Sura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni. Hili linamaanisha kwamba tutarudi kutoka kwa nyama hadi kwa mwili wa awali. Hii ndiyo maana ya kweli ya “kurudi Sayuni.” Hii pia ndiyo maana ya kweli na lengo la mpango Wangu mzima wa usimamizi, na hata zaidi sehemu muhimu zaidi ya mpango Wangu wa usimamizi, ambayo hakuna anayeweza kuizuia, na ambayo itatimizwa mara moja. Kama nyinyi mko katika nyama hamtawahi kamwe kuondoa mawazo na fikira za binadamu, sembuse kutupa mbali hewa ya kidunia, kutoa vumbi, na nyinyi daima mtakuwa udongo; ni wakati mko katika mwili tu ndio mtastahiki kufurahia baraka. Je, baraka ni nini? Je, mnakumbuka? Katika mwili hakuwezi kuwa na fikira ya baraka, hivyo kila mwana wa kwanza kuzaliwa lazima afuate njia kutoka kwa nyama hadi kwa mwili. Katika nyama mnadhulumiwa na kuteswa na joka kubwa jekundu (hii ni kwa sababu nyinyi hamna nguvu, hamjapata utukufu wowote), lakini katika mwili itakuwa tofauti sana, na mtajivunia na kuwa na furaha: Siku za kukandamizwa zitaenda kabisa na nyinyi daima mtakuwa mmefunguliwa na kuachwa huru. Lazima iwe hivi kama Ninafaa kuongeza kile Mimi Nilicho na kile Ninacho ndani yenu. Vinginevyo, nyinyi mtakuwa tu na sifa Zangu. Haijalishi jinsi mtu huiga mtu mwingine kwa nje, hawawezi kuwa sawa kabisa. Katika mwili mtakatifu wa kiroho tu (hii inarejelea mwili) ndio tunaweza kuwa sawa kabisa. (Hii inarejelea kuwa na sifa sawa, kuwa na nafsi sawa, mali sawa, na kuweza kuwa wenye mawazo sawa, kuungana, bila kugawanyika na kutengeka, kwa kuwa yote ni mwili mtakatifu wa kiroho).

Kwa nini sasa mnaanza kuchukia dunia, na kuchukizwa na kila aina ya mambo yanayokera kama kula, kuvaa, na kadhalika, na msiweze kusubiri kuzitupa mbali? Hii ndiyo ishara kwamba mtaingia katika dunia ya kiroho (mwili), na nyinyi nyote mna jakamoyo ya haya (ingawa si wote kwa kiwango sawa). Nitatumia kila aina ya watu tofauti, matukio tofauti, na mambo tofauti kutumikia hatua Yangu muhimu zaidi, na yote yatatoa huduma kwa ajili Yangu. Lazima Nifanye hivyo. (Bila shaka Mimi siwezi kukamilisha hili katika nyama, na Roho Wangu mwenyewe tu ndiye Anayeweza kufanya kazi hii, kwa sababu wakati haujawasili.) Hii ndiyo sehemu ndogo ya mwisho ya kazi kwa ajili ya ulimwengu dunia wote. Kila mtu atanisifu na kunipokea Mimi kwa shangwe. Kazi Yangu kuu ni kamili: Vitasa saba vya mapigo vinamwagika kutoka mkono Wangu, ngurumo saba zinatoa sauti, mabaragumu saba yatoa sauti, na mihuri saba inafunguliwa, kwa ulimwengu dunia, kwa mataifa yote na watu wote, na kwa milima, mito na kila kitu. Je, vitasa saba vya mapigo ni vipi? Je, vimeelekezwa kwa nini? Kwa nini Ninasema kwamba vitamwagika kutoka kwa mkono Wangu? Muda mrefu utapita kabla ya kila mtu kuridhishwa, na kabla ya kila mtu kuelewa kabisa. Hata Nikiwaambia sasa nyinyi mtaelewa sehemu ndogo tu. Kulingana na fikira za binadamu, vitasa saba vya mapigo vinaelekezwa kwa nchi zote na watu wote wa dunia, lakini kwa kweli hali haiko hivi. Vitasa hivi saba vya mapigo vinarejelea ushawishi wa Shetani ibilisi na njama ya joka kubwa jekundu (chombo ambacho Mimi hutumia kutoa huduma kwa ajili Yangu). Wakati huo Nitamfungulia Shetani na joka kubwa jekundu kuadibu wana na watu, na hapo litafichuliwa wana ni akika nani na nani ndio watu. Wale ambao wamedanganywa ni wale ambao hawakuwa walengwa wa kujalia Kwangu kabla, huku wazaliwa Wangu wa kwanza kwa wakati huu watakuwa wakitawala na Mimi. Kupitia hili wana na watu wanafanywa wakamilifu. Kumwagika kwa vitasa saba vya mapigo hakutaathiri mataifa yote na watu wote, lakini tu wana Wangu na watu Wangu, Baraka hazikuji rahisi, na gharama nzima lazima ilipwe. Wakati wana na watu watakua vitasa saba vya mapigo vitaondolewa kabisa na baadaye havitakuwepo. Je, ni nini ngurumo saba zinazotoa sauti? Hili si ngumu kuelewa. Wakati wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tunakuwa mwili, ngurumo saba zitatoa sauti. Hili litatisika ulimwengu wote, kana kwamba mbingu na dunia zimepinduliwa juu chini. Kila mtu atajua hili, na hakuna mmoja ambaye hatalijua hili. Wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tutakuwa pamoja katika utukufu na tutaanza hatua ifuatayo ya kazi. Watu wengi watapiga magoti kwa ajili ya huruma na msamaha kwa sababu ngurumo saba zinatoa sauti. Lakini hii haitakuwa tena Enzi ya Neema: itakuwa wakati wa ghadhabu. Na kuhusu watu wote watendao uovu (wale ambao huzini, au hujihusisha na fedha chafu, au wana mipaka isiyo wazi kati ya wanaume na wanawake, au ambao hukatiza au kuharibu usimamizi Wangu, au ambao roho zao zimezibwa, au waliopagawa na mapepo mabaya, na kadhalika—wote isipokuwa wateule Wangu), hakuna kati yao ataachiliwa, wala yeyote kusamehewa, lakini wote watatupwa chini Kuzimu na kufa milele! Mabaragumu saba kutoa sauti hakurejelei mazingira makubwa mabaya, wala hakurejelei chochote kutangazwa kwa dunia, ambayo ni dhana ya binadamu kabisa. Mabaragumu saba yanarejelea matamko Yangu ya ghadhabu. Wakati sauti Yangu (hukumu ya adhimu na hukumu ya ghadhabu) inatoka, mabaragumu saba hutoa sauti. (Sasa hivi, nyumbani Mwangu, hili ndilo la nguvu zaidi, ambalo hakuna anayeweza kulitoroka.) Na mapepo wote katika kuzimuni na jahanamu, wakubwa kwa wadogo, watafunika vichwa vyao mikononi mwao na kukimbia kwa pande zote, wakilia na kusaga meno yao, wakiwa na aibu na bilapopote pa kujificha. Kwa sasa si mabaragumu saba yanayoanza kutoa sauti, lakini ni ghadhabu Yangu na pia hukumu Yangu kali zaidi, ambayo hakuna anayeweza kutoroka, na wote lazima wapitie. Kwa wakati huu kile ambacho kimefichuliwa si yaliyomo kwa mihuri saba. Mihuri saba ni baraka mtakayofurahia baadaye. Kile kinachodaiwa kuwa nafasi wazi hurejelea kuwajuza tu, lakini bado hamjafurahia baraka hizi. Wakati mtazifurahia baraka hizi, basi mtajua yaliyomo kwa mihuri saba. Sasa mnagusia tu sehemu ambayo bado si kamili. Naweza tu kuwaambia hatua kwa hatua katika kazi ya baadaye, hivyo mtaipitia binafsi na kuhisi utukufu usioweza kufananishwa, na mtakuwa katika hali ya raha isiyoisha.

Kuwa na uwezo wa kufurahia baraka za wazaliwa wa kwanza si kitu rahisi, wala si kitu mtu wa kawaida anaweza kufikia. Nitahimiza mara moja tena na kusema kwa nguvu zaidi kwamba lazima Niweke mahitaji makali kwa wazaliwa Wangu wa kwanza. Vinginevyo hawawezi kutukuza jina Langu. Nimekataa kwa uthabiti yeyote anaye sifa mbaya duniani, na hata zaidi Ninakataa yeyote ambaye ni mzinzi. (Hawana mgao katika kuwa watu wa Mungu—kuhusu hili Nasisitiza hasa.) Msifikiri kwamba yaliyopita yameenda—kunawezaje kuwa na kitu kizuri hivi! Je, ni rahisi sana kupata hadhi ya wazaliwa wa kwanza? Na kwa njia sawa Nakataa yeyote ambaye ananipinga, yeyote ambaye hanitambui katika mwili Wangu, yeyote ambaye anaingilia kati Ninapofanya mapenzi Yangu, na yeyote ambaye ananitesa—Mimi ni mkali sana (kwa sababu Nimechukua tena nguvu Yangu kabisa)! Hatimaye, kwa njia sawa Nakataa yeyote ambaye katika maisha yake hajakuwa na vikwazo. Nataka wale ambao, kama Mimi, hutoka katika mateso yao, hata kama ni mateso madogo. Vinginevyo, Nitawafukuza watu kama hawa nje. Msiwe bila aibu, ukitaka kuwa mzaliwa Wangu wa kwanza, ukijionyesha mbele Yangu. Kujeni ghafula kwa haraka kwa upande Wangu! Umeniambia awali mambo ya upuuzi, ukitafuta kushinda furaha Yangu! Huu ni upofu! Je, hujui kwamba Nakuchukia wewe, bazazi! Je, unafikiri Mimi sijui biashara yako isiyo halisi? Unajificha tena na tena! Je, hujui kwamba umefichua uso wako wa kishetani? Ingawa watu hawawezi kuuona, unafikiri kwamba Mimi siwezi kuuona? Wale wanaotoa huduma Kwangu si vitu vizuri bali ni kikundi cha mabazazi. Mimi lazima Niwashughulikie na Nitawarusha katika shimo lisilo na mwisho na kuwachoma!

Mtu ambaye huongea kwa njia isiyo ya kumcha Mungu, anayetenda bila imani, na ambaye hashirikiani na wengine vizuri, mtu kama huyu angetaka kuwa mfalme. Je, wewe huoti ndoto? Je, wewe hujadanganyika? Je, wewe huoni ulicho? Wewe ni bazazi! Je, kuna matumizi ya mtu kama huyu? Nendeni haraka kutoka kwa macho Yangu! Kila mtu anapaswa kuwa na uelewa wazi wa Ninachosema, atiwe moyo na maneno Yangu, atambue kudura Yangu, na kujua hekima Yangu. Mara nyingi imesemwa kwamba mwili mtakatifu wa kiroho umeonekana. Hata hivyo, mnasema mwili mtakatifu wa kiroho umeonekana au la? Kile Ninachosema ni usemi mtupu? Ni nini mwili mtakatifu wa kiroho? Ni katika hali gani kuna mwili mtakatifu wa kiroho? Kwa wanadamu haiwezi kufikirika na haiwezi kueleweka. Nawaambia: Katika nafsi Yangu kuna ukamilifu, na yote ni wazi, na kila kitu ni huru (kwa sababu Nafanya kilicho cha hekima na Naongea bila kuzuiwa). Miongoni mwa mambo Mimi hufanya, hakuna ya kuaibisha, na kila kitu hufanywa katika mwanga, ili kila mtu aweze kuridhishwa kabisa. Zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kunyakua chochote ambacho kinaweza kutumika dhidi Yangu. Haya ni maelezo ya “mtakatifu” katika mwili mtakatifu wa kiroho. Hivyo Nimesisitiza tena na tena kwamba Mimi sitaki wowote ambao hufanya vitu vya aibu, Hiki ni kitu kimoja cha amri Yangu ya utawala na pia ni sehemu moja ya tabia Yangu. “Mwili wa kiroho” unarejelea tamko Langu. Ninachosema daima kina madhumuni, daima kina hekima, lakini si chini ya udhibiti. (Mimi husema Ninachotaka kusema, na ni Roho Wangu kutamka sauti Yake na ni nafsi Yangu kuongea). Kile Ninachosema hutolewa kwa huru, na wakati hakiridhishi dhana za watu, basi huo ndio wakati wa kufichua watu. Ni mpangilio Wangu sahihi. Kwa hivyo, kila wakati ambapo mtu Niliye ananena au kutenda, daima ni nafasi nzuri kufichua kiini cha Shetani. Wakati ambapo mtu Niliye amewekwa wakfu, mwili mtakatifu wa kiroho unaibuka. Katika siku zijazo mwili mtakatifu wa kiroho hurejelea mwili, na kuna vipengele viwili kwa maana. Kuna kipengele kimoja cha maana kwa sasa, na kuna kipengele kingine cha maana baadaye. Lakini kwa siku zijazo, mwili mtakatifu wa kiroho utakuwa tofauti sana na wa sasa—utakuwa tofauti kati ya mbingu na dunia, Hakuna anayeweza kuuelewa na itanibidi kuufichua kwenu kibinafsi.

Iliyotangulia: Sura ya 93

Inayofuata: Sura ya 95

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp