Sura ya 111

Mataifa yote zyatabarikiwa kwa sababu Yako; watu wote watanikaribisha kwa shangwe na kunisifu kwa sababu Yako. Ufalme Wangu utafanikiwa na kukua, na utabaki milele. Hakuna mtu ataruhusiwa kuukanyaga na hakuna kitu kitaruhusiwa kuwepo ambacho hakikubaliani na Mimi, kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye uadhama na asiyekosewa Mwenyewe. Sikubali mtu yeyote anihukumu na Sikubali mtu yeyote kutolingana na Mimi. Hili linatosha kuonyesha tabia Yangu na uadhama Wangu. Mtu yeyote anaponipinga, Nitamwadhibu kwa wakati Wangu mwenyewe. Kwa nini hakuna mtu ambaye ameniona Nikimwadhibu mtu yeyote? Ni kwa sababu tu wakati Wangu haujafika bado na mkono Wangu bado haujatenda kweli. Ingawa maafa makubwa yametolewa kwa kishindo, hili linazungumzia tu kile ambacho maafa makubwa yanajumuisha, wakati uhalisi wa maafa makubwa haujamfikia hata mtu mmoja. Je, mmeelewa chochote hata kidogo kutoka kwa maneno Yangu? Nitaanza kuachilia uhalisi wa maafa makubwa leo. Baada ya hili, yeyote atakayenipinga atapigwa chini na mkono Wangu. Zamani Nimewafichua tu watu fulani, na hakuna maafa yoyote makubwa yamefika. Leo ni tofauti na zamani. Kwa kuwa Nimewaambia nyote kuhusu kile kinachojumuisha maafa makubwa, kwa wakati uliopangwa Nitatangaza kwa umma uhalisi wa maafa makubwa. Kabla ya hili, hakuna mtu ambaye ameguswa na maafa makubwa, kwa hivyo watu wengi (yaani, wana wa joka kubwa jekundu) wameendelea kutenda kwa kutojali na kiholela. Wakati ambapo uhalisi unafika vitu hivi vitaridhishwa kabisa. Vinginevyo kila mtu atakuwa na shaka kunihusu, na hakuna mtu atakayekuwa wazi kunihusu. Hii ni amri Yangu ya utawala. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba njia Yangu ya kufanya kazi (ikirejelea njia Yangu ya kufanya kazi katika watu wote) imeanza kubadilika: Katika uzao wa joka kubwa jekundu Ninaonyesha ghadhabu Yangu, Ninaonyesha hukumu Yangu na laana Yangu, na mkono Wangu umeanza kuwaadibu wote wanaonipinga. Kwa wazaliwa wa kwanza Ninaonyesha rehema Yangu na upendo Wangu. Hata zaidi katika wazaliwa wa kwanza Ninaonyesha tabia Yangu takatifu na isiyokosewa, Ninaonyesha mamlaka Yangu, na Ninaonyesha nafsi Yangu. Watendaji huduma wametulia kunitolea huduma, na wazaliwa Wangu wa kwanza wanatambulishwa zaidi na zaidi. Kwa kuwapiga chini wale wanaonipinga Ninawaacha watendaji huduma kuona mkono Wangu usiojizuia ili waweze kunitolea huduma kwa hofu na kutetemeka, na Ninawaacha wazaliwa Wangu wa kwanza waone mamlaka Yangu na kunielewa bora zaidi ili waweze kukua katika maisha. Maneno Niliyoyasema katika kipindi cha mwisho (yakiwemo amri za utawala, unabii, na hukumu ya kila aina za watu) yanaanza kutimizwa kwa kufuatana, yaani, watu wataona maneno Yangu yakifanikishwa mbele ya macho yao, waone kwamba hakuna neno lolote Langu ni bure; yote ni ya utendaji. Kabla ya maneno Yangu kutimizwa watu wengi wataondoka kwa sababu hayajatimizwa. Hivi ndivyo Ninavyofanya kazi—si kazi ya fimbo Yangu ya chuma pekee, lakini hata zaidi ni hekima ya maneno Yangu. Kutoka kwa haya, mtu anaweza kuona kudura Yangu na kuona chuki Yangu kwa joka kubwa jekundu. (Hili linaweza kuonekana tu baada ya Mimi kuanza kazi Yangu. Sasa watu wengine wanafichuliwa—ni sehemu ndogo tu ya kuadibu Kwangu, lakini haiwezi kujumuishwa katika maafa makuu. Hili si gumu kuelewa. Hivyo inaweza kuonekana kwamba kuanzia sasa kuendelea njia Yangu ya kufanya kazi itakuwa ngumu hata zaidi kwa watu kuelewa. Leo Nawaambia ili msiwe wadhaifu kwa sababu ya hili wakati utakapofika. Hili ndilo Ninalowaaminia kwa sababu mambo yatafanyika ambayo watu hawajayaona tangu nyakati za zamani, na hilo litafanya kuwa kugumu kwa watu kuweka kando hisia zao na kujidai kwao.) Sababu ya Mimi kutumia mbinu tofauti kuliadhibu joka kubwa ni kwa sababu ni adui Yangu na ni mshindani Wangu. Ni lazima Niangamize uzao wake yote—ni hapo tu ndipo Ninaweza kuondoa chuki kutoka kwa moyo Wangu, na ni hapo tu ndipo Naweza kuliaibisha joka kubwa jekundu vizuri. Huku tu ndiko kuangamiza joka kubwa jekundu kabisa na kulitupa katika ziwa la moto na kibiriti na shimo lisilo na mwisho.

Sio tu jana, lakini leo pia, na muhimu zaidi, kesho, Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza kutawala na Mimi na kuungana na Mimi katika kuongoza mataifa yote na katika kufurahia baraka. Nimekamilisha kazi Yangu kwa ufanisi—Nimekuwa nikisema hivyo muda huu wote, na pia inaweza kusemwa kwamba Nilianza kusema hivyo tangu mwanzo wa uumbaji, lakini binadamu hawaelewi kile Ninachokisema. Tangu uumbaji hadi sasa Sijafanya kazi Mimi binafsi; kwa maneno mengine, Roho Wangu hajawahi kumshukia mwanadamu kikamilifu kusema na kufanya kazi. Lakini leo ni tofauti kuliko zamani: Roho Wangu anafanya kazi Yeye binafsi kila mahali katika ulimwengu dunia. Kwa sababu katika siku za mwisho Ninataka kupata kundi la watu watakaotawala mamlakani na Mimi. Kwanza Ninampata mtu ambaye analingana na Mimi, ili aweze kufikiria mzigo Wangu, na baadaye Roho Wangu atamshukia Yeye kabisa kuonyesha sauti Yangu na kuachilia amri Zangu za utawala na kufichua siri Zangu kwa ulimwengu dunia. Roho Wangu atamkamilisha binafsi; Roho Wangu atamfundisha nidhamu binafsi. Kwa sababu Anaishi katika ubinadamu wa kawaida, hakuna mtu anayeweza kuona kwa wazi. Wakati ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanaingia katika mwili utakuwa wazi kabisa iwapo kile Ninachokifanya sasa ni uhalisi. Bila shaka, machoni pa binadamu, katika dhana ya binadamu, hakuna mtu anayeamini na hakuna mtu anayeweza kuwa mtiifu. Lakini huu ndio uvumilivu Wangu kwa watu. Kwa sababu uhalisi haujakuja bado, kwa hivyo watu hawawezi kuamini na hawawezi kuelewa. Hakujawahi kuwa na yeyote ambaye angeamini maneno Yangu katika dhana zake za binadamu. Watu wote wako namna hii: Wanaamini tu kile ambacho nafsi Yangu ya mwili inasema, au waamini tu sauti ya Roho Wangu. Hili ndilo jambo gumu zaidi kulishughulikia katika watu. Kama hawajaona kitu kikifanyika na macho yao wenyewe, hakuna mtu anaweza kuachilia dhana zake mwenyewe, na hakuna mtu anayeweza kuamini kile Ninachokisema, kwa hivyo Natumia amri Zangu za utawala kuwaadhibu wale wana wa kutotii.

Nimesema mambo kama haya awali: Mimi ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na pia Mimi nasimamia kila kitu kutoka mwanzo hadi mwisho. Katika siku za mwisho, Nitawapata wana washindi wa kiume 144,000. Mnaelewa kiasi kuhusu haya maneno “wana washindi wa kiume”, lakini hamko wazi kuhusu 144,000. Katika dhana za binadamu nambari lazima irejelee idadi ya watu au idadi ya vitu. Kuhusiana na “144,000” kuwabadilisha “wana washindi wa kiume”—“wana 144,000 washindi wa kiume”—watu wanafikiri kwamba kuna wana washindi wa kiume 144,000. Na aidha watu wengine wanafikiri ni maelezo ya kabla na wanaeleza hiyo 140,000 na 4,000 kando. Lakini haya maelezo mawili si sahihi. Hairejelei nambari halisi, na hata zaidi, hairejelei maelezo ya kabla. Kwa binadamu, hakuna mtu ambaye anaweza kupenya hili—watu wote wa vizazi vilivyopita walifikiri inaweza kuwa maelezo ya kabla. Mia moja na arubaini na nne elfu inashirikishwa na wana washindi wa kiume. Kwa hivyo, 144,000 inarejelea kundi la watu katika siku za mwisho ambao watatawala, na ambao Ninawapenda. Yaani, 144,000 inatafsiriwa kuwa kundi la watu waliotoka Sayuni na ambao watarudi Sayuni. Maelezo kamili ya wana washindi wa kiume 144,000 ni kama yafuatayo: Wao ndio watu waliotoka Sayuni kuja kwa dunia na walipotoshwa na Shetani, na ambao hatimaye watapatwa na Mimi na watarudi Sayuni na Mimi. Kutoka kwa maneno Yangu mtu anaweza kuona hatua za kazi Yangu, kumaanisha kwamba si kitu cha mbali sana kwamba ninyi mtaingia katika mwili. Kwa hivyo Nimeeleza kwa kurudia na kuwakumbusha kuhusu hili. Mtaona kwa wazi, na kutoka kwa maneno Yangu mtatambua njia ya kutenda; kutoka kwa maneno Yangu mtatambua hatua ya kazi Yangu. Ili kutambua hatua ya kazi ya Roho Mtakatifu, ni lazima muimaizi kutoka kwa siri Ninazofichua (kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuona na hakuna mtu anayeweza kupenya kazi ya Roho Mtakatifu). Hiyo ndiyo maana Nafichua siri katika siku za mwisho.

Nyumbani Kwangu hakutakuwa na kitu kisichopatana na Mimi, na kutoka sasa kuendelea Nitaanza kusafisha na kutakasa, kidogo kidogo. Miongoni mwa watu, hakuna mtu anayeweza kuingilia kati, na hakuna mtu anayeweza kufanya kazi hii. Hii inafichua kwa nini Nafanya kazi mwenyewe katika siku za mwisho. Na hii ndiyo maana Nimewaambia mara nyingi kwamba mnahitaji tu kufurahia wenyewe na hamhitaji kufanya juhudi yoyote. Ni kupitia hili ambapo nguvu Yangu inafichuliwa, haki Yangu na uadhama vinafichuliwa, na siri Zangu zote ambazo watu hawawezi kuzifungua zinafichuliwa. (Kwa sababu watu hawajawahi kuwa na maarifa yoyote ya mpango Wangu wa usimamizi au ufahamu wowote wa hatua za kazi Yangu, zinaitwa “siri”.) Kile Nitakachopata na kile Nitakachofanya katika siku za mwisho ni siri. Kabla ya wakati Nilipoiumba dunia, Sikuwahi kufanya kile Ninachokifanya leo na Sikuwahi kuwaonyesha watu uso Wangu wa utukufu au sehemu yoyote ya nafsi Yangu; Roho Wangu tu ndiye amefanya kazi kwa watu wengine. (Kwa sababu, tangu wakati wa uumbaji, hakuna mtu ameweza kunidhihirisha na hakuna mtu ameweza kunionyesha, Sijawahi kuwaruhusu watu kuona nafsi Yangu, na Roho Wangu amefanya kazi kwawatu wengine.) Ni leo tu ndiyo Nimefichua sura Yangu ya utukufu na nafsi Yangu kwa watu, na ni sasa tu ambapo wameyaona. Lakini kile mnachoona leo bado hakijakamilika, na bado si kile Ninachowataka muone. Kile Ninachowataka muone kiko katika mwili tu, na sasa hivi bado hakuna mtu anayefikia sharti hili. Katika maneno mengine, hakuna mtu anayeweza kuona nafsi Yangu kabla ya yeye kuingia katika mwili. Kwa hivyo Nasema kwamba Nitafichua nafsi Yangu kwa ulimwengu dunia Mlimani Sayuni. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba kuingia katika Mlima Sayuni ndiyo sehemu ya mwisho ya mradi Wangu. Wakati wa kuingia katika Mlima Sayuni, ufalme Wangu utakuwa umejengwa kwa ufanisi. Kwa maneno mengine, nafsi Yangu ndiyo ufalme. Wakati ambapo wazaliwa wa kwanza wanaingia katika mwili ni hasa wakati ambapo ufalme utafanyika, kwa hivyo Nimesema kwa kurudia kuhusu suala la wazaliwa wa kwanza kuingia katika Mlima Sayuni. Hii ndiyo sehemu kuu ya mpango Wangu wote wa usimamizi, ambao hakuna mtu amewahi kuelewa awali.

Punde Ninapobadili njia Yangu ya kufanya kazi kutakuwa na hata vitu zaidi ambavyo vinazidi fikira za binadamu, kwa hivyo kuwa makini kuhusu jambo hili. Kuna vitu ambavyo vinazidi fikira za binadamu, lakini hili halimaanishi kwamba kile Ninachokisema si sahihi. Ni kwamba tu ni muhimu hata zaidi kwa watu kuteseka, na ni muhimu hata zaidi kushirikiana na Mimi. Usiwe asiyezuiwa kwa utukutu au kufuata tu dhana zako mwenyewe. Kwa kuwa wengi wa wale wanaonitolea huduma wanaaguka katika jambo hili. Natumia maneno Yangu kufichua asili ya binadamu na kufichua dhana za binadamu. (Lakini wale wanaonitolea huduma, kwa sababu Sijabadili dhana zao, wanaanguka tu, ilhali Nimebadili dhana za wale walio wazaliwa Wangu wa kwanza na Nimeondoa fikira zao kupitia hili.) Kwa hivyo mwishowe, wazaliwa Wangu wa kwanza wote watakamilishwa kwa sababu ya siri ambazo Nimefichua.

Iliyotangulia: Sura ya 110

Inayofuata: Sura ya 112

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp