180 Ninaahidi Maisha Yangu Kumfuata Mungu Kwa Uaminifu

1

Nilikamatwa na kuteswa na CCP kwa sababu ya kumshuhudia Mungu.

Huku nikiwa nimenaswa kwenye pango la pepo, nililala kwenye sakafu inayoganda.

Walitumia vifaa vya kila aina kuutesa mwili wangu uliodhoofishwa.

Kufedheheshwa na pepo kulifanya kifo kionekane kuwa bora kuliko maisha.

Nilihisi dhaifu mara nyingi sana, nilimamia kwa maumivu,

Niliteswa mara nyingi sana, nilikoroma kwa maumivu.

Maumivu na kukata tamaa vilinizingira, moyo wangu ulilia.

Sikuweza kujua mateso na maumivu haya makali yangeisha lini.

Nilimwomba Mungu mara nyingi sana katika usiku wa giza kuu.

Maneno ya Mungu yalinipa imani ya kusimama imara.

2

Nilifikiri kuhusu wakati huo mzuri nilioshinda pamoja na Mungu.

Wakati huo wa furaha uliibuka akilini mwangu.

Ningewezaje kusahau kiapo nilichokula wakati huo,

kuwa shahidi wa ushindi na kueneza neno la nguvu ya watu wa Mungu?

Hata kama bado sijaondolewa maumivu haya, lakini yanaendelea,

hata dhoruba zikiendelea kuvuma na tufani za mvua ghafla kuanguka,

hata nikifa baada ya kuamka,

acha damu yangu inayotiririka iondoe woga wangu unaonyonga.

Kwa ushupavu, niliimba wimbo wa shangwe wa ushindi ili kumsifu Mungu,

na nikashuhudia ushuhuda mkubwa sana ili kulitukuza jina takatifu la Mungu.

3

Kupitia majaribio na dhiki, mwishowe naamka.

Ninaona kuwa Shetani ni mwenye kustahili kudharauliwa, mkatili na mwovu.

Miale ya hasira inawashwa moyoni mwangu.

Naahidi maisha yangu kulitelekeza joka kubwa jekundu na kumshuhudia Mungu.

Ni heshima yangu sasa kuweza kumfuata Kristo wa siku za mwisho.

Mateso mepesi na ya mara moja hufanya kazi kwa utukufu usio na kifani.

Nikiwa na neno la Mungu kando yangu, sitahisi tena mpweke au mwenye hofu.

Mungu akiniongoza kupitia kwenye dhiki, natembea kwa utulivu.

Nipitapo katika majaribio na taabu, ninajawa na imani.

Ninaahidi maisha yangu kumfuata Kristo hadi mwisho kabisa.

Iliyotangulia: 179 Kuinuka Katikati ya Giza na Dhuluma

Inayofuata: 181 Nimeamua Mumfuata Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp