Sura ya 100

Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote. Hakuna mtu anayeweza kuyayumbisha au kuyabadilisha. Mimi mwenyewe na wana Wangu wapendwa tutaishi pamoja ndani yake na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuyakanyaga, hakuna chochote kitakachoruhusiwa kuishi humo na hata zaidi hakuna kitu chochote kibaya kitakachoruhusiwa kutokea kamwe. Yote itakuwa sifa na kushangilia tu, yote yatakuwa mandhari ambayo mwanadamu hawezi kudhania. Natamani tu kwamba mtatoa nguvu zenu zote Kwangu kwa mioyo yenu yote na akili zenu zote na kadri ya uwezo wenu. Kama leo au kesho, kama wewe ni mtu ambaye anatoa huduma kwa ajili Yangu au mtu anayepata baraka, nyote mnapaswa kutumia sehemu ya nguvu zote kwa ajili ya ufalme Wangu. Huu ni wajibu ambao watu wote walioumbwa wanapaswa kutekeleza, nao unapaswa kufanywa na kutekelezwa kwa njia hii. Nitavihamasisha vitu vyote vitoe huduma kwa uzuri wa ufalme Wangu ili ufanywe mpya daima, na nyumba Yangu ifanywe kuwa yenye mpangilio mzuri na yenye umoja. Hakuna mtu anayeruhusiwa kunipinga Mimi, na anapaswa kupitia hukumu na kulaaniwa. Sasa laana Zangu zinaanza kuyashambulia mataifa yote na watu wote na laana Zangu ni kali hata zaidi kuliko hukumu. Sasa ni wakati wa kuanza kuwahukumu watu wote, kwa hivyo inasemwa kuwa ni laana. Hii ni kwa sababu sasa ni enzi ya mwisho na si wakati wa uumbaji. Kwa kuwa enzi zimebadilika, kasi ya kazi Yangu sasa ni tofauti sana. Kutokana na mahitaji ya kazi Yangu, watu Ninaowahitaji pia ni tofauti; wale ambao wanapaswa kutelekezwa watatelekezwa; wale ambao wanapaswa kutengwa watatengwa; wale ambao wanapaswa kuuawa watauawa na wale ambao wanapaswa kuachwa lazima waachwe. Huu ni mwenendo usioepukika ambao hautegemei dhamira ya mwanadamu na hakuna mtu anayeweza kuubadilisha. Lazima ufanyike kulingana na mapenzi Yangu! Nawaacha wale ambao Nitawaacha na kuwaondoa wale ambao Nitawaondoa; hakuna atakayetenda kiholela. Nawaacha wale ambao Nataka kuwaacha na Ninawapenda wale ambao Nataka kuwapenda; lazima jambo hili lifanyike kulingana na mapenzi Yangu! Sitendi kwa kusukumwa na hisia; Pamoja nami kuna haki, hukumu na hasira tu—hakuna hisia hata kidogo. Hakuna dalili hata kidogo ya ubinadamu ndani Yangu, kwa maana mimi ni Mungu Mwenyewe, nafsi ya Mungu. Kwa sababu watu wote wanaona kipengele Changu ambacho ni ubinadamu Wangu na hawajaona kipengele ambacho ni uungu Wangu. Wao kweli hawatambui nao wamevurugika sana!

Lazima mzingatie Ninachowaambia mioyoni mwenu, lazima muuelewe moyo Wangu kupitia kwa maneno Yangu na muufikirie kwa makini mzigo wangu, na hivyo mtakuja kuujua uweza Wangu na kuiona nafsi Yangu. Kwa kuwa maneno Yangu ni maneno ya hekima na hakuna mtu anayeweza kufahamu kanuni au sheria za maneno Yangu. Watu wanadhani kwamba natenda ulaghai na udanganyifu nao hawanijui kupitia kwa maneno Yangu, lakini badala yake wananikufuru. Wao ni wazembe na wajinga sana! Na hawana ufahamu wowote. Kila sentensi Ninayotamka huwa na mamlaka na hukumu na hakuna mtu anayeweza kuzibadilisha. Mara tu maneno Yangu yanapotoka, mambo yatafanyika kwa mujibu wa maneno Yangu, na hii ndiyo tabia Yangu. Maneno Yangu ni mamlaka na yeyote anayeyarekebisha hukosea kuadibu Kwangu na ni lazima Nimwangamize. Hali ikiwa mbaya hayo husababisha uharibifu katika maisha yao wenyewe nao huenda kuzimu, au huenda jahanamu. Hii ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo Ninawashughulikia wanadamu na mwanadamu hawezi kuibadilisha—hii ni amri Yangu ya utawala. Kumbuka hili! Hakuna mtu anayeruhusiwa kuikosea amri Yangu; lazima hili lifanyike kulingana na mapenzi Yangu! Zamani Nilikuwa mpole sana kwenu nanyi mlikabiliwa na maneno Yangu tu. Maneno Niliyonena kuhusu kuwaangamiza watu hayajatokea bado. Lakini kuanzia leo, majanga yote (haya yanayohusiana na amri Zangu za utawala) yatatokea moja baada ya lingine ili yawaadhibu wale wote wasiotii mapenzi Yangu. Lazima kuwe na ujio wa ukweli, vinginevyo watu hawataweza kuona ghadhabu Yangu lakini watapotoshwa tena na tena. Hii ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi nayo ni njia ambayo kwayo Mimi kushughulikia hatua inayofuata ya kazi Yangu. Nawaambieni hivi mapema ili muweze kuepuka kufanya makosa na kupitia mateso milele. Hiyo ni kusema, kuanzia leo Nitawafanya watu wote ila wazaliwa Wangu wa kwanza kuchukua nafasi zao halisi kwa mujibu wa mapenzi Yangu, nami Nitawaadibu mmoja baada ya mwingine. Sitamsamehe hata mmoja wao. Hebu thubutu tu kuwa wapotovu tena! Hebu thubutu tu kuwa mwasi tena! Nimesema mbeleni kuwa Mimi ni mwenye haki kwa wote bila hisia yoyote, na huu ni mfano kwamba tabia Yangu haipaswi kukosewa. Hii ni nafsi Yangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha jambo hili. Watu wote husikia maneno Yangu na watu wote huuona uso Wangu mtukufu. Watu wote wanapaswa kunitii kabisa na kwa ukamilifu—hii ni amri Yangu ya utawala. Watu wote katika ulimwengu mzima na katika miisho ya dunia wanapaswa kunisifu na kunitukuza, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, kwa maana Mimi ni nafsi ya Mungu. Hakuna mtu anayeweza kubadili maneno na matamshi Yangu, usemi na mwenendo Wangu, kwa kuwa haya ni mambo Yangu peke Yangu, na kile ambacho Nimemiliki tangu milele na kile ambacho kitakuwepo milele.

Watu wana nia ya kunijaribu, nao wanataka kutafuta kitu ambacho wanaweza kutumia dhidi Yangu ndani ya maneno Yangu, ili wanikashifu. Je, Ninapaswa kukashifiwa nawe? Je! Ninapaswa kuhukumiwa kiholela? Je, shughuli Zangu zapaswa kujadiliwa kiholela? Kweli ninyi ni kikundi cha watu wasiojua kinachowafaa! Hamnijui kabisa! Mlima Sayuni ni nini? Makao Yangu ni nini? Nchi nzuri ya Kanaani ni nini? Msingi wa uumbaji ni nini? Kwa nini Nimekuwa Nikiendelea kutaja maneno haya kwa siku chache zilizopita? Mlima Sayuni, makao Yangu, nchi nzuri ya Kanaani, msingi wa uumbaji, vyote vinasemwa kuhusu nafsi Yangu (kuhusu mwili). Watu wote wanadhani kuwa hayo ni maeneo ambayo yapo kihalisi. Nafsi Yangu ni Mlima Sayuni nayo ni makao Yangu. Yeyote anayeingia katika ulimwengu wa kiroho ataupanda Mlima Sayuni, naye ataingia katika makao Yangu. Niliumba vitu vyote ndani ya nafsi Yangu, yaani, vitu vyote viliumbwa ndani ya mwili, kwa hiyo ni msingi. Kwa nini Nasema kwamba mtarudi katika mwili pamoja na Mimi? Humo mna maana ya asili. Kama vile tu jina “Mungu,” majina haya hayana maana kwayo yenyewe, bali ni majina tofauti Ninayozipa sehemu tofauti. Kwa hiyo usizingatie sana maana yao halisi, lakini sisitiza tu katika kusikia maneno Yangu. Lazima uyaelewe kwa njia hii na kisha utaweza kufahamu mapenzi Yangu. Kwa nini Nawakumbusha tena na tena kwamba kuna hekima katika maneno Yangu? Ni wangapi kati yenu wamejaribu kufahamu maana ya jambo hili? Ninyi nyote mnayachunguza bila kufikiri na mnakosa mantiki!

Bado sasa hamwelewi mambo mengi ambayo Nimesema katika siku zilizopita. Mnabaki katika hali ya shaka na hamuwezi kuukidhi moyo Wangu. Wakati wowote mnaweza kuwa na uhakika kuhusu kila sentensi Ninayonena, huo utakuwa wakati ambao maisha yenu yanakua. Kwangu, siku moja ni kama miaka elfu na miaka elfu kama siku moja; Je! Mnaonaje kuhusu wakati Ninaozungumzia? Je, mnauelezeaje? Mnauelewa vibaya! Na zaidi ya hayo watu wengi bado wanashindana kuhusu jambo hili nami, wakitamani kupata kitu cha kutumia dhidi Yangu—hamjui ni nini kinachowafaa! Kuwa mwangalifu, kwani vinginevyo Nitakuangamiza! Siku itakapowadia ambapo kila kitu kinafafanuliwa mtaelewa kabisa. Bado Siwaambii sasa (sasa ni wakati wa kuwafunua watu na sharti kila mtu awe mwangalifu na mwenye busara ili aweze kuyakidhi mapenzi Yangu). Nitawafichua watu wote kupitia maneno Yangu na maumbo yao ya asili yatafichuliwa ili kuonyesha kama ni kweli au la. Ikiwa mtu ni kahaba au malaya, lazima Nimfichue. Nimesema awali kwamba Ninafanya mambo bila kujitahidi kufanya lolote na kwamba Ninatumia maneno Yangu pekee kuwafichua watu. Mimi siogopi hila yoyote; baada ya kunena maneno Yangu, bila shaka lazima ufichue umbo lako la asili, na haijalishi jinsi unavyojificha kwa hakika Nitatambua hilo. Hii ni kanuni ya matendo Yangu—kutumia matamshi tu na sio kutumia nguvu yoyote ile. Watu huwa na woga na wasiwasi kuhusu kama maneno Yangu yatatimizwa au la, wanakuwa na wasiwasi kwa ajili Yangu na wanahangaika kwa ajili Yangu, lakini jitihada hizi hazihitajiki kwa kweli nao ni matokeo ambayo hayafai. Una wasiwasi juu Yangu lakini je, maisha yako mwenyewe yamekomaa? Je kuhusu kudura yako mwenyewe? Jiulize mara nyingi na usiwe hobelahobela. Watu wote wanapaswa kuizingatia kazi Yangu na—kupitia matendo Yangu na maneno Yangu—waione nafsi Yangu, wawe na ujuzi zaidi kunihusu Mimi, wajue uweza Wangu, wajue hekima Yangu na wajue njia na mbinu ambazo kwazo Niliumba vitu vyote, na hivyo kunipa sifa ya kudumu. Nitawafanya watu wote waone mikono ya amri Zangu za utawala ziko juu ya nani, nani ambaye Ninafanyia, ni nini Ninachotaka kufanya na ni nini Ninachotaka kukamilisha. Hili ni jambo ambalo kila mtu anapaswa kutimiza, kwa maana hii ni amri Yangu ya utawala. Nitatimiza kile Ninachosema. Hakuna mtu anayepaswa kuyachambua maneno Yangu kwa kawaida, wote wanapaswa kuona kanuni za matendo Yangu kupitia kwa maneno Yangu, na kutoka kwa maneno Yangu wajue hasira Yangu ni nini, laana Yangu ni nini na hukumu Yangu ni nini. Mambo haya yote yanategemea maneno Yangu na ni mambo ambayo yanapaswa kuonekana na kila mtu ndani ya kila moja ya maneno Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 99

Inayofuata: Sura ya 101

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp