Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele
Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kumiliki, wala si kitu ambacho kila mtu anaweza kufikia kwa urahisi. Hii ni kwa sababu uzima unaweza kutoka tu kwa Mungu, ambayo ni kusema, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayemiliki kiini cha uzima, na ni Mungu Mwenyewe pekee aliye na njia ya uzima. Na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Tangu uumbaji wa dunia, Mungu amefanya kazi kubwa sana inayobeba pamoja nayo uzima uhai wa uzima, Amefanya kazi nyingi ambayo inamletea mwanadamu uzima, na Amelipa gharama kubwa inayomwezesha mwanadamu apate uzima. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ndiye njia ambayo kwayo mwanadamu anaweza kufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kuwepo moyoni mwa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa wanadamu wakati wote. Yeye ndiye nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuendelea kuishi kwa mwanadamu, na rasilmali kubwa ya kuwepo kwa mwanadamu baada ya kuzaliwa. Yeye huwasababisha watu kuzaliwa upya, na kuwawezesha kuishi kwa ushupavu katika jukumu lao binafsi. Akitegemea uwezo Wake, na nguvu Yake ya uzima isiyozima, mwanadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, huku nguvu ya uzima wa Mungu imekuwa ikitoa utegemezi miongoni mwa binadamu, na Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; hata zaidi ya hayo, zinapita mamlaka yoyote. Uzima Wake ni wa milele, nguvu Zake ni za ajabu, na nguvu Zake za uzima haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za uzima wa Mungu zipo na hung’aa kwa mwangaza ulio mzuri sana, bila kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko ya ajabu, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote yanaweza kupita, lakini uzima wa Mungu bado utakuwepo. Hii ni kwa sababu Mungu ndiye chanzo cha kuwepo kwa vitu vyote, na mzizi unaotegemewa na kila kitu ili kiendelee kuishi. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.
Pengine, sasa, unataka kupokea maisha, au labda unataka kupata ukweli. Vyovyote vilivyo, unataka kumpata Mungu, kumpata Mungu unayeweza kutegemea, na ambaye anaweza kukupa uzima wa milele. Ukitaka kupata uzima wa milele, lazima kwanza uelewe chanzo cha uzima wa milele, na lazima kwanza ujue Mungu yuko wapi. Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, lazima kwanza uelewe aliko Mungu, na jinsi ya kupata njia hii ya uzima wa milele. Hebu sasa tushiriki kwa masuala haya mawili tofauti.
Kama kweli unataka kupata njia ya uzima wa milele, na kama wewe unayo tamaa katika utafutaji wako kwa ajili yake, basi kwanza ulijibu swali hili: Mungu yuko wapi leo? Labda utajibu kwamba Mungu anaishi mbinguni, bila shaka—Hangekuwa akiishi nyumbani kwako, sivyo? Labda unaweza kusema, kawaida Mungu anaishi kati ya mambo yote. Au unaweza kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa kila mtu, au kwamba Mungu yuko katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sipingi lolote kati ya haya, lakini lazima nifafanue suala hilo. Sio sahihi kabisa kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa mwanadamu, wala si makosa kabisa. Hayo ni kwa sababu, miongoni mwa wanaomuamini Mungu, wapo ambao imani yao ni ya kweli na wale ambao imani yao ni ya uwongo, kuna wale ambao Mungu amewaridhia na wale ambao Amewachukia, wapo wanaomridhia na wale anaowachukia, na wapo ambao anawafanya kuwa wakamilifu na wale anaowaondoa. Na kwa hivyo Ninasema kwamba Mungu anaishi ndani ya mioyo ya watu wachache tu, na watu hawa bila shaka ni wale wanaomwamini Mungu kweli, wale ambao Mungu anawakubali, wale wanaompendeza Yeye, na wale ambao Yeye huwakamilisha. Wao ni wale wanaoongozwa na Mungu. Kwa kuwa wanaongozwa na Mungu, kwa hivyo ni watu ambao tayari wamesikia na kuona njia ya Mungu ya uzima wa milele. Wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya uongo, wale ambao hawajaidhinishwa na Mungu, wale ambao wanadharauliwa na Mungu, wale ambao wamechujwa na Mungu—wamefungwa katika kukataliwa na Mungu, wamefungwa kubaki bila njia ya maisha, na wamefungwa kubaki wajinga wa kujua aliko Mungu. Kwa upande mwingine, wale ambao Mungu anaishi katika mioyo yao wanajua aliko Mungu. Wao ndio watu ambao Mungu amewapa njia ya uzima wa milele, na wao ndio wanaomfuata Mungu. Je, unajua, sasa, aliko Mungu? Mungu yuko katika moyo wa mwanadamu na upande wa mwanadam. Hayupo tu katika ulimwengu wa kiroho, na juu ya vitu vyote, lakini hata zaidi Yupo duniani ambapo mwanadamu huishi. Na hivyo kuwasili kwa siku za mwisho kumechukua hatua za kazi ya Mungu katika eneo jipya. Mungu ana ukuu juu ya vitu vyote katika ulimwengu, na Yeye ndiye mhimili mkuu wa mwanadamu katika moyo wake, na zaidi ya hayo, Yuko miongoni mwa mwanadamu. Ni kwa njia hii pekee Anaweza kuleta njia ya uzima kwa mwanadamu, na kumleta mwanadamu katika njia ya uzima. Mungu amekuja duniani, na Anaishi kati ya wanadamu, ili wanadamu wanaweza kupata njia ya uzima, na hivyo binadamu anaweza kuwepo. Wakati huo huo, Mungu pia naamuru vitu vyote katika ulimwengu, ili viweze kushirikiana na usimamizi Wake miongoni mwa wanadamu. Na hivyo, kama wewe unakiri tu kwamba Mungu yuko mbinguni na katika moyo wa mwanadamu, lakini usikiri ukweli wa kuwepo kwa Mungu miongoni mwa watu, basi kamwe hutapata uzima, na kamwe hutapata njia ya kweli.
Mungu Mwenyewe ni uzima, na ukweli, na uzima Wake na ukweli vipo pamoja. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli hawatapata uzima kamwe. Bila mwongozo, usaidizi, na utoaji wa ukweli, utapata tu barua, mafundisho, na, zaidi ya hayo, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, unaamini tu katika kivuli cha Mungu kilichoachwa tangu Alipofanya kazi hapo awali miongoni mwa wanadamu, na unaamini tu katika njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi Wake katika nyakati za awali. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asioweza kubadilika, huwezi kusikiza wosia!
Mungu aliyepata mwili anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna chochote cha kupita kiasi kuhusu hili, kwa kuwa Anamiliki kiini cha Mungu, na ana tabia ya Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kufikiwa na mwanadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa uliochukuliwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kuonyesha tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu vizuri, na kumpa binadamu uzima. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, kwani ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote kinachohusiana na kiini cha Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba uhalali wa Kristo hauwezi kuelezwa na mwanadamu, bali unajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa njia hii, kama kweli unataka kutafuta njia ya uzima, lazima kwanza ukiri kuwa ni kwa kuja duniani ndiyo Mungu hutekeleza kazi ya kumpa mwanadamu njia ya uzima binadamu, na lazima ukiri ni katika siku za mwisho Yeye anakuja duniani kumpa mwanadamu njia ya uzima. Haya si ya wakati wa zamani; yanatendeka leo.
Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta njia ya kweli ya kudumu na ya milele. Ukweli huu ndiyo njia ambayo kwayo binadamu anapata uzima, na ndiyo njia pekee ambayo mwanadamu atamjua Mungu na kukubaliwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maneno, na minyororo ya historia kamwe hawataweza kupata uzima wala kupata njia ya kudumu ya uzima. Hii ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Ukitafuta tu kushikilia yaliyopita, ukisimama tu bila kusonga na kuweka mambo jinsi yalivyo, na usitafute kubadilisha hali iliyopo na kuitupilia mbali historia, hivyo hutakuwa ukimpinga Mungu kila wakati? Hatua za kazi ya Mungu ni zenye nguvu na kuu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—lakini wewe unakaa tu bila kufanya chochote ukisubiri maangamizo, ukikwamilia yale ya zamani na kusubiri vitu vikuangukie miguuni. Kwa njia hii, unaweza kuchukuliwaje kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Unaweza kuonyeshaje kwamba Mungu unayeshikilia ndiye Mungu ambaye ni mpya daima na kamwe si wa zamani? Na maneno ya vitabu vyako vilivyochuchuka yanawezaje kukubeba hadi katika enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi mwako ni maneno tu ambayo yanaweza tu kukupa furaha ya muda mfupi, wala sio ukweli unaoweza kukupa uzima. Maneno ya maandiko unayosoma yanaweza tu kuuimarisha ulimi wako; hayo siyo maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua uzima wa binadamu, sembuse hayo kuwa njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwenye ukamilifu. Je, tofauti hii haikupi sababu ya kutafakari? Je, haikupi umaizi ndani ya siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujipeleka mwenyewe mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Ninakusihi, basi, uache kuota na uangalie ni nani anayefanya kazi sasa—tazama uone ni nani sasa anayetekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu katika siku za mwisho. Kama huwezi, kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wenye mzaha mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba wale ambao hawamkubali Kristo wa siku za mwisho watachukiwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, na hakuna ambaye anaweza kumpita Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unamwamini Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kulitii neno Lake. Usifikiri tu kuhusu kupata baraka huku ukikosa kuweza kupokea ukweli na ruzuku ya uzima. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili Aweze kuwatolea uzima wale wote ambao wanamwamini kwa dhati. Kazi hii ipo kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuiingia enzi mpya, na kazi hii ndiyo njia ambayo lazima ifuatwe na wale wote ambao wataingia katika enzi mpya. Kama humtambui Kristo, na zaidi ya hayo umhukumu, umkufuru au kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Hii ni kwa sababu Kristo huyu Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani, na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unamkufuru Roho Mtakatifu.Adhabu inayostahili kwa wale wanaomkufuru Roho Mtakatifu ni dhahiri kwa wote. Pia nakuambia hili: Ukimpinga Kristo wa siku za mwisho, ukimkataa Kristo wa siku za mwisho, basi hakuna mtu mwingine anayeweza kubeba matokeo ya hili kwa niaba yako. Zaidi ya hayo, kuanzia wakati huo na kuendelea hutawahi kuwa na nafasi ya kupata kibali cha Mungu kamwe; hata ukitaka kujikomboa, hutaweza kuutazama uso wa Mungu tena. Hii ni kwa sababu unayempinga si mwanadamu, unayemkataa si mtu asiye na maana, bali ni Kristo. Je, unajua matokeo ya hili ni yapi? Hufanyi kosa dogo, bali unatenda dhambi mbaya sana. Na kwa hivyo namshauri kila mtu asitoe kucha na meno au kutoa maoni kiholela mbele ya ukweli, kwa maana ukweli pekee ndio unaoweza kukuletea uzima, na hakuna chochote isipokuwa ukweli kinachoweza kukuwezesha kuzaliwa upya na kuutazama uso wa Mungu tena.
Tanbihi:
a. Kipande cha gogo lililokufa: Nahau ya Kichina yenye maana “-siyoweza kusaidiwa.”