Sura ya 120

Sayuni! Salamu! Sayuni! Ita kwa sauti! Nimerudi kwa ushindi, Nimerudi nikiwa mshindi! Watu wote! Harakisheni mpange foleni kwa utaratibu! Vitu vyote! Mtakuja kusimama kabisa, kwa sababu nafsi Yangu inaukabili ulimwengu mzima na nafsi Yangu inaonekana katika Mashariki ya dunia! Nani anayethubutu kutopiga magoti katika ibada? Nani anayethubutu kutoniita Mungu wa kweli? Nani anayethubutu kutoangalia juu kwa kumcha? Nani anayethubutu kutotoa sifa? Nani anayethubutu kutangaza kwa shangwe? Watu wangu wataisikia sauti Yangu, Wanangu watasalia ndani ya ufalme Wangu! Milima, mito, na vitu vyote vitashangilia bila kukoma, na kurukaruka bila kupumzika. Wakati huu, hakuna atakayethubutu kurudi nyuma, hakuna atakayethubutu kusimama katika upinzani. Hili ni tendo Langu la ajabu, na hata zaidi ni nguvu Yangu kuu! Nitafanya kila kitu kiniche Mimi katika moyo wake na hata zaidi Nitafanya kila kinisifu Mimi. Hili ni lengo la msingi la mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, nami Nimeamua hili. Hakuna hata mtu mmoja, hakuna hata kitu kimoja wala jambo moja, linathubutu kusimama kunipinga Mimi, au linathubutu kusimama kushindana na Mimi. Watu wangu wote wataelekea mlimani Kwangu (hili linaonyesha dunia ambayo Nitaiumba baadaye) nao watatii mbele Zangu kwa sababu Ninao uadhama na hukumu, nami Nina mamlaka. (Hili linahusu wakati Niko katika mwili. Pia Ninayo mamlaka katika mwili lakini kwa sababu upungufu wa muda na nafasi hayawezi kuzidi kiwango katika mwili, kwa hiyo haiwezi kusemwa kwamba Nimepata utukufu kamili. Ingawa Nawapata wazaliwa wa kwanza katika mwili, bado haiwezi kusemwa kwamba Nimepata utukufu. Ni wakati tu Nitakaporudi Sayuni na kubadilisha sura Yangu ndipo inaweza kusemwa kwamba Nina mamlaka, yaani, Nimepata utukufu.) Hakuna kitu kitakuwa kigumu Kwangu. Kila kitu kitaharibiwa kwa maneno kutoka kinywani Mwangu, na ni kwa sababu ya maneno kutoka kinywani Mwangu ndipo yatatukia na kufanyika kamili, hiyo ni nguvu Yangu kuu na hayo ni mamlaka Yangu. Kwa sababu Nina nguvu tele na nimejawa na mamlaka, hakuna mtu anayeweza kuthubutu kunizuia Mimi. Tayari Nimepata ushindi juu ya kila kitu na Nimewashinda wana wote wa uasi. Nawaleta wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja kurudi Sayuni. Si Mimi pekee Yangu Ninayerejea Sayuni. Kwa sababu hii wote watawaona wazaliwa Wangu wa kwanza na hivyo watakuza moyo wa uchaji kwa ajili Yangu. Hili ni lengo Langu katika kuwapata wazaliwa Wangu wa kwanza na umekuwa mpango Wangu tangu wakati Wangu wa kuiumba dunia.

Wakati kila kitu kiko sawa, hiyo ndiyo siku ambayo Nitarudi Sayuni, na siku hii itakumbukwa na watu wote. Nitakaporudi Sayuni, vitu vyote duniani vitakuwa kimya na vitu vyote duniani vitakuwa na amani. Wakati ambapo Nimerudi Sayuni, kila kitu kitarejelea sura yake ya awali. Wakati huo, Nitaianza kazi Yangu katika Sayuni, Nitawaadhibu waovu na kuwatuza wazuri, Nitaleta mamlakani haki Yangu nami Nitatekeleza hukumu yangu. Nitatumia maneno Yangu kukamilisha kila kitu na kumfanya kila mtu na kila kitu kipitie mkono Wangu unaoadibu. Nitawafanya watu wote wauone utukufu Wangu mzima, waione hekima Yangu nzima, wauone ukarimu Wangu mzima. Hakuna mtu yeyote atathubutu kusimama kutoa hukumu kwani yote imekamilika nami. Katika hili, kila mtu ataiona heshima Yangu yote na wote watapata uzoefu wa ushindi Wangu wote kwa kuwa kila kitu kimewekwa wazi nami. Kutokana na haya, mtu anaweza kuuona uwezo Wangu mkubwa vizuri, na kuyaona mamlaka Yangu. Hakuna mtu atathubutu kunikosea Mimi, hakuna mtu atathubutu kunizuia Mimi. Yote yamewekwa waziwazi nami, nani angethubutu kuficha kitu chochote? Nina uhakika wa kutomwonyesha huruma! Mafidhuli mno kama wao lazima waipokee adhabu Yangu kali na watu wabaya kabisa kama wao lazima waondolewe kutoka machoni Pangu. Nitawatawala kwa fimbo ya chuma nami Nitayatumia mamlaka Yangu kuwahukumu, bila huruma yoyote na bila kutowaudhi kabisa, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe Nisiye na hisia na ambaye ni mwadhimu na Siwezi kukosewa. Hii inapaswa kueleweka na wote na kuonekana na wote ili kuepuka “bila kusudi au sababu” kuangushwa nami, kuangamizwa nami, wakati utakapofika, kwa kuwa fimbo Yangu itawaangusha wote ambao wananikosea. Sitajali kama wanajua amri Zangu za utawala au la; hilo halitakuwa muhimu Kwangu kwa kuwa nafsi Yangu haiwezi kuvumilia kosa la mtu yeyote. Hii ndiyo sababu imesemwa kwamba Mimi ni simba; yeyote Ninayemgusa, Nitawaangusha. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa sasa kusema kwamba Mimi ni Mungu wa huruma na wema ni kunikufuru. Kwa asili Mimi si Mwanakondoo bali ni simba. Hakuna mtu anayethubutu kunikosea na yeyote anayenikosea Nitamwadhibu mara moja kwa kifo, bila hisia hata kidogo! Kutokana na hili, mtu anaweza kuiona tabia Yangu vizuri. Kwa hiyo, katika enzi ya mwisho kundi kubwa la watu likijitoa, hilo ni jambo ambalo ni gumu kwa wanadamu kuvumilia, lakini Nina raha na furaha na sioni hii kama kazi ngumu hata kidogo, hiyo ni tabia Yangu.

Natarajia kwamba watu wote watakuwa na moyo mtiifu ili kufuata yote yanayotokana na Mimi. Kwa njia hiyo, bila shaka Nitawabariki wanadamu sana kwa sababu Nimesema kwamba wale ambao wanalingana nami watahifadhiwa huku wale ambao ni maadui Kwangu watalaaniwa. Nimeamua hili na hakuna yeyote anaweza kulibadilisha. Mambo hayo ambayo Nimeamua ni mambo ambayo Nimekamilisha na yeyote atakayekwenda kinyume nayo ataadibiwa mara moja. Nina kila kitu ninachohitaji Sayuni na kila kitu ambacho Nina hamu nacho. Hakuna dalili ya dunia Sayuni na ukilinganishwa na dunia ni kasri tajiri na kuu, lakini hakuna mtu ameingia ndani yake na hivyo haipo kabisa katika mawazo ya mwanadamu. Maisha Sayuni ni tofauti na maisha duniani; duniani, maisha ni kula, kuvaa, kucheza, na kutafuta furaha, ilhali Sayuni ni tofauti sana. Ni maisha ya Baba na wana waliozama katika furaha, wakiijaza daima nafasi yote ya ulimwengu, lakini kila mara pia wakija pamoja kwa umoja. Kwa kuwa sasa mambo yamefika katika kiwango hiki leo, Nitawaambia mahali ambapo Sayuni uko. Sayuni uko Ninapoishi, ni eneo la nafsi Yangu. Kwa hiyo, lazima Sayuni uwe mahali patakatifu, na ni lazima iwe mbali sana na dunia. Kwa hiyo, Nasema kwamba Ninawadharau watu, vitu na masuala ya dunia, Ninachukia sana kula, kunywa, kucheza na kutafuta raha kwa mwili, kwa sababu bila kujali jinsi anasa za dunia zinavyofurahisha, haziwezi kulinganishwa na maisha katika Sayuni; ni tofauti kati ya mbingu na dunia na hakuna njia ya kulinganisha hizi mbili. Sababu ambayo kuna mafumbo mengi ambayo mwanadamu hawezi kufumbua duniani yote ni kwa sababu watu hawajasikia chochote kuhusu Sayuni. Naam, Sayuni uko wapi hata hivyo? Je, iko katika anga za juu kama watu wanavyoifikiria kuwa? Hapana! Hayo ni mawazo tu katika akili za wanadamu. Mbingu ya tatu ambayo Nimeitaja inafikiriwa na watu kuwa na maana ya ishara, lakini ufahamu uliodhaniwa katika akili za wanadamu ni kinyume kabisa cha maana Yangu. Mbingu ya tatu ambayo Ninanena kuihusu hapa si uongo hata kidogo. Hii ndiyo sababu Nasema kwamba Sitaviharibu jua, mwezi, nyota, na miili ya mbinguni, nami Sitaziondoa mbingu na dunia. Je, Naweza kuharibu makazi Yangu? Naweza kuuondoa Mlima Sayuni? Je, hili si jambo la kuchekesha? Mbingu ya tatu ni makazi Yangu, ni Mlima Sayuni, na jambo hili ni hakika. (Kwa nini Nasema kwamba hii ni halisi? Ni kwa sababu Ninachosema sasa hakiwezi kueleweka kabisa na mwanadamu, anaweza tu kukisikia. Upeo wa kufikiri wa mwanadamu hauwezi kukijumuisha kabisa, na kwa hiyo Nitasema tu kiasi hiki kuhusu Sayuni ili kuwaepusha watu kuiona kama hadithi tu.)

Baada Yangu kurudi Sayuni, wale walio duniani wataendelea kunisifu Mimi kama zamani. Wale watendaji huduma waaminifu wanabaki wakisubiri kutoa huduma Kwangu lakini kazi yao itakuwa imefika mwisho. Jambo bora zaidi wanaloweza kufanya ni kutafakari hali Yangu kuwa duniani. Wakati huo, Nitaanza kushusha maafa juu ya wale ambao watakabiliwa na maafa makubwa; ilhali kila mtu anaamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye haki. Bila shaka Sitawaadhibu wale watendaji-huduma waaminifu, bali nitawaruhusu tu wapokee neema Yangu. Maana Nimesema kuwa nitawaadhibu watenda dhambi wote, na kwamba wale wanaotekeleza matendo mema watapata starehe yakinifu iliyokirimiwa nami, huu ni ufunuo kwamba Mimi ni Mungu wa haki na uaminifu Mwenyewe. Nitakaporudi Sayuni, Nitaanza kugeuka kuelekea kila taifa duniani; Nitawaleta Waisraeli kwa wokovu na kuwaadibu Wamisri. Hii ni hatua inayofuata katika kazi Yangu. Kazi Yangu wakati huo haitakuwa sawa kama siku hizi: Haitakuwa kazi katika mwili lakini itauzidi mwili kabisa, na kwa kuwa Nimenena, itafanyika, na kama Nilivyoagiza, itasimama imara. Mradi imesemwa nami, itatimizwa mara moja katika hali halisi, na hii ndiyo maana ya kweli ya neno Langu kunenwa na kutimizwa kwake kufanyika kwa wakati mmoja, kwa sababu Ninachosema ni mamlaka yenyewe. Sasa Ninanena kuhusu baadhi ya mambo ya jumla ili kuwasaidia watu duniani kuwa na dalili chache bali si kufahamu ovyo ovyo. Wakati huo utakapofika, kila kitu kitapangwa nami na hakuna anayepaswa kutenda kimakusudi ili kuepuka kuangushwa kwa mkono Wangu. Katika mawazo ya wanadamu, yote Ninenayo si dhahiri, kwa sababu hata hivyo namna ya mwanadamu ya kufikiri ni finyu, na mawazo ya mwanadamu na yale ambayo Nimesema yako mbali sana kama mbingu na ardhi. Kwa hiyo, hakuna anayeweza kuyafumbua na jambo bora zaidi ni kukubaliana na kile Ninachosema, huu ni mwelekeo usiobadilika wala kuzuilika. Nimesema: “Katika siku za mwisho, mnyama ataibuka kuwatesa watu Wangu na wale ambao wanaogopa kifo watawekewa alama na muhuri ili kunyakuliwa na mnyama. Wale ambao wameniona watauawa na mnyama.” “Mnyama” katika maneno haya bila shaka inarejelea Shetani ambaye huwadanganya watu, hiyo ni kusema kwamba Nitakaporudi Sayuni, kundi kubwa la watendaji huduma litajiondoa, yaani, litanyakuliwa na mnyama. Viumbe hawa wote watarudi katika shimo lisilo na mwisho kupokea kuadibu Kwangu kwa milele. “Wale ambao wameniona” inaashiria wale watendaji huduma waaminifu ambao wameshindwa nami. “Baada ya kuniona” inamaanisha wao kushindwa nami. “Kuuawa na mnyama” inahusu Shetani, kushindwa na Mimi, asithubutu kusimama kunipinga Mimi, hiyo ni kusema, Shetani hatathubutu kufanya kazi yoyote juu ya watendaji huduma hawa. Kwa hiyo, nafsi za watu hawa zitakuwa zimehifadhiwa, na hii inachangia uwezo wao wa kuwa waaminifu Kwangu, ambayo ni kusema kwamba wale watendaji huduma waaminifu watakuwa na uwezo wa kuipokea neema Yangu na baraka Yangu. Kwa hiyo, Nasema kwamba nafsi zao zitakuwa zimeokolewa (hii haimaanishi kupaa hadi mbingu ya tatu, ambayo ni dhana tu ya mwanadamu). Lakini wale watumishi wabaya watafungwa tena na Shetani na kisha watatupwa katika shimo lisilo na mwisho. Hii ni adhabu Yangu kwao, ni adhabu kwa ajili yao, na ni kile ambacho makosa yao yanastahili.

Kufuatia kuharakisha hatua kwa kazi Yangu, wakati Wangu duniani unapungua hatua kwa hatua. Tarehe ya kurudi Kwangu Sayuni yanakaribia. Wakati ambapo kazi Yangu duniani imefika mwisho, utakuwa wakati wa kurudi Kwangu Sayuni. Sipendi kuishi duniani kamwe, lakini kwa ajili ya usimamizi Wangu, kwa ajili ya mpango Wangu, Nimevumilia mateso yote. Leo, wakati umekwishafika. Nitaharakisha hatua Zangu, na hakuna mtu anayeweza kuenda kwa mwendo sawa nami. Kama watu wanaweza kulielewa au la, Nitawaambia kwa kina yote ambayo mwanadamu hawezi kuelewa lakini wale kati yenu mlio duniani mnahitaji kujua. Kwa hiyo, Nasema kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe Ninayeushinda wakati na nafasi. Isingekuwa ili kuwapata wazaliwa wa kwanza na hivyo kumshinda Shetani, Ningekuwa tayari nimerudi Sayuni, au hasa nisingekuwa Nimewaumba wanadamu. Ninaudharau ulimwengu wa mwanadamu, Nawachukia sana watu walio mbali nami, hata kufikia kiwango cha kufikiria kuwaangamiza wanadamu wote kwa dharuba moja. Hata hivyo, kazi Yangu inayo utaratibu na muundo, ina kadiri na kiasi, haiko bila taratibu. Yote ambayo Ninafanya ni ili kumshinda Shetani, na hata zaidi ili Niweze kuwa pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza haraka iwezekanavyo. Hili ni Lengo langu.

Iliyotangulia: Sura ya 119

Inayofuata: Utangulizi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp