Sura ya 117

Wewe Ndiwe unayefungua kitabu, Wewe Ndiwe unayefungua mihuri saba, kwa sababu siri zote hutoka Kwako na baraka zote hufichuliwa na Wewe. Mimi sina budi kukupenda Wewe milele, na Mimi sina budi kuwafanya watu wote wakuabudu Wewe, kwa sababu Wewe ni nafsi Yangu, Wewe ni sehemu ya onyesho Langu kamili lenye ukarimu, sehemu ya msingi ya mwili wangu. Kwa hiyo, ni lazima Mimi Nitoe ushahidi maalum. Ni nani mwingine kando na Yule mmoja aliye ndani ya nafsi Yangu anayefuata Moyo Wangu? Si Wewe Mwenyewe ambaye hutoa ushahidi kwa ajili Yako, lakini Roho Wangu ambaye hutoa ushahidi kwa ajili Yako, na kwa hakika Mimi sitamsamehe yeyote ambaye huthubutu kukupinga Wewe, kwa kuwa hili huhusu amri Zangu za utawala. Yote ambayo Wewe husema kwa hakika Nitayatimiza, na yote ambayo Wewe hufikiri kwa hakika Nitayakubali. Kama mtu fulani si mwaminifu kwako Wewe basi ananipinga Mimi kwa wazi, na kwa hakika Mimi Sitamsamehe. Mimi Nitawaadhibu kwa ukali wote ambao humpinga Mwanangu, na Mimi Nitawabariki wale ambao wanalingana na Wewe. Haya ndiyo mamlaka ambayo Mimi Ninakutunukia Wewe. Kwa yale yaliyosemwa zamani—matakwa na viwango vilivyowekwa kwa wana wa kiume wazaliwa wa kwanza—Wewe ni mfano mzuri. Hivyo ni kusema, vile Ulivyo ndiyo Nitakayohitaji kwa wazaliwa wa kwanza. Hiki si kitu ambacho binadamu wanaweza kufanya, lakini ni kile ambacho Roho Wangu Mwenyewe hufanya. Kama mtu yeyote huamini kuwa ni wanadamu ambao hushuhudia kwa ajili Yako basi kiumbe huyo bila shaka ni wa Shetani na adui Yangu! Kwa hiyo, shahidi ni mwenye kuondoa shaka, milele habadiliki, na kile ambacho Roho Mtakatifu huthibitisha! Hakuna yeyote anayeruhusiwa kubadilisha hilo kwa urahisi, na yeyote atakayefanya kitendo hicho, Mimi Sitasamehe! Kwa kuwa wanadamu hawawezi kuwa na ushuhuda kwa ajili Yangu, Mimi Mwenyewe hushuhudia kwa nafsi Yangu, na watu hawapaswi kuingilia kazi Yangu! Haya ni maneno ya hukumu kali ambayo kwayo kila mtu lazima awe mzingatifu!

Mnapaswa kufikiria na kuzingatia kila kitu katika yale Ninayoyasema Mimi. Usichukulie maneno Yangu kikawaida, bali sikiliza kwa makini. Kwa nini Mimi Ninasema kuwa wana wa kiume wazaliwa wa kwanza ni nafsi Yangu? Na sehemu ya msingi ya ufalme Wangu? Kabla ya enzi zote tuliishi pamoja na hatukuwahi kutengana kamwe. Kwa sababu ya mvurugo wa Shetani, baada ya Mimi kuwa mwili mara ya kwanza Mimi Nilirudi tena Sayuni. Kuendelea kutoka hapa, sisi sote tulikuja katika dunia, na baada ya Mimi kupata ushindi katika siku za mwisho—yaani, baada ya mimi kuwapata nyinyi tena kutoka kwa mwili ambao Shetani amepotosha—Mimi nitawaleta tena Sayuni ili nafsi Yangu iweze kuungana tena, kutotenganishwa tena kamwe. Baada ya hayo Mimi Sitapata mwili upya tena, na nyinyi hakika hamtatoka katika mwili Wangu. Hiyo ni kusema, baada ya hapo Mimi Sitaiumba dunia tena, lakini Nitabaki milele bila kutenganishwa na wanangu wa kiume wazaliwa wa kwanza katika Sayuni, kwa sababu kila kitu kimekamilishwa kwelikweli, na Mimi Nimekaribia kuhitimisha enzi nzee nzima. Ni katika Sayuni tu ambako kuna maisha ya mbingu na nchi mpya, kwa kuwa nafsi Yangu hupatikana Sayuni. Hakutakuwa na mbingu mpya au dunia mpya zaidi ambazo zipo bali na hii. Mimi ni mbingu mpya, na Mimi pia ni nchi mpya, kwa sababu nafsi Yangu hujaza Sayuni nzima. Pia inaweza kusemwa kwamba wanangu wa kiume wazaliwa wa kwanza ni mbingu mpya, wana Wangu wa kiume wazaliwa wa kwanza ni nchi mpya. Wanangu wa kiume wazaliwa wa kwanza na Mimi ni wa mwili mmoja, wa kutotenganishwa. Kusema juu Yangu ni lazima kujumuishe wana wa kiume wazaliwa wa kwanza, na Mimi hakika Sitamsamehe yeyote ambaye hujaribu kututenganisha. Wakati Ninayafanya mataifa yote na watu kurejea mbele ya kiti Changu cha enzi, mashetani yote yatafedhehiwa na mapepo machafu yatatoroka kwa woga mbali na Mimi. Halafu ni hakika kuwa haki itakuwepo miongoni mwa watu wote (kumaanisha miongoni mwa wana Wangu wa kiume na watu), na ni hakika kuwa hakutakuwa na vurugu zozote za Shetani katika mataifa yote, kwa maana Mimi Nitakuwa Nikishikilia uongozi juu ya ulimwengu dunia wote na watu wa mataifa, na mashetani yatakuwa yameharibiwa kwelikweli, kushindwa kabisa, na watakuwa wakipokea adhabu ya amri Zangu za utawala.

Mimi Ninaendelea na kazi miongoni mwa watu wote, lakini wao wana nuru ya Roho Wangu tu, na hakuna hata mmoja kati yao mwenye sifa zinazostahili kufunua mafumbo Yangu, hakuna yeyote mwenye sifa zinazostahili kunionyesha Mimi. Ni Yule tu mtu ambaye huja kutoka Kwangu tu mwenye sifa zinazostahili za kufanya kazi Yangu, jinsi ilivyo kwa wengine, Mimi huwatumia tu watu hao kwa muda. Roho Wangu hatamshukia mtu kiholela, kwa kuwa kila kitu ndani Yangu ni cha thamani. Kwa Roho Wangu kushuka juu ya mtu fulani na kwa Roho Wangu kufanya kazi kwa mtu fulani ni vitu tofauti kabisa. Roho Wangu hufanya kazi kwa watu walio nje Yangu, lakini Roho Wangu hushuka juu ya Yule mtu ambaye hutoka Kwangu. Haya ni mambo mawili yasiyohusiana kabisa. Kwa vile mtu Huyo atokaye Kwangu ni mtakatifu, lakini wale walio nje Yangu si watakatifu, bila kujali ni wazuri kiasi gani wanaweza kuwa. Roho Wangu hatamshukia mtu kwa sababu yoyote ndogo. Watu hawapaswi kuwa na wasiwasi. Mimi huwa Sifanyi makosa yoyote, na Mimi ni asilimia mia moja kwa uhakika kuhusu Ninayofanya! Kama ambavyo Nimemshuhudia Yeye, kwa hakika Nitamlinda Yeye pia; Mtu huyo waziwazi hutoka Kwangu na ni sehemu ya msingi ya nafsi Yangu. Kwa hiyo, Natumaini watu wanatenga dhana zao wenyewe, waache mawazo waliyopewa na Shetani, waamini kila tamko Langu kuwa ni la kweli, na hawayaruhusu mashaka kuingia katika mawazo yao. Hili ndilo Agizo Langu kwa binadamu, ushawishi Wangu kwa binadamu. Kila mtu lazima ayashike mambo haya, kila mtu lazima kwa kweli ayatii, na ni lazima ayachukue Ninayoyasema Mimi kuwa ndicho kiwango.

Mimi sipaswi tu kuanza kazi Yangu kati ya mataifa yote na watu wote tu, lakini pia Mimi kuanza kazi Yangu kila mahali katika ulimwengu dunia, na hii inaonyesha hata zaidi kuwa siku ya kurudi Kwangu Sayuni haiko mbali sana (kwa sababu ni muhimu Kwangu kurudi Sayuni kabla Niweze kuanza kazi kati ya watu wote na kote katika ulimwengu dunia). Je, kuna mtu yeyote ambaye anaweza kuzielewa hatua za kazi Yangu na njia ambayo Mimi hufanya kazi? Sababu ya Mimi kusema Nitakutana na wageni katika roho ni kwa sababu hili kimsingi haliwezi kufanyika katika mwili, na kwa sababu Mimi sitaki kubahatisha hatari kwa mara ya pili. Hizi ndizo sababu za kuwasiliana kwa karibu na wageni katika roho. Hii itakuwa katika dunia ya kweli ya kiroho, siyo dunia fulani ya kiroho isiyo dhahiri kama inavyowazwa na wale[a] wanaoishi katika mwili. Kile Ninachokisema wakati huo kitakuwa ni tofauti tu katika jinsi Mimi husema kwani itakuwa ni enzi tofauti. Kwa hiyo, Mimi Nawakumbusha binadamu tena na tena kuhakiki jinsi ambavyo Mimi hunena, na Mimi Nawakumbusha wanadamu pia kwamba kuna siri katika kile ambacho Mimi husema ambacho watu hawawezi kukifunua. Lakini hakuna anayeelewa kwa nini Mimi Nasema vitu hivi, na kwa sababu tu Mimi Nawaambia hili leo ndipo muweze kuelewa kidogo, lakini bado si kabisa. Baada ya enzi hii katika kazi Yangu, Mimi nitawaarifu hatua kwa hatua. (Bado Mimi Ninataka kuondoa baadhi ya watu kupitia hili, hivyo Mimi Sitasema chochote kwa sasa.) Hii ndiyo njia ya hatua ifuatayo katika kazi Yangu. Kila mtu anapaswa kuhakiki na kuona wazi kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni wa busara.

Tanbihi:

a. Maandiko ya awali hayana maneno “kama inavyowazwa na wale.”

Iliyotangulia: Sura ya 116

Inayofuata: Sura ya 118

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp