Swali la 5: Kwa nini inasemwa kwamba wanadamu potovu lazima waokolewe na Mungu mwenye mwili? Hili ni jambo ambalo watu wengi sana hawalielewi—tafadhali shiriki ushirika kuhusu hili.

Jibu:

Sababu ya wanadamu wapotovu lazima kuokolewa na kupata mwili kwa Mungu ni kwamba mwili wa mwanadamu umedanganywa na kupotoshwa kabisa na Shetani. Wanadamu wote wanamilikiwa na Shetani, hawawezi kubainisha kati ya mema na maovu, uzuri na ubaya. Hawawezi kutofautisha kati ya chanya na hasi. Wanaishi kulingana na falsafa, sheria na asili ya Shetani, ni wenye kiburi, wa kujidai wasiojali, na wahalifu. Wote ni mifano halisi ya Shetani na wamegeuka kuwa wapotovu wakiungana na Shetani kumpinga Mungu, lakini hawatambui kwamba. Mungu ni Muumba, Mungu pekee ndiye Anajua kabisa asili ya kweli ya wanadamu, wamepotoshwa kwa kiwango kipi. Na Mungu pekee ndiye Anaweza kufichua na kuchangua asili ya kishetani na tabia potovu ya mwanadamu, Anaweza kumwambia mwanadamu namna ya kuishi na kutenda kama wanadamu, na Anaweza kuwashinda, kuwatakasa, na kuwaokoa wanadamu kabisa. Isipokuwa Mungu, hakuna mwanadamu aliyeumbwa anaweza kubaini kiini cha upotovu wa mwanadamu na bila shaka hawezi kumpa mwanadamu ukweli wa namna ya kutenda kama wanadamu. Kwa hiyo, ikiwa Mungu anataka kuwapokonya wanadamu wapotovu sana kutoka kwa fumbato za Shetani na kuwaokoa, basi ikiwa tu kupata mwili kwa Mungu ataonyesha mwenyewe ukweli na tabia ya Mungu na Amwambie mwanadamu kuhusu ukweli wote ambao anapaswa kumiliki, Akimruhusu mwanadamu kufahamu ukweli, kumjua Mungu, na abaini njama zenye uovu za Shetani na uwongo mbalimbali, wakati huo tu ndipo mwanadamu anaweza kumwacha na kumkataa Shetani na kurudi mbele za Mungu. Pia, kazi ya kupata mwili kwa Mungu hufichua kila aina za wanadamu. kwa sababu wanadamu wote ni wenye kiburi na hukataa kusalimu amri. Wakati Mungu anapata mwili kuonyesha ukweli, Wanadamu huitikia kila wakati kwa dhana zao, upinzani na hata vita. Kwa hivyo, ukweli wa upinzani na usaliti wa wanadamu wapotovu kwa Mungu hufichuliwa kwa ukamilifu na Mungu hutoa hukumu Yake kwa mwanadamu kutegemea upotovu wanaofichua na asili yao ya kweli. Ni kwa njia hii tu, ndio kushindwa, kutakaswa, na kukamilisha kwa wanadamu na Mungu kunaweza kutekelezwa kwa urahisi. Kupitia hukumu kwa maneno ya Mungu, mwanadamu anashindwa na anatakaswa polepole. Mwanadamu anaposhindwa kabisa, anaanza kutii Mungu mwenye mwili, anaanza kukubali na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu na anapitia kazi ya Mungu, anaamua kutafuata ukweli na kutoishi kamwe kwa kufuata falsafa na sheria za Shetani. Mwanadamu anapoishi kabisa kulingana na neno la Mungu, basi Mungu amemshinda Shetani kabisa na mwanadamu mpotovu anatumika kama mateka wa ushindi Wake dhidi ya Shetani. La msingi, Mungu anawapokonya wanadamu wapotovu kutoka kwa kukamata kwa Shetani. Kazi ya Mungu mwenye mwili tu ndiyo inaweza kuwa na athari kama hiyo. Hii ndiyo haja kamili ya Mungu kupata mwili ili kuwaokoa wanadamu, na Mungu mwenye mwili tu ndiye Anaweza kuwashinda na kuwaokoa wanadamu kabisa. Watu wanaotumiwa na Mungu hawawezi kufanya kazi ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu.

Mwanadamu mpotovu kweli anahitaji Mungu apate mwili kumhukumu na kumtakasa yeye mwenyewe ikiwa anataka kuokolewa. Katika harakati za uingiliano wa Mungu mwenye mwili na mwanadamu, Anamruhusu mwanadamu kumfahamu na kumjua Mungu uso kwa uso. Kwa sababu watafutaji halisi wa ukweli hukubali hukumu na utakaso wa Kristo wa siku za mwisho, kwa kawaida wanaweza kumtii Mungu na kuhisi upendo moyoni mwao kwa Mungu na waokolewe kabisa kutoka kwa milki ya Shetani. Je, hii si njia bora zaidi ya Mungu kuwaokoa na kuwakamilisha wanadamu? Kwa kuwa Mungu amepata mwili, tumekuwa na nafasi ya kumkaribia Mungu uso kwa uso na kupitia kazi Yake halisi, na tumekuwa na nafasi ya kupokea utoaji wa neno sahihi la Mungu na kuchungwa na kunyunyiziwa naye moja kwa moja ili tuanze kumtegemea Mungu, kumtii Mungu, na kumpenda kweli. Kama Mungu hangepata mwili kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu, athari hii halisi isingeweza kutimizwa. …

Mungu anapopata mwili ili kuwaokoa wanadamu wapotovu, Anaweza kutumia lugha ya wanadamu kuwaambia wanadamu waziwazi kuhusu matakwa ya Mungu, mapenzi Yake, tabia Yake na chote ambacho Anacho na Alicho. Kwa namna hii, bila kuhitaji kutafuta huku na huko, mwanadamu anaweza kufahamu mapenzi ya Mungu kwa dhahiri, ajue matakwa ya Mungu na njia ambayo anapaswa kutenda. Pia anaweza, kwa hivyo, kuwa na ufahamu na maarifa halisi kuhusu Mungu. Kama vile tu katika Enzi ya Neema, Petro alimwuliza Bwana Yesu, “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba?” (Mathayo 18:21). Yesu akamwambia Petro moja kwa moja: “Sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba(Mathayo 18:22). Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu aliyepata mwili aliwalisha na kuwasaidia wanadamu wakati wowote na kokote Alikoenda, Akimpa mwanadamu ruzuku halisi na kamili. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amepata mwili miongoni mwa wanadamu, Akionyesha ukweli ili kushughulikia hali halisi ya mwanadamu, Akionyesha tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho ili kuwasaidia na kuwakimu wanadamu. Akieleza upungufu na uwongo wote ulio ndani ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, Akimwarifu mwanadamu kuhusu mapenzi ya Mungu na matakwa Yake, Akiwapa wanadamu ruzuku na riziki ya maisha halisi na sahihi zaidi. Kwa mfano, wakati tunaishi katika uasi na upinzani kwa Mungu bila kujua, Neno la Mungu linatufichua na kutuhukumu moja kwa moja, likituruhusu kuona, katika neno la Mungu, jinsi asili yetu ya kishetani inampinga Mungu. Tunapomfuata Mungu kwa manufaa yetu binafsi na tunajidai kwa kufanya hivyo, Mungu hufichua udhaifu wetu na hutwambia ni imani gani tunapaswa kushikilia kama wafuasi wa Mungu. Tunapomwelewa Mungu visivyo katika kupitia hukumu Yake, Neno la Mungu hutukumbusha kuhusu makusudi ya ari ambayo Mungu hutumia kuwaokoa na kuwahukumu wanadamu, Akitatua kutoelewa kwetu visivyo kuhusu Mungu, n.k. Wateule wote wa Mungu wamepitia kabisa vile Mungu mwenye mwili Anatusaidia na kuturuzuku sisi siku zote ili tusihitaji kutafuata huku na huko. Tunachohitaji kufanya tu ni kusoma neno la Mwenyezi Mungu zaidi ili kupata kulishwa na kunyunyiziwa halisi kwa Mungu. Kupitia kwa neno hilo Mungu anaonyesha, tunapata ufahamu wa kweli kiasi wa mapenzi ya Mungu, tabia Yake na chote ambacho Anacho na Alicho na kupitia kwa ufahamu huu, na kupitia kwa ufahamu huu, kwa namna ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli na kujifunza jinsi ya kubaini njama za woga za Shetani, tukiona waziwazi jinsi sisi wenyewe tumepotoshwa na Shetani kabisa, na kwa kufanya hivyo, tunaacha polepole dhambi zetu na ushawishi wa Shetani wa giza. Kutokana na hilo, tabia yetu ya maisha hubadilika na tunaishika njia sahihi, tukiishi kulingana na uhalisi wa ukweli. Kupata mwili kwa Mungu amewezesha haya yote.

Mungu amepata mwili kufanya kazi na kuonyesha neno Lake, Akimruhusu mwanadamu kupata ruzuku na riziki ya maisha iliyo halisi zaidi. Licha ya kuwa mwanadamu ana dhana nyingi kuhusu kazi ya hukumu ya Mungu mwenye mwili, Mungu amemletea mwanadamu njia ya uzima na wokovu wa milele. Na mwanadamu amekuja kumtegemea! ... Licha ya kuwa Mungu amechukua umbo la Mwana wa Adamu wa kawaida katika kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ili kuwaokoa na kuwakamilisha wanadamu, licha ya Yeye kutofanya ishara na maajabu, na kutokuwa na sifa zinazozidi za mwanadamu au kimo kikubwa na Yeye kuwa shabaha la dhana za mwanadamu, kukana kwao, upinzani, na kukataa, ukweli ambao Kristo anaonyesha na kazi ya hukumu ambayo Anatekeleza vimempa mwanadamu ugavi wa neno la Mungu, na vimewaruhusu kufikia ukweli na kuona kuonekana kwa Mungu. Ingawa hatujaona nafsi halisi ya Mungu, tumeona tabia Yake ya asili, na kiini Chake kitakatifu, ambayo ni sawa tu na kana kwamba tulikuwa tumeiona nafsi Yake halisi. Tumemwona Mungu akiishi miongoni mwetu kwa kweli. Tunahisi kwa kweli kwamba tumenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi, tukiipitia kazi ya Mungu uso kwa uso na Mungu, na tukifurahia ruzuku ya maji hai ya uzima yanayotiririka kutoka kwa kiti cha enzi. Baada ya kupitia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, tumekuja kutambua polepole makusudi ya ari ambayo Mungu anatumia kuwakokoa wanadamu, na tumeona kwamba gharama anayolipa Mungu na mateso Anayovumilia ili kuwaokoa wanadamu ni makubwa kweli. Yote ambayo Mungu anatufanyia sisi ni maonyesho ya upendo Wake na lengo lake ni wokovu wetu. Tunajidharau kwa ajili ya uasi na upumbavu wetu wa awali na tunaanza kumpenda na kumtii Mungu kweli. Baada ya kupitia kazi ya Mungu kufikia sasa, sote tumetambua kwamba mabadiliko tunayoyaona ndani yetu yote ni matokeo ya wokovu wa kupata mwili kwa Mungu! Kriso wa siku za mwisho ni wokovu mkuu wa wanadamu wapotovu. Yeye ndiye njia pekee ya kuelekea kwa ufahamu wa Mungu na kupokea sifa za Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: Swali la 4: Katika Enzi ya Sheria, Mungu alimtumia Musa kutenda kazi Yake, hivyo kwa nini Mungu hamtumi mtu kutekeleza kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini Mungu mwenye mwili Mwenyewe lazima aifanye?

Inayofuata: Swali la 6: Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na alitumika kama dhabihu ya dhambi kwa ajili ya wanadamu, akiwakomboa kutoka kwa dhambi. Mungu amepata mwili tena katika siku za mwisho na ametamka ukweli na kufanya kazi ya hukumu, akiwatakasa kikamilifu na kuwaokoa wanadamu. Kwa nini Mungu anahitaji kupata mwili mara mbili ili kufanya kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu? Ni nini umuhimu wa kweli wa Mungu kujipatia mwili Mwenyewe mara mbili?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp