Sura ya 110

Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu. Sayuni ndipo Ninapoishi na ndiyo hatima Yangu; ni hapo ambapo Mimi hufichua uweza Wangu, na ni hapo ndipo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja Nami tutashiriki furaha zetu za familia. Ni hapo ndipo Mimi nitaishi nao milele yote. Sayuni, mahali pazuri; Sayuni, mahali ambapo watu hutamani sana; watu wasiohesabika wamepatamani katika enzi zote, lakini kutoka mwanzo, hakuna mtu hata mmoja ambaye ameingia Sayuni. (Wala hata watakatifu na manabii wowote tangu enzi zilizopita. Hii ni kwa sababu Nawachagua wazaliwa Wangu wa kwanza katika siku za mwisho; na wote wanazaliwa wakati huu; na kupitia hii rehema Yangu na neema Yangu ambayo Nimezungumzia ni dhahiri zaidi.) Kila mtu ambaye sasa ni mzaliwa Wangu wa kwanza ataingia Sayuni pamoja na Mimi na kufurahia baraka hiyo. Mimi nawainua wazaliwa Wangu wa kwanza hadi kiwango fulani kwa sababu wana uhodari Wangu na mfano Wangu wenye utukufu na wana uwezo wa kuwa na ushuhuda Wangu na pia kunitukuza na kuishi kwa kunidhihirisha. Hata zaidi, wana uwezo wa kumshinda Shetani na kuliaibisha joka kubwa jekundu. Na ni kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza ni mabikira safi; wao ni kile Ninachokipenda, na ni wale ambao Nimewachagua na kupendelea. Sababu ya Mimi kuwainua wao ni kuwa wana uwezo wa kusimama katika nafasi zao wenyewe na wana uwezo wa kunitumikia kwa unyenyekevu na kimya na kuwa na ushuhuda Wangu mkubwa Nimetumia nguvu Yangu yote kwa wazaliwa Wangu wa kwanza na kwa makini Nimepanga watu, matukio, na mambo ya aina zote kwa ajili ya huduma zao. Mwishowe Mimi nitamfanya kila mtu aone utukufu Wangu mzima kutoka kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, na Nitamfanya kila mtu aridhike kabisa na Mimi kwa sababu ya wazaliwa Wangu wa kwanza. Sitamlazimisha pepo yeyote, na Sina hofu nao kukimbia kote au kutojali kwao kwa sababu Ninao washahidi, na Nina mamlaka mikononi Mwangu. Sikilizeni, watu wa aina ya Shetani! Makusudi ya kila neno ambalo Ninalitamka na kila kitu ambacho Ninafanya ni ili kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. Kwa hivyo ni lazima wewe usikilize kwa makini amri Zangu na kutii Wazaliwa Wangu wa kwanza; vinginevyo Nitakushughulikia kwa kukufanya upitie maangamizo ya mara moja! Wazaliwa Wangu wa kwanza tayari wameanza kutekeleza amri Zangu za utawala kwa sababu ni wao tu wanaostahili kushikilia kwa nguvu kiti Changu cha enzi, na tayari Nimewapaka mafuta. Yeyote ambaye hatii wazaliwa Wangu wa kwanza kwa hakika hana manufaa. Bila shaka ametumwa na joka kubwa jekundu kuvuruga mpango Wangu wa usimamizi, na mwovu wa aina hiyo atasukumwa nje ya nyumba Yangu mara moja. Sitaki kitu cha aina hiyo kinifanyie huduma—kitakumbana na uharibifu wa milele, na kitakumbana nao haraka sana, bila kuchelewa! Wale ambao hunihudumia ni lazima tayari wamepokea idhini Yangu; lazima wawe watiifu na wasitilie maanani gharama wanayolipa. Kama ni waasi hawastahili kutoa huduma Kwangu na Sihitaji kiumbe kama huyo. Watakimbia kwa haraka—Mimi siwataki kabisa! Lazima uwe na hakika kuhusu hili sasa! Wale ambao hufanya huduma kwa ajili Yangu ni lazima waifanye vizuri na wasisababishe matatizo. Ukihisi kuwa huna matumaini na uanze kusababisha matatizo—Nitakumaliza mara moja. Je, ninyi ambao mnatoa huduma kwa ajili Yangu mna uhakika kuhusu hilo? Hii ni amri Yangu ya utawala.

Kuwa na ushuhuda Wangu ni jukumu la wazaliwa Wangu wa kwanza, hivyo Siwahitaji ninyi kwamba mfanye lolote kwa ajili Yangu—Nitaridhishwa mradi tu mtekeleze wajibu wenu vizuri na kufurahia baraka ambazo Nimewapa. Niliposafiri katikaulimwengu mzima na miisho ya dunia, Niliwachagua na kuwafanya wazaliwa Wangu wa kwanza wawe wakamilifu. Hili ni jambo ambalo Nilikamilisha kabla ya Mimi kuumba ulimwengu; hakuna mtu kati ya wanadamu analijua hilo, lakini kazi Yangu ilitimizika kwa utulivu. Hilo halikubaliani na fikira za binadamu! Lakini ukweli ni ukweli na hakuna anayeweza kuubadilisha. Mapepo wakubwa kwa wadogo wamefichua umbo lao la kweli kutoka kwa unafiki wao, na wamekuwa chini ya adhabu Yangu kwa viwango tofauti. Kuna hatua katika kazi Yangu na kuna hekima katika maneno Yangu. Je, mmeona kitu chochote kutoka kwa kile Ninachosema na kufanya? Je, ni kufanya tu vitu na kusema mambo? Je, maneno Yangu ni makali, au ya kuhukumu, au ya kufariji tu? Hiyo ni rahisi sana, lakini kwa watu, kuona hiyo si rahisi hata kidogo. Hakuna hekima, hukumu, haki, uadhama, na faraja pekee katika maneno Yangu, lakini hata zaidi lina kile Nilicho nacho na kile Nilicho. Kila mojawapo ya maneno Yangu ni mafumbo ambayo hayawezi kufichuliwa na watu. Maneno Yangu hayaeleweki kabisa, na ingawa mafumbo yamefichuliwa, kulingana na uwezo wa wanadamu bado ni nje ya wigo wao wa mawazo na ufahamu. Neno rahisi sana Kwangu kuelewa ni jambo gumu zaidi kwa watu kuelewa, kwa hivyo tofauti kati ya Mimi na mwanadamu ni tofauti kati ya mbingu na nchi. Hii ndiyo sababu Nataka kubadilisha kabisa umbo la wazaliwa Wangu wa kwanza na kuwafanya wao kuingia katika mwili kabisa. Katika siku zijazo, hawataingia tu katika mwili kutoka kwa nyama, lakini watabadilisha umbo lao ndani ya mwili kwa viwango tofauti. Huu ni mpango Wangu. Hili ni jambo ambalo wanadamu hawawezi kulifanya—wao hawana namna ya kufanya hivyo kabisa—hivyo sasa hata kama Ningewaambia kwa kina, bado msingeelewa. Unaweza tu kuingia katika hali isiyo ya kawaida. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye busara.

Mnapoona mafumbo nyote mna mjibizo kiasi. Hata ingawa hamkubali au kukiri hayo katika nyoyo zenu, mnayakiri kwa maneno yenu. Mtu wa aina hii ni yule mdanganyifu zaidi, na Ninapofichua mafumbo, Nitawaondoa na kuwaacha mmoja baada ya mwingine. Lakini kila kitu Nifanyacho ni kwa hatua. Sitendi mambo kwa haraka au kufikia hitimisho bila kufikiri; hii ni kwa sababu Nina tabia ya uungu. Watu hawawezi kabisa kuona bayana Ninachofanya sasa, Nitakachofanya katika hatua Yangu ifuatayo. Nitakaponena tu kuhusu mbinu Yangu ya kufanya kazi katika hatua ifuatayo ndipo watu wataweza kunifuata na kupiga hatua moja mbele. Kila kitu hufanyika ndani ya maneno Yangu, kila kitu hufichuliwa ndani ya maneno Yangu, hivyo hakuna yeyote anayetakiwa kuwa na pupa—kutoa huduma Kwangu vizuri kunatosha. Kabla ya enzi Nilifanya utabiri kuhusu mtini, lakini katika enzi zote hakuna yeyote aliyekuwa ameuona mtini na hakuna yeyote ambaye angeweza kuuelezea, na hata ingawa maneno haya yalitajwa katika sifa za awali, hakuna aliyejua maana yake ya kweli. Maneno haya yaliwachanganya watu kama tu “janga kubwa,” na lilikuwa fumbo ambalo kamwe Sikutandua kwa wanadamu. Watu walidhani kuwa mti wa tini labda ulikuwa aina ya mti mzuri wa matunda, au labda kuwa zaidi ya hayo uliashiria watakatifu, lakini bado walikuwa mbali sana na maana halisi. Nitawaambia hili wakati ambapo Nitafungua kitabu Changu katika siku za mwisho. (Kitabu kinahusu maneno yote ambayo Nimeyanena, maneno Yangu katika siku za mwisho—haya yote yako ndani yake.) Mti wa tini unahusu amri Zangu za utawala, na kila mojawapo ya amri Zangu za utawala, lakini hii ni sehemu moja tu ya hayo. Kuchipua kwa mtini kunahusu Mimi kuanza kufanya kazi na kuzungumza katika mwili, lakini amri Zangu za utawala hazikuwa zimetambulishwa bado (ndio sababu hilo lilikuwa kabla ya kushuhudiwa kwa jina Langu na hakuna yeyote aliyejua amri Zangu za utawala). Wakati ambapo jina Langu linashuhudiwa na kuenea, wakati ambapo linasifiwa na watu wote, wakati ambapo amri Zangu za utawala kuzaa matunda, huo ndio wakati wa mti wa tini kuzaa matunda. Haya ni maelezo kamili na hakuna kitu kilichoachwa—vyote vinafichuliwa (Nasema hivi kwa sababu katika maneno Yangu ya awali, kulikuwa na sehemu ambayo bado Sikuwa Nimefichua kikamilifu; kwa hivyo mlihitajika kusubiri na kutafuta kwa uvumilivu.)

Nitakapowafanya wazaliwa Wangu wa kwanza kamili, Nitafichua utukufu Wangu kamili, kuonekana Kwangu kamili kwa ulimwengu dunia katika mwili, na juu ya watu wote, kwa nafsi Yangu mwenyewe; itakuwa katika Mlima Wangu wa Sayuni, katika utukufu Wangu, na itakuwa hasa katikati ya makelele ya sifa, na maadui Zangu watarudi nyuma kandokando Yangu, wakiteremka katika shimo la kuzimu, ziwa la moto wa jahanamu. Kile ambacho watu wanaweza kuwaza leo kina mpaka na hakilingani na nia Yangu ya asili; hii ndiyo sababu Mimi hulenga dhana na fikira za watu kila siku Ninaponena. Kutakuwa na siku (siku ya kuingia katika mwili), ambapo kile Ninachosema kitakuwa cha kuwafaa kabisa na hakutakuwa na upinzani wowote kabisa, na wakati huo ninyi hamtakuwa tena na mawazo yenu, na baada ya hapo Sitazungumza tena. Kwa kuwa hamna mawazo yenu wenyewe tena, Mimi nitawapa nuru moja kwa moja tu—hii ni baraka inayofurahiwa na wazaliwa Wangu wa kwanza, na huo utakuwa wakati ambapo watatawala pamoja na Mimi kama wafalme. Wanadamu hawaamini katika mambo ambayo hawawezi kufikiria, na hata kama kuna baadhi ya watu ambao wanaamini hayo, ni kwa sababu hasa ya kupatiwa nuru na Mimi. Vinginevyo hakuna yeyote ambaye angeamini, na hili ni jambo ambalo lazima lipitiwe. (Bila kupitia hatua hii, nguvu Yangu kubwa haingeweza kufichuliwa kupitia hiyo, ambayo ina maana kwamba Mimi huyatumia maneno Yangu kuwaondolea watu fikira zao. Hakuna yeyote mwingine anayeweza kufanya kazi hii, na hakuna yeyote anayeweza kuchukua nafasi Yangu. Mimi tu ndimi Ninayeweza kuimaliza, hata hivyo, hiyo si kamili. Lazima Nifanye kazi hii kupitia kwa wanadamu.) Watu hujihisi kuchangamshwa baada ya kusikia maneno Yangu, lakini mwishowe wao wote wanarudi nyuma. Hawana budi ila kufanya hivyo. Wakati huo huo, kuna mafumbo ambayo watu hawawezi kuyafahamu. Hakuna yeyote anayeweza kufikiria kile ambacho kitatokea na Nitawawezesha kuona hili katika kile ambacho Ninafichua. Kwa njia hiyo mnaweza kuona maana halisi ya msemo Wangu: “Nitang’oa wale wote ambao hawafai kwa ajili ya matumizi Yangu.” Wazaliwa Wangu wa kwanza wana maonyesho mbalimbali na vilevile maadui Wangu. Wote watafichuliwa kwenu, mmoja mmoja. Kumbuka! Yeyote isipokuwa wazaliwa Wangu wa kwanza ana kazi ya pepo wabaya. Wote hao ni vikaragosi wa Shetani. (Hivi punde watafichuliwa mmoja baada ya mwingine, lakini kuna baadhi ambao wanahitaji kufanya huduma hadi mwisho, na baadhi ambao wanahitaji kufanya huduma kwa kipindi cha muda.) Chini ya kazi ya maneno Yangu, wote wataonyesha hali zao za kweli.

Kila taifa, kila mahali, na kila dhehebu kinafurahia ukwasi wa jina Langu. Kwa sababu sasa hivi janga linajiandaa, na liko katika mshiko Wangu, na Ninajiandaa kulimuaga polepole, kila mtu anatafuta njia ya kweli kwa haraka, ambayo ni lazima itafutwe hata kama inamaanisha kulipa gharama nzima. Katika mambo yote Nina muda Wangu mwenyewe. Wakati wowote Ninaposema itakamilishwa, itakamilishwa wakati huo, kwa dakika, kwa sekunde. Hamna yeyote anayeweza kuizuia au kuisimamisha. Hata hivyo, joka kubwa jekundu ni adui Yangu aliyeshindwa. Linatenda huduma kwa ajili Yangu, na linafanya chochote Ninacholiambia bila upinzani wowote. Kweli ni mnyama Wangu wa mzigo. Wakati ambapo kazi Yangu imekamilika, Nitalitupa katika shimo la kuzimu, ndani ya ziwa la moto wa jahanamu (ambayo inarejelea wale ambao wanaangamizwa). Watakaoangamizwa hawataonja kifo tu, lakini wataadhibiwa vikali kwa ajili ya mateso yao Kwangu. Hii ni kazi ambayo bado Nitafanya kupitia watendaji huduma—Nitamfanya Shetani ajichinje mwenyewe na kujiangamiza, kuondoa kabisa ukoo wa joka kubwa jekundu. Hii ni sehemu moja ya kazi Yangu, na baada ya hapo, Nitayageukia mataifa yasiyo ya Uyahudi. Hizi ndizo hatua za kazi Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 109

Inayofuata: Sura ya 111

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp