Sura ya 101

Sitakuwa mwenye huruma kwa yeyote anayeingilia usimamizi Wangu ama anayejaribu kuiharibu mipango Yangu. Kila mtu anapaswa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Ninayosema na lazima aelewe vizuri kile Ninachozungumzia. Kwa kuzingatia hali iliyopo, kila mtu anapaswa kujichunguza: Ni wajibu gani unaotekeleza? Unaishi kwa ajili Yangu, au unamtumikia Shetani? Je, kila moja ya matendo yako hutoka Kwangu, au hutoka kwa Shetani? Haya yote yapaswa kuwa dhahiri ili kuepuka kukosea amri Zangu za utawala na hivyo kupata ghadhabu Yangu. Tukiangalia nyuma, daima watu hawajakuwa waaminifu na wamenikaidi, wamenikosea heshima, na zaidi ya hayo, wamenisaliti. Kwa sababu hizi watu hawa wanapitia hukumu Yangu leo. Japo Ninaonekana kama mwanadamu tu, wale wote ambao Sijawakubali (unapaswa kuelewa maana Yangu kutokana na hili: Sikuhusu jinsi unavyoonekana kuwa mrembo ama jinsi unavyopendeza, bali kama Nimekujaalia na kukuchagua) watakuwa walengwa wa kuangamizwa na Mimi. Huu ni ukweli kabisa. Kwa kuwa Ninaweza kuonekana kama mwanadamu, lakini unahitaji kutozingatia ubinadamu Wangu ili uufahamu uungu Wangu. Nimesema mara nyingi, “Ubinadamu wa kawaida na uungu kamili ni sehemu mbili zisizotengana za Mungu Mwenyewe mkamilifu.” Hata hivyo, bado hamnielewi, na bado mnamzingatia tu Mungu wenu asiye dhahiri. Ninyi ni watu msioelewa mambo ya kiroho. Lakini watu wa aina hiyo bado wanataka kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza. Ni fedheha iliyoje! Hawaoni hadhi yao wenyewe ilivyo kwa kweli! Hata hawastahili kuwa watu Wangu, wangewezaje kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza ambao wangekuwa wafalme pamoja na Mimi? Watu wa aina hii hawajijui, ni wa kabila la Shetani; hawastahili kuwa nguzo katika kaya Yangu, na hawafai kunitumikia hata kidogo. Kwa hivyo Nitawaondoa mmoja baada ya mwingine, na Nitafichua tabia zao za kweli.

Kazi Yangu inaendelea hatua kwa nyingine bila kuzuiliwa na bila pingamizi lolote kwa sababu Nimepata ushindi na kwa sababu Nimetawala kama Mfalme ulimwenguni kote. (Kile Ninachozungumzia ni kuwa baada ya kumshinda ibilisi Shetani Nimetwaa upya uongozi Wangu.) Ninapowapata wazaliwa Wangu wa kwanza wote, basi bendera ya ushindi itapepea juu ya Mlima Sayuni. Hiyo ni kusema, wazaliwa Wangu wa kwanza ni bendera Yangu ya ushindi, utukufu Wangu, sababu Yangu ya kujisifia; wao ni ishara kuwa Nimemuaibisha Shetani nao ni mbinu ambayo kwayo Ninafanya kazi. (Kupitia kwa kundi la watu waliopotoshwa na Shetani baada Yangu kuwajaalia, lakini waliorudi upande Wangu upya, Ninaliaibisha joka kuu jekundu na kuwatawala wana wote wa uasi.) Wazaliwa Wangu wa kwanza wako mahali uenyezi Wangu uko, wao ni ufanisi Wangu mkuu, wasiobadilika na wasiopingika. Ni kupitia kwa wazaliwa Wangu wa kwanza ndipo Nitakapoukamilisha mpango Wangu wa usimamizi, Nilimaanisha hivi kitambo Niliposema: “Ni kupitia kwenu ndipo Nitayasababisha mataifa yote na watu wote kurudi mbele ya kiti Changu cha enzi.” Zaidi ya hayo, ndivyo Nilivyomaanisha kwa kusema “mzigo mzito mabegani mwenu.” Hilo ni dhahiri? Mnaelewa? Wazaliwa wa kwanza ni dhihirisho la mpango Wangu wote wa usimamizi. Kwa hiyo, Sijawahi kulitendea kundi hili kwa upole, na kila mara Nimewafundisha nidhamu kwa ukali(adhabu hiyo kali ikiwa ni mateso yanayopitiwa duniani, misiba ya familia, kuachwa na wazazi, waume, wake, na watoto. Kwa jumla, kuachwa na ulimwengu na kutelekezwa na enzi), na hii ndiyo maana una bahati nzuri ya kuja mbele Zangu leo. Hili ndilo jawabu la swali ambalo mmeuliza mara kwa mara kuhusu “Kwa nini watu wengine hawakulikubali jina hili, lakini Mimi Nililikubali?” Sasa Mnajua!

Leo hakuna chochote kilicho sawa na hapo zamani. Mpango Wangu wa usimamizi umechukua mbinu mpya, kazi Yangu ni tofauti hata zaidi na ilivyokuwa hapo zamani na matamshi Yangu sasa ni ya kipekee hata zaidi. Kwa hiyo, Nimesisitiza mara kwa mara kwamba sharti mnitumikie kwa usahihi (hili linasemwa kwa watendaji huduma). Msijitendee kwa njia isiyofaa, lakini endeleeni kufuatilia kwa bidii. Je, haipendezi kupata neema kiasi? Ni bora zaidi kuliko kuteseka duniani. Nakuambia! Usiponihudumia kwa moyo wote, na badala yake ulalamike kwamba nimekuwa mdhalimu, basi kesho utaelekea kuzimu na jahanamu. Hakuna mtu anayetaka kufa mapema, sivyo? Hata ikiwa ni siku moja zaidi tu, ni siku yenye thamani, sasa utajitolea kabisa kwa mpango Wangu wa usimamizi na baadaye usubiri hukumu Yangu kwako na usubiri kuadibu Kwangu kwa haki kukufike. Usidhani Niyanenayo ni upuuzi; Ninanena kutoka kwa haki Yangu na kutoka kwa tabia Yangu, na zaidi ya hayo Ninatenda kwa uadhama na haki Yangu. Watu wanasema kuwa Mimi ni mdhalimu. Hii ni kwa sababu hawanifahamu. Ni dhihirisho wazi la tabia yao ya uasi. Kwangu hakuna hisia, badala yake kuna haki, uadhama, na ghadhabu tu. Kadri muda unavyoendelea kusonga ndivyo mtakavyoiona tabia Yangu. Wakati huu ni kipindi cha mpito, nanyi mnaweza kuona sehemu ndogo tu ya jambo hili, kuona baadhi ya mambo ya nje. Wazaliwa Wangu wa kwanza watakapojitokeza, basi Nitawaruhusu kuona kila kitu na kuelewa kila kitu. Kila mmoja atashawishika moyoni mwake na katika maneno yake. Nitawafanya mseme kwa sauti ili mnishuhudie, mnisifu milele, na mnitukuze milele. Hili haliepukiki na haliwezi kubadilishwa na yeyote. Watu hawawezi kuwazia jambo hili, sembuse kuliamini.

Wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza wanaendelea kuwa dhahiri kuhusu maono hayo, upendo wao Kwangu unazidi kuwa mwingi. (Huu si upendo wa mahaba, ambao ni Shetani kunishawishi, jambo linalohitaji kutambuliwa. Kwa hiyo zamani Nilinena kuwa kulikuwa na watu waliojigamba mbele Yangu. Watu wa aina hii ni vikaragosi wa Shetani, wakiamini kuwa Ningevutiwa na sura zao. Hawana haya! Mafidhuli duni!) Hata hivyo, watu wasiokuwa wazaliwa wa kwanza, kupitia katika maneno haya ambayo Nimezungumza katika kipindi hiki, wamezidi kutokuwa dhahiri kuhusu maono hayo na wamepoteza imani kwa mtu Niliye. Baadaye hatua kwa hatua wanakuwa wasiojali hadi hatimaye wanaanguka. Hawa watu hawawezi kujisaidia. Hili ndilo lengo la mambo Ninayoyasema wakati huu, kila mtu anapaswa kuona haya (Nikizungumza na wazaliwa Wangu wa kwanza), na kupitia kwa matamshi na matendo Yangu, watazame maajabu Yangu. Mbona inasemwa kuwa Mimi ni Mfalme wa Amani, Baba wa Milele, kuwa Mimi ni wa Ajabu, kuwa Mimi ni Mshauri? Haitoshi kabisa kufafanua jambo hili kutoka kwa utambulisho Wangu, matamshi Yangu, ama kutoka kwa yale Ninayofanya: Hata haistahili kutajwa. Sababu ya kuniita Mfalme wa Amani ni uwezo Wangu wa kuwakamilisha wazaliwa wa kwanza, hukumu Yangu kwa Shetani, na baraka zisizo na kifani ambazo Nimewatunuku wazaliwa wa kwanza. Hiyo ni kusema, ni wazaliwa wa kwanza pekee ndio wanaostahili kuniita Mfalme wa Amani, kwa kuwa Ninawapenda wazaliwa Wangu wa kwanza, na wasifu “Mfalme wa Amani” unafaa kutoka kwa vinywa vyao. Kwao, Mimi ni Mfalme wa Amani. Kwa wanangu na watu Wangu, Ninaitwa Baba wa Milele. Kwa sababu ya uwepo wa wazaliwa Wangu wa kwanza, kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza wanaweza kushikilia nguvu ya ufalme pamoja nami na kuyatawala mataifa yote na watu wote (wana na watu), kwa hiyo, wana na watu wanapaswa kuniita Baba wa Milele, kumaanisha Mungu Mwenyewe, aliye juu ya wazaliwa wa kwanza. Mimi ni wa Ajabu kwa wale wasiokuwa wana, watu na wazaliwa wa kwanza. Kwa sababu ya ajabu ya kazi Yangu, wasioamini hawawezi kuniona kamwe (kwa maana Nimeyafunika macho yao), na hawawezi kuona kazi Yangu vyema kabisa, kwa hivyo kwao Mimi ni wa Ajabu. Kwa mapepo wote na kwa Shetani Mimi ni Mshauri kwa sababu yote Niyafanyayo yanawatia aibu, na yote Nifanyayo ni kwa ajili ya wazaliwa Wangu wa kwanza. Kila hatua Yangu huenda taratibu na Ninapata ushindi kwa kila hatua. Zaidi ya hayo, Ninaweza kuitambua mipango yote ya Shetani na kutumia mipango yake kunitumikia, Nikimfanya kuwa chombo cha kutumikia makusudi Yangu kutoka kwa upande hasi. Hii ndiyo maana ya Mimi kuwa Mshauri, ambayo hakuna anaweza kubadilisha na hakuna anayeweza kuelewa kabisa. Lakini kuhusu nafsi Yangu, Mimi ni Mfalme wa Amani, pamoja na Baba wa Milele, na vile vile Mshauri na wa Ajabu. Hakuna kitu katika mambo haya ambayo si kweli. Ni ukweli usiopingwa na usiobadilika!

Nina mengi sana ya kusema, hayafananishwi kabisa. Kwa hiyo, Nawahitaji muwe na subira na kungoja. Chochote mfanyacho, msifanye kutokana na msukumo fulani wa kuondoka. Kwa sababu mlichokielewa siku za nyuma kimepitwa na wakati leo, hakitumiki tena, na mambo ya sasa ni wakati wa mabadiliko—kama mpito kati ya nasaba za wafalme, kwa hiyo Nawahitaji mbadili mawazo yenu na mtupe fikira zenu za kale. Hii ndiyo maana ya kweli ya “kuvalia joho takatifu la haki”. Ni Mimi pekee Ninayeweza kufafanua maneno Yangu mwenyewe, na ni Mimi pekee Ninayejua Ninayojiandaa kufanya. Kwa hiyo, ni maneno Yangu pekee yasiyo na najisi, ni yale Ninayokusudia kabisa, na kwa hiyo ni kuvalia joho takatifu la haki. Ufahamu wa akili ya binadamu ni mawazo tu; ufahamu wao ni wenye najisi na hauwezi kutimiza makusudi Yangu. Kwa hiyo Mimi mwenyewe Ninanena, na Mimi mwenyewe Ninaeleza, na hii ndiyo maana iliyokusudiwa ya “Ninaifanya kazi mwenyewe.” Ni sehemu muhimu ya mpango Wangu wa usimamizi, na ni sharti watu wote wanitukuze na kunisifu. Kuhusu kuelewa maneno Yangu, Sijawahi kuwapa watu uwezo huo na hawana ustadi wa hayo kamwe. Hii ni mojawapo ya mbinu Zangu za kumdhalilisha ibilisi. (Iwapo watu wangeelewa matamshi Yangu na wangeweza kuchunguza makusudi Yangu katika kila hatua, basi Shetani angewamiliki watu wakati wowote, na hivyo watu wangenigeuka na kufanya iwe vigumu Kwangu kutimiza lengo Langu la kuwateua wazaliwa wa kwanza. Kama Ningeelewa kila siri, na mtu Niliye angeweza kunena matamko ambayo hakuna yeyote angeweza kuelewa, Mimi, pia ningeweza kumilikiwa na Shetani. Hii ndiyo sababu Nikiwa katika mwili Mimi si wa mwujiza kabisa.) Lazima kila mtu afahamu vizuri umuhimu wa maneno haya na kufanya mambo akifuata uongozi Wangu. Msijaribu ninyi wenyewe kufahamu maneno na mafundisho ya dini ya kina.

Iliyotangulia: Sura ya 100

Inayofuata: Sura ya 102

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp