Sura ya 114

Niliumba ulimwengu dunia; Nilitengeneza milima, mito, na vitu vyote; Niliunda ulimwengu na miisho ya dunia; Niliwaongoza wana Wangu na watu Wangu; Niliamuru vitu na mambo yote. Sasa, Nitawaongoza wazaliwa Wangu wa kwanza warudi kwenye Mlima Wangu Sayuni, kurudi mahali ambapo Naishi, ambayo itakuwa hatua ya mwisho katika kazi Yangu. Yote ambayo Nimeyatenda (kila kitu kilichofanyika kutoka uumbaji mpaka sasa) yalikuwa kwa sababu ya hatua ya leo ya kazi Yangu, na zaidi ni kwa sababu ya utawala wa kesho, ufalme wa kesho, na kwa ajili ya Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza kuwa na furaha ya milele. Hili limekuwa lengo Langu katika kuumba vitu vyote na yatakuwa mafanikio Yangu ya mwisho wa uumbaji. Kuna kusudi na mpango kwa kile Ninachosema na kufanya; hakuna kinachofanyika ovyo ovyo. Ingawa Ninasema kuwa na Mimi yote ni uhuru na haki ya kujiamulia la kufanya, hata hivyo kila kitu Ninachofanya ni chenye maadili, yote Ninayofanya yamewekwa kwa msingi wa hekima na tabia Yangu. Je, mmeona chochote kuhusu hili? Kuanzia uumbaji mpaka leo, kando na wazaliwa Wangu wa kwanza, hawapo ambao wamenijua Mimi na hawapo ambao wameuona uso Wangu wa kweli. Jambo la pekee Nililofanya kwa wazaliwa Wangu wa kwanza ni kwa sababu kimsingi wao ni sehemu ya nafsi Yangu.

Nilipouumba ulimwengu, Nilimtengeneza mwanadamu katika makundi manne ya safu kwa mujibu wa mahitaji Yangu, ambayo ni: wana Wangu, watu Wangu, wale wanaotoa huduma, na wale ambao wataangamizwa. Ni kwa nini wazaliwa Wangu wa kwanza hawako kati ya orodha hii? Ni kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza si wa asili ya uumbaji; wanatoka Kwangu na sio wa wanadamu. Nilifanya mipango kwa ajili ya wazaliwa Wangu wa kwanza kabla Sijapata mwili; ni kaya gani ambayo wangezaliwa kwayo na ni akina nani wangekuwa huko kuwahudumia—vitu vyote hivi vilipangwa na Mimi. Nilipanga pia ni wakati upi ambapo ni yupi kati yao angepatwa tena na Mimi na mwishowe tutarudi Sayuni pamoja. Haya yote yalipangwa kabla ya uumbaji, kwa hivyo hakuna mtu anayejua jambo hilo na halijaandikwa katika kitabu chochote kwa sababu hayo ni mambo ya Sayuni. Zaidi ya hayo, Nilipopata mwili, Sikumpa mwanadamu welekevu huu, kwa hiyo hakuna mtu aliyejua mambo hayo. Mtakaporejea Sayuni, mtajua jinsi mlivyofanana zamani, jinsi mnavyofanana sasa, na kile ambacho mmefanya katika maisha haya. Hivi sasa ni kuwa tu Ninawaambieni mambo haya wazi na kidogo kidogo, vinginevyo hamngeelewa hata mfanye bidii namna gani, na mngezuia usimamizi Wangu. Leo, ingawa Nimejitenganisha kutokana na miili ya wengi wa wazaliwa Wangu wa kwanza, kwa suala la mwili, sisi tu wa Roho mmoja, na ingawa sura yetu ya mwili inaweza kuwa tofauti, sisi, tangu mwanzo hadi mwisho, tu Roho mmoja. Hata hivyo, dhuria ya Shetani haitatumia hii kama nafasi ya kunyonya. Haijalishi jinsi unavyojificha, inabakia ya juu juu, na Sitaiafiki. Kwa hiyo mtu anaweza kuona kutoka kwa hili kuwa wale ambao wanasisitiza mambo ya juu juu na kutafuta kuniiga kwa nje wana uhakika asilimia mia moja kuwa ni Shetani. Kwa sababu roho zao ni tofauti na wao si wa wapendwa Wangu, haijalishi wananiiga namna gani hawafanani na Mimi. Zaidi ya hayo, kwa kuwa kimsingi wazaliwa Wangu wa kwanza ni wa Roho moja pamoja nami, hata kama hawaniigi, wanasema na kutenda sawasawa na Mimi, na wote ni waaminifu, safi, na wazi (kwa wale ambao hawana hekima ni kwa sababu tu ya uzoefu wao mdogo ulimwenguni, na hivyo kukosa hekima si dosari ya wazaliwa Wangu wa kwanza; wakati ambapo watarudi katika mwili yote yatakuwa sawa). Kwa hiyo ni kwa sababu iliyoelezwa hapo awali kuwa watu wengi bado hawabadili asili yao ya kale bila kujali namna Ninavyowashughulikia. Lakini kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanakubali makusudi Yangu bila Mimi kulazimika kuwashughulikia na hii ni kwa sababu sisi ni wa Roho mmoja. Wanahisi ndani ya roho zao nia ya kujitumia kabisa kwa ajili Yangu. Kwa hiyo mbali na wazaliwa Wangu wa kwanza, hakuna mtu ambaye anajali kwa kweli na kwa dhati makusudi Yangu; ni baada tu ya Mimi kumshinda Shetani ndiyo wako tayari kunifanyia huduma.

Hekima Yangu na wazaliwa Wangu wa kwanza husimama juu ya yote, hushinda yote, na hakuna kitu au mtu au jambo linalothubutu kuwazuia. Zaidi ya hayo, hakuna mtu, jambo, au kitu ambacho kinaweza kuwashinda, na badala yake yote yanajisalimisha kwa utii mbele ya nafsi Yangu. Huu ni ukweli ambao unatokea mbele ya macho ya mtu na ukweli ambao tayari Nimekwisha kuutimiza. Yeyote anayeng’ang’ania kutotii (wale wasiotii bado wanamtaja Shetani na wale wanaomilikiwa na Shetani bila shaka ni Shetani), kwa hakika Nitawaangamiza kabisa ili kusiwe na shida ya baadaye; watakufa mara moja kutokana na kuadibu Kwangu. Aina hii ya Shetani ni wale ambao hawana nia ya kutoa huduma Kwangu na vitu hivi daima vimenipinga kwa ukaidi tangu uumbaji, na leo vinang’ang’ania kutonitii (watu hawawezi kuona hili kwa sababu ni jambo linalohusu roho tu. Mtu wa aina hii anawakilisha Shetani wa aina hii). Nitawaangamiza kwanza kabla kitu kingine chochote kiwe tayari, Nikiwafanya wapokee adhabu kali milele (“kuangamiza” hapa hakumaanishi kutokuwepo tena, lakini badala yake kunamaanisha kiwango cha ukatili ambacho watapitia, na neno “kuangamiza” hapa ni tofauti na neno “kuangamiza” linalotumika kwa wale ambao wataangamizwa), na watalia na kusaga meno milele na milele, bila kikomo. Mwanadamu hawezi kufikiria mandhari hayo kwa vyovyote. Kwa mawazo ya wanadamu yenye kufa, hawawezi kufahamu mambo ya kiroho, kwa hivyo, mtaelewa mambo mengi zaidi baada ya kurudi Sayuni tu.

Katika nyumba Yangu ya baadaye, hakutakuwa na yeyote isipokuwa wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi na wakati huo tu ndipo lengo Langu litafikiwa na mpango Wangu utazaa matunda, kwa kuwa yote yatarejeshwa kwa hali yake ya awali na yote yataainishwa kulingana na mfano wake. Wazaliwa Wangu wa kwanza watakuwa Wangu, wana Wangu na watu watakuwa miongoni mwa viumbe na watendaji huduma na wale walioangamizwa watakuwa wa Shetani. Baada ya kuuhukumu ulimwengu, Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza tutaanza tena maisha ya kiungu na hawataniacha kamwe na daima watakuwa pamoja na Mimi. Siri zote ambazo zinaweza kueleweka na akili za kibinadamu zitafichuliwa kwenu kidogo kidogo. Katika historia yote, kumekuwa na watu wengi ambao wameuawa kishahidi kwa sababu Yangu, wakijitolea kikamilifu Kwangu, lakini wanadamu ni viumbe hata hivyo na haijalishi ni wazuri namna gani, hawawezi kuainishwa kama Mungu; huu ni mwenendo usioepukika na hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Hata hivyo, ni Mungu ambaye Anaumba vitu vyote na watu ni viumbe, na Shetani ni, hata hivyo, anayelengwa kwa uharibifu na adui Wangu wa kuchukiwa—hii ndio maana ya kweli zaidi ya maneno “ijapokuwa milima na mito yaweza kuhama na kubadilika, asili ya mtu haitabadilika.” Kuwa katika hali hii na hatua hii sasa ni ishara kwamba Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza tutaingia katika pumziko. Hii ni kwa sababu kazi Yangu katika ulimwengu imekamilika kabisa na hatua inayofuata ya kazi Yangu itanihitaji Nirudi kwenye mwili kuikamilisha. Hizi ni hatua za kazi Yangu na Nilizipanga vizuri zamani. Hoja hii inapaswa kuonekana wazi, vinginevyo watu wengi watakiuka amri Zangu za utawala.

Iliyotangulia: Sura ya 113

Inayofuata: Sura ya 115

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp