41. Kesi ya Zhaoyuan ya Mnamo Mei 28 Lasababisha Upeo wa Tatizo la Familia

Na Enhui, China

Mimi ni mwanamke wa kawaida wa mashambani, na mizigo mizito ya majukumu ya nyumbani kwangu yalikuwa yakinichosha sana kiasi kwamba sikuweza kupumzika. Kwa hivyo, nilianza kuwa mwepesi sana kukasirika, na mimi na mume wangu tulikuwa tukigombana kila siku. Hatukuweza hasa kuendelea kuishi kwa namna hiyo. Kila nilipokuwa nikiteseka, ningelia, “Mbingu! Tafadhali niokoe!” Na kisha mnamo mwaka wa 2013, injili ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ilinijia. Kupitia kusoma maneno ya Mungu na kuhudhuria mikutano na kina ndugu, nilikuwa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye niliyekuwa nikimlilia katika mateso yangu, na kwa hivyo nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kwa furaha.

Nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Tangu uumbaji wa ulimwengu Nimeanza kuamulia kabla na kuchagua kundi hili la watu, yaani, ninyi leo. Tabia yako, ubora wa tabia, sura, kimo, familia ambayo ulizaliwa kwayo, kazi yako na ndoa yako, nafsi yako yote, hata rangi ya nywele yako na ngozi yako, na wakati wa kuzaliwa kwako vyote vilipangwa na mikono Yangu. Hata mambo unayofanya na watu unaokutana nao kila siku hupangwa na mikono Yangu, sembuse ukweli kwamba kukuleta katika uwepo Wangu leo kwa kweli ni mpango Wangu. Usijitupe katika vurugu; unapaswa kuendelea kwa utulivu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 74). Kutoka kwa maneno haya ya Mungu hatimaye niligundua kuwa vitu vyote viko mikononi mwa Mungu, na kwamba mimi kuwa na bahati nzuri ya kuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, kukubali wokovu wa Mungu katika siku za mwisho, na kupata unyunyiziaji na riziki ya maneno Yake yote yalikuwa yamepangwa kabla na Mungu dahari zilizopita. Aina ya mume na familia niliyo nayo pia ilikuwa imeamuliwa kabla na Mungu. Nilijua kuwa nilipaswa kukubali na kujisalimisha kwa kile Mungu amekisababisha na kukipanga. Kuanzia wakati huo, wakati wowote mambo niliyoona kuwa yasiyopendeza yalipotokea, sikulalamika tena kama nilivyokuwa nimefanya hapo awali. Badala yake, nilikuwa na imani kwamba yalipangwa na Mungu na nilikuwa tayari kujisalimisha ili aweze kunielekeza na kuniongoza kujifunza kuishi kwa amani na familia yangu. Baada ya muda, niliweza kuacha kugombana na mume wangu. Alipoona mabadiliko yaliyokuwa yamefanyika kwangu tangu nilipomwamini Mungu, mume wangu pia alianza kuunga mkono imani yangu sana. Kina ndugu walipokuja nyumbani kwangu kwa ajili ya mkutano alikuwa mwenye heshima sana kwao, na wakati mwingine angeshiriki katika masihara. Wakati huo nilikuwa nikisoma neno la Mungu kila siku na kila mara kuhudhuria mikutano na kushiriki uzoefu na ndugu wengine. Nilihisi kusitawishwa katika roho yangu na nilifurahia aina fulani ya amani na furaha ambayo kamwe sikuwahi kuwa nayo hapo awali. Nilihisi kwamba imani katika Mungu ni jambo la ajabu kweli.

Lakini mambo yote mazuri lazima yafikie kikomo, na baada ya tukio la Zhaoyuan, Shandong kutokea mnamo Mei 28, mwaka wa 2014, siku hizo patanifu na tulivu nyumbani kwetu hazikuwapo tena. Hii kiasili ilikuwa kesi ya kawaida ya jinai, lakini siku tatu baadaye ilichukua sura mpya—serikali ya Chama cha Kikomunisti cha China ilitambulisha kesi hiyo kama kitu kilichofanywa kutokana na nia za dini. Katika kisingizio hiki, serikali ya CCP ilifanya Kanisa la Mwenyezi Mungu kuwa kilengwa chake; ilitumia vyombo vya habari kutungia ushahidi wa uwongo kwa utukutu, kufungua mashtaka ya uwongo, na kuharibu jina la Kanisa la Mwenyezi Mungu. Muda si muda, watu walisongwa na kila aina ya uvumi unaoweza kufikirika kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Mume wangu aliona jambo hili likiwa limeripotiwa kwenye habari na alidanganywa na propaganda ya serikali ya CCP. Ilikuwa kana kwamba mabadiliko ya papo hapo yalikuwa yamemjia. Alianza kufanya kila kitu ambacho angeweza ili kupinga imani yangu katika Mwenyezi Mungu.

Jioni moja, mume wangu alikuja nyumbani akifoka kwa ghadhabu na kunisuta kwa sauti kubwa: “Je, dini hii unayoamini ni gani kweli?” Nilikanganywa kabisa na mtazamo huo wake usio wa kawaida yake na kujibu, “Ninayemwamini ni Bwana Yesu aliyerudi, Mwenyezi Mungu, Ambaye tulikuwa tukimtaja kama ‘Mbingu.’” Alisema, “Unamwamini Mwenyezi Mungu! Tazama wanachokisema kwenye runinga!” Huku akisema haya, aliwasha runinga, na papo hapo kesi ya mnamo Mei 28 ya mauaji huko Zhaoyuan, Shandong ilikuwa pote katika taarifa za habari. Walikuwa wakisema kila aina ya mambo wakilaani Kanisa la Mwenyezi Mungu, na waliendelea kusema kwamba waumini katika Mwenyezi Mungu walikuwa watu wanaovuruga amani ya umma, na Idara ya Usalama wa Umma huko Shandong ilikuwa tayari kuzindua mashambulio makali ya kujibu na kuwakusanya bila huruma. Jambo hili lilinijaza hasira yenye haki, na nilimwambia mume wangu mara moja, “Jambo hili ni kashfa na uvumi tu. Muuaji huyu si muumini katika Mwenyezi Mungu hata kidogo! Kanisa la Mwenyezi Mungu lina kanuni katika kazi yake ya kiinjili, ambayo ni kuishiriki tu na watu wazuri wanaoamini katika uwepo wa Mungu na ambao ni wema. Kamwe hatushiriki na watu waovu. Watu wabaya kama Zhang Lidong hawafuati hata kidogo kanuni hizi za Kanisa la Mwenyezi Mungu za kushiriki injili, kwa hivyo bila shaka hawawezi kuwa waumini wa Mwenyezi Mungu. Jambo lingine—Zhang Lidong alipomtaka mwanamke huyo ampe nambari yake ya simu na akakataa, ilikuwa kutokana na aibu kwamba Zhang alighadhabika kwa ghafla na kumuua. Sisi, ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, kamwe hatujaribu kuwalazimisha watu wakubali kazi ya Mungu tunapokuwa tukieneza injili, kwa sababu Mungu alisema waziwazi katika ‘Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii’ kwamba ‘Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani. Amri hii inaelekezwa kwa kila mwanadamu. Kuhusu hili jambo mnapaswa kuchunguza, mfuatilie na mkumbushane, na hakuna anayepasa kukiuka amri hii.’ Kina ndugu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu wanapoeneza injili, kamwe hawalazimishi wengine—hili ni jambo ambalo hakuna mtu anayeweza kulikiuka. Habari hii ni kashfa tu, uwongo. Ni serikali ya CCP kueneza uvumi na kuharibu jina la Kanisa la Mwenyezi Mwenyezi tu.” Lakini ni nani angekisia—baada ya kusikia haya, mume wangu alifungua macho yake wazi na kunifokea, “Haijalishi ikiwa ni kweli au la. Alimradi CCP inapinga jambo hilo, huwezi kuhusika katika jambo hili! Sitaki serikali ije hapa kupekua nyumba. Mtoto wetu hata bado hajaoa!” Nilipomwona mume wangu amedanganywa na uvumi na uwongo huo kwenye runinga uliotungwa bila sababu, moyo wangu ulijawa na chuki: Serikali ya CPP inaweza kufanya chochote iwezacho kuzuia na kutesa Kanisa la Mwenyezi Mungu ili kufuta tu imani ya kidini. Ilikuwa ikitumia kesi ya Zhaoyuan kutunga na kutoa mashtaka ya uwongo dhidi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—mbinu mbaya sana!

Hakuna hata mmoja wetu aliweza kupata usingizi mzuri wa usiku baada ya hapo. Mume wangu alinisihi sana niende mafichoni na kukificha vizuri kitabu changu cha maneno ya Mungu, au kukirudisha kanisani endapo polisi wa CCP wangevamia nyumba yetu. Kumsikia akisema hayo yote kulinikumbusha matukio ya kina ndugu niliyokuwa nimesikia kuhusu, waliokuwa wamekamatwa, ambao nyumba zao zilikuwa zimepekuliwa, na ambao walikuwa wametozwa faini au kutiwa gerezani; niliwaza pia kuhusu binamu yangu mwenyewe. Aliingia katika ugomvi na mkuu wa kituo cha polisi cha mtaa wake kwa sababu hangeweza kumvumilia mtu aliyekuwa akirandaranda kwa mikogo, akiwadhulumu watu wa kawaida, na kuishia kuhukumiwa mwaka mmoja wa kuelimishwa upya kupitia kazi. Kila mtu katika familia yetu aliteseka pia, wakubwa kwa wadogo. Serikali ya CPP ni pepo ambaye hawezi kutolewa sababu ili kushawishiwa. Ikiwa ningekamatwa na kutiwa gerezani kwa sababu ya imani yangu, na ikiwa nyumba yetu ingevamiwa, je, jambo hilo lingekuwa la haki kwa mume na mtoto wangu? Niligaagaa na kugeuka, nikishindwa kulala, nikifikiria juu ya mpangilio wa matukio yangu ya baadaye ya kukamatwa na nyumba yangu kuvamiwa na polisi wa CCP, na mume wangu na mtoto kutiwa lawamani…. Sikuweza kujizuia kuhisi wimbi la ukiwa na hofu moyoni mwangu. Nilihisi jinsi ilivyo vigumu kumwamini Mungu, kuwa mtu mzuri, na kufuata njia sahihi nchini China, na kwamba maisha yangu yalikuwa hatarini kila wakati. Lakini ikiwa ningemsaliti Mungu kutokana na kuogopa mateso ya serikali ya CCP, dhamiri yangu ingenilaumu katika maisha yangu yote. Hata kama ningekuwa nikiishi maisha yangu bila mwelekeo, nikiishi bila kusudi, kimsingi ningekuwa maiti inayotembea na baada ya kufa singekuwa na uso wa kumwona Mungu tena. Nilikuwa nimechanganyikiwa na niliumia moyoni mwangu; nilihisi asiye na nguvu hata kidogo, hasi na dhaifu mno.

Katikati ya mateso yangu, nilikumbuka maneno haya ya Bwana Yesu, “Msiwe na hofu ya wao wanaoua mwili, lakini hawana uwezo wa kuifisha roho: ila heri uwe na hofu ya yeye anayeweza kuiangamiza roho pamoja na mwili katika kuzimu(Mathayo 10:28). “Kwa maana atakayeyaokoa maisha yake atayapoteza: na yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa sababu yangu atayapata(Mathayo 16:25). Maneno ya Bwana Yesu yalinipa imani na nguvu, na kuondoa wasiwasi na hofu kutoka moyoni mwangu. Niliwaza: “Mungu ni mkuu juu ya vitu vyote na viumbe vyote vilivyo hai, na maisha yangu na familia yangu pia iko chini ya mamlaka ya Mungu. Yote ambayo ninayo yaliyoka kwa Mungu, na siwezi kumsaliti katika wakati huu muhimu.” Kisha niliwaza juu ya mali ya familia ya Ayubu ikiibiwa na watoto wake kuondolewa kutoka kwake; aliachwa bila chochote, lakini bado aliweza kudumisha upendo wake kwa Mungu. Alisifu jina takatifu la Yehova Mungu na kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Na hata hivyo, nilipokabiliwa na uvumi na vurugu tu iliyotungwa na serikali ya CCP, bila kukamatwa au nyumba yangu kupekuliwa, nilikuwa dhaifu na hasi. Niliona kwamba kimo changu kweli kilikuwa cha chini kiasi cha kusikitisha, na kwamba sikuwa na hata chembe kimoja cha imani ya kweli katika Mungu. Wazo hili lilijaza moyo wangu aibu mbele za Mungu na niliazimia kimoyomoyo: Bila kujali chochote, lazima nisimsaliti Mungu, na nitadumisha imani yangu bila kujali kiasi cha mateso au matatizo ninayoweza kukabiliwa nayo!

Mume wangu alikuja nyumbani wakati wa adhuhuri siku iliyofuata, akaitupa gazeti mikononi mwake mbele yangu, na kusema, “Angalia vizuri! Inasema hapa kwamba yeyote anaweza kukamatwa alimradi anagunduliwa kumwamini Mwenyezi Mungu. Gereza si mahali ambapo ungetaka kutumia wakati wowote hata kidogo. Sio tu kwamba watu hupigwa, lakini wengi husongwa kwenye jukwaa moja la kulala. Mtu akienda msalani katikati ya usiku, hatakuwa na mahali pa kulala atakaporudi. Ukikamatwa, familia yetu haiwezi kumudu kukutoa kwa dhamana, kwa hivyo wakikukamata na uhukumiwe kwa miaka mingi, utakuwa tayari zaidi kutii!” Kusikia maneno hayo yasiyo mema kutoka kwa mume wangu kulinihuzunisha sana, na niliichukia serikali ya CCP ya kishetani hata zaidi. Isingekuwa udanganyifu, uvumi, ukandamizaji, na mateso yake, mume wangu angeniunga mkono katika imani yangu. Katu hangekuwa akinishinikiza kwa namna hiyo. Katika kutojiweza kwangu, nilichoweza kufanya tu ni kumwomba Mungu moyoni mwangu: “Mwenyezi Mungu! Najua kuwa serikali ya CCP inaeneza tu uvumi, kashfa, dhalala, na kufuru dhidi Yako. Serikali ya CCP ni Shetani tu, adui Yako. Lakini sasa ninahisi udhaifu kiasi moyoni mwangu, na ningependa Unilinde, Unipe hekima, na kuniwezesha nifahamu hila na ujanja wa Shetani ili niweze kusimama kidete upande Wako na nisitishwe na nguvu za uovu za serikali ya CCP.” Baada ya kuomba, sikuwa na hamu yoyote moyoni mwangu ya kumuepuka Mungu, na nilikumbuka maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Bwana Yesu alipofanya kitu kama vile kumleta Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa ithibati kwa wanadamu na Shetani aweze kuona, na kuacha wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amekuwa mwili ilivyo kama siku zote, Alibaki katika mamlaka juu ya ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu kimo mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kumfunza na kumwelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua thabiti ambapo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kuwatolea wanadamu. Ilikuwa njia bila matumizi ya maneno kwa Muumba ya kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya viumbe vyote. Ilikuwa njia Yake ya kuwaambia binadamu kupitia kwa hatua za kimatendo kwamba hamna wokovu mbali na kupitia Yeye. Mbinu za aina hii za kimya za Yeye kuwaelekeza wanadamu zinadumu milele—hazifutiki, na iliweza kuleta katika mioyo ya wanadamu mshtuko na kupatikana kwa nuru ambayo haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hali hii inayo athari ya kina katika kila mojawapo wa wafuasi wa Mungu. Inakita mizizi kwa kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III). Ukweli huu wa Mungu kumruhusu Lazaro kufufuka kutoka kwa wafu ulinitia moyo sana. Kwa mara nyingine tena nilikuwa na nguvu moyoni mwangu na niliinuka tena imara: Ndiyo! Mungu anadhibiti vitu vyote ulimwenguni, na maisha ya watu na vifo viko mikononi mwa Mungu. Nilijua kuwa hakuna mtu anayeweza kudhibiti jambo hili, na ikiwa nilikamatwa au la pia ilikuwa mikononi mwa Mungu. Maneno ya Mungu yalinilinda tena, na imani yangu kwa Mungu ndani ya moyo wangu iliongezeka tena. Hofu na woga uliokuwa ndani ya moyo wangu pia ulitulizwa sana.

Uvumi wa serikali ya CCP ulikuwa umeharibu amani na furaha ambayo tulikuwa nayo hapo nyuma katika kaya yetu. Ilinibidi niwe mwenye hadhari sana, mwangalifu sana katika kuhudhuria mikutano na kufanya wajibu wangu ili kuepuka vurugu yoyote zaidi katika maisha yetu ya nyumbani; jambo hili lilikuwa dhalimu sana kwangu. Na baadaye baba yangu aliposikia kuhusu tukio la Zhaoyuan la mwezi Mei tarehe 28, alianza kunizuia pia. Alisema, “Unaweza kuamini chochote unachotaka, lakini huwezi kwenda nje ukieneza injili kwa mtu mwingine yeyote au kwenda kuhudhuria mikutano. Katika umri wangu sitaweza kushughulikia tatizo lolote. Lazima ukumbuke familia nzima, vijana na wazee! Kumwamini Mungu ni jambo zuri, lakini hukuzaliwa katika nchi iliyo na uhuru wa imani. Mkono hauwezi kupiga mguu mwereka—CCP, ‘mguu,’ hufanya watu wa imani kuwa wafungwa wa kisiasa. Unajua haya yote, kwa hivyo usituadhiri na aina ya hofu unayohisi.” Shinikizo kutoka kwa familia yangu mwenyewe na ukosefu wao wa uelewa ulinitesa sana. Katika kipindi hicho, nilihisi kana kwamba nilikuwa katika hatari kubwa kila wakati, nikiishi kwa hofu kwamba ningekamatwa na serikali ya CCP na kuletea familia yangu tatizo ikiwa ningefanya kosa dogo zaidi. Kwa hivyo kila nilipotoka, nilificha kwa uangalifu kitabu changu cha maneno ya Mungu na kitu chochote kilichohusiana na kumwamini Mungu. Nilipoenda kwenye mikutano niliogopa sana kuwa ningeshtakiwa na mtu na kwamba familia yangu ingetiwa mashakani, kwa hivyo nilikuwa katika hali ya tahadhari kuu na kujihadhari; kila nilipoona gari la polisi au afisa nilijawa na wasiwasi. Haya yalikuwa mateso yasiyoelezeka, na nilihisi kwamba kumwamini Mungu nchini China kulikuwa kama kuishi maisha yenye wasiwasi mwingi. Sikuweza kujizuia kuhisi chuki kubwa hata zaidi kwa chama hiki kibaya cha kumkana Mungu: Je, nini kibaya na kuwa na imani na kufuata njia sahihi? Kwa nini hawawezi kuwaruhusu tu watu wamwamini Mungu? Kwa nini wanamkandamiza sana, kumkamata, na kumtesa mtu yeyote wa imani? Kwa nini wanawachukia sana watu wanaomwamini Mungu? Jambo hili ni baya mno!

Baadaye, hatimaye nilikuja kuelewa ukweli wa mambo niliposoma maneno ya Mwenyezi Mungu. Yanasema: “Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani? … Swala hili limeufanya uso wenye sura mbaya wa Shetani na kiini chake kuwa wazi kabisa. Shetani yuko vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV). Kupitia maneno ya Mungu, niliona nuru ghafla: Nilipochunguza jambo hili kutoka nje, ilikuwa serikali ya CCP ikiwatesa wale wetu ambao ni waumini, lakini kisirisiri ilikuwa vita vya kiroho vikijiri; ilikuwa Shetani akishindana na Mungu kwa ajili ya watu. Kwa sababu Shetani ni adui mkubwa wa Mungu na ni pepo ambaye humsaliti na kumpinga Mungu, tangu alipowapotosha wanadamu amekuwa akitaka kuwadhibiti; hawaruhusu watu wamwabudu Mungu au kumruhusu Mungu kuwapata wanadamu, ambao Mungu aliwaumba. Kwa hivyo, tangu mwanzo wa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu hadi sasa, Shetani amekuwa akifanya kila linalowezekana kusababisha vurugu na kuvuruga kazi ya Mungu. Shetani hutumia kila njia yenye kustahili dharau ili kuwazuia watu wanaomrudia Mungu. Nilijua kuwa wakati huo, ili kuzuia imani yangu, Shetani alikuwa akitumia uvumi kueneza ugomvi ndani ya familia yangu. Alikuwa akitumia hisia zangu kwa familia yangu na mbinu za vita vya kisaikolojia kunitishia, kunishawishi, kunihamanisha, na kunishambulia. Lengo lake la kufanya haya yote lilikuwa kunifanya nimwepuke, nimkatae, na kumsaliti Mungu, na kujaribu kuniingiza katika mfumbato wake na kunifanya niwe mtumwa wake, ili kwamba hatimaye niangamizwe na Mungu pamoja naye. Nia za serikali ya CCP ni za kudhuru kwa siri kweli; inampinga Mungu sana na ni adui wa Mungu. Kweli ni pepo anayeteketeza nafsi za watu. Kama vile inavyosema katika maneno ya Mungu: “Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II). Ufunuo katika maneno ya Mungu uliniruhusunifahamu uso wa kweli wa serikali ya CCP, nione kwamba kwa kweli ni mfano halisi wa Shetani, na kwamba ni utawala mbaya zaidi wa shetani unaompinga Mungu. Ilikuwa ikitumia kesi ya mnamo mwezi Mei tarehe 28 ya Zhaoyuan kuanzisha uvumi na kusingizia Kanisa la Mwenyezi Mungu katika jaribio la kuwadanganya watu na kuwakasirisha, na kuwachochea wale wasioelewa ukweli wa mambo wasimame upande wake na kumpinga Mungu pamoja nayo. Lengo la serikali ya CCP katika kutunga kesi ya uwongo ya Zhaoyuan na kubadili lawama kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuwa kutafuta sababu na visingizio vya kuwakusanya na kuwatesa Wakristo. Ni jaribio lisilofanikiwa la kuwakusanya Wakristo wote kwa dharuba moja, na kuwaondoa kabisa, na kulifuta kikamilifu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wanataka hata kufanikisha lengo lao katili la kuanzisha ukanda wa imani kwamba hakuna Mungu nchini China. Asili ya serikali ya CCP kweli ni ile ya usaliti na uovu mwingi!

Mara nilipogundua uhalisi wa vita vya kiroho na asili mbaya ya serikali ya CCP, swali lingine liliibuka akilini mwangu: Je, Mungu si mwenye kudura? Kwa nini Mungu aruhusu serikali ya CCP itutese? Kwa sababu ya kutoweza kutatua mkanganyiko huu ndani yangu, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “Wakati mmoja Nilisema kwamba hekima Yangu hutumiwa kutegemea njama za Shetani. Kwa nini Nilisema hilo? Je, huo si ukweli unaounga mkono Ninachosema na kufanya wakati huu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)). “Mungu anakusudia kutumia sehemu ya kazi ya pepo wachafu ili kuikamilisha sehemu ya mwanadamu, ili watu hawa waweze kufahamu matendo ya mapepo, na kuwawezesha watu wote wawafahamu kwa kweli mababu zao. Ni kwa njia hii pekee wanadamu wanaweza kujinasua kabisa, sio tu kutoroka kizazi cha mapepo, lakini hata zaidi mababu wao. Hili ndilo kusudi la asili la Mungu kulishinda kabisa joka kubwa jekundu, kufanya hivyo ili wanadamu wote wajue umbo halisi la joka kubwa jekundu, Aambue kinyago chake kabisa, na kuona umbo lake halisi. Hili ndilo Mungu anataka kutimiza, nalo ni lengo Lake la mwisho duniani ambalo Amefanyia kazi nyingi sana; Ananuia kulifanikisha hili ndani ya watu wote. Hili linajulikana kama ushawishi wa vitu vyote kwa ajili ya kusudi la Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 41). Nilielewa kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba Alikuwa akitumia ukandamizaji wa nguvu mbaya ya shetani ya serikali ya CCP kufanya huduma kwa ajili ya ukamilifu wa watu Wake wateule. Kupitia upinzani wa serikali ya CPP, kulaani, na kueneza uvumi kuchafua jina la Kanisa la Mwenyezi Mungu, na ukandamizaji wake na kuwakamata Wakristo, Mungu ameturuhusu tufahamu asili ya shetani, yenye pepo mbaya ya serikali ya CCP kama kitu kinachochukia ukweli na kumchukia Mungu. Jambo hili limeturuhusu tupate utambuzi wa kweli, kuikataa, na kamwe kutodanganywa tena nayo. Badala yake, tunaweza kutoka kwa utawala wa Shetani na kurudi mbele za Mungu. Zaidi ya hayo, Mungu anatumia kukamatwa na mateso ya pepo wa CCP kuwaweka wazi watu kwa kile walicho, kuwatenganisha watu kulingana na namna yao. Wale ambao ni waoga, wasio wa kweli katika imani yao, au ni kina Yuda wanawekwa wazi na kuondolewa kupitia mateso makali ya serikali ya CCP. Hata hivyo, wale wanaomwamini Mungu kwa kweli, hufuatilia ukweli na ambao wamejitolea kwa Mungu huwa shahidi kwa Mungu chini ya mateso katili ya serikali ya CCP na kuwa washindi waliofanywa na Mungu. Mara nilipokuwa nimeelewa haya yote, suitafahamu yangu, malalamiko, na mkanganyiko wangu kuhusu Mungu yalitatuliwa yote. Zaidi ya hayo, niliona jinsi Mungu ni mwenye hekima na mwenye uweza, na kwamba Hekima ya Mungu kwa kweli hutumika kulingana na hila za Shetani.

Pia nilisoma maneno haya ya Mungu: “Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Maneno ya Mungu yalinionyesha tabia Yake ya haki na tukufu, na niliona kwamba hakuna nguvu inayoweza kupita uweza na mamlaka ya Mungu. Ijapokuwa serikali ya CCP humpinga Mungu daima kwa hasira, na huwakandamiza, huwakamata, na kuwatesa watu Wake wateule na pia hutunga uvumi wa kila aina ili kuwapotosha watu na kuwazuia kurudi kwa Mungu, kazi ya Mungu bado inaenea kote nchini China. Zaidi ya hayo, kikundi cha washindi kimeundwa nchini China, na injili ya ufalme wa Mungu kwa sasa unaenea kote ulimwenguni. Hakuna mtu anayeweza kuzuia kazi ya Mungu. Wale wanaompinga Mungu, wanaozuia na kudhoofisha kazi ya Mungu, wameandikiwa kupata adhabu Yake ya haki na kuangamizwa. Hii imeamuliwa na tabia ya Mungu ya haki. Maneno ya Mwenyezi Mungu yalinipa utambuzi wa ghafla na nilipata nuru papo hapo. Sikuweza kujizuia kustaajabu moyoni mwangu na kusifu kazi ya Mungu ya miujiza. Hekima ya Mungu kweli ni kubwa zaidi kuliko mbingu; Mungu kutumia serikali ya CCP kufanya huduma ni jambo la busara sana. Wokovu wa Mungu kwa wanadamu ni wa vitendo sana—nimesadiki kabisa na siwezi kuacha kumsifu! Nilimwomba Mungu kisirisiri kutoka kwa moyo wangu, “Mungu! Sitaki kuwa makapi ambayo Utatupa kutoka kwa uga, na sitaki kupeperushwa na upepo mbaya wa serikali ya CCP. Ninataka kuwa ngano Unayovuna. Mungu! Kamwe sijawahi kukuridhisha, lakini katikati ya ukandamizaji mkali wa serikali ya CCP, natumaini kuwa ninaweza kuonyesha uaminifu wangu, kufuatilia ukweli kabisa, na sio kujisalimisha ninapokabiliwa na nguvu mbaya za serikali ya CCP. Natumaini kuwa mtu anayetamani haki na kutamani sana nuru, kuwa shahidi Kwako ili Upate utukufu….”

Kwa ajili ya kuwa na ufahamu huu, nilizidi kuwa thabiti moyoni mwangu. Nilielewa kuwa ninapokabiliwa na suitafahamu na vizuizi vya familia yangu, haya yote ni kwa ruhusa ya Mungu, na ni Mungu ndiye hupanga kwa uangalifu haya yote ili kukamilisha imani yangu, kujitolea kwangu, na utiifu wangu. Sikulalamika tena kuhusu mazingira yaliyonizunguka, wala sikubanwa na mazingira ya karibu. Badala yake, nilimshukuru Mungu, na kuamua kimoyomoyo kuwa bila kujali ni aina gani ya mazingira Mungu ananipangia, lazima niwe shahidi Kwake daima na kufanya wajibu wangu kwa uaminifu; sitamsaliti Mungu hata kidogo! Baadaye niliona matendo ya Mungu—mume wangu hakuwa akinipinga tena au kuwa mkandamizaji kama vile alivyokuwa akifanya. Badala yake, aliniambia: “Sio kwamba sitaki uwe na imani. Ninakubali kuwa umebadilika tangu ulipoanza kumwamini Mungu; ni kwamba tu siku zijazo sharti uwe mwangalifu, lazima ujihadhari unapoenda nje kuhudhuria mikutano.” Kumsikia akisema jambo hili kulileta machozi machoni pangu. Nilimshukuru na kumsifu Mungu ndani ya moyo wangu kwa ajili ya matendo Yake, kwa sababu niliona kuwa ukweli na haki unaweza kushinda yote ambayo ni ya giza na mabaya. Nguvu mbaya za Shetani hatimaye zitaondolewa kabisa kupitia kazi ya Mungu! Ingawa nilipitia taabu kiasi za kusafishwa kupitia tukio hili, nilipata ufahamu kiasi wa kazi ya Mungu ya hekima. Pia nilipata uwezo kiasi wa kutofautisha kati ya vitu chanya na vitu hasi—haya yote ni utajiri fulani katika maisha yangu ambayo umeamsha azimio langu la kufuatilia ukweli na kutamani nuru.

Iliyotangulia: 40. Kuja Nyumbani

Inayofuata: 42. Dhoruba ya Talaka Yazimwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

27. Kukutana na Bwana Tena

Na Jianding, AmerikaNilizaliwa katika familia ya Kikatoliki, na tangu nikiwa na umri mdogo mamangu alinifunza kusoma Biblia. Wakati huo,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp