Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inavyozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi. Kuzindua roho za watu hawa waliopotoka pakubwa na kudanganywa kabisa ndiyo shabaha ya aina hii ya hukumu. Mwanadamu hana roho, yaani, roho yake ilikufa kitambo na hajui kwamba kuna Mbingu, hajui kwamba kuna Mungu, na bila shaka hajui kwamba yeye mwenyewe anang’ang’ana kwenye lindi kuu la kifo; anaweza kujuaje kwamba anaishi katika kuzimu hii yenye maovu hapa ulimwenguni? Angewezaje kujua kwamba maiti hii yake ambayo imeoza, kwa kupotoshwa na shetani, imeanguka Kuzimuni kwenye kifo? Angewezaje kujua kwamba kila kitu hapa ulimwenguni kimeharibiwa kitambo kiasi cha kutokarabatika na mwanadamu? Na angewezaje kujua kwamba Muumba amekuja ulimwenguni leo na anatafuta kundi la watu waliopotoka ambao Anaweza kuokoa? Hata baada ya mwanadamu kupitia kila usafishaji na hukumu inayowezekana, ufahamu wake wa chini unashtuka kwa shida na kwa kweli hauitikii chochote. Binadamu wamezoroteka kweli! Ingawa aina hii ya hukumu ni kama mvua katili ya mawe inyeshayo kutoka mbinguni, ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa binadamu. Kama isingekuwa ya kuhukumu watu hivi, kusingekuwa na matokeo yoyote na haingewezekana kabisa kuwaokoa watu dhidi ya janga la umaskini. Kama isingekuwa kwa kazi hii, ingekuwa vigumu sana kwa watu kutoka Kuzimuni kwa sababu mioyo yao imekufa kitambo na roho zao kukanyagiwa kitambo na Shetani. Kuwaokoa nyinyi ambao mmeanguka kwenye kina kirefu cha uozo kunahitaji kuwaita kwa bidii sana, kuwahukumu kwa bidii sana, na kwa kufanya hivi tu ndipo mioyo hiyo yenu migumu itakapozinduka.

Miili yenu, matamanio yenu ya kupita kiasi, ulafi wenu, na ashiki yenu vyote vimekita mizizi ndani yenu. Mambo haya yanaidhibiti sana mioyo yenu kiasi kwamba hamna nguvu za kutupa huo utumwa wa mawazo hayo ya kikabaila na yaliyooza. Hamtamani kubadilisha hali yenu ya sasa, wala kuukimbia ushawishi wa giza. Mmefanywa kuwa watumwa tu wa mambo hayo. Hata kama mnajua kwamba maisha kama hayo ni yenye maumivu sana na kwamba ulimwengu kama huo ni wenye giza la kupindukia, bado, hakuna hata mmoja wenu anao ujasiri wa kubadilisha maisha ya aina hii. Mnatamani tu kutoroka aina hii ya maisha halisi, kuondoa nafsi zenu kutoka kwenye mahali pa mateso ya muda na kuishi katika mazingira yenye amani, furaha na yafananayo na mbinguni. Hamko radhi kuvumilia magumu ili kuweza kubadilisha maisha yenu ya sasa; vilevile hamko radhi kutafuta ndani ya hukumu hii na kuadibu huku maisha ambayo mnafaa kuyaishi. Badala yake, mnaziota ndoto zisizo na uhalisi kabisa kuhusu ulimwengu mzuri wa nje ya miili yenu. Maisha mnayotamani ni yale mnayoweza kupata kwa urahisi bila kupitia maumivu yoyote. Hayo si ya kihalisi kamwe! Kwa sababu kile mnachotumainia si kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana katika mwili na kupata ukweli kwenye harakati ya maisha yenu, yaani, kuishi kwa ajili ya ukweli na kutetea haki. Haya siyo yale maisha ambayo mngedhani ni ya kupendeza, ya kusisimua. Mnahisi kwamba haya hayatakuwa maisha yanayovutia au ya maana. Machoni mwenu, kuishi maisha kama hayo kutatoa hisia za kudhalilishwa! Hata Ingawa mnakubali kuadibu huku leo, hata hivyo kile mnachofuatilia si kupata ule ukweli au kuishi kwa njia ya ukweli katika wakati wa sasa, bali kuweza kuingia katika maisha yenye furaha nje ya miili yenu baadaye. Hamtafuti ukweli wala hamtetei ukweli, wala hamtetei ukweli na bila shaka hampo kwa ajili ya kweli. Hamtafuti kuingia leo, lakini badala yake kila wakati mnafikiria “siku moja,” huku mkitazama mbingu ya samawati na kudondokwa na machozi machungu, na mkitarajia kuchukuliwa kuenda mbinguni siku moja. Je, hamjui kwamba kufikiria huku kama kwenu tayari kumeondokwa na uhalisi? Unaendelea kufikiria kwamba Mwokozi mwenye upole na huruma isiyoisha bila shaka atakuja siku moja kukuchukua pamoja na Yeye, wewe ambaye umevumilia ugumu na mateso ulimwenguni humu, na kwamba Yeye bila shaka atalipiza kisasi kwa ajili yako wewe ambaye umedhalilishwa na kunyanyaswa. Je, si kweli kwamba umejaa dhambi? Wewe pekee ndiwe ambaye umeteseka ulimwenguni humu? Umemilikiwa na Shetani wewe mwenyewe na kuteseka—je, bado Mungu anahitaji kukulipizia kisasi? Wale wasioweza kutosheleza mahitaji ya Mungu—kwani wao wote si adui wa Mungu? Wale wasioamini katika Mungu mwenye mwili—kwani wao si wapinga Kristo? Matendo yako mazuri yana maana gani? Yanaweza kuchukua nafasi ya moyo unaomwabudu Mungu? Huwezi kupokea baraka za Mungu kwa kufanya baadhi ya matendo mazuri tu, naye Mungu hatakulipizia kisasi yale mabaya uliyofanyiwa kwa sababu tu umeonewa na kukandamizwa. Wale wanaomwamini Mungu ilhali hawamjui Mungu, lakini wanaofanya matendo mazuri—kwani wao nao hawaadibiwi pia? Unamwamini Mungu tu, unataka Mungu akushughulikie na Akulipizie kisasi tu kwa mabaya uliofanyiwa wewe, na unataka Mungu kukupa njia ya kimbilio kutoka kwa umaskini wako. Lakini unakataa kutilia maanani ukweli; wala hutamani kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Hata zaidi, huwezi kuyakimbia maisha haya magumu na yasiyo na maana. Badala yake, huku ukiishi maisha yako katika mwili na maisha yako ya dhambi, unamwangalia Mungu kwa matarajio ya kusahihisha manung’uniko yako na kuondoa ukungu wa kuwepo kwako. Haya yanawezekanaje? Ukimiliki ukweli, unaweza kumfuata Mungu. Kama unaishi kwa kudhihirisha, unaweza kuwa onyesho la neno la Mungu. Kama unao uzima, unaweza kufurahia baraka ya Mungu. Ni wale tu walio na ukweli wanaweza kufurahia baraka ya Mungu. Mungu huhakikisha kwamba anawafidia wale wote wanaompenda kwa moyo wao wote pamoja na pia wanaovumilia magumu na mateso, na wala si kwa wale wanaojipenda tu na wamejipata kwenye mtego wa uwongo wa Shetani. Kunawezaje kuwa na wema miongoni mwa wale wasiopenda ukweli? Kunawezaje kuwa na haki miongoni mwa wale wanaopenda mwili tu? Si kweli kwamba haki na wema vyote vinarejelea ukweli? Si kweli kwamba vyote hivi vimehifadhiwa wale wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote? Wale wasiopenda ukweli na ambao ni maiti zinazooza—je, watu hawa wote huwa hawajaficha maovu? Wale wasioweza kuishi ukweli—hawa wote si adui wa ukweli? Na je ninyi?

Kama unaweza kutoroka ushawishi huu wa giza na kujitenga na mambo hayo machafu, kama unaweza kuwa mtakatifu, inamaanisha kwamba unao ukweli. Si kwamba asili yako yamebadilika, lakini tu kwamba unaweza kuweka ukweli katika matendo na unaweza kuunyima mwili wako. Haya ndiyo yanayopatikana kwa wale waliotakaswa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kuwatakasa binadamu ili mwanadamu aweze kuwa na ukweli, kwa sababu mwanadamu sasa anauelewa ukweli kidogo sana! Kufanya kazi ya kushinda kwa watu hawa ni jambo la umuhimu mkubwa mno. Nyote mmeanguka katika ushawishi wa giza na mmeumizwa mno. Shabaha ya kazi hii, basi, ni kuwawezesha kujua asili ya binadamu na hivyo basi kuishi kwa ukweli. Kukamilishwa ni kitu ambacho viumbe wote wanafaa kukubali. Kama kazi ya awamu hii inahusu tu kufanya watu kuwa wakamilifu, basi inaweza kufanywa Uingereza, au Amerika, au Israeli; inaweza kufanywa kwa watu wa taifa lolote. Lakini kazi ya kushinda ni kuwa inachagua. Hatua ya kwanza ya kazi ya kushinda ni ya muda mfupi; aidha, itatumika kumdhalilisha Shetani na kuushinda ulimwengu mzima. Hii ndiyo kazi ya mwanzo ya kushinda. Mtu anaweza kusema kwamba kiumbe yeyote anayemwamini Mungu anaweza kufanywa kuwa kamili kwa sababu kukamilishwa ni kitu ambacho mtu anaweza kufikia tu baada ya mabadiliko ya muda mrefu. Lakini kushindwa ni tofauti. Kielelezo na mlengwa wa kushinda lazima awe yule anayebaki nyuma zaidi, akiishi kwenye giza totoro kabisa, na vilevile mwenye hadhi kidogo kabisa, na asiyekuwa radhi kumkubali Mungu zaidi, na asiyetii Mungu zaidi. Huyu ndiye aina ya mtu anayeweza kutoa ushuhuda wa kushindwa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kumshinda Shetani. Shabaha kuu ya kufanya watu kuwa wakamilifu, kwa upande mwingine, ni kuwapata watu wale. Ni kwa ajili ya kuwawezesha watu kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa ndio kazi ya kushinda imewekwa hapa, kwa watu kama ninyi. Lengo ni kuwafanya watu kutoa ushuhuda baada ya kushindwa. Watu hawa walioshindwa watatumika kufikia shabaha ya kumdhalilisha Shetani. Kwa hivyo, mbinu kuu ya ushindi ni gani? Kuadibu, hukumu, kutupilia mbali laana, na kufichua—kutumia tabia ya haki katika kuwashinda watu ili waweze kushawishika kabisa kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu. Ili kutumia uhalisi wa neno na kutumia mamlaka ya neno ili kuwashinda watu na kuwashawishi kabisa—hii ndiyo maana ya kushindwa. Wale waliofanywa kuwa wakamilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa ya kazi ya hukumu, kubadilisha tabia yao na kumjua Mungu. Wanapitia njia ya kumpenda Mungu na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo hiari zao wenyewe. Wale waliokamilishwa ni wale walio na ufahamu halisi wa ukweli kutokana na kupitia neno la Mungu. Wale walioshindwa ni wale wanaojua kuhusu ukweli lakini hawajakubali maana halisi ya ukweli. Baada ya kushindwa, wanatii, lakini utiifu wao wote unatokana na hukumu waliyopokea. Hawana uelewa kabisa wa hali halisi ya ukweli mwingi. Wanautambua ukweli kwa matamshi, lakini bado hawajapitia ukweli; wanauelewa ukweli, lakini hawajapitia ule ukweli. Kazi inayofanywa kwa wale wanaokamilishwa inajumuisha kuadibiwa na kuhukumiwa, pamoja na kupokea uzima. Mtu anayethamini kuingia katika ukweli ni mtu anayefaa kukamilishwa. Tofauti kati ya wale watakaofanywa kuwa wakamilifu na wale walioshindwa ni iwapo wanaingia ukweli. Wale wanaouelewa ukweli, wameingia katika ukweli, na wanauishi ukweli huo ndio wale waliokamilishwa; wale wasioelewa ukweli, hawauingii ukweli, yaani, wale wasioishi ukweli, ni watu wasioweza kukamilishwa. Ikiwa watu kama hao wanaweza sasa kutii kabisa, basi wameshindwa. Kama wale walioshindwa hawatafuti ukweli—kama wanafuata lakini hawaishi kwa njia ya ukweli, kama wanaona na kuusikia ukweli lakini hawathamini kuthamini kuishi kwa njia ya ukweli—basi hawawezi kukamilishwa. Watu ambao ni wa kufanywa kuwa wakamilifu wanatenda ukweli kulingana na mahitaji ya Mungu kwao katika njia ya ya kuelekea kukamilishwa. Kupitia haya, wanatimiza mapenzi ya Mungu, na wanapata kufanywa kuwa wakamilifu. Yeyote anayefuata hadi mwisho kabla ya kazi hiyo ya ushindi kuhitimishwa ni aliyeshindwa, lakini hawezi kusemekana kuwa ndiye aliyekamilishwa. Waliokamilishwa kunarejelea wale ambao, baada ya kumalizika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kumilikiwa na Mungu. Kunaashiria wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanasimama imara katika majaribio na wanaishi kwa kudhihirisha ukweli. Kile kinachotofautisha kushindwa na kukamilishwa ni zile tofauti katika hatua za kufanya kazi na tofauti katika kiwango ambacho watu huelewa na kuingia katika ukweli. Wale wote ambao hawajaingia katika njia ya kukamilishwa, kumaanisha wale wasio na ukweli, mwishowe bado wataondolewa. Ni wale tu walio na ukweli na wanaoishi ukweli wanaoweza kumilikiwa kabisa na Mungu. Yaani, wale wanaoishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro ndio wanaofanywa kuwa wakamilifu, huku wengine wote ndio ambao wameshindwa. Kazi inayofanywa kwa wale wote wanaoshindwa inajumuisha tu kuweka laana, kuadibu, na kuonyesha hasira, na yale yanayowajia ni haki na laana tu. Kushughulikia mtu kama huyo ni kufichua waziwazi—kufichua tabia potovu iliyo ndani yake ili aweze kuitambua mwenyewe na kushawishika kabisa. Punde binadamu anapokuwa mtiifu kabisa, kazi ya ushindi inakamilika. Hata kama watu wengi wangali hawatafuti kuelewa ukweli, kazi ya ushindi itakuwa imekamilika.

Kunacho kigezo cha kufikiwa iwapo utakamilishwa. Kupitia kwa uamuzi wako, ustahimilivu wako, na dhamiri yako, na kupitia ufuatiliaji wako, utaweza kupitia maisha na kutimiza mapenzi ya Mungu. Haya ndiyo kuingia kwako na kile kinachohitajika kwenye njia ya kuwa mkamilifu. Kazi ya kuwa mkamilifu inaweza kufanywa kwa watu wote. Yeyote anayemfuatilia Mungu anaweza kufanywa kuwa mkamilifu na anayo fursa na sifa za kufanywa kuwa mkamilifu. Hakuna sheria ngumu na ya haraka hapa. Ikiwa mtu anaweza kukamilishwa hasa kunategemea kile anachofuatilia. Watu wanaopenda ukweli na walio na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli bila shaka wanaweza kufanywa kuwa wakamilifu. Watu wasioupenda ukweli hawasifiwi na Mungu; hawamiliki maisha ambayo Mungu anadai, na hawawezi kufanywa kuwa kamilifu. Kazi ya kufanywa kuwa mkamilifu ni kwa minajili tu ya kuwamiliki watu, na wala si hatua katika kupigana na Shetani; kazi ya ushindi ipo tu kwa minajili ya kupigana na Shetani, kumaanisha kwamba kutumia ushindi wa mwanadamu ili kumzidi Shetani nguvu. Sehemu hii ya nyuma ndiyo kazi kuu, kazi mpya zaidi ambayo haijawahi kufanywa katika enzi zote. Mtu anaweza kusema kwamba shabaha ya hatua hii ya kazi kimsingi ni kuwashinda watu wote ili kuweza kumshinda Shetani. Kazi ya kufanya watu kuwa wakamilifu—hiyo si kazi mpya. Kazi yote katika kipindi ambapo Mungu anafanya kazi katika mwili inayo shabaha yake kuu kama ushindi wa watu. Hii ni sawa na ile Enzi ya Neema. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubishwa ndiyo iliyokuwa kazi kuu. “Kuwapata watu” kulikuwa nyongeza katika kazi ya mwili na kulifanywa tu baada ya kusulubishwa. Wakati Yesu alipokuja na kufanya kazi Yake, shabaha Yake ilikuwa hasa kutumia kusulubishwa Kwake kushinda utumwa wa kifo na Kuzimu, kuweza kushinda ushawishi wa Shetani, kumaanisha kumshinda Shetani. Ilikuwa tu baada ya kusulubishwa kwa Yesu ndipo Petro alipoanza hatua kwa hatua kushika njia ya kuwa ukamilifu. Bila shaka alikuwa miongoni mwa wale waliomfuata Yesu wakati Yesu alipokuwa akifanya kazi, lakini hakufanywa kuwa mkamilifu wakati huo. Badala yake, ilikuwa ni baada ya Yesu kumaliza kazi Yake ndipo Petro alipoanza kuelewa taratibu ukweli na kisha akafanywa kuwa mkamilifu. Mungu mwenye mwili huja ulimwenguni tu kukamilisha hatua muhimu na ya maana sana ya kazi katika kipindi kifupi cha muda, si kuishi kwa kipindi kirefu miongoni mwa watu ulimwenguni na kuwafanya kuwa kamili kwa makusudi. Huwa hafanyi kazi hiyo. Hasubirii mpaka wakati ule ambao binadamu amefanywa kuwa mkamilifu kabisa ili kuhitimisha kazi Yake. Hiyo siyo shabaha na umuhimu wa kupata mwili Kwake. Yeye huja tu ili kufanya kazi ya kipindi kifupi ya kuwaokoa binadamu, na wala si kufanya ile kazi ya kipindi kirefu sana ya kuwafanya binadamu kuwa wakamilifu. Kazi ya kuwaokoa binadamu ni ya uwakilishi, inayoweza kuzindua enzi mpya na inaweza kukamilishwa katika kipindi kifupi cha muda. Lakini kuwafanya binadamu kuwa wakamilifu kunahitaji kuwaleta binadamu hadi kiwango fulani na ni kazi inayoweza kuchukua muda mrefu. Kazi hii lazima ifanywe na Roho wa Mungu, lakini inafanywa kwa msingi wa ukweli unaozungumzwa wakati wa kazi Yake akiwa mwili. Au aidha Yeye huwainua mitume kufanya kazi ya uchungaji ya kipindi kirefu, ili kufikia shabaha Yake ya kuwafanya binadamu kuwa wakamilifu. Mungu mwenye mwili hafanyi kazi hii. Huongea tu kuhusu njia ya maisha ili watu waweze kuelewa na kuwapatia tu binadamu ukweli, badala ya kuandamana na mwanadamu bila kusita katika kutenda ukweli kwani kufanya hivyo hakumo ndani ya huduma Yake. Kwa hivyo Hatakuwa akiandamana na mwanadamu mpaka siku ile ambayo mwanadamu ataelewa kabisa ukweli na kupata kabisa ukweli. Kazi Yake akiwa mwili inahitimishwa wakati mwanadamu anapoingia rasmi kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu, wakati mwanadamu anapoingia kwenye njia sahihi ya kufanywa kuwa mkamilifu. Hapa, bila shaka ndipo pia wakati ambapo atakuwa Ameshinda Shetani kabisa na kuutawala ulimwengu. Hajali kama mwanadamu hatimaye ameingia ukweli wakati huo, wala kujali kuhusu kama maisha ya binadamu ni makubwa au madogo. Hakuna kati ya hayo ambayo Yeye akiwa katika mwili anafaa kusimamia; hakuna kati ya hayo iko ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili. Punde Anapomaliza kazi aliyonuia, Yeye huhitimisha kazi Yake katika mwili. Kwa hiyo, kazi ambayo Mungu mwenye mwili anafanya ni kazi ile tu ambayo Roho wa Bwana hawezi kufanya moja kwa moja. Aidha, ni ile kazi ya wokovu ya kipindi kifupi, na wala si kazi ya kipindi kirefu hapa ulimwenguni.

Kuinua ubora wa tabia zenu hakumo ndani ya eneo la kazi Yangu. Ninawaomba kufanya hivi tu kwa sababu ubora wa tabia yako uko chini sana. Kwa ukweli hii si sehemu ya kazi ya kukamilisha; badala yake, ni kazi ya ziada mnayofanyiwa ninyi. Kazi inayokamilishwa kwenu leo inafanywa kulingana na kile mnachohitaji. Imebinafsishwa, na wala si njia fulani inayofaa kuingiwa na kila mtu ambaye anafanywa kuwa mkamilifu. Kwa sababu ubora wenu wa tabia uko chini zaidi kuliko yeyote yule aliyefanywa kuwa mkamilifu kitambo, kazi hii, inapokuja kwenu, inakabiliwa na vizuizi vingi. Nimo miongoni mwenu nikifanya kazi hii ya ziada kwa sababu malengo ya kukamilisha ni tofauti. Kimsingi, wakati Mungu anapokuja ulimwenguni, Yeye hubaki ndani ya eneo Lake la kufaa na kutekeleza kazi Yake, bila kujishughulisha sana na shughuli nyingine. Hahusiki katika masuala ya familia au kushiriki katika maisha ya watu. Hajali kabisa kuhusu mambo hayo madogomadogo; yote haya si sehemu ya huduma Yake. Lakini ubora wako wa tabia uko chini zaidi kuliko vile Nilivyohitaji—hakuna ulinganifu kamwe—kiasi cha kwamba unakuwa kizuizi katika kazi. Aidha, kazi hii lazima ifanywe miongoni mwa watu katika nchi hii ambayo ni Uchina. Hamjapata elimu sana kiasi cha kwamba Sina chaguo lolote ila kuamuru kwamba muweze kupata elimu. Nimewaambieni kwamba hii ni kazi ya ziada, lakini pia ni kitu ambacho lazima muwe nacho, kitu kinachowafaidi nyinyi katika kufanywa kuwa mkamilifu. Kwa hakika, mnafaa kupata elimu, maarifa ya kimsingi kuhusu mienendo yenu binafsi, na maarifa ya kimsingi kuhusu maisha yaliyo mbele yenu; Sifai kuwazungumzia kuhusu mambo haya. Lakini kwa sababu hamna mambo haya, Sina chaguo jingine ila kufanya kazi ya kutia vitu hivi ndani yenu baada ya kuzaliwa humu ulimwenguni. Hata kama mna dhana nyingi kunihusu, bado Ninahitaji hiki kutoka kwenu, bado nahitaji kwamba muinue ubora wenu wa tabia. Si nia Yangu kuja na kufanya kazi hii, kwa sababu kazi Yangu ni kuwashinda tu, kupata imani yenu kamili kwa kuwahukumu nyinyi tu, hivyo basi kuonyesha njia ya maisha mnayofaa kuingia. Nikisema kwa njia nyingine, vile ambavyo mmeelimika na kama mna maarifa kuhusu maisha visingenihusu Mimi kamwe kama isingekuwa kwamba Nahitaji kuwashinda kwa neno Langu. Vyote hivi vinaongezewa ili kuhakikisha kuna matokeo yanayopatikana kutoka kwa kazi ya ushindi na kwa minajili ya kufanywa kwenu kuwa wakamilifu kutakakofuata. Si hatua ya kazi ya ushindi. Kwa sababu ubora wenu wa tabia ni wa hali ya chini, na nyie ni wavivu, na wazembe, wajinga, na wapumbavu, na wagumu na washenzi—kwa sababu nyie mmekithiri mipaka ya kutokuwa wenye akili razini—Nahitaji kwanza muinue ubora wenu wa tabia. Yeyote anayetaka kufanywa mkamilifu lazima afikie vigezo fulani. Ili kufanywa kuwa mkamilifu, lazima mtu awe wa akili razini na yenye umakinifu na awe radhi kuishi maisha yenye maana. Kama wewe ni mtu usiye radhi kuishi maisha matupu, mtu anayefuatilia ukweli, mtu aliye mwenye bidii katika kila kitu anachofanya, na mtu aliye na ubinadamu wa kawaida kabisa, basi wewe una sifa zinazostahili kufanywa kuwa mkamilifu.

Kazi hii miongoni mwenu inatekelezwa kwenu kulingana na ile kazi inayohitajika kufanywa. Baada ya ushindi wa watu hawa, kundi la watu litafanywa kuwa kamilifu. Kwa hivyo, kazi nyingi ya sasa pia inatayarisha shabaha ya kuwafanya kuwa wakamilifu, kwa sababu wapo wengi sana walio na hamu ya ukweli ambao wanaweza kufanywa kuwa wakamilifu. Kama kazi ya kushinda ilifaa kutekelezwa kwenu na baadaye kusiwe kazi ya ziada kufanywa, basi ni kwamba baadhi ya wale wanaotamani ukweli hawangepata? Kazi ya sasa inalenga kufungua njia ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu baadaye. Ingawa kazi Yangu ni ya ushindi tu, njia ya maisha iliyotamkwa na Mimi hata hivyo ni inatayarisha kuwafanya watu kuwa wakamilifu baadaye. Kazi inayokuja baada ya ushindi inaweka msingi wa kukamilisha hukukamili, na hivyo basi ushindi unafanywa ili kuweka msingi wa kule kufanywa kuwa wakamilifu. Mwanadamu anaweza kufanywa kuwa mkamilifu baada ya kushindwa tu. Sasa hivi kazi kuu ni kushinda; baadaye wale wanaotafuta na kutamani ukweli watafanywa kuwa wakamilifu. Kufanywa kuwa mkamilifu kunahusisha dhana nzuri za watu kuhusu maisha: Je, unao moyo unaompenda Mungu? Kina cha yale umeyapitia ulipotembea kwenye njia hii ni kipi? Upendo wako wa Mungu ni safi vipi? Kutenda kwako ukweli ni sahihi vipi? Ili kufanywa kuwa mkamilifu, lazima mtu awe na maarifa ya kimsingi ya vipengele vyote vya ubinadamu. Hili ni hitaji la kimsingi. Wale wote wasioweza kufanywa kuwa wakamilifu baada ya kushindwa hugeuka na kuwa vyombo vya huduma na hatimaye bado watatupwa kwenye ziwa la moto na kibiriti na bado wataanguka ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho kwa sababu ya tabia yao ambayo haijabadilika na wangali ni wa Shetani. Mtu akikosa sifa za kukamilishwa, basi yeye ni bure—hana manufaa, ni chombo, kitu ambacho hakiwezi kustahimili majaribio ya moto! Upendo wako wa Mungu sasa hivi ni mkubwa kiasi gani? Chuki yako kwako ni kubwa kiasi gani? Je, kweli unamjua Shetani kwa kina kiasi gani? Umekaza uamuzi wenu? Maisha yako katika ubinadamu yamethibitiwa vyema? Maisha yako yamebadilika? Unayaishi maisha mapya? Mtazamo wenu wa maisha umebadilika? Kama mambo haya hayajabadilika, huwezi kufanywa kuwa mkamilifu hata kama hurudi nyuma; badala yake, wewe umeshindwa tu. Wakati ukifika wa kukujaribu, unakosa ukweli, ubinadamu wako si wa kawaida, na wewe ni wa kiwango cha chini kama mnyama. Umeshindwa tu, umekuwa tu mtu aliyeshindwa tu na Mimi. Kama vile tu, punde punda anapopitia mjeledi wa bwana wake, yeye huwa na woga na hofu ya kufanya chochote kila wakati anapomwona bwana wake, ndivyo pia wewe ulivyo kama punda huyo aliyedhibitiwa. Kama mtu anakosa vipengele hivyo vizuri na badala yake yeye ni wa kutoonyesha hisia na mwenye woga, mwepesi kutishwa na wa kusitasita katika mambo yote, asiyeweza kutambua chochote kwa njia iliyo wazi, asiyeweza kukubali ukweli, ambaye bado hana njia ya kutendea, na hata zaidi asiye na moyo wa upendo wa Mungu—kama mtu hana uelewa wa namna ya kumpenda Mungu, namna ya kuishi maisha yenye maana, au namna ya kuwa mtu halisi—mtu kama huyu anawezaje kumshuhudia Mungu? Hii inaonyesha kwamba maisha yako yanayo thamani ndogo na wewe si kingine ila punda aliyedhibitiwa. Wewe umeshindwa, lakini hilo linamaanisha tu kwamba umelikataa lile joka kubwa jekundu na umekataa kumilikiwa nalo; hiyo inamaanisha kwamba wewe unaamini kuwa kunaye Mungu, unataka kutii mipango yote ya Mungu na huna malalamiko yoyote. Lakini je, katika vipengele vyema, unaweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kumbainisha Mungu? Ikiwa huna lolote kati ya haya, inamaanisha kwamba hujamilikiwa na Mungu, na kwamba wewe ni punda aliyedhibitiwa tu. Hakuna chochote cha kutamanika ndani yako, na Roho Mtakatifu hayumo kazini ndani yako. Ubinadamu wako unakosa mengi na haiwezekani Mungu kukutumia. Lazima uidhinishwe na Mungu na kuwa bora zaidi mara mia moja kuliko wanyama wasioamini na kuliko wanaotembea wakiwa wafu—wale tu wanaofikia kiwango hiki ndio wanaostahili kufanywa kuwa wakamilifu. Ni iwapo tu mtu anao ubinadamu na dhamiri ndio anafaa kutumiwa na Mungu. Ni wakati tu ambapo mnakamilishwa ndio mnaweza kufikiriwa kuwa binadamu. Wale waliofanywa kuwa wakamilifu tu ndio wale wanaoishi maisha yenye maana. Watu kama hawa tu ndio wanaoweza kumshuhudia Mungu hata pakubwa.

Iliyotangulia: Kuhusu Majina na Utambulisho

Inayofuata: Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp