Sura ya 99

Kwa sababu mwendo wa kazi Yangu unaongeza kasi, hakuna anayeweza kuenda mwendo sawa na nyayo Zangu, na hakuna anayeweza kupenya akili Yangu, bado hii ndiyo njia tu ya kwenda mbele. Hii ni “mfu” (ikiashiria kukosa uwezo wa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Yangu; hii ni njia mbadala ya kueleza “mfu”, na haimaanishi “kuachwa na Roho Wangu”) katika msemo “kufufuka kutoka wafu”, ambako kumeshazungumziwa. Wakati nyinyi na Mimi tumebadilika kutoka kwa awamu hii hadi kwenye mwili, basi maana halisi ya “kufufuliwa kutoka wafu” itatimizwa (yaani, hii ni maana halisi ya ufufuko kutoka kwa wafu). Sasa, hii ni hali ambamo nyote mko: Hamwezi kufahamu mapenzi Yangu na hamwezi kupata nyayo Zangu. Zaidi ya hayo, hamwezi kuwa kimya katika mioyo yenu, hivyo mnahisi msio na utulivu katika akili. Hali ya aina hii hasa ni “mateso” Niliotaja, na ndani ya haya mateso, ambayo watu hawawezi kustahimili, mnafikiri kuhusu siku zenu za baadaye wenyewe, na kwa upande mwingine mnakubali kuchomwa na Mimi, hukumu Yangu, yakija ghafla kwenu kutoka kila upande. Zaidi ya hayo, kwa sauti na jinsi ambavyo Mimi huongea, hamwezi kufahamu kanuni zozote, na kwa siku moja ya tamko kuna aina kadhaa ya sauti, ili mteseke sana. Hizi ndizo hatua katika kazi Yangu. Hii ndiyo hekima Yangu. Baadaye mtapitia, mateso makubwa zaidi kuhusu hili, yote ambayo ni ili kufichua watu wote wanafiki—hili linapaswa kuwa dhahiri sasa! Hii ndiyo njia Nifanyayo kazi. Kuwa na motisha ya aina hii ya mateso, na baada ya kuupitia uchungu huu ambao ni sawa na kifo, mtaingia katika eneo jingine. Mtaingia katika mwili na kutawala mataifa yote na watu wote nami.

Kwa nini hivi karibuni Nimekuwa nikiongea kwa sauti kali zaidi? Kwa nini sauti Yangu imebadilika mara kwa mara sana na kwa nini njia Yangu ya kufanya kazi pia imebadilika mara kwa mara sana? Hekima Yangu imekuwa katika vitu hivi. Maneno Yangu yanasemwa kwa ajili ya kila mtu ambaye amekubali jina hili (iwapo wanaamini maneno Yangu yanaweza kutimizwa au la), hivyo maneno Yangu yanapaswa kusikizwa na kuonwa na kila mtu, na sharti yasikandamizwe kwa sababu Nina njia Yangu ya kufanya kazi na Nina hekima Yangu. Natumia maneno Yangu kuhukumu watu, kufichua watu, na kuweka wazi asili ya binadamu. Kwa hivyo, Nateua wale ambao Nachagua, na kwa hivyo Naondoa wale ambao Sijajaalia au kuchagua. Haya yote ni hekima Yangu na ajabu ya kazi Yangu. Hii ni mbinu Yangu hasa katika awamu hii ya kazi Yangu. Kati ya watu, kuna yeyote anayeweza kufahamu mapenzi Yangu? Kati ya watu, kuna yeyote anayeweza kufikiria mzigo Wangu? Anayefanya kazi ni Mimi, Mungu Mwenyewe. Kutakuwa na siku, mtakapoelewa kabisa umuhimu wa maneno haya Yangu, na mtakuwa dhahiri kabisa kuhusu kwa nini Nataka kuongea maneno haya. Hekima Yangu haina mwisho, haina kikomo, na haiwezi kupimika, na haiwezi kupenyeka kabisa na wanadamu. Wanaweza kuona tu sehemu yake kutoka kwa vitu Mimi hufanya, lakini kile wanachoona bado kina dosari na bado si kamili. Wakati ambapo mmebadilika kabisa kutoka kwa awamu hii hadi kwa awamu inayofuata, basi mtakuwa na uwezo wa kuiona dhahiri. Kumbukeni! Sasa ndiyo enzi ya thamani zaidi—ni awamu ya mwisho ambayo mtakuwa katika mwili. Maisha yenu sasa hivi ni mwisho wa maisha yenu ya kimwili. Mnapoingia dunia ya kiroho kutoka kwa mwili, wakati huo maumivu yote yatawaacha. Mtafurahia na kushangilia sana, na mtaruka kwa shangwe bila kuacha. Lakini lazima muwe dhahiri kwamba maneno haya Ninayoongea ni ya wazaliwa wa kwanza tu, kwa sababu wazaliwa wa kwanza tu ndio wanaostahili baraka hii. Kuingia katika dunia ya kiroho ndiyo baraka kuu zaidi, baraka ya juu zaidi, na raha ya thamani zaidi. Sasa kile mnachopata kula na kile mnachopata kuvaa si chochote zaidi ya raha za mwili, na ni neema, ambayo Sijali kamwe. Lengo la kazi Yangu liko katika awamu inayofuata (kuingia katika dunia ya kiroho na kukabili ulimwengu dunia).

Nimesema kwamba joka kubwa jekundu tayari limerushwa chini na Mimi na kupondwa. Mnawezaje kukosa kuyaamini maneno Yangu? Kwa nini bado mnatamani kuvumilia mateso na dhiki kwa ajili Yangu? Je, hii si gharama ya isiyofaa nyinyi kuilipa? Nimewakumbusha mara nyingi kwamba mnahitaji tu kuona raha, wakati Nafanya kazi kibinafsi: Kwa nini mna hamu sana ya kuchukua hatua? Kwa kweli hamjui jinsi ya kuona raha! Nimetayarisha kabisa kila kitu kwa ajili yenu: Kwa nini hakuna kati yenu ambaye amekuja Kwangu kukichukua? Bado hamna uhakika kuhusu kile Nimesema! Hamnielewi! Mnadhani kwamba Ninaongea masihara matupu na nyinyi ni wapumbavu kweli! (Matayarisho kamili Ninayoongea kuhusu yanamaanisha kwamba mnapaswa kuniheshimu zaidi na kuomba zaidi mbele Yangu, wakati Nitafanya kazi kibinafsi kulaani kila mmoja ambaye hunipinga, na kuadhibu kila mmoja anayewatesa.) Nyinyi hamjui chochote kuhusu maneno Yangu! Nafichua mafumbo Yangu yote kwenu, na wangapi kati yenu wanayaelewa kweli? Wangapi kati yenu wanayaelewa kwa kina? Kiti Changu cha enzi ni nini? Fimbo Yangu ya chuma ni nini? Nani kati yenu anajua? Kiti Changu cha enzi kinapotajwa, watu wengi zaidi hufikiri hapo ndipo Ninapoketi, au kwamba kinarejelea makazi Yangu, kwa Yule mtu Niliye. Huu wote ni ulewa usio sahihi—ni fujo yenye mkanganyo kabisa! Hakuna kati ya uelewa huu ambao ni sahihi, sivyo? Hii ndiyo njia nyinyi nyote mnalielewa na kulifahamu—huku ni kupotoka kwa kukithiri kwa ufahamu! Mamlaka ni nini? Ni nini uhusiano kati ya mamlaka na kiti cha enzi? Kiti cha enzi ni mamlaka Yangu. Wazaliwa Wangu wa kwanza wanapotukuza kiti Changu cha enzi, huo ndio wakati ambao wazaliwa Wangu wa kwanza watapokea mamlaka kutoka Kwangu. Mimi tu ndiye niliye na mamlaka, hivyo Mimi tu ndiye niliye na kiti cha enzi. Kwa maneno mengine, baada ya wazaliwa Wangu wa kwanza kuteseka kwa njia sawa na Nilivyoteseka, watakubali kile Nilicho na kile Ninacho, na watapokea kila kitu kutoka kwangu, na huu ndio mchakato ambao kwao watafikia hadhi ya mzaliwa wa kwanza. Utakuwa wakati wazaliwa Wangu wa kwanza watakapotukuza kiti Changu cha enzi, na utakuwa wakati ambapo watakubali mamlaka kutoka kwangu. Sasa mnapaswa kuelewa hili! Kila kitu Ninachosema ni dhahiri na kisichokuwa na utata kabisa ili kila mtu aelewa. Wekeni kando dhana zenu wenyewe, na ngojeni kukubali mafumbo ambayo Nafichua kwenu! Hivyo ni nini fimbo ya chuma? Katika awamu iliyopita ilimaanisha maneno Yangu makali, lakini sasa ni tofauti na zamani: Sasa fimbo ya chuma hurejelea matendo Yangu, ambayo ni misiba mikuu inayobeba mamlaka. Kwa hivyo, kwa kutajwa fimbo ya chuma, iko pamoja na mamlaka, Maana ya awali ya fimbo ya chuma inarejelea misiba mikuu—ni sehemu ya mamlaka. Kila mtu lazima aone hili dhahiri na hivyo tu ndipo anaweza kufahamu mapenzi Yangu na kupokea ufunuo kutoka kwa Maneno Yangu. Yeyote ambaye ana kazi ya Roho Mtakatifu hushikilia fimbo ya chuma katika mkono wake, na ni yeye ambaye ana mamlaka na ana haki ya kutekeleza misiba yoyote mikuu. Hiki ni kishazi kimoja cha amri Yangu ya utawala.

Kila kitu kiko wazi kwenu (kurejelea sehemu ambayo imesisitizwa dhahiri), na kila kitu kinafichwa kutoka kwenu (kurejelea sehemu ya siri ya maneno Yangu) Nazungumza hekima: Nawaruhusu muelewe tu maana halisi ya baadhi ya maneno Yangu, Nikiwaruhusu kufahamu maana ya mengine (lakini watu wengi zaidi hawana uwezo wa kuelewa), kwa sababu huu ndio mpangilio wa kazi Yangu. Ninaweza tu kuwaambia maana ya kweli ya maneno Yangu wakati mtafika kimo fulani. Hii ni hekima Yangu na haya ni matendo Yangu ya ajabu (ili kuwakamilisha na ili kumshinda Shetani kabisa na kuaibisha maibilisi). Si hadi muingie katika eneo jingine ndipo mtakuwa na uwezo wa kuelewa kabisa. Lazima Nifanye kwa njia hii kwa sababu katika dhana za binadamu kuna vitu vingi watu hawawezi kuelewa kabisa, na hata Nikiongea dhahiri bado hamtaelewa. Akili za watu ni, hata hivyo, finyu, na kuna vitu vingi ambavyo Ninaweza tu kuwasilisha kwenu baada ya nyinyi kuingia katika dunia ya kiroho; vinginevyo, mwili wa binadamu ni hafifu na hili linaweza tu kuvuruga usimamizi Wangu. Hii ndiyo maana ya kweli ya “mpangilio wa kazi Yangu” Ninayoongea kuhusu. Katika dhana zenu mnanielewa kwa kiasi gani? Uelewa wenu hauna dosari? Je, ni maarifa mnayo katika roho? Kwa hivyo, lazima Niwaruhusu mbadilike kuingia katika eneo jingine ili mkamilishe kazi Yangu na kufanya mapenzi Yangu. Hivyo ni nini hasa eneo hili jingine? Je, kwa kweli ni, aina ya mtazamo wa uvukaji mipaka, kama wafikiriavyo watu? Je, kwa kweli ni kitu kama hewa ambacho hakiwezi kuonekana ama kuguswa, ilhali kipo? Kama Nilivyosema, hali ya kuwa katika mwili ni ile ya kuwa na nyama na mfupa—iliyo na muundo na umbo. Hili ni kweli kabisa na la kuaminika, na kila mtu lazima aliamini. Huu ndio uhalisi katika hali ya kimwili. Zaidi ya hayo, katika mwili hakuna mambo ambayo watu huchukia. Lakini hali hii ni nini hasa? Watu wanapopita kutoka kwa nyama hadi kwa mwili, kundi kikubwa lazima kijitokeze. Hiyo ni kusema, watatoroka kutoka kwa makazi yao ya kimwili, na inaweza kusemwa kwamba kila atafuata aina yake mwenyewe: Nyama hukusanyika kwa nyama na mwili hukusanyika kwa mwili. Sasa wale wanaotoroka kutoka kwa makazi yao, wazazi wao, wake, waume, wana, na binti, huanza kuingia katika dunia ya kiroho. Mwishoni, ni njia hii: Hali katika dunia ya kiroho ni kwamba wazaliwa wa kwanza wanakusanyika pamoja, wakiimba na kucheza, kusifu na kushangilia jina Langu takatifu. Na hili ni tukio ambalo ni zuri na jipya daima. Wote ni wana Wangu wapendwa, daima wakinisifu bila kuacha, daima wakitukuza jina Langu takatifu. Hii ndiyo hali baada ya kuingia katika dunia ya kiroho, hii pia ni kazi baada ya kuingia katika dunia ya kiroho, na hii pia ndiyo hali ambayo Nimeongea kuhusu, ya kuchunga kanisa katika dunia ya kiroho. Zaidi ya hayo, ni kwamba nafsi Yangu huonekana katika kila taifa la ulimwengu na kati ya mataifa yote na watu wote, ikiwa na mamlaka Yangu, ghadhabu Yangu, na hukumu Yangu, na hata zaidi, ikiwa na fimbo Yangu ya chuma kutawala mataifa yote na watu wote. Hili, kati ya watu wote na ulimwengu mzima, hutoa ushahidi Kwangu unaotetemesha mbingu na ardhi, ukisababisha watu wote na vitu vyote juu ya milima, ndani ya mito, ndani ya maziwa, na katika miisho ya dunia kunisifu na kunitukuza, na kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, Muumba wa vitu vyote, Anayeongoza kila kitu, husimamia kila kitu, huhukumu kila kitu, hufanikisha kila kitu, huadhibu kila kitu, na huangamiza kila kitu. Huku, basi, ni kuonekana kwa nafsi Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 98

Inayofuata: Sura ya 100

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp