Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote. Sasa hakuna yeyote kati yenu anayeelewa maana ya maneno ambayo Ninasema, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuelewa maana ya maneno haya. Ni wakati tu kila kitu kitafichuliwa kwenu ndipo mtaelewa kwa nini Ninasema maneno haya. Mimi si wa ulimwengu na Mimi sio hata wa ulimwengu kwa sababu Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee. Ninashikilia ulimwengu dunia wote mkononi Mwangu, Mimi Mwenyewe Ninatawala, na watu wanaweza tu kutii mamlaka Yangu, kulitaja jina Langu takatifu, kunishangilia na kunisifu. Kila kitu kitafunuliwa kwenu hatua kwa hatua. Ingawa hakuna kitu kilichofichwa, ninyi bado hamwezi kuelewa njia Yangu ya kuzungumza, na sauti ya maneno Yangu. Bado hamwelewi mpango Wangu wa usimamizi unahusu nini. Kwa hiyo, Nitawaambia baadaye kuhusu mambo yote ambayo hamwelewi kwa yale Niliyoyasema kwa sababu, Kwangu Mimi, kila kitu ni rahisi na wazi wakati, kwenu, ni vigumu sana, hamwelewi tu kabisa. Kwa hiyo, Nitabadili njia Yangu ya kuzungumza, Sitaunganisha mambo pamoja Ninaponena lakini Nitafafanua kila hoja moja baada ya nyingine.

Kufufuka kutoka kwa wafu kunahusu nini? Je, ni kufa katika mwili na kisha kurudi kwenye mwili baada ya kifo? Je, huku kunaitwa kufufuka kutoka kwa wafu? Je, ni rahisi vile? Mimi ni mwenyezi Mungu, unajua nini kuhusu hili? Je, mnaelewaje hili? Je, kufufuka kutoka kwa wafu wakati wa kupata Kwangu mwili mara ya kwanza kwa kweli kunaweza kuchukuliwa neno kwa neno? Je, mchakato huo ulikuwa kama ulivyoelezwa katika maandiko? Nimesema kuwa kama Sizungumzi kwa uwazi, kama Sielezi wazi, hakuna mtu atakayeweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Hakuna mtu hata mmoja katika enzi zote ambaye hakufikiri kwamba kufufuka kutoka kwa wafu kulikuwa vile. Tangu uumbaji wa dunia hakuna mtu aliyeelewa maana halisi ya hili. Je, nilipigwa misumari msalabani kwa kweli? Na, baada ya kifo, je, nilitoka kaburini? Ilikuwa namna hii kwa kweli? Je, hili linaezekana kweli? Hakuna mtu katika enzi zote ambaye ameweka jitihada yoyote katika hili, hakuna mtu ambaye amenijua kutoka kwa hili na hakuna mtu hata mmoja ambaye haamini, kila mtu anadhani kuwa hili ni kweli. Hawajui kwamba kila neno Langu lina maana ya ndani. Basi, kufufuka kutoka kwa wafu ni nini hasa? (Hivi karibuni, mtapitia jambo hili, kwa hivyo Nitawaambia kuhusu hilo mapema.) Kila kiumbe aliyeumbwa anataka kuishi kuliko kufa. Kutoka kwa mtazamo Wangu, kifo cha mwili sio kifo halisi. Wakati Roho Wangu anarudishwa kutoka kwa mtu, mtu huyo hufa. Kwa hiyo, Ninawaita wale mapepo wote waliopotoshwa na Shetani (wale ambao hawana imani, wasioamini wote) wafu. Tangu kuumbwa kwa dunia, Nimeongeza Roho Wangu kwa kila mtu Niliyemchagua. Hata hivyo, baada ya awamu iliyofuatia uumbaji, watu walimilikiwa na Shetani kwa kipindi cha muda. Kwa hiyo Niliondoka na watu wakaanza kuteseka (mateso Niliyovumilia Nilipopata mwili na kusulubishwa msalabani, kama ilivyoelezwa). Hata hivyo, kwa wakati uliopangiwa kabla na Mimi (wakati ambapo kuwaacha Kwangu watu kulimalizika), Niliwarejesha Kwangu watu Niliowaamulia kabla na Nikaweka tena Roho Wangu ndani yenu ili mpate kufufuka. Hii inaitwa “kufufuka kutoka kwa wafu.” Sasa, wale wanaoishi kwa kweli katika Roho Wangu wote wameshashinda uwezo wa binadamu, na wote wanaishi katika mwili. Hata hivyo, kabla ya muda mrefu, ninyi nyote mtaondoa fikira zenu, mtupe mawazo yenu, na kutupa mtego wote wa kidunia. Lakini, sivyo, kama watu wanavyofikiria, kufufuka kutoka kwa wafu baada ya mateso. Kwamba ninyi mnaishi sasa ni sharti la awali la kuishi katika mwili, ni njia muhimu ya kuingia katika ulimwengu wa kiroho. Kuzidi uwezo wa ubinadamu wa kawaida Ninaozungumza kuhusu kunamaanisha kutokuwa na familia, kutokuwa na mke, kutokuwa na watoto na mahitaji ya kibinadamu. Ni kuzingatia tu kuishi kwa kudhihirisha mfano Wangu, kuzingatia tu kuingia ndani Yangu na kutofikiria juu ya mambo mengine nje Yangu. Mahali popote unapoenda ni nyumbani kwako, huku ni kuvuka mipaka kwa ubinadamu wa kawaida. Ninyi mmeelewa visivyo kabisa maneno haya Yangu, ufahamu wenu ni wa kina kifupi sana. Je, Nitaonekanaje kwa mataifa yote na watu wote? Katika mwili leo? Hapana! Wakati utakapokuja, Nitaonekana katika mwili Wangu katika kila taifa la ulimwengu. Wakati ambapo wageni wanawahitaji muwachunge bado haujafika. Wakati huo ninyi mtahitaji kuja nje ya mwili na kuingia katika mwili ili muwalishe. Huu ni ukweli lakini sio “kufufuka kutoka kwa wafu” ambao watu wanafikiria. Wakati uliowekwa, mtatoka katika mwili bila kujua na kuingia katika ulimwengu wa kiroho na kutawala mataifa yote pamoja nami. Wakati haujafika bado. Ninapowahitaji kuwa katika mwili mtakuwa katika mwili (kulingana na mahitaji ya kazi Yangu, ninyi lazima muwe na fikira sasa, bado lazima muishi katika mwili, hivyo mnapaswa bado kufanya mambo ambayo mnapaswa kufanya katika mwili kulingana na hatua Zangu; msisubiri bila kufanya lolote kwa sababu hii itachelewesha mambo). Ninapowahitaji kutenda katika mwili kama wachungaji wa kanisa, ninyi mtatoka nje ya mwili, muache mawazo yenu, na kunitegemeana kabisa ili kuishi. Muwe na imani katika nguvu Zangu, muwe na imani katika hekima Yangu. Kila kitu kitafanywa na Mimi binafsi. Mnahitaji tu kusubiri kufurahia. Baraka zote zitawajia, na ninyi mtakuwa na ruzuku isiyoisha. Siku hiyo itakapokuja, mtaelewa kanuni ya jinsi Ninavyofanya hivi, mtajua matendo Yangu ya ajabu na kuelewa jinsi Ninavyoleta wana Wangu wazaliwa wa kwanza katika Sayuni. Hili sio gumu kama mnavyofikiria lakini pia si rahisi kama mnavyofikiria.

Najua Ninaposema hili hamwezi hata kwa kiwango cha chini kuelewa madhumuni Yangu katika hilo na huchanganyikiwa zaidi. Mtayachanganya na yale Niliyosema hapo awali ili msiweze kuelewa chochote, itaonekana kama kwamba hakuna njia nyingine. Hata hivyo, msijali, Nitawaambia kila kitu. Kila kitu Ninachosema kina maana. Nimesema kuwa Ninaweza kufanya vitu vilivyopo virudi kuwa bure na Ninaweza kufanya vitu viwe vingi kutoka kwa utupu. Katika mawazo ya binadamu, kuingia katika mwili kutoka kwa mwili, mtu lazima afufuliwe kutoka kwa wafu. Katika siku za nyuma, Nilitumia njia hii na Nikadhihirisha muujiza Wangu mkuu zaidi, lakini leo si kama zamani. Nitawachukua moja kwa moja kutoka kwa mwili hadi ndani ya mwili. Je, hii sio hata ishara kubwa zaidi na muujiza? Je, huu sio udhihirisho mkubwa zaidi wa kudura Yangu? Nina mpango Wangu, Nina nia Zangu. Nani asiye katika mikono Yangu? Ninafanya kazi na Ninajua. Njia Zangu za kufanya kazi leo ni, hata hivyo, tofauti na zilizopita. Ninabadilisha mbinu Zangu za kufanya kazi kulingana na mabadiliko ya enzi. Wakati Nilipigwa misumari msalabani, hiyo ilikuwa ni Enzi ya Neema, lakini sasa ni enzi ya mwisho. Kasi ya kazi Yangu inaongezeka, sio kasi sawa na ilivyokuwa hapo zamani, sembuse kuwa polepole kuliko siku za nyuma lakini, badala yake, ni haraka zaidi kuliko zamani. Hakuna njia ya kuielezea, hakuna haja ya michakato mingi migumu. Mimi Niko huru kufanya chochote; si kweli kwamba inachukua tu neno moja la mamlaka kutoka Kwangu kuamua jinsi mapenzi Yangu yatakamilishwa na jinsi Nitawakamilisha? Kila kitu Ninachosema hakika kitafanyika. Katika siku za nyuma, mara nyingi Nilisema kuwa nitateseka, na Sikuwaruhusu watu wataje mateso Niliyoyastahimili awali; kutaja hili kulikuwa kunikufuru. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu Mwenyewe na Kwangu hakuna ugumu; unapotaja mateso haya unawafanya watu walie. Nimesema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa na kutanafusi na hakutakuwa na machozi. Inapaswa kuelezwa kutoka kwa mtazamo huu, na kisha maana ya maneno Yangu yanaweza kueleweka. Maana ya “wanadamu hawawezi kustahimili mateso haya” ni kwamba Ninaweza kuondoka kutoka kwa dhana zote za binadamu na fikira, kuachana na hisia za mwili, kuacha dalili yoyote ya kuwa wa kupenda anasa za ulimwengu na kuondoka katika mwili, na bado Ninaweza kusimama wakati kila mtu ananikana Mimi. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee. Nimesema, “Kila mwana mzaliwa wa kwanza lazima aingie katika ulimwengu wa kiroho kutoka kwa mwili; hii ndiyo njia ambayo wanapaswa kuchukua ili kutawala pamoja nami kama wafalme.” Maana ya sentensi hii ni kwamba unapokumbana na kitu ambacho mnacho, zamani, mlifikiri, mtaondoka rasmi katika nyama na kuingia katika mwili ili muanze kuwahukumu rasmi wale wana wa wafalme na wafalme hao. Wao watahukumiwa kulingana na mambo yanayotokea wakati huu. Hata hivyo, sio ngumu kama mnavyofikiria, itafanyika papo hapo. Hamtahitaji kufufuka kutoka kwa wafu na hamtahitaji hata kuteseka (kwa sababu mateso na shida zenu duniani tayari zimekamilika na Nimekwisha kusema kuwa Sitashughulika tena na wanangu wazaliwa wa kwanza baada ya hapo). Wazaliwa wa kwanza watafurahia baraka zao, kama ilivyoongelewa, kwa kweli kwamba mtaingia katika ulimwengu wa kiroho bila kujua. Kwa nini Nasema kuwa hii ni rehema Yangu na neema? Ikiwa mtu angeweza tu kuingia katika ulimwengu wa kiroho baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, hii ingekuwa mbali na kuwa ya huruma na neema. Kwa hivyo haya ndiyo maonyesho ya dhahiri zaidi ya rehema Yangu na neema na, zaidi ya hayo, yanafichua uamuzi Wangu kabla na uteuzi Wangu wa watu. Inatosha kuonyesha jinsi amri Yangu ya utawala ilivyo kali. Nitakuwa mwenye huruma kwa yeyote Nitakayetaka na kuwa mwenye huruma kwa yeyote Nitakayetaka. Hakuna mtu atakayepinga au kupigana. Nitaamua yote haya.

Watu hawawezi kuelewa hilo na wanajiwekea shinikizo mpaka wasiweze kupumua na bado wanajifunga. Mawazo ya watu ni finyu sana, kwa hiyo ni lazima watupilie mbali mawazo na dhana za binadamu. Kwa hivyo, ni lazima Nitoke katika mwili na kuingia katika ulimwengu wa kiroho kuchukua udhibiti wa kila kitu, kusimamia kila kitu. Hii ndiyo njia pekee ya kutawala watu wote na mataifa yote na kutimiza mapenzi Yangu. Sio mbali sana. Hamna imani katika kudura Yangu, hamjui mwanadamu Niliye. Mnafikiri kwamba Mimi ni mtu tu, hamwezi kuona uungu Wangu hata kidogo. Mambo yatakuwa kamili wakati wowote Ninapotaka yawe kamili. Kinachohitajika tu ni neno kutoka katika kinywa Changu. Ninyi mmetilia maanani tu kipengele cha ubinadamu Wangu katika kile ambacho Nimesema hivi karibuni na kila Ninachofanya, lakini hamjatilia maanani kipengele cha uungu Wangu. Hiyo ni kusema kwamba mnadhani kwamba Mimi pia nina mawazo na dhana. Lakini Nimesema kuwa fikira Zangu, mawazo na akili, kila Ninachofanya, kila kitu Ninachotenda na kila kitu Ninachosema ni udhihirisho kamili wa Mungu Mwenyewe. Je, mmesahau yote haya? Ninyi nyote ni watu waliochanganyikiwa! Hamwelewi maana ya maneno Yangu. Nimewaruhusu kuona kipengele cha ubinadamu Wangu wa kawaida kutoka kwa kile Nilichosema (Nimewawezesha kuona ubinadamu Wangu wa kawaida katika maisha Yangu ya kila siku, kwa kweli, kwa sababu ninyi bado hamwelewi kipengele cha ubinadamu Wangu wa kawaida kutokana na kile Nilichosema wakati huu), ilhali hamwelewi ubinadamu Wangu wa kawaida, na mnajaribu kushikilia tu kitu ambacho kinaweza kutumiwa dhidi Yangu na mnakuwa bila nidhamu mbele Yangu. Ninyi ni vipofu! Ninyi ni wapumbavu! Hamnijui Mimi! Nimenena bure kwa muda mrefu, ninyi hamnijui Mimi kabisa, hamuchukulii ubinadamu Wangu wa kawaida kama sehemu ya Mungu Mwenyewe mkamilifu kabisa! Ninawezaje kukosa kuwa na hasira? Ninawezaje kuwa mwenye huruma tena? Ninaweza tu kuwajibu watoto hawa wa kutotii na hasira Yangu. Wenye kiburi sana, wasionijua sana! Mnafikiria kwa mwanadamu Niliye amefanya makosa! Naweza kufanya makosa? Ningechagua bila mpango kuuchukua mwili wowote? Ubinadamu Wangu na uungu Wangu ni sehemu mbili zisizoweza kutenganishwa ambazo zinajumuisha Mungu Mwenyewe mkamilifu. Sasa mnapaswa kuelewa vizuri kuhusu hili! Maneno Yangu tayari yamefikia kilele chayo, na maneno Yangu hayawezi tena kuelezwa kwa urefu zaidi!

Iliyotangulia: Sura ya 97

Inayofuata: Sura ya 99

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp