Sura ya 115

Kwa sababu yako, Moyo Wangu utakufurahia sana; kwa sababu yako, mkono Wangu utacheza kwa furaha juu yako, na Nitakupa baraka zisizo na mwisho, kwa kuwa kabla ya uumbaji, ulitoka Kwangu, na leo lazima urejee upande Wangu, kwa kuwa wewe si wa dunia ama ulimwengu bali, badala yake, wewe ni Wangu. Nitakupenda milele, Nitakubariki milele na Nitakulinda milele. Ni wale tu ambao wametoka Kwangu wanaoyajua mapenzi Yangu, na ni wao tu wataudhukuru mzigo Wangu na kufanya kile ambacho Ninataka kukifanya. Sasa, kila kitu tayari kimekwisha kutimizwa. Moyo Wangu ni kama mpira wa moto, ukiwaonea shauku wana Wangu wapendwa kuunganishwa tena nami hivi punde, ukitamani sana nafsi Yangu kurejea Sayuni kikamilifu hivi karibuni. Una ufahamu kiasi juu ya hili. Ingawa mara nyingi hatuwezi kufuatana katika roho, mara nyingi tunaweza kuandamana katika roho na kukutana katika mwili. Baba na wana daima hawatenganiki, wanaunganishwa kwa urafiki wa karibu sana. Hakuna anayeweza kukutoa katika upande Wangu hadi siku ya kurudi katika Mlima Sayuni. Ninawapenda wazaliwa Wangu wote wa kwanza wanaotoka Kwangu na Ninawachukia maadui wote wanaonipinga. Nitawarudisha wale Ninaowapenda Sayuni na kuwatupa wale wote Ninaowachukia kuzimuni, katika jehanamu. Hii ndiyo kanuni kuu ya amri Zangu za utawala. Kila kitu ambacho wazaliwa Wangu wa kwanza husema au kutenda ni maonyesho ya Roho Wangu. Kila mtu lazima awe na ushuhuda kwa wazaliwa Wangu wa kwanza kwa ufahamu dhahiri juu yake. Hii ndiyo hatua inayofuata ya kazi Yangu, mtu yeyote akipinga, Nitawaomba wazaliwa Wangu wa kwanza kuwashughulikia. Ni tofauti sasa. Wale Ninaowapenda wakinena neno la hukumu, Shetani atakufa mara moja huko kuzimuni kwa sababu tayari Nimewapa mamlaka wazaliwa Wangu wa kwanza. Hii ni kusema kuwa kuanzia sasa kuendelea, ni wakati wa wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi kutawala kwa pamoja. (Hili ni katika awamu ya nyama. ambayo ni tofauti kidogo na kutawala pamoja katika mwili.) Yeyote anayeasi katika fikira atapitia hatima sawa na wale ambao hupinga mtu Niliye. Wazaliwa Wangu wa kwanza wanapaswa kutendewa jinsi Ninavyotendewa kwa sababu sisi tu wa mwili mmoja na hatuwezi kutenganishwa asilani. Leo wazaliwa Wangu wa kwanza wanapaswa kushuhudiwa kama Nilivyoshuhudiwa hapo zamani. Hii ni mojawapo ya amri Zangu za utawala; kila mtu lazima asimame na kuwa na ushuhuda.

Ufalme Wangu huenea hadi miisho ya dunia, wazaliwa Wangu wa kwanza husafiri hadi miisho ya dunia na Mimi. Kuna vitu vingi ambavyo Mimi huvizungumzia ambavyo hamvielewi kwa sababu ya vipingamizi vya mwili wenu hivyo zaidi ya nusu ya kazi lazima ifanywe baada ya kurudi Sayuni. Inaweza kuonekana kutoka katika maneno Yangu kuwa hili haliko mbali sana, liko karibu kutimia. Kwa hivyo tena na tena Ninazungumza juu ya Sayuni na masuala katika Sayuni. Je, mnajua nia ya maneno Yangu ni gani? Je, mnajua ni nini kilicho ndani ya moyo Wangu? Moyo Wangu unatamani sana kurudi Sayuni punde, kutamatisha enzi nzima ya kale, kumaliza maisha yetu duniani (kwa kuwa Ninachukizwa sana na watu, mambo, vitu vya dunia, na kuchukia maisha katika mwili hata zaidi, na vizuizi vya mwili ni vikuu na kila kitu kitakuwa na usitawi baada ya kurudi Sayuni tu), na kupata tena maisha yetu katika ufalme. Madhumuni ya kupata mwili Kwangu mara ya kwanza yalikuwa kuweka msingi kwa ajili ya kupata mwili Kwangu mara ya pili. Hii ilikuwa njia ambayo ilipaswa kusafiriwa. Ni katika kujipeana kikamilifu kwa Shetani tu, ndipo Ningeweza kuwakomboa kuingia katika mwili Wangu wakati wa hatua ya mwisho. (Kama si kupitia kupata mwili Kwangu mara ya kwanza, Nisingeweza kutukuzwa, Nisingeweza kuchukua tena sadaka ya dhambi, hivyo mngekuja duniani kama wenye dhambi.) Kwa kuwa Nina hekima isiyo na kikomo, maadam Niliwaongoza kutoka Sayuni, Nitahakikisha Kuwarejesha Sayuni. Majaribio ya Shetani ya kuweka kizuizi njiani hayatafaulu kwa sababu kazi Yangu kuu ilitimizwa zamani sana. Wazaliwa Wangu wa kwanza ni sawa na Mimi, wao ni watakatifu na hawana mawaa na hivyo bado Nitarudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza na hatutatengana daima.

Mpango Wangu mzima wa usimamizi unafichuliwa kwenu polepole. Nimeanza kutekeleza kazi Yangu katika mataifa yote miongoni mwa watu wote. Hili limetosha kuthibitisha kuwa wakati Nitakaporudi Sayuni hauko mbali sana kwa sababu kutekeleza kazi Yangu katika mataifa yote na miongoni mwa watu ni kitu ambacho kitafanywa baada ya kurejea Sayuni. Mwendo Wangu unaanza kupata kasi zaidi na zaidi. (Kwa kuwa siku ambapo Nitarudi Sayuni inawadia, Nataka kumaliza kazi Yangu duniani kabla Nirudi.) Nazidi kushughulika zaidi na zaidi na kazi Yangu na ilhali kuna kazi kidogo zaidi na zaidi Mimi kufanya duniani, nusra iwe haipo kabisa. (Kuwa na kazi Kwangu kunaelekezwa kwa kazi katika Roho, ambayo haiwezi kuonekana na mwanadamu kwa macho ila inaweza kupatika kidogo tu kutoka katika maneno Yangu; Kujishughulisha Kwangu sio kama ilivyo kuwa na shughuli katika mwili, bali kunaashiria kupanga Kwangu kwa kazi nyingi.) Hii ni kwa sababu, kama ambavyo Nimesema, kazi Yangu duniani tayari imekwisha kumalizwa kikamilifu na kazi Yangu iliyobaki lazima isubiri hadi Nirejee Sayuni. (Sababu ya kuwa lazima Nirudi Sayuni ili kufanya kazi ni kuwa kazi ya baadaye haiwezi kutimizwa ndani ya mwili na iwapo kazi hizi zingefanywa katika mwili, ingeleta fedheha kwa jina Langu.) Wakati ambapo Nitawashinda maadui Wangu na kurudi Sayuni, maisha yatakuwa mazuri zaidi na yenye amani kuliko maisha ya kabla ya enzi. (Hii ni kwa sababu Nimeshinda dunia kabisa, na kwa usaidizi wa kupata mwili Kwangu mara ya kwanza na kupata mwili Kwangu mara ya pili Nimetukuzwa kabisa. Katika kupata mwili Kwangu mara ya kwanza, Nilitukuzwa kwa sehemu tu lakini, katika kupata mwili Kwangu mara pili, nafsi Yangu inatukuzwa kabisa, na hivyo hakuna nafasi nyingine tena za Shetani kutumia. Kwa hivyo, maisha ya baadaye Sayuni yatakuwa mazuri na yenye amani hata zaidi.) Nafsi Yangu itaonekana kwa utukufu hata zaidi mbele ya dunia na Shetani ili kulifedhehesha joka kuu jekundu, hiki ndicho kiini cha hekima Yangu yote. Kadiri Ninavyozidi kuzungumzia vitu vya nje, ndivyo mnavyoweza kuelewa zaidi; kadiri Ninavyozungumzia vitu vya Sayuni ambavyo wanadamu hawawezi kuviona, ndivyo mtakavyofikiri zaidi kuwa vitu hivi ni bure na ndivyo itakavyokuwa vigumu zaidi kwenu kuviwazia, na mtafikiri kuwa Ninawaeleza hadithi za vichimbakazi. Hata hivyo, lazima muwe waangalifu, hamna maneno matupu kinywani Mwangu, maneno yanayotoka kinywani Mwangu ni maaminifu. Ingawa ni vigumu kuyaelewa kwa njia yenu ya kufikiri, hii ni kweli kabisa. (Kwa sababu ya udhaifu wa mwili, wanadamu hawawezi kuelewa kabisa na kikamilifu kile Ninachosema, na mambo mengi ambayo Nimesema Sijayafichua kabisa, lakini tutakaporejea Sayuni, Sitahitaji kuelezea, mtakuwa na ufahamu kwa kawaida.) Hii inapaswa kuchukuliwa kwa uzito.

Ingawa wanadamu wana upungufu wa mwili na dhana, bado Nataka kuyaimarisha mawazo yenu ya kufisha na kupigana dhidi ya dhana zenu kwa njia ya mafumbo yaliyofichuliwa kwa sababu Nimesema mara nyingi kwamba hii ni hatua ya kazi Yangu (kazi hii haitakoma hadi katika kuingia Sayuni). Kuna Mlima Sayuni akilini mwa kila mtu na ni tofauti kwa kila mtu. Kwa kuwa Ninaendelea kutaja Mlima Sayuni, Nitawaambia maelezo ya jumla juu yake ili mweze kuujua kidogo. Kuwa juu ya Mlima Sayuni ni kurudi katika dunia ya kiroho. Ingawa inahusu dunia ya kiroho, si pahali ambapo watu hawawezi kuona wala kugusa; hii inahusika na mwili. Sio usioonekana kabisa au usioshikika kwa sababu wakati ambapo mwili unaonekana una sura na umbo lakini wakati ambapo mwili hauonekani hauna sura au umbo. Katika Mlima Sayuni, hakutakuwa na wasiwasi juu ya chakula, nguo, mahitaji ya kila siku na makazi, wala hakutakuwa na ndoa au familia na hakutakuwa na mgawanyiko wa jinsia (wote walio juu ya Mlima Sayuni ni nafsi Yangu, wako katika mwili mmoja, kwa hivyo hakuna ndoa, familia au mgawanyiko wa jinsia), na kila kitu ambacho nafsi Yangu huzungumzia kitafanyika. Wakati ambapo watu hawajihadhari, nafsi Yangu itaonekana kati yao na wakati ambapo watu hawatilii maanani, nafsi Yangu itatoweka. (Watu wa nyama na damu hawawezi kufikia hili, kwa hivyo ni vigumu kwenu kufikiri sasa.) Katika siku zijazo bado kutakuwa na jua, mwezi na mbingu na dunia ya asili, lakini kwa sababu nafsi Yangu itakuwa Sayuni, hakutakuwa na kuchomwa na jua au mchana na hakutakuwa kuteswa na maafa ya asili. Niliposema kuwa hatutahitaji taa au nuru ya jua kwa kuwa Mungu atatupa nuru, Nilikuwa nikizungumza juu ya kuwa Sayuni. Kulingana na dhana ya wanadamu, kila kitu katika ulimwengu lazima kiondolewe na watu wote wanaishi katika mwanga Wangu. Wanafikiri hii ni maana halisi ya “hatutahitaji taa au nuru ya jua kwa sababu Mungu atatupa nuru,” lakini ni tafsiri isiyo sahihi ya hiyo. Niliposema “kila mwezi, mti ule utazaa aina kumi na mbili ya matunda,” Nilikuwa nikimaanisha mambo katika Sayuni. Sentensi hii inawakilisha kila kitu kuhusu maisha katika Sayuni. Katika Sayuni, wakati hautakuwa mdogo na hakutakuwa na upungufu wa jiografia wala nafasi. Ndiyo maana Nilisema “kila mwezi.” “Aina kumi na mbili ya matunda” haiwakilishi tabia unayodhihirisha unapoishi leo, inahusu maisha ya uhuru huko Sayuni. Maneno haya ni majumuisho ya maisha katika Sayuni. Kutoka kwa hili mtu anaweza kuona kwamba maisha katika Sayuni yatakuwa yenye fahari na yenye namna nyingi (kwa sababu hapa “kumi na mbili” inahusu ukamilifu). Yatakuwa maisha bila huzuni na machozi, hakutakuwa na unyonyaji au ukandamizaji hivyo wote watakombolewa na kuwa huru. Hii ni kwa sababu kila kitu kipo ndani ya nafsi Yangu, hakuna atakayevitenga, na kila kitu kitakuwa mandhari ya uzuri na upya wa milele. Utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa tayari, utakuwa mwanzo wa maisha yetu baada ya kurudi kwetu Sayuni.

Ingawa kazi Yangu duniani imekamilishwa kabisa, bado Nahitaji wazaliwa Wangu wa kwanza kufanya kazi duniani, hivyo Siwezi kurudi Sayuni bado. Siwezi kurudi Sayuni peke Yangu, Nataka kurudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza baada ya wao kumaliza kazi yao duniani. Kwa njia hii, kunaweza kuitwa kupata utukufu kwa pamoja, hili litakuwa dhihirisho kamili la nafsi Yangu. (Nasema kuwa kazi ya wazaliwa Wangu wa kwanza duniani haijamalizwa bado kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza bado hawajadhihirishwa. Kazi hii lazima ifanywe na watendaji huduma watiifu na waaminifu.)

Iliyotangulia: Sura ya 114

Inayofuata: Sura ya 116

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp