuwa na shauku. Leo mnaona kwamba mtu yeyote anayeweza kumhudumia Mungu akiwa mbele Yake anafanya hivyo kwa sababu wana mwongozo wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa sababu wao ni watu wanaofuata ukweli. Haya ndiyo mahitaji ya kiwango cha chini zaidi ambayo wote wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa nayo.

Umetoholewa kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 606 Mungu Hutumia Asili ya Mwanadamu Kumpima

Inayofuata: 608 Jinsi ya Kuhudumu Kwa Uuwiano na Mapenzi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp