Sura ya 93

Ukweli unatimizwa mbele ya macho ya mtu na mambo yote yametimizwa. Kazi Yangu inapata hatua, ikipanda juu kama roketi iliyofyatuliwa, ambayo hakuna mtu aliwahi kutarajia. Ni baada ya vitu kufanyika ndipo mtaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu. Watoto wa joka kubwa jekundu si wa pekee na lazima wafanywe kushuhudia matendo Yangu ya ajabu kwa macho yao wenyewe. Usidhani kwamba Sitakutelekeza, sasa kwa kuwa una uhakika kunihusu baada ya kuona matendo Yangu—si rahisi hivyo! Yote ambayo Nimesema na mambo ambayo Nimeamua hakika Nitatimiza, na hayatarudi Kwangu yakiwa matupu. Nchini China, kando na walio wachache ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza, kuna wachache ambao ni watu Wangu. Kwa hivyo leo Nasema wazi kwenu (watoto wa joka kubwa jekundu, ambao wamenitesa vibaya sana) kwamba lazima msishikilie matumaini yoyote makubwa, na kwamba lengo la kazi Yangu (tangu uumbaji wa dunia) limekuwa kwa wazaliwa Wangu wa kwanza na kwa mataifa kadhaa nje ya Uchina. Kwa sababu hii, wakati wazaliwa Wangu wa kwanza wamekomaa, mapenzi Yangu yatatimizwa. (Punde wazaliwa Wangu wa kwanza wamekomaa, mambo yote yatafanyika, kwa kuwa kazi iliyo mbele imepewa wao.) Sasa Naruhusu watu hawa kuona sehemu ya matendo Yangu ya ajabu ili tu kwamba joka kubwa jekundu liaibishwe. Watu hawa hawawezi kabisa kupata raha katika hilo ila wanaweza tu kufurahi kwamba wananitolea huduma. Na hawana mbadala, kwa kuwa Nina amri Zangu za utawala na hakuna anayethubutu kuzikosea.

Sasa Nitashiriki kuhusu hali zinazohusiana na kuja kwa wageni, ili mweze kuzijua kabla zitokee, mtayarishe kila kitu vizuri ili kushuhudia jina Langu, na kuwa juu yao na kuwatawala. (Kwa sababu mkubwa zaidi kati yao bado ndiye mdogo zaidi miongoni mwenu, Nasema ninyi muwe juu yao na kuwatawala.) Watu hawa wote wamepata ufunuo wa Roho Mtakatifu na baadaye wote watakusanyika Uchina, kana kwamba kwa mpango wa kabla. Joka kubwa jekundu linastuliwa na linajaribu kufanya kila linaloweza kupinga, lakini kumbukeni jambo moja! Mpango Wangu wa usimamizi umetimika kabisa, na hakuna kitu na hakuna mtu anayethubutu kuzuia hatua Zangu. Ninawapa ufunuo kila wakati, na wanatenda kwa kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu. Bila shaka hawatateseka vifungo vya joka kubwa jekundu, kwa kuwa nami yote ni ufunguliwaji na uhuru. Nimepanga mambo yote kwa njia ya kufaa, Nikiwangoja mwandae kazi ya matayarisho kuwaongoza. Nimesema hili daima kwenu zamani, lakini wengi wenu mnaamini kwa njia nusu bado. Hali ni gani sasa? Mmepigwa na bumbuazi, sivyo?

Mambo haya yote ni ya baadaye; jambo kuu ni kwenu kuandaa kazi yote ya matayarisho haraka iwezekanavyo. Msishtuke. Yule anayefanya kazi ni Mimi na, wakati utakapofika, Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe. Nimelivunja joka kubwa jekundu vipande vipande. Yaani, Roho Wangu ametoka kwa watu wote isipokuwa wazaliwa Wangu wa kwanza (sasa kuifanya kuwa rahisi zaidi kufichua nani ni watoto wa joka kubwa jekundu). Watu hawa wamemaliza kunitolea huduma na Nitawatuma tena kwa shimo lisilo na mwisho. (Inamaanisha kwamba Sitamtumia hata mmoja wao. Kutoka sasa kuendelea wazaliwa Wangu wa kwanza watafichuliwa kabisa na wale ambao wako kando Yangu na wanaofaa kwa matumizi Yangu watakuwa wazaliwa Wangu wa kwanza.) Wazaliwa Wangu wa kwanza, mnafurahia kirasmi baraka Ninazowapa (kwa kuwa wale Ninaowachukia sana wameonyesha tabia yao ya kweli), na kuanzia hapo na kuendelea hakuna kitu kitakachofanyika tena na ninyi ambacho kinaniasi. Mna uhakika asilimia mia moja kunihusu. (Ni leo tu ndipo hili linakamilishwa kikamilifu, na Nilikuwa nimeagiza kabla wakati huu.) Yote mnayofikiri mioyoni na akilini mwenu ni upendo usio na mwisho Kwangu, uchaji Kwangu, na mnanisifu na kunitukuza nyakati zote. Kweli mnaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo Wangu, mkiishi katika mbingu ya tatu. Furaha na ridhaa kubwa isiyo na kifani! Ni ufalme mwingine ambao watu wanaona kuwa mgumu kufikiria—dunia ya roho ya kweli!

Maafa yote yanaibuka kwa kufuatana, kila likiwa kali kuliko la awali, na hali inakuwa yenye wasiwasi kila siku. Huu ni mwanzo tu wa maafa, na maafa makali zaidi ambayo yatakuja baadaye hayafikiriki kwa mwanadamu. Acha wanangu wayashughulikie: hii ni amri Yangu ya utawala na ndiyo Niliyopanga kitambo. Ishara na maajabu yote, ambayo hayajawahi kuonwa awali na mwanadamu, huibuka kutoka Kwangu, yakionekana moja baada ya lingine kwa kila mtu (kumaanisha watu wote wa ufalme Wangu). Lakini hili ni jambo ambalo litafanyika katika siku za baadaye za karibu. Msiwe na wasiwasi. Watu wote wamezungumza awali kuhusu kuingia katika ufalme, kwa hivyo hali za kuingia katika ufalme ni zipi? Na ufalme ni nini? Ni mji yakinifu? Mnaelewa visivyo. Ufalme hauko duniani, wala hauko katika mbingu yakinifu, lakini badala yake ni dunia ya roho ambayo haiwezi kuonwa au kuguswa na mwanadamu. Ni wale tu ambao wanafanywa kuwa kamili kabisa na Mimi na kufurahia baraka Zangu baada ya kukubali jina Langu wataweza kuingia ndani. Dunia ya roho ambayo imetajwa awali mara nyingi ni sehemu ya juu ya ufalme. Kuingia katika ufalme kwa kweli, hata hivyo, si jambo rahisi. Wale ambao wanauingia lazima wapate ahadi Yangu na lazima wawe watu ambao Nimewajaalia na kuwachajua Mwenyewe. Kwa hivyo dunia ya roho si mahali ambapo watu wanaweza kuja na kuenda watakavyo. Ufahamu wa watu wa hili ulikuwa wa juu juu sana na ilikuwa dhana ya mwanadamu tu. Wale wanaoingia katika ufalme tu ndio wanaoweza kufurahia baraka, kwa hivyo baraka hizi haziwezi kufurahiwa na mwanadamu tu, lakini hata zaidi haziwezi kuonekana, na hii ndiyo amri Yangu ya mwisho ya utawala.

Iliyotangulia: Sura ya 92

Inayofuata: Sura ya 94

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp